Chombezo : Nelly Muosha Magari Wa Posta
Sehemu Ya Nne (4)
Alipoambiwa hivyo, si akakumbuka kwamba Doreen alimpatia simu ambayo mpaka muda huo hakumuonesha fundi Yassin akajikuta akiachia tabasamu lililoonwa na fundi.
“Vipi naona umefurahi!” fundi Yassin alimwambia.
Kutokana na kauli hiyo, kumzuga fundi wake, Nelly alimwambia alimfurahisha sana alipomwambia atakapoanza kwenda kwenye site nyingine wataenda wote.
“Ndiyo hivyo, siwezi kukutupa mdogo wangu,” fundi Yassin alimwambia Nelly bila kujua mwenzake alifurahi kukumbuka alikuwa kapewa simu ambayo ingemsaidia kuwasiliana na mpenzi wake Doreen.
Wawili hao walipotosheka kwa kinywaji waliondoka na kuelekea nyumbani, walipokaribia Nelly alimwambia fundi wake kwamba anakwenda kumsalimia rafiki yake Ipyana ambaye hakuonana naye kama siku nne hivi.
“Dogo ukiwa na hela hutulii, au unakwenda kuongeza mbili za kulalia nini?” fundi alimwuliza.
“Hapana, naenda tu kumwona mshkaji wangu huenda atanipa mchongo wa kazi maana kuanza kushinda nyumbani bila kazi kwa mtoto wa kiume haipendezi,” Nelly alimwambia.
Kutokana na maneno ya Nelly , fundi alimfagilia na kumweleza alikuwa na mawazo mazuri, akamwambia waonane kesho jioni ili ajue alifikia wapi.
“Poa bro wangu, kanisalimie shemeji yangu,” Nelly alimwambia.
Walipoachana, kijana huyo alikwenda kwenye genge la Chinga akamwambia amkatie tango, Chinga akamtania kwamba mambo yake yalikuwa mazuri maana kila jioni alikuwa akipasha kilaji.
“Hamna bwana, rafiki yangu kanipa tubia tuwili sasa kwenda homu na harufu ni so kwa washua,” Nelly alimwambia wakati huo alikuwa akila ndizi mbivu.
Alipoamliza kula ndizi na tango akaenda nyumbani kwa akina Ipyana na kumkuta akiwa ameketi kwenye moja ya mairi ya gari waliyoyafukia ardhini nyumbani kwao kuzuia magari yasipite.
Marafiki hao walipoona walifurahi sana, katika maongezi yao Nelly alimsimulia kila kitu Ipyana kuhusu kule site na alivyosimamishwa kwenda.
“Da! Wewe kweli balaa, siku mbili tu za kwenda site umempata mtoto wa kishua na kakupa hadi simu, kijana unatisha,” Ipyana alimfagilia Nelly .
“Si ujuaga mambo yangu, mimi huwa sirembi hata siku moja, sasa unafikiri mtoto kajipendekeza mwenyewe mara sijui maziwa, mayai sijui mazagazaga gani, sasa ukimuacha mtoto kama huyo si utapata dhambi za bure kaka!” Nelly alimwambia Ipyana wakaishia kucheka.
Baada ya mazungumzo, Ipyana alimwuliza Nelly kama anaweza kujitoa ufahamu ili siku iliyofuata waongozane kwenda Posta kufanya kazi ya kuosha magari ya wafanyakazi wa serikali, wafanyabiashara na mabosi mbalimbali.
“Kaka kwa hali ilivyo sasa sichagui kazi kinachotakiwa ni kupata fedha tu, wewe unafikiri kama nisingeenda na fundi Yassin kule site ningempaje mtoto wa kishua Doreen aliyenipa hii simu kali?” Nelly alimwambia Ipyana, wakacheka.
“Kama ndiyo hivyo basi poa sana, wewe si unaona jinsi geto langu lilivyo na kila kitu cha maana na ninavyopiga pamba za kishua, kazi ya kuosha magari kaka!” Ipyana alimwambia Nelly .
“Hivi kazi ya kuosha magari inalipa eh?” Nelly alimwuliza.
“Kaka acha, kwa siku mimi kurudi homu na shilingi thelathini mpaka hamsini ni jambo la kawaida, halafu kule dili zipo kibao mfano bosi anaweza kukutuma sehemu ukirudi anakupa teni au zaidi,” Ipyana alimwambia Nelly aliyeishia kushangaa.
“Ipyana bwana si ungeniambia muda mrefu si nami saa hizi si ningekuwa na geto kali kama lako na watoto wakali wangenikoma?” Nelly alimwambia.
Ipyana alicheka sana na kumweleza kwa jinsi alivyokuwa akimuona sharobaro alijua asingeweza kufanya kazi ya kuosha magari ndiyo maana hakumwambia.
“Kaka kama ndiyo hivyo kesho mimi na wewe mguu na njia hadi Posta, kweli jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza, kumbe kila siku unapiga hela ya maana namna hiyo?” Nelly alimwuliza Ipyana.
“Ndiyo hivyo, kikubwa ni kuchakarika tu, wewe kesho twende nikakufundishe kazi,” Ipyana alimwambia.
Baada ya kukubaliana siku iliyofuata kwenda Posta, waliagana ndipo Nelly akaenda kwao na kuwakuta wazazi wake wakiwa wanamalizia kula, walisalimiana kisha akaenda kuoga.
Kwa kuwa valikuwa ameshiba, mama yake alipomwuliza suala la msosi alimwambia kuna sehemu walipitia na fundi Yassin wakala ndipo mama mtu akamwuliza kuhusu kazi.
Aliwaambia ilikuwa nzuri kisha akaenda chumbani kwake akachukua shilingi elfu kumi na tano na kumkabidhi mama yake akamwambia kesho yake anunue mboga.
Wazazi wake walifurahi sana, baba alimsifia na kumwambia kweli alikuwa amekua na kumwuliza aliona faida ya kujishughulisha, akamwambia aliiona.
“Hivyo ndivyo kijana unatakiwa kuwa, wewe unafikiri nisingeshauri utafute kazi ya kufanya leo hii ungempatia mama yako hela ya kukununua mboga, safi sana tena sana,” baba yake Nelly mzee Reli ya Uhuru alimwambia.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nelly aliwashukuru wazazi wake kisha aliwaaga kwamba alihisi uchovu hivyo anakwenda kulala, wakampa pole na kumtakia usiku mwema akaenda chumbani kwake bila kuwaambia kama fundi Yassin alimwambia asiende site.
“Hawa siwaambii chochote kuhusu ishu ya site, kukicha kesho naenda Posta ila nikitoka huko ndipo nitamwambia mama,” Nelly aliwaza.
Akiwa chumbani, alichukua simu aliyopewa na Doreen, akaweka kadi yake na kuiweka kwenye chaji huku akiwa mwenye furaha kwani hakutegemea kama angepata simu siku za karibuni.
“Tena ikipata chaji kidogo mtu wa kwaza kumpigia atakuwa Doreen, halafu nitampigia Atu na yule demu niliyekutana naye siku ya kwanza wakati tunaenda site,” Nelly aliwaza.
Kijana huyo akiwa kalala chali huku kava bukta pekee, alimlaani sana Zakayo kwa kumchongea kwa fundi Yassin na kusababisha kusimamishwa kufanya kazi kule site.
“Ningekuwa mchawi ningemrogelea mbali Zakayo aanze kuumwa na kurudishwa kijijini kwao, au ningekuwa namiliki bastola ningempiga risasi za kichwa afie mbali kwa roho yake mbaya,” Nelly aliwaza.
Baada ya kutumia dakika kadhaa kumfikiria Zakayo, alipitiwa na usingizi hadi alipokuja kushtuka ilikuwa saa tano, alipoiangalia simu akakuta imejaa chaji fulu akaamua kumbipu Doreen.
Nelly alifurahi sana alipobaini Doreen alikuwa hewani, akiwa katika hali hiyo simu yake ikaanza kuita na mpigaji alikuwa Doreen akapokea.
“Sema mpenzi wangu, nimefurahi kweli ulivyonibip maana tangu nilipopanda kitandani mawazo yangu yote yalikuwa kwako, si unajua tena ulivyouteka moyo wangu kwa muda mfupi?” Doreen alimwambia.
“Hunishindi mimi, yaani kila nikikumbuka joto lako, mahaba yako na hizo embe zako zinazoshika vizuri, nimeshindwa kulala na simu ilipojaa chaji nikaamua kukupigia, yaabu d sijui nikwambieje,” Nelly alimwambia Doreen.
Wawili hao walizungumza kwa muda mrefu kisha Doreen akamwuliza kama simu yake ilikuwa na vocha ya kutosha, Nelly akamwambia alinunua ya mia tano.
“Ngoja nikutumie muda wa maongezi wa kutosha ili tuchati hadi kuna kucha,” Doreen alimwambia.
Kama alivyomuahidi, baada ya kukata simu hazikupita hata sekunde 50 Nelly alisikia mlio wa ujumbe alipofungua akaona ametumiwa muda wa maongezi wa shilingi elfu tano.
“D, asante sana, haya niambie kitu kizuri sana nifutahi usiku huu,” Sharobaro Nelly akamwambia.
“Kitu kizuri ni kwamba nakupenda sana natakamani hata muda huu tungekuwa wote hapa kitandani ukinifanyia mambo yote mazuri ya kunipa raha,” Doreen alimjibu.
“Jamani mpenzi wangu, kwa kuwa uko mbali nami ndiyo hivyo, kama hutajali tukutane hapo kwa njia ya meseji,” Nelly akamwambia Doreen kupitia meseji.
Doreen ambaye alikuwa akipenda sana kuchati alimwambia sawa ndipo sharobaro Nelly akaanza kumvurumishia meseji za kimahaba zilizomchanganya mtoto wa kishua na kujikuta yuko hoi.
Doreen alipomwambia Nelly kwamba alikuwa anajisikia ovyo, kijana huyo akaamua kumpigia wakaanza kuzungumza mambo ya malovee na kuhamasishana hadi Doreen akafikia kilele cha mlima wa Kilimanjaro kupitia simu zao.
Kufuatia Doreen kufika kilele cha mlima, alimfagilia sana Nelly kwa kujua kutumia simu yake maana ilikuwa kama walikuwa wotelaivu, Nelly naye alimshukuru kwa ushirikiano wake, kisha waliagana kwamba wangekutana kesho yake.
Nelly alimwambia poa lakini hakutaka kumweleza kuhusu fundi Yassin kumzuia kwenda site, alipanga kumpigia simu mishale ya saa tatu ya siku iliyofuata kumweleza jambo hilo.
Kutokana na uchovu, msichana huyo akiwa kama alivyozaliwa akapitiwa na usingizi hadi aliposhtuka saa kumi na moja alfajiri, alipojiangalia na kukumbuka kilichojiri baina yake na Nelly wakati wakichati akaishia kutabasamu.
Doreen alipoachia tabasamu, akajikuta akijisemea moyoni:
“Mh! Huyu Nelly ni balaa, tukikutana laivu ni moto na kwenye simu pia ni moto zaidi!” Doreen aliwaza.
Msichana huyo aliyekuwa amekolezwa na penzi tamu na sharobaro Nelly aliendelea kumfikiria kijana huyo hadi alipopitiwa tena na usingizi.
Kulipokucha alimsikia Anne akiwa bize kufanya usafi akajiuliza amwambie kuhusu uhusiano wake na Nelly au ampotezee kuhofia huenda naye angelitamani penzi la kijana huyo kutoka Tandale.
“Haina haja, kama atahisi halafu akiniuliza nitamwambia lakini nitampiga mkwara asimzoee na kumtishia siku nikimbamba anajicheketua kwa Nelly ndiyo utakuwa mwisho wa kufanya kazi,” Doreen aliwaza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Anne alipomaliza kufanya alijiandaa akanywa chai kisha alimuaga Doreen aliyekwishaamka akaelekea chuo, huku nyuma Doreen akawasha runinga na kwenda kukaa sebuleni.
Binti huyo wa kishua alichukua simu yake na kumpigia Nelly kwa lengo la kumjulia hali na kujua muda ule walikuwa wako wapi, cha kusikitisha hakupatikana hewani.
“Huyu atakuwa hajawasha simu yake, ngoja nimsubiri,” Doreen alijisemea moyoni.
Akiwa katika hali hiyo ya kusubiri, akasikia kengele ya getini ikilia akaachia tabasamu, akiwa kava pensi iliyoishia juu ya mapaja yake iliyombana na kuzifanbya hipsi zake zionekane vyema na singilendi iliyozionesha vyema chuchu zake akatoka kwenda kufungua.
Alipofungua akamuona Zakayo, almanusura asonye lakini akapotezea na kumsalimia kisha msaidizi huyo wa fundi akaingia ndani, Doreen akafunga geti na kurudi sebuleni bila kuzungumza zaidi na Zakayo.
“Huyu mtoto jamani kaumbika, sema tu ni haya mambo ya kazi, maana ukijifanya kidume halafu baba yake agundue hakika utalambwa shaba na maiti yako isionekane milele,” Zakayo alijisemea moyoni.
Kule ndani,Doreen alizidi kumuwaza Nelly kwani alitamani sana kumuona ndipo akasikia tena kengele ya getini ikilia, akatoka mbio kwenda kufungua akiwa na imani alikuwa fundi Yassin na Nelly kwani walikuwa na kawaida ya kufika pamoja.
Alipofungua akakutana na Haruni, kama ilivyokuwa awali alitamani kutoa msonyo akajizuia, Doreen akamsalimia ndipo kijana huyo licha ya kumtamani Doreen kwa jinsi alivyokuwa kanona, hakuthubutu kumwangalia mara mbili wala kusema chochote zaidi ya kuelekea eneo la kazi.
Kitendo cha fundi Yassin na Nelly kutowasili, kilimkosesha raha binti huyo wa kishua, hata hivyo hakukata tama kwa kuhisi huenda foleni ilichangia kuchelewa.
Doreen alikwenda mezani akamimina maziwa ya moto kwenye kikombe akachukua na soseji mbili na kurejea sebuleni kusubiri kusikia kengele ya getini ikilia.
Alipokunywa mafunda mawilina nusu soseji, akasikia kengele, aliachia tabasamu pana kwani alikuwa akijua sasa Nelly wake kawasili, akatoka na kwenda kufungua geti, badala ya kumuona Nelly akamuona fundi Yassin.
“Shikamoo fundi!” alimsabahi.
“Marahaba,hujambo Doreen?” fundi Yassin alimsalimia.
“Sijambo!” msichana huyo alimsalimia.
Fundi akiwa ameingia ndani, Doreen alimwuliza Nelly alikuwa wapi akamwambia siku ile asingefika, jibu la fundi lilimnyong’onyesha binti huyo wa kishua aliyemuuliza alikuwa na tatizo gani.
Fundi Yassin hakutaka kumwambia ukweli akamdanganya kwamba alimweleza hakujisikia vizuri nahisi kutokana na uchovu wa kazi, kauli hiyo ilimfanya Doreen kumuonea huruma mpenzi wake.
“Jamani pole yake,” msichana huyo alimwambia fundi Yassin kisha akafunga geti na kuelekea ndani kwao akiwa hana raha.
Akiwa ameketi kwenye sofa alijaribu kumpigia simu Nelly lakini hakupatikana ndipo kwa hasira akaenda chumbani kwake na kujitupa kitandani na kuendelea kumuwa za Nelly .
Wakati Doreen akiwa katika hali hiyo, asubuhi Nelly alikwenda nyumbani kwa rafiki yake Ipyana aliyemkuta akimsubiri na baada ya salamu walikwenda kituoni walikopanda daladala la Posta.
Kama ilivyokuwa kawaida ya sharobaro Nelly kupenda mademu, alikuwa akimtazama kwa matamanio sistaduu mmoja aliyekuwa amesimama naye karibu kwa sababu wote walikosa siti.
Kufuatia kumkazia sana macho, mrembo huyo akawa anaangalia pembeni kwa aibu jambo lililompa nguvu Nelly ya kuendelea kumtazama. Kila mrembo alipomtazama Nelly macho yao yaligongana mwishowe mtoto wa kike akaachia tabasamu.
Gari lilipofika Keko Fenicha, abiria waliokaa siti ya karibu yao waliteremka ndipo Nelly na yule mrembo wakaichangamkia siti hiyo, walipokaa tu Nelly akamsabahi yule dada.
“Mambo vipi mrembo?”
“Poa, ila wewe mkaka ni mchokozi sana, unajua ilibakia kidogo nicheke kwa ulivyokuwa ukinitazama,” yule mrembo alimwambia Nelly .
“Utanisamehe, na wewe si umezidi kuwa mrembo?” Nelly alimfagilia yule mrembo aliyeishia kutabasamu.
“Acha masihara yako, hivi kwa mfano warembo miamoja wakipanga mstari na mimi naweza kuwemo?” yule dada aliyeonekana anapenda sana stori alimwuliza Nelly .
“Siyo mia moja, hata wakiwa kumi wewe lazima uwe wa tatu,” Nelly alimfagilia.
Alipoambiwa hivyo, yule dada alicheka na kumwambia haya bwana kama ni kweli kisha akamwambia akumbuke kama angekuwa mrembo wala asingepanda daladala.
Nelly alicheka na kumfahamisha kila kitu na wakati wake, hivyo awe na subira gari lake lilikuwa njiani kutoka Ulaya.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Da! Wewe kaka una maneno sana, eti gari langu linakuja kutoka Ulaya haya bwana kama maneno yako yawe ya heri,” yule mrembo alimwambia Nelly , wakacheka.
Kwa kuwa asubuhi hiyo hakukuwa na foleni, kufumba na kufumbua wakajikuta wapo Mnazi Mmoja, kama kawaida Nelly aliona atafanya kosa kubwa asipoomba namba ya simu ya yule mrembo.
“Unahitaji namba yangu ya nini?” mrembo alihoji.
“Si gari lako likifika nikupigie uje ulichukue!” Nelly alimwambia.
Mrembo alicheka sana na kufuatia ucheshi wa sharobaro Nelly , akajikuta akimuomba kijana huyo ampatie simu yake ndipo Nelly aliiotoa akaiwasha na kumpatia, akaaindika na kumwambie asevu jina la shangazi.
“Unaitwa shangazi au unapenda niwe nakuita hivyo?” Nelly akamwuliza.
“Ndiyo jina langu, wengi wanapenda kuniita Aunt lakini wewe niite shangazji,” yule mrembo alimwambia Nelly bila kujua asingeweza kumaliza muda mrefu bila kuingia kwenye kumi na nane za kijana huyo mpenda mademu wazuri.
“Sawa, lakini mimi nitakuwa nakuita Aunt,” Nelly alimwambia, wakacheka.
Gari lilipofika Posta, yule wote waliteremka ambapo yule mrembo alisema anakwenda Masaki ndiko alikokuwa akifanya kazi, walipoagana Ipyana akamfagilia Nelly kwa ushapu wake mpaka kuozoeana na yule mrembo kwa muda mfupi.
“We acha tu ndugu yangu tena mpaka namba yake kanipa,” Nelly alimwambia Ipyana.
Ipyana ambaye hakuwa mpenzi sana wa mambo ya wasichana akaishia kucheka, wakati marafiki hao wanaelekea kwenye ofisi za wizara moja ambayo Ipyana alikuwa akifanya ujasiriamali wa kuosha magari, Nelly alikumbuka akuzima simu baada ya kusave namba ya yule mrembo, akaizima.
Alifanya hivyo kuhofia kupigiwa simu na Doreen ambaye hakutaka kabisa kuzungumza naye muda huo, kwa kuwa ofisi hizo za wizara hazikuwa mbali, waliwasili ndipo Nelly akashangazwa na jinsi wafanyakazi wa serikali na madereva walivyomchangamkia Ipyana.
“Dogo vipi hujambo?” dereva mmoja alimsalimia Ipyana.
Si huyo pekee, wafanyakazi mbalimbali walimsalimia kwa furaha ambapo wengine walimwambia atayakuta magari yao sehemu aliyokuwa akioshea hivyo ayaoshe.
Ipyana aliwaambia sawa huku akimtambulisha Nelly kwamba alikuwa ndugu yake, alifanya hivyo mpaka kwa walinzi ambao kwa jinsi walivyomuamini dogo huyo hawakuwa na wasiwasi.
Ipyana na Nelly walipofika eneo la kazi, waliyakuta magari manne ya mabosi ambayo walipaswa kuyaosha, Ipyana alimuelekeza jinsi ya kufanya kazi hiyo Nelly .
Hadi ilipofika saa tatu na nusu walikwishamaliza kuosha magari manne, kwa gharama ya shilingi 4,000 kwa gari moja na tayari walikuwa wana ukakika wa kupata shilingi 16,000.
“Umeona besti, haya magari manne tayari tuna uhakika wa kupata shilingi 16,000,” Ipyana alimwambia Nelly ambaye alimwambia aliamini ile kazi ililipa.
Wakati wakiwa wanapiga stori wamekaa eneo la kuoshea magari, alikuja dada mmoja wa idara ya uhasibu mwenye shepu matata sana, akawasalimia akina Ipyana.
“Sisi hatujambo da Fatu, vipi kazi?” Ipyana alimsabahi.
Dada huyo ambaye kwa jinsi alivyoumbika na nguo alizovaa kumkaa sawa, Nelly akajikuta anameza tu mafunda ya mate na kujisemea moyoni kwamba wakubwa walikuwa wanafaidi sana.
“Vipi Ipyana, naona leo umetuletea mwenzako, kazi zinakuzidi nini?” Fatu alimwuliza Ipyana kabla hajamweleza shida yake.
“Nimeamua tu kuja na ndugu yangu maana nimeona yupoyupo tu homu,” Ipyana alimwambia.
“Vizuri sana na huo ndiyo urafiki wa kweli, anaitwa nani?” Fatu alimwuliza dada huyo aliyeonekana kuvutiwa na kitu f’lani kwa sharobaro Nelly .
“Nelson, ila wengi wanapenda kumuita jina lake kwa kifupi yaani Nelly ,” Ipyana akamwambia.
“Oke, karibu sana Nelly , tena kwa kuwa leo ndiyo mara yako ya kwanza kufika hapa nataka gari langu ulioshe wewe, nitakupa shilingi elfu sita kama ofa ya kukukaribisha,” Fatu alimwambia Nelly , kijana huyo ambaye hakuamini alichokisikia akasema asante.
“Leo Ipyana ni zamu ya rafiki yako mgeni, wewe umekula sana hela zangu, sasa gari langu lile pale nataka kuona rafiki yako atakavyoling’arisha,” Fatuma alimwambia Ipyana.
“Dada Fatu bwana kwa visa, haya bwana wewe kaendelee na kazi lakini elewa wadogo zako bado hatujanywa chai,” Ipyana akamtania.
“Kwani mimi ndiye nimewaleta mjini, mtakula jeuri yenu,” Fatu alimtania Ipyana kisha akaingiza mkono kwenye sketi yake iliyombana na kutoa noti ya shilingi 5,000 akampatia Ipyana.
Ipyana na Nelly walimshukuru ndipo dada huyo akaenda kuendelea na kazi, hata hivyo alivutiwa sana na muonekano wa Nelly ambaye alikuwa mrefu wa wastani, maji ya kunde, ana vidiponsi vilivyomfanya anapotabasamu au kucheka vionekane.
“Ukiwa na kijana kama huyo mbona ni raha tupu siyo kama mzee wangu hajiwezi kabisa eneo la kujidai, huyu nitafanya kila njia nimpate,” Fatuma ambaye wengi walipenda kulikatisha jina lake aliwaza.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kaka umeona mambo ya Posta hayo? Mpaka muda huu tayari tuna shilingi 21,000 hata saa tano haijafika, halafu una nyota ya kupendwa, si umemuona dada Fatu alivyokuchangamkia na kutoa hela ya chai?” Ipyana alimwambia Nelly .
“Siyo mchezo kaka, halafu dada yupo bomba mbaya, kweli wakubwa wanafaidi da!” Nelly alimwambia Ipyana.
“Siyo wakubwa, hata wewe ukiamua kujitosa mazima unachukua mzigo, hawa madada wa maofisini huwa wanawapenda sana vijana kama sisi,” Ipyana alimwambia Nelly .
“Acha kunitania Ipyana, dada kama yule mwenye hela zake na alivyo vile anaweza kutoka na vijana kama sisi tusio na mbele wala nyuma?” Nelly alimwuliza rafiki yake.
“Kwani unafikiri wana tofauti gani na mtoto wa kishua aliyekupa hadi simu, mapenzi hayanaga sera hizo ni sawa na kipepeo asiyechagua ua la kutua,” Ipyana alimwambia Nelly .
Nelly alifurahishwa na kauli ya Ipyana na kujikuta akicheka na kumwambia hakujua kama alikuwa na maneno mengi namna ile, rafiki yake huyo alimwambia kauli yake ilikuwa kweli tupu!
Kabla hata hawajaenda lilipokuwa gari la Fatu, alitokea dada mwingine mfupi wa wastani, mweusi wa kung’aa, nyuma ana kiwowowo cha kuleta fujo mjini, miguu ya bia, macho makubwa akikutazama ni kama vile anakukonyeza na midomo f’lani hivi ya mahaba.
Kwa tabia ya kupenda wanawake kuliko hata chakula, Nelly alipomuona tu moyo ukapiga paa.
Dada huyo alimsalimia kwa kumchangamkia Ipyana na kumwuliza kama alikuwa na gari la kuosha muda ule.
“Hapa sista Jully, vipi gari lako chafu nini?” Ipyana alimwuliza.
“Hapana, ila nataka nikutume Mtaa wa Makunganya mara moja,” dada Jully alimwambia Ipyana.
Ipyana alimwambia hakukuwa na tatizo ndipo yule dada akatoa bahasha ya khaki na kumweleza ilikuwa na shilingi laki tatu aende kwenye ofisi za kusajili vizazi na vifo akamuulize dada mmoja aitwaye Milka akimkuta ampe fedha hizo.
Baada ya dada Jully kumwagiza hivyo Ipyana alimwangalia Nelly na kumwuliza Ipyana kama alikuwa ndugu yake, akamjibu ndiyo.
“Naye upo naye hapa?” aliuliza.
Ipyana alimwambia atakuwanaye ndipo dada huyo aliyekuwa kavaa sketi nyekundu na blauzi iliyokuwa na maua ya rangi mchanganyiko, mavazi yaliyompendeza sana akamkaribisha Nelly .
Nelly aliposema asante, dada huyo alimwuliza Ipyana ndugu yake alikuwa anaitwa nani, akamwambia Nelly,
“Haya mdogo wangu karibu sana hapa!” Jully alimwambia Nelly .
“Asante dada yangu, nafurahi kukufahamu,” Nelly alimwambia.
“Mh! Hawa akina dada wa hapa wana mambo balaa yaani kila anayekuona anakushobokea, hongera kaka kwa zali la kupendwa!” Ipyana alimtania Nelly .
Nelly alipoambiwa hivyo kichwa kilivimba kwa sifa akacheka sana, kwa kuwa alikuwa akipenda sana mademu akamwambia rafiki yake lazima atamtafuna mmoja ili kujenga heshima!
Baada ya mazungumzo hayo, vijana hao walikwenda kuosha gari la dada Fatu kwa ushirikiano. Wakati wakiendelea na zoezi hilo Fatu akiwa ofisini akili yake ilikuwa kwa sharobaro Nelly .
Si kwa Fatu tu, hata Jully naye alikuwa kavutiwa na kijana huyo ambaye ndiyo kwanza alimuona siku hiyo, alivutiwa na Nelly kwani alifanana vitu vingi na serengeti boy wake aliyeitwa Peter aliyekwenda kusoma Canada.
“Huyu kijana utafikiria wako pacha na Peter wangu, lazima nifanye kila kitu nimnase kabla hata hajazoeana na wanawake wa hapa maana nawajua kwa kupenda vivulana,” Jully aliwaza bila kujua Fatu naye alimhitaji sana Nelly .
Baada ya kumaliza kuosha gari la Fatu, walikwenda kunywa chai kisha walirudi ndipo Ipyana akamwambia Nelly kwamba amsubiri anakwenda mtaa wa Makunganya alikotumwa.
“Usijali kamanda wangu we nenda, utanikuta,” Nelly alimwambia Ipyana.
Ipyana alipoondoka, Nelly alikumbuka alizima simu muda mrefu akaiwasha, hakukaa hata sekunde mbili Doreen binti wa ushuani aliyekosa raha tangu alfajiri baada ya kumkosa Nelly kisha kuambiwa na fundi Yassin kwamba asingefika site akapiga.
Nelly alipokea simu hiyo, Doreen alipomjulia hali yake alimwuliza alipatwa na masaibu gani yaliyomfanya asifike site, akamwambia ameambiwa asiende.
“Unasemaje d nani kakuzuia?” Doreen alihoji.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nelly hakuona sababu ya kumficha akamsimulia kila kitu, msichana huyo alisema atafanya kila awezalo Zakayo aondoke pale kama alivyomfanyia mpenzi wake Nelly .
Baada ya kuzungumza kwa muda, msichana huyo alimbusu Nelly na kumuuliza kijana huyo kama alikuwa na nanafasi siku hiyo wakutane sehemu ili wapeane raha.
“Kwa leo haitawezekana mpenzi wangu,nimepata kazi nyingine,” Nelly alimwambia.
Doreen alipoambiwa hivyo alishtuka na kumuuliza alikuwa akifanya kazi gani na wapi, Nelly alimfahamisha kwamba ni kibarua tu huko Posta, msichana huyo akashangaa.
Wakati wapenzi hao wakizungumza Nelly alimuona mama mmoja mtu mzima akija pale walipokuwa wanakaa kusubiri tenda za kuosha magari, mama huyo akamsalimia.
Nelly akiwa ameiacha simu hewani aliitikia salamu ya mama huyo na kumwamkia kisha akamwambia Doreen asubiri atampigia baadaye, msichana huyo aliyesikia wakati Nelly akimwamkia yule mama akasema sawa.
“Ipyana yuko wapi?” mama huyo ambaye licha ya kuwa mtu mzima alionekana alikuwa moto wa kuotembea mbali enzi zake maana aliumbika haswa alimwuliza Nelly .
Nelly alimfahamisha kwamba alitoka kidogo, akamwuliza kama naye alikuwa akishirikiana naye kufanya kazi, Nelly akamwambia ndiyo.
Mama huyo ghafla akatokea kumpenda Nelly kwani ulipita muda mrefu bila kunjunju.
“Ila hujaanza kuja hapa muda mrefu eh?” mama huyo katibu muhtasi aliyefiwa na mumewe miaka minne iliyopita alimwuliza Nelly .
“Nimeanza leo,” Nelly alimfahamisha.
“Oke, akija mwenzako nitarudi nataka munioshee gari langu maana leo ni siku ya tano halijaoshwa,” mama huyo ambaye naye alivutiwa na Nelly alimwambia.
“Hakuna shida mama yangu,” Nelly alimfahamisha.
Mama huyo alipogeuka na kuanza kuelekea ofisini, Nelly aliyagandisha macho yake kwenye wowowo lake tata lililokuwa likitikisika na kuonekana kama lilitaka kudondoka.
“Kudadeki kumbe huku Posta ndivyo kulivyo? Kila demu mpaka akina mama wote wazuri, asante besti yangu Ipyana kwa kunitoa uswahili, maana hawa wanawake wazuri ningewaona wapi?” Nelly aliwaza.
Mama huyo alipotoweka kabisa, Nelly aliyekuwa na namba za mademu wote aliokutana nao tangu siku ya kwanza kwenda site Madale, aliamua kumpigia demu huyo.
“Haloo! Halooo nani mwenzangu?” yule msichana wa kwanza waliyeachana na Nelly kituo cha daladala Mwenge alimwuliza Nelly baada ya kupokea simu.
Nelly alipojitambulisha, yule dada alifurahi kumsikia na kumwuliza habari za tangu walipoachana, Nelly akamwambia zilikuwa poa kisha alimfahamisha ile ilikuwa namba yake na alikuwa hewani.
Pamoja na yote, Nelly alimwomba dada huyo kama atakuwa na nafasi waonane, akamwambia haikuwa na shida na kupanga Jumapili iliyofuata wakutane Temeke Mwisho.
Alipopewa jibu hilo, Nelly alifurahi sana na kujisemea demu huyo siku hiyo asingechomoa lazima atatafunwa kisawasawa kwani kama ni fedha alikuwanazo.
Baada ya kumalizana na demu huyo, alimwendea hewani Atu ambaye tangu walipoachana siku ile walipobilingishana katika gesti ya Keko hawakukutana.
Msichana huyo ambaye hakuwa na namba ya Nelly alipomwuliza alikuwa na nani, sharobaro Nelly akajitambulisha, Atu alifurahi na kumwambia kwa nini alikuwa kimya namna ile.
“Jamani si nilikwambia simu yangu iliibiwa,hiyo ndiyo namba yangu halafu naaamu mno ya kukutana na wewe,” Nelly aliyeamua kufungulia mbwa bandani yaani kutaka kuwashughulikia vilivyo viumbe hao alimwambia.
“Ni wewe tu! Mimi hata ukisema leo nipo tayari!” Atu alimwambia Nelly .
Kitendo cha msichana huyo kumwambia Nelly hata sikuile alikuwa na chansi, kijana huyo mpenda mademu wazuri akaona atafanya kosa kubwa sana kumuachia ndege huyo aliyeingia tunduni mwenyewe.
“Oke! Mimi kwa sasa nipo tauni, nikimaliza mambo ya hapa nitakupigia na kukuelekeza sehemu ya kumiti, au iwe pa siku ile?” Nelly alimwambia Atu aliyesema sawa.
Wakati Nelly akiendelea kuzungumza na Atu, Ipyana alirudi ndipo akamuaga Atu na kumfahamisha kuhusu yule mama mtu mzima ambaye alijaaliwa bambataa matata.
“Umesema mnene mfupi kajazia nyuma?” Ipyana alimwuliza Nelly .
“Yeah! Tena akitembea utafikiri mzigo unataka kuanguka wenyewe yaani kaka wanawake wa hapa wazee kwa vijana wote moto kwa kwenda mbele,” Nelly alimwambia Ipyana.
“Mimi naangalia kazi tu, kama ningewaendekeza nisikuwa nimefanya chochote,hivi unajua kama nimenunua uwanja nataka mwakani nianze kujenga?” Ipyana alimwambia Nelly .
Nelly alipoambiwa hivyo alicheka sana na kumwambia kweli hakuutendea haki ujana, badala ya kufurahia maisha eti anafikiria kujenga wakati mshua wake ana nyumba tatu kali na mbili kapangisha.CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Zile ni za mshua mimi nataka niwe na nyumba yangu,” Ipyana alimwambia Nelly aliyeishia kucheka.
“Ndiyo hivyo, baada ya kumwambia haupo akaniuliza maswali mawili matatu akaniaga na kusema atarudi ukija ngoja tumsubiri,” Nelly akamwambia Ipyana.
“Huyo mama anaitwa mama Maduu alifiwaga na mumewe kitambo tu na siyo bahili wa fedha zake,kwani kuna wakati nikimuoshea gari lake hunipa mpaka shilingi elfu kumi,” Ipyana alimwambia rafiki yake na kuongeza;
“Halafu mama huyo anapenda sana vijana wadogo,” Ipyana alimwambia Nelly ambaye moyo wake ulipiga paa kwa kupata taarifa hiyo.
Wakati wakiendelea na maongezi yao, kumbe mama Maduu ambaye ofisi yake ipo ghorofani aliwaona akatoka na kushuka kwa lifti na kuelekea kwa akina Ipyana.
“Ipyana hujambo?” alimsabahi.
Baada ya salamu alimwambia kwamba alimuona ndugu yake na kumtania kama alikuja kumfundisha kazi ya kuosha magari,” Ipyana akamwambia alikuwa anajua.
Mama huyo alipopewa jibu hilo alimwambia hakuwa na muda mrefu alitaka wamuoshee gari lake na kwamba atafurahi sana kama kazi hiyo nitaifanya mimi, akaahidi liking’aa atanipa zawadi ya kunikaribisha kisha akawa anaelekea ofisini.
“Da! Ukisikia mtu nyota yake inang’aa bila kwenda kwa mganga ndiyo mimi, yaani hata huyu mama inavyoonekana ananitaka, dalili zote zipo wazi,” Nelson Nzamba aka Nelly aliwaza.
“Kaka si nilikuambia kuhusu wanawake wa hapa, umemsikia alivyokuambia mama?” Ipyana alimwuliza Nelly .
“Kaka sina cha kusema ila ndani ya wiki yule sijui dada Jully, Fatu au huyu mama lazima mmoja nitakupa ripoti kwamba nimeua, wewe subiri kwani siwezi kuwaacha viumbe wenye hela zao wajishaueshaue wakati fyekeo ninalo.
Ipyana alicheka sana na kumwambia awe makini lakini kwa sababu pale wizarani ngoma ilikuwa njenje, Nelly akamwambia hakuna binadamu atakayeishimilele acha ale ujana.
Siku hiyo waliosha magari na kupata shilingi 46,000 achilia shilingi elfu kumi aliyopewa Nelly na yule mama Maduu aliyejifanya kampa ofa ya kumuoshea gari lake vizuri kumbe alikuwa na lake jambo!
Kufuatia urafiki wao, baada ya kumaliza kazi Nelly na Ipyana walioga na kuvaa pamba zao na kuelekea kituo cha daladala cha Posta Mpya kupanda basi la Tandika.
Wakiwa kituoni Nelly ambaye mfukoni alikuwa na shilingi elfu 15 alimwambia Ipyana kwamba akifika Keko atashuka anataka kwenda kumuona mshkaji wake mmoja, Ipyana aliyemshtukia kwamba yalikuwa ni masuala ya mademu akacheka sana.
“Mbona unacheka?” Nelly alimwuliza.
“Wewe si useme unataka kwenda kuonana na mtoto unafikiri sikufahamu Nelly ?” Ipyana akamwambia.
Kama kawaida yake,Nelly alicheka ndipo Ipyana aliyekuwa akipenda sana maendeleo akafungua waleti yake akachomoawekundu wawili wa msimbazi akampatia Nelly aliyeshia kuporomosha tabasamu kwani alijua ishu yake ya kukutana na Atu itakwenda vizuri.
Wakiwa pale kituoni basi la Tandika lilifika wakapanda na kukaa siti moja,
Gari lilipoondoka, akapigiwa simu na Doreen ambaye alimtaka afanye awezavyo kesho yake waonane lakini Nelly alimwambia amsubiri mpaka wikiendi kwani sehemu aliyoanza kazi walikuwa bize sana.
Doreen hakuwa na jinsi zaidi ya kuwa mpole na kumwomba usiku wakutane kwa njia ya meseji ili amkate kiu kwa kutumia usanii wake kama alivyomfanyia siku ile.
“Usijali mpenzi mpenzi wangu,nitafanya hivyo,” Nelly alimwambia Doreen.
Gari lilipofika Keko, Nelly alimuaga Ipyana, Ipyana akaishia kucheka na kumtakia Nelly kazi njema.
Nelly alipoambiwa hivyo huku akishuka kwenye gari akawa anacheka kwani alijua alichokimaanisha Ipyana, gari lilipoondoka akiwa pembeni ya baraba alimpigia simu Atu.
“Niambie mpenzi wangu umeshafika nini hapo?” Atu alimwuliza.
“Yeah! Wewe uko wapi?”
Baada ya kuulizwa hivyo, Nelly alimwambia alikuwa kituo cha daladala ndipo Atu akamwambia kwa kuwa eneo lile watu walikuwa wakimfahamu atangulie katika gesti waliyokutana siku ya kwanza
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sharobaro Nelly alipoambiwa hivyo, aliachia tabasamu kwani alikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba siku hiyo angemchinjia mtu baharini.
Alipofika pale gesti hakutaka kusubiri, alichukua rumu kabisa kisha alimwomba mhudumu ampelee bia mbili, akavua shati, suruali na kubaki na boksa pekee akawa anamsubiri Atu.
“Huyu kiumbe akifika tu baada ya salamu jambo la kwanza nikumpatia mkomboti ndiyo mambo mengine yatafuata,nataka mpaka tutakapoachana niwe nimempa mikomboti miwili au mitatu,” Nelly aliwaza.
Hakumaliza hata dakika kumi na tano simu yake iliita alipoangalia mpigaji alikuwa ni Atu akapokea na kumwelekeza amuulize mhudumu amuoneshe namba ya chimbo alilokuwepo.
“Oke mpenzi wangu,” Atu alimwambia Nelly .
Ile kijana huyo mpenda mademu wazuri anaweka glasi iliyokuwa na pombe juu ya meza iliyokuwa mle chumbani akasikia mtu akigonga, akamfungulia na mtoto Atu aliyekuwa kapendeza akaingia.
Atu alipoingia alianza kucheka baada ya kumuona Nelly akiwa na boksa pekee huku mkuu wake wa kaya akiwa kachangamka, akajisemea moyoni; ‘Leo hapa ni kazi tu!”
Nelly hakutaka kusubiri, alimkumbatia na kumpiga mabusu kadhaa ya fasta midomoni, shavuni na masikioni, kufuatia msichana huyo kufanyiwa hivyo na kwa vile alimuona mkuu wa kaya wa Nelly alivyochangamka mwili ukamsisimka si kidogo.
Wawili hao, kwa dakika kadhaa walisahau kabisa shida za dunia wakawa wanakula tu denda a.k.a mua huku wakishikana maeneo mbalimbali ya miili yao hasa yale yenye shoti ya umeme.

ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment