Search This Blog

Wednesday, November 2, 2022

KIVURUGE WA TANDALE - 4

 






Chombezo : Kivuruge Wa Tandale

Sehemu Ya Nne (4)





Siku hiyo ilikuwa ya kipekee sana kwangu kwa sababu kwa mara ya kwanza nilikutana na mwanamke aliyekuwa tofauti kabisa na wale wote niliokuwa nikikutana nao. Hali hiyo ilisababisha niwe nataka ‘tuendelee’ tena na tena, kila ngwe moja ilipoisha na kupumzika kidogo, nilikuwa nataka tuingie kwenye ngwe nyingine, ikafika mahali Ruqaiya akashindwa kwenda sawa na mimi.

Akaniomba tukatishe mpambano mpaka siku nyingine kwa sababu alikuwa amechoka sana, nikamkubalia kwa shingo upande. Kutazama saa ya ukutani, tayari ilishakuwa imegonga saa tano za usiku, Ruqaiya akakurupuka haraka kwa sababu alisema hajawahi hata siku moja kuchelewa kiasi hicho kurudi nyumbani kwake.

“Lakini si umesema mista kasafiri?”

“Hata kama... unajua naishi na ndugu za mume wangu, wasije kumfikishia taarifa halafu ikawa matatizo,” alisema Ruqaiya, harakaharaka akakimbilia bafuni. Sikutaka kumwacha aende peke yake kwa sababu kwenye sekta ya mahaba niue na mimi nilikuwa vizuri, hasa pale ninapokutana na ‘chombo’ kipya.

Basi na mimi nilimfuata, nikamuogesha kama mtoto mdogo na kusababisha moto wa mapenzi uzidi kuwaka kwenye moyo wake. Mpaka tunatoka, Ruqaiya alikuwa akinisisitiza sana kwamba nisicheze na moyo wake kwa sababu tangu aolewe hajawahi kufikiria hata siku moja kwamba anaweza kuja kutoka nje ya ndoa yake.

Akaniambia kwamba hata hivyo, licha ya kwamba anajua amefanya makosa makubwa kwa kumsaliti mumewe, hajutii kwa sababu eti hatimaye nimemfanya ajihisi kuwa mwanamke aliyekamilika na kumuonesha ulimwengu ambao awali alikuwa akihadithiwa tu.

“Najua kwamba hujatulia lakini siwezi kuacha kukupenda, nakuomba tulia na mimi utafurahi na moyo wako,” alisema Ruqaiya na cha ajabu, japokuwa wakati tunaingia alikuwa akiogopa hata kuongozana na mimi, wakati tukitoka alikuwa ameniegamia begani huku akiwa amenikumbatia bila kuogopa chochote.

Tulitoka mpaka kwenye maegesho ya magari, akaniuliza kama najua kuendesha gari, nikatingisha kichwa kukataa kwa sababu ukweli ni kwamba sikuwa najua, akaniambia natakiwa kujifunza na hata kama sina fedha, yeye atanilipia niende ‘driving school’.

Tulipoingia kwenye gari, alinikumbatia tena na kunimwagia mvua ya mabusu, akawa anaendelea kunisisitiza kwamba nitulie na yeye kwa sababu anataka kuyabadilisha maisha yangu. Baada ya kama dakika ishirini za kumwagiana mvua ya mabusu ndani ya gari, aliwasha na kulitoa taratibu, huku akionesha kuchoka sana.

Njia nzima Ruqaiya alikuwa kimya kabisa, mara kwa mara akawa ananitazama na kuishia kutabasamu mwenyewe, muziki laini ndani ya gari ukawa unatuburudisha. Kwa kuwa alikuwa dereva mzuri, hatukuchelewa kufika Tandale, akanishusha Kwa Mtogole na kabla sijashuka, alitoa bahasha kwenye mkoba wake na kunipa.

“Siku nyingine nitataka nifike mpaka nyumbani kwako.”

“Siyo leo?”

“Hapana, nimechelewa sana ujue,” alisema huku akitabasamu, basi nikamshukuru na kumtakia safari njema. Akaondoa gari lake, harakaharaka nikaiweka ile bahasha mfukoni, nikaanza kukatisha vichochoro haraka kuelekea nyumbani kwangu.

Kwa bahati nzuri, japokuwa muda ulikuwa umeenda sana, sikukutana na vibaka kama ilivyo kawaida kwenye mitaa ya kwetu, nikafika nyumbani kwangu salama. Nilitoa simu na kuiwasha, nikajilaza kwenye kochi na kuwasha redio, nikawa nasikiliza muziki taratibu.

Kwa jinsi nilivyokuwa nimechoka, haikupita muda mrefu nikapitiwa na usingizi mzito, kwa bahati nzuri nilikuwa nimeshafunga milango. Nilipokuja kuzinduka, ilikuwa ni karibu saa nane za usiku, nikazima redio na kujizoazoa mpaka chumbani. Nikajitupa kitandani na kuendelea kuuchapa usingizi.

Kesho yake asubuhi, niliwahi kuamka kama kawaida, ni hapo ndipo nilipokumbuka kwamba jana yake usiku, Ruqaiya alikuwa amenipa bahasha, nikaichukua suruali yangu niliyokuwa nimevaa na harakaharaka nikaitoa ile bahasha.

Nilipoifungua, sikuamini macho yangu, ilikuwa na noti kumi za dola miamia za Kimarekani, mpya kabisa. Nilizitoa na kuzitandaza kitandani, nikajikuta nikiishia kuchekacheka mwenyewe kama mwendawazimu.

Hata hamu ya kwenda kazini iliniisha, nilichokifanya nilichukua simu yangu kwa lengo la kumpigia Madam Bella, bosi wangu ili nimdanganye kwamba sitaweza kwenda kazini kutokana na ugeni uliokuwa umenitembelea pale nyumbani.

Kabla sijapiga simu, niligundua kwamba simu yangu ilikuwa na ‘missed calls’ nyingi sana pamoja na meseji, nikashusha pumzi ndefu na kuanza kuzitazama, moja baada ya nyingine. Zilikuwepo za Madam Bella, za Nancy, za Salma na nyingine za Ruqaiya.

Niliamua kuanza na za Ruqaiya, kumbe jana alipofika tu nyumbani kwake alinipigia na kunitumia meseji akinitaarifu kwamba amefika salama na anashukuru kwa kila kitu nilichomfanyia. Lakini meseji nyingine alikuwa ametuma alfajiri, akiniuliza kama nimeamka salama.

Ilibidi nimpigie, harakaharaka akapokea ambapo huku akizungumza kwa uchangamfu sana, aliniuliza kama nimeshaamka, nikamwambia kwamba nimeamka na najiandaa kwenda kazini, nikamshukuru sana kwa mzigo alionipa, akacheka kwa furaha na kuniambia nisijali, hayo ni mambo madogo tu.

Basi baada ya stori za hapa na pale, tuliagana. Nikampigia Madam Bella ambaye naye alikuwa amenipigia mara kadhaa bila mafanikio na kunitumia meseji, akiniambia kwamba nitakapoona ‘missed calls’ zake nimpigie.

Alipopokea, kitu cha kwanza kilikuwa ni lawama, akawa ananiuliza kwa nini tangu jana yake usiku sikuwa napokea simu zake wala kujibu meseji mpaka muda huo, nikamdanganya kwamba nilikuwa bize na wageni ndiyo maana sikupata muda wa kuzungumza naye.

Nilitumia chansi hiyohiyo kumuomba ruhusa, akanikubalia lakini kwa masharti kwamba lazima jioni nikakutane naye kwa sababu alikuwa na mazungumzo muhimu. Nikamkubalia ambapo aliniuliza kama zile fedha alizonipa eti zilikuwa zimenitosha!

Nilicheka na kumshukuru kwa sababu ukweli ni kwamba nilishasahau kwamba kuna fedha alinipa. Ruqaiya ni kama alikuwa ameenda kufuta kumbukumbu zote kwenye kichwa changu kuhusu watu wote niliokuwa kwenye uhusiano nao.

Basi baada ya kumalizana na Madam Bella, bosi wangu wa nguvu, niliiweka simu pembeni na kutoka nje kwa lengo la kuchota maji ili nianze kufanya usafi kwa sababu chumba kilikuwa kimechafuka sana. Nilipotoka tu, nilikutana na mama mwenye nyumba, macho yangu na yake yakagongana.

“Shikamoo mama,” nilimsalimu, akanitazama usoni bila kunijibu kitu. Siku zote nilikuwa nikimsalimia anaitika, sijui kwa nini siku hiyo hakuitika zaidi ya kuwa ananitolea macho tu.

“Jana ulirudi saa ngapi?” aliniuliza kwa sauti ya chini huku akigeuka huku na kule, kama anayehakikisha kwamba hakuna mtu anayetusikiliza.

“Nilichelewa kidogo,” nilimjibu, akanitazama huku akionesha kama ana jambo anataka kuzungumza na mimi lakini anahisi kama mtu anatusikiliza.

“Uko na nani humo ndani kwako?”

“Niko mwenyewe, nataka kufanya usafi,” nilimwambia, akawa anahisi kama namdanganya, akaniuliza kama namruhusu aende kuhakikisha, nikacheka tu kwa sababu sikuona mantiki yoyote ya kile alichokisema.

Nilifungulia bomba nikawa nachota maji, kumbe kweli aliamua kuingia ndani kwangu, ile naingiza ndoo zangu za maji nikashtuka kumuona akiwa amekaa juu ya kochi, akinitazama huku akitabasamu.

“Jana ulikuwa na mwanamke ndiyo maana ulichelewa kurudi nyumbani, unabisha?” aliniuliza, nikatabasamu huku nikitingisha kichwa kwa sababu nilikuwa najua alichokuwa anakitaka.

“Muongo, mbona unaonekana umechoka namna hiyo? Kama hukuwa na mwanamke nithibitishie kwa vitendo,” alisema huku akiinua miguu yake kihasara, khanga nyepesi aliyokuwa ameivaa ikafunuka upande mmoja na kunifanya nisisimke sana.

Tatizo nililokuwa nalo sijui ni mapepo au jini mahaba! Nilikuwa mwepesi sana wa kusisimka na kila nikisisimka, ‘mashetani’ yangu yanapanda, hata kama muda mfupi uliopita nimetoka mchezoni. Nilichokifanya, nilirudi nyuma na kufunga mlango kwa ndani ili asije akaingia mtu na kutufuma, nikavua singlendi niliyokuwa nimeivaa juu na kumsogelea pale kwenye kochi alipokuwa amekaa kihasarahasara.

Nilimgusa kwa ufundi f’lani hivi sehemu zake za kwenye mbavu, akaruka kwa nguvu na kutoa yowe la chini kwa chini kisha akanikumbatia kwa nguvu, akafungua fundo la ile khanga yake na kuiachia, ikadondoka chini, akabaki kama alivyo, ‘Ashrafu’ naye akawa amekasirika mno.





Nilimuinamia pale chini, akanidaka shingoni na kunivutia kwake, tukagusanisha ndimi zetu huku akionesha kuwa na hisia nzito juu yangu, yaani usingeweza kuamini kama ndiyo yule mama Abdul niliyekuwa namheshimu sana, alivyokuwa ananidekea ndivyo ‘hasira’ zangu zilivyokuwa zikizidi kunipanda.

Sijui nini kilinitokea, nilishtukia akimshika ‘Ashrafu’ na kumsokomezea kwenye chungu cha asali, nikafumba macho na kutoa mguno kidogo kwa sababu ni kitu ambacho sikukitarajia, basi utamu wa asali ukanifanya niwe najilamba midomo kwa raha.

Kwa ufundi wa hali ya juu, alijibinua, mimi nikawa chini na yeye kwa juu, basi akawa ni kama anaendesha baiskeli hivi! Waliosema ukubwa dawa hawakukosea, kweli alinionesha ukubwa wake na kiukweli, alinifanya niianze vyema sana siku yangu.

Basi pilikapilika ziliendelea, akiwa amenizidi kwa kila kitu, mpira ukawa unachezwa nusu uwanja. Hakuchukua muda mrefu, akatangaza kuliona lango, akafumua shuti kali lililomshinda golikipa na kutinga moja kwa moja nyavuni, basi akanidondokea kama mzigo.

Ilibidi niwe mjanja kwa sababu ningeweza hata kuishiwa pumzi kwa sababu alikuwa na mwili mkubwa kuliko mimi, haukupita muda mrefu akawa anakoroma. Harakaharaka niliamka na kwenda kujimwagia maji kwa sababu kiukweli nilikuwa na uchovu wa siku kadhaa mfululizo.

Nilipojimwagia maji ya baridi, nilipata nguvu mpya, nikarudi ndani na kumkutabado amelala palepale kwenye kochi, akiwa hajitambui, anakoroma tu. Basi nilikaa pembeni yake, nikawa namtazama huku nikijiuliza maswali mengi ndani ya kichwa changu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mwanamke kama huyu hivi amekosa nini kwa mumewe mpaka anaingia kwenye kumi na nane za kijana kama mimi ambaye ni sawa na mdogo wake, tena wa mbali kabisa,” nilijiuliza huku nikiendelea kumtazama, mkono wangu mmoja ukipitapita kwenye ‘nundu’ yake iliyokuwa imenona. Nikiwa naendelea na utalii wa ndani, mara alianza kujinyonganyonga pale kwenye kochi, mara akaamka na kukaa, akapiga miayo mfululizo na kujinyoosha.

“Ahsante baba’angu, hata sijui nikupe nini kwa raha ulizonipa! Sijawahi kunanii tangu nilipoolewa miaka kumi na tano iliyopita,” alisema na kujizoazoa pale alipokuwa amekaa, akainuka na kuja kunibusu kwa mahaba, akanikumbatia huku mikono yake laini ikinipapasa hapa na pale.

“Nenda kajimwagie maji upate nguvu upya,” nilimwambia, kweli akatoka na kuchungulia huku na kule alipohakikisha hakuna mtu, aliingia ndani kwake na kwa sababu walikuwa na vyoo vya ndani kwa ndani (self container), muda mfupi baadaye alitoka akiwa ameshaoga na angalau alikuwa amechangamka.

Aliingia huku akiwa anajitingisha, uso wake ukizungumza lugha niipendayo huku akinitazama kwa macho yake aliyokuwa akiyarembua na kunipa raha fulani ndani ya moyo wangu!

Nikajikuta nikianza kuchaji upya na safari hii, sikutaka tena ngwe ya pili ipigwe pale kwenye uwanja ule, niliamini pengine hata kunichezea kwake nusu uwanja kulisababishwa na ubovu wa uwanja, basi nikamkokota kuelekea chumbani.

“We mtoto utaniua mwenzio, siyo kwa mahaba haya! Natamani hata leo niachike kwa mume wangu unioe wewe,” alisema kwa sauti iliyotokea kwenye matundu ya pua zake, akapiga magoti na kunisukumia juu ya uwanja wa fundi seremala, mara nikashtukia ameichomoa mic kutoka kusikojulikana na kuanza kurap, kwa mara nyingine nikajikuta nikitoa mguno wa nguvu.

Unajua alichokuwa ananipatia ni kwamba alikuwa akifanya mambo kwa kushtukiza sana, kwanza sikutegemea kama na yeye anajua haya mambo ya vijana ya kurap, kwa hiyo likawa ni bonge la ‘sapraiz’ ambalo katika sanaa za kikubwa, huongeza sana mshawasha.

Basi ali-rap kwa ufundi wa hali ya juu, ni hapo ndipo nikagundua kwamba kumbe mechi za kuvizia huwa zinawanyima sana nafasi wachezaji wa timu zote mbili kuonesha viwango vyao uwanjani.

Sikutaka kubaki nyuma maana nilihisi anaweza kuniona mshamba, basi wakati yeye akiendelea ku-rap na mimi nilijikunja kama mwanasarakasi na kujigeuza upande wa mapaja yake, nikavamia chungu cha asali na kuanza kuilamba kwa uroho.

Na yeye kitendo hicho kilikuwa ni kama sapraizi kwake, akashtuka mno na kuanza kujinyonganyonga kama chatu aliyemeza mbuzi mzima.

Niliongeza kasi, sasa nikawa natumia ncha ya ulimi wangu kufanya yangu, nikawa nalamba asali kutoka juu kwenda chini kisha kutoka chini kwenda juu, akawa anatoa ukelele ambao kuna wakati ulinifanya nihisi kwamba kama kuna mtu yeyote pale uani anaweza kusikia na ‘kuunguza picha’.

Kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kusonga mbele ndivyo alivyokuwa akizidi kuishiwa nguvu, nikaona hakuna haja ya kuendelea kupoteza muda kwa sababu kama ni maji yalikuwa yamechemka kisawasawa, kazi iliyobaki ilikuwa ni kutia mchele tu.

Basi alikaa mkao wa kula na kipyenga kilipopulizwa tu, shughuli ilianza na safari hii sikutaka anizidi tena ujanja, nikawa napiga mashuti ya mbali mfululizo, ndani ya muda mfupi tu tayari nilikuwa nimemuelemea, sasa mpira ukawa unachezwa nusu uwanja kwenye goli lake, nikaongeza mashambulizi kwa nguvu na kumfanya awe anagugumia mno.

Nilipiga shuti moja kwa umahiri mkubwa, kwa staili ambayo kule kwetu uswazi tunaita ‘mwana ukome’, basi bila kutarajia akajikuta akiunganisha shuti langu kwenye goli lake, akajifunga mwenyewe na kudondoka pembeni kama mzigo, akawa anahema kwa nguvu kama mtu aliyetoka kukimbia mbio za mita mia moja.

“Hapana! Basi inatosha, this is too much,” alimwaga kimombo akimaanisha maji ‘yamezidi unga’ huku akijizoazoa kuinuka pale eneo la tukio, akajifunga khanga yake na kukimbilia sebuleni, nikabaki nacheka mwenyewe kwa sababu kiukweli ni kwamba nilikuwa nimemuweza.

Kabla hajatoka nje kabisa, nilimuwahi pale sebuleni, nikamzuia mlangoni na kumkumbatia na kumbusu, naye akanibusu.

“Sasa unaniachaje katika hali kama hii, nivumilie kidogo,” nilimwambia, akamtazama ‘Ashrafu’ na kunitazama usoni.

“Umetumia dawa gani? Au vumbi la Kongo?”

“Ndiyo nini? Wala sijatumia chochote ndivyo nilivyo,” nilimwambia huku nikicheka, naye akacheka kichovu na kurudia kauli yake kwamba nitamuua, nikamwambia hawezi kufa, basi akakubali kwa shingo upande huku akinisisitiza kwamba amechoka sana anaweza kudondoka muda wowote.

Kwa kuwa mwenyewe alishasalimu amri, niliona njia pekee ya kumaliza utata uliokuwepo, ni kutumia ile staili yangu ya ‘cheka nao’, nikamuelekeza nini cha kufanya na muda mfupi baadaye, kazi ilikuwa ikiendelea, palepale mlangoni kwa ndani.

Mipango yangu ilienda kama ilivyopangwa, ndani ya muda mfupi tu tayari nilikuwa kwenye nafasi nzuri ya kumaliza ubishi, kitu ambacho sikukielewa ni kwamba kumbe na yeye tayari alikuwa amekaribia sana kuvunja dafu, basi matukio yote yakatokea kwa pamoja! Kila mmoja akadondokea upande wake, ama kwa hakika nilikuwa nimemfaidi.

Katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea, kumbe pale nje kulikuwa na mtu aliyekuwa akifuatilia kila kilichokuwa kikiendelea na kwa sababu mlango wa sebuleni ulikuwa umeungana na dirisha, alishuhudia kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kushtukia mchezo baada ya kuhisi kama kuna mtu anatutazama kutokea dirishani, nilipotazama pale nilipohisi kama pana mtu, kweli bwana nilishtukia mtu akijificha haraka kuonesha kwamba alikuwa akifuatilia kila kilichokuwa kikiendelea mle ndani, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio kuliko kawaida na harakaharaka nilipata nguvu.

“Kuna mtu anatuchungulia!”

“Mtu? Nani?”

“Hata sijui ni nani.”

“Mungu wangu, asije kuwa mume wangu amerudi,” alisema huku akiinuka haraka na kujifunga upande wake wa khanga, tukawa tunatazama kwa hofu.

“Sasa itakuwaje?”

“Hebu toka kamuangalie!”

“Mh! Kama ni mume wako kweli si ataniua? Kwa nini usitoke wewe?”

“We... we! Mimi ndiyo anaweza kunichinja kabisa.”

“Sasa tufanyeje?” nilimuuliza huku nikiwa natokwa na kijasho chembamba, nikajua ule msemo wa za mwizi arobaini umetimia. Mara tukasikia mlango ukigongwa, ngo! Ngo! Ngo!





“Kaka Ashrafu!” sauti ya kike ilisikika na kutuondolea ile hofu kubwa iliyokuwa imetanda ndani ya mioyo yetu, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama mama mwenye nyumba usoni.

“Ni Khazija huyo.”

“Khazija ndiyo nani?”

“Si huyo mpangaji mpya anayekaa hicho chumba cha pili?”

“Kwani hicho chumba kilishapata mpangaji?”

“Ndiyo, wewe huwa hushindi nyumbani siyo rahisi kujua, ana wiki mbili sasa.”

“Mh! Sasa amelijuaje jina langu na atakuwa anataka nini?”

“Sasa hayo ni maswali ya kuniuliza mimi kweli? Hebu mfungulie umsikilize, ikiwezekana muulize kwa nini alikuwa anatuchungulia, kumbe hana adabu kiasi hiki,” alisema mama mwenye nyumba kwa sauti ya kunong’ona.

Bado mlango ulikuwa ukigongwa na baada ya kupata uhakika kwamba alikuwa ni mpangaji mwenzangu, sikuona hata umuhimu wa kuvaa nguo, nilijifunga taulo na kufungua kidogo mlango.

“Samahani kaka, wewe ndiyo Ashrafu?”

“Ndiyo, vipi kwani?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni kwa sababu ukweli ni kwamba nilikuwa simfahamu vizuri wala sikuwa nimewahi kukutana naye uso kwa uso. Japokuwa hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukutana naye, nikiri kwamba nilijikuta nikivutiwa kuendelea kumtazama kwani alikuwa na uzuri fulani hivi ‘amazing’.

Macho yake yalikuwa madogo na mdomo fulani hivi wenye lipsi nyeusi za kuvutia sana. Hakuwa mrefu wala mfupi, hakuwa mweusi wala mweupe, alikuwa na rangi fulani hivi ya chocolate, kifua kidogo kama msichana kigori huku uso wake ukionesha wazi kwamba alikuwa na aibu sana.

Alipoona namkodolea sana macho, na yeye alijikaza na kunitazama usoni, macho yangu na yake yakagongana huku akiwa na tabasamu fulani hivi la aina yake. Kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba alikuwa akipiga chabo muda mfupi uliopita, maana yake ni kwamba alikuwa ameshuhudia kila kitu kilichokuwa kimetokea.

Hali hii ilinifanya nikwepeshe macho yangu haraka kutokana na aibu niliyokuwa naihisi. Cha ajabu wakati mimi nikikwepesha macho yangu, eti na yeye alikuwa akinitazama usoni huku akiwa ni kama mtu anayetaka kusema jambo lakini anahofia kitu, aibu za kikekike zikiwa zimemjaa usoni.

“Samahani, naomba niazime chaja ya smartphone, mimi ni jirani yako wa chumba cha pili nimehamia siku chache zilizopita,” alisema huku akiendelea kunitazama kwa macho ya kuibia, nikawa kama siamini kile alichokuwa anakisema.

Yaani kugonga kote mlango kumbe hiyo ndiyo ilikuwa shida yake? Nilishusha pumzi ndefu na kulazimisha tabasamu kwenye uso wangu.

Niliingia ndani bila kusema chochote na wala hata sikujiuliza zaidi ya mara moja, nikatoa chaja na kumpa, akanishukuru na akawa anaondoka, alitembea kwa maringo mithili ya twiga awapo mbugani.

Nadhani kuna jambo alikuwa amelikusudia kwa sababu hiyo ondoka yake ilikuwa ni balaa, alitembea kwa kujitingisha sana, ni hapo ndipo nikagundua kwamba licha ya upande wa kuanzia kiunoni kuja juu alikuwa kama msichana kigori, kuanzia kiunoni kushuka chini ilikuwa ni balaa, kumbe alikuwa na ‘chura’ mkubwa, ukichanganya na ‘pensi nyanya’ aliyokuwa amevaa, nilijikuta kwenye wakati mgumu sana.

Alipofika mlangoni kwake, aligeuka, macho yangu na yake yakagongana, halafu akaachia katabasamu fulani hivi kakichokozi na kunifanya nibaki nimeganda kama ‘zombie’.

“Alikuwa anasemaje?”

“Eti alikuwa ananiomba chaji ya simu.”

“Jana alikuja kuniomba, nikamwambia labda akusubiri wewe maana ya kwangu aliondoka nayo mume wangu. Msichana mcheshi sana huyo, yaanihakawii kumzoea mtu,” alisema huku akinitazama usoni, nadhani alikuwa akitaka kunisoma kitu.

Kwa bahati mbaya, mimi nilikuwa mjanja zaidi yake, basi nikajifanya kuzuga kwamba huwa sipendi mazoea na wanawake kiasi hicho kwani ni rahisi watu wengine kunihisi vibaya.

“We jishaue tu! Nikikuona mmeanza kuzoeana mazoea yasiyofaa nitajua cha kukufanya,” alisema huku akionesha kumaanisha kile alichokisema. Basi nikacheka sana, nikamuuliza kwa sababu gani amesema hivyo? Jibu lake likawa eti ni kwa sababu ananipenda sana na hajawahi kukutana na mwanaume kama mimi.

Wakati mazungumzo yakiendelea, kichwani mwangu bado sura ya yule msichana ilikuwa ikizunguka ndani ya kichwa changu. Hata sijui kwa nini nilikuwa nimebadilika na kuwa na ‘uchu’ kiasi hicho kwa sababu hakukuwa na sababu yoyote ya mimi kuhangaika na wanawake wengine kwani muda mfupi tu uliopita, nilikuwa nimetoka kuelea kwenye bahari yenye kina kirefu.

“Utakula nini?” aliniuliza mama mwenye nyumba wakati akiinuka na kujinyoosha huku akipiga miayo mfululizo. Nikamjibu kwamba chochote atakachotaka yeye mimi sina tatizo, akaniambia kwamba ngoja aingie jikoni akaniandalie madikodiko kama shukrani kwangu kwa kazi nzuri niliyoifanya.

Basi alinisogelea na kunikumbatia, akanimwagia mvua ya mabusu na kunitaka nikaangalia pale mlangoni kama hakuna mtu anayeweza kumuona. Basi nilichungulia lakini hakukuwa na dalili za mtu yeyote, ukiachilia mbali yule msichana ambaye naye alikuwa amejifungia mlango wake kwa ndani.

Harakaharaka alitoka na kwenda kwake, na mimi nikaenda bafuni kujimwagia maji ili kuondoa uchovu ambao sasa ni dhahiri ulishaanza kunielemea. Dakika chache baadaye, nilitoka na kurudi ndani, nikaenda kutandika na kuweka mazingira vizuri kwani kila kitu ndani kilikuwa vululuvululu.

Nilipomaliza nilitoka na kujilaza sebuleni, nikaongeza feni na kuchukua simu yangu. Ilikuwa imejaa meseji ambazo hazijasomwa pamoja na missed call kibao.

Basi nikaanza na meseji ambazo nyingi zilikuwa ni za kutoka kwa Ruqaiya ambaye ilionesha ile shughuli ya usiku uliopita imemchanganya kabisa kiasi cha kuanza kuwa na mahaba mazito kwangu.

Nilimjibu meseji zake zote harakaharaka, muda mfupi baadaye akanipigia. Nilipopokea nilipokelewa na busu mwanana, akaniambia kwamba eti ameshindwa kwenda kazini kwa sababu amechoka sana, hivyo amelala tu nyumbani.

Nilicheka sana, tukapiga stori za hapa na pale lakini kikubwa ni kwamba alikuwa akinisifia sana kwa jinsi nilivyoweza kumfanya avunje madafu, kitu ambacho tangu usichana wake hakuwahi kukutana nacho.

Basi na mimi nilimsifia sana kwa sababu ukweli ni kwamba alikuwa tofauti sana na wanawake wote niliowahi kukutana nao kwenye kumi na nane zangu. Nikiwa naendelea kuongea na Ruqaiya kwenye simu, tukifurahi na kucheka pamoja, mlango wangu ambao haukuwa umefungwa, ulifunguliwa kidogo kisha mtu akaingiza kichwa na kuchungulia.

Alikuwa ni yule msichana, basi ikabidi nimkatishe Ruqaiya kwa muda, kweli alinielewa na kukata simu. Eti yule msichana akaniuliza kama nipo peke yangu ndani, sikuelewa kwa nini ameniuliza hivyo, nikamjibu nipo peke yangu na kumkaribisha. Harakaharaka aliingia ndani na cha ajabu, alikuja kukaa pembeni yangu, jirani kabisa.

Kama mtu angeingia haraka, angeweza kudhani mimi na yeye ni wapenzi, mkononi alikuwa ameshika simu yake na ile chaja niliyompa.

“Simu yangu haiingizi chaji halafu nilikuwa naomba ukanisaidie kitu, unajua bado sijapanga vizuri vitu ndani kwangu kwani sina mtu wa kunisaidia, leo nimekuona upo nyumbani nimefurahi,” alisema huku akinitazama kwa macho fulani hivi, na mimi nikawa namtazama huku nikimuitikia kwa kutingisha kichwa tu kwani akili zangu zilishaanza kuhama.

Moyoni nikawa najisemea ‘hawa wanawake’ wataniua sasa, yaani hata sipati muda wa kupumzika! Basi nilimuuliza anataka nimsaidie nini, akaniambia kwanza anataka nikamchomekee simu yake kwenye chaji kule ndani kwake halafu nimsaidie na kupanga baadhi ya vitu.

Kitu kisicho cha kawaida kilitokea, kwa kuwa nilikuwa nimejifunga taulo tu, kitendo cha kuendelea kutazamana naye kihisia, kilisababisha ‘Ashrafu’ aamke tena kwa fujo na kwa kuwa hakukuwa na kizuizi, yule msichana aliweza kuona kila kitu, akawa ni kama ameshtuka hivi na kujiziba usoni eti ili asione kilichotokea.

Hata sijui nilipata wapi ujasiri kwa mtu ambaye hatujazoeana, nilimgusa shingoni na kumsogeza kwangu, naye bila kikwazo chochote akasogea mzimamzima, nikajisemea ‘liwalo na liwe’, nikamkubatia kwa nguvu huku mikono yangu ikienda moja kwa moja kwenye ‘chura’ wake, akashtuka kidogo na kuanza kunitazama kwa macho ya kurembua.

“Unataka kuni..fanya ni..ni,” aliuliza kwa sauti ya kudeka kama mtoto mdogo.



.

Sikumjibu kitu, nikamsogeza zaidi na kugusanisha ndimi, tukawa tunawaigiza njiwa wanavyoyalisha makinda yao. Khazija alikuwa mtundu sana, yaani ilionesha wazi kwamba alikuwa mtoto wa mjini kwani alikuwa akijinyonganyonga kama chatu aliyemeza mbuzi na kuzidi kunipandisha mizuka.

Sijui alifanyaje, nikashtukia lile taulo limedondoka, akajikunja kama mwanasarakasi na kuikamata ‘microphone’, akaipeleka usawa wa mdomo na kuanza kurap kwa staili ya kufokafoka huku akiwa ameishika kwa mikono yake yote miwili.

Huwezi kuamini, mimi huwa mgumu sana kupiga kelele tuwapo kwenye sanaa hiyo ya kikubwa lakini umahiri wake ulinifanya nishindwe kujizuia na mimi nikawa namfuatisha anavyorap, sauti yangu ilikuwa ikizidi kuongezeka kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.

Waliosema kila mjanja na mjanja wake hawakukosea, Khazija alikuwa mjanja wangu, ndani ya dakika chache tu za kupasha misuli, tayari alikuwa ameshaibuka mshindi kwa sababu mambo aliyokuwa ananifanyia ama kwa hakika yalikuwa mageni kabisa.

Kuna wakati alikuwa anarap mpaka anailamba ‘microphone’ upande wa nyuma, nyaya za kupeleka sauti kwenye spika zinapoanzia, basi nikajikuta macho yanapoteza utulivu wake, yakawa yanazunguka kama goroli, mdomoni nikawa kama natafuna ‘bablish’ wakati ukweli ni kwamba hakukuwa na chochote, nilikuwa nimepatikana.

“Shhh!” alisema Khazija huku akinioneshea ishara ya kuacha kupiga kelele, nadhani mayowe niliyokuwa napiga sasa yalikuwa yamekolea kiasi cha kumfanya hata yeye awe na hofu.

Ilibidi harakaharaka niinuke na kwenda kuongeza sauti ya redio, nikaufunga mlango vizuri kwa ndani ili kusitokee usumbufu wa aina yoyote.

Niliporudi kwa Khazija, tayari alikuwa ameitoa ile ‘pensi nyanya’ aliyokuwa ameivaa na sasa alikuwa akimalizia kuitoa blauzi. Kwa sababu ya udogo wa kifua chake, wala hakuwa na ulazima wa kuvaa ‘bra’, kwa hiyo alipomaliza alikuwa saresare na mimi, mimacho ikanitoka nikiwa ni kama siamini nilichokuwa nakiona mbele ya macho yangu.

Khazija alikuwa na umbo zuri mno, nikawa namtazama kuanzia juu mpaka chini, mimate ikawa imenijaa mdomoni kwa uchu. Yaani usingeamini kama ni mimi ndiye ambaye muda mfupi uliopita nilikuwa ‘msambweni’ na mama mwenye nyumba mpaka mwenyewe akaomba ‘poo’.

Alitembea kwa maringo huku akijitingisha na kunisogelea pale nilipokuwa nimesimama, nikaendelea kubabaika mwenyewe, ‘Ashrafu’ akiwa amefura kwa hasira na kuongezeka ‘saiz’.

Basi alinishika mkono na kunielekeza nini cha kufanya, basi nikawa namfuata kama kondoo anayepelekwa machinjioni.

Chumba kilikuwa changu lakini nilikuwa kama mgeni, akanipeleka mpaka chumbani na kunitaka nilale kifudifudi, hata sijui ilikuwajekuwaje, nikashtukia amekamata ‘microphone’ tena na kuanza kuimba ila safari hii hakuwa akirapu bali alikuwa akiimba nyimbo za taratibu zilizonifanya niwe najinyonganyonga kama nacheza ‘mabreka’.

Nikiwa nimeshakolea kisawasawa, alimkamata ‘Ashrafu’ aliyekuwa amefura kisawasawa na kumuelekeza njia ya kupita, raha niliyoisikia ilinifanya niwe nataka kufumbua macho lakini muda huohuo nataka kuyafumba, kwa hiyo yakawa hayajafumbuliwa wala hayajafumbwa, hebu vuta picha!

Nadhani na yeye aligundua kwamba alikuwa amenipatia kisawasawa, akawa ni kama anaendesha baiskeli hivi, kwa mara nyingine nikajikuta naanza kubwabwaja kwa sauti ya juu, hata sijui nilikuwa nazungumza nini ila ninachojua ni kwamba nilikuwa natoa sauti.

Alipoona nimezidiwa, naye aliongeza kasi, basi akili zangu zikawa nusu zipo eneo la tukio na nusu nyingine sijui ziko wapi, nikawa naweweseka tu na haukupita muda, tayari nilishaanza kuiona theluji juu ya Mlima Kilimanjaro, nikaongeza kasi ya kukwea juu na sekunde chache baadaye, tayari nilishakuwa juu kabisa ya kilele.

Kumbe kile kitendo cha kuongeza kasi Khazija hakukitegemea, kwa hiyo kikamfanya na yeye aongeze kasi ya kuifuata ile theluji kule kileleni na katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea, wote tulifika kwa wakati mmoja, mimi nikatoa sauti nzito na yeye akapiga ukelele fulani ulioleta raha ya ajabu masikioni mwangu, nikajitupa pembeni na haukupita muda, nilianza kuhisu usingizi mzito kuliko kawaida.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Muda huohuo nilimsikia Khazija akiinuka na kuchukua nguo zake, baada ya muda kidogo nikasikia mlango ukifunguliwa, sikumbuki nini kiliendelea lakini nilikuja kuzinduka baadaye sana na kujikuta nimelala peke yangu pale kitandani.

Niliinuka nikiwa nimechoka sana, harakaharaka nikachukua taulo na kujifunga kiunoni, nikatoka sebuleni na kukuta msosi umewekwa pale mezani na bila hata kuuliza, nilijua lazima umetoka kwa mama mwenye nyumba.

Sikumbuki alileta saa ngapi lakini kwa kuwa ulikuwa kwenye ‘hotpot’ bado ulikuwa wa motomoto.

Kwa jinsi nilivyokuwa na njaa niliufakamia harakaharaka na ndani ya muda mfupi tu, vyombo vilikuwa vitupu, nikashushia na glasi mbili za maji kisha nikatoka na kwenda bafuni kuoga. Angalau sasa nilirudiwa upya na nguvu lakini kuna kitu cha tofauti nilikuwa nakisikia ndani ya mwili wangu.

Nilikuwa mwepesi sana, yaani kuna wakati nilikuwa nahisi kwamba hata upepo mkali ukija unaweza kuniangusha. Nilijizoazoa mpaka ndani, nikajilaza pale sebuleni na kuwasha runinga, nikawa naendelea kutazama huku akili zangu zote zikiwa kwa mtoto Khazija.

Japokuwa jana yake nilikuwa naamini kwamba Ruqaiya ni mwanamke wa kipekee sana ambaye sijawahi kukutana na mtu kama yeye maishani mwangu, Khazija alikuwa ni habari nyingine! Tofauti yao ni kwamba Ruqaiya alikuwa na ile ladha ya asili wakati Khazija yeye alikuwa ‘fundi’ kwelikweli.

Kila nilipokuwa navuta picha jinsi alivyonipelekesha, nilikuwa naishia kucheka mwenyewe, nikawa nakarudiarudia kale kamsemo ka wahenga kwamba kila mjanja na mjanja wake.

Kwa kuwa watoto wa mama mwenye nyumba walikuwa wamesharudi shuleni, nadhani mwenyewe alishindwa kuja kuvifuata vyombo vyake, kwa hiyo nilichokifanya nilivichanganya na vyombo vyangu na kuvitoa nje, nikaviweka kwenye karo la vyombo.

Nilirudi ndani na kukaa mkao wa kutazama kwenye mlango wa Khazija, nilitaka japo nimuone tu sura yake ili roho yangu ifurahi kwa sababu alikuwa ameniweza kisawasawa lakini huwezi kuamini mpaka giza linaanza kuingia, sikumuona.

Nilitamani kwenda kugonga mlango wake lakini moyo ukawa unasitasita kwa sababu kiukweli kila mtu angenishangaa.

Japokuwa nilikuwa napigiwa sana simu siku hiyo kuanzia na Salma, Madam Bella, Ruqaiya na Nancy, wote nilikuwa nawajibu kimkatomkato isipokuwa Ruqaiya peke yake, muda wote macho yangu yalikuwa kwenye mlango wa Khazija.

Muda ulizidi kuyoyoma, kwenye majira ya kama saa tatu hivi, nilisikia mlango wa chumba cha Khazija ukifunguliwa, harakaharaka nikainuka na kufungua pazia, nikamuona akitoka.

Nilifungua mlango wangu harakaharaka na kutoka nje.

“Jirani vipi, naomba nipitishie chaja yangu,” nilizuga kwa sababu nilijua lazima mama mwenye nyumba na wapangaji wengine wanatusikia, basi alipomaliza kufunga mlango wa chumba chake, akaja mlangoni kwangu.

Alikuwa amejipodoa na kupodoka kisawasawa, kinguo alichokuwa amevaa, kigauni fulani hivi chenye rangi za kung’aa, kilimfanya aonekane kama malaika, ukizingatia na ile shepu yake ya kukata na shoka, alipendeza mno na uzuri wake kuongezeka maradufu.

Yote tisa, kumi alikuwa akinukia sana na begani alikuwa na mkoba mdogo wa kisasa.

“Umependeza sana jamani,” nilimwambia, akanijibu kwa kifupi ‘ahsante’.

“Wapi mida hii?”

“Naenda kwa rafiki yangu, ana bethidei yake.”

“Wapi?”

“Masaki.”

“Nikusindikize?”

“Hapana, tutaonana kesho.”

“Kesho? Ina maana hurudi leo?”

“Hapana, mpaka kesho,” alisema huku akigeuka na kuanza kutembea kwa maringo kuelekea getini, huwezi kuamini kwa mara ya kwanza nilijisikia wivu wa kupindukia kwenye moyo wangu, nikatamani nimfuate lakini nikaona nishai, nikabaki nimeduwaa tu pale mlangoni kama msukule. Mara nikasikia mlango wa mama mwenye nyumba ukifunguliwa.





“Vipi ulikuwa unaongea na nani?”

“Huyu dada mgeni alikuwa ananiomba nifunge mlango anatoka,” nilimdanganya mama mwenye nyumba, akasogea mpaka getini na kuhakikisha kama kweli ametoka.

“Mbona sasa hujafunga?”

“Nilikuwa nataka kuja kufunga ndiyo nikakusikia unafungua mlango,” nilizidi kuutetea uongo wangu, akaufunga mlango na kunisogelea.

“Mtoto mshenzi huyu, anaenda kwenye biashara zake saa hizi kurudi mpaka asubuhi!”

“Biashara gani?”

“Hee! Kumbe hujui... anafanya biashara ya kujiuza pale Kona, Sinza Afrika Sana, kila siku asubuhi mimi ndiyo namfungulia mlango, alisema mama mwenye nyumba, moyo ukanilipuka paah! Japokuwa kulikuwa na baridi, kijasho chembamba kilianza kunitoka.

“Changudoa?” niliuliza nikiwa ni kama siamini.

“Ndiyo, hawa wasichana wa siku hizi mchana ukimuona utadhani mtu wa maana kweli, ngoja giza liingie,” alizidi kushindilia msumari mama mwenye nyumba.

Hata sikumbuki tuliagana naye vipi, nilikuja kujikuta nimekaa sebuleni nikiwa nimejikunyata, mawazo tele yakipita ndani ya kichwa changu.

Pamoja na ujanja wangu wote, hakuna kitu nilichokuwa nakiogopa kama kutoka na machanguoa, kibaya zaidi ni kwamba nilipokutana na Khazija nilikuwa nimeuza mechi. Niliingia mzimamzima bila tahadhari yoyote.

Kama umewahi kupiga gemu na mtu halafu baadaye ukaanza kuwa na hofu kuhusu usalama wako, unaweza kuelewa ni hofu kiasi gani niliyokuwa nayo. Nilibaki nikiwa nimejikunyata kwa muda mrefu, yaani nimekaa tu! Sitazami runinga wala sisikilizi redio, muda wote natetemeka tu.

Mpaka inafika saa saba za usiku, nilikuwa nimekaa tu pale sebuleni, mawazo mengi yakiendelea kukisumbua kichwa changu. Nilikuwa nikipiga picha jinsi nitakavyokonda, jinsi nitakavyokuwa nakohoa na kutokwa na madonda mwili mzima. Hakika yajayo yalikuwa yakitisha.

Hata sijui nilipitiwa na usingizi saa ngapi, nilipokuja kuzinduka ilikuwa ni tayari saa kumi na mbili alfajiri na kilichoniamsha ni baada ya kusikia mlango wa geti ukifunguliwa, nikakurupuka na kusogea dirishani, nikawa nachungulia nje.

Kweli alikuwa ni Khazija, alikuwa akitembea kwa kuyumbayumba, mkononi akiwa ameshika chupa ya pombe kali. Nilimuona mama mwenye nyumba akipita haraka na kurudi kwake, Khazija akawa anahangaika kufungua mlango wa chumba chake.

“Kwa nini umeniua Khazija? Kwa nini? Why?” nilijikuta nikijisemea huku machozi yakianza kunitoka, donge kubwa lilinikaba kooni, machozi yakawa yanamwagika kwa wingi na kuulowanisha uso wangu.

Niliona kama nitaendelea kukaa ndani naweza hata kuchukua uamuzi wa kujidhuru, nikaona bora nijiandae na kwenda kazini labda kidogo nitachangamka. Basi nilitoka na kwenda bafuni kinyonge, nikajimwagia maji huku nikiendelea kuumia mno ndani ya moyo wangu.

Nilijikuta namchukia sana Khazija na nikajiapiza atakapokuja kunishibokea tena, naweza hata kumtia makofi.

Nilirudi ndani na kujiandaa, muda mfupi baadaye nikatoka kimyakimya, sikutaka hata mtu yeyote anione, nafsi yangu ilikuwa inanisuta mno na nikiri kwamba sijawahi kuwa kwenye majuto kwenye moyo wangu kama kuanzia nilipopewa taarifa kwamba Khazija ni changudoa.

Kwa kawaida kila ninapoondoka kwenda kazini nawasalimu majirani zangu, washkaji na watu wote ninaowafahamu lakini siku hiyo tangu natoka ndani mpaka nafika kituoni, sikuwa nimemsemesha mtu yeyote, muda wote nilikuwa natembea huku nimeinamisha kichwa chini, machozi yakinilengalenga.

Hakuna kitu nilichokuwa nakiogopa kama kufa kwa Ukimwi, nikawa natamani kila kilichotokea kiwe ndoto. Nilijuta kumfahamu Khazija na kubwa zaidi nilijuta mno kumvamia mtu nisiyemjua, tena bila kutumia kinga.

nilipofika kazini, ilibidi kwanza nitafute sehemu na kutulia kabla sijapanda ngazi kuelekea juu ofisini, kwa sababu nilikuwa na hali mbaya sana. Nilinunua maji na kunawa usoni ili hata mtu akinitazama asijue kwamba nilikuwa nalia.

Baada ya kuhakikisha nipo sawa, nilipanda ngazi mpaka juu, mtu wa kwanza kukutana naye alikuwa ni Salma wa mapokezi. Aliponiona tu, aliacha kila kitu alichokuwa anafanya, akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu huku akinibusu shingoni.

“Kwa nini hupatikani hewani? Halafu hata ukiwa unapatikana mbona unakuwa mzito kupokea simu zangu?” Salma aliniuliza kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba na upole, tofauti kabisa na jinsi alivyokuwa siku zote.

“Bado naumwa, nimejikaza tu kuja kazini!”

“Ooh! Maskini pole, hata uso wako unaonesha unaumwa,” alisema huku akiniachia, mwili wangu wote ukabaki na harufu ya pafyumu aliyokuwa amejipulizia. Sikuzungumza naye mambo mengi, nikapita na kwenda ofisini kwangu.

Bado kazi nilizoziacha zilikuwa palepale, kompyuta kadhaa zilizokuwa zinahitaji marekebisho, simu za ofisi na vifaa vya kuunganishia intaneti, vyote vilikuwa vinanisubiri. Nikaweka begi langu sehemu yake na kuchukua vifaa vyangu vya kazi. Niliamua kuelekeza nguvu kwenye kazi nikiamini nitasahau majanga niliyokuwa nayo.

Niliifungua kompyuta ya kwanza na kuanza kuitengeneza, nilibadilisha ‘hard drive’ na kuweka nyingine mpya, nikarekebisha na vitu vingine muhimu kisha nikaichomeka kwenye umeme, nikaiwasha lakini haikuwaka.

Nilirudia kuikagua tena na tena, nikarekebisha kila nilichokuwa nadhani ndiyo tatizo lakini kila nilipokuwa naiwasha, bado ilikuwa ikigoma. Nikaachana nayo na kuanza kuitengeneza nyingine, nayo nikarekebisha kila kitu lakini nilipoiwasha, haikuwa ikiwaka.

Ni hapo ndipo nilipogundua kwamba kichwa changu hakipo sawa kwa sababu kwa jinsi nilivyobobea kwenye masuala ya teknolojia ya mawasiliano, hata kama kompyuta ni mbovu kiasi gani, ikishafika kwangu lazima itapona. Nilivyoona kompyuta zote mbili zimenishinda, niliamua kuachana nazo, nikawa nafanya kazi nyingine.

Niliingia kwenye website ya kampuni na kuanza kukagua baadhi ya mambo kama ilivyokuwa kawaida yangu, vitu vingi havikuwa sawa na kila nilichokigusa kwa lengo la kurekebisha, nilijikuta nazidi kuharibu, nikaamua kuachana nayo.

“Sasa nitafanya kazi gani leo?” nikiwa nado najiuliza, simu ya mezani iliita. Nilipoipokea alikuwa ni Salma, akaniambia bosi ananiita ofisini kwake, nilishusha pumzi ndefu na kujifuta jasho, nikaacha kila kitu na kwenda mpaka ofisini kwa Madam Bella.

Nilipofungua mlango tu, aliacha kila alichokuwa anakifanya na kusimama, akaja mbiombio na kunikumbatia kwa mahaba, tukagusanisha ndimi zetu huku mikono yake ikifanya utalii wa ndani kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wangu.

“Nimekumiss jamani mume wangu,” alisema baada ya kuniachia, akanibusu tena na kunikaribisha kiti.

“Mbona umepooza namna hiyo, tatizo nini?” alisema Madam Bella huku akinikazia macho, nikamuungia humohumo kwamba nilikuwa naumwa sana na kwamba nimejilazimisha kuja kazini.

“Pole mume wangu, nakuona kabisa hauna furaha! Basi we nenda tu kapumzike, tutawasiliana baadaye, nikitoka naweza kuja kukuona nyumbani mgonjwa,” alisema Madam Bella, akanibusu mdomoni na kuifuata pochi yake. Alitoa noti tano za shilingi elfu kumikumi na kuniwekea kwenye mfuko wa shati, akanibusu tena.

Nilimshukuru na kutoka, nikaenda ofisini kwangu na harakaharaka nilichukua begi langu na kutoka mpaka mapokezi. Nikamuaga Salma ambaye alibaki ananishangaa.

“Naenda hospitali, nisije nikakufia bure,” nilimtania, akacheka na kunibusu kwa mbali, nikateremka kwenye ngazi na muda mfupi baadaye nilikuwa nimeshafika chini.

“Ebwana kuna mgeni wako anakutafuta kwelikweli.”

“Nani?”

“Yule dada uliyekuwa naye siku ile mkakaa pale, anasema hupatikani hewani kila akikupigia,” alisema mlinzi.

“Dah! Yuko wapi kwani?”

“Yule amekaa pale mlipokuwa mmekaa siku ile, tena naona amekuona maana anasimama,” alisema mlinzi, nikageukia kule alikokuwa ananionesha. Alikuwa ni Nancy, nilimfuata na kuzungumza naye juujuu, nikamwambia naumwa sana na naenda hospitali.

Kwa jinsi uso wangu ulivyobadilika, kweli aliamini naumwa, akataka anisindikize lakini nilimkatalia, nikaondoka huku akionesha wazi kwamba hakufurahishwa na nilichokifanya. Niliingia kwenye Bajaj na kumuelekeza dereva sehemu ya kunipeleka.

“Nipeleke Muhimbili.”

“Hospitali au?”

“Ndiyo,” nilisema huku nikishusha pumzi ndefu. Niliamua liwalo na liwe, lazima nikapime nijue mbivu na mbichi.



..

Basi tulielekea mpaka Muhimbili, kwa kuwa sikuwa nimewahi kwenda kupima ‘ngoma’ sehemu yoyote, hata sikuwa najua utaratibu ukoje, ikabidi niende mpaka kwenye jengo la ‘emergency’.

“Samahani nesi, naomba kuuliza.”

“Bila samahani, halafu wewe kama nakujua vile? Wewe si unaitwaa... unaitwaa...” alisema nesi niliyemsimamisha na kutaka kumuuliza kuhusu taratibu za kupima Virusi vya Ukimwi, akawa anajaribu kunikumbuka jina langu.

Kiukweli sikuwa namjua na sikukumbuka kama nimewahi kukutana naye mahali, basi akawa anahangaika kukumbuka jina langu. Alinikata sana ‘stimu’ kuniambia kwamba ananijua kwa sababu kama alikuwa ananijua, hata nitakapomueleza kilichonipeleka pale maana yake lazima atafuatilia majibu kutaka kujua kama ninao au la!

“Sasa akijua kama ninao si atanitangaza huyu?” nilikuwa nikijiuliza huku nikimtazama machoni akijaribu kukumbuka jina langu.

“Baada ya kuona ameshindwa kabisa kunikumbuka, aliniuliza swali ambalo lilinifanya niamini kama kweli ananijua.

“Si unaishi Tandale wewe?”

“Ndiyo.”

“Unamfahamu Jemima?”

“Aah! Jemima tena, nitaachaje kumfahamu mke wangu wa zamani?”

“Kwani mlishaachana? Mimi naitwa Penny, rafiki yake Jemima.”

“Aah! Unajua tena pilikapilika za maisha zinatutenganisha,” nilibabaika kwa sababu ukweli ni kwamba Jemima alikuwa miongoni mwa wasichana ambao nilivunja sana mioyo yao.

Huyu alikuwa mpenzi wangu wa kwanzakwanza wakati natoka chuo na kuyaanza maisha ya kujitegemea na huyu nesi aliyekuwa amesimama mbele yangu, sasa nilikuwa nimemkumbuka.

Alikuwa rafiki yake mkubwa Jemima, kipindi hicho wote wawili wakiwa wanasomea unesi na kuna siku aliwahi kuja naye nyumbani kwangu usiku na kumtambulisha kwangu. Sikuweza kumkumbuka kwa sababu kwanza siku hiyo nilikuwa nimelewa sana.

“Umeacha pombe siku hizi?”

“Nimeacha, mimi na pombe wapi na wapi?”

“Lakini mbona kama umekonda na kuchakaa kiasi hicho? Kwani unaishi na nani siku hizi?” alizidi kunidadisi maswali yaliyozidi kunichanganya kichwa.

“Eh! Mpaka nimesahau kama unataka kuniuliza kitu naona nimenogewa kukuuliza maswali. Ulikuwa unasemaje shemeji yangu wa zamani? Kwa nini lakini umeachana na Jemima?” aliniuliza huku bado akiendelea kupachika swali juu ya swali.

Miongoni mwa vitu ambavyo huwa sivipendi, ni mtu kuanza kunihoji kuhusu maisha yangu bila kuangalia tupo kwenye mazingira gani.

Dakika chache tu nilizosimama na msichana huyo, alikuwa ameniboa vya kutosha na japokuwa mwanzo nilikuwa naficha hisia zangu, safari hii niliweza kumuonesha waziwazi kwamba sipendezwi na maswali yake.

“Aah! Basi kuna mtu nilitaka kukuulizia habari zake lakini nimeshamuona, bye!” nilisema huku nikigeuka na kuanza kupiga hatua ndefundefu, hata sikuwa naelekea wapi ndani ya hospitali hiyo ya Muhimbili kwa sababu sikuwa mwenyeji.

Nadhani bado alikuwa hajatosheka, akanikimbilia na kunisimamisha, nikamgeukia huku nikiwa nimekunja ndita.

“Mbona umekasirika?”

“Mwenzio nina mgonjwa nimekuja hapa kwa matatizo lakini wewe hujali unachojua ni kunisanifu tu.”

“Aah! Jamani basi nisamehe mbona sikuwa na lengo lolote baya,” aliniambia kwa sauti ya upole, sikutaka hata kumtazama usoni, akaingiza mkono mfukoni na kutoa simu yake ya kisasa kwenye gauni la kazi alilokuwa amevaa.

“Naomba nitafute baadaye kama hutajali, naona sasa hivi haupo sawa,” alisema kwa upole huku akinitazama machoni, nikaichukua simu harakaharaka na kuandika namba yangu kisha nikamrudishia.

“Nisamehe bwana kama nimekuudhi, nna zawadi yako baadaye naomba nikikupigia simu upokee,” alisema huku akigeuka, nikabaki kumtazama.

Japokuwa alikuwa amevaa yunifomu, ‘nundu’ kubwa iliyokuwa imechomoza upande wa nyuma haikuweza kujificha, nikajikuta navutiwa kuendelea kumtazama.

Akawa anatembea harakaharaka na ni kama alijua kwamba namtazama kwani alipofika mbele kidogo, aligeuka, akanibamba nikiwa namkodolea macho, akacheka na kupotelea kwenye kundi la wagonjwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Kwa sekunde chache zile chache nilijikuta nasahau kwa muda kilichonipeleka hospitalini hapo, nikashusha pumzi ndefu na kuanza kujiuliza sehemu ya kuanzia kwa sababu tayari alishanipotezea ‘taiming’. Nilitamani nimuite na kumwambia ile namba niliyompa nilikuwa nimekosea namba moja kwa makusudi lakini sikuupata muda huo.

Ilibidi niende mpaka kantini kuzuga nikiwa najipanga upya sehemu ya kuanzia, nilipanga nikikutana hata na mlinzi nimuulize sehemu ya kupima Ukimwi. Wakati nikielekea kantini, nilishtuka nikitokea mbele ya kundi kubwa la watu ambao wengi walikuwa wakilia huku wengine wakiwa na huzuni kali, ilionesha kwamba wapo kwenye maombolezo.

Kumbe nilikuwa nimetokezea mochwari, kwa wale wanaofahamu vizuri mazingira ya Muhimbili, watakuwa wanaelewa kwamba mochwari inatazama na kantini ndogo, achana na ile kantini kubwa iliyopo nyuma ya jengo la Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Basi sijui kwa nini nilipowapita wale waombolezaji, nilianza kujiona eti na mimi ndiyo tayari nimeshaumwa sana na kukonda kutokana na Ukimwi na sasa mauti yameshanifika kwa hiyo ndugu zangu wapo msibani, kwenye msiba wangu.

Nilijikuta mwili ukitetemeka na kusisimka mno, yaani nilitamani kama siku zirudi nyuma nibadilishe kabisa tabia na kuacha kurukaruka hovyo na wanawake na hata pale inavyotokea hivyo, basi nisiuze tena mechi bali nivae kinga.

Mawazo ya hofu ya kufa kwa ngoma, yalinifanya niendelee kutembea kuifuata ile barabara inayopita kati ya mochwari na kantini, kuja kushtukia nilijikuta nikiwa kwenye geti la kutokea, nikawa najiuliza nimefikaje?

Akili nyingine ilinituma labda niondoke na kurudi nyumbani ili nijipange vizuri siku ya kuja kupima, akili nyingine ikawa inaniambia nikapime hivyohivyo, liwalo na liwe. Lakini mwili ulikuwa ukitetemeka sana nilipokuwa nikifikiria kwenda kupima, vilio vya wale waombolezaji vikawa vinaendelea kusikika kwenye masikio yangu.

Siku za nyuma nimewahi kuwa mtumiaji mzuri wa pombe lakini tatizo langu ni kwamba nilikuwa na kichwa kibovu kwelikweli, yaani bia mbili tatu kichwani zilikuwa zinanifanya nionekane kama nimekunywa kreti zima.

Nilichokuwa naamini ni kwamba pombe zinakupa ujasiri wa kufanya hata yale ambayo ukiwa macho makavu huwezi kuyafanya maana nakumbuka kuna siku nilikunywa na kujikuta namtongoza mwanaume mwenzake nikifikiri ni mwanamke kwani alikuwa mnene, sitasahau fujo zilizoibuka baada ya kitendo hicho.

“Ngoja nikapige bia mbili kwanza ili nipate ujasiri wa kwenda kupima,” niliwaza wakati nikitoka kwenye geti la Muhimbili, nikakatiza kwenye baa moja iliyokuwa jirani na hospitali hiyo.

Kwa kuwa ilikuwa ni siku ya kazi na pombe hazikuwa zikiruhusiwa kunywewa mchana, ilibidi muuzaji anifanyie njama za kuifunga kwenye gazeti na kunipa, akaniambia nikikamatwa yeye hahusiki, basi harakaharaka nikaanza kuigida bia ya kwanza huku bado nikiwa natetemeka.

Haukupita muda, nikawa nimeshaikata, akaniletea nyingine, nikawa naigida kwa kasi na ilipofika nusu, tayari mafaili yalikuwa yameanza kupandana kichwani. Hata sikumbuki kama niliimalizia hiyo bia ya pili au laa, na pia sikumbuki niliondokaje.

Baadaye nilijikuta nimeshafika kwenye kituo cha mabasi cha Faya, jasho likiwa linanitoka kwelikweli, nikawa najiuliza hivi tayari nimeshapima? Sikuwa na majibu. Na kama nimepima, hivi nimepewa majibu kweli? Pia sikuwa na majibu, nikaona isiwe kesi, ngoja nikapumzike kwanza nyumbani maana nilikuwa najihisi kama nimelewa sana.

Nilipanda kwenye daladala na nilipokaa kwenye siti tu, nilipitiwa na usingizi mzito. Nilipokuja kushtuka, tayari gari lilikuwa limefika Sinza kijiweni, kwa lugha nyepesi nilikuwa nimepitishwa kituo, nikashuka huku nikiwa napepesuka na kuingia ndani ya Bajaj, nikamuelekeza dereva kunipeleka nyumbani.

Kwa bahati nzuri alinielewa, tukaondoka mpaka nyumbani, nikamlipa kisha nikaingia ndani. Nilipofungua tu mlango na kuingia ndani, huku pombe sasa zikiwa ndiyo zimekolea kisawasawa, nilisikia mtu akinifuata kwa nyuma. Japokuwa nilikuwa na akili za pombepombe, nilikuwa kumtambua kwamba ni Khazija. Nilipomuona tu, nikaanza kuangua kilio.

“Kwa nini umeniua Khazija? Kwa nini umenipa ngoma?” alishtuka sana kusikia maneno hayo, akafunga mlango kwa funguo na kunisogelea pale kwenye kiti nilipojitupa huku nikindelea kulia kipombepombe.

“Umepatwa na nini wewe?”

“Niachee! Niacheee! Mwanamke muuaji sana wewe,” nilisema kwa sauti ya juu, akazidi kupigwa na butwa, hata sijui kilitokea nini lakini ninachokumbuka, nilimuona akivua kufuli lake. Sikuelewa tena kilichoendelea, nilikuja kushtuka na kujikuta nikiwa juu ya kitanda na Khazija. Hata sikumbuki nguo zangu zilitokaje mwilini.





“Unalia nini sasa, au hutaki nikupe?” aliniuliza huku akiniweka mkao mzuri wa kulamba asali, hata sikumbuki nilimjibu nini, nikajikuta tayari nimezama kwenye bahari ya kina kirefu, nikawa nafanya yangu huku nikiendelea kugugumia kwa kilio cha chinichini ambacho kadiri tulivyokuwa tukiendelea ndivyo kilivyokuwa kinazidi kushuka.

Unajua aliyesema mwanamke siyo mtu wa kushindana naye hakukosea kabisa, yaani kumbadilisha mwanaume mawazo ni jambo la sekunde chache sana, akijua kukupumbaza akili hata kama wewe ni mkuu wa majeshi unaweza kuiingiza nchi kwenye vita bila kutegemea ilimradi tu umfurahishe.

“Nani amekwambia kwamba mimi nimeathirika?”

“Ni mama mwenye nyumba, ameniambia eti wewe unajiuza,” niliropoka hata bila kufikiria mara mbilimbili madhara ya majibu niliyokuwa nampa, naye ni kama alijua kwamba nimefika kwenye kile wazungu wanachoita ‘a point of no return’, basi akaongeza mbwembwe huku akinipiga maswali mfululizo, na mimi nikawa namwaga tu mchele kwenye kuku wengi.

Mpaka kipyenga kinapulizwa kuashiria kumalizika kwa mpambano, nilikuwa nimesahau kabisa ile hofu kubwa niliyokuwa nayo ndani ya moyo wangu kwamba ‘nimeungua’, basi Khazija akawa anaendelea kunipetipeti huku akiniambia kwamba eti mimi ni dume la mbegu niliyekamilika kila idara.

“Lakini Khazija, hebu niambie ukweli mama, hivi kweli wewe huna ngoma?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni, hofu ikawa imeanza kurudi upya ndani ya moyo wangu. Basi Khazija alicheka kwa nyodo za kikekike na kunitazama usoni, akawa anajikaza kuzishinda aibu zake za kikekike.

“Hivi ukiniangalia nafanana na mwanamke anayefanya biashara ya ukahaba? Hivi ukiniangalia unaona nafanana na mtu mwenye Ukimwi?”

“Lakini wanasema huwezi kumtambua mwathirika kwa kumtazama kwa macho.”

“Wala usiwe na wasiwasi, mimi nataka tuongozane mguu kwa mguu mpaka hospitalini tukapime, najua umeshalishwa sumu ya hatari mpaka ukaamini kwamba mimi ni mgonjwa.

“Umenikosea nini mpaka nikuambukize virusi kwa makusudi? Au kwa sababu ‘nilijilengesha’ kwako ndiyo unanifikiria mimi ni mwanamke wa hovyo kiasi hicho?” alisema Khazija huku safari hii akiwa ‘siriasi’.

“Niliamua kujilengesha kwako kwa sababu nilikupenda, nakumbuka siku ya kwanza kukuona tulipishana pale dukani lakini sidhani kama wewe uliniona. Lakini pia nimekushuhudia zaidi ya mara tatu ukiwasulubu wanawake watatu tofauti, moyo ukawa unaniuma sana kwa sababu ya wivu.

“Isitoshe mimi ndiyo nilitakiwa niwe na hofu kama hujaniambukiza virusi kwa sababu ndani ya siku chache tu nimekufuma na wanawake watatu tofauti, tena mara zote ulikuwa ‘unauza mechi’ na kibaya zaidi kumbe huwa unakunywa pombe kama hivi, sasa ukilewa si utakuwa unawaparamia mabaamedi hovyohovyo?” alisema Khazija na kunifanya nishtuke sana.

Kikubwa kilichonishtua ni kauli yake kwamba amenishuhudia mara tatu nikiwa naivunjilia mbali amri ya sita na wanawake tofautitofauti, ikabidi nimhoji ili nipate uhakika.

“Mara tatu?”

“Ndiyo, unataka nikupe uthibitisho? Mara ya kwanza ulikuwa na dada mmoja mrefumrefu hivi amejazia ila hajanizidi mimi, mara ya pili ulikuwa na jimama fulani hivi jeupee na mara ya mwisho ulikuwa na mama mwenye nyumba, bisha tena,” alisema Khazija.

Nilishangaa sana kugundua kwamba kumbe alikuwa ananifuatilia bila mwenyewe kujijua, nikashindwa hata kuendelea kumtazama usoni na kujiinamia. Kwa maelezo yake hayo, ilionesha kwamba kumbe siku ile nilipokuja na Nancy pale nyumbani aliniona na alishuhudia kila kitu, siku nilipokuja na Madam Bella, bosi wangu pia alishuhudia kila kitu na kibaya zaidi kumbe ni yeye ndiye aliyekuwa akitupiga chabo wakati tukibingirishana na mama mwenye nyumba.

“Kama kweli unaogopa virusi kama ulivyokuwa unaniletea uchuro kwa kulia na kudai mimi ndiyo nimekuambukiza, unatakiwa kubadilisha mwenendo wako! Mungu amekujaalia zawadi ya kuwa ngangari kwenye sita kwa sita lakini hii inatakiwa iwe zawadi kwa mwanamke mmoja tu atakayekuwa mkeo na si kugusagusa kila mahali, mimi nakupenda ndiyo maana nakwambia maneno haya.”

“Kwani huwa ukiondoka usiku unaenda wapi?” nilijikakamua na kumuuliza, lengo likiwa ni kupata uhakika kama kweli nipo salama.

“Mimi nafanya kazi ya ‘customer care’ kwenye kampuni ya simu pale Mlimani City, naweza kuingia shift ya usiku hata wiki tatu mfululizo lakini mimi sijiuzi wala siwezi kufanya upuuzi huo, mshahara ninaolipwa unanitosha kuishi maisha yoyote ninayotaka, upo?”

Hiyo ndiyo kauli ambayo hasa nilikuwa naihitaji kutoka kwake, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama usoni huku katabasamu hafifu kakiwa kameanza kuchanua kwenye uso wangu. Kwa maelezo hayo, ile hofu yote niliyokuwa nayo ndani ya moyo wangu, iliyeyuka kama barafu iyeyukavyo juani.

Niliinuka na kwenda kuwasha redio, nikaweka CD ninayoipendaga, yenye nyimbo za kulalia na kuchagua wimbo wa George Michael uitwao Careless Whisper, nikabonyeza kitufe kwenye rimoti ili wimbo huo uwe unajirudia, nikarudi kitandani na kumvaa Khazija ambaye bado alikuwa akiendelea kutoa maneno mazuri ya kuniusia juu ya tabia yangu.

Kwa furaha niliyokuwa nayo, ya kuhakikisha kwamba kumbe hakuwa changudoa kama mama mwenye nyumba alivyoniaminisha, niliamua kuingia upya uwanjani, nikiwa na nguvu mpya, ari mpya na kasi mpya huku muziki laini uliokuwa ukipiga kwenye redio yangu kubwa ukizidi kunidatisha.

Akiwa anaendelea kuongea kwa upole, nilianza kumfanyia vituko vya hapa na pale na kusababisha kauli zake ziwe zinakatakata, haikuchukua muda tayari naye alishaanza kunionesha ushirikiano, safari hii ikawa zamu yangu.

Nilimuweka sawa, nikapitisha mikono yangu kwa nyuma yake na kuukamata mlima wake kwa staili fulani hivi ya kipekee sana, nikamuona akijikunjakunja kama nyoka aliyemeza mbuzi mzima, nikaweka mwiko kwenye chungu na kuanza kufanya kama nasonga ugali hivi!

Nadhani kilikuwa kitu kipya kabisa kwake kwani miguno aliyokuwa akiitoa haikuwa ya kawaida, akawa anahema kama anataka kuzama kwenye maji ya kina kirefu, basi nikazidisha mbwembwe huku nikimtazama usoni jinsi alivyokuwa akibadilikabadilika kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.

Ilifika mahali akaanza kuweweseka kama mtu aliyepo kwenye njozi, mara azungumze hili mara azungumze lile, basi ilikuwa ni tafrani ya aina yake.

Haukupita muda mrefu akatangaza kuiona theluji iliyopo juu kabisa ya Mlima Kilimanjaro unaoongoza kwa kupendwa na watalii, sikutaka kumchosha sana, na mimi nikaongeza spidi ya kukwea juu ya mlima na muda mfupi baadaye, na mimi niliiona theluji, nikamuachia na kila mmoja akadondokea upande wake.

Baada ya kama dakika kumi hivi kupita, aliinuka na kuja kunilalia kifuani kwangu, akazungumza jambo ambalo sikulitegemea kabisa kutoka kwake.

“Nataka unioe niwe mke wako! Mi nakupenda mwenzio na nakuahidi nitakupenda siku zote za maisha yako na nitakubadilisha, sasa hivi unahangaika hovyo na wanawake kwa sababu hujampata mtu anayeweza kukubadilisha,” alisema kwa hisia za hali ya juu huku akinibusu kila baada ya sekunde kadhaa.

Japokuwa wakati naingia nilikuwa nimelewa chakari, ‘dawa’ aliyonipa Khazija ilinifanya hata nisikumbuke kama nilikuwa nimekunywa. Nilibaki namkodolea macho nikiwa ni kama siamini kama kile alichokuwa anakisema kimetoka kwenye kinywa chake.

Nilieleza mara ya kwanza kwamba japokuwa nilikuwa na muda mfupi tangu nifahamiane na Khazija, alikuwa na uzuri fulani wa kipekee ambao ama kwa hakika ulikuwa ukinichanganya sana kichwa changu, hasa jinsi alivyokuwa amegawanyika nyonga yake na kubeba mzigo wa kutosha upande wake wa nyuma.

Sikuwa na malengo ya kuoa lakini kwa jinsi Khazija alivyokuwa amenichanganya kichwa changu kwa penzi motomoto alilokuwa ananipa, nilijikuta nikishawishika.

“Kwa hiyo unataka nikuoe?” niliuliza nikiwa hata sijui nataka kujibiwa nini kwa sababu tayari alikuwa amefunguka kila kitu.

“Nakupenda sana mwenzio, mimi ni mgumu sana kujirahisi kwa mwanaume, wapo watu walikuwa wanakuja kunifuata kazini na magari yao ya thamani lakini hakuna aliyewahi kunivutia lakini tangu nilipokuona wewe, nimejikuta nikikupenda na kuridhika mno na wewe, hata sijui moyo wangu utahitaji nini cha ziada nikiwa mkeo,” alizidi kulalama Khazija kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba yaliyotukuka.

“Lakini Khazija, mimi mwenzio nina... nina...” nilitaka kusema jambo lakini maneno yakawa yanaishia ndani kwa ndani, nilitaka ‘nimchane’ ukweli kwamba mwenzake sijatulia hata kidogo na sijui kama nitaweza kutulia japokuwa nilikuwa ‘nimemuelewa’ sana.

Kabla hata sijamalizia kauli yangu, alidakia juu kwa juu na kuniambia kwamba anajua kwamba sijatulia lakini amenipenda hivyohivyo na atahakikisha ananibadilisha. Aliposema hivyo, akili zangu zilienda kwa Ruqaiya, nikajiuliza kweli nawezaje kumuacha mwanamke kama yule? Yaani raha zote zile tulizopeana halafu ghafla eti nimwambie mimi na wewe basi, nimepata mchumba? Niliona ni jambo lisilowezekana.

Nilimfikiria Nancy, jinsi alivyokuwa akinipenda na kujituma kwa moyo wake wote kuhakikisha nafurahi, akafikia hatua mpaka ya kurudi nyumbani kwao usiku wa manane, naanzaje kumwambia mimi na yeye basi?

Yote tisa, kumi nilikuwa namfikiria bosi wangu, Madam Bella, nawezaje ‘kumchomolea’ kirahisi eti kisa nimepata mwanamke anayetaka tuoane na kuishi kama mume na mke?

“Haiwezekani!” nilijikuta nimetamka, Khazija akashtuka akiwa ni kama haamini alichokisikia.



“Haiwezekani! Haiwezekani kabisa,” nilisema kwa sauti ya juu huku nikiwa najitoa kwenye mikono yake, akazidi kupigwa na butwaa.

“Umepatwa na nini?”

“Sijapatwa na chochote, mimi sijajiandaa kuoa kwa sasa, kwanza mimi bado mdogo.”

“Hujajiandaa kivipi? Mdogo kwani una umri gani wewe?” Khazija alitaka kunibana kwa hoja lakini nazidi kumkwepa kwa kusisitiza kwamba sikuwa tayari kumuoa.

“Kwa hiyo nimefanya makosa kukupenda?”

“Hapana, siyo hivyo mpenzi wangu, wala hujakosea chochote na mimi napenda tuendelee kuwa wapenzi lakini hilo suala la ndoa naomba tuliache kwanza,” nilisema, nikamuona akibadilika, uso wake ukajawa na huzuni isiyoelezeka.

Ilibidi nianze kazi ya kumbembeleza Khazija, nikamwambia asiwe na wasiwasi sina lengo lolote la kumuacha bali nataka kwanza tufahamiane kwa kina kisha mambo mengine yote yatafuatia, kwa mbali nikamuona kama ameanza kuelewa ‘saundi’ zangu.

Basi siku hiyo aliniganda kuliko kawaida, ikawa kila baada ya muda mfupi ananipeleka ‘msambweni’ mpaka nikawa hoi bin taaban, hata sikumbuki nililala saa ngapi, ninachokumbuka nilikuja kuzinduka baada ya kusikia jogoo akiwika kuashiria mwanzo wa siku mpya, mapambazuko!

Nilishtuka kugundua kwamba sikuwa nimelala peke yangu, nilipogeuka pembeni yangu, nilimuona Khazija akiwa amelala fofofo, wote tukiwa watupu na tukiwa tumejifunika shuka moja. Nilijikuta nikitamani kumkumbatia Khazija, nikawa najiuliza ilikuwaje mpaka akalala na mimi? Hajaenda kazini usiku kama kawaida yake?

Nilipomkumbatia, ni kama na yeye alizinduka nusunusu kutoka usingizini, kwani naye alinikumbatia na kunibusu kisha akajilaza kwenye kifua changu. Baadaye aliamka, akanibusu kwa mahaba mazito na kuniuliza nimeamkaje, nikawa nachekacheka tu mwenyewe.

Usingeweza kuamini kwamba ndiyo mimi ambaye siku moja iliyopita nilikuwa nahaha, nikiwa nimekata tamaa kabisa na kuamini kwamba tayari nilikuwa nimenasa ‘ngoma’, kweli akili ya binadamu ina uwezo wa kusahau jambo kwa haraka sana.

“Umejisikiaje kulala na mimi mpaka asubuhi?”

“Nimejisikia poa sana, lakini naomba nikuulize, kwani jana hukwenda kazini?”

“Sikwenda kwa sababu nimeshamaliza shift yangu ya usiku, wiki yote hii nitakuwa naingia mchana,” alisema huku akijinyoosha, akaamka na kujifunga upande wa khanga, akaendelea kujinyoosha huku akipiga miayo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nilishindwa kuvumilia kumuona katika hali ile, nikamvutia kwangu na muda mfupi baadaye, tulikuwa uwanjani, tukapelekeshana puta na japokuwa asubuhi ile kulikuwa na kaubaridi fulani, wote wawili tulijikuta tukitokwa na kijasho chembamba.

Baada ya hapo, nilijikuta nikilala tena, nilipokuja kushtuka tayari ilikuwa ni kama saa tatu hivi za asubuhi. Haikuwa kawaida yangu kuchelewa kuamka kiasi hicho kwa sababu siku zote saa kumi na mbili nakuwa nimeshaamka lakini siku hiyo mpaka saa tatu asubuhi! Haikuwa kawaida yangu.

Nilipoamka, yeye hakuwepo pembeni yangu, nadhani alishaamka na kwenda kwake, basi nikatoka nikiwa na mswaki wangu, kiunoni nikiwa nimejifunga taulo, ile natoka tu nikakutana uso kwa uso na mama mwenye nyumba, akanikata jicho mpaka nikawa najiuliza ‘nimemkosea nini huyu mama?’.

Nilimsalimu lakini hakunijibu, nikaenda mpaka bafuni huku nikijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu. Nilioga na angalau mwili ukapata nguvu, wakati natoka, nilikutana na baba mwenye nyumba ambaye kimsingi huwa tunaheshimiana sana na hakuwepo hapo nyumbani kwa muda kwa sababu yeye ni mtu wa kusafirisafiri sana.

Alinichangamkia vizuri na nadhani alirudi usiku maana bado alionesha kuwa mchovu, basi nikaingia zangu ndani huku moyoni nikijisikia kuwa na hatia sana, nikawa najiuliza siku akigundua kwamba akiwa hayupo natia mkono kwenye chungu chake cha asali itakuwaje?

Akili nyingine ikawa inaniambia kwamba eti mimi sina kosa kwa sababu mkewe ananishobokea mwenyewe. Basi nilipoingia ndani tu, mara nilisikia mlango ukifunguliwa, kutazama alikuwa ni Khazija, mkononi akiwa na chupa ya chai na sahani ya vitafunwa, nikamkaribisha akaingia mpaka ndani.

Aliandaa chai, tukakaa na kuanza kunywa huku tukipiga stori za hapa na pale, nikajikuta nikizidi kumpenda. Tulipomaliza kunywa chai, Khazija alinisaidia kufanya usafi mle ndani kwangu kwa sababu huwa sina kawaida ya kufanya usafi mara kwa mara.

Nyumba ikabadilika na kuanza kuwa na hadhi katika suala zima la usafi, alitoka na kwenda kwake akiwa amebeba vile vyombo, muda mfupi baadaye akarudi akiwa na kitezo kilichokuwa na mkaa, akafungua kikopo kidogo kilichokuwa na udi maalum nasikia kutoa Uarabuni, akauweka juu ya mkaa kwenye kitezo na kufukiza chumba kizima, harufu ikabadilika.

Kiukweli sikuwa nimeyazoea kabisa mambo hayo, kwa kifupi mimi nimekulia bara na huko kwetu mambo kama hayo hayapo kabisa! Nimewahi kusikia kwamba maeneo kama Tanga, Pemba na Mombasa ndiyo kwenye mambo hayo ya kufukiza nyumba nzima marashi, ukiingia utadhani upo kwenye dunia nyingine ya tofauti.

Basi tulishinda na Khazija mpaka majira ya kama saa saba hivi ambapo aliniaga kwamba anaenda kazini, lakini tayari alikuwa ameshaniandalia chakula na kuniwekea kwenye ‘pot’, kabla hajaondoka tukaingia tena uwanjani ‘kuagana’ ambapo kama kawaida yake, alinitoa jasho kisawasawa.

Alipoondoka kwenda kujiandaa, nilijikuta nikitamani kwenda ndani kulala, nikainuka kichovu na kuingia chumbani, nilipojitupa kitandani, sikuamka mpaka ilipofika majira ya kama saa kumi na moja jioni na kilichoniamsha, ilikuwa ni njaa.

Haikuwa kawaida yangu kulala hovyo kiasi hicho, basi nikaamka na kwenda tena bafuni kuoga, nikakutana tena na mama mwenye nyumba lakini safari hii alikuwa amekaa na mumewe kwenye jamvi pale uani wakicheza karata.

Japokuwa alikuwa na mumewe lakini bado nilimuona akinitazama kwa macho yaliyobeba ujumbe wa mahaba mazito ingawa ilionesha wazi kwamba moto mkali wa wivu ulikuwa ukikiunguza kifua chake.

Nilioga na kurudi ndani harakaharaka, nikakaa na kuanza kuufakamia msosi alioniandalia Khazija. Nilichokigundua hata aina yake ya upishi ilikuwa tofauti kabisa kwani chakula kilikuwa kimewekwa viungo vilivyokifanya kiwe kizuri sana, nikajikuta nazidi kumpenda Khazija.

Ni mpaka nilipomaliza kula ndipo nilipoishika simu yangu na kuiwasha maana tangu jana yake nilikuwa nimeizima, meseji mfululizo zikaanza kumiminika. Nyingi zilikuwa ni za kutoka kwa bosi wangu, Madam Bella ambaye alikuwa akitaka kujua naendeleaje pamoja na meseji nyingine za kimapenzi.

Lakini pia zilikuwepo meseji za kutoka kwa Ruqaiya naye akitaka kujua naendeleaje, zilikuwepo nyingine kutoka kwa Nancy na kwa Salma, basi ilikuwa tafrani. Ndani ya muda mfupi tu simu yangu ilikuwa imeingia meseji karibu thelathini na muda huohuo ilianza kupigwa.

Wa kwanza alikuwa ni Ruqaiya ambapo nilipoona namba yake tu, uso wangu ulijawa tabasamu, nikapokea yake ambapo kitu cha kwanza alianza kunilaumu eti kwa nini namuweka roho juu kiasi hicho, meseji sijibu na simu haipatikani wakati naumwa. Kwa jinsi alivyokua akilalama kwa hisia nzito, nilijikuta nikitamani nimuone ili kama ni kunilaumu, anilaumu nikiwa namuona.

Kabla hata sijasema chochote, alianza mwenyewe kwa kuniambia kwamba anahitaji sana kuonana na mimi, nimuelekeze mahali popote alipo atanifuata. Nilijua nikisema nimlete nyumbani, naweza kugonganisha ‘magari’, nikamwambia nitajitahidi anikute Magomeni Kanisani, akaniambia anakuja muda si mrefu.

Nilipomaliza tu kuzungumza na simu, mara nilisikia mlango ukigongwa, niliinuka na kwenda kufungua, katika hali ambayo sikuitegemea, nilikutana uso kwa uso na Madam Bella ambaye naye alionesha kama amekuja akiwa na manung’uniko yake moyoni kwamba kwa nini sijamjibu meseji na hewani sipatikani, akaingia na kwenda kitandani moja kwa moja.







“Kwa nini unakuwa Mswahili kiasi hicho,” Madam Bella alianza kuwaka huku akisaula viwalo vyake, kimoja baada ya kingine. Sikutaka kuwa na maneno mengi kwani niliamini kwa shoo atakayoipata, mwenyewe atatulia na kunisamehe yote.

Nilimsogelea na kujifanya bado naumwa sana, akanidaka mzimamzima na kunivutia kwake, akanimwagia mvua ya mabusu huku akiniambia kwamba hapendi tabia yangu ya kutokuwa napokea simu anaponipigia.

Nilimdanganya kwamba nakunywa dawa kali sana kiasi kwamba nikishameza tu, napitiwa na usingizi ndiyo maana hata simu ikiita siisikii. Uongo huo ulionekana kumuingia kisawasawa, akanipa pole na kuniambia kwamba hata kama naumwa, anataka ‘nimvuruge’.

Tayari mwenzangu alishaonesha injini imeshachanganya, kilichotakiwa ni kuingiza gia namba moja ili safari ianze. Hata hivyo, tofauti kabisa na siku zote, kuna hali isiyokuwa ya kawaida ilikuwa inanitokea. ‘Mkuu wa kaya’ ni kama hakuwa na habari kabisa juu ya kilichokuwa kinataka kuendelea kwani hakuonesha ushirikiano kabisa.

Jambo hilo pia lilimshtua Madam Bella, ikabidi ajaribu kutumia mbinu zake ili kumrudisha mchezoni lakini ilikuwa ni kazi bure, aligoma kabisa.

“Una nini wewe?”

“Hata mimi sielewi.”

“Ulikuwa namwanamke humu ndani si ndiyo?”

“Mimiii?”

“Wewe ndiyo, kwa nini iwe hivi wakati mimi nakujua wewe ni mwanaume wa shoka?”

“Labda ni kwa sababu ya dawa ninazokunywa, wala usiwe na wasiwasi mambo yatakuwa mazuri.”

“Mambo yatakuwa mazuri saa ngapi bwana?” alisema huku akimvamia tena mkuu wa kaya na kujaribu kumfanyia kukurukakara lakini wapi... alikuwa amelala fofofo.

Kwa mara ya kwanza niliyaona machozi ya Madam Bella, alilia kwa uchungu, alinilaumu sana kwa kumfanyia ukatili wa kiasi kile, alilalama mpaka nikatamani nifanye kitu ili kumridhisha lakini sikuwa na namna.

Basi niliendelea kujitetea kwamba ni kwa sababu ya dawa lakini moyoni nilikuwa najua kilichotokea. Ni kweli muda mfupi uliopita nilikuwa na Khazija na kiukweli ni kwamba alinishughulisha sana, sasa nikawa nahisi pengine hali ile ndiyo iliyosababisha gari lishindwe kuwaka.

Madam Bella alisusa na kugeukia ukutani, akajilaza huku akiwa hataki kabisa kuzungumza na mimi. Mara simu yangu ilianza kuita, harakaharaka nikaichukua na kutazama namba ya mpigaji, alikuwa ni Ruqaiya na nadhani alikuwa akitaka kujua nimefikia wapi kama tulivyokubaliana.

Kiukweli sikuweza kuipokea, nilibonyeza kitufe cha kutoa mlio, nikaiacha iite mpaka ilipokata. Mara meseji ikaingia; Leo nimejiandaa kikamilifu, nimekunywa bakuli la supu ya pweza kwa ajili yako, kazi ni kwako!

Nilijikuta nikizidi kuchanganyikiwa, nikashusha pumzi ndefu na kuitoa simu mlio, nikaiweka chini ya mto na kuanza kutafakari ndani ya kichwa changu nini cha kufanya. Mara nilipata wazo la kutoka na kwenda dukani kwa Mangi ‘kubusti’ kama kawaida yangu.

“Naenda dukani mara moja, nikuletee nini?”

“Sitaki chochote,” madam Bella hakujibu chochote, nikajua kazi ninayo. Basi harakaharaka nilitoka na kwenda kwa Mangi, nikaagiza kinywaji ninachopenda kukitumia ili ‘kubusti’ mambo yetu yale, nikachukua na tangawizi, nikaitafuna nzimanzima mpaka machozi na kamasi vikawa vinanitoka.

Nilipojiona niko fiti, nilirudi nyumbani fasta, nikamkuta Madam Bella kajiweka kihasara pale juu ya kitanda, sikusubiri kuuliza, nikamvamia mzimamzima, ile kupiga ‘stata’ jino moja, gari likawaka.

Madam Bella naye hakutaka stori, alikamata kisawasawa na kuanza kuukwea mnazi kwa pupa huku akiendelea kunililia eti kwa sababu gani namnyanyasa. Sikumjibu chochote zaidi ya kuendelea kupiga mashuti ya mbali, akawa anatoa miguno ya hapa na pale iliyonizidisha munkari.

Hakuchukua raundi, akatangaza kuangua madafu mawili kwa mpigo, akanikamata kwa nguvu utafikiri tupo kwenye ule mchezo unaopendwa sana wa miereka. Aliponiachia, alijitupa pembeni kama mzigo na muda mfupi baadaye, alikuwa akikoroma.

Licha ya kufanikiwa kuitii kiu yake, bado nilikuwa na maswali mengi ndani ya kichwa changu juu ya kilichotokea, kwa nini hali kama ile inikumbe wakati haijawahi kunitokea hata mara moja? Mara nilisikia mlango ukigongwa, harakaharaka nikaamka na kwenda kuchungulia.

Mapigo yangu ya moyo yalishtuka mno baada ya kugundua kwamba alikuwa ni Khazija, mkononi akiwa na kisinia kidogo ambacho juu yake kilikuw ana glasi mbili za juisi. Kwa jinsi ilivyoonesha, moja ilikuwa yake na nyingine yangu, nikawa natetemeka nitafanyaje ili anielewe?

Basi nilijikaza kiume huku nikijiambia kuwa liwalo na liwe, nikafungua mlango. Nilitaka kuanza kumpanga Khazija lakini katika hali ambayo hata sikuitegemea, alinikatisha na kuniambia eti nisijali, anajua kwamba niko na mgeni na ndiyo maana ameniletea juisi glasi mbili.

Mwanzo nilikuwa nimetoa kichwa tu lakini mshangao ulinifanya niuachie mlango, akalitazama tauli nililokuwa nimelivaa huku akililazimisha tabasamu kwenye uso wake, akanikabidhi ule mzigo na kuondoka zake. Kiukweli nilijisikia vibaya kuliko kawaida, niliyahisi maumivu aliyoyapata Khazija kwenye moyo wangu.

Nilirudi ndani na kufunga mlango, nikaweka zile glasi mbili za juisi mezani, nikawasha runinga na kukaa, muda mfupi baadaye Madam Bella alitoka na kuja pale nilipokuwa nimekaa.

“Whaoo, umejuaje kama nahitaji juisi,” alisema huku akikaa na kuichukua glasi moja ya juisi, akaigida na alipoishusha chini, ilikuwa nusu. Nikazidi kujisikia vibaya ndani ya moyo wangu.

Basi tuliendelea na stori za hapa na pale, Madam Bella akaniambia kwamba alikuja mara moja kunijulia hali lakini ana ratiba ngumu siku hiyo, akanishukuru na kuniomba radhi eti kama alikuwa amenikwaza katika mazungumzo yake.

Moyoni nilikuwa nataka aondoke tu, basi nikawa najichekesha pale, akaenda kuoga na aliporudi, alivaa na kunitaka nimsindikize. Kabla hajatoka, alitoa bahasha iliyokuwa na noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi na kuniambia eti hizo ni kwa ajili ya juisi ya mgonjwa.

Nilimsindikiza mpaka mahali alipokuwa amepaki gari lake, akaingia na kunitaka na mimi pia niingie na kukaa upande wa pili, tukawa tunapiga stori za hapa na pale na katika mazungumzo yake, aliniambia jambo ambalo lilinishtua sana.

Aliniambia eti anataka nimuoe ili awe mke wangu halali, amechoka kuishi kwa kuibia penzi langu wakati anaamini nampenda sana na yeye ananipenda sana, akaniambia nilifikirie hilo kisha tutaonana kesho yake.

Alinibusu kimahaba mdomoni kisha nikateremka, nikamsaidia kumuongoza kutoa gari na muda mfupi baadaye, aliondoka huku akinipungia mkono. Nilirudi haraka mpaka nyumbani kwangu na kabla sijaingia, nilienda kumgongea Khazija, akafungua mlango kidogo na kuchungulia.

“Unasemaje?” aliniuliza huku akionesha kutokuwa tayari kuzungumza na mimi.

“Samahani naomba tuongee Khazija,” nilimwambia, akajifikiria kwa zaidi ya dakika nzima kisha akashusha pumzi ndefu na kufungua mlango, lakini akawa anakwepa nisimuangalie usoni.

Na mimi niliendelea kukazania kumuangalia usoni huku nikimsemesha, aliponitazama, nilijikuta nikimuonea huruma kupita kiasi, macho yake yalikuwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu sana kuonesha kwamba kumbe alikuwa analia, nikamsogelea na kutaka kumkumbatia lakini alikataa, nikatumia nguvu na kumkumbatia hivyohivyo, na yeye akanikumbatia huku akianza upya kuangua kilio.







“Kwa nini unanifanyia hivi lakini?”

“Nisamehe Khazija.”

“Unanipenda?”

“Ndiyo nakupenda.”

“Malengo yako ni nini kwenye maisha yangu?”

“Nataka nikuoe, nataka uwe mke wangu, mama wa watoto wangu,” nilijikuta nikiropoka huku nikiendelea kumbembeleza Khazija ambaye nikiri wazi kwamba alishaanza kuniingia moyoni.

Basi tulibembelezana pale kwa muda mrefu na mwisho tukajikuta tukiishia juu ya kitanda kikubwa kilichokuwa ndani ya chumba cha Khazija. Miongoni mwa vitu ambavyo Khazija alikuwa ananipatia, ilikuwa ni kwenye suala zima la mbinu na medani za aina yake tuwapo kwenye uwanja wa fundi seremala.

Nililigundua hilo kwa sababu muda mfupi tu uliopita nilikuwa nimetoka kuchoshana nguvu na Madam Bella, tena gari likawaka kwa mbinde kwelikweli lakini kwa Khazija ilikuwa tofauti kabisa. Mpaka kipyenga cha mwisho kinalia kuashiria kumalizika kwa mpambano, nilikuwa hoi bin taaban.

Nakumbuka kwa mara ya kwanza, nilishindwa kusimama kutokana na jinsi miguu ilivyokuwa inatetemeka huku mwili ukiwa umeishiwa kabisa nguvu. Basi harakaharaka akanirudisha pale kitandani na kunichanganyia ‘glucose’ kwenye maji na kuninywesha, kisha glasi ya juisi ikafuatia.

Nikiwa nimeanza kurejewa na nguvu zangu, yeye aliamka na kuanza kuandaa maakuli huku akinipigisha stori za hapa na pale. Nilikuwa nimefanikiwa kabisa kumuondolea huzuni aliyokuwa nayo ndani ya moyo wake, akawa ananihimiza kwamba nisirudie tena kumuumiza.

“Unajua kwetu Pemba kuna uchawi wa kumfunga mwanaume, ukiendelea na mambo yako itabidi nikakufunge maana nakupenda na nataka uwe wangu peke yangu,” alisema huku akiendelea kukaangiza.

“Unakuwaje huo uchawi!”

“Ukichepuka tu gari haliwaki, hata ufanyeje ila ukirudi ndani mambo yanakuwa safi,” aliniambia, nikashtuka sana kwa sababu ni kweli hicho ndicho kilichotokea nilipokuwa na Madam Bella na kama nisingefanya juhudi za ziada, huenda ningedhalilika.

Japokuwa mwenyewe alikuwa akizungumza kama masihara, tena akicheka, kwangu mimi niliona ‘nimepatikana’. Basi tuliendelea na mazungumzo na baadaye msosi ulipokuwa tayari, aliandaa, tukakaa mezani tayari kwa kula.

Kabla sijaanza kula, alianza yeye kunilisha kisha akanibusu! Kiukweli Khazija alikuwa anajua sana kunidekeza kiasi kwamba mpaka chakula kinaisha, sikutamani kutoka kurudi kwangu. Nilishasahau kama nina ‘appointment’ na mtu muhimu sana, Ruqaiya.

Huwezi kuamini, tuliendelea ‘kubebishana’ na Khazija mpaka usiku na kilichokuja kunishtua ni baada ya kugundua kwamba sikuwa nimefunga mlango wangu.

Khazija naye alivyo mjanja, akaniambia nimuelekeze ataenda kufunga mwenyewe, kidume nikalainika, akaenda kufunga harakaharaka na muda mfupi baadaye alirejea akiwa na funguo zangu.

Kilichoendelea hata sikumbuki ni nini lakini nilipokuja kuzinduka, tayari kulikuwa kumepambazuka, nikiwa juu ya kitanda kimoja na Khazija, tukiwa tumejifunika shuka moja na msichana huyo mrembo ambaye kiumri alikuwa ‘saizi yangu’.

Waliosema kwamba mchovya asali hachovyi mara moja, hawakukosea. Kwa Khazija ni kama nilikuwa nimechovya asali, huwezi kuamini kwamba siku iliyofuatia sikuwa na habari na kazi wala simu yangu, nilishinda kutwa nzima nikiwa ndani na Khazija!

Naye alikudanganya kazini kwao kwamba anaumwa kwa hiyo muda pekee aliotoka ulikuwa ni wa kwenda kununua vitafunwa pamoja na mboga, baada ya hapo tulijifungia kutwa nzima ndani.

Jioni majira ya kama saa kumi na mbili, ilibidi nitoke nikaangalie kama ndani kwangu kulikuwa salama, nikamuacha Khazija akiwa amejilaza kitandani. Ile natoka tu, niligongana macho na mama mwenye nyumba, akaachia msonyo mmoja mkali sana.

“Kuna nini kwani mke wangu,” sauti ya mumewe aliyekuwa ndani ilisikika, nadhani alishtuka kumsikia mkewe akiachia msonyo, akamdanganya kwamba eti kuna kitu kilikuwa kimemkwaza huku akijifanya hana habari na mimi.

Sikumjali, nilienda mpaka mlangoni kwangu na kufungua, nikawasha redio na taa maana kigiza cha jioni kilishaanza kisha nikachukua ndoo ya maji kwa ajili ya kwenda kujimwagia ili kupunguza uchovu. Mama mwenye nyumba aliendelea kunikata jicho lakini nikawa najifanya kama vile simuoni.

Baada ya kumaliza kuoga, nilitoka bafuni na kuelekea ndani. Ile naingia tu, nilisikia rafiki yangu Ras akiniita kwa bashasha.

“Ulikuwa wapi mwanangu, nimekutafuta kinoma kuanzia asubuhi,” alisema rafiki yangu huyo ambaye huwa anashinda stendi, pale kwa Mtogole.

“Dah, naumwa mwanangu, nimeshinda hapahapa nyumbani, sijatoka kabisa.”

“Aunt, ingia,” alisema Ras huku akimuoneshea ishara mtu aliyekuwa amesimama koridoni, nikashtuka kugundua kwamba alikuwa amekuja na mtu. Nikiwa bado nang’aang’aa macho, nilishtukia Ruqaiya akitokezea, mshtuko nilioupata almanusra nidondoke.

“Ooh! Karibu sana mgeni, daah! Karibu sana,” nilisema kwa kujibaraguza huku uso ukiwa umenishuka. Ruqaiya hakunionesha bashasha kama nilivyozoea, nikazidi kupata hofu ndani ya moyo wangu.

Ili kuepusha ‘kuuza gazeti’, harakaharaka nilimkaribisha ndani, nikamshukuru sana Ras kwa kuniletea mgeni wangu, nikachukua shilingi elfu mbili pale mezani na kumkabidhi.

“Dah, inabidi umuombe radhi aunt maana amekutafuta kinoma, tangu saa nne asubuhi tunahangaika kukutafuta,” alisema Ras huku akiniaga, akanipa ‘tano’ kisha akaondoka zake, Ruqaiya akawa amekaa juu ya kiti huku akiwa amejiinamia.

Nilijihisi kuchanganyikiwa, nilichokifanya nilienda kufunga mlango kwa ndani kisha nikaenda kuvaa bukta chumbani nakurudi pale sebuleni, nikaenda kukaa pembeni ya Ruqaiya. Nilishtuka sana kumuona akilia, ikabidi kazi ya kumbembeleza ianze.

“Nataka uniambie ulikuwa wapi ndiyo mambo mengine yataendelea, unajua ni kwa kiasi gani nimehangaika kukutafuta?”

“Sijaenda popote mke wangu, nimeshinda hapa nyumbani yaani nimekamatwa na tumbo la kuendesha tangu jana usiku mpaka nahisi kufa,” nilidanganya, akanitazama huku akiendelea kutokwa na machozi.

“Nimekupigia simu mara ngapi? Nimekutumia meseji ngapi? Kwa nini hunijibu? Kwa nini unanifanya niwe na wasiwasi kiasi hiki?” alisema huku akiendelea kulia, nikamkumbatia na kuendelea kumbembeleza.

Kitendo cha Ruqaiya kunililia kiasi kile kilinitisha kwa sababu kama nilivyowahi kueleza, alikuwa ni mwanamke wa nguvu haswaa! Kwanza alikuwa mzuri kuanzia sura mpaka umbo lakini kubwa zaidi, alikuwa na fedha za kutosha na aliolewa na mwanaume anayejimudu kwelikweli kimaisha!

Kwa hadhi yake, hakutakiwa kabisa kumwaga machozi kwa sababu ya ‘kivuruge’ mimi, nikajihisi kuwa na hatia kubwa ndani ya moyo wangu. Wakati nikimbembeleza, akili yangu nyingine ilikuwa ikimfikiria Khazija, maana nilipoondoka pale kwake nilimwambia nitarejea muda si mrefu, nikawa najiuliza akiamua kunifuata itakuwaje?

Yaani nishinde kutwa nzima nikiwa naye ndani kwake halafu atoke anikute na mwanamke mwingine ndani, tena siku moja tu baada ya kutokea kwa tatizo lingine kama hilohilo lililomliza sana! Itakuwaje?

“Inawezekana wewe una mwanamke mwingine ndiyo maana unanifanyia hivi, kwa nini lakini unanitesa jamani?”

“Ha..pana! Sina mwanamke mwi..ngine Ruqaiya, nisamehe mama, nakupenda sana,” nilijiumauma kwenye maelezo yangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Sasa kwa nini unanitesa mwenzio kiasi hiki? Angalia nalia machozi kwa sababu yako,” alisema huku akianza kufungua ushungi aliokuwa amevaa kwa sababu alikuwa anapenda sana kujistiri mwili mzima.

Niliendelea kumbembeleza lakini akawa bado analalamika huku akiendelea kupunguza nguo kwenye mwili wake, moja baada ya nyingine huku akionesha kuwa na ‘kiu’ iliyopitiliza, moyo ukawa unanidunda kwelikweli.

Kilichofanya moyo unidunde ni kwa sababu Khazija alikuwa amekombeleza kila kitu kwenye chungu cha asali kiasi kwamba sikuwa na uwezo wa kumlambisha Ruqaiya asali kama alivyokuwa akitaka.

Nikiwa bado naendelea kujiuliza nini cha kufanya, nilimshuhudia akimalizia nguo ya mwisho kisha akasimama na kujinyonganyonga kimadaha mbele yangu kama wafanyavyo wanamitindo, akahamia kwenye bukta yangu na kuitoa, akamvamia ‘mkuu wa kaya’ kwa mbwembwe zilizopitiliza.







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog