Chombezo : Ni Shiida!
Sehemu Ya Tatu (3)
"Una uhusiano na nani?"
"Mimi?"
"Wewe ndiyo, mwingine nani?"
"Sina."
"Si kweli. Ile hereni ilikuwa pale iko wapi?"
"Hereni gani?"
"Pale chini palikuwa na hereni sasa hivi haipo, we umeiokota. Na ndiyo nathibitisha kwamba kweli wewe ulikuwemo ndani."
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Hapana, siijui mbona."
"Nikupapase?"Bitungu hakutaka kupapaswa kwani ni kweli aliiweka hereni hiyo kwenye mfuko wa bukta.
"Ina maana huniamini baby?"
"Ndiyo sikuamini. Tena kuna kitu nafuatilia kama ni kweli mimi na wewe basi."
"Kitu gani tena baby jamani?"
"Nakijua mwenyewe."
***
Mama Juliana alihisi dakika zinakatika binti yake hajarudi, akampigia simu.
Juliana alishtuka sana kuona simu ya mama yake ikiingia kwenye simu yake…
"Huyo ni mama, please naomba subiri kwanza kufanya lolote lile kwa sasa," alisema Juliana ili apokee simu hiyo…
"Mama…"
"Uko wapi wewe?"
Ili ajulikane yupo njiani anatembea, Juliana aliwahi kwenye dirisha na kuongelea hapo ili kelele za nje ya gesti hiyo ziingie kwenye simu na kumfikia mama yake…
"Mama natembea nakuja."
"Na huyo Bitte?"
"Hapana mama, nimemkuta ana kazi nyingi sana lakini atakuja kesho asubuhi sana."
Mama alikata simu, Juliana akamgeukia Bitungu…
"Naomba hiyo hereni Bitungu please."
"Yaani dear hayajaisha tu?"
"Hayawezi kwisha labda uamue kuwa wazi kwangu kuhusu mwanamke aliyekuwemo ndani na uhusiano wake na hiyo hereni uliyoiokota."
"Sikia nikwambie ukweli baby wangu…"
"Nakusikiliza."
"Ni kweli nilikuwa na mwanamke kabla yako. Lakini ni yule mke wa mtu niliyewahi kukwambia kwamba ananing'ang'ania mimi simtaki."
"Ulikuwa naye humu ndani ya chumba hiki?"
"Ndiyo."
"Mnafanya nini?"
"Yeye alichukua hiki chumba, akaniita akisema anataka kunipa kazi nimfanyie ili anipe pesa lakini si suala la mapenzi."
"Amekupa hiyo kazi?"
"Ndiyo.""Kwanza huyo mwanamke anaitwa nani?"
?Mh! Jina lake linanitokaga sana.?
?Kwa nini ushindwe kumjua mtu anayekufuatafuata kila wakati mpaka mnaitana gesti??
?Imetokea tu.?
?Anaishi wapi??
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
?Mwenyewe anasemaga Ilala.?
Moyo ulimlipuka Juliana, alianza kuuona ukaribu wa mama yake kutembea na Bitungu. Alitamani sana kumuuliza lakini alishindwa, akaendelea kutumia maswali ili kumchimba kwa undani.
?Umewahi kufika nyumbani kwake??
?Sijawahi.?
?Ni Ilala gani??
?Sijui Ilala gani!?
?Yukoje??
?Mwanamke f?lani hivi hajatulia ndiyo maana mimi namkataa maana najua nitaangukia pabaya.?
?Ameolewa??
?Hapana, shangingi tu,? alijibu Bitungu kwa kukwepesha ukweli kwani alijua akikubali kwamba ameolewa, ataonekana anacheza na hatari kwa wake za watu lakini hakujua kama jibu hilo lilipunguza kiwango cha mawazo cha Juliana kutaka kumhusisha mama yake.
?Kwa hiyo humu chumbani ulikuwa na huyo mwanamke wako??
?Ndiyo.?
?Umesema ndiye aliyekodi chumba??
?Yes baby.?
?Kwa hiyo mimi umeniingiza kwenye chumba alichochukua mwanamke mwenzangu siyo??
?Juliana, punguza hasira mama, punguza maswali pia, usimuwazie sana huyo malaya, wewe shughulika na mimi tu, mimi ni mumeo mtarajiwa Juliana, mtoto mzuri kama wewe unataka kujilinganisha na mwanamke mtu mzima, mzee yule.?
Maneno hayo yalimpa faraja kubwa Juliana, akajijua tena kwamba kumbe yeye ni mzuri sana na anapendwa pia kumbe anaweza kuwa mke wa mtu ndoto ambazo zimekuwa zikimkaa kichwani muda mrefu kwamba atafurahi sana siku moja atakapobahatika kuolewa na kuwa nyumbani kwake.
Kwa mbali, Juliana alianza kuchangamka huku akipeleka mkono wake kumshikashika mwilini kijana huyo na kuachia tabasamu, akasema?
?Lakini ujue baby mimi ni msichana mwenye wivu mkubwa. Kwa hiyo uwe unaangalia unapotaka kunitenda kwani utakuwa unaniumiza sana.?
?Miye wala sikutendi mpenzi wangu, unajua kama ningekuwa na nia mbaya nisingekuita uje hapa.?
Bitungu naye baada ya kumwona Juliana amelegeza uzi aliitumia nafasi hiyohiyo kuhakikisha wanaangukia kitandani na kuanza mechi ya haraka maana dakika zilikuwa zimekatika sana.
?Jamani, nitalala mwenyewe,? alisema Juliana wakati akipelekwa kitandani?
?Si nakusaidia tu baby wangu jamani na wewe!?
?Nitajisaidia mwenyewe jamani sweet,? alilalamika Juliana kwa sauti isiyokuwa na msisitizo, akaenda kitandani na kuangukia puu!
Macho yalishamlegea, sehemu kubwa ya mwili wake ikawa kitandani huku akianza kuongeza mhemo na mhemko wake. Hali ilikuwa mbaya kwa Juliana?
?Baby njoo basi, si umenitanguliza mwenyewe,? alisema Juliana kwa sauti tamu, sauti nzuri, sauti ya kumtoa mwanajeshi kwenye handaki.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Juliana huyohuyo alimvuta Bitungu kitandani na kuanza kumvua bila kujali tabu zake. Bitungu naye alikuwa akijipindapinda, akijinyonganyonga ili kuruhusu nguo zake kutoka mwilini wakati wa kuvuliwa.
Wote wakawa kama walivyozaliwa, Juliana alimwangalia Bitungu kwa macho malegevu sana, kusinzia si kusinzia, kulala si kulala?
?Baby,? akaita?
?Yes dear.?
?Nakupenda,? alisema Juliana kwa sauti iliyotoka nje kwa kupitia tundu za pua?
?Hata mimi baby nakupenda pia.?
?Kweli baby?? aliuliza Juliana akipeleka mkono na kushika maiki ambapo alianza kuimba nyimbo nzuri za mapenzi huku macho yake yakimwangalia Bitungu usoni hali iliyomchanganya kijana huyo na kujikuta akitetemeka kwa kiu ya kulisataka kabumbu.
?Baby,? aliita tena Juliana?
?Yes??
?Mimi tayari.?
?Tayari nini sweet wangu??
?Aaah! Bwana, unajua namaanisha nini!?
Bitungu alimtega vizuri Juliana na kuanza naye soka huku akitembeza mikiki ya mbali na kumfanya Juliana kuhema sana na kutoa mlio wa kubembeleza kwa mbali.
Kitu kimoja ambacho alikisahau Juliana ni kuacha simu yake palepale kitandani hivyo akailalia. Sasa wakati makasheshe yakiendelea, aliiminya na mgongo, akajikuta anabonyeza vitufe mpaka akafika eneo la namba ya mama yake ambayo alimpigia yeye kwenye ?received call?.
Mama Juliana aliipokea haraka simu ya binti yake akijua huenda kuna tatizo kwani walishatoka kuongea muda mfupi tu uliopita?
?Huyu anasemaje tena?? alijiuliza mwenyewe akiwa anaipokea bila kujua kwamba upande wa Juliana, simu hiyo ilijipiga yenyewe.
?Haloo?? alipokea na kuita?
?Haloo??
?Halooo?wee Juliana!?
Mama Juliana alishtuka wakati akiita kwenye simu, upande wa pili alisikia maneno haya?
?Baby?baby jamani?oooo?.baby??
Alisimama?
?Wewe Juliana??
"Juliana si naongea na wewe?"
"Halooo..."
Alihisi presha ya ajabu kumtembelea, hakutaka kuamini kile alichokuwa akiendelea kukisikia kwenye simu.
Muda wote Bitungu na Juliana bado walikuwa katika mechi ngumu, mechi ilikuwa imeshawazidia kwani tayari walikuwa wamefungana mabao ya kutosha na wapo katika mapumziko ya kipindi cha pili.
Juliana hakushtuka kama ile simu ilikuwa imempigia mama yake, ndiyo kwanza aliendeleza mahaba kwa Bitungu.
"Baby..."
"Sema mpenzi wangu..."
"Tupumzike tuendelee basii, ila leo umeniweza kweli!"
"Tena una bahati leo!"
"Bahati? Bahati wapi wakati kawaida yangu kumaliza mechi na ushindi."
Wakiwa katikati ya maongezi, Bitungu akaiona simu kwa Juliana, simu ambayo Juliana alikuwa ameikalia bila kujitambua kuwa imejipiga na mbaya zaidi imempigia mama yake.
"Mpenzi mbona umeikalia simu..."
"Simu? Simu ipi?"
"Ina maana huijui simu yako, au si ya kwako hiyo?"
Harakaharaka Juliana alijisogeza na kuichukuwa ile simu yake, ilikuwa bado iko hewani kwani maneno yote mama yake alikuwa bado anaendelea kuyasikia. Juliana akaanza kutetemeka sambamba na kuumana meno. Akaikata simu ile na kuanza kuangua kilio kana kwamba yupo msibani.
"Nini tena sweet?"
"Hapana..."
"Hapana nini?
"Niache kwanza, niache tu..."
"Siwezi kukuacha sweet wangu wakati umeiangalia simu yako na kuanza kulia kama ni msiba nijuze kuliko kupeana presha..."
"Bora ingekuwa msiba Bitungu..."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ila! Nini sasa kinachokufanya uendelee kulia tena kwa sauti ya juu hapa na unajua hapa ni gesti?"
"Bitungu, yale yote tuliyokuwa tunafanya na kuongea mama ameyasikia!"
"Unasemaje?"
"Mama ameyasikia yote!"
"Sweet ina maana hukuweka loki kwenye simu yako?"
"Hapana! Wakati tupo kwenye mechi simu yangu ilijipiga yenyewe bila kujua, mama akapokea na kusikiliza yote..."
"Kwa hiyo ndo ameshajua kila kitu.."
"Ndiyo amesikia Bitungu!"
"Ahhh! Haiwezekani sweet, mama yako amesikia kila kitu?"
Bitungu alihisi kuwa mdogo kama piritoni, bado alikuwa mtupu kama alivyozaliwa, mzuka wote wa kuendelea na mechi ukawa umekwisha rasmi, alichokifanya alitupa shuka upande wa pili huku ghadhabu ya hali ya juu ikiendelea kumtoka...
"Lakini..."
"Lakini nini niache kwanza Bitungu..."
"Unatakiwa kwanza tuyazungumze na kupanga jinsi ya kumwambia mama yako..."
"Bitungu unajua kabisa kitumbua kimeshaingia mchanga hapa na hakuna cha kukipangusa, ni bora kiliwe hivyohivyo tu!"
"Una maana gani Sweet?"
"Mambo yameshaharibika hapa, si salama tena!"
"Ngoja, ngoja! Tuliza kwanza jazba."
"Hapana Bitungu... hapana!"
Juliana alikuwa hataki kusikia lolote, ile raha ya mechi iliyokuwa imemtembelea aliona kama moto, moto tena ule wa kuni. Alitamani ardhi ipasuke atumbukie pengine angefarijika.
Alichokifanya, alichukua nguo zake zote na kuanza kuvaa moja baada ya nyingine huku akiendelea kulia kwa sauti ya juu iliyochanganyika na kwikwi. Muda wote Bitungu alikuwa akimtazama tu pasipo kumsogelea karibu, alishajiona ni mkosaji wa hali ya juu kwa kuwachanganya.
Ndani ya muda mfupi, Juliana alikuwa ameshamaliza kuvaa nguo, kitendo cha kuweka nywele zake sawa, mara simu yake ikaita tena."Ona sasa! Mama anapiga simu tena!"
"Sasa?"
"Sasa nini? Ndiyo hivyo anapiga tena..."
"Cha kufanya simu yake usipokee iache kama ilivyo..."
"Hapana Bitungu ni bora nipokee pengine hasira zake zitakwisha maana namjua mama yangu kwa hasira!"
"Juliana! Juliana nisikilize kwanza ninavyokwambia!"
Juliana alitii yale aliyokuwa ameambiwa na Bitungu, hakuipokea ile simu ya mama yake, aliiacha ikaita hadi ikakata yenyewe. Alitoka nje ya ile gesti na kuongoza moja kwa moja nyumbani kwao huku akimwacha Bitungu akimalizia kuvaa nguo mule ndani. Hakuwa Juliana wa kawaida kwa jinsi alivyokuwa amechanganyikiwa akili mpaka mwili.
Muda wote Mama Juliana alikuwa ametulia nje ya kibaraza amefura kwa hasira akimsubiri Juliana, alishaujua mchezo wote aliokuwa anachezewa. Kitendo cha kuonana uso kwa uso na Juliana hasira zikamzidia.
"Juliana?"
"Abee mama! Shikamooo!"
"Sitaki shikamooo yako!"
"Niambie ulikuwa wapi?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mama nisamehe nilikuwa..."
Kabla Juliana hajamalizia kujibu alishangaa kupigwa vibao mfululizo kutoka kwa mama yake.
"Usifikiri sijui chochote, najua kila kitu, niambie ukweli ni nani ulikuwa naye gesti...
Kifupi ni kwamba, mama Juliana alimsikia mwanaume akizungumza lakini hakujua kama ni Bitungu, ila kilichomshangaza sana ni kubaini kumbe binti yake ameanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume.
"Mama nisamehe."
"Niko tayari kukusamehe, niambie ulikuwa na nani?"
"Nilikuwa na kijana mmoja hivi."
"Anaitwa nani? Hana jina?"
"Mama mi simjui jina lake."
"Wee, koma kama ulivyokoma kunyonya kwenye ziwa langu, uingie na mwanaume gesti halafu uwe humjui jina?"
Juliana aliamua kumdanganya mama yake akiamini si vizuri kumtaja jina Bitungu...
"Anaitwa Sylvester."
"Anaishi wapi?"
"Kigamboni."
"Mmeanza uhusiani tangu lini?"
"Siku ya tatu leo."
"Umeshalala naye mara ngapi?"
"Mara ya kwanza leo."
"Ina maana amekutoa usichana wako?"
"Hakuweza mama."
"Kwa sababu gani asiweze?"
"Hakuweza tu."
"Unataka nikukague?"
"Hapana mama."
"Sasa kwa nini unanidanganya?"
"Sikudanganyi mama."
"Kwanza hebu niambie, hiyo gesti iko wapi?"
"Ipo Sinza."
"Ipo Sinza? Ina maana wewe hapo muda huu unatokea Sinza?"
"Ndiyo mama."
"Sinza sehemu gani?"
"Mimi siyo mwenyeji sana wa Sinza mama," alijibu Juliana bila kujua kuwa, mama yake alitaka kujua Sinza sehemu gani kwa sababu na yeye alitoka huko muda si mrefu....
"Shekilango unapajua?"
"Ndiyo mama."
"Ukitoka Shekilango ni kituo cha ngapi?"
"Sikumbuki, nilikwenda na bodaboda."
"Hebu nenda ndani haraka sana. Usije ukarudia tena," alisema mama Juliana huku akiiseti simu yake vizuri ili kumtwangia Bitungu. Lakini huku akiwaza...
"Isije ikawa alikuwa na Bitungu! Halafu isijekuwa Bitungu ndiyo yule Bitu wa kwenye simu yake akasema ni Bitte alikosea kusevu? Huyu mtoto isije ikawa anatuchanganya mimi na mwanangu?
"Lakini haiwezekani. Kwa mechi tuliyoicheza leo pale kitandani sidhani kama angeweza kumudu mchezo mwingine tena."
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Simu ya Bitungu ilipokelewa, mama Juliana akaanza kumuuliza maswali...
"Baby, wewe ni msaliti kwangu siyo?"
"Wala, kwa nini baby?"
"Huna mpenzi mwingine kweli wewe?"
"Wala! Nani amekwambia?"
"Sijaambiwa na mtu, nawaza mwenyewe tu."
"Ondoa hayo mawazo mpenzi, mimi ni wako peke yako."
"Kweli mpenzi wangu?"
"Kabisa mpenzi."
"Basi nimefurahi sana kusikia hivyo," alisema mama Bitungu na kukata simu. Roho yake ikawa imefarijika kwa siku hiyo.
***
Asubuhi ya siku iliyofuata, Juliana aliamka akiwa na wogawoga wa kuonana na mama yake ana kwa ana. Lakini alipokumbuka kuhusu ile hereni aliyoiona gesti akiwa na Bitungu ambayo ni moja kati ya hereni alizomnunulia mama yake, aliamua kuanza upelelezi wake hapo.
Kwanza alimvizia mama yake amekwenda kuoga, yeye akazama chumbani maana baba yake naye alishakwenda kazini mapema.
Alifungua kwenye kikopo ambacho mama yake anakitumia kuwekea hereni zake, hakuona hereni hata moja. Akaangalia juu ya dressing table, akaiona hereni moja tu, akatingisha kichwa huku akisema moyoni...
"Ile niliyoiona gesti hii mwenzake, kwa vyovyote vile. Ina maana mama ndiye mwanamke aliyekuwa na Bitungu gesti...itakuwa yeye na ndiyo maana alinibana kuhusu Sinza sehemu gani niliyokuwepo mimi," alisema moyoni Juliana huku akichomoka kutoka chumbani humo.
Aliendelea na mambo yake mengine lakini kuanzia muda huo akawa hamwogopi tena mama yake kufuatia kubaini uozo wake na Bitungu.
Jiliana alianza kufanya utafiti wake kwa kutumia akili ya kujiongeza. Aliamua kwamba siku mama yake akitoka na yeye atoke, amfuate kwa nyuma kwa siri mpaka atakapoingia na yeye aingie.
Lakini pia aliamua kuendelea na uhusiano na Bitungu akiamini kwamba, atatumia akili yake ya ziada ili kijana huyo ammwage mama yake.
Akili ya kujiongeza aliyokuwa nayo Juliana ilikuwa ni kuhakikisha kila mama yake anapopigiwa simu yupo pembeni akisikiliza japo kwa kujificha. Alishajitoa mhanga kwa lolote...
"Haiwezekani hata siku moja, kama kula tutaendelea kula wote tu, lakini kwa nini mama anizidi akili? Hata kama ni mama yangu haiwezekani!"
Maisha ya Juliana na mama yake bado yalikuwa ya kuwindana, Juliana hakutaka kumuachia mama yake hata sekunde, kila simu ilipokuwa ikipigwa Juliana hakosi, kama siyo pembeni yake basi atakuwa eneo hilohilo akisikiliza ni nani amepiga.
Siku moja Juliana akiwa katika kufanya usafi katika chumba cha mama yake alisikia simu ya mama yake ikiita, kipindi hiki mama yake alikuwa bafuni akioga.
"Juliana!"
"Abee mama"
"Niletee simu yangu!" Mama Juliana alikuwa tayari ameshaisikia simu yake ikiita, akili yake ilishajiweka ni lazima atakuwa Bitungu, hakutaka hata kidogo Juliana aishike lakini kutokana na kujua kuwa yupo chumbani kwake karibia na hiyo simu akifanya usafi ikambidi amuagizie tu.
"Mbona huji?"
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nakuja mama, halafu simu yenyewe imeshakata!"
alisema Juliana huku akihema na kusogelea eneo la bafuni alipokuwepo mama yake, jina la kwenye simu iliyokuwa ikiita kwa mama yake lilimkera sana kiasi cha kuamua kuikata kwa makusudi, alikuwa ni Bitungu.
"Shika mama, lakini imeshakatika"
"Alikuwa nani?"
"Hata sikuangalia mama, nadhani atapiga tena!"
"Unadhani? Embu nipe huko!"
Alisema mama Juliana kwa jazba huku akishika simu ile na mapovu ya sabuni mkononi sambamba na majimaji. Harakaharaka akaangalia ‘missed call' lakini hakukuwa na jina alilodhani zaidi ya kukutana na jina la Mama Zai.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment