Search This Blog

Wednesday, November 2, 2022

TIPWATIPWA TETEMA... OOH TETEMA! - 5

 







    Chombezo : Tipwatipwa Tetema... Ooh Tetema!
    Sehemu Ya Tano (5)




    “Nambie!” alisema kwa pozi alipopokea.

    “Poa da Jack, mambo yanaendaje?”

    “Fresh! Umenikumbuka mpaka jina, una kumbukumbu wewe! Nambie muuza samaki!”

    “Mi siitwi muuza samaki bwana, naitwa Chande.”

    “Haya nambie muuza samaki Chande, leo kuna nini mpaka umenikumbuka?”

    “Nimekumiss mshkaji wangu, nataka kukuona kibonge wangu wa ukweli.”

    “Mh! Siyo bure, kunimiss huko vipi?” alisema huku akichekacheka, ikabidi niwe ‘siriasi’ kidogo, nikaanza kumchombeza. Kwenye sekta hiyo nilifanikiwa kumteka kwani kila nilichokuwa naongea, yeye kazi yake ilikuwa ni kucheka tu, mwisho akanielekeza alipokuwa anaishi.

    “Nakaa Sinza Mori, hapa nyuma ya Lachaaz,” aliniambia, nikashusha pumzi ndefu na kumshukuru, nikamwambia asubuhi nitakuwa mgeni wake.

    “Tena ndiyo vizuri uje unisaidie kufua,” alisema huku akicheka, moyoni nikawa najua kwamba ‘imeisha hiyo’, nikakata simu huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wangu. Sikuwahi kutoka na mwanachuo kama Jack, ingawa nilikuwa na uzoefu sasa na wanawake wenye mwili kama wa kwake, huku mtaani tunawaita vibonge au matipwatipwa.

    Baada ya kumaliza kuweka mambo sawa, nilirudi kitandani na kujilaza, angalau mawazo ndani ya kichwa changu yakawa yamepungua. Haukupita muda mrefu, nikapitiwa na usingizi. Nilikuja kuzinduka baada ya kusikia mlango wangu ukigongwa kwa nguvu.

    Nikaamka harakaharaka na kwenda kufungua, hamadi! Nikakutana uso kwa uso na baba mdogo ambaye alikuwa akinitazama, akiwa amenikazia macho, nikajua nimekwisha.

    “Shika..moo baba!” nilimsalimia kwa kubabaika, hakuitikia salamu yangu na badala yake, alinionesha ishara kwamba nirudi ndani, naye akanifuata, akaja na kukaa kwenye uchago wa kitanda changu, huku akiwa bado amenikazia macho.

    “Chande! Najua kuna mambo unayoyajua kuhusu mama yako mdogo lakini hutaki kuniambia. Mimi nakuchukulia kama mwanafamilia lakini inawezekanaje uone mambo yanayonihusu hayaendi sawa halafu ukanyamaza? Huoni kama huo ni usaliti?” aliniuliza baba mdogo, nikawa natetemeka kwelikweli kwa sababu sikuwa najua kilichokuwa ndani ya kichwa chake.

    “Nimekuchagua wewe kuwa msimamizi wa hii biashara ya samaki ambayo siyo siri inanisaidia sana kuitunza familia lakini inakusaidia na wewe mwenyewe. Kwa nini unakuwa sehemu ya kunihujumu?” alisema, nikashusha pumzi ndefu na sasa nikawa naamini kwamba kumbe alichokisema mama mdogo kwamba hakuwa anajua chochote kuhusu masuala ya uhusiano wetu, yalikuwa ni ya kweli.

    “Baba kiukweli mimi unanilaumu bure tu, hakuna ninachokijua. Ma’mdogo ndiye aliyeniambia kwamba nisiende kuuza samaki kwa sababu kuna mteja wa jumla, jana aliniambia hivyohivyo na leo ameniambia hivyohivyo, nikajua una taarifa,” nilisema huku nikijitahidi sana kukwepesha macho yangu yasikutane na yake maana nilijua anaweza kuujua ukweli kwa kunitazama machoni.

    “Hawa wanawake siyo ndugu zetu kabisa, hata wewe ukija kufikia hatua ya kuoa unatakiwa kuwa makini sana, mwanamke anakuwa rafiki yako mambo yako yanapokwenda vizuri tu, mambo yakianza kwenda mrama anakuwa wa kwanza kukukimbia.

    “Huyu mamaako mdogo si unaona anavyoanza kunihujumu hapa, mambo yakianza kwenda vibaya nikakosa fedha za kumpa anunue anachokitaka, utasikia anatembea hata na muuza genge, hawana maana kabisa hawa,” alisema baba mdogo, safari hii akionesha kuwa mpole kwangu.

    Zile hasira zake zote zilimalizwa na maelezo ya uongo niliyompa, akaendelea kuzungumza na mimi kwa kirefu na kunitaka nisimamie vizuri biashara na mtu wa mwisho ambaye natakiwa kupokea maagizo kutoka kwake, ni yeye na si mtu mwingine yeyote.

    “Ikitokea anakwambia chochote, unatakiwa kuniuliza mimi kwanza. Akikwambia sijui kuna mteja wa jumla sijui nini, unatakiwa unipigie mimi simu kwanza usikie nitasema nini,” alisema, nikawa natingisha kichwa kuonesha kwamba namuelewa.

    Baada ya mazungumzo marefu, aliinuka na kutoka, akaniacha angalau nikiwa na amani ya moyo. Nilichokuwa nimekiamua kuanzia mwanzo ndicho nilichoendelea kukishikilia ndani ya moyo wangu, ilikuwa ni lazima nianze kumkwepa ma’mdogo kwa sababu tukiendelea tu, siku si nyingi baba mdogo angekuja kuujua ukweli na sijui nini ambacho kingekuja kutokea.

    Basi niliendelea kujilaza chumbani kwangu, chakula cha usiku kilipokuwa tayari, ma’mdogo ambaye sasa alikuwa na mumewe kule ndani, alimuagiza mwanaye mmoja aje kuniletea chakula kama ilivyokuwa utaratibu wa siku zote.

    Msosi huu haukuwa na u-spesho wowote, kilikuwa ni chakula nilichozoea kula siku zote, nikajua lazima ameogopa kufanya kama alivyofanya ndani ya siku mbili hizi kwa sababu mumewe alikuwepo. Nilikula na baada ya kumaliza, nilitoa vyombo na kwenda kuviweka kwenye karo pale nje.

    Wakati nanawa mikono, nilisikia mlango wa chumba cha yule mpangaji ukifunguliwa, akachomoza kichwa na kunitazama huku akigeuka huku na kule kuangalia kama hakukuwa na mtu aliyekuwa akitutazama. Akanionesha ishara kwa mkono kwamba niende, nikatabasamu.

    Nilitazama huku na kule na nilipojiridhisha kwamba hakukuwa na mtu anayetutazama, harakaharaka nilielekea kwenye chumba chake, nikachoma ndani mzimamzima.

    “Vipi! Umeshakula?”

    “Ndiyo!”

    “Nilikuwa nimekuandalia msosi wa nguvu nilipotaka kuja kukwambia nikamsikia baba’ako mdogo anaongea na wewe. Vipi kuna nini kwani maana nasikia muda mrefu ni kama wanavutana na mkewe. Amekushtukia nini?”

    “Aah! Hamna, ni ishu za kifamilia.”

    “Mi nakushauri Chande achana na mama’ako mdogo, siku mwenyewe akijua itakuwa kizaazaa hapa. Kwani mimi sikutoshi?” alisema kwa sauti ya kunong’ona, huku akijigeuzageuza kwa pozi za kikekike, mtandio mwepesi aliokuwa amejifunga ukalifanya umbo lake zuri lijichore, nikameza mate kama fisi aliyeona mfupa.





    “Kwani unataka kuse..ma we...we upo si...ngo,” nilisema kwa sauti ya kunguruma, huku shetani akionesha kutaka kunizidi nguvu. Alijibu kwa tabasamu pana kwamba hakuwa na mtu, kwa lugha nyepesi alikuwa singo.

    “Kweli?”

    “Kweli, ina maana huniamini?”

    “Basi sawa!” nilimjibu kwa sauti ya kunguruma, akawa tayari ameshanifikia mwilini na nikiwa bado nababaika nikiwa sijui cha kufanya, aliingiza mkono wake kwenye bukta niliyokuwa nimeivaa, akamkamata mkuu wa kaya ambaye tayari alishaanza ‘kufyumu’, nikiwa bado nagugumia kama dume la njiwa, si akapiga magoti kwa adabu na kuanza kuimba?

    Lilikuwa ni tukio lililotokea bila kuwa nimejiandaa, yaani sikufikiria kabisa kama angeweza kufanya hivyo, basi nikawa nababaika ile mbaya, japokuwa mdomoni sikuwa natafuna kitu chochote lakini nilikuwa ni kama natafuna ‘bablish’, utulivu uliniisha kabisa.

    Na yeye alipoona nimeyaelewa mashairi aliyokuwa ananiimbia, alizidisha mbwembwe huku akioneshwa kufurahishwa sana na jinsi alivyozibamba hisia zangu. Haukupita muda mrefu, nilianza kuhisi kama anataka kunihujumu kwa kunicheleweshea huduma ya muhimu niliyokuwa naisubiri.

    Nilimkamata kichwani utafikiri tuna ugomvi, nikajaribu kumuinua ambapo alikuwa mgumu kidogo, akionesha kunogewa na ‘kipaza sauti’. Nilitumia nguvu kidogo, akainuka na muda huohuo nilimnyanyua juujuu, kwa kuwa yeye hakuwa ‘tipwatipwa’, sikupata ugumu wowote kutekeleza kile nilichokuwa nimekikusudia.

    Nikambwaga kwenye uwanja wa fundi seremala, nikamalizia kuvua magwanda yaliyokuwa yamesalia mwilini, nikautoa na ule mtandio aliokuwa amejifunga kichokozi. Nilichojishangaa ni kwamba mchecheto niliokuwa nao, ungeweza kudhani pengine nimekaa hata miezi sita bila kukutana faragha na kiumbe wa jinsia tofauti na mimi.

    Haukupita muda mrefu tayari shughuli ya kutwanga mpunga ilikuwa imeanza. Nilikuwa nikitwanga kwa nguvu na kazi kubwa kwa lengo la kupata mchele haraka, badi naye akawa ananionesha ushirikiano mzuri kwa kukitegesha ‘kinu’ vizuri, huku akinihamasisha kuendelea na kasi ileile.

    Ilifika mahali nikawa naona kabisa kwamba kasi yangu inaelekea kumshinda kwa sababu alianza kuzungumza mambo yasiyoeleweka, wakati mwingine akitukana matusi mazitomazito, nikawa ni kama simsikii.

    Niliendelea kutwanga kwa nguvu, kasi na ufanisi wa hali ya juu na hakuchukua raundi, akawa tayari ameshakwea mpaka juu kabisa ya mnazi, akaangua madafu mawili na kuyapasua kwa mfululizo, akanikwida kwa nguvu huku akitoa ukelele fulani uliozidisha raha masikioni mwangu!

    Sikutaka kumuachia, niliendelea na kile nilichokuwa nakifanya, kwa kasi ileile, akatetemeka kama jenereta kwa sekunde kadhaa na kutulia tuli mithili ya maji mtungini, macho yake akiwa ameyafumba.

    Haukupita muda alifumbua tena macho yake na alipoona bado naendelea kutwanga ili kuzitenganisha pumba na mchele, na yeye alianza kunisaidia, safari hii akawa anapepeta kwa ufanisi wa hali ya juu.

    Mtanange wa nguvu uliendelea, kwa mara nyingine akakwea mpaka juu kabisa ya mnazi na safari hii sikutaka kumuacha aangue madafu peke yake, na mimi nilimfuata hukohuko, tukapasua wote madafu, kila mtu na la kwake! Yowe alilopiga, ungeweza kudhani labda ametokewa na jambo la kutisha sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akadondokea upande wa pili na hakuchukua hata dakika moja, akawa anakoroma kama jenereta bovu. Kwa jinsi nilivyokuwa najisikia, kama na mimi ningesema nijilaze kidogo tu basi ningepitiwa na usingizi palepale mpaka kesho yake asubuhi, jambo ambalo sikuwa tayari kuona linatokea.

    Kwa hiyo nilijikongoja na kuvaa magwanda yangu, nikafungua mlango kidogo na kuchungulia nje, nilipohakikisha hakuna mtu anayenitazama, nilichomoka kama mshale na kuingia bafuni, nikajimwagia maji harakaharaka na kuelekea chumbani kwangu.

    Nilipoingia, nilijifungia mlango kwa ndani kwa sababu sikuwa nataka tena usumbufu. Mpaka muda huo ba’mdogo hakuwa amekuja kunipa fedha kwa ajili ya kwenda kuchukua mzigo, kwa hiyo nikawa bado sina uhakika kuhusu ratiba zangu za asubuhi.

    Nilichokuwa nakiombea ndani ya moyo wangu ni kwamba ratiba ya kwenda kufuata mzigo wa samaki iahirishwe ili nipate nafasi ya kwenda Sinza Mori kuonana na ‘mtoto’ Jack. Kutokana na uchovu niliokuwa nao, haikuchukua muda mrefu, nikapitiwa na usingizi mzito.

    Nilipokuja kuzinduka, tayari kulikuwa kumeshapambazuka kabisa. Nilikurupuka kitandani na kwenda kujimwagia maji ili kuondoa uchovu na kikubwa kilichonisukuma kuamka haraka, nilikuwa nahofia kwamba baba mdogo akija kugundua kwamba sikuwa nimeamka mpaka muda huo, anaweza kufikiria kwamba zile hujuma alizozisema zinaendelea.

    “Vipi, mbona umeamka mbiombio? Nenda tu kapumzike, biashara utafuata kesho,” alisema baba mdogo baada ya kuwa nimeshamaliza kujiandaa na kwenda kule ndani kwake kumuuliza kuhusu fedha za kufuatia mzigo.

    Aliponiambia maneno hayo, japokuwa kwa nje nilijifanya kusikitika, lakini ukweli ni kwamba ndani ya moyo wangu nilikuwa nachekelea kwelikweli. Niliporudi chumbani kwangu, kitu cha kwanza ilikuwa ni kumtafuta ‘Jack Bonge’ kwenye simu na ili kuwa na uhakika, nilimuendea hewani.

    “Mambo!”

    “Poaa,” aliitikia kichovu.

    “Bado umelala?”

    “Ndiyo! Nimechoka kwelikweli, si unajua leo ndiyo siku yangu ya kupumzika?”

    “Nakuja basi.”

    “Upo siriasi?”

    “Ndiyo, kwani ulihisi nakutania?”

    “Mh! Una mambo wewe! Njoo basi nakusubiri,” alisema, nikakata simu na kuanza kushangilia utafikiri mchezaji aliyefunga goli kwenye mechi muhimu. Harakaharaka nilibadilisha nguo zangu, nikatafuta ‘pamba’ kali na kujipigilia kisawasawa, nikatoka kwa kunyata kwa sababu sikutaka mama mdogo anione.

    “Safari ya wapi mwenzetu? Mbona umependeza hivyo?”





    Kauli ya mam’dogo ilinizindua, nikatahayari kwa sababu sikuwa nimetegemea kama atanifuma, nilikuwa natoka kwa kunyata huku nikiwa natazama kule mlangoni kwake, kumbe mwenyewe alikuwa nje ya geti akifanya usafi.

    “Aah! Kuna sehemu naenda mara moja, vipi umeamkaje?”

    “Mh! Saa hizi ndiyo unaniuliza nimeamkaje?”

    “Aah! Nilishindwa kufanya chochote si najua kwamba mzee baba bado yupo?”

    “Kaondoka mapema sana leo, ana hasira tunataka kumuangusha mtaji wa samaki,” alisema mam’dogo ambaye sasa alikuwa ameacha kila kitu akawa ananitazama usoni. Ile angalia yake tu ilikuwa imebeba ujumbe fulani lakini kwa kuwa nilishakuwa nimefikia maamuzi ndani ya moyo wangu, niliamua kumuepushia mbali shetani.

    “Hapa nilikuwa nataka nikimaliza kufanya usafi nije kukugongea! Nina mazungumzo na wewe.”

    “Mazungumzo?” nilisema huku nikishusha pumzi ndefu, niliona kama ananichelewesha kwenye mishemishe zangu kwani tayari Jack nilishamwambia kwamba ndiyo natoka.

    “Ndiyo! Mbona unashtuka? Rudi ndani kwanza nakuja hukohuko, si unajua tena hapa nje wachawi wengi,” alisema, nikajaribu kumshawishi kwamba anisubiri nikirudi lakini aligoma katakata, nikawa sina ujanja, ikabidi nirudi ndani.

    Nilishajua ni nini alichokuwa anakitaka. Aliacha kufanya usafi, akapita mbiombio na kwenda ndani kwake, muda mfupi baadaye nikawa namsikia yupo bafuni anaoga. Ama kwa hakika alikuwa ameniweza kwenye ‘taiming’.

    Muda mfupi baadaye, mlango wa chumba changu ulifunguliwa, akaingia akiwa amejifunga upande wa kitenge ambacho kilikuwa kimelowa na kusababisha kishikane na mwili wake mkubwa, nikajikuta nikivutiwa kumtazama hasa maeneo ya nyuma.

    “Mwenzangu, mume wangu sijui ameanza kushtukia? Nahisi kuna mtu anaweza kuwa amemwambia kitu kuhusu mimi na wewe.”

    “Kwani vipi?” nilimuuliza huku mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio kuliko kawaida.

    “Jana kuna swali kaniuliza kuhusu wewe, inaonesha kabisa kuna kitu anakihisi.”

    “Si nilikwambia ukawa unanibishia?”

    “Hapana, siyo kwamba anajua chochote kama wewe ulivyokuwa unasema, anahisi tu. Imebidi nifanye kazi kubwa kumshawishi asinihisi vibaya, sikuwa na mpango wa kumpa lakini ilibidi nifanye hivyo ili asinielewe vibaya, lakini tukiwa katikati ya shughuli, aliniuliza kitu kingine kilichonifanya niishiwe nguvu.”

    “Kitu gani tena?”

    “Eti ameniuliza mbona ‘pango la mfalme Suleiman’ limeongezeka ukubwa kama kuna mtu ametoka kuingia muda mfupi uliopita?”

    “Weee? Ikawaje?”

    “Mh! Yaani we acha tu, mambo ni moto kwelikweli! Ikabidi niwe mkali na kumwambia anafikiria baada ya kunizalisha watoto wawili sasa nitabaki kuwa msichana kigori? Nimemchamba sana mpaka kaniomba msamaha. Lakini haya yote umeyasababisha wewe,” alisema huku akinipiga kakibao begani.

    “Sasa mimi nimesababisha nini tena?”

    “Huyu ndiyo kasababisha,” alisema, safari hii akimkamata mkuu wa kaya na kumvuta kidogo.

    “Unamuonea bure!”

    “Ila nimemsamehe! Mlete acheze na mwenzake,” alisema, kauli iliyonifanya nicheke sana, sikutegemea kwamba baada ya yale yote aliyonieleza bado anaweza kuzungumza kitu kama kile.

    “Hapana mam’dogo! Utasababisha mwenzako niuawe bure! Hivi unajua mke anauma sana? Na kama hivyo ameshaanza kuhisi mambo kama hayo unafikiri itakuwaje?”

    “Hawezi kujua, tutakuwa makini sasa hivi.”

    “Sasa umakini wenyewe ndiyo huu?”

    “Acha maneno weka muziki bwana!” alisema huku akinivutia kifuani kwake, ule upande wa kitenge aliokuwa amejifunga, tayari ‘alishautegua’ na kubaki na suti yake ya kulalia, akaanza kunitoa magwanda yangu na muda mfupi baadaye, wote tulikuwa saresare maua.

    Kiukweli moyoni sikuwa na furaha, kwanza kwa sababu amenikatisha safari yangu ya muhimu sana ya kwenda kuonana na Jack, hata nikienda kuonana naye sitakuwa na ule ‘moto’ ninaoutaka lakini pia, taarifa kuhusu baba mdogo zilinikosesha sana amani ndani ya moyo wangu. Nikawa najiuliza itakuwaje siku atakapotufuma ‘laivu’ maana huko ndiko tulikokuwa tunaelekea.

    Hali hiyo ilimfanya mkuu wa kaya awe mgumu kutoa ushirikiano kwa wakati, kama nilivyowahi kusema kwamba mam’dogo alikuwa mtoto wa mjini kwelikweli, haraka sana aligundua kwamba akili yangu haikuwa mchezoni, akaamua kutumia maarifa yake kupata kile alichokuwa anakitaka.

    Katika uchokozi wake wa hapa na pale sijui alifanya nini bwana, nilishtukia mkuu wa kaya akikurupuka kutoka kwenye maficho yake na kusimama mguu sawa kama yupo kwenye gwaride, nikawa sina namna zaidi ya kutii sheria bila shuruti.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Muda mfupi baadaye, ‘kiliwaka’ mle ndani, hata sijui mawazo yalipotelea wapi lakini nilijikuta nikiwa katikati ya shughuli ya kumuadhibu mam’dogo kwa uchokozi aliokuwa ananifanyia!

    Ajabu ni kwamba alionesha kufurahishwa sana na adhabu kali niliyokuwa naitoa, akawa ananipa ushirikiano wa hali ya juu, ‘bakora’ zikaendelea kwa kasi kubwa, nikamtandika kisawasawa mpaka kwa ule mtindo ambao Wazaramo huwa wanauita ‘mwana ukome’. Hakuchukua raundi, akatangaza kuiona theluji iliyopo juu kabisa ya kilele cha Mlima Kilimanjaro, akadondokea upande wa pili kama mzigo.

    Mara nikashtuka kusikia mlango wa chumba changu ukigongwa! Mwanzo nilihisi kama nimesikia vibaya lakini haikuwa hivyo, ni kweli mlango ulikuwa ukigongwa, nikakurupuka huku macho yakiwa yamenitoka pima, nikajua hatimaye ndege mjanja nimenasa kwenye tundu bovu!





    “Chandeee! We Chandeee!”

    “Naaam!”

    “Funguaa,” sauti ya baba mdogo ilisikika nje huku akiendelea kugonga mlango kwa nguvu, nikajua nimekwisha. Nilichokifanya, nilirudi pale kitandani ambako mama mdogo alikuwa amekaa, amekodoa macho akiwa hajui nini cha kufanya! Ama kwa hakika arobaini za mwizi zilikuwa zimetimia.

    “Ingia uvunguni,” nilimwambia, harakaharaka akafanya kama nilivyomwambia, nikasokomeza nguo chafu kule uvunguni na kumfunika kabisa. Nikaenda kufungua mlango huku kijasho chembamba kikinitoka.

    “Mbona umechelewa kufungua mlango kiasi hiki?”

    “Nilikuwa nimelala ba’mdogo, shikamoo!”

    “Ulikuwa umelala? Halafu mbona unatokwa na jasho jingi kiasi hiki?”

    “Najihisi kama nina homa, na feni ya humu ndani mbovu,” nilimwambia huku nikitetemeka mwili mzima. Hofu niliyokuwa nayo moyoni mwangu ilikuwa haielezeki, nikajiinamia.

    “Sasa weweee...” alisema baba mdogo huku akiingia chumbani kwangu, nilitamani nitoke nduki kali kwelikweli, ila mwili haukuwa hata na nguvu za kukimbia, nikarudi na kukaa kitandani huku nikitumia shuka langu kujifuta jasho.

    Laiti kama baba mdogo angejiongeza kidogo tu, angeweza kugundua kwamba nilikuwa namdanganya kwa sababu mazingira ya mle ndani yalikuwa yanaonesha wazi kabisa kwamba kuna tukio lilikuwa limetoka kufanyika, tena muda huohuo!

    “Kama unaumwa kwa nini huniambii? Au kwa nini hata humwambii mama’ako mdogo? Utakuja kufa humu ndani buree,” alisema huku akinitazama kwa macho yaliyoonesha kwamba ameukubali uongo wangu.

    “Jiandae uende ukapime malaria,” alisema huku akitoa noti ya shilingi elfu kumi na kunikabidhi.

    “Nilitoka asubuhi sana leo, kuna mahali nilikuwa nimeenda kufuatilia fedha zangu fulani hivi, ukisharudi hospitali uje nina mazungumzo na wewe kuhusu biashara yetu,” aliniambia huku akiinuka kutaka kutoka, ghafla akawa ni kama amekumbuka kitu.

    “Mama’ako mdogo yuko wapi?”

    “Hata sijui, huko nje sijatoka kabisa!”

    “Tena nimekumbuka!” alisema baba mdogo huku akirudi na kukaa pale kitandani kwangu, akanionesha na mimi ishara nikae pembeni yake.

    “Ujue Chande wewe ni mwanaume mwenzangu na siku hizi umeshakuwa mkubwa kwa sababu kwanza unaingiza wanawake wakubwa humu ndani kuliko hata mama yako mdogo! Katika siku za hivi karibuni unamuona mama’ako mdogo yupo karibu na mwanaume gani hapa mtaani maana nyendo zake zinanitia mashaka.”

    “Mh! Kwa kweli sifahamu baba kwa sababu muda mwingi mimi huwa sikai nyumbani, lakini muda mwingi ninapokuwa hapa huwa namuona yupo bize na biashara yake.”

    “Ujue hawa wanawake siyo watu wa kuwaamini kabisa! Nahisi kuna mjinga mmoja ananilia mali zangu! Siku nikimgundua nitaua mtu haki ya nani tena! Nampenda sana mke wangu.

    “Sasa nakupa kazi, hebu mfanyie uchunguzi wa chinichini bila mwenyewe kujua! Nataka jina tu la huyo anayecheza na mali za watu, nitamchinja kama mbuzi na nitahakikisha natenganisha kabisa kichwa, bora nikafie gerezani!

    “Yaani mimi nahangaika kumlea mwanamke anapendeza halafu mtu mwingine aje kujilia kirahisirahisi tu, tena siku nikimkamata itabidi kwanza nimuoe ndiyo nimchinje,” alisema baba mdogo huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.

    Mapigo ya moyo yalinilipuka na kuanza kunienda mbio kwelikweli, nikawa navungavunga kwa kumtetea mama mdogo, ila nikamhakikishia kwamba nitaifanya kazi yake kama alivyonituma.

    “Wahi kwenda hospitali, akija usimwambie kwamba nilirudi,” alisema baba mdogo huku akitoka na kuurudishia mlango, nikashusha pumzi ndefu na kutoka kuhakikisha kama kweli ameondoka. Ilibidi kwanza nikimbilie msalani kwa sababu hali niliyokuwa nayo ilikuwa haielezeki, nadhani kama angeendelea kunibana kidogo tu haja ndogo ingenitoka.

    Harakaharaka nilirudi ndani na kutoa mafurushi ya nguo kule chini ya kitanda, nikampa ishara mama mdogo atoke, akatoka huku na yeye akitetemeka kuliko kawaida. Hakukuwa na mazungumzo, harakaharaka alijifunga kitenge chake vizuri, akaelekea ndani kwake mbiombio.

    “Ooh! Ahsante Mungu,” nilisema huku nikiinua mikono juu kama ishara ya kumshukuru Mungu wangu, ama kwa hakika nilikuwa nimeponea kwenye tundu la sindano. Baada ya mama mdogo kwenda kule ndani kwake, harakaharaka nilienda bafuni kujimwagia maji kwa sababu hali niliyokuwa naihisi ilikuwa haielezeki.

    Nilirudi chumbani kwangu na kuanza kujiandaa, zile nguo nilizokuwa nimezivua awali, nilizivaa tena na kujiweka sawa. Muda huohuo nilimsikia mam’dogo akiwa anajimwagia maji bafuni!

    Nikafunga mlango harakaharaka na kutoka huku bado nikiwa na hofu kubwa ndani ya moyo wangu, bado nilikuwa siamini kama nimenusurika kwenye mtego ule hatari. Wakati namalizia kufunga mlango, mam’dogo naye alikuwa anatoka bafuni, akaniangalia kwa macho ya kuibia kisha harakaharaka akaelekea ndani kwake.

    Nadhani maneno ya mumewe yalikuwa yamemjaza hofu kubwa ndani ya moyo wake kuliko kawaida kwa sababu hata lile tabasamu lake la siku zote lilipotea kwenye uso wake. Nilitoka kimyakimya na safari ya kuelekea ‘hospitali’ ilianza.

    Kumbe baba mdogo hata hakuwa ameenda mbali kwa sababu wakati natoka getini, nilikutana naye akiwa anaingia, mkononi akiwa amebeba mkate, nadhani ni kwa ajili ya kunywea chai.

    “Ndiyo unaenda hospitali?”

    “Ndiyo baba!”

    “Sawa, basi usichelewe! Kama hela haitakutosha utanipigia simu,” aliniambia huku akinipisha nipite, nikaondoka ‘wanguwangu’ na kupotelea mitaani, huku moyoni nikiwa sijui nini kitakachotokea kule ndani kati yake na mkewe.

    Licha ya misukosuko hiyo iliyotokea, bado mipango yangu ya kwenda kuonana na Jack ilikuwa palepale, nilipofika kituoni, nilimpigia simu, akapokea na kuanza kulalamika eti kwa nini sijafika mpaka muda huo.

    “Foleni mama, nipo jirani nakuja lakini kuna bonge la foleni, usijali nakuja!”

    “Fanya haraka bwana,” alisema Jack kwa sauti ya kudeka flani hivi, nikakata simu na kushusha pumzi ndefu.





    Akili yangu haikuwa imetulia kabisa, muda mwingine nikawa natetemeka mwenyewe kwa hofu huku maneno ya baba mdogo yakijirudia ndani ya kichwa changu.

    “Yaani mimi nahangaika kumlea mwanamke anapendeza halafu mtu mwingine aje kujilia kirahisirahisi tu, tena siku nikimkamata itabidi kwanza nimuoe ndiyo nimchinje!” kile alichokisema baba mdogo kilijirudia ndani ya kichwa changu, nikawa naitafakari kauli hiyo.

    Mambo ya mwanaume kumuoa mwanaume mwenzake, kisha baada ya hapo amchinje na kutenganisha kichwa? Eti kisa cha yote hayo ni mwanamke tu? Niliona kama nikifanya mchezo kweli naweza kujikuta kwenye matatizo makubwa.

    “Hapana! Hapana! Nimekoma,” nilisema huku nikiendelea kutetemeka kwelikweli, kijasho chembamba kikawa kinanitoka.

    “Vipi, unaumwa kijana wangu?”

    “Aah! Hapana, hapa...na! Najisikia vibaya.”

    “Ooh! Maskini polee! Unaelekea wapi kwani?”

    “Naenda Sinza Mori!”

    Mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa abiria waliokuwa wakisubiri daladala pale kituoni, aliniuliza baada ya kuona hali yangu ikiwa si ya kawaida. Mara tu baada ya kumaliza kuzungumza na Jack na kumdanganya kwamba nipo kwenye foleni, nilianza kujisikia hali isiyo ya kawaida.

    Mwili ulikuwa kama unachemka, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio, jasho linanitoka lakini wakati huohuo, nikitetemeka utafikiri nimewekwa kwenye friji. Ni sababu hiyo ndiyo iliyomshtua abiria huyo ambaye naye alikuwa akisubiri usafiri.

    “Ooh! Maskini polee, jaribu kunywa maji yanaweza kukusaidia,” aliniambia kwa upole, nikamuona akienda kununua maji ya baridi kwa muuzaji aliyekuwa pale kituoni na kuniletea. Ujue wanawake wengi ni viumbe walioumbwa na huruma sana! Ni rahisi sana mwanamke kukupa msaada anapokukuta ukiwa kwenye hali ya uhitaji, kuliko mwanaume.

    Basi niliyapokea yale maji na kuanza kuyagida mfululizo! Ndani ya muda mfupi tu, chupa nzima ilikuwa imeisha, nikashusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye kiti, yule abiria mama akawa amekaa pembeni yangu akiwa ananitazama kwa makini.

    “Vipi unajisikiaje?”

    “Aah! Najisikia ahueni kubwa sana, asante mama! Ahsante sana.”

    “Maji ni dawa! Tena dawa nzuri kwelikweli!” aliniambia, basi nikamshukuru sana. Muda mfupi baadaye, daladala ilikuja, hata sijui yule mama alipotelea wapi maana nilitaka kumshukuru tena na kumuaga kabla sijaondoka kwa sababu huo ndiyo uungwana, niligeuka huku na kule nikimtafuta lakini sikumuona, basi nikamshukuru kimoyomoyo kisha nikapanda kwenye daladala.

    “Njoo ukae! We dada mpishe huyo kijana anaumwa nimemuwekea siti,” alisema yule mama huku akinionesha ishara. Kumbe wakati mimi nikiwa nimezubaa pale kituoni, yeye aliwahi kupanda kwenye daladala na kwenda kunikabia siti!

    Kiukweli nilifurahi sana ndani ya moyo wangu kwa upendo aliokuwa akiuonesha yule mama ambaye kiumri naweza kusema kwamba ni mwanamke wa makamo, akiwa na kati ya umri wa miaka thelathini na tano hadi arobaini.

    Nilijisikia amani ndani ya moyo wangu, basi haikupita muda mrefu yale mawazo ndani ya kichwa changu ambayo ndiyo yaliyosababisha niwe kwenye hali ile yalianza kujirudia tena.

    “Unaitwa nani kijana.”

    “Naitwa Chande.”

    “Unaonekana haupo sawa! Nini kinakusumbua, hebu nieleze labda naweza kukupa msaada, ujue wewe ni kama mwanangu!”

    “Mh! Mama, kuna mambo yananichanganya sana kichwa hata sielewi cha kufanya,” nilisema huku nikimtazama machoni. Alionesha kuwa mwanamke mwenye moyo wa kipekee sana na japokuwa hakuwa amefikia ‘levo’ ya kulingana na mama, kwa heshima niliamua kumpa cheo hicho.

    “Nimekuona kuanzia kule kituoni ndiyo maana nikakushauri unywe maji. Unasumbuliwa na nini kwani? Mchumba wako amekukataa?” aliniuliza swali ambalo sikulitegemea, nikajikuta nikitabasamu na kukwepesha macho kwa aibu.

    Sikutaka kumueleza kila kitu ndani ya daladala kwa sababu ningewafaidisha watu wengine lakini kutoka ndani kabisa ya moyo wangu, nilikuwa nahitaji mtu wa kumshirikisha mambo yaliyokuwa yananisibu kwa sababu nilikuwa najihisi kuchanganyikiwa.

    “Ni stori ndefu kidogo, siwezi kukuhadithia hapa kwenye gari,” nilisema, akiwa anataka kuzungumza kitu, kisimu changu kilianza kuita mfululizo, basi harakaharaka nikaingiza mkono mfukoni na kukichomoa lakini katika hali ambayo sikuitegemea, kiliniponyoka na kudondoka chini, basi betri ikaangukia upande wake, laini upande wake na mfuniko upande wake.

    Lilikuwa ni tukio la aibu kwangu kwa sababu nilijitahidi kuvaa vizuri na kupendeza lakini simu niliyokuwa naitumia ilikuwa inaniangusha sana. Aliyekuwa akinipigia alikuwa ni Jack na nakumbuka siku ile aliponiona nayo kwa mara ya kwanza alinicheka sana na kuniambia kwamba atanipa simu yake ndogo anayotumia lakini kwa bahati mbaya tukapotezana mpaka siku hiyo.

    Yule mama alinisaidia kwa kila kitu, akanipa simu yangu ikiwa imesharudishiwa jinsi ilivyokuwa mwanzo, nikajihisi aibu kubwa ndani ya moyo wangu.

    “Makumbusho mwisho wa gari!” konda alisema kwa sauti ya juu, ni hapo ndipo nilipogundua kwamba kumbe tulishafika mwisho wa gari!

    Kwa kuwa mimi nilikuwa nimekaa dirishani, ilibidi yule mama ambaye bado sikuwa najua anaitwa mama nani mpaka muda huo au anajishughulisha na kazi gani, alinyanyuka na kuchukua mkoba wake, akanishika mkono kama mama anavyomshika mkono mwanaye wanapovuka barabara ili asije akagongwa na magari.

    “Tunaomba njia jamani, nipo na mwanangu mgonjwa,” alisema yule mama ambaye alikuwa na lafudhi fulani hivi ya kama Mzanzibari, basi tukashuka mpaka chini huku akiwa bado amenishika mkono, tukasogea pembeni ambako kidogo kulikuwa na utulivu.

    “Kwa hiyo hapa Mori si unaweza kufika mwenyewe?”

    “Ndiyo mama! Nashukuru sana.”

    “Haya! Mimi naelekea Mikocheni! Hapa inabidi nichukue Bajaj, au nikufikishe unakoenda?”

    “Aah! Hapana mama, nashukuru! Nashukuru sana.”

    “Sawa mwanangu! Hebu andika jina lako na namba yako ya simu hapa, najua una mengi ya kuniambia lakini muda hautoshi,” alisema huku akitoa simu yake kubwa na nzuri ambayo ilinifanya niduwae kidogo nikiishangaa. Basi nikaandika namba yangu na jina.

    “Mh! Kumbe unaitwa Chande?”

    “Ndiyo mama!”

    “Haya mwanangu, yangu ni hiyo inayoishia na kumi na mbili, nitakuflash ukiwasha simu,” alisema huku akianza kutembea kuelekea upande wa pili kulikokuwa na Bajaj, nikamsindikiza kwa macho mpaka alipopanda kwenye Bajaj na kuondoka! Nilifurahi sana kutokana na wema alionionesha ambao ulinisahaulisha kabisa msala uliotokea nyumbani.

    Harakaharaka nikaelekea kwenye daladala za kuelekea Sinza, nikawasha kisimu changu na kumpigia tena Jack ili nimwambie kwamba nimeshakaribia.





    “Uko wapi kwani?”

    “Nipo hapa jirani, sasa hivi nashuka hapo Sinza Mori.”

    “Muda wote huo hufiki tu? Kama hauji niambie bwana,” alisema kwa sauti fulani ya kudeka hivi, basi nikamhakikishia kwamba ni kweli ndani ya muda mfupi nitakuwa nimeshafika, akakata simu.

    Muda huo bado nilikuwa Makumbusho lakini nikiwa nimeshapanda daladala zinazoenda Kariakoo kwa kupitia Sinza. Daladala ilianza safari, nikashusha pumzi ndefu na kutulia, huku nikiwa na shauku kubwa ya kuonana na Jack.

    Hatimaye niliwasili Sinza Mori, nikalipa nauli nakuteremka pale kituoni, nikawa nashangaashangaa huku na kule. Sikuwa nimewahi kufika Sinza Mori zaidi ya kuwa napasikiasikia tu, nikatafuta sehemu ya kukaa na kutoa kisimu changu.

    Nilipoishika tu, ilianza kuita kuonesha kwamba Jack alikuwa ananipigia.

    “Nimeshuka hapa kituoni tayari,” nilimjibu harakaharaka, nikamsikia akishusha pumzi ndefu, akanielekeza sehemu ya kuelekea.

    “Fuata hiyo barabara ya lami inayoingia ndani upande huohuo ulioshukia, njoo mbele utaniona,” aliniambia, nikageuka na kuanza kuitafuta barabara aliyonielekeza. Muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa nikifuata uelekeo alionipa.

    Nilitembea na kupita lile eneo lililochangamka sana, mbele kidogo nikamuona Jack akiwa amesimama kwenye kibaraza cha nyumba moja iliyokuwa jirani kabisa na barabara, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio.

    “Whaoo! Siamini kama kweli umekuja,” alisema Jack huku akinikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu, na mimi nikapitisha mikono yangu kwenye mwili wake mkubwa, nikamkumbatia kwa furaha.

    “Karibu jamani! Nilikumiss mpaka naumwa mwenzio, angalia nilivyokonda,” alisema na kusababisha wote tucheke sana, basi akanishika mkono kwa upendo na kuanza kuniongoza kwenda ndani kwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa anakaa chumba cha uani, basi tulipoingia kwenye geti, kuna wanawake walikuwa wakifuafua pale uani, Jack akavunja ukimya.

    “Mnamuona mchumba wangu? Kila siku mnaniulizauliza haya huyu hapa sasa,” alisema Jack na kusababisha wote wacheke na kuinua shingo zao kunitazama.

    “Karibu mchumba wa Jack,” alisema mwanamke mmoja mweupe, naye kibonge hivi huku uso wake ukiwa na tabasamu.

    “Ahsante sana,” niliitikia huku nikiinamisha kichwa chini kwa aibu. Ujasiri wangu mimi ni kwa mwanamke akiwa mmoja, lakini wakishakuwa wengi tu, basi huwa najihisi aibu isiyo na kifani, ama kwa hakika Jack alikuwa ameniweza.

    “Kila siku wananiuliza eti mbona nakaa peke yangu, nikawaambia mume wangu yupo bize, naona leo wamekuona watafyata mikia yao,” alisema Jack huku akionesha kuwa na furaha kubwa ndani ya moyo wake, moyoni nikawa nachekelea kwa sababu sasa kazi ilikuwa nyepesi kuliko nilivyokuwa nimefikiria.

    Jack alikuwa anaishi kwenye chumba kimoja lakini kilichokuwa na mpangilio wa hali ya juu. Alikuwa na kitanda kimoja matata sana, kikubwa na cha kisasa, alikuwa na sofa moja mle ndani, dressing table na runinga kubwa aliyokuwa ameibandika ukutani.

    Japokuwa alikuwa mwanafunzi kama mwenyewe alivyoniambia, lakini alikuwa amejikamilisha kwelikweli. Moyoni nikawa najua kwamba lazima yupo jamaa ambaye ndiyo anayesimamia ‘shoo’ nzima ingawa sikutaka kumhoji chochote kuhusu suala hilo.

    “Najua hujanywa chai, ngoja nikuandalie fastafasta mume wangu,” alisema Jack na kuzidi kuukosa mno moyo wangu. Akawasha jiko la gesi lililokuwa kwenye kona moja ya chumba chake na kuanza kukaangiza, nikawa nimekaa pale kwenye sofa kwa adabu kwelikweli, huku nikitafakari yangu ndani ya kichwa changu.

    Muda mfupi baadaye, tayari alikuwa ameshakamilisha, akaniandalia na kunisogezea meza ndogo ya kioo ilikuwa na kifungua kinywa cha nguvu, akaja kuninawisha mikono, na yeye akanawa, tukaanza kula huku stori za hapa na pale zikiendelea.

    “Mbona umekaa kimachalemachale kama unataka kukimbia!”

    “Mh! Ndani kwako kuzuri sana Jack mpaka naogopa,” nilisema na kumfanya acheke sana.

    “Hapa ndipo ninapoishi! Kama nilivyokueleza sijaolewa wala sina mchumba, usipate kichwa kisa nimekutambulisha kwamba wewe ndiyo mchumba wangu, mi nipo singo na sitaki mwanaume kwa sasa,” aliniambia na kusababisha nicheke sana. Nilikumbuka ile kauli yake siku ile wakati ananipa namba yake ya simu, eti akaniambia lakini usinitongoze tafadhali, nakuomba!

    “Wala sitakutongoza usiwe na wasiwasi naona umeanza kujishtukia,” nilisema na kusababisha acheke sana, nadhani na yeye alikumbuka siku ile ya kwanza tulipokutana. Tulipomaliza kupata kifungua kinywa, alitoa vyombo, tukawa tunaendelea na stori za hapa na pale.

    Katika mazungumzo yake, nilimsoma Jack kwamba ni kweli hakuwa na mwanaume lakini alionesha sana kuwa na hamu ya kuwa kwenye mahusiano, kama kawaida yangu nikaanza kumchombeza kwa maneno matamu huku nikiw ana uhakika kwamba mpaka muda wa kuondoka ukifika, kitakuwa kimeshaeleweka.

    “Nakupenda Jack!”

    “Si umesema hautanitongoza wewe? Nini kimekusibu,” alijibu kimasihara, nikaona kama sitakuwa ‘siriasi’ kweli naweza kuambulia patupu, ikabidi nihame pale kwenye sofa nilipokuwa nimekaa na kuhamia kwenye kitanda kikubwa kilichokuwa mle ndani, nikapitisha mkono wangu kichokozi na kumshika kiuno, akaruka huyo utafikiri amechomwa na mwiba!

    “Usinifanyie hivyo please, naweza kufa mwenzio,” aliniambia, safari hii yale masihara yakianza kupungua, nikamvutia kifuani kwangu na kumbusu, kitendo kilichomfanya ajisikie aibu sana.

    “Niko siriasi Jack, kweli nataka mwanamke wa kuanzisha naye uhusiano, aje kuwa mama wa watoto wangu na wewe ndiyo chaguo langu,” nilimbembeleza kwa sauti ya kimahaba, akawa anakwepeshakwepesha macho yake huku wakati mwingine akinitazama kwa macho ya kurembua.

    “Mimi nawaogopa sana wanaume, nitakuaminije?”

    “Niamini mama, nakupenda sana Jack, nakupenda mwenzio,” nilizidi kubembeleza huku mikono yangu ikiendelea kupita kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumfanya awe anajinyonganyonga mithili ya chatu aliyemeza mbuzi, taratibu nikaanza kuhisi kwamba mkuu wa kaya anachaji.

    “Kafunge mlango kwanza!” aliniambia, nilitamani kuruka juu na kushangilia, nikajua mambo yanaenda kujipa, harakaharaka niliinuka na kwenda kufunga mlango kwa ndani, nikageuka na kumtazama akiwa bado palepale kitandani. Mkuu wa kaya alishafyumu kiasi cha kushindwa kujificha, akainyanyua nguo yangu upande wa mbele kwa jazba kali.

    “Khaaa! Hicho nini?”







    “Aah! Kawaida tu, usiogope!” nilisema huku nikimrudisha mkuu wa kaya kwenye himaya yake kwa sababu sasa alikuwa anataka kuniaibisha.

    “Umesema unanipenda si ndiyo?”

    “Ndiyo!”

    “Upo siriasi?”

    “Nipo siriasi, nataka nikuoe.”

    “Nataka ufanye jambo moja tu ambalo litanithibitishia kwamba kweli unanipenda na upo sirias unataka kuanzisha maisha na mimi.”

    “Niambie chochote! Nipo tayari mama.”

    “Nataka tuongozane mguu kwa mguu tukapime afya zetu,” alisema Jack, kauli iliyofanya mapigo ya moyo wangu yalipuke na kuanza kunienda mbio kwelikweli. Mkuu wa kaya alinywea ghafla na kuwa mdogo kama ‘piriton’, ama kwa hakika nilipatwa na mshtuko mkubwa mno.

    Kilichonishtua na kunifanya niwe na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wangu ni kutokana na nyendo zangu. Nilikuwa nimejisahau mno kiasi kwamba sikuwa najali tena kuhusu afya yangu, nilichokuwa nimekiweka mbele ilikuwa ni kutimiza haja za mwili wangu tu.

    Kibaya zaidi ni kwamba sikuwa nakumbuka kabisa suala la kutumia kinga! Nilianza kuhesabu ndani ya kichwa changu idadi ya wanawake niliokuwa nimeangukia nao dhambini kizembe bila hata kinga, watoto wa mjini wanaita kuuza mechi.

    Kabla ya kuangukia kwa tipwatipwa Sandra wa Magomeni, nilikuwa na orodha ndefu ya mahausigeli niliokuwa nimeangukia nao dhambini kutokana na kazi yangu ya kuuza samaki. Kama nilivyoeleza mwanzo, kazi yangu ya kuuza samaki ilikuwa inanikutanisha na wanawake wa kila aina.

    Awali wakati natoka kijijini nilikuwa nawaogopa sana wanawake lakini baada ya kuja mjini na kuianza kazi ya kuuza samaki hapo ndipo mambo yalipoanza kubadilika.

    Mahausigeli wengi walikuwa wakinizoea sana na wengine wakawa wanataka niwapunguzie bei au wakati mwingine niwape bure samaki kwa makubaliano ya kutembea nao!

    Ushamba wa kutoka bush ulinifanya nisiwe naona mbele, nikawa kazi yangu ni kuwapanga foleni na kiukweli, sikuwa hata nakumbuka idadi ya mahausigeli niliokuwa nimeangukia nao dhambini, tena wengi tukifanyia uchafu kwenye vitanda vya mabosi zao wakiwa kazini.

    Nilipokutana na tipwatipwa Sandra na kuonja ladha ya vibonge, ndipo nilipoamua kubadilisha gia angani na sasa nikawa sitaki tena mahausigeli! Baada ya kutoka na Sandra ambaye nilimpeleka mpaka magetoni kwangu na kusababisha ma’mdogo anifume nikiwa namtoa asubuhi, ni kama nilikuwa nimefungulia bomba.

    Ndani ya kipindi kifupi tu nilimgalagaza Mimah kisawasawa na kibaya zaidi kumbe alikuwa mke wa mtu, mumewe alisafiri kwenda nje ya nchi!

    Kama hiyo haitoshi, nikajikuta pia nikishindwa kuruka mtego wa ma’mdogo, naye nikaangukia naye dhambini mara kibao! Yule mpangaji aliyeshuhudia mchezo nikitoka kuvunja amri ya sita na mamdogo, naye nikampitia na sasa nilikuwa na Jack.

    Kama nilivyosema, huko kote sikuwa nakumbuka kabisa kutumia kinga! Ni kama nilikuwa nalamba asali kwenye ncha ya kisu chenye makali huku na huku!

    “Vipi mbona unatokwa na jasho jingi kiasi hicho?”

    “Aah! Si unajua tena feni yako haipepei vizuri na hili joto la Dar ndiyo kabisaa!” nilisema nikijaribu kuvunga mbele ya Jack kuhusu kilichokuwa kinapita ndani ya kichwa changu. Aliamka na kwenda kuongeza kasi ya feni mpaka mwisho lakini bado kijasho kikawa kinaendelea kunitoka.

    “Nasubiri jibu lako! Vipi mbona kama unasitasita,” Jack aliniambia huku akiwa amenikazia macho. Kiukweli ule urembo wote aliokuwa nao, haukuonekana tena machoni mwangu, ile shauku kubwa ya kuonja asali yake niliyokuwa nayo, yote iliyeyuka na moyoni nikawa najilaumu sana kwa kukubali kwenda kuonana naye.

    “Ha...hai..na tatizo Jack,” nilisema kwa kubabaika, eti kauli yangu hiyo ikamfanya afurahi sana na kuja kunibusu shavuni na kunikumbatia. Harakaharaka akainuka pale alipokuwa amekaa na kuanza kubadilisha nguo mbele yangu lakini huwezi kuamini mkuu wa kaya alikuwa ni kama amewekwa kwenye friji.

    Zile mbwembwe zake zote ziliisha kabisa! Hakufukuta wala kuleta fujo na kujifanya amefyumu kama kawaida yake anapoona kitoweo mbele yake. Ama kwa hakika nilikuwa nimepatikana.

    Akavaa suruali iliyombana vizuri mapaja yake yaliyokuwa yamenona kwelikweli na kumfanya ‘chura’ wake mkubwa atune kwa upande wa nyuma, akavaa na fulana f’lani hivi ya kijanja, akajipulizia manukato mazuri na kuchukua kipochi chake kidogo, kisha akanipa ishara kwamba niinuke.

    Nilisimama huku nikiwa natetemeka kwelikweli lakini nikawa najificha ili asijue kilichokuwa kinaendelea ndani ya moyo wangu.

    “Yaani tukipima na kama wote tuko salama, nitakupa zawadi ya mwili wangu na leo sitataka uondoke ikiwezekana ulale hapahapa, kazi itakuwa moja tu,” alisema huku akinikumbatia na kunibusu tena, nikawa nalilazimisha tabasamu.

    Tulitoka, Jack akawaaga majirani zake kwa uchangamfu eti akisema ‘mista’ yaani mimi nimeamua kumtoa kwenda kula ‘lunch’, basi wale wanawake wakawa wanacheka kwa furaha lakini moyoni mwangu nilikuwa kwenye wakati mgumu kwelikweli.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tulitoka mpaka barabarani, akasimamisha Bajaj, tukapanda, akamuelekeza dereva sijui atupeleke hospitali gani siikumbuki vizuri jina, nikajua kweli Jack amedhamiria. Mle kwenye Bajaj kulikuwa kumefunguliwa muziki mkubwa, ule wimbo wa Jebby uitwao Marehemu Ameacha Orodha ukawa unapigwa kwa sauti kubwa na kuzidi kuniongezea mchecheto.

    Nilivuta picha na kujiona nikiwa nimekonda sana, mwili mzima ukiwa na vidonda na nikikohoa sana kutokana na maambukizi ya Ukimwi, mapichapicha ya majeneza, watu wakiwa msibani na misalaba makaburini yakawa yanapitapita kwenye kichwa changu na kuzidi kunipagawisha.

    “Hebu ngoja kwanza, dereva hebu simama!” nilisema kwa sauti ya juu, Jack akanigeukia kwa mshangao.







    “Vipi tena?”

    “Nimepigiwa simu kuna dharura nyumbani! Wewe nenda mimi nitakuja siku nyingine,” nilimwambia huku nikiwa tayari nimeshasimama na kwa kuwa nilikuwa nimepanda upande wa mlangoni, Bajaj iliposimama tu, niliruka na kuzunguka upande wa nyuma, nikavuka barabara mbiombio huku nikikoswakoswa na magari na bodaboda.

    “Chandeee! Una nini wewe?” aliita Jack kwa sauti ya juu lakini tayari alishachelewa, daladala iliyokuwa inatokea upande wa Shekilango ikielekea Makumbusho ilikuwa imenikaribia, nikaipungia mkono, ikasimama! Nikajichoma ndani na safari ikaanza huku nikigeuka kumtazama Jack na yule dereva wa bodaboda ambao walikuwa wamepigwa na butwaa.

    Niliwaona wakigeuza Bajaj na wakawa wanaifuata ile daladala yetu kwa nyuma, Jack akawa ananipigia simu yangu, nikapokea.

    “Mbona sikuelewi Chande!”

    “Nimepigiwa simu Jack! Nyumbani kuna matatizo.”

    “Muongo! Muda wote upo na mimi mbona sijaona simu yako ikiita?”

    “Imeita Jack, kweli tena.”

    “Unakimbia kwenda kupima si ndiyo?”

    “Ha...pa...na! Sijakimbia.”

    “Kwa hiyo kumbe wewe unajijua una ngoma ulikuwa unataka kuniambukiza si ndiyo?”

    “Mimi sina ngoma Jack! Kweli tena, huwa natumia kinga,” nilidanganya huku nikitetemeka. Hofu ya kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ilinifanya niwe mithili ya kifaranga cha kuku kilicholowanishwa na mvua.

    “Sasa sikia! Najua hujapigiwa simu wala nini ila umekwepa kupima ngoma! Nakupa nafasi ya mwisho, shuka kwenye daladala sisi tupo nyuma yako, mguu wangu mguu wako mpaka hospitali tukapime. Ukikataa kwenda kupima leo basi naomba usinitafute tena.”

    “Nitakuja Jack lakini siyo sasa hivi! Nakuomba unielewe! Nitakuja, kweli tena, siyo kwamba naogopa kupima,” nilisema lakini Jack akakata simu akionesha kupandwa na jazba. Mbele kidogo niliishuhudia ile Bajaj ikigeuza na kurudi kule ilikotoka, nikashusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye siti yangu.

    Kumbe wakati naongea na Jack, nilikuwa naongea kwa sauti ya juu kiasi cha kufanya abiria wengine wote wawe wananitolea macho huku wengine wakibonyezana. Nikasikia wengine wakianza kucheka chinichini huku wakinitazama kwa macho ya kuibia.

    “Vipi kijana, unaogopa kupima ngoma? Inaonesha una mambo mengi wewe.”

    “Aah! Hamna mzee, huyu dada anataka kunichanganya.”

    “Sasa unaogopa nini? Si bora ukapime ili ujue moja! Siku hizi kuna dawa na ukifuata masharti unaweza kuishi miaka mingi tu, nakushauri nenda kapime,” yule mzee niliyekuwa nimekaa naye siti moja alianza kunihubiria kwa sauti kubwa, nikaona kama anazidi kuniletea ‘uchawi’.

    “We mzee vipi wewe? Nakuheshimu ujue,” nilisema kwa sauti ya juu huku nikisimama pale nilipokuwa nimekaa, abiria wengine wakaanza kuchangia hoja, eti kila mtu akinishauri nikapime.

    “Nyie mmepima? Mbona mnanishikia bango mimi? Kwanza sijawahi kufanya mapenzi, mimi bado mdogo,” nilisema kwa sauti ya kupaniki na kusababisha abiria wote ndani ya daladala waangue vicheko kwa nguvu.

    “Hata macho yako yanaonesha kwamba wewe ni mjanjamjanja sana wa wanawake! Naona umepatikana leo, kapime kijana,” walizidi kunishambulia nikaona njia nyepesi ya kuepukana na zogo hilo ni kuteremka kwenye daladala.

    “Konda shusha hapo!”

    “Unashuka umefika kweli? Au ndiyo umevurugwa?” yule mzee akizidi kuniandamana, abiria wote wakawa wanacheka hawana mbavu. Daladala ilipopunguza mwendo kwa sababu ya foleni, nilienda kushuka kwa nguvu, konda wala hakunidai nauli, naye akawa anacheka sana.

    “Mnapenda kuuza mechi mkiambiwa kupima mnakuwa wakali! Kapime mdogo wangu, ngoma kitu gani kwani,” alisema kondakta nikiwa nimeshateremka, nikasikia gumzo kubwa likiibuka mle ndani ya daladala, kila mtu akisema lake.

    Hata sikuwa najua pale niliposhukia ni wapi, niliiona siku hiyo kuwa ya mkosi mkubwa kwangu!

    Nyumbani baba mdogo anatishia kwamba akimgundua anayemlia mali zake atamuoa kisha kumchinja, Jack ananing’ang’aniza nikapime virusi vya Ukimwi, abiria ambao hata hawanifahamu nao wananishikia bango nikapime! Ama kwa hakika ilikuwa siku mbaya sana kwangu.

    “Broo eti hapa ni wapi?”

    “Bamaga!”

    “Hapa nikitaka kwenda Kinondoni napanda magari ya wapi?”

    “Panda yanayoenda Makumbusho, ukifika pale kituoni ndiyo kuna magari! Vipi mbona jasho linakutoka sana?”

    “Aah! Kawaida tu,” nilimjibu kijana mmoja aliyekuwa anauza maji pale kituoni, nikawa naelekea kwenye sehemu ya kuvuka barabara ili nikapande magari ya Makumbusho kama alivyoniambia! Kichwa kilikuwa kimechanganyikiwa kabisa.

    Ni hapo ndipo nilipomkumbuka yule mama niliyekutana naye kwenye daladala wakati nikimfuata Jack, nikaona anaweza kuwa msaada mzuri kwangu kwa muda huo kwani nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa.

    “Haloo mama!”

    “Haloo mwanangu! Umefika Mori?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimefika mama na sasa narudi! Nilikuwa nataka kuonana na wewe, ulisema nitakupataje?”

    “Hapo ulipo kuna dereva yeyote wa bodaboda?”

    “Ndiyo!”

    “Hebu mpe simu niongee naye!” aliniambia, nikamsogelea dereva mmoja wa bodaboda ambaye baada ya salamu, nilimpa simu, akawa anaongea na yule mama.





    Baada ya muda, alinirudishia simu yake na kuniambia kwamba wameshaelewana. Akanipa ishara kwamba nipande na safari ikaanza nikiwa sielewi ni wapi tunapoelekea. Tulienda mpaka Mikocheni, dereva akawa anakata mitaa tu na muda mfupi baadaye, alipunguza mwendo na kusimama.

    “Mpigie mwambie tumeshafika,” alisema, nikatoa simu huku nikishangaa huku na kule, mandhari ya eneo hilo yalinifanya nishikwe na ushamba. Nyumba zote zilikuwa za maana kwelikweli, zikiwa na mageti makubwa! Mtaa wote ulikuwa kimya kabisa.

    “Nimefika mama!”

    “Haya ngoja nakuja, usimlipe huyo bodaboda tumeshaelewana,” alisema kisha nikakata simu. Muda mfupi baadaye, geti moja lilifunguliwa, nikamuona yule mama akitoka, safari hii akiwa amebadilisha nguo na kuvaa kinyumbaninyumbani, mkononi akiwa ameshika noti ya shilingi elfu kumi.

    Alikuja mpaka pale tuliposimama, tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake, akampa dereva bodaboda ile hela kisha akanipa ishara kwamba nipokee chenji kutoka kwa yule bodaboda.

    “Haya ahsante kijana, hebu mpe namba yako ya simu ili baadaye akupigie,” alisema, basi yule dereva wa bodaboda akanitajia namba yake, nikawa nahangaika kusevu kwenye kisimu changu huku nikiwa nakifichaficha. Baada ya kumalizana naye, tuliongozana na yule mama mpaka ndani.

    Lilikuwa jumba la maana kwelikweli, mle ndani kulikuwa na bustani nzuri za maua zilizotunzwa vizuri. Kumbe wakati nampigia simu, alikuwa amekaa bustanini akiwa anasoma ‘novel’ huku mezani kukiwa na laptop ya kisasa! Ilionesha yule mama alikuwa anaishi maisha ya ‘kishua’ kwelikweli tofauti kabisa na nilivyomdhania nilipomuona kwa mara ya kwanza. Nilijiuliza kama hayo ndiyo maisha yake, kwa nini ahangaike kupanda daladala? Sikupata majibu.

    “Vipi Chande, kwema?”

    “Kwema mama, shikamoo!”

    “Si tulishasalimiana jamani? Haya marahaba, umefurahi sasa,” alisema huku akitabasamu, nikajikuta na mimi nimetabasamu.

    “Unaendeleaje?”

    “Aah! Bado mama, natembea kigumu tu lakini hata siko poa,” nilimwambia, akashusha pumzi ndefu na kusogeza kiti chake karibu yangu, akawa anaongea na mimi kwa upole akitaka nimueleze ni nini kilichokuwa kinanisibu. Kwa hali ilivyokuwa, sikuwa na ujanja zaidi ya kumueleza.

    Nilianza kwa kumueleza historia yangu tangu nilipofika jijini Dar es Salaam baada ya kuchukuliwa kijijini na baba mdogo. Nilimuleza jinsi nilivyoanza kufanya biashara ya samaki na jinsi pepo mchafu alivyonikumba kiasi cha kunifanya niwe nabadilisha wanawake hovyo, tena bila tahadhari.

    Sikumficha kitu, nilimueleza yote mpaka nilivyojikuta nikiangukia dhambini na ma’mdogo na yote yaliyokuwa yanaendelea mpaka kilichotokea asubuhi hiyo nilipoenda kuonana na Jack na kunishinikiza nikapime ‘ngoma’.

    Nilipofika hapo, alishindwa kujizuia, akacheka sana mpaka machozi yakawa yanamtoka.

    “Kwa nini unajihusisha na mambo yote hayo wakati nikikuangalia umri wako bado mdogo? Kwa nini unacheza kwenye miiba tena ukiwa huna viatu? Hujui dunia imeharibika sana siku hizi?” aliniambia huku akikaa vizuri. Akaanza kunipa darasa la nguvu, alinieleza madhara ninayoweza kuyapata kutokana na tabia yangu ya kubadilisha wanawake hovyo na mwisho akaja kwenye ‘point’ ya kupima.

    Alinipa ushauri nasaha wa nguvu, akanitaka niondoe hofu ndani ya moyo wangu na kukubali kupima kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee inayoweza kunifanya nikajua kuhusu hali yangu ya kiafya na kujua nini cha kufanya.

    “Siku hizi kuna dawa za kufubaza makali ya virusi vya Ukimwi lakini pia wapo watu ambao hata mimi nawajua wameishi miaka mingi tu wakiwa na virusi, cha msingi ni kufuata masharti, nikazidi kuchanganyikiwa.

    Kutokana na ushawishi mkubwa alioutumia, hatimaye nilijikuta nikifanya maamuzi magumu kwamba liwalo na liwe. Akaniambia ndani kwake ana vipimo vya Ukimwi ambavyo hutoa majibu kwa usahihi zaidi ndani yamuda mfupi na akanihakikishia kwamba kama nitakuwa nimeathirika, atanisaidia kwa kila kitu.

    Aliinuka na kwenda ndani, muda mfupi baadaye alitoka na kipimo, sikuwa najua kwamba siku hizi kumbe unaweza hata kupima Ukimwi nyumbani. Akanitoboa kidogo kwenye kidole na kuchukua damu, nikawa natetemeka kuliko kawaida.

    “Ukikutwa una virusi vya Ukimwi utachukua uamuzi gani?” aliniuliza, nikawa nababaika nikiwa hata sijui nini cha kumjibu, akabadilisha swali.

    “Ukijikuta huna virusi vya Ukimwi utafanyaje?”

    “Nitashukuru sana, nitamshukuru Mungu na kamwe sitarudia tena makosa. Nitatulia na kusubiri mpaka muda wa kuoa ufike, na ukifika nitahakikisha naenda kumpima huyo mchumba wangu, nimekoma,” nilisema huku bado nikiwa natetemeka, akachukua kile kipimo alichokuwa amekiweka mezani kikiendelea kusoma majibu.

    “Habari njema ni kwamba huna maambukizi ya virusi vya Ukimwi ila kwa uhakika inabidi tuje turudie tena baada ya miezi mitatu,” alisema, furaha niliyokuwa nayo nilijikuta nikimrukia mwilini na kumkumbatia kwa nguvu, na yeye akanikumbatia.

    “Unaonaje kama ukihamia na kuja kukaa hapa? Nina hakika nitakudhibiti na utakuwa umeondokana na hatari kubwa ya kuja kufumaniwa na mama’ako mdogo.”

    “Nashukuru mama! Nipo tayari hata kuwa nakutunzia bustani zako na kufanya usafi, kwani hapa unaishi na nani?”

    “Naishi mwenyewe na dada wa kazi! Wanangu wanasoma nje ya nchi.”

    “Na mzee je?”

    “Mzee gani tena! Mume wangu alifariki miaka mingi tu iliyopita! Naishi mwenyewe na nimeshazoea,” aliniambia, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama. Kiukweli nilimshukuru sana na sikutaka kupoteza muda, tulikubaliana kwamba nirudi nyumbani na kwenda kuaga, nitumie njia yoyote ilimradi niondoke kwa usalama.

    Kweli nilifanya hivyo, nilirudi nyumbani ambako nilimdanganya baba mdogo kwamba nataka kwenda kusalimia kijijini mara moja kisha nitarejea. Mama mdogo alikuwa mgumu sana kukubaliana na suala hilo lakini niliposhikilia msimamo, alikubali.

    Nikaenda kuyaanza maisha mapya ya Mikocheni, huku nikibadilisha namba ya simu, nikapewa simu mpya nzuri ambayo ndiyo niliyoweka laini yangu mpya na nikaanza ukurasa mpya wa maisha yangu.

    Baada ya miezi kama mitatu hivi kupita, nilikuja kumtafuta tena Jack na kumweleza kwamba nipo tayari kwenda kupima lakini aliniambia kwamba tayari alishapata mwanaume mwingine ambaye walienda kupima na sasa hivi wapo kwenye mipango ya ndoa, japo niliumia moyoni lakini niliamua kuyaacha mambo yasonge mbele.

    Nikamtakia kila la heri kwenye maisha yake na tukaendelea kuwa marafiki wa kawaida. Mwishoni mwa mwaka, watoto wa yule mama walirejea kutoka nchini Uingereza walikokuwa wanasoma, nao wakafurahi sana kunikuta pale kwao, nikiwa namsaidia mama yao majukumu ya hapa na pale.

    Siku zilizidi kusonga mbele, baadaye nikajikuta katika penzi na mtoto wa yule mama aliyekuwa anaitwa Trixie, tukapendana sana na mama yake akaona hakuna tatizo kwa sisi kuwa wapenzi lakini hakutaka tugusane kabisa mpaka tutakapofunga ndoa na kuwa mume na mke.

    Kwa kuwa Trixie hakuwa amemaliza masomo, shule zilipofunguliwa, alisafiri na wenzake kwenda kumalizia masomo, tukawa tunaendelea kuwasiliana kwa karibu, huku nyuma yule mama sasa akawa ananichukulia kama mkwewe ambapo aliniambia natakiwa kurudi shule ili angalau na mimi niwe na msingi imara kwenye maisha yangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilipelekwa VETA ambako nilianza masomo ya ujenzi wa minara ya simu, nikaelekeza nguvu zangu zote huko na taratibu maisha yangu yakaanza kubadilika. Mwaka mmoja baadaye, mimi na Trixie tulifunga ndoa baada ya kuwa tumepima afya zetu na hatimaye tukawa mke na mume.

    Namshukuru Mungu kwamba mpaka sasa maisha yanaendelea vizuri, mimi ni fundi wa minara ya simu, Trixie anafanya kazi benki na tayari tuna mtoto mmoja, makazi yetu yakiwa ni Mbezi Beach.





    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog