Chombezo : Utamu Wa Shemeji Flora
Sehemu Ya Tano (5)
**************
"Kesho na mimi nitaaga hapa na kumpigia simu Japhet anielekeze huko alipohamia ili tukaishi wote siwezi kuishi mbali naye" alisema Rozi huku akitoka chumbani kwake na kuelekea jikoni kuendelea tena na kazi yake ya kupika chakula na muda huohuo naye Flora akaingia. Rozi alishangaa kwani akujua ni muda gani Flora alikuwa amerudi hapa nyumbani akitokea kule saloon kwake.
"Vipi mbona unanishangaa kama vile ndio kwanza unaniona leo?" Flora alimuuliza Rozi kwa Shari huku akiingia humo jikoni.
"Hapana wala sikushangai, nikushangae kwa lipi ulilokuwa nalo?” Rozi naye alihoji kwa ujeuri. Flora akachukia sana baada ya kumsikia Rozi amesema hivyo. " Yaani wewe Rozi unathubutu kweli kuniambia mimi hivyo?" Flora aliuliza kwa hasira.
"Kwani dada hasira zinatokea wapi tena, au ni kwa vile Japhet hayupo amekukimbia?" Rozi alimuuliza hivyo Flora kwa makusudi aone atajibu nini.
"Naona sasa hivi heshima imepungua Rozi enhe? hayaa utakipata hicho kitu unachokitaka" alisema Flora na kuondoka humo jikoni huku akiwa amekasirika.
Huku nyuma Rozi alibakia anacheka tu çhini kwa chini. "Nikuheshimu mtu kama wewe unayeshindwa kujiheshimu, hadi unafikia hatua ya kufanya mapenzi na Shemeji yako" alijisemea moyoni Rozi na halafu akaendelea na kazi zake za jikoni. Kumbe Lukasi aliweza kuyasikia hayo mazungumzo yao yote akiwa amekaa kule sebuleni akaamua tu kunyamaza.
Muda wa kula chakula ulipofika wakala na baada ya hapo wakatawanyika na kuingia vyumbani mwao kulala. Lukasi na mkewe Flora wakaingia chumbani kwao na Rozi naye akaingia chumbani kwake.
Rozi akiwa amejilaza kitandani mawazo yake yote yalikuwa yapo kwa Japhet akaona ngoja kwanza ajaribu kumpigia simu usiku huohuo. Bahati nzuri simu ya Japhet ilikuwa inapatikana ikaanza kuita.
"Aloo niambie Rozi mpenzi wangu" sauti ya Japhet ilisema baada ya kupokea simu. "Mmh nikuambie nini baby zaidi tu ya kukumiss Mume wangu" Rozi alisema.
"Hee mara hii tayari nimeshakuwa Mume wako? hebu acha kuniletea balaa huko" alisema Japhet kwa utani huku akicheka.
"Kwahiyo leo unanikana Japhet baada ya kuhama huku si ndio enhe?" Rozi naye alijifanya kuuliza kwa sauti ya kudeka.
"Hapana mpenzi wangu siwezi kukukana kabisa, bila ya wewe leo nisingekuwa huku najinafasi kwa raha zangu" alisema Japhet. "Sasa huko kujinafasi ndio nataka na mimi nije ili tujinafasi wote my love" alisema Rozi huku akichekacheka.
"Duuh mbona mapema hivyo mpenzi wangu? subiri angalau kidogo hata zipite siku nne ndio nikuelekeze uje huku" Japhet alisema kwa sauti ndogo iliyopoa.
"Weee nisubiri nini tena hapa? sikiliza Japhet kesho jioni naaga huku, halafu keshokutwa asubuhi nakufuata wewe huko ujiandae kunipokea" alisema Rozi kwa msisitizo. "Lakini Rozi hauoni kama hapo nyumbani kaka pamoja na Shemeji watashtukia kama umekuja kwangu?" Japhet aliuliza. Rozi akacheka kidogo na halafu akasema: "Sioni sababu ya wewe kuogopa kama ikiwa hata uhusiano wetu kaka yako anaujua na ananiita mimi Shemeji, sasa sijui unaogopa nini Japhet?" Rozi aliuliza huku akionyesha kuchukizwa na huo uoga wa Japhet.
"Hapana mimi sio kama naogopa ila nilikuwa nataka huyo Shemeji Flora asijue kama wewe unakuja kuishi huku na mimi" alisema Japhet. "Kama wewe hautaki ajue kama nakuja kuishi kwako, sasa mimi ndio nataka ajue hivyo ili aache kukusumbua au na wewe bado unampenda huyo Shemeji yako? hebu niambie basi nijue" Rozi alisema huku akionekana kukasirika. "Sio hivyo mpenzi wangu naomba usinielewe vibaya, basi kesho wewe waage huko nyumbani, halafu utanijulisha nitakupa maelekezo ya kufika huku" alisema Japhet. Rozi sasa hapo akafurahi baada ya kusikia hivyo.
"Hayo sasa ndio maneno mtoto wa kiume, kesho nitakujulisha baby wangu" alisema Rozi kwa furaha. Baada ya hapo wakaagana na kutakiana usiku mwema halafu wakakata simu zao na kulala.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi ya siku nyingine mpya ikafika.
Japhet akiwa ndio anaamka huko kwenye makazi yake mapya alipopanga chumba mawazo yake yote alikuwa anawaza Yale aliyoyaongea na Rozi Jana usiku kwenye simu. "Huyu binti naye vipi mbona sasa anataka kuniganda?" Japhet alijiuliza hivyo na kusahau Yale yote aliyoyapanga na binti huyo pale mwanzoni. "Mimi kwa sasa wala sijajiandaa kuishi na mwanamke, basi tu nilikubali kufanya hivi kwa sababu ya kuepuka usumbufu wa Shemeji kule nyumbani kwa kaka" Japhet bado aliendelea kujisemea. Baada ya hapo akaamka kitandani na kwenda kupiga mswaki pamoja na kunawa uso wake alipomaliza kujifanyia usafi Japhet akaenda zake dukani kununua mkate pamoja na Blue band bila kusahau na mayai halafu akarudi chumbani kwake na kujipikia Chai yake ya kiselasela. Baada ya kumaliza kunywa Chai akabakia humo chumbani kwake akiangalia TV kwa kuwa hakuwa na sehemu nyingine ya kwenda kutembea kwani kwa muda huo wa asubuhi yule rafiki yake aitwae Mussa alikuwa ameenda kwenye kazi zake na pale nyumbani kwake alibakia mkewe tu pamoja na mtoto wao mdogo. Hivyo kwa Japhet aliona ni ngumu yeye kwenda huko aliona ni bora asubiri mpaka rafiki yake atakaporudi ndio aende kupiga story kwenye muda huohuo Japhet akiwa bado yupo chumbani kwake ndipo akaona simu yake inapigwa. Na alipoangalia ni nani huyo anaempigia simu Japhet akaweza kumgundua ni Shemeji yake Flora ndio anaepiga simu hiyo. "Khaa! Huyu Shemeji naye vipi, mimi nimeshahama kumkwepa yeye sasa mbona bado ananiandama kwa kunipigia simu kwani anataka nini tena kwangu?" Japhet alijiuliza na mwishowe akaamua kukata na kuizima hiyo simu kabisa hakutaka mawasiliano na huyo Shemeji yake. "Na akiendelea kunisumbua sana nitabadilisha na hii namba ya simu, sitaki anisumbue" alisema Japhet na kuisubiri jioni ifike aende nyumbani kwa rafiki yake Mussa. Na kweli Japhet aliweza kusubiri mpaka jioni ilipofika ndio akaenda kumtembelea rafiki yake Mussa na kwa Bahati nzuri akamkuta amesharudi nyumbani.
"Ooho niambie best yangu mwenyewe" alisema Mussa kwa furaha baada ya kumuona Japhet amekuja kumtembelea.
"Daah ndio hivyo ndugu yangu nipo tu nanyoosha miguu" alisema Japhet.
"Enhe makazi mapya yanasemaje huko?" Mussa alimuuliza Japhet. Kwanza Japhet akatabasamu halafu akasema: "Makazi mapya kusema ukweli ni pazuri sana na tayari nimeshaanza kupazoea" alisema Japhet. "Utapazoea vipi na wakati upo peke yako? inabidi sasa ndio umuite huyo mpenzi wako mfurahie maisha pamoja" Mussa alisema huku akitabasamu.
"Halafu hicho ndio kitu kilichonileta hapa kwako naomba unipe ushauri wako ndugu yangu" alisema Japhet. Mussa akajiweka sawa na kuuliza kwa umakini:
"Nikupe ushauri gani tena ndugu yangu?"
"Nimeona bora nimuache yule binti ambaye ni mfanyakazi wa ndani kule nyumbani kwa kaka, na halafu nitafute msichana mwingine huku wa kuwa naye" alisema Japhet. Mussa akashusha pumzi halafu akauliza: "Kwanini sasa umuache huyo binti na wakati uliniambia hapo mwanzo kuwa ndio yeye aliyekupa huo ushauri wa kuhama nyumbani kwa kaka yako ili umkwepe Shemeji yako anayekusumbua kimapenzi?" Mussa alimuuliza Japhet. "Ni kweli kabisa yeye ndie alienishauri na pia hata pesa ya kodi amenipa" Japhet alisema. "Sasa kama pesa ya kodi amekupa kwanini unafikiria kumuacha? hebu acha mawazo hayo ndugu yangu, ukijaribu kumuacha ujue umejitafutia matatizo kwa kaka yako" Mussa alisema kwa msisitizo.
"Nitajitafutia matatizo kivipi tena kwa kaka yangu endapo nikimuacha?" Japhet alihoji. "Namaanisha hivi huyo binti atakutolea siri yako iliyosababisha wewe uhame kule nyumbani kwa kaka yako" alisema Mussa. Japhet akajifikiria kidogo halafu naye akasema: "Sawa rafiki yangu nimekuelewa ngoja nitampigia simu na kumuelekeza aje huku tuishi wote" alisema Japhet kwa upole. "Yes hayo ndio mambo sasa, na usijichanganye kabisa kumuacha huyo binti utakuja kujuta ndugu yangu nakuambia" alisema Mussa akimpa ushauri huo Japhet.
Basi baada ya hapo wakaendelea kupiga story zingine mbalimbali za kiurafiki.
Majira ya usiku kule nyumbani kwa Lukasi napo baada ya kumaliza kula chakula Rozi naye akaona ngoja na yeye leo aliamshe Dude kama vile alivyofanya mpenzi wake Japhet kwa kuaga hapa nyumbani. "Shemeji na dada Flora leo na mimi ningependa kuwaaga rasmi kuwa natarajia kuondoka hapo kesho asubuhi" alisema Rozi kwa sauti ya upole. Flora pamoja na mume wake Lukasi kwanza wakashtuka sana baada ya kumsikia Rozi anasema hivyo. "Rozi kwanini uondoke hapa nyumbani ghafla kiasi hicho enhe?" Lukasi alimuuliza Rozi. "Basi tu Shemeji nimeamua hivyo nimewakumbuka sana ndugu yangu kijijini kwetu Iringa" Rozi aliamua kudanganya. "Sawa hata kama umewakumbuka ndugu zako ndio uage ghafla namna hiyo kama vile kuna ugomvi?" Lukasi bado aliendelea kumuuliza Rozi. Kwa upande wa Flora tayari alishaanza kuhisi kitu juu ya huku kuaga kwa Rozi. "Mmh huyu binti nahisi atakuwa anamfuata Japhet huko alipohamia, na inawezekana ikawa ni mipango yao waliyoipanga kunikimbia mimi humu ndani" Flora alijisemea.
"Eti mke wangu unachukuliaje huku kutaka kuondoka kwa Rozi naye hapa nyumbani?" Lukasi alimgeukia mkewe Flora na kumuuliza hivyo. "Sasa kama yeye mwenyewe ndio anataka kuondoka sisi tumzuie wa nini? tumuache aondoke" alisema Flora. Rozi kimoyomoyo alifurahi sana. "Hapana mke wangu mimi nahisi hapa kuna tatizo kuanzia kule kuhama kwa Japhet na mpaka kutaka kwa huyu binti nahisi wewe mke wangu utakuwa unajua kila kitu, sasa nataka uniambie bila ya kunificha, nini tatizo mpaka Rozi naye anataka kuondoka humu ndani?" Lukasi alichachamaa na kumuuliza hivyo mkewe Flora kwa sauti ya ukali. Flora sasa alibakia anatetemeka kwa hofu.
"Unasema mimi najua kila kitu, sasa mimi najua nini mume wangu kuhusu Rozi kutaka kuondoka?" Flora aliuliza kwa sauti ya kulalamika. Lukasi akatabasamu kiunafiki na halafu akamuambia hivi mkewe Flora: "Nilikuwa naumiza sana kichwa changu kujua ni sababu gani iliyomfanya mdogo wangu Japhet mpaka akahama humu ndani, sasa sababu hiyo karibia nitaijua na pia utaniambia kwanini na Rozi naye anataka kuondoka" alisema Lukasi na kunyanyuka kwenye kochi halafu akamsogelea mke wake Flora na kumpiga Kofi usoni. "Wewe mwanamke leo utaniambia ukweli wote unaoujua" alisema Lukasi kwa hasira. Rozi sasa naye akajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani hakutegemea kama haya mambo yangeweza kufikia hatua hii.
"Mmh yaani huku kuaga kwangu tu ndio kumesababisha balaa hili jamani?" Rozi alijiuliza moyoni huku akiwa anatetemeka na kumshuhudia Flora akilia machozi baada ya kupigwa lile Kofi na mumewe!.
"Mmh yaani huku kuaga kwangu tu ndio kumesababisha balaa hili jamani?" Rozi alijiuliza moyoni huku akiwa anatetemeka na kumshuhudia Flora akilia machozi baada ya kupigwa lile Kofi na mumewe.
Lukasi sasa alikuwa amecharuka ile vibaya sana alipandisha hasira sana kupita kiasi. "Nasema hivi sitaki mnifanye mimi mpumbavu, hapa nataka mniambie ukweli wote bila hata ya kunificha" Lukasi aliunguruma. Flora akazidi kulia machozi huku akiuliza: "Sasa Mume wangu jamani unataka tukuambie ukweli gani tena?" Flora aliuliza huku akilia kwa kwikwi.
"Tena wewe hapo ndio nakutaka sana uniambie, inaonyesha unajua kila kitu kinachoendelea" Lukasi alisema huku akimkaba mkewe shingoni. Kwa hakika Flora sasa alikuwa anatia huruma sana.
"Rozi njoo unisaidie jamanii ,,, mdogo wanguuu ,,,ananiuaaa hukuuu" Flora alijikuta akimuomba Rozi msaada kwa sauti ya shida. Rozi huruma ikaweza kumuingia na kumuambia Lukasi hivi: "Jamani Shemeji naomba umsamehe dada basi amekosa atorudia tena" Rozi alijaribu kumtetea Flora na kumuombea msamaha kwa Lukasi. "Rozi naomba uniache kabisa kumbuka na wewe pia nilikuuliza tena kistaarabu tu, lakini ukanificha sasa ngoja nitumie nguvu" alisema Lukasi kwa hasira na kumpiga tena Flora bonge la Kofi usoni. PAAAAA!
"Jamanii Lukasi utaniuwa mume wangu naomba unisamehe sirudii tena ,," Flora alilia na kuomboleza kwa uchungu sana.
"Kufaaa kabisa Malaya mkubwa wewee ," Lukasi aliendelea kufoka kwa hasira.
Baada ya hapo akaanza kumvuta na kum'buruza chini mkewe Flora kumpeleka ndani chumbani kwao wanapolala huku akimuacha Rozi sebuleni akiendelea bado kutetemeka. Lukasi alitisha sana!
Lukasi aliweza kum'buruza mkewe Flora mpaka chumbani na halafu akachukua mkanda wa suruali yake na kumuambia hivi: "Nitakurudia tena muda sio mrefu sana mpumbavuu mkubwa wewe" Lukasi alisema kwa hasira na kutoka kwa kasi humo chumbani huku mkanda wa suruali akiwa ameushika mkononi na kuweza kumfungia mlango kwa nje na ufunguo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Halafu Lukasi akarudi tena mpaka sebuleni na kumkuta Rozi amejikunyata kwenye kochi huku akitetemeka kwa hofu kubwa sana. "Na wewe nimekuja kwako nataka uniambie ukweli, kwanini Japhet amehama humu ndani na halafu na wewe pia kwanini unataka kuondoka hiyo kesho kama ulivyoaga?" Lukasi alimuhoji Rozi kwa hasira. "Shemeji mimi kweli vile sijui kwanini Japhet alihama hapa nyumbani" alisema Rozi kwa sauti ya kutia huruma huku akilia machozi. WAAAAAA! huo ni mlio wa mkanda wa suruali ukitua mwilini kwa Rozi baada ya kupigwa na Lukasi.
"Mamaaa weeee nakufaaaa, Shemeji mimi unanionea sijui kitu chochote ,," Rozi alipiga mayowe na kusema hivyo.
"Uwe unajua ukweli au haujui mimi hapa ninachotaka mniambie nini kinaendelea" Lukasi alisema na halafu akaanza kumvuta na Rozi pia akampeleka mpaka kwenye chumba anacholala binti huyo na kujifungia mlango kwa ndani akiwa na Rozi humo chumbani. "Sikiliza Rozi naomba uniambie ukweli bila hata ya kunificha ni kitu gani kilikuwa kinaendelea humu ndani wakati mimi nipo safarini?" Lukasi aliuliza kwa sauti ya taratibu.
"Shemeji naomba uniamini kweli vile mimi sijui kitu chochote" Rozi bado aliendelea kukataa na kuficha ukweli.
"Rozi ujue mimi sitanii hapa, sema ukweli wote unaoujua vinginevyo na wewe pia utaumia nimewasikieni pale mwanzo mlipokuwa jikoni mkilumbana na dada yako Flora inaonyesha kuna kitu kati yenu kinaendelea juu ya Japhet" alisema Lukasi kwa hasira huku akionekana hana mzaha hata kidogo. Rozi akaona hapa asiposema ukweli anaweza kufa hivihivi lakini akajifikiria ataanzaje kusema kile anachokifahamu yeye. Hivyo akaamua kumrudishia Flora msala wake mwenyewe. "Sikiliza Shemeji nenda kwa dada Flora yeye anajua kila kitu, kuhusu mambo yote yanayoendelea atakuambia" alisema Rozi. Lukasi alishusha pumzi ndefu baada ya kumsikia Rozi amesema hivyo. "Una uhakika ataniambia bila ya kunificha, na asiponiambia Je?" Lukasi aliuliza kwa mashaka. "Nina uhakika atakuambia tu vizuri, na asipokuambia njoo tena kwangu mimi nitakuambia" Rozi sasa aliamua kujitoa muhanga.
"Ok hebu ngoja niende nikamjaribu" alisema Lukasi huku akitoka kwa kasi humo chumbani kwa Rozi na halafu akamfungia mlango kwa nje na ufunguo.
Lukasi akarudi tena kule chumbani kwao ambapo alimfungia Flora pale mwanzo na kuingia mpaka ndani akamkuta Flora amenyamaza kulia na amejilaza juu ya kitanda. "Sikiliza mke wangu nataka uniambie ukweli wote kuhusu uhusiano wako wewe na mdogo wangu Japhet, kama utanificha damu itamwagika humu ndani" Lukasi alisema kwa hasira.
"Wala haina sababu ya kunitisha mume wangu nitakuambia kila kitu, kiukweli mimi nampenda sana Shemeji Japhet" Flora aliamua kufunguka ukweli wake.
Lukasi alishtuka sana hakuamini hiki kitu alichokisikia kutoka kwa mkewe Flora.
"Unasemajee mke wangu, hivi una kichaa wewe!?" Lukasi aliuliza kwa mshangao.
"Ndio nina kichaa tena cha Mapenzi mdogo wako amejua kunikoleza na kunifikisha Kimahaba pale ambapo wewe pamekushinda kunifikisha, hivyo nina haki zote za kumpenda yeye nampenda sana Shemeji Japhet" Flora alisema kama vile mtu aliyechanganyikiwa. Lukasi alibakia ameduwaa anamuangalia mkewe Flora Mara mbili mbili hammalizi kabisa.
"Flora mke wangu hicho unachosema ni cha kweli?" Lukasi aliuliza huku machozi yakimlengalenga machoni mwake.
"Kwanini nikufiche mume wangu, au wewe unajiona unaniridhisha kimapenzi?" Flora alimuuliza Lukasi huku akiwa anatabasamu. Lukasi akaona hii sasa ni dharau kubwa sana kwake. "Noooo mke wangu siwezi kuvumilia dharau hiyoo" alisema Lukasi na moja kwa moja akaenda kumvamia Flora pale kitandani na kunyanyuka naye wakasimama wima.
"Mke Flora umejua kunidhalilisha sana, hivi wewe ni wa kufanya mapenzi na mdogo wangu Japhet kweli?" Lukasi aliuliza huku akitetemeka kwa hasira.
"Ndio nimeshafanya naye sasa, na hapa natamani nifanye naye zaidi na zaidi kila siku nampenda sana Japhet" alisema Flora kwa kujiamini na kujitoa ufahamu.
"Hapanaaaa inatoshaaa Floraaaa" alijikuta anabwata hivyo Lukasi na kumkamata kwa nguvu mkewe Flora akaenda kumpigiza kichwa chake kwa nguvu kwenye kabati kubwa la nguo.
"Mamaaa nakufaaaa unaniuaa Lukasi ,," alipiga yowe la uchungu Flora baada ya kupigizwa kichwani kwenye kabati. Kwa Bahati mbaya sana Flora alifikia usoni kabatini hapo na kujipigiza sehemu ya kwenye Kioo na kupasuka kabisa halafu vipande vya Kioo vikamchana vibaya sana usoni na kupelekea damu nyingi sana kumvuja. "Hayo ndio malipo yako ya Usaliti Malaya mkubwa wewe" alisema Lukasi kwa hasira. Flora alilia sana kwa maumivu huku akijishika usoni mwake.
"Sawa ndio nakubali kama haya ndio malipo yangu, lakini naomba utambue jambo moja mume wangu kuwa Utamu wa Shemeji ni zaidi kukushinda wewe" alisema Flora. Lukasi alikasirika sana akachukua kipande kikubwa cha Kioo na kwenda kumpiga nacho kichwani mkewe Flora. "Jamaniiii Lukasi unaniuaa mume wanguu ,," alisema Flora na baada ya hapo akaanguka chini na kutulia kimya.
Huo ndio ulikuwa mwisho wa Flora kwani alifariki dunia hapohapo. Lukasi alibakia akiuangalia mwili wa mkewe Flora ambao ulikuwa hauna uhai kabisa kwa wakati huo. "Nisamehe sana mke wangu Flora imenibidi kufanya hivi ili kulinda heshima yangu" alisema Lukasi huku akibubujikwa na machozi ya uchungu.
Kwa upande wa Rozi naye kule chumbani alipofingiwa na Lukasi aliweza kuzisikia zile purukushani zote zilizokuwa zikiendelea kati ya Lukasi na mkewe Flora kule chumbani kwao. "Ooohoo Mungu wangu sijui kama kuna usalama kweli huko" alijisemea Rozi baada ya kuhisi ukimya wa ghafla. Ikabdi ajaribu kuufungua mlango wa humo chumbani kwake lakini kwa Bahati mbaya ndio vile ulikuwa umefungwa kwa nje na ufunguo muda ule na Lukasi alipotoka humu ndani. "Mimi nahisi huko hakutakuwa na usalama mbona siwasikii tena wakigombana?" Rozi aliendelea kujiuliza huku akizungukazunguka humo chumbani hapohapo Rozi akapata wazo la kumpigia simu mpenzi wake Japhet amuambie hiki kinachoendelea huku nyumbani. Akachukua simu yake iliyokuwa ipo kitandani na kuanza kuitafuta namba ya Japhet na kwa Bahati nzuri akaipata na kuipiga ikawa inaita. Rozi alibakia kusubiri Japhet apokee simu na aweze kumpa taharifa. Mara ghafla akaweza kusikia sauti za RAIA ambao nao walikuwa wamesikia Tafrani hiyo na wakaweza kusogea hadi hapo kwenye eneo la tukio nyumbani kwa Lukasi.
RAIA hao ambao wengi wao walikuwa ni majirani baada ya kusogea mpaka mlangoni ndipo wakagundua milango yote ya kuingilia ndani ya nyumba hii ya Lukasi ilikuwa imefungwa kwa ndani hivyo wakaanza kubisha hodi kwa nguvu na kuomba wafunguliwe ili waingie ndani.
Lukasi akiwa bado yupo kule chumbani kwake akiushangaa mwili wa mkewe Flora ambaye mpaka muda huo alikuwa ameshakufa. Mara ghafla ndipo akasikia sauti ya kugongwa kwa mlango Mkubwa wa kuingilia ndani ya nyumba yake.
"Daah majirani hao wamesikia na wamekuja, sasa sijui nitafanya nini hapa?" Lukasi alijiuliza huku mikono yake yote miwili akiwa amejishika kichwani mwake.
Hapohapo akajikuta anapata na wazo la kujiua ili kukwepa mkono wa sheria kwa kosa la kusababisha kifo cha mkewe Flora. "Nisamehe sana Mungu wangu kwa haya niliyoyafanya najutia sana, Japhet mdogo wangu nimekusamehe yote najua sio makosa yako" alisema Lukasi halafu akaokota kipande kikubwa cha Kioo chenye Ncha Kali na kufumba macho yake. "Mungu baba naomba na mimi unipokee sasa ni muda wangu wa kurejea kwako umewadia" alisema Lukasi na halafu akakikamata kwa mikono yake Kioo hicho na kukishusha kwa nguvu sana Tumboni mwake na kujichoma.
Damu nyingi sana iliweza kumtoka baada ya kujichoma na Kioo hicho ambacho kilimchana na kuzama kabisa ndani ya Tumbo lake na kumpelekea Lukasi kuanguka chini na kuanza kutapatapa na baadae akatulia kimya na kufariki dunia!.
Damu nyingi sana iliweza kumtoka baada ya kujichoma na Kioo hicho ambacho kilimchana na kuzama kabisa ndani ya Tumbo lake na kumpelekea Lukasi kuanguka chini na kuanza kutapatapa na baadae akatulia kimya na kufariki dunia.
Kwa upande wa Japhet naye akiwa kule kwenye chumba chake ajui hili wala lile kuhusu Yale mambo yaliyotokea kule nyumbani kwa kaka yake Lukasi. Majira haya ya usiku Japhet ndio sasa alikuwa anajiandaa kulala Mara baada ya kutoka kupiga story kwa yule rafiki yake Mussa.
Ghafla Japhet akaweza kuisikia simu yake ya mkononi inaita na alipoangalia ni nani huyo anaempigia simu akagundua ni Rozi. "Mmh basi huyu binti ameshaanza tena usumbufu wake wa kutaka kuja huku" alijisemea Japhet huku akiwa anatabasamu na kuipokea simu hiyo.
"Enhe niambie mpenzi wangu, vipi tayari umeshaaga hapo nyumbani?" Japhet aliuliza Mara baada ya kupokea simu.
"Japhet naomba uache chochote unachokifanya sasa hivi njoo huku nyumbani haraka sana" Rozi alisema kwa pupa baada ya kuisikia sauti ya Japhet.
"Wee Rozi kuna nini tena kimetokea huko nyumbani? hebu niambie kwanza" Japhet naye alijikuta anauliza kwa wasiwasi.
"Nimekuambia njoo haraka sana, haya mambo ya huku utakuja kuyajua pindi utakapofika naomba uzingatie hiki ninachokuambia Japhet" alisema Rozi na kukata simu yake ghafla. Japhet alibakia njia panda hakujua ni kitu gani tena hicho kilichokea huko nyumbani kwa kaka yake Lukasi. "Mmh kuna nini huko? mbona sasa naanza kupata wasiwasi" Japhet alijisemea kwa sauti ndogo. Hapohapo akapata wazo la kumpigia simu yake Lukasi ili ajue kinachoendelea lakini kwa Bahati mbaya simu ya kaka yake huyo ilikuwa inaita tu bila hata ya kupokelewa.
"Sasa naanza kupata mashaka kuwa huko hali itakuwa sio shwari, hebu ngoja niende" alisema Japhet na hapohapo bila ya kupoteza muda akanyanyuka kwenye kitanda alipokuwa amejilaza na kuanza kujiandaa harakaharaka kwa kuvaa nguo za kutokea na halafu akaufunga vizuri mlango wa chumba chake na kuondoka.
"Hebu ngoja kwanza nipitie kwa rafiki yangu Mussa" alisema Japhet huku akikatiza mitaani usiku huo kwenda kwa rafiki yake Mussa kumuomba ushauri na ikiwezekana hata amsindikize huko nyumbani kwa kaka yake Lukasi. Japhet alipoangalia saa kwa kupitia simu yake ya mkononi ikamjulisha kuwa ni majira ya saa 4:56 za usiku Japhet akaondoka.
Rozi naye akiwa bado yupo chumbani alipofungiwa na Lukasi. Baada ya kukata simu yake ghafla pale alipokuwa anaongea na mpenzi wake Japhet sasa Rozi aliweza kusikia sauti ya zogo la majirani huko nje ya nyumba ambao nao walikuwa wamekuja hapo baada ya kusikia ile Tafrani iliyosababishwa na Lukasi. Ikabidi Rozi ajiongeze kwa kusogea hadi dirishani na kuanza kupiga makelele ya kuomba msaada kwa watu hao ambao wapo nje. "Jamaniii msaada hukuu nipo hapa dirishaniiii" Rozi alipaza sauti yake kwa nguvu. Bahati nzuri sauti hiyo ya Rozi iliweza kuwafikia vyema Raia hao na kwa haraka wakasogea mpaka dirishani iliposikika sauti ya binti huyo na wakaweza kumuona akiwa amesimama kwa ndani. "Vipi binti mbona hivyo tumesikia makelele na milango yote ya kuingilia ndani imefungwa, kwani nini kimetokea?" Mzee mmoja wa makamo ambaye ndie mjumbe wa nyumba kumi (10) kwenye mtaa huo alimuuliza Rozi.
"Babu yaani hata mimi sijui kilichotokea, kwani nimefungiwa humu chumbani na Shemeji kwa nje" alisema Rozi. Kwa hayo maelezo kidogo ya Rozi yalitosha kabisa kuwajulisha Raia hao kuwa humu ndani ya hii nyumba kuna hatari imetokea. Hivyo baada ya kushauriana wote kwa pamoja hatimaye mjumbe huyo wa nyumba kumi akaamuru mlango Mkubwa wa kuingilia ndani hapa nyumbani kwa Lukasi uvunjwe ili waweze kuingia ndani wakaone kuna nini kimetokea. Vijana wenye nguvu wakafanya kazi hiyo ya kuvunja mlango na baada ya muda mfupi waliweza kufanikisha zoezi hilo na wakaweza kuingia mpaka ndani ya mjengo huo na kujionea hali halisi. Kwa hakika ulikuwa ni mshtuko Mkubwa sana pamoja na majonzi yaliweza kuwakumba Raia baada ya kuikuta miili ya wanandoa hao (Lukasi na mkewe Flora) ikiwa ipo imelala chini chumbani kwao huku ikivuja damu bila ya kuwa na dalili ya uhai. Ikabidi kwanza wamfungulie na Rozi naye kule chumbani kwake alipofungiwa na baada ya hapo ikapigwa simu mpaka kituo cha Polisi na kutoa taharifa ya hili tukio. Rozi hakuweza kuyaamini macho yake baada ya kufunguliwa chumbani na kuonyeshwa miili ya mabossi wake wote wawili wakiwa wamefariki dunia. Rozi alijikuta anaangusha kilio cha uchungu na kuwalilia mabossi wake hao. Japo jibu lilikuwa ni rahisi kuwa Lukasi ndie chanzo cha mauaji haya kwa kumuua mkew Flora na baadae kujiua yeye mwenyewe. Lakini majirani nao hawakuwa nyuma katika kuusaka 'Ubuyu' (Umbeya) kwa kumdadisi Rozi awaeleze nini kilitokea mpaka hawa wanandoa wamekumbwa na mauti. Kwa jinsi Rozi alivyokuwa amechanganyikiwa hakuweza kutoa jibu lolote la maana kwa Raia hao zaidi tu ya kulia machozi. Basi wakaamua kutulizana na kuwasubiri Askari Polisi waje hapa eneo la tukio na huku kundi kubwa la Raia wakipiga picha za tukio hilo kwa kutumia simu zao na kurusha kwenye mitandao ya kijamii.
Wakati gari mbili aina ya DEFENDER za jeshi la Polisi zikifunga break Kali hapa nyumbani kwa Lukasi ndipo na muda huohuo nao Bajaj iliyompakia kijana Japhet na rafiki yake Mussa nayo pia ilikuwa ndio inawasili maeneo haya. Japhet na Mussa walishangazwa na huu wingi wa watu waliowakuta hapa na kilichowashtua zaidi ni kuona hizo gari mbili za Polisi pamoja na Askari wake.
"Mmh Mussa ndugu yangu hapa hakuna usalama kabisa" alisema Japhet huku mapigo yake ya moyo yakimuenda mbio.
"Usipagawe ndugu yangu hebu twende huko ndani tukaone kuna nini ambacho kimetokea" alisema Mussa huku akilipia Pesa ya Bajaj iliyowaleta hapa. Baada ya hapo Mussa akamshika mkono Japhet aliyeonekana kuchanganyikiwa au kama sio kupagawa kabisa na halafu akaanza kumuongoza kwa kuingia ndani.
Baada ya kuingia ndani ya nyumba sasa kila kila kitu kilikuwa Hadharani kwani Japhet akaweza kuishuhudia kwa macho yake miili ya marehemu hao ambao ni kaka yake Lukasi pamoja na Shemeji yake Flora. Hapo Japhet sasa alijikuta anakaribia kuwa mwendawazimu kwa haya aliyoyaona hapa. Mussa akapata kazi ya ziada kumtuliza rafki yake huyo.
Japhet alilia machozi kama vile mtoto mdogo watu wengi sana walimuhurumia na hata Polisi nao baada ya kumgundua kuwa huyu ni mdogo wa marehemu Lukasi wakamsogelea na kujaribu kumuuliza maswali mawili matatu lakini kutokana na kupagawa Japhet akashindwa kujibu vyema maswali ya Askari hao na kuishia tu kulia machozi.
Basi baada ya Askari kufanya uchunguzi wao wakaichukua miili ya marehemu hao na kuipakia kwenye gari ya Polisi tayari kwa kwenda kuhifadhiwa hospitalini. Rozi naye akajikuta anaingia matatani kwenye mikono ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi. "Inabidi tumchukue huyu binti kwanza tunaenda kufanya naye mahojiano juu ya tukio hili, halafu pia na wewe tutakuhitaji baada ya kumaliza taratibu zote za mazishi ya ndugu yako pamoja na Shemeji yako" alisema mmoja wa Askari aliyeonekana kuwa na cheo kikubwa. "Lakini afande huyo binti anahusikaje na hili tukio?" Japhet alijikuta anauliza hivyo. "Sikiliza kijana sisi atujasema kama huyu binti anahusika na hili tukio, tunachohitaji ni kujua nini chanzo cha ugomvi wao mpaka vifo vyao vikatokea" alisema Askari huyo. Basi ikabidi Japhet akubali kuwa mpole. Gari za Polisi zikaondoka eneo hilo huku gari moja ikielekea hospitli ya Taifa kwenda kuhifadhi miili ya marehemu na ile gari nyingine ikielekea kituo cha Polisi kumpeleka Rozi ambaye alikuwa anashikiliwa kwa mahojiano zaidi. Japhet na Mussa walibakia nyumbani hapo kwa marehemu na kuanza kutoa taharifa za msiba huo Mkubwa kwa ndugu na jamaa wote usiku huohuo kwa njia ya simu.
Japhet licha ya kupagawa na msiba huo wa kaka yake pamoja na Shemeji yake lakini hakuacha kujiuliza maswali ndani ya kichwa ni kitu gani kilitokea mpaka haya mambo yakafikia hatua hii mbaya kiasi hiki cha kusababisha mpaka vifo.
Bahati mbaya sana akuwahi kuongea na Rozi baada ya kufika hapa na kumuuliza kilichotokea kwani ndio vile tena Rozi yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi.
"Mmh nahisi Rozi atakuwa ametoa siri kwa kaka Lukasi mpaka amefikia hatua ya kumuua Shemeji Flora na halafu na yeye pia akajiua, na kama ataenda kusema hivyo hadi huko Polisi basi tumeisha" alisema Japhet kwa sauti ndogo ya chini huku machozi yakimtiririka machoni.
Baada ya siku tatu kupita taratibu zote za msiba ziliweza kufanyika na hatimaye siku ya kwenda kuwazika marehemu hao ilifika. Ndugu na jamaa wa pande zote mbili waliweza kukusanyika nyumbani kwa Lukasi yaani ndugu wa Flora pamoja na ndugu wa Lukasi mwenyewe nao pia walikuwepo huku kila mmoja akijiandaa na maswali ya kumuuliza Japhet kwani ndie ndugu waliyekuwa wanamfahamu anaishi na marehemu kabla ya vifo vyao kutokea. Hivyo walikuwa na uhakika kuwa Japhet atakuwa anajua chanzo chote cha tukio hilo baya na la kutisha. Kila mmoja alijiandaa kumuuliza Japhet anachokijua juu ya vifo hivyo mara baada ya kumaliza kabisa mazishi. Kwa upande wa Japhet ilikuwa ni siku ngumu sana pale Masanduku (Majeneza) yaliyobeba miili ya marehemu yalipowasili hapo nyumbani kwa ajili ya kuagwa kabla ya kusafirishwa kwenda kuzikwa. Japhet alikumbuka mengi sana aliyoahidiwa na kaka yake Lukasi kuhusu kutafutiwa kazi na pia akakumbuka hata hivi karibuni alivyomnunulia vile vitu vya kwenda kuanza navyo maisha pindi pale alipoaga kuwa anaenda kuanza maisha ya kujitegemea kumkimbia Shemeji yake Flora aliyekuwa anamsumbua kimapenzi.
"Lakini yote haya ameyasababisa Shemeji Flora na mimi pia nina makosa kama ningeweka msimamo wa kukataa kufanya naye mapenzi leo tusingefikia hatua hii" alijisemea moyoni Japhet huku akilia. Pia akaenda mbali ña kujilaumu ni bora tu hata angetoroka wakati ule alipopata wazo la kutoroka nyumbani kwa kaka yake Lukasi. "Lakini ndio hivyo nguvu ya mapenzi yangu kwa Rozi ndio ilinifanya mpaka nibakie, na kuona bora twende tukapange chumba ili kuepuka usumbufu" aliendelea kujisemea Japhet huku akijifuta machozi. Rafiki yake Mussa bado alikuwa naye bega kwa bega katika kumliwaza na kumfariji rafiki yake huyu (Japhet) Baada ya kukamilisha zoezi la kutoa heshima za mwisho (Kuaga) kwa miili ya marehemu hao sasa safari ya kuelekea mkoani Dodoma kwa mazishi ikaanza na Bahati nzuri Lukasi pamoja na mkewe Flora wote walikuwa wanatokea mkoa mmoja isipokuwa vijiji tu ndio tofauti hivyo Mabasi mawili madogo aina ya (COSTA) yalitumika kubeba msiba na waombolezaji. Japhet akiwa yupo njiani akielekea mkoani Dodoma kumzika kaka yake Lukasi pamoja na Shemeji yake Flora. JJaphet alikuwa anawaza na alijua kwa vyovyote vile huko ataulizwa na ndugu nini chanzo cha vifo hivyo. Na kibaya zaidi kinachomchanganya Japhet ni huku kutakiwa kuripoti kituoni (Polisi) pindi akirudi kutoka mazishini akaungane na mpenzi wake Rozi kwenye mahojiano. Wakati Japhet akiendelea kuwaza juu ya jambo hilo Mara ghafla akapata wazo. Wazo lenyewe ni kutoroka na kukimbilia sehemu isiyojulikana baada ya kumaliza mazishi. "Yes ngoja nikimbie nimuachie Rozi peke yake hii kesi ya kujibu" Japhet alijisemea moyoni na kuona hiyo ni njia bora zaidi kuyaepuka maswali ya Polisi!.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**************
Wakati Japhet akiendelea kuwaza juu ya jambo hilo Mara ghafla akapata wazo.
Wazo lenyewe ni kutoroka na kukimbilia sehemu isiyojulikana baada ya kumaliza mazishi. "Yes ngoja nikimbie nimuachie Rozi peke yake hii kesi ya kujibu" Japhet alijisemea moyoni na kuona hiyo ni njia bora zaidi kuyaepuka maswali ya Polisi.
Lakini wazo hilo la kutaka kukimbia na kutoroka Japhet hakutaka kulipa nafasi kabisa ndani ya Akili yake. Kwani alijua kama endapo atafanya hivyo kukimbia basi anaweza kujitafutia matatizo zaidi.
"Acha tu nimalize kuzika halafu nirudi mjini nikaripoti kituoni wakanihoji na mimi" Japhet alijisemea ndani ya moyo wake. Mpaka kufikia hapo mawazo yake yakaenda mbali sana Kwani pia akuacha kumuwaza Rozi binti ambaye alimuona kama vile anateseka huko Mahabusu ya Polisi anaposhikiliwa kwa mahojiano zaidi. "Yote haya ameyasabisha Shemeji Flora, endapo kama angenipotezea basi sidhani kama kaka Lukasi angeweza kuhisi kitu kati yetu" Japhet aliendelea kujisemea kimoyomoyo huku lawama zote akimtupia Shemeji yake huyo (Flora) ambaye kwa muda huu alikuwa tayari ni marehemu. "Kulazimisha kwake mapenzi kwangu hatimaye ndio hivi sasa kumeleta balaa mpaka kupelekea vifo vya ghafla" Japhet alijisemea moyoni huku akijifuta machozi yaliyokuwa yakimtiririka.
Wakati Japhet akiendelea kutafakari hayo huku safari ya kuelekea Dodoma kumzika kaka yake (Lukasi) ikiendelea baadhi ya waombolezaji ambao wengi wao ni ndugu na jamaa bado walikuwa na Sintofahamu ya kujiuliza maswali yasiyo na majibu. Wengi walikuwa wanajiuliza nini kisa na mkasa kilichotokea mpaka Lukasi kaka yake Japhet akafikia hatua ya kumuua mkewe Flora na halafu pia na yeye kujiua. Hilo ndio swali ambalo liliwaumiza vichwa wengi bila ya majibu.
Hisia za wengi walipata kuhisi labda itakuwa ni wivu wa kimapenzi ndio uliosababisha ugomvi wao kabla ya kifo kutokea mwishoni. Japhet alionekana ndie mwenye majibu ya maswali yote yaliyokuwa yanawasumbua wengi hivyo kwanza walimuacha mpaka wamalize kuzika halafu ndio wamuulize na awape majibu ya hayo maswali yao.
Hatimaye kwenye majira ya usiku sana ndio walikuwa wanawasili Dodoma mpaka kijijini kabisa kwa akina Japhet. Kwa kuwa Dar es salaam walitoka majira ya jioni ndio maana waliweza kufika muda huo wa usiku. Gari hiyo aina ya COSTA ambayo ndio ilikuwa imetumika kusafirisha msiba pamoja na waombolezaji iliposimama mbele ya uwanja wa nyumbani kwa wazazi wa Japhet vilio viliweza kusikika japokuwa ilikuwa ni usiku lakini huzuni na majonzi vilipata kutawala maeneo hayo. Jeneza lenye mwili wa Lukasi lilipoteremshwa kwenye gari na kuingizwa ndani ya nyumba Japhet aliwashuhudia wazazi wake wakilia kwa uchungu mwingi sana wakimlilia kijana wao Lukasi ambaye ndio alikuwa ni tegemeo na mwenye msaada.
Japhet alijisikia vibaya sana na kujiona kama vile ndio yeye msababishaji wa kifo cha kaka yake. "Ni bora hata ningekataa kufanya mapenzi na Shemeji, labda haya yasingetokea" Japhet alijisemea moyoni kwa huzuni halafu akaungana pamoja na wazazi wake kuomboleza msiba huo wa kaka yake huku wakisubiria asubuhi ipate kufika wafanye mipango ya mazishi.
Mwili wa Flora nao ulisafirishwa mpaka kijijini kwao kwa kuwa mkoa ulikuwa ni mmoja huohuo wa Dodoma isipokuwa vijiji tu ndio vilikuwa ni tofauti na kule kwa akina Japhet. Baada ya kufika hapo kijijini nyumbani kwa wazazi wa Flora ndugu na jamaa na wao pia walikuwa wanasubiria asubuhi ifike ndio mpango wa kumzika mpendwa wao Flora upate kufanyika yaani ilikuwa ni huzuni tupu.
Asubuhi ya siku nyingine mpya ikaweza kufika na baada ya taratibu zote kuweza kukamilika ikiwemo wazazi na ndugu wengine waliokuwa wapo huku kijijini nao kumuaga marehemu Lukasi kaka yake Japhet sasa moja kwa moja mwili wake ukapelekwa makaburini kuzikwa. Kwa hakika hiyo ilikuwa ni siku mbaya sana kwa kijana Japhet kuona kaka yake aliyekuwa anamtegemea kwa kila kitu na hata kumuahidi kumtafutia kazi na mambo mengine mengi ya kimaisha leo ndio anazikwa eti kwa sababu tu ya upuuzi wa siku moja alioufanya na Shemeji yake Flora mke wa kaka yake huyo wakati alipokuwa yupo safarini. "Daah siamini kama Utamu wa Shemeji leo umegeuka kuwa uchungu kwangu, pumzikeni kwa Amani huko muendako" Japhet alisema huku akiweka mashada ya mauwa kwenye kaburi la kaka yake Lukasi Mara baada ya kufukiwa. Wakati Lukasi huku akiwa anazikwa na mkewe Flora naye alikuwa anazikwa huko kijijini kwao alipokuwa anatokea Flora.
Baada ya hapo waombolezaji wote wakaweza kurudi nyumbani kuendelea na taratibu zingine za kumalizia msiba. Japhet mpaka muda huo bado alikuwa na wasiwasi vipi kuhusu Rozi kule mjini kituo cha Polisi anaposhikiliwa kwa ajili ya mahojiano. "Sijui Rozi atakuwa amewaambia ukweli wote wale maaskari kuhusu kifo cha kaka pamoja na Shemeji?" Japhet alijiuliza mwenyewe na jibu asilipate asilani. "Na hapa nyumbani napo wakitaka kufahamu ukweli juu ya vifo vile nitawaambia nini" Japhet bado alizidi kupagawa hakujua hata aseme nini kwa wakati huu ukiachana na huko Polisi ambapo pia anatakiwa aende akahojiwe.
Kwa kuwa kifo cha Lukasi na mkewe Flora kilikuwa kimeleta taharuki kwa familia zote mbili yaani familia ya akina Lukasi pamoja na ya mkewe Flora. Hivyo ndugu na jamaa wa upande wa akina Flora nao baada ya kukamilisha mazishi waliweza kuja mpaka kijijini nyumbani kwa akina Japhet wakiamini hapa labda wanaweza kuupata ukweli wote juu ya vifo vya wanandoa hao. Ukizingatia Japhet ndio mtu pekee ambaye ndie alikuwa anaishi nyumba moja na marehemu hao kabla hawajafariki dunia.
Kikao cha kifamilia kiliweza kuitishwa Mara moja na Japhet akawekwa mtu kati apate kutoa maelezo ya nini kilitokea.
"Hayaa Japhet kijana wetu tunajua kama wewe ndie ndugu pekee uliyekuwa unaishi pamoja na marehemu kaka yako na Shemeji yako, hivyo tunaomba hapa utuambie nini kimesababisha mpaka ugomvi ukaweza kutokea na kaka yako akamuua mkewe na halafu yeye pia kujiua?" Mjomba wa Japhet aliyepewa dhamana ya kuendesha kikao hicho alianza kumchachafya Japhet. Kwa upande wa Japhet mwenyewe hakujua hata aeleze nini hapa kwa wanandugu ili apate kueleweka mwisho akaamua kujitetea. "Ni sawa inajulikana hivyo kuwa nilikuwa naishi nyumba moja na marehemu kaka pamoja na Shemeji, lakini mimi siku za hivi karibuni nilikuwa nimehama nyumbani kwao nina maisha yangu ya kujitegemea" Japhet alisema ili kujivua na msala huo. Baba yake Japhet akaingilia kati: "Hilo la kusema umehama nyumbani kwa kaka yako sisi hatulijui kabisa, tunachojua wewe ulikuwa unaishi na kaka yako tuambie nini kilitokea?" Baba yake Japhet alisema na watu wote wakamuunga mkono kumsapoti.
"Lakini baba mimi sijui nini chanzo cha ugomvi wa kaka na Shemeji mpaka wakafikia hatua ya kuuana" Japhet alisema. Mjomba wake naye akauliza:
"Sasa nani anajua hicho chanzo cha ugomvi wao?" Mjomba aliuliza. Japhet akajifikiria kidogo halafu akasema: "Mimi pia sijui labda mwenye majibu hayo ni yule binti aliyekuwa anawasaidia kufanya kazi za ndani" Japhet alisema. Wanandugu wakabaki wanajidaliana pale kidogo halafu mjomba wake na Japhet akauliza tena: "Sawa tumepata taharifa za huyo binti kuwa anashikiliwa kituo cha Polisi kwa mahojiano zaidi, lakini pia kesho tutaenda wote mpaka huko mjini pamoja na wewe hadi kituoni ili kujua huyo binti amesema nini kwa maaskari pia tunaomba utuambie ni kwanini ulihama nyumbani kwa kaka yako?" Mjomba wake alimuuliza Japhet na watu wote kwenye hicho kikao cha kifamilia walikuwa wanasubiri kujua nini sababu ya Japhet kuhama ghafla nyumbani kwa marehemu kaka yake na Shemeji yake.
Japhet hapo alibakia ameduwaa na kujiuliza ataanzaje kusema ukweli kuwa eti alihama kumkimbia Shemeji yake Flora aliyekuwa anamsumbua kwa kumtaka kimapenzi? Hilo Japhet akaona haliwezekani kusema mbele ya familia.
Japhet akabakia kimya anakuna kichwa.
"Tunasubiri jibu lako Japhet, tuambie ni kwanini ulihama nyumbani kwa kaka yako?" Mjomba alizidi kumkomalia.
"Mimi niliamua kuhama nyumbani kwa kaka pamoja na Shemeji, ili niende nikaanze maisha yangu ya kujitegemea na sio vinginevyo" Japhet alijbu kwa kujiamini. "Ok basi hakuna shida maelezo yote tutaenda kuyajua hiyo kesho baada ya kufika mjini ndio tutajua na huyo binti ameeleza nini huko kituoni" Mjomba alisema na kikao kikaweza kufungwa.
Japhet licha ya kujitetea hapa mbele ya wanandugu na kujisafisha asionekane kama yeye ndio chanzo cha ugomvi wa marehemu kaka yake na mkewe Flora baada ya kuwahisi wana mahusiano ya kimapenzi. Hofu yake Japhet ilikuwa ni kwa Rozi huko kituoni anaposhikiliwa endapo kama atakuwa amewaambia ukweli maaskari juu ya tukio lilivyokuwa.
Japhet alizidi kuchoka baada ya kugundua na yeye pia atatakiwa kutoa maelezo yatakayofanana na maelezo ya Rozi ili kuondoa utata juu ya kifo cha kaka yake pamoja na Shemeji yake Flora ambao ugomvi wao mpaka uliopelekea vifo ukidaiwa ni wivu wa kimapenzi.
Kijana Japhet alijikuta anapagawa zaidi!.
Kijana Japhet alijikuta anapagawa zaidi.
Basi hakuwa na ujanja tena wa kufanya kitu chochote Kwani ndio vile lile wazo la kukimbia pale mwanzo alishalikataa. Na sasa alichokuwa anakisubiri ni kurudi tu mjini na kwenda kuripoti kituo cha Polisi kama alivyotakiwa na wale maaskari waliokuja kufanya uchunguzi kule mjini nyumbani kwa marehemu kaka yake Lukasi wakati alipomuua mkewe Flora na halafu pia na yeye kujiua. Usiku ukaweza nao kuingia baada ya shughuli na pilika za msiba zote kukamilika waombolezaji wakalala wakisubiri asubuhi ya siku inayofuatia waanze safari ya kurudi tena Dar es salaam Kwani kama ni shughuli ya mazishi iliyowaleta Dodoma kumzika Lukasi pamoja na mkewe Flora walikuwa wameshaimaliza. Japhet usiku huo hakuweza kupata usingizi wa kueleweka mawazo yake yote alikuwa anafikiria ni jinsi gani atakapofika mjini atavyotoa maelezo yake mbele ya Askari Polisi.
"Sitakiwi kuwa na uoga kupita kiasi kama ingekuwa ni tatizo sana basi na mimi pia wangenikamata kama walivyofanya kwa Rozi, na wasingeniruhusu kuja kuzika" Japhet alijisemea moyoni na kujifariji.
Basi akapitiwa na usingizi mzito akalala.
Asubuhi ya siku nyingine ikaweza kufika na baada ya kuamka zikafanyika taratibu nyingine ndogondogo za hapo nyumbani na baada ya hapo safari ya kurejea tena mjini Dar es salaam ikaanza huku ndugu muhimu nao wakiwemo kama vile wazazi wa Japhet baadhi ya ndugu wengine wao walibakia kijijini hapo wakimalizia msiba (Matanga) kama inavyotakiwa kimila.
Kwenye Majira ya jioni ndio waliweza kufika salama kabisa mjini Dar es salaam moja kwa moja safari ikahitimishwa pale pale nyumbani kwa marehemu Lukasi na Flora ambapo ndio palipotokea msiba.
Baada ya kufika hapo wakaingia ndani ya nyumba hiyo huku kila mmoja akiwa yupo na huzuni moyoni mwake akikumbuka wahusika wakuu wa nyumba (Lukasi na mkewe Flora) ndio hivyo hawapo tena hapa duniani. Kwa upande wa Japhet yeye maumivu ndio yalimzidi maradufu.
Basi baada ya hapo kama inavyokuwa marehemu akishazikwa na msiba tena nao ndio unahesabika umeisha. Hivyo ndugu na jamaa baadhi yao kila mmoja akaenda nyumbani kwake kupambana na maisha yake kwa ajili ya familia yake. Hapo kwenye nyumba ya nyumba ya Lukasi walibakia wazazi wa marehemu Lukasi pamoja na mjomba bila kumsahau na Japhet mwenyewe naye alikuwepo huku ndugu wa marehemu Flora alibakia kaka pamoja na dada yake (Flora) baada ya hapo kikaitishwa tena kikao kidogo cha kifamilia kujadili ni nani ambaye atakuwa anasimamia hapo nyumbani na kuangalia vitu vyote vilivyoachwa na hao wapendwa wao waliotoka kuwazika. Kwa kuwa Lukasi na Flora hawakubahatika kuwa na mtoto katika maisha yao yote ya ndoa basi Japhet akapendekezwa kuwa ndio atakuwa msimamizi mkuu wa Mali za marehemu kaka yake. Hakukuwa na aliyepinga wazo hilo wote wakakubaliana na maamuzi hayo. "Kesho asubuhi wote tutaenda huko kituoni kusikiliza kama Polisi wameweza kubaini chochote juu ya chanzo cha vifo vya ndugu zetu" Mjomba wa Japhet alisema. Japhet naye akapata muda wa kutafakari na kupanga ni jinsi gani ataenda kujibu maswali ya Polisi hao watakapokuwa wanamuhoji kituoni. Baada ya kuoga na kumaliza kula chakula wote wakaingia vyumbani kulala huku Japhet akienda kulala na kaka yake Flora kwenye kile chumba chake alichokuwa analala hapa kabla ya kuhama. Japhet alikumbuka mengi sana na kuwaza ni vipi ataweza kuishi bila ya kaka yake (Lukasi) Kwani ndio alikuwa ni tegemeo na msaada Mkubwa sana kwake. "Kweli nimepata pigo maishani kuondokewa na kaka yangu, naomba Mungu anisamehe kwa dhambi ya usaliti niliyoifanya na Shemeji yangu mpaka ikasababisha lile balaa" Japhet alijisemea moyoni kwa huzuni. "Nikifanikiwa kumaliza hili jambo salama, kuanzia kesho nitaenda kanisani na nitatubu dhambi zangu zote kwa Mungu na kuokoka kabisa!" Japhet alijiapiza ndani ya moyo wake. Ndio hivyo tena maji yakimwagika hayazoleki yote yaliyotokea ndio tayari yameshatokea yanabakia kuwa majuto ndani ya Nafsi.
Asubuhi ikafika na wote wakaamka Pole pamoja na rambirambi za majirani wa hapo mtaani walizidi kuzipokea kwa wingi. Muda wa kwenda kituoni ulipofika Japhet pamoja na baba yake na mjomba wake bila kumsahau na yule kaka wa Flora wakaingia kwenye gari ya mjomba wake na Japhet wakaanza safari ya kuelekea kituoni kusikiliza kama Rozi atakuwa amesema kitu chochote labda cha kuwasaidia kujua nini kilisababisha mpaka marehemu walikuwa na ugomvi mpaka kufikia hatua ya kuuana. Japhet japo alikuwa anajua kila kitu ambacho kilitokea lakini aliamua 'kupiga kimya' (Kunyamaza) mpaka atakapofika huko kituoni kusikiliza Rozi atakuwa ametoa maelezo gani. Baada ya kufika mpaka kituoni moja kwa moja wakaingia ofisini kwa Askari anayeshikilia kesi hiyo na baada ya kuonana na Askari huyo wakaanza mazungumzo rasmi. "Ndio Bwana Afande sisi tumerejea kutoka mazikoni, vipi yule binti ameweza kusema chanzo cha tukio?" Mjomba wa Japhet alimuuliza huyo Polisi.
"Kwanza nawapeni pole nyingi sana kwa kuondokewa na wapendwa wenu, hapa sisi kwa upande wetu tumeshindwa kujua nini chanzo kilichopekea mpaka wale wanandoa kuwa na ugomvi ambao ndio uliosababisha vifo vyao" Polisi huyo alitoa maelezo kwa kirefu sana. "Sawa je yule binti aliyekuwa anafanya kazi za ndani kule nyumbani kwao naye amesemaje?" Baba yake Japhet naye aliuliza.
"Kusema ukweli tangu yule binti tulipomchukua kwa ajili ya mahojiano naye amesema hajui kitu chochote juu ya ugomvi Kwani aliwasikia tu wanagombana na baadae yeye kufungiwa chumbani kwa ndani mpaka alipokuja kufunguliwa mlango na majirani" Polisi huyo alisema. Hapo kidogo hata Japhet akajikuta anapata afueni kwa kusikia hivyo. "Duuh siamini kama Rozi ameweza kuepusha hii kesi kwa kuficha siri" Japhet alijisemea moyoni na kumpongeza Rozi.
"Kwahiyo Bwana Afande ndio tufanye imeshindikana kabisa kujua hata chanzo cha ugomvi wao wale marehemu?" Kaka yake Flora akauliza. Afande akakohoa kidogo na halafu akasema: "Kiukweli labda niseme tu imeshindikana, na ndio maana sisi kama Polisi tulihitaji na huyu kijana aje hapa baada ya kumaliza kuzika tumuhoji, kwa kuwa yeye ni mdogo wa marehemu labda anaweza kujua kitu chochote" alisema Polisi huyo huku akimuangalia usoni Japhet. Kijana Japhet mapigo ya moyo yakaanza kumwenda mbio. "Lakini hata na huyu kijana pia anaweza akawa hajui kitu, Kwani yeye alihama pale nyumbani kwa kaka yake na kwenda kuanza maisha ya kujitegemea" mjomba wake Japhet alisema na kumtoa kabisa Japhet kwenye kesi hiyo bila ya kujua. Bwana Afande akakuna kichwa na halafu akauliza: "Ok kama ni hivyo basi hakuna tena sababu ya kumuhoji, sasa vipi kuhusu huyu binti tunaemshikilia hapa kituoni maana tulikuwa tunawasubiri nyinyi ndugu mfike kutoa kauli yenu ya mwisho?" Afande aliuliza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nafikiri huyo binti tunawaombeni mumuachie huru Kwani ahusiki na tukio hilo zaidi ataendelea kuteseka tu bure" Baba yake Japhet alisema hivyo. Basi na ndio ilivyokuwa Rozi aliachiwa huru na Faili la kesi hiyo likafungwa hapohapo hakukuwa tena na mahojiano kwa Japhet na mchezo ndio ukaishia hapo. Siri ya kifo cha Lukasi na mkewe Flora inabakia kuwa ni ya Rozi na Japhet pekee labda na marehemu wenyewe walioamua kwenda nayo kaburini bila hata kuacha ushahidi wa maandishi kusema nini chanzo.
Rozi na Japhet walishindwa kabisa kuzuia hisia zao baada ya kuonana wote wawili wakajikuta wanakumbatiana kwa furaha na kuonyeshana Mahaba hadharani. Watu wazima hapo wakapata kuhisi kitu kinachoendelea hivyo tena hakukuwa na muda wa kujadili chochote safari ya kurudi nyumbani ikaanza huku wakiwa pamoja na Rozi ndani ya gari Japhet hakuweza kuamini kabisa kama hili jambo lingeisha kirahisi namna hiyo.
Baada ya kufika nyumbani Rozi akajifanyia usafi wa mwili wake pamoja na mavazi na baada ya muda mfupi tu akapendeza na kuwa mrembo zaidi.
"Binti kwanza tunakuomba sana msamaha kwa kitendo cha wewe kushikiliwa na Polisi haijamaanisha kuwa wewe ndio muuaji, Bali ni sheria ndio imefanya hivyo ili kutaka kuubaini ukweli" baba ya Japhet alisema. Rozi akajikuta anatabasamu na kusema: "Wala usijali kabisa baba hayo kwa upande wangu tayari yameshapita, nawapeni pole sana kwa kufiwa na wapendwa wenu huku na mimi pia nikihuzunika kwa kuwapoteza mabossi wangu walionijali na kunithamini" Rozi alisema kwa hisia Kali huku machozi yakimlengalenga machoni.
"Ndio hivyo tena binti yote kwa yote inatubidi tumshukuru Mungu hatuna wa kumlaumu, Je vipi baada ya kufariki kwa mabossi wako upo tayari kuendelea tena kuishi hapa au utahitaji kuondoka?" Mjomba wake Japhet alimuuliza Rozi.
Rozi akatabasamu na kumgeukia Japhet akamuangalia usoni halafu akasema:
"Kuhusu hilo nilikuwa naombeni kidogo nikajidiliane na Japhet halafu nitakuja kutoa jibu" alisema Rozi na kuwafanya watu wote hapo wapigwe na butwaa na kujiuliza ni nini hicho wanachotaka kukijadili. "Hayaa Bwana Japhet binti hapo anataka mkajadiliane kidogo, sasa sijui tutoke nje tuwapeni nafasi?" Mjomba aliuliza huku akitabasamu na kumuangalia Japhet usoni alishahishi kitu. "Hapana sisi ndio tutatoka halafu tutarudi tena hapa sebuleni baada ya muda mfupi" alisema Rozi na hapohapo bila ya kuchelewa akamshika mkono Japhet na kuondoka naye kuelekea chumbani kwake. Japhet alijikuta anashindwa hata kuzuia hili jambo na kumfuatisha Rozi vile anavyotaka. Moja kwa moja wakaenda mpaka kwenye chumba alichokuwa analala Rozi hapo mwanzoni na Rozi akafunga mlango kwa ndani. "Rozi kwanini sasa mpenzi wangu umenileta huku chumbani, si tungeongea palepale sebuleni mbele ya wazee!?" Japhet aliuliza. Rozi akatabasamu na halafu akasema: "Nataka kuisikia kauli yako Japhet, Je mpaka muda huu bado unanipenda?" Rozi alimuuliza Japhet.
"Ndio Rozi mimi bado nakupenda sana" Japhet alijibu. Rozi akafurahi kusikia hivyo halafu akauliza tena: "Vipi sasa tutaishi hapa au tutaenda kuishi kule ulipohamia?" Japhet bila ya kupoteza muda akasema: "Tutaishi wote hapa vile vyombo alivyoninunulia kaka Lukasi kule tutavihamisha, nimechaguliwa kuwa msimamizi wa Mali za kaka yangu" alisema Japhet. "Oohoo kama ni hivyo basi ni vizuri baby ,," alisema Rozi kwa furaha na hapohapo akamrukia Japhet mwilini na kumkumbatia. "Basi taratibu mpenzi wangu inatosha, twende kwa wazee sebuleni tukawape jibu" alisema Japhet huku akijaribu kumuondoa Rozi mwilini mwake. "Sawa baby nimekuelewa lakini mwenzio nna hamu ya ,,,, nimemiss sana Penzi lako jamonii" alisema Rozi huku akimrembulia macho yake Japhet na kuzidi kumkumbatia kwa Mahaba.
"Vumilia mpenzi taratibu, hata na mimi pia nimelimiss sana Penzi lako, usijali tutafanya baadae ,," alisema Japhet ili kumtuliza Rozi. Lakini wapi Rozi hakukubali kumuachia hivihivi kijana huyo akamvuta na kumpeleka Kitandani taratibu huku akimnyonya denda Japhet!.
"Vumilia mpenzi taratibu, hata na mimi pia nimelimiss sana Penzi lako, usijali tutafanya baadae ,," alisema Japhet ili Rozi. Lakini wapi Rozi hakukubali kabisa kumuachia hivihivi kijana huyo akamvuta na kumpeleka Kitandani taratibu huku akimnyonya denda Japhet.
Hapo sasa ikabidi Japhet atumie nguvu ya ziada kujinasua kwenye himaya ya binti huyo aliyeonekana kuwa tayari Mizuka yake ya 'Kingono' imeshampanda.
"Rozi nimekuambia baadae tutafanya, sasa kwanini hautaki kunielewa?" Japhet aliuliza kwa sauti ya ukali kidogo.
"Sio kama sitaki kukuelewa baby, unajua mwenzio hapa nilipo nimezidiwa na Nyege ,," Rozi alisema kwa kubana sauti.
"Sawa hata kama umezidiwa, kwahiyo ndio unataka tufanye Mapenzi saa hizi huku wazee kule sebuleni wakitusubiria sasa ndio tutainjoy vipi hayo Mapenzi?" Japhet alimuuliza Rozi. Basi tena ikabidi Rozi akubaliane na alichokisema Japhet kuwa kwa muda huo sio vyema kufanya hayo mambo na wakati huko sebuleni bado kuna kile kikao cha kifamilia kilichokuwa kinaendelea hivyo wazee wangeweza kuwahisi vibaya kwa ukimya wao huku chumbani. "Lakini baby ujue umenikata stimu we basi tu ," alisema Rozi kwa kulalamika huku akiirekebisha vizuri Blauzi yake. Japhet akacheka kidogo na halafu akasema: "Sio wewe tu peke yako, hata mimi huku pia nina hali mbaya kinoma hebu angalia mwenyewe" alisema Japhet kwa Utani huku akifungua zipu ya suruali yake na kulichomoa kwenye boksa 'Gobole' lake lililokuwa limedinda ile kiroho mbaya mpaka Yale majimaji mepesi ya 'Mlenda' kuchuruzika.
Rozi kitendo tu cha kuliona hilo 'Gobole' la Japhet akajikuta maruhani yake ya kimahaba yanampanda upya mwilini.
"Kwahiyo ndio umeamua kunilingishia huo Utamu wako si ndio enhe?" Rozi aliuliza huku akijilamba midomo yake kwa matamanio. Japhet akalirudisha tena 'Gobole' ndani ya boksa halafu akasema:
"Sio kama nimekulingishia, nimekuonyesha ili ujue hata na mimi huku nipo na hali mbaya moto hauzimi" alisema Japhet kwa masihara. Wote wawili wakajikuta wanaangua kicheko kidogo cha chinichini halafu wakatoka humo ndani chumbani na kuelekea tena sebuleni kulipokuwa na kikao kurudisha majibu. "Enhe vipi maamuzi ya binti yanasemaje?" Mjombake Japhet aliuliza.
"Kusema ukweli binti ameamua kubakia hapa na tutaendelea kuishi naye kama zamani" Japhet alisema kwa kujiamini.
"Ni vizuri kama ameamua na kukubali kuishi hapa, Je tungependa kujua katika kipindi chote alichokuwa anaishi huku ndani alikuwa na deni lolote na mabossi wake ambao hivi sasa ni marehemu?" Mjomba aliuliza tena. Rozi akatabasamu na kusema: "Kiukweli mimi sina deni lolote nililokuwa nawadai, Kwani pesa yangu ya mshahara walikuwa wananilipa kwa wakati na hata kama lingekuwepo deni ningesamehe nimeishi nao vizuri" alisema Rozi. Maneno hayo ya Rozi yalionyesha kumfurahisha kila mtu hapo na kumuona kweli ni binti mwenye busara. "Ok tunakupongeza sana binti, lakini pia tungependa kujua kwa kipindi utakachokua unaishi hapa tukuchukulie kama ni mwanafamilia au mfanyakazi?" Mjomba aliuliza swali lenye mtego. Hapo Rozi akajikuta anabakia kimya bila kujua atoe jibu gani. Japhet akaingilia kati na kumjibia swali hilo kwa mjomba. "Binti huyu ataishi hapa kama vile mke wangu mtarajiwa Kwani nampenda sana, hivyo tunaombeni mtupatie Baraka zenu" Japhet aliamua kuupasua ukweli wote na kuyaweka hadharani mahusiano yake yeye na Rozi. Makofi ya furaha yakaweza kupigwa na kuwapongeza sasa wakawa wametoka kwenye huzuni ya msiba na kuingia kwenye furaha. Basi Basi wazazi wa Japhet wakaweza kutoa Baraka zao kwa wawili hao na kuwasisitiza sana kama wameamua kupendana kweli kwa Dhati na wapendane wafunge ndoa ili waishi kihalali. Kikao ndio kikaishia hivyo wale ndugu wa Flora wakaaga na kuondoka bila hata ya kuchukua kitu chochote cha ndugu yao huyo (Flora) zaidi tu dada yake akasema yeye ndie atakaesimamia ile Saloon ya kike ambayo marehemu Flora alikuwa ndio anaimiliki. Basi mambo ndio yalienda hivyo mjomba wa Japhet naye akaondoka na kurudi nyumbani kwake. Hapo nyumbani kwa Lukasi akabakia Japhet na mpenzi wake Rozi pamoja na wazazi wa Japhet. Rozi akamshauri Japhet awashawishi wazazi wakubali kuishi hapo na wasirudi tena kuendelea na maisha ya kule kijijini. Wazazi wake Japhet wakakubali kuishi nyumbani hapo maisha ya furaha yakaendelea.
Majira ya usiku Japhet na Rozi wakiwa wapo chumbani kitandani wamelala ndipo Japhet akasema Yale mawazo yake aliyowaza ya kwenda kanisani kutubu dhambi zake mbele ya Mungu Kwani kila anapokumbuka ile dhambi ya usaliti aliyoifanya na Shemeji yake Flora anaona Kama vile amemkosea sana kaka yake (Lukasi) kwa kufanya Mapenzi na mkewe huyo. "Sawa baby hilo ni wazo zuri sana la kwenda kujitakasa mbele ya Mungu, lakini usihuzunike sana kumbuka ni Shemeji yako ndio alieanza kukutaka" Rozi alisema. "Hata kama ni Shemeji ndio alinitaka lakini dhambi ya uzinzi bado itaniandama, yule alikuwa ni Shemeji yangu na nilipaswa kumuheshimu na yeye pia aniheshimu angalia sasa haya mambo yaliyotokea mwishoni mpaka kugharimu maisha yao" Japhet alisema kwa huzuni.
"Na wewe naye ulizidisha mautundu kwa Shemeji yako, mpaka akanogewa na kumsahau Mumewe akajikuta sasa anautaka Utamu wa Shemeji" Rozi alisema kwa utani akimtania hivyo Japhet. Wakaishia kucheka tu maana mambo Yale sio ya kuyakumbuka ni mabaya sana. Rozi naye akaanza kuleta uchokozi kwenye mwili wa kijana Japhet ambaye alimuelewa vizuri na kuanza kumpa ushirikiano binti huyo. Japhet kama kawaida yake akayavamia matiti ya Rozi ambayo mara nyingi huwa anapenda kuyatomasa na kunyonya chuchu zake. Ndani ya muda mfupi mtoto wa kike Rozi alikuwa yupo ndembendembe akisubiria Dozi ya kusuguliwa na 'Gobble' la kijana huyo. Japhet akaingia mzigoni na kumpa huduma hiyo muhimu ya kimwili binti huyo (Rozi) na kumuacha akiweweseka Kimahaba na raha alizokuwa anazisikia. Usiku huo ukapita kwa wawili hao kupeana Mapenzi na Mahaba motomoto kuridhishana na kukata Kiu ya miili yao wote kwa pamoja. Asubuhi baada ya kuamka na kufanya shughuli ndogondogo za hapo nyumbani ikiwemo na kunywa Chai ya kifamilia pamoja Japhet na Rozi wakawaaga wazazi na kwenda Kanisani kutimiza ahadi ya kutubu dhambi mbele ya Mungu kama vile walivyokuwa wamepanga Japhet na Rozi japo kwa wazee hao walificha kusema hicho kitu ambacho kinawapeleka huko Kanisani.
Siku zilizidi kwenda hatimaye miezi sita ikaweza kupita maisha ya furaha yalizidi kutawala ndani ya nyumba. Japhet akarithi biashara alizokuwa anafanya marehemu kaka yake (Lukasi) hapo mwanzoni kwa kupitia msaada wa Marafiki wa kaka yake huyo ambao walimsaidia sana Japhet kumuongoza kibiashara na kufanya kama vile alivyokuwa anafanya kaka yake wakati alipokuwa bado yupo Hai hajafariki. Hivyo Japhet akamudu na kujiongezea kipato zaidi cha kuitunza familia yake na mkewe mtarajiwa Rozi ambaye kwa muda huo tayari alishapata Ujauzito wa kijana huyo (Japhet) na kuwazidishia furaha kwenye maisha yao. Pia Rozi akampeleka mpenzi wake Japhet mpaka kijijini kwao kwa wazazi wake kumtambulisha na huko pia wakapata Baraka za wazazi wa Rozi na baada ya Mwaka mmoja kupita mbele wakaweza kufunga Ndoa kubwa sana ya kifahari na maisha ya furaha kwa upande wao Rozi kwa muda huo wote alikuwa tayari ameshajifungua watoto wawili mapacha huku mmoja akiwa ni wa kiume na mwingine wa kike Ndoa yao ilizidi kuwa tamu. Mussa yule rafiki yake Japhet na Japhet naye alikuwa yupo karibu zaidi na familia ya Japhet huku wakishirikiana kwenye mambo mbalimbali ya kifamilia na pia kibiashara. Japhet vile vitu vyote alivyonunuliwa na marehemu kaka yake wakati alipoaga anaenda kuanza maisha ya kujitegemea alivitunza na kuvifanya kuwa ni kumbukumbu kubwa maishani mwake. Na hata pia zile zawadi alizowahi kupewa na Shemeji yake (Flora) nazo pia alizitunza. Maisha ndio yalienda hivyo.
"Japhet Mume wangu, nakuomba katika maisha yetu tujitahidi sana kuepuka neno Usaliti katika Mapenzi yetu, tujifunze kwa kupitia mkasa uliowahi kututokea wa kumpoteza Shemeji yangu Lukasi na mkewe Flora" Rozi alisema akimwambia Japhet na kumkumbushia lile tukio baya.
Japhet akatabasamu halafu akasema:http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ni kweli Mke wangu unachosema Usaliti haufai katika Mapenzi Kwani madhara yake ni makubwa sana" alisema Japhet.
Basi wakaendelea na maisha yao kwa Raha Mustarahe huku Amani ikitawala.
Huku pia mara kwa mara wakienda kuyatembelea makaburi ya Lukasi pamoja na Mkewe Flora kama vile kuwaenzi!.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment