Search This Blog

Wednesday, November 2, 2022

KIVURUGE WA TANDALE - 5

 





    Chombezo : Kivuruge Wa Tandale

    Sehemu Ya Tano (5)









    Hata hivyo, jambo lisilo la kawaida lilitokea. Mkuu wa kaya hakutaka kabisa kuonesha ushirikiano, hata sijui alikuwa amekumbwa na balaa gani kwani muda wote alinywea na licha ya jitihada zilizofanywa na Ruqaiya za kumrudisha mchezoni, aligoma kabisa.

    “Una nini wewe?”

    “Hata sijui, mimi mwenyewe nashangaa.”

    “Siyo kawaida yako, au huwa unatokewa na hali kama hii?”

    “Hapana! Mimi mwenyewe najishangaa.”

    “Ulikuwa na mwanamke humu ndani si ndiyo?”

    “Mimi?”

    “Ndiyo wewe kwani naongea na nani?”

    “Hapana Ruqaiya, siyo kweli! Unanihisi vibaya tu jamani.”

    “Sasa kwa nini imekuwa hivi? Unafikiri itakuwaje wakati hali yangu ndiyo kama unavyoiona na nimehangaika kutwa nzima ya leo kukutafuta ili uutibu moyo wangu, kwa nini lakini unanifanyia hivi,” alisema Ruqaiya huku machozi yakianza kumlengalenga.

    “Ukinilaumu unakosea Ruqaiya!”

    “Nakosea? Nakosea nini? Kama hukuwa na mwanamke aliyemaliza kila kitu humu ndani kwa nini imekuwa hivi?” Ruqaiya alicharuka. Tangu nimfahamu sijawahi kusikia akizungumza kwa sauti ya ukali kiasi hiki, nikawa na kazi ya kumbembeleza.

    Licha ya kujitahidi kumbembeleza kwa muda mrefu hakutaka kusikia la muadhini wala la mchota maji, alikuwa akilia kama mtu aliyepokea taarifa za msiba huku mkono wake mmoja ukiwa kwenye chungu cha asali!

    Nilijisikia vibaya sana kwa kushindwa kufanya kile kilichomfanya awali akanipenda na kuniheshimu kiasi cha kufikia hatua ya kuacha kila kitu chake na kufunga safari kunifuata.

    Mara nilipata wazo la kutoka kwenda kwa Mangi ‘kubusti’, nikajishangaa kwa nini sikupata wazo hilo haraka?

    “Nisubiri naenda dukani mara moja,” nilimwambia lakini hakunijibu chochote, harakaharaka nikavaa na kutoka, ili kuzuia Khazija asije akaingia na kuharibu mambo, nilifunga mlango kwa nje na funguo, nikanyata kimyakimya na wakati nikimalizikia kutoka getini, nilisikia ‘msonyo’ mkali kutokea ndani, bila hata kuuliza niligundua kwamba ni mama mwenye nyumba.

    Tabia aliyokuwa ameamua kuianzisha mama mwenye nyumba, ya kunitolea misonyo kila anaponiona na mwanamke, ilinifanya nijisikie vibaya sana ndani ya moyo wangu. Ni kweli nilikuwa nimeangukia naye dhambini mara kadhaa lakini ukweli ambao hata yeye alikuwa anaujua ni kwamba sikuwa nampenda.

    Ilitokea tu kwamba tumeangukia dhambini lakini si kweli kwamba nilikuwa na mapenzi naye, na hata kama alikiri kwamba nimemfanya ajisikie tofauti kabisa katika uwanja wa huba, hicho hakikuwa kigezo cha yeye kuanza kuingilia maisha yangu na kuniamulia nini cha kufanya.

    “Mbona yeye analala na mume wake lakini mimi simsemeshi chochote?” nilijisemea wakati nikiongeza mwendo kuelekea dukani kwa Mangi.

    “Mbona siku hizi unabusti sana babaake? Zina madhara hizo, siku nyingine utakuwa huwezi kabisa,” Mangu muuza duka aliniambia wakati akiniohudumia lakini sikumjali. Najua utakuwa na hamu kubwa ya kutaka kujua nilikuwa nabusti vipi, potezea nitakueleza siku nyingine.

    Nilijibusti harakaharaka, nikanunua na ‘big g’ na kuchangamsha mdomo, harakaharaka nilimlipa na kuondoka kurudi kwangu, huku mkononi nikiwa nimenunua vocha na juisi ili hata akiniuliza nilifuata nini niwe na majibu.

    Nilifanikiwa kuingia ndani kimyakimya bila mtu yeyote kushtukia, nikaufunga mlango kwa ndani huku nikijitahidi sana kuvuta pumzi ndefu na kuzitoa ili kutuliza akili maana kama akili haijatulia hata ukijibusti ni kazi bure.

    “Nimekuletea juisi.”

    “Aliyekwambia nimefuata juisi kwako ni nani?”

    “Jamani Ruqaiya mbona unakuwa mkali kiasi hicho?”

    “Hiki ni nini?” alisema Ruqaiya huku akinionesha kitu ambacho kilinshtua mno moyo wangu.

    “Umeipata wapi kwani?”

    “Nijibu swali langu,” alisema huku safari hii akiinuka na kukaa kitako pale kitandani. Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio nikiwa hata sijui nitamjibu nini. Kumbe mara ya mwisho Khazija alipoingia mle ndani tukavurugana kisawasawa, aliacha ‘kufuli’ lake pale chini bila mimi kujua.

    “Aah, unajua jana nilifua nguo, sasa wakati wa kuanua nilichelewa nikaanua usiku na hapa kuna mabinti wana kawaida ya kuanika nguo zao hadharani, inawezekana nilijichanganya lakini nakuhakikishia hakuna mtu aliyeingia humu ndani,” kidume nilimwaga uongo wenye kasi ya 4G, hata sijui nilipata wapi akili hiyo lakini huwezi kuamini, Ruqaiya aliniamini kabisa.

    “Kwani hawajafundwa mpaka waanike nguo za siri hadharani, wasichana wengine sijui wakoje! Kaitupe nje,” alisema huku akiisukumia pembeni na mguu wake, nikaona hapohapo ndiyo muda wa kujaribu tena bahati yangu.

    Nilifanya kama kumshtua kidogo hivi kwenye mbavu zake, basi akaruka mzimamzima utafikiri amekanyaga moto na kutoa kasauti fulani hivi ‘amaizing’, nikajikuta nimesisima mno.

    “Unanitesa bure wakati unajua huwezi kuninanii!”

    “Kufanyeje?” nilimuuliza huku nikiisogeza sura yangu karibu na yake. Mkono mmoja nikalishika shavu lake la kushoto na kumsogeza karibu, nikambusu, naye akafanya hivyohivyo, nikafanya hivyo tena huku roho yangu ikipata burudani ya aina yake kutokana na jinsi alivyokuwa mzuri, muda mfupi baadaye tukagusanisha ndimi zetu na kuanza kuelea kwenye ulimwengu wa tofauti kabisa.

    Hatua zile zilifanikisha azma yangu kwani gari liliwaka ‘fasta’, alipopeleka mkono na kukutana na kitu kigumu, nilimuona akinitazama kwa kushtuka kisha akawa anayarembua macho yake huku tabasamu fulani hivi la aina yake likiupamba uso wake na kumfanya azidi kuwa mrembo.

    Hakuwa na muda wa kusubiri, alijiweka katika mkao wa kula, akanivuta mzima mzima na kumuelekeza ‘mkuu wa kaya’ kwenye sehemu anayotakiwa kuwepo kwa wakati huo. Kwa jinsi alivyokuwa amenibana, ungeweza kudhani tuna ugomvi au anahisi naweza kuchoropoka na kukimbia, moyoni nikawa najiambia kwamba ‘utaomba po mwenyewe’.

    Basi mtanange wa kukata na mundu uliendelea, utafikiri mechi ya fainali ya UEFA kati ya Ral Madrid na Liverpool ilivyokuwa kali, ikawa ni piga nikupige! Niliamua kufanya kweli kwa sababu lawama alizokuwa amenitolea zilikuwa kali sana, kazi yangu ikawa ni kufuta makosa.

    Nilimvuruga kwelikweli, ikafika mahali akaniachia mwenyewe huku akitoa kiguno ya hapa napale ambayo ilizidi kunihamasisha, nikaendelea kuonesha umahiri wa kucheza na mpira, mara nipige danadana, mara nimpige tobo, mara nimpige darizi, basi ilikuwa burudani kwelikweli.

    “Kwani tuna ugomvi baba?”

    “Hapana mama!”

    “Mbona kama unanikomoa sasa?”

    “Mimi? Mbona unanisingizia mama?” nilisema huku nikitabasamu, nikaendelea kufanya mambo na muda mfupi baadaye, Ruqaiya alijifunga bao moja matata sana, bila kutegemea akajikuta akishangilia kwa sauti ya juu ambayo bila hata kuuliza nilijua lazima itafika kwa Khazija.

    Sikujali sana, nikawa naendelea kulisakata kabumbu huku nikilishambulia sana lango lake na muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa nimewamaliza mabeki wake wote, nikabaki mimi na golikipa tu, wakati najiandaa kupiga shuti kali, mara nilisikia mlango ukigongwa.

    “Ngo! Ngo! Ngo!”





    Akili ilihama kutoka mchezoni na kwenda mlangoni, nikawa najiuliza ni nani anayeweza kuwa anagonga kwa muda huo? Hata hivyo, huwezi kuamini nilipuuzia na kurudisha akili mchezoni, nikapiga shuti kwa nguvu na mpira ukaenda moja kwa moja nyavuni.

    Ruqaiya alinikamata kwa nguvu sana huku macho yake akiwa ameyafumba kisha taratibu akaanza kuniachia, nikadondokea upande wa pili huku miguu ikitetemeka utafikiri nimetoka kufanyishwa mazoezi makali ya kutingisha misuli gym.

    Bado mlango uliendelea kugongwa lakini sikujali, nikawa nimejilaza huku nikipumua utafikiri nimetoka kukimbia mbio za marathon, kijasho chembamba kikinitoka.

    “Mume wangu!” Ruqaiya aliniita kwa sauti ya chini. Kwa jinsi alivyoniita kimahaba, nilijikuta nikisisimka sana, nikamsogelea na kumtazama machoni, naye akawa ananitazama kwa macho yake ya kurembua.

    “Nani tena huyo anagonga mlango?”

    “Watakuwa ni hao watoto wa mwenye nyumba, achana naye mke wangu,” nilisema na kumbusu kwenye paji la uso, akanikumbatia tena kisha tukagusanisha ndimi zetu.

    “Yaani ningekuwa sijaolewa, lazima wewe ndiyo ungekuwa mume wangu, unanifanya nijisikie kama mwanamke niliyekamilika, ahsante sana baba,” aliniambia kwa sauti ya kunong’ona iliyopenya kwenye masikio yangu na kunifanya nijihisi kama nipo kwenye ulimwengu wa tofauti kabisa.

    Unajua miongoni mwa ‘maradhi’ waliyonayo wanaume wengi, ni kupenda kusifiwa baada ya kumaliza kulisakata kabumbu. Na baadhi ya wanawake nao ni kama wameshajua huu udhaifu, akitaka kukuchuna hata kama umecheza chini ya kiwango atakupamba kwa sifa kedekede ilimradi apate anachokitaka.

    Hata hivyo, mimi nilikuwa najua kwamba Ruqaiya anachokisema kinatoka ndani ya moyo wake kwa sababu ni kweli nilikuwa nimemuweza na ukitaka kujua kama kweli umemuweza mwenzi wako, zipo dalili za waziwazi ambazo huwa hazijifichi anapofika pale anapopataka muwapo faragha.

    Unajua kukua kwa sayansi na teknolojia, kumewafanya wanawake kujifunza uongo mwingi sana wawapo faragha na wanaume wao. Kuna wakati mwingine anaweza kukuektia kama ameiona theluji ya Mlima Kilimanjaro kumbe hakuna chochote, anataka kukufariji tu lakini moyoni anakudharau kwa jinsi ulivyoshindwa kuonesha ukakamavu wa kumtoa chozi la utamu.

    “Unasema kweli mke wangu?”

    “Kweli baba, unajua nilishakwambia kuanzia mwanzo mimi kuwa na wewe siyo kwamba nina tabia ya kutokatoka hovyo na wanaume, mume wangu ananipa kila kitu ninachokihitaji, wewe ni shahidi kwamba sina shida ndogondogo lakini kuna kitu kikubwa sana nakikosa kwa mume wangu,” aliniambia kwa sauti ya chini.

    Akanibusu tena na kuendelea kunieleza kile alichonieleza siku chache zilizopita kwamba mumewe alikuwa na tatizo la kushindwa kumfanya afike mwisho wa safari yake wawapo faragha, jambo ambalo limemtesa kwa kipindi kirefu mpaka alipokutana na mimi.

    “Ilifika mahali nikawa nachukia hata kukutana naye maana najua tu kwamba hata ajitahidi vipi, ataniacha mwenzake kwenye hali mbaya, lakini siyo wewe,” alisema huku akinipigapiga kifuani, nikafurahi sana.

    “Lakini nakuomba sana, huo ‘ukivuruge’ wako hebu achana nao, nitakupa kila utakachokihitaji. Unajua mimi ni mwanamke mwenye heshima zangu sasa kushea mapenzi na visichana viruka njia ni jambo ambalo siwezi kabisa kulivumilia, naomba unielewe sana kwenye hili suala,” alisema Ruqaiya, nikajifanya mtiifu sana na kuitikia kila alichokuwa ananiambia.

    “Najua lazima utakuwa na visichana vyako ulivyotoka navyo huko nyuma, nakupa muda wa kuweka mambo yako sawa, ukiwa mwaminifu kwangu utafaidi sana lakini usiponiheshimu basi...” alisema Ruqaiya huku akionesha kumaanisha kwelikweli kile alichokisema.

    “Usijali mama, mbona nimeshabadilika sana, unajua tangu nilipokutana na wewe, umenibadilisha kwa vitu vingi sana, inawezekana wewe mwenyewe hujui lakini huo ndiyo ukweli,” nilizidi kumpiga fiksi.

    Yule mtu aliyekuwa akigonga mlango hakuendelea tena kugonga lakini kwa ugongaji ule, nilijua lazima atakuwa ni Khazija, kichwani nikawa napanga mistari ya namna ya kumdanganya.

    Unajua watu wengi hawajui lakini ukweli ni kwamba mwanaume au mwanamke msaliti, hawezi kuwa na amani ndani ya moyo wake hata kidogo. Yaani muda wote anakuwa anafikiria jinsi ya kudanganya ili kuweka mambo sawa au kufikiria nini kitatokea endapo usaliti wake utagundulika.

    Ndiyo maana mtu msaliti, kila anapokaa anakuwa mtu wa machale tu, hataki kukaa mbali na simu yake na hata akiiacha mbali, basi ujue imewekwa password kila sehemu na imetolewa mlio na kugeuziwa chini ili hata mtu akipiga asijue mtu yeyote.

    Ukiona uko na mwenzi wako lakini simu ameweka silence halafu ameigeuzia kioo chini, na muda wote anaitazamatazama jua kuna namna hapo, hiyo ni tabia ya watu wasio waaminifu.

    “Mbona kama unawaza, unafikiria nini?” Ruqaiya alinizindua kutoa kwenye lindi la mawazo, nikajifanya kujichekeshachekesha pale lakini ukweli ni kwamba nilikuwa naifikiria sana kauli aliyoitoa Khazija kwa sababu naye alinitishia kwamba eti kama sitabadilika kitabia na kutulia, ataenda kuniroga ili jogoo wangu asiwe anapanda mtungi ninapofikiria kumsaliti.

    “Potelea mbali,” nilijiambia ndani ya moyo wangu kwa sababu ni kweli Khazija alikuwa ananipatia sana tuwapo faragha lakini kuwa na watu kama Ruqaiya kwenye maisha yangu, lilikuwa ni jambo muhimu sana.

    “Nakuahidi nitakuwa mwaminifu sana kwako na nitajitahidi kutunza siri ili nisikuharibie ndoa yako,” nilimwambia, basi akafurahi sana na kunikumbatia huku akinimwagia mvua ya mabusu.

    Haukupita muda tukarudi tena uwanjani, safari hii aliniomba niende naye ‘mdogo-mdogo’ kwani hakuwa amezoea ‘masebene’ kama yule msanii wa Bongo Fleva aliyewahi kuimba ‘sijazoea masebene miee’, hata sijui jina lake anaitwa nani.

    Wakati tukiendelea kulisakata kabumbu katika kipindi cha pili, kuna wakati mwenzangu uzalendo ulikuwa ukimshinda na kumfanya atoe miguno ya hapa na pale ambayo ilipaa na kutoka mpaka nje.

    Nikaanza kusikia misonyo ya mama mwenye nyumba ikiambatana na vicheko vya kebehi, mimi nikawa sijali, nikajifanya kama sisikii chochote. Mtanange wa nguvu uliendelea na baadaye, Ruqaiya alizifumania nyavu na muda mfupi na mimi nikazifumania, ikawa ngoma droo.

    Kutokana na uchovu niliokuwa nao, nilijikuta nikipitiwa na usingizi mzito, Ruqaiya naye akalala fofofo. Nilipokuja kuzinduka baadaye, tayari ilikuwa ni usiku, nikamuamsha Ruqaiya ambaye alipogundua kwamba tayari ni usiku alishtuka kuliko kawaida.

    “Nisindikize.”

    “Si ukaoge kwanza?”

    “Hapana, nimechelewa sana, daah! Kwa nini umeniacha nimelala hivi?” Ruqaiya alianza kunilaumu, ikabidi nimtulize kwanza mpaka alipotulia. Sikuona kama ni busara kwa yeye kuondoka vilevile alivyokuwa, kwa bahati nzuri alikubaliana na mimi kwenda kuoga.

    Nilitembea kwa kunyata mpaka mlangoni, nikafunua pazia na kuchungulia nje kupitia kitundu cha funguo na nilipojiridhisha kwamba hakuna mtu yeyote pale nje, nilifungua mlango taratibu sana.

    Nikaenda kumchukua Ruqaiya na kwa sababu zangu maalum, niliamua tuongozane mpaka bafuni. Yeye aliamini kwamba mahaba mazito ndiyo yanayonisukuma kufanya hivyo kumbe mimi nilikuwa na sababu zangu nyuma ya pazia. Basi tulioga pamoja huku nikiendelea ‘kumuektia’, akaniambia mume wake hajawahi kwenda naye bafuni kuoga hata mara moja.

    Tulirudi ndani na ile tunaingia tu, nilisikia mlango wa chumba cha Khazija ukifunguliwa, mapigo ya moyo yakanilipuka na kuanza kudunda kwa nguvu, nikawa sijui nini kitakachotokea.



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ni kama Khazija alikuwa anajua kila kinachoendelea na sasa alitaka kupata ushahidi tu maana alipofungua mlango wake, wala hakujishughulisha kuja kwangu kama nilivyokuwa nimefikiria bali alitoka na kukaa mlangoni huku macho yote yakiwa kule kwenye mlango wangu.

    “Aah, potelea mbali, liwalo na liwe!” nilisema huku na mimi nikianza kujiandaa kwa ajili ya kumsindikiza Ruqaiya. Baada ya kumaliza kujiandaa, na yeye akiwa ameshamaliza kujiandaa, nilimtanguliza yeye nje.

    Bila hata kujua kwamba nje kulikuwa na hali ya hatari, Ruqaiya alimsalimu Khazija, naye akaitikia kwa uchangamfu kama hakuna kilichotokea. Na mimi nilitoka na kufunga mlango kwa funguo kisha tukawa tunatoka na Ruqaiya.

    Kumbe si Ruqaiya tu aliyekuwa ametoka nje, hata mama mwenye nyumba naye alikuwa ametoka nje na baada ya kuhisi kama sijamuona, alijikoholesha kwa makusudi na kuanza kuimba nyimbo za taarabu zenye mafumbo.

    “Huku kwenu Uswahilini kwelikweli, naona hata watu wanaoishi huku wote akili zao zinafanana,” alisema Ruqaiya wakati tukitoka, nikamuuliza kwa nini?

    “Wewe si umeona yule sijui ndiyo mama mwenye nyumba wako anavyoimba taarabu kwa mafumbo? Hajui kama mafumbo na ‘mastashtiti’ hapa yamelala? Halafu kile kisichana nacho kwa nini kimekaa pale nje kwa makusudi?”

    “Inabidi uyazoee tu mazingira ya huku mama, hakuna namna.”

    “Akuu, mi siwezi kuzoea Uswahili wa kiasi hiki! Kwanza unaonaje nikikutafutia nyumba sehemu nyingine tofauti na Tandale? Mi nataka mahali ambapo nitakuwa huru,” alisema Ruqaiya, nikacheka sana.

    Nilicheka kwa jinsi alivyokuwa amelichukulia suala hilo lakini kubwa nilicheka kwa furaha baada ya kuona kwamba nimefanikiwa kumtoa salama maana sasa tulikuwa tukikaribia kufika pale alipokuwa amepaki gari lake.

    “Sasa mimi naongea na wewe mambo ya maana halafu unanicheka, kwa nini?” alisema Ruqaiya huku akinikumbatia bila hata woga. Unajua mapenzi yana sifa moja kubwa ambayo inawezekana wengi hawaijui.

    Mnaweza kuwa na uhusiano wa kisiri wa mapenzi lakini yatakapokolea tu, mtajikuta mkifanya mambo ambayo kwa watu wanaoelewa, wanaweza kabisa kugundua kwamba mpo kwenye uhusiano wa kimapenzi.

    Hivyo ndivyo ilivyotokea kwa Ruqaiya kwa sababu nakumbuka siku ya kwanza hata kumgusa mkono wake tu alikuwa hataki mpaka tuwe sehemu ambayo hakuna mtu mwingine anayeweza kutuona lakini ajabu ni kwamba siku hiyo yeye ndiyo alikuwa akinikumbatia mara kwa mara.

    Yaani kama angetokea mtu anayemfahamu, halafu akamuona alivyokuwa akinifanyia, ni dhahiri taarifa zingeenda moja kwa moja kwa mumewe.

    “Huogopi kunifanya hivyo hadharani?” nilimuuliza.

    “Niogope nini?”

    “Wapambe wakimwambia mumeo je?”

    “Hata akiambiwa hana cha kufanya, kwa jinsi anavyonipenda nitamuomba msamaha na yataisha. Hata akiniacha wewe si utanioa?” alisema huku akinikumbatia tena na kunibusu, tukaishia kucheka.

    “Inabidi twende kwa yule rafiki yako Ras kumshukuru maana bila yeye sijui kama ningekupata leo.”

    “Aah! Usijali, nitaenda kumshukuru mimi, twende nikusindikize uende zako maana huku kwetu siyo salama kabisa, wanaweza kukuvua hizo dhahabu zako,” nilimwambia, akacheka sana. Tayari tulishafika pale alipokuwa amepaki gari lake, tukaingia.

    “Yaani japokuwa nimechelewa kiasi hiki lakini eti huwezi kuamini bado natamani kuendelea kukaa na wewe,” alisema Ruqaiya, wote wawili tukacheka sana na tukaishia kukumbatiana kimahaba.

    “Nakupenda sana baby! Nakuomba zingatia nilichokwambia, nataka utulie na mimi tu nitakupa chochote ukitakacho,” alisema kwa sauti ya kimahaba huku akiwa amenikumbatia, nikatingisha kichwa kama ishara ya kumkubalia, akanibusu kwenye mdomo wangu na muda mfupi baadaye, tulikuwa tumegusanisha ndimi zetu.

    Ilibidi mimi ndiyo nimhimize awahi kuondoka maana muda ulikuwa ukizidi kuyoyoma, nikafungua mlango wa gari ili nishuke.

    “Nilikuletea zawadi yako, chukua,” alisema huku akitoa bahasha kwenye ‘dash-board’ ya gari na kunikabidhi. Ilikuwa imetuna na kwa haraka sikujua ndani yake ina nini, nikamshukuru kisha nikamsaidia kumuelekeza namna ya kutoa lile gari mpaka alipoingia barabarani, akanipigia honi ya kuniaga na kuondoka zake.

    Niliingiza mkono mfukoni na kuitoa ile bahasha, sikuamini nilichokutana nacho. Ilikuwa imejaa noti mpya za shilingi elfu kumikumi, nikajikuta nikishindwa kujizuia, nikapiga kelele za kufurahia kisha nikaisokomeza mfukoni na kuanza kutembea harakaharaka kwenda kwa Ras.

    Nilitaka nikamshukuru kwa kumleta Ruqaiya kwa sababu kama asingemleta, nisingepata fedha nyingi kiasi hicho na mahaba juu.

    “Dah! Umempata wapi mwanamke mzuri kiasi kile na unamfanyiaga nini maana inaonesha anakupenda kwelikweli, mpaka alikuwa analia machozi hapa, waulize washkaji.”

    “Kweli mwanangu, amekaa sana hapa anakusikilizia mpaka akawa analia! Ukimcheki mtu mwenyewe daah! Ebwana unatembea na hirizi nini wewe?”

    “Hamna washkaji, kawaida tu,” nilisema huku nikivunga. Sikutaka kabisa kutoa siri ya kambi kwa washkaji, isitoshe hata akili yangu haikuwa imetulia kwa sababu mfukoni nilikuwa na fedha nyingi sana.

    Basi nilizugazuga pale, nikatoa shilingi elfu kumi na kumshikisha Ras bila mtu yeyote kuona kisha nikaaga na kuondoka, huku nyuma nikaacha gumzo kubwa kwa sababu kila mtu alikuwa anataka kujua nimefanya nini mpaka mwanamke mrembo kama yule anizimikie kiasi cha kumwaga machozi hadharani.

    Wakati natembea nilikuwa najiuliza maswali mengi sana ndani ya kichwa changu kwa sababu hata mimi mahaba aliyokuwa akinionesha Ruqaiya yalinifanya nikose msimamo na nishindwe kuelewa nini cha kufanya.

    Ni kweli nilikuwa nimeshaanza kumpenda Khazija lakini mahaba ya nguvu aliyonipa Ruqaiya, ukichanganya na zawadi zake, nilijikuta nikijiuliza tena kama kweli nataka kuingia kwenye uhusiano ‘siriasi’ na Khazija au la!

    “Mwana FA unaoa lini... bado niponipo kwanza! Bado niponipo mwana...” nilijikuta nikiimba huku nikipiga na mbinja. Nilikuwa najiimbia tu kwa sababu napenda sana muziki wa Bongo Fleva lakini kumbe kwa wengine, walikuwa wakinitafsiri tofauti kabisa.

    Walioniona nikipita na Ruqaiya walidhani eti naimba hivyo kama ishara ya kujisifia kwa jinsi ninavyoweza ‘kung’oa’ wanawake wazuri wakati mimi mwenyewe sina mbele wala nyuma.

    “Bado niponipo sa...” nilishindwa kumalizia kuimba baada ya kugongana uso kwa uso na Khazija. Kumbe kwa muda wote huo alikuwa amejibanza nje akinisubiri na inavyoonesha aliuwa akinifuatilia hata wakati namsindikiza Ruqaiya.

    “Yule ni nani?” aliniuliza kwa ukali huku sauti yake ikitoka kwa kutetemeka.

    “Khazija... kwa nini tusiende kuzungumzia ndani?”

    “Nataka unipe majibu hapahapa, yule ni nani?” alisema Khazija huku akipandisha sauti kiasi cha kuwashtua watu waliokuwa pale dukani kwa Mangi, nikawaona wote wakigeuka na kututazama.

    “Jamani Khazija, mambo gani tena hayo unayotaka kunifanyia mke wa...” hata sikumalizia kauli yangu, nikashtukia kofi kali likitua kwenye paji langu la uso, Khazija akanivaa mzimamzima na kunidondosha chini na katika kile ambacho sikukitegemea, nilishangaa akichomoa kisu na kukishika kwa mkono wake wa kulia huku mkono wa kushoto akiwa amenikaba, akawa anataka kukizamisha kifuani kwangu.

    “Leo nakuua, shetani wewe. Hauwezi kucheza na moyo wangu halafu nikuache,” alisema huku akitetemeka kwa jazba.





    “Sikia Khazija, nakuomba mama tukayaongee ndani.”

    “Ukaongee na mimi nini? Wewe si unajifanya kidume sana, sasa leo ndiyo utanijua,” alisema Khazija huku akiwaka kama moto wa gesi, nikajua nisipofanya jambo anaweza kweli kuniua.

    Tayari watu walishaanza kujaa, kama unavyojua tena mitaa ya uswahilini kwetu hata tukio litokee saa nane za usiku watajaa watu mpaka utashangaa walikotokea.

    Basi niliamua kutumia uanaume wangu, nikapitisha mguu kutokea mgongoni kwa Khazija na kwenda kuubana ule mkono aliokuwa ameshika kisu, kufumba na kufumbua nikamsukuma kwa kutumia ule mguu, akadondokea upande wa pili.

    Kwa kasi kubwa niliinuka na kutimua mbio kukimbilia ndani, kwa bahati nzuri geti lilikuwa wazi, nikaingia na kwenda ndani kwangu moja kwa moja, nikajifungia mlango kwa ndani. Kelele nilizoendelea kuzisikia nje zilikuwa kubwa sana, kuonesha kwamba Khazija alikuwa ananifuatilia huku wapambe wakiwa wanashangilia.

    Tangu nimfahamu Khazija sikuwahi kudhani kama anaweza kuwa na akili mbovu kiasi hicho, ni kweli nilikuwa nimemkosea lakini sasa ndiyo anishikie kisu? Ukisalitiwa basi ndiyo umuue aliyekusaliti? Nilishindwa kupata majibu, moyoni nikawa naijutia nafsi yangu kwa kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Khazija.

    Unajua kwa kipindi kirefu nilikuwa nikishangaa sana kusikia stori kwamba sijui mwanamke fulani amemuua mumewe baada ya kugundua kwamba anamsaliti, mara sijui mwanaume amekatwa nyeti na mkewe kwenye fumanizi na nyingine kama hizo. Nilikuwa naamini kwamba kwa jinsi wanawake walivyoumbwa, hawawezi kuwa na roho mbaya kiasi hicho lakini sasa yalikuwa yamenifika kooni.

    “Nakwambia toka nje kama wewe kidume kweli,” alisema Khazija huku akigongagonga mlango wangu kwa nguvu. Yaani kama isingekuwa kufunga kabisa mpaka geti la chuma kwa funguo, huenda angeniingilia mpaka ndani.

    Kwa bahati nzuri, mama mwenye nyumba alitoka na kitu cha kwanza alichokifanya, ilikuwa ni kumtaka Khazija aache kumjazia watu kwenye nyumba yake. Harakaharaka akawatoa wapambe waliokuwa wakishadadia wakitaka kujua nini kinachoenda kutokea na kufunga mlango mkubwa wa geti.

    “Wewe, unamshikia nani kisu? Kumbe tunaishi na mwendawazimu humu ndani? Mnataka kuuana hapa kwangu mniletee kesi si ndiyo? Kesho unahama,” alisema mama mwenye nyumba kwa hasira, Khazija akakitupa kile kisu na kuanza kulia kwa sauti ya juu.

    Nilijikausha ndani kama siyo mimi, akalia sana pale nje na baadaye nilimsikia akiinuka na kwenda chumbani kwake, nikawa na wasiwasi kwamba huenda baada ya kunikosa, anaweza hata kujiua.

    Sikuwahi kukutana na mwanamke mwenye hasira kali kama Khazija, moyoni niliapa kama sakata hilo litapita salama basi huo ndiyo mwanzo na mwisho wa kuwa naye karibu kwa sababu kweli siku anaweza kuja kuniua.

    “Hebu fungua mlango,” sauti ya mama mwenye nyumba ilisikika, nikashtuka maana bado nilikuwa nimekaa kwenye kochi kama sanamu. Nilifungua mlango wa ndani lakini geti sikufungua, tukawa tunatazamana na mama mwenye nyumba huku nikiwa na hofu kubwa.

    “Unaona ujinga wako unavyotaka kusababisha maafa hapa nyumbani kwangu? Hivi wewe una nini? Huwezi kabisa kutulia na mwanamke mmoja, au umerogwa mwenzetu?” aliniuliza mama mwenye nyumba, nikakosa cha kujibu zaidi ya kujiinamia chini.

    “Una bahati mume wangu amesafiri jioni hii, angekuwepo leo wote mngeenda kulala ndani, wewe na huyo changudoa wako! Na nimeshamwambia atafute nyumba ya kuishi, siyo hapa kwangu, siwezi kuishi na vichaa mimi. Na wewe...” alisema huku akinitazama usoni, nikajua tu kauli inayofuata ni kuniambia ‘uhame hapa kwangu, sikutaki’.

    “Lakini mimi sina kosa mama, yeye ndiye aliyenishikia kisu,” nilimkatisha, akanitazama kisha akameza funda la mate, akageuka huku na kule kuangalia kama hakuna mtu aliyekuwa akitutazama.

    “Fungua mlango nakuja tuongee vizuri,” alisema kwa sauti ya chini, akageuka na kuanza kutembea kwa maringo kuelekea ndani kwake.

    “Hapana mama naomba tuongee kesho, sipo vizuri kabisa kwa sasa,” nilisema, akageuka na kunitazama kwa jicho la ukali kama anayesema ‘unasemaje?’, harakaharaka nikakwepesha macho yangu, akaondoka zake kwa mbwembwe.

    Kimsingi nilikuwa nimechoka mno, ukichanganya na tukio la Khazija ndiyo nilizidi kuchanganyikiwa. Kwa jinsi ninavyomjua mama mwenye nyumba, alichokuwa anakitaka kutoka kwangu hakikuwa mazungumzo wala nini, alikuwa na hasira na mimi kwa yote niliyomfanyia na njia pekee ya kumalizia hasira zake nilikuwa najua anachokitaka.

    Nilifunga mlango vizuri na ili kuonesha kwamba sikuwa tayari kwa alichokuwa akikitaka, nilizima kabisa na taa, nikaenda kujilaza kitandani huku mawazo tele yakipita ndani ya kichwa changu.

    Japokuwa upande mmoja nilikuwa nimechoka lakini upande mwingine nilikuwa najifikiria, nitaachaje kuitumia nafasi ile ya ofa ya bure kutoka kwa mama mwenye nyumba? Nilisimama na kujaribu kujipima ubavu, nikapiga pushapu mbili tatu, nikaona bado nina nguvu.

    Nikarukaruka kidogo, nikaona viungo vinakubali. Nilichokifanya, harakaharaka nilibadili maamuzi, nilivua nguo na kujifunga taulo, nikapulizia ‘air freshner’ maana chumba chote kilikuwa kinanukia manukato ya Ruqaiya! Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea.

    Baada ya hapo nilitoka na kwenda bafuni kuoga ili kuamsha nguvu mpya, shukrani kwa Mangi kwani ‘busta’ aliyonipa bado ilikuwa ikifanya kazi mwilini. Nilitoka kwa kunyata maana nilijua mwendawazimu Khazija akisikia nafungua mlango anaweza kuja kuliamsha tena dude.

    Nilienda mpaka kwenye mlango wa Khazija na ili kuwa na uhakika wa usalama wangu, niliamua kubana komeo la geti lake la chuma kwa nje. Kwa ujanja huo, hata kama angeamka asingeweza kutoka, angalau nikawa na uhakika na usalama wangu.

    Nilienda bafuni na kujimwagia maji harakaharaka, nikiwa naendelea kuoga nilisikia mlango wa mama mwenye nyumba ukifunguliwa kisha ukafungwa, nikasikia vishindo nje, nikajua moja kwa moja anaelekea eneo la tukio.

    Nilimalizia kuoga na kutoka bafuni, nikaenda mpaka ndani kwangu, tayari alikuwa ameshajaa tele, akawa ananitazama kwa macho yaliyobeba ujumbe mzito.

    “Huu mchezo wako wa kubadilisha wanawake kama nguo, mwenyewe unaona ni ujanja sana si ndiyo?” aliniuliza swali ambalo sikulitegemea.

    “Hamna, wala mimi sipo hivyo sema unakuwa unanihisi vibaya tu,” nilianza ‘saundi’ zangu kama kawaida. Akaniuliza kwa nini nasema hivyo wakati ushahidi wa kila kitu ulikuwa wazi? Nikamwambia kwamba Ruqaiya hakuwa mpenzi wangu kama yeye au Khazija walivyohisi bali alikuwa ndugu yangu.

    “Ndugu yako ndiyo mnajifungia kutwa nzima ndani, baadaye mnatoka kwenda kuoga pamoja? Huo undugu gani?” alinibana kwa maswali, nikakosa cha kujibu, akaniuliza pia kuhusu Khazija.

    “Tumezoeana tu bwana wala hakuna chochote kinachoendelea, nashangaa yeye anaanza kuniletea wivu wa kimapenzi,” nilidanganya waziwazi, akawa ananikazia macho usoni.

    “Lakini kwa nini unanibana kwa maswali namna hiyo, kwa nini usinipe hata pole mwenzako nilitaka kuchinjwa leo?” nilisema huku nikimgusa kijanja kwenye maeneo ambayo nilikuwa najua kwamba lazima mazungumzo yatabadilika.

    Nilichokihisi ndicho kilichotokea, alikatisha mazungumzo yake na kunivaa mzimamzima, tukagusanisha ndimi na kuanza kuelea kwenye bahari ya huba. Mkono wake mmoja aliupeleka kwa ‘mkuu wa kaya’ na kuanza kuzungumza naye kwa lugha ya vitendo, hali iliyosababisha nisahau kwa muda kilichotokea kwa Khazija.

    “Unajua kwamba nakupenda ndiyo maana unanitesa kwa kubadilibadili wanawake kama nguo,” alisema kwa sauti iliyotokea kwenye matundu ya pua zake, nikawa najibu kwa kugugumia tu kama dume la njiwa, sijui alinipinduaje bwana, nikajikuta nipo kwa chini yeye juu, tunatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana.

    “Nisamehe,” nilinguruma kwa sauti ya kiume, akatabasamu bila kujibu kitu na katika hali ambayo sikuitegemea, alishika kipaza sauti kwa bashasha za hali ya juu na kuanza kughani mashairi matamu, kuonesha kwamba msamaha wangu umepita, nikawa nazidi kugugumia tu ndani kwa ndani.

    Baada ya kumaliza kughani ubeti wa kwanza, alimkamata ‘mkuu wa kaya’ na kumuelekeza sehemu ya kwenda, naye akatii bila shuruti.





    Kilichofuata baada ya hapo ilikuwa ni mwendelezo wa burudani na kiukweli mwili wangu ulikuwa umechoka mno kiasi kwamba baada ya mama mwenye nyumba kutangaza kuiona theluji ya Mlima Kilimanjaro, sikupoteza muda na mimi nikatangaza kufika mwisho na muda huohuo, nilipitiwa na usingizi mzito.

    Hata sikumbuki mama mwenye nyumba aliondoka saa ngapi lakini nilipokuja kuzinduka, tayari ilikuwa ni karibu saa nane za usiku. Bahati mbaya ni kwamba nilikuwa nimemfungia Khazija ndani kwa muda wote huo.

    Harakaharaka niliinuka kitandani, kumbe hata mlango wangu sikuwa nimeufunga, nikatoka huku macho yakiwa yamefumbuka nusu kutokana na kuzidiwa na usingizi. Sijui nini kilichokuwa kimetokea kwani nilipokaribia tu mlango wa Khazija, nilisikia akiniita kwa jina langu.

    “Naomba nifungulie mlango, sijui mshenzi gani amenifungia kwa nje,” alisema Khazija kwa sauti ya juu, nikasita kidogo kwa sababu bado mimi na yeye hatukuwa tumefikia muafaka kwenye tatizo lililokuwa limetokea mpaka akataka kunichoma kisu.

    “Najua una wasiwasi na mimi, wala siwezi kukufanya chochote, hasira zangu zimeshaisha na isitoshe nahitaji kuzungumza na wewe,” alisema Khazija kwa upole, nikashawishika kwenda kumfungulia huku moyoni nikijiambia kwamba liwalo na liwe.

    “Wewe ndiye uliyenifungia mlango, si ndiyo?”

    “Mimi? Hapana.”

    “Kama siyo wewe ulikuwa unakuja mlangoni kwangu muda huu kufanya nini?”

    “Nilitaka kuhakikisha kama upo salama,” nilimdanganya, akanitazama kwa macho yaliyojaa uchovu kisha akanisogelea mwilini, na mimi nikawa najihami kwani kwa kitendo alichonifanyia saa chache zilizopita kilinifanya niwe naye makini sana.

    “Lakini kwa nini umenifanyia uliyonifanyia mpenzi wangu? Ina maana sikuridhishi baba?”

    “Hapana siyo hivyo Khazija.”

    “Sasa kwa nini ulale na mwanamke mwingine kwenye kitanda unacholala na mimi, tena muda mfupi baada ya mimi kukupa kila ulichokuwa unakitaka mpenzi wangu?” alisema Khazija huku akinikumbatia, machozi mengi yakaanza kumtoka na kuchuruzika mpaka kwenye shingo yangu.

    Kimsingi nilimuonea huruma, na mimi nikamkumbatia, ukichanganya na kile kibaridi cha usiku ule, nilijikuta nikitamani kuendelea kumkumbatia, akawa anazidi kulia huku maneno mengi ya kunilaumu yakimtoka.

    “Lakini Khazija, mimi nimeshakwambia kwamba hakukuwa na jambo lolote baya bali wewe umehisi vibaya, nakupenda sana na mimi siyo mchoyo wa fadhila kiasi hicho, kwa nini nikutese wakati nakupenda,” kidume nilianza kumwaga sera.

    Miongoni mwa masuala ambayo nilikuwa najiamini kwamba niko fiti, ilikuwa ni kwenye suala zima la kuwadanganya wanawake. Nilimpanga kwa maneno matamu, akawa anaendelea kulia, ikafika mahali na mimi nikamgeuzia kibao.

    “Hata kama ingekuwa ni kweli nimekusaliti, ndiyo utake kunichoma kisu Khazija?”

    “Hapana, nisingeweza ila nilitaka tu kukutishia.”

    “Muongo, kunitishia kivipi wakati ulikuwa ‘serious’ kabisa unataka kuniua?”

    “Hapana, siwezi kufanya hivyo. Hata kuku tu sijawahi kuchinja, ndiyo itakuwa wewe kipenzi changu, mwanaume wa roho yangu? Siwezi! Siwezi,” alisema Khazija, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama usoni.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Unajua kwa kipindi kirefu mimi nilikuwa najifanya mjanja lakini kwa Khazija nilikuwa nimegonga mwamba. Na yeye alikuwa fundi wa kuzungumza kiasi kwamba akiamua kukupangia maneno, huwezi kupinga chochote.

    “Mimi na wewe tumeshapanga mambo mengi sana mume wangu, hayo yote unataka yavurugike kwa hiki kilichotokea? Naomba nisamehe kama nimekukosea na wewe nimekusamehe,” alisema huku akiniachia maana bado alikuwa amenikumbatia, akataka anivutie chumbani kwake.

    “Basi tutaongea vizuri kesho asubuhi kabla sijaenda kazini,” nilimwambia lakini hakutaka kunielewa kwa chochote, akanivutia ndani. Kwa kuwa nilikuwa nimepumzika kwa zile saa chache nilizolala, niliona basi isiwe kesi.

    “Basi naomba nikafunge mlango,” nilimwambia, akaniambia nisiwe na wasiwasi, anaenda kufunga yeye mwenyewe. Basi sikuwa na ujanja, ilibidi nitulie. Akaenda chumbani kwangu na kufunga vizuri milango, akarudi akiwa na funguo.

    “Mbona kitanda chako kimevurugika namna ile, ulikuwa umelala na nani?”

    “Nitalala na nani tena kama wewe mke wangu hunitaki?” nilimwambia, akanisogelea taratibu pale kitandani na kujilaza pembeni huku akijinyonganyonga umbo lake zuri kimitego, akawa ananitazama kwa macho yaliyokuwa yamebeba ujumbe mzito huku mikono yake laini ikipita taratibu kwenye mwili wangu.

    Kile kibaridi kilichonipiga pale nje wakati nazungumza naye, kilinifanya niwe na shauku ya kumsogeza mwilini mwangu, nikamuinua taratibu na kumsogeza kwenye kifua changu, tukawa tunatazamana.

    “Unajua wewe ni ‘daktari’ mzuri sana lakini tatizo lako unazingua.”

    “Nazingua nini tena jamani?”

    “Unapenda sana wanawake, yaani wewe kivuruge haswaa, na hilo jina limekukaa kisawasawa,” alisema huku akitabasamu, mkono mmoja akiwa anaupitisha taratibu kuelekea katikati ya miguu yangu.

    “Na wewe tatizo lako una hasira sana, mwanamke gani anamshikia mumewe kisu? Nitakuwa sikuoi, ohooo!” niliongeza kimasihara, akacheka sana na muda mfupi baadaye, tulikuwa tumegusanisha ndimi zetu.

    Nafsi ilikuwa inataka lakini mwili ulikuwa unakataa, nikaona ngoja nijifosi kidogo kwa sababu ili kumtuliza Khazija, ilikuwa ni lazima nifanye jambo ambalo lingemfurahisha. Kwa bahati nzuri, kwa sababu tayari nilikuwa nimepumzika vya kutosha, sikupata tabu sana kuliwasha gari, ukichanganya na mbwembwe za Khazija usiku ule, basi haikuchukua muda tukawa tayari mchezoni.

    “Nakupenda sana mume wangu, ukinisaliti tena nitakuua,” alisema Khazija wakati nikiendelea kupiga naye mbizi kwenye bahari ya huba yenye kina kirefu.

    “Ukiniua na mimi nitakuua,” nilisema huku nikiendelea na kazi, akacheka sana na kuniambia kwamba hawezi kuniua bali ananitania isipokuwa nikiendelea kumsaliti, kweli ataenda kuniroga kama alivyoniahidi tangu awali.

    Haikuwa mara ya kwanza kwa Khazija kuzungumza kauli hii kiasi cha kufanya nianze kuamini kwamba kweli anaweza na mawazo hayo kichwani mwake, hasa ukizingatia kwamba kwao Pemba, kunasifika kuwa na waganga wenye nguvu kubwa za kishirikina.

    Basi hata sijui tulilala saa ngapi, nilikuja kuzinduka alfajiri na kujikuta nikiwa kwenye kifua cha Khazija, tena akiwa amenikumbatia kisawasawa.

    Nilichokigundua ni kwamba Khazija alikuwa ananipenda sana na kamwe hakuwa tayari kunipoteza kwa namna yoyote ile kwa sababu, kwa mwanamke mwingine isingekuwa rahisi kulala tena na mimi mpaka asubuhi baada ya purukushani iliyotokea usiku uliopita.

    Yaani kama ungetuona, usingeamini kwamba ni sisi ndiyo tuliojaza watu nje ya nyumba hiyo usiku uliopita, baada ya Khazija kutaka kunichoma na kisu baada ya kunifumania.

    “Hivi nashindwa nini kutulizana na mtoto mzuri kama huyu? Kwanza kiumri huyu ndiyo rika langu, hivi nimerogwa nini?” nilijiuliza wakati nikijitoa taratibu kwenye mikono yake maana nilitaka nikaanze kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini.

    Wakati nikitaka kujitoa, alizinduka kutoka usingizini, akazidi kunikumbatia huku akinimwagia mvua ya mabusu. Hata sijui alitumia ujanja gani bwana, nikashtukia ‘mkuu wa kaya’ akikurupuka kutoka kwenye himaya yake, naye wala hakuwa na hiyana, akampa kile alichostahili na kusababisha kijasho chembamba kianze kunitoka asubuhi hiyo.

    “Usiende kazini mpenzi wangu, waambie kwamba unaumwa na leo tushinde wote,” aliniambia lakini nikamkatalia katakata. Alinielewa, akanibusu tena na kuniruhusu nikajiandae.

    Nilitoka nje huku miguu ikiwa haina nguvu kabisa kiasi cha kunifanya niwe napepesuka kama mlevi wa gongo. Awali nilidhani ni hali ya muda tu lakini huwezi kuamini, niliendelea kutetemeka miguu hata baada ya kuoga.

    “Hata iweje lazima niende kazini,” nilisema huku nikijikakamua kiume, nikafungua kabati na kutoa suruali niliyokuwa naipenda. Cha ajabu, nilipoivaa, eneo la kiunoni kulibaki na uwazi mkubwa ulionishtua.

    Ni suruali hiyo ndiyo niliyokuwa naivaa mara kwa mara na siku zote ilikuwa inanibana, iweje leo inipwelepwete? Ilibidi nijitazame vizuri, nikashtuka mno kugundua kwamba nilikuwa nimekonda sana, yaani kiuno kilipungua mno na kunifanya niwe kituko kwa ile suruali niliyokuwa nimeivaa.

    Cha ajabu zaidi ni kwamba nilikuwa nimekonda ghafla kuanzia kiunoni kushuka chini.





    Hapohapo nilianza kusikia kizunguzungu kikali, miguu ikawa inatetemeka na nikaishiwa nguvu. Nilishindwa kufanya chochote na bahati nzuri ni kwamba Khazija alikuja chumbani kwangu kwa lengo la kuniaga vizuri, akanikuta nikiwa nimelala kwenye kochi nikiwa hoi.

    “Vipi tena?”

    “Hata siele...wi!”

    “Unaumwa?”

    “Ha..pa..na ila mwili hauna nguvu,” nilisema, naye akawa ni kama amechanganyikiwa. Alitoka mbiombio na kwenda kutafuta usafiri, muda mfupi baadaye alirejea akiwa na dereva Bajaj, wakasaidiana kunibeba na kunitoa nje.

    “Duh! Mbona umekuwa mwepesi kiasi hiki mwanangu?” alisema yule dereva teksi wakati akinisaidia kuingia kwenye Bajaj, sikuwa na cha kumjibu, muda mfupi baadaye safari ya kuelekea hospitali ikaanza.

    Kwa jinsi hali niliyokuwa nayo, tulienda moja kwa moja mpaka Hospitali ya Mwananyamala ambapo tulipofika tu eneo hilo la hospitali, nilizidi kuzidiwa, nikawa natapika huku mwili ukiwa hauna nguvu kabisa. Sikuelewa tena kilichoendelea.

    Nilipokuja kupata akili zangu nilijikuta nikiwa nimelala kitandani huku dripu ikitiririka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yangu. Khazija alikuwa amekaa pembeni yangu huku akiwa amejiinamia, muda mfupi baadaye akaingia dokta na kuanza kunipimapima.

    Japokuwa nilikuwa na uwezo wa kuona kila kilichokuwa kinaendelea, sikuwa na uwezo wa kujibu chochote, nikamsikia daktari akimuuliza Khazija ana uhusiano gani na mimi.

    “Ni mume wangu!”

    “Mh! Ana wake wangapi au ni wewe peke yako?”

    “Ni mimi peke yangu, kwani vipi dokta?” aliuliza Khazija lakini hakumjibu chochote, akaendelea kunipimapima na baadaye, alitoka na kutuacha na nesi aliyekuwa amekaa pembeni akiendelea na shughuli zake.

    “Unajisikiaje mume wangu,” aliniuliza Khazija, nikatingisha kichwa kuonesha kwamba naendelea vizuri. Tayari dripu ya maji ilikuwa imeisha, nesi akaja kunibadilishia na kuniwekea nyingine ambayo nayo iliendelea kuteremka kwa kasi kuingia kwenye mishipa yangu.

    “Aliishiwa maji kabisa nesi eeh! Kwani hii ni dripu ya ngapi?”

    “Alikuwa na hali mbaya, hii dripu ya tano inakatika sasa ndiyo maana unaona anaweza hata kufumbua macho,” alisema, maneno yaliyopenya kwenye masikio yangu vizuri. Baadaye Khazija aliambiwa anatakiwa kutoka ili nipate muda wa kupumzika, kweli akatoka na kuniacha pale kitandani na muda mfupi baadaye nilipitiwa na usingizi mzito.

    “Vipi unaendeleaje?” alisema daktari baada ya kuzinduka kutoka usingizini na kumkuta akiwa ananipima.

    “Naendelea vizuri,” nilisema kwa sauti ya chini, akawa anatingisha kichwa kuonesha kwamba anaelewa nilichokuwa nakisema. Akaniuliza kama naweza kumsikia vizuri, nikamjibu kuwa namsikia vizuri.

    “Una wake wangapi?”

    “Mmoja tu!”

    “Mara ya mwisho ulishirikiana kimapenzi na wanawake wangapi?”

    “Mmoja tu,” nilisema huku nikigeuza kichwa changu pembeni kwa sababu sikufurahishwa na maswali yake, nikahisi sasa ananiingilia maisha yangu binafsi.

    “Kwa uzoefu wangu, hali uliyokuwa nayo wakati unafikishwa hapa, huwa inawapata watu wenye wapenzi wengi na wanaoshiriki sana tendo la ndoa bila kupata muda wa kupumzika,” alisema huku akinitazama usoni.

    Nilijikuta nikishikwa na aibu sana kwa sababu alichokuwa anakisema kilikuwa ni kweli kabisa.

    Kwa siku chache zilizopita, nilikuwa nimeshirikiana kimwili sana, tena na wanawake tofauti tofauti, kuanzia Madam Bella, Salma sekretari wetu, mama mwenye nyumba, Khazija na Ruqaiya, achana na wale wa zamani wasio na idadi, hali ambayo ilinifanya nikose kabisa muda wa kupumzika.

    “Jinsi kiuno chako kilivyokondeana inaonesha wazi kwamba huwa hakipati muda wa kupumzika, wewe ni kijana mwenzangu kwa hiyo lazima nikwambie ukweli, ipo siku utakuja kufia kifuani kwa kuendekeza haya mambo,” alisema daktari.

    Ninavyojua mimi madaktari huwa wanafundishwa kuwa na lugha nzuri na za kutia matumaini kwa wagonjwa wao lakini huyu alikuwa akinikandia waziwazi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mtu una mke mzuri kama huyu lakini inaonesha bado unaendekeza michepuko, tumekupima mkojo una karibu aina sita za UTI, tena sugu,” aliendelea kuninanga, akaniambia kwamba eti kiumri mimi ni kijana mdogo sana kuendekeza mambo kama hayo.

    “Na bahati yako nimekupima ngoma huna, ukiendelea na mchezo huo muda si mrefu utakanyaga miwaya, we mtu gani unashiriki ngono mpaka unakaukiwa maji?”

    “Dokta, mbona kama unakiuka miiko ya kazi yako? Kwa nini unanitolea maneno machafu kiasi hicho?”

    “Wagonjwa wengine wa kujitakia kama wewe mimi huwa nawachana tu, hata ukiniona mnoko ndiyo nimekuchana, achana na ‘hizo mambo’ babu! Ungekuwa unaumwa Malaria au ugonjwa wowote wa kawaida ningekuonea huruma lakini siyo kwa hili tatizo lako la kujitakia,” alisema na kwa bahati nzuri, daktari mwingine ambaye kimamlaka alikuwa akionesha kama ana cheo kuliko yeye, aliingia.

    Jinsi daktari huyo alivyo mnafiki, eti akabadilisha mada muda huohuo na kujifanya kama ananipa matumaini ya kupona kisha akawa ananikata jicho kama anayesema ‘ole wako unichongee’!

    Kimsingi nilimchukia daktari huyo, unajua mara zote mtu anayesema ukweli hawezi kupendwa, niliona kama anaingilia mambo yasiyomhusu lakini kwa upande fulani kuna maneno aliyoyazungumza yalijirudia ndani ya kichwa changu na kunifanya nishindwe kuamini kama ni kweli au la.

    “Na bahati yako nimekupima ngoma huna, ukiendelea na mchezo huo muda si mrefu utakanyaga miwaya, we mtu gani unashiriki ngono mpaka unakaukiwa maji?” maneno yaliyosemwa na daktari huyo bishoo ambaye alikuwa amevaa cheni shingoni yalijirudia kwenye kichwa changu.

    Nikageuka na kumtazama, naye akanitazama kwa jicho la ukali, nikashusha pumzi ndefu na kuamua kuwa mpole.

    “Kwa hiyo dokta, hebu sogea nikuulize vizuri,” nilisema kiungwana, basi akasita kidogo kisha akanisogelea huku akiwa amekunja uso wake.

    “Kwa hiyo unasema kweli kwamba umenipima ngoma sina?”

    “Demu wako ndiye aliyeniambia nikupime ngoma, na yeye amepima.”

    “Majibu yakoje?”

    “Huna, ila muda siyo mrefu utapata, we mtu gani unapenda ngono kuliko kula,” alisema na kuendelea ‘kunikazia’ kama mwanzo.

    “Vipi mke wangu?”

    “Hana, sema mwanangu demu wako kifaa kwelikweli,” alisema huku safari hii akianza kujichekesha. Nilishaelewa kwa nini anakuwa na chuki za kiasi hicho kwangu, unajua sisi wanaume, ukimuona mwenzako ana demu mkali au mke mzuri sana, basi hata kama hajakukosea kitu unaweza kujikuta tu ukianza kumchukia.

    “Ninao wengi tu, tena wote wakali, nikupe pande mmoja nini?” nilimuuliza, akacheka sana na kunitania kwamba eti ndiyo maana nilikuwa nakaukiwa maji. Basi huo ulikuwa mwanzo wa urafiki kati yangu na daktari huyo ambaye naye alionesha kuwa ni mtu wa ‘totoz’ sana.

    Hata hivyo, bado aliendelea kunisisitiza kwamba natakiwa kubadili mfumo wangu kwani nikiendelea kwa mtindo huo, kweli naweza kupata tatizo kubwa kiafya, ikiwa ni pamoja na kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

    Basi nilimuelewa kwa sababu safari hii alikuwa akizungumza nami kirafiki, kuna wakati mwingine pia alimshauri Khazija kwamba natakiwa kupata mapumziko ya kutosha siyo kila wakati nafanya tendo la ndoa tu.

    “Huwa mwenyewe ndiyo anataka, sasa nashindwa kumkatalia,” alisema na kusababisha wote tucheke, akanigeukia.





    Kiukweli moyoni nilifurahi sana kuambiwa kwamba licha ya sarakasi zote zile nilizokuwa nazifanya, sikuwa nimepata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na japokuwa mwenyewe aliniambia kwamba natakiwa kupima tena baada ya miezi mitatu ili niwe na uhakika, kwangu mimi nilishajihesabia kwamba nipo salama.

    Nilimshukuru sana Khazija kwa uamuzi alioufanya wa kunipima bila mwenyewe kujua kwa sababu kiukweli sikuwa na ujasiri wa kwenda kupima na hata siku niliyojaribu, nilijikuta nikiishia kutoka nduki kutokana na hofu.

    Basi niliendelea kupata tiba nyepesi za kurudisha nguvu mwilini kwani daktari alinieleza kwamba sikuwa naumwa isipokuwa mwili uliishiwa nguvu na maji kwa sababu ya kukosa muda wa kutosha wa kupumzika kwa sababu ya kuendekeza sanaa za kikubwa.

    Baada ya kupumzishwa vya kutosha, ikiwa ni pamoja na kutundikiwa dripu, jioni niliruhusiwa kurudi nyumbani na daktari akanipa masharti kwamba natakiwa nisishiriki tendo mpaka baada ya siku saba, akanisisitiza kwamba natakiwa kula vizuri, kupata muda wa kupumzika na kufanya mazoezi mepesi angalau mara tatu kwa wiki.

    Nilimshukuru sana, Khazija akalipa gharama za matibabu na tukatoka mpaka nje ambako tuliingia kwenye Bajaj na safari ya kurudi nyumbani ikaanza. Angalau sasa mwili wangu ulikuwa na nguvu japokuwa nilikuwa nimepungua uzito kwa kiasi kikubwa mpaka mwenyewe nikawa najishangaa.

    Tulipofika nyumbani, Khazija alinishauri nifikie kwake ili aniandalie msosi, wazo ambalo nililiona kuwa la busara. Kweli dada wa watu alijitahidi sana kunihudumia, kwanza alinipelekea maji bafuni ambako baada ya kuoga kidogo nilijisikia ahueni.

    Niliporudi ndani tayari alikuwa ameniandalia supu, baadaye kidogo akaandaa chakula kizuri na baada ya kula, hatimaye tulilala. Kwa mara ya kwanza tuliweza kulala mpaka asubuhi bila kufanya chochote kulingana na masharti ya daktari.

    Kesho yake pia sikuweza kwenda kazini kwani bado sikuwa vizuri kiafya, kwa kuwa tayari walikuwa wanajua kwamba naumwa, hakukuwa na tatizo. Kutwa nzima nilishinda ndani na Khazija akinihudumia kwa kila kitu kama mtoto mdogo.

    Siku iliyofuatia niliweza kujikongoja na kwenda kazini ingawa nililazimika kuvaa nguo kubwakubwa ili kuficha wembamba wa ghafla uliokuwa umenikumba.

    Kama tulivyokuwa tumekubaliana na Khazija usiku uliopita, nilikuwa na kibarua kigumu cha kuwaeleza wanawake wangu wote kwamba nimepata mchumba na najiandaa kuoa kwa hiyo tupunguze mazoea.

    Khazija alikuwa amenipa ‘option’ hiyo kwa sababu ilibidi niwe mkweli kwake, nikamwambia kwamba kabla ya kukutana naye nilikuwa na wanawake wengi ambao kila mmoja aliniganda kama ruba na sijui namna ya kuwaacha.

    Wa kwanza kukutana naye alikuwa ni Salma, mfanyakazi mwenzangu ambaye yeye alikuwa kitengo cha reception, aliponiona tu aliinuka kwenye kiti chake na kuja kunikumbatia kwa nguvu, akawa ananipa pole kwa kuugua.

    “Kweli umepatikana baby wangu, cheki ulivyokonda ndani ya siku mbili tu,” alisema Salma huku akitabasamu kwa bashasha, akaona kama haitoshi, anibusu mdomoni, akawa ananiambia jinsi alivyonimisi.

    Nilijitahidi sana kuukwepa ukaribu wake lakini haikuwa rahisi, akawa anaendelea kunipigisha stori za hapa na pale huku akiwa bado amening’ang’ania mwilini. Ilibidi nimtoke kijanja na kwenda ofisini kwangu. Kazi zote zilikuwa zimesimama na kubaki vilevile kama nilivyoziacha, waliosema penzi kitovu cha uzembe hawakukosea.

    Mambo ya wanawake yalikuwa yamesababisha nishindwe kabisa kufanya kazi kama ilivyokuwa awali na kwa picha ile niliyoiona, nilijua kabisa kwamba kama nitashindwa kujirekebisha, hata kazi yenyewe naweza kuipoteza.

    Moyoni nilijihisi kuwa na hatia kwa sababu sikutimiza wajibu wangu ipasavyo na kwa namna moja au nyingine, nilikuwa naiibia kampuni kwa kuwa nilikuwa nalipwa mshahara ambao sikuufanyia kazi. Kwa upande mwingine, nilimtupia lawama bosi, Madam Bella kwani naye pia alikuwa chanzo cha mimi kuzembea baada ya kuanza kuingiza masuala ya mapenzi.

    Nikiwa nawaza nianze na kazi ipi, simu ya mezani iliita, nilipopokea alikuwa ni Salma, mdada wa mapokezi, akaniambia kwamba bosi amesema niende ofisini kwake, nikajua picha limeanza upya. Nilitoka na kwenda mpaka ofisini kwa bosi, nilipoingia tu akainuka pale alipokuwa amekaa na kunikimbilia, akanikumbatia kwa nguvu huku akionesha kuguswa sana na hali yangu maana nilikuwa nimepungua ghafla.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pole sana mume wangu,” aliniambia huku akinibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu, akaniambia kama bado nahisi sijapata nguvu, kwa nini nisipumzike tu nyumbani?

    “Mh! Na kazi zangu atafanya nani bosi? Bora nijikaze tu, nimeshapona bado mwili kukaa sawa tu,” nilimwambia, akaniambia anataka nipone haraka kwani amemisi sana ‘mambo yetu’, tukacheka na kugongesheana mikono, akanikumbatia tena na kusababisha manukato mazuri aliyojipulizia yapenye kwenye pua zangu na kunipa burudani ya aina yake.

    Kitu kimoja nilichokuwa nampendea Madam Bella, alikuwa anajipenda sana, muda wote ukimuona yuko ‘smart’, ananukia vizuri hadi raha. Wakati yeye akifurahia kuniona tena, mimi nilikuwa na mtihani mkubwa wa namna ya kumfikishia ujumbe kwa sababu kiukweli alionesha kunipenda mno mpaka nikawa najisikia vibaya.

    “Nitamwambia siku nyingine,” niliwaza na angalau tabasamu lilirudi na kuwa halisi kwa sababu muda wote nilikuwa na wasiwasi mkubwa ndani ya moyo wangu kuhusu jinsi anavyoweza kupokea taarifa hizo.

    “Nataka upone haraka bwana, unajua mume wangu anakaribia kurudi kutoka Sweden alikokuwa ameenda kimasomo sasa najua akija nitakuwa nakosa uhuru wa kukufaidi,” alisema, nikashtuka sana kusikia maneno hayo.

    “Mbona unashtuka? Kwani nimeongea jambo lolote baya?” aliniuliza, nikatingisha kichwa kuonesha kwamba hakuna lolote baya aliloliongea. Akaniambia kwamba mumewe alisafiri kwenda nje ya nchi miaka minne iliyopita na walikuwa wakiwasiliana karibu kila siku japokuwa hakuwahi kurudi kutokana na kubanwa na masomo.

    “Lakini nakuhakikishia wewe ndiyo utakuwa mume wangu mkubwa, yeye mume mdogo, unamzidi kwa kila kitu maana hata shughuli unayonipa, yeye hafikii hata robo,” alisema na kunifanya nicheke.

    Moyoni nilifurahi kutokana na kauli yake hiyo kwa sababu alikuwa amenirahisishia sana kazi ingawa kwa upande mwingine nilijisikia wivu sana kugundua kwamba kumbe alikuwa na mume wake.

    “Kwani unanipenda eeh, maana naona umebadilika nilipokwambia masuala ya mume,” aliniuliza, na mimi nikapata sehemu nzuri ya kumdanganya. Nilimwambia kwamba nampenda sana na sijawahi kukutana na mwanamke kama yeye, nikawa nampamba kwa maneno matamu.

    Ukweli ni kwamba nilikuwa nataka kumuweka sawa tu ili aendelee kunibeba kazini na kunipa fedha maana alikuwa mhongaji mzuri.

    “Umeongea maneno matamu sana jamani, mpaka nahisi kusisimkwa mwenzio,” alisema huku akianza kubana miguu yake mizuri kuonesha kwamba tayari wadudu walishaanza ‘kumnyevua’.

    Ajabu ni kwamba nilipokuwa namtazama akifanya vile, na mimi nilianza kuhisi haki isiyo ya kawaida, nikashtukia tu tumegusanisha ndimi zetu huku mikono yake laini ikiperuzi na kudadisi kuelekea kwa mkuu wa kaya.

    “Nimeambiwa nisubiri mpaka baada ya siku sa..ba,” niliongea huku nikifumbafumba macho kutokana na msisimko niliokua naupata.

    “Sawa usijali, mi nataka nikuimbie tu kidogo mgonjwa,” alisema kwa sauti ya kudeka, sijakaa sawa nikashtukia amekamata ‘mic’, si akaanza kuimba bwana! Alikuwa akiimba kwa ufundi wa hali ya juu kiasi cha kunifanya nitupilie mbali masharti ya daktari, nikamsogeza mpaka kwenye sofa kubwa lililokuwa mle ndani ya ofisi yake.

    Wakati akiendelea kuimba, nilifanya utundu wa kujipindua kama mwanasarakasi, nikavamia mzimamzima kwenye chungu chake cha asali, nikatoa mfuniko na kuanza kuilamba taratibu, akawa anatoa ukelele fulani huku akiendelea kuimba, hali iliyoyaamsha mno mashetani yangu.







    Muda mfupi baadaye tayari tulikuwa kwenye ulimwengu mwingine tofauti kabisa, na japokuwa bado sikuwa na stamina za kutosha, lakini niliweza kwenda naye sawa na kweli ilionesha alikuwa amenimisi kisawasawa.

    Sikukumbuka kabisa kwamba daktari alinisisitiza kukaa wiki moja bila kushiriki kwenye sanaa hiyo ya kikubwa.

    Muda mfupi baadaye, Madam Bella alipasua madafu mawili kwa mkupuo, akanikumbatia kwa nguvu na kunipiga kabali kama wale vibaka wa kwetu Tandale, akashusha pumzi ndefu na taratibu akawa ananiachia, nikamsaidia kulala pale kwenye sofa.

    Miongoni mwa udhaifu mkubwa aliokuwa nao Madam Bella, ilikuwa akishafanikiwa kupasua dafu hata moja, lazima kausingizi kampitie bila kujali yupo wapi.

    Hicho ndicho kilichotokea na ili kumsaidia asije akathubutu kukutwa na mtu mwingine, niliyaweka vizuri ‘magwanda’ yake ikiwa ni pamoja na kumsogezea kufuli lake ili akiamka alione kwa urahisi, kisha nikatoka kimyakimya na kufunga mlango kwa nje kwa kutumia funguo, kisha funguo hizo nikazipitisha chini ya mlango kama nilivyofanya siku ya kwanza aliponiruhusu nilambe asali yake.

    Nilirudi ofisini kwangu na kukaa, nikashtukia mapigo ya moyo yakianza kuongezeka kwa kasi huku mwili ukiishiwa nguvu. Zile dalili nilizokuwa nazo siku ile nilipozidiwa na kukimbizwa hospitali, zilianza kujirudia.

    “Mungu wangu, nimefanya nini sasa,” niliwaza huku nikihofia mno kitakachotokea. Kwa bahati nzuri kwenye begi langu la laptop ambalo huwa natembea nalo kulikuwa na Glucose, nikaitoa na kuanza kuilamba harakaharaka.

    Kwa kawaida Glucose huwa na uwezo mkubwa wa kumuongezea mtu nguvu ndani ya muda mfupi. Ilinisaidia sana, nikaona niongeze na Redbull. Nilimuita Salma ambaye harakaharaka alikuja na kunisogelea mwilini. Nikamueleza kwamba sijisikii vizuri na naomba akaninunulie Redbull na maji makubwa.

    “Umepatwa na nini tena?”

    “Naona mwili unaishiwa nguvu na mapigo ya moyo yananienda mbio,”

    “Ooh, maskini pole! Inaonekana bado hujapona wewe,” alisema huku akinishika kwenye mashavu yangu kwa mikono yake laini, nikataka kutoa hela ya kwenda kununulia vitu nilivyomuagiza lakini aliniambia nisijali, atatumia hela yake.

    Basi alitoka na muda mfupi baadaye, alirejea akiwa na vitu nilivyomuagiza lakini pia alikuwa na bakuli la supu mikononi mwake, akaniandalia kila kitu vizuri. Nilimshukuru sana kwani alinionesha upendo mkubwa sana. Nilianza kwa kugonga ile supu, nikafuta bakuli lote, nikahamia kwenye maji, nikapiga karibu nusu nzima ya chupa kisha nikawa nashushia na Redbull taratibu.

    “Hapo vipi?”

    “Hapo sawa!” nilimjibu, akacheka kisha tukagongesheana mikono, tangu mara ya kwanza nilipofanikiwa ‘kuona ndani’, Salma alikuwa amebadilika sana jinsi anavyozungumza na mimi.

    Kama nilivyowahi kueleza, kabla hatujaanzana, Salma alikuwa na nyodo kwelikweli, muda wote anajifanya yupo siriasi, kila anachoongea anatanguliza jazba na hasira lakini sasa hakuwa tena na ujanja wa kunifanyia mambo hayo. Sijui kama kwa watu wengine alikuwa anaendelea kuwakazia lakini kwangu mimi alibadilika mno.

    “Hapo ukipewa mchezo unaweza kweli?”

    “Unataka kunijaribu si ndiyo? Mimi sijaribiwi!” nilisema huku nikibadilisha lafudhi na kuongea kama Wasukuma wanavyokandamiza maneno, akacheka mno na kuja kunikumbatia. Katika hali ambayo sikuitegemea, alinibusu, tena mdomoni huku akipitisha mikono yake nyuma ya shingo yangu.

    Sijui nini kilinishawishi, na mimi nikajikuta nikipeleka mikono yangu kwenye kiuno chake kama dondola, akashtuka kidogo kama aliyechomwa na mwiba huku mihemo yake ikibadilika, tukagusanisha ndimi zetu na kuanza kubadilishana ‘juisi ya miwa’ huku akijiweka vizuri na kunikalia kwenye mapaja yangu.

    “Nilikumisi mno mpenzi wangu,” aliniambia huku akinitazama kwa macho yake yaliyojaa aibu za kikekike, ambayo sasa yalikuwa yamelegea mithili ya mtu anayesikia usingizi, akanibusu tena mdomoni.

    “Nilikumisi pia kipenzi cha moyo wangu, nikiwa mbali kidogo na wewe nazidi kuumwa,” nilimwambia. Kauli yangu hiyo ilikuwa ni kama imeamsha mashetani kwani alinikumbatia tena kwa hisia zaidi, akalegeza vifungo vya blauzi yake kisha katika hali ambayo sikuitegemea kabisa, alisimama akiwa ni kama amesahau kitu.

    Alitembea harakaharaka mpaka pale mlangoni, akafunga kwa funguo kisha akarudi pale nilipokuwa nimekaa kwenye kiti, akalishusha kufuli lake na kulitoa kabisa, akalitupia pembeni, mapigo ya moyo yakanilipuka paah! Nikameza mate kama fisi aliyeona mfupa huku nikishangazwa na ujasiri wake wa kucheza na sharubu za simba.

    Yaani kama kuna mtu aliyenilogezea kwenye haya mambo, basi alikuwa ameniweza kwelikweli.

    Kuna wakati huwa naamini kwamba ile haikuwa akili yangu kwa sababu inawezekanaje nimetoka kumvuruga Madam Bella mpaka nimeishiwa nguvu, lakini muda mfupi baadaye baada ya kunywa supu na kunywa Redbull kisha Salma kujilengesha, najikuta tena nikiwa na uchu kama mtu aliyetoka jela?

    Basi Salma alinisogelea akiwa anatembea kama miss, akijinyonganyonga huku na kule, akanisogelea pale nilipokuwa nimekaa na kukaa kama vile alivyokuwa amekaa mara ya kwanza, kwenye mapaja yangu.

    ‘Mkuu wa kaya’ alikuwa amefura kwa jazba kali, akawa anahisi kama namchelewesha. Nilichokifanya, nilimuelekeza Salma kuinuka kidogo, nikamtoa nyoka pangoni, Salma akawa anachekacheka kama mtoto aliyeona Ice cream huku na yeye akijilamba midomo yake.

    Hata sijui nini kiliendelea, nilijikuta tu napiga mashuti marefu huku Salma akitoa miguno ya hapa na pale, mikono yake ikiwa imeshika vidole vya miguu yake na kunipa mgongo huku akiwa ni kama anayegoma kwenda mbele, eneo la katikati lote likiwa juu.

    Basi niliendelea kupiga mashuti kwa nguvu, naye akawa anaendelea kulalama huku akilitaja jina langu na kunisihi nisiwe na kasi uwanjani kama yule mchezaji kinda wa Ufaransa, Mbappe aliyechukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi kwenye kombe la dunia.

    Haukupita muda mrefu, nilimbabatiza na shuti la kushtukiza, akajifunga bao moja matata sana na kuanza kushangilia ushindi huku akitetemeka mwili wote wakati kiuhalisia mimi ndiye niliyetakiwa kushangilia. Alitaka kunyanyuka lakini nikamzuia, nikapiga pasi ndefu kwa namna ile ambayo wataalamu wa soka wanaita ‘counter attack’, yaani unapiga mpira juu kidogo kuelekea mbele halafu na wewe unatimua mbio kuufukuzia ukiwaacha wachezaji wa timu pinzani wanakanyagana.

    Niliwahi na bila kupoteza muda, nilifumua shuti lingine kali zaidi, likajaa moja kwa moja wavuni, kipyenga kikapulizwa kuashiria kumalizika kwa ngwe ya kwanza.

    “Halafu wewee! Yaani hapo unaumwa ndiyo umenifanyia hivi, ungekuwa mzima si ungeniua kabisa? Mgonjwa gani una miguvu kama faru aliyejeruhiwa?” alisema Salma kwa sauti iliyokuwa inatokea kwenye matundu ya pua zake, akanikumbatia na kunibusu kisha akaninong’oneza sikioni.

    “Unajua sana namna ya kuitii kiu yangu ndiyo maana nakupenda na kukuheshimu sana kivuruge wangu,” nilijikuta nacheka baada ya kauli hiyo, akawa ananiambia eti nisicheke kwa sababu anachokisema anamaanisha.

    Basi aliendelea kunishukuru huku akinimwagia misifa kibao, mara simu ya mezani ikaanza kuita mapokezi ambapo kimsingi ndipo ilipokuwa ofisi yake. Harakaharaka alikurupuka na kwenda kufungua mlango, akaenda kupokea simu hiyo huku akiliacha kufuli lake palepale alipokuwa amelitupa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kuogopa linaweza kuonwa na mtu mwingine na kuleta picha isiyofaa, nililiokota na kuliweka kwenye mfuko wa pembeni wa begi langu la laptop. Mara alirudi akiwa anatembea kwa kuyumbayumba kama mlevi, nadhani dozi aliyoipata ilikuwa imefika mahali pake.

    “Bosi amepiga simu anasema uende ofisini kwake na laptop yako,” alisema huku akinitazama kwa macho yaliyobeba ujumbe mzito ndani yake.

    Salma alishaanza kuwa ananipenda kwa dhati na hakuweza kujificha, angejua jinsi mwenzake nilivyokuwa na mambo mengi kichwani, wala asingekubali kunikabidhi moyo wake kiasi kile, kwa sababu mtu anaweza kukutazama kikawaida lakini pia anaweza kukutazama huku uso wake na macho yake vikizungumza lugha nzito kutoka ndani kabisa ya moyo, kama yeye alivyokuwa akifanya kwa wakati huo.

    “Ok poa,” nilisema huku nikiinuka na kukimbilia maliwatoni kwani nisingeweza kwenda nikiwa na hali ile, Madam Bella ni mtu mzima kwa hiyo lazima angenishtukia, tofauti na Salma ambaye alishindwa kabisa kugundua kwamba muda niliokuwa nampa haki yake, nilikuwa nimetoka pia kumvuruga Madam Bella.

    Nilijiswafi fastafasta kisha nikatoka na kurudi ofisini kwangu, yaani siku ya kufa nyani miti yote huteleza na za mwizi arobaini, waliosema misemo hii hawakukosea kabisa.

    Sijui nini kilitokea kwani nilijikuta nimesahau kabisa kwamba lile kufuli la Salma nimeliweka kwenye begi la laptop, nikainuka huku na mimi nikipepesuka kwani miguu haikuwa na nguvu kabisa, nikabeba begi langu la laptop na kuelekea kule ofisini kwa bosi.







    “Jamani ndiyo nini umenifanyia?” Madam Bella alisema baada tu ya mimi kuingia, akajizoazoa maana bado alikuwa amekaa pale kwenye sofa kichovu, akaenda kufunga mlango kwa ndani, akachomoa kabisa funguo kisha akanisogelea na kunikumbatia na kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu.

    Akalivua lile begi la laptop nililokuwa nimelivaa, akaliweka mezani na kunikumbatia kwa uhuru zaidi, tukagusanisha ndimi zetu huku na mimi mikono yangu nikiipeleka kwenye kiuno chake na kukishika kwa ustadi wa hali ya juu, akawa anajikunjakunja kama nyoka. Tulikaa kwenye hali hiyo kwa dakika kadhaa.

    “Ahsante kwa kunitoa chozi la utamu!” nilikuwa siyajui mimi mambo haya,” aliniambia huku akinitazama kwa macho yake ambayo yalikuwa yamelegea kwelikweli, nikamwambia asijali, nipo kwa ajili yake.

    “Unisamehe sana, mwenzio nikishafika kwenye ‘naniliu’ mwili unachoka sana na najikuta tu napitiwa na usingizi,” alisema huku safari hii akinitazama kwa aibu za kikekike kama mwari.

    “Halafu wewe huwa unafanyeje? Mbona mume wangu hajawahi kunifanya nijisikie hivi hata mara moja? Kabla sijaolewa pia niliwahi kuwa na wanaume wawili kwa nyakati tofauti lakini hakuna aliyenifanya nikaweza kupanda juu ya mnazi na kuangua madafu kama wewe,” alisema huku akicheka, na mimi nikacheka, tukakumbatiana tena.

    Taratibu Madam Bella alinikalisha kwenye lile sofa, moyoni nikawa najiambia asije akataka tena maana nitakufa.

    Bado nilikuwa kwenye kipindi cha uangalizi maalum kama daktari alivyoniambia na sikutakiwa kabisa kufanya hayo mambo, sema tu uroho wangu na mitego niliyokumbana nayo asubuhi hiyo kutoka kwa Madam Bella na Salma vilinifanya nipuuzie ushauri wa daktari.

    Nilichokihisi ndicho kilichotokea, Madam Bella aliponikalisha pale kwenye sofa mle ndani ya ofisi yake, nilimuona akilichomoa tena kufuli lake ambalo hata sijui alilirudisha sehemu yake muda gani, akalitupa na kwa bahati mbaya, lilidondokea pale kwenye mkoba wangu wa laptop, tena palepale nilipokuwa nimelificha lile la Salma.

    Alitoa kipaza sauti na kama kawaida yake akaanza tena kuimba na safari hii, alikuwa akiimba kwa mtindo wa tofauti kidogo, nikajikuta mawazo juu ya lile kufuli lake yakiyeyuka ghafla, sasa nikawa nasikiliza utamu wa mashairi aliyokuwa akighani.

    Tatizo langu jingine ni kwamba mkuu wangu wa kaya, huwa hana kabisa subira! Ule msemo wa subira yavuta heri yeye ulimpitia mbali kabisa kiasi kwamba nikifanyiwa uchokozi kidogo tu, yeye anafura kwa jazba kama nyoka koboko anayetaka kutema sumu.

    Kile alichokuwa akikifanya Madam Bella, kilimfanya azidi kututumka kadiri muda ulivyokuwa unaenda, nadhani na yeye alikuwa akifurahia muziki laini uliokuwa ukiimbwa na bosi wetu, Madam Bella.

    Aliendelea na alichokuwa anakifanya na muda mfupi baadaye, alifanya kama wakwezi wanaoangua nazi na madafu juu ya mnazi wanavyofanya. Mguu mmoja aliukanyaga juu ya sofa, pembeni kidogo ya kiuno changu, ule mwingine akaupitisha upande wa pili kisha akaukwea mnazi kwa pupa, akaanza kujisevia.

    Kwa jinsi alivyokuwa na papara, hakuchukua muda akawa ameshafika juu kabisa ya mnazi, akaangua madafu mawili na kuyapasua mfululizo! Kama nisingewahi kumshikilia, pengine angedondoka na kujiumiza kwani alikuwa akipaparika kama kuku aliyekatwa kichwa.

    Ilibidi pia nitumie mkono wangu kumziba mdomo wake kwani alikuwa akipiga ‘nduru’ kwa sauti ya juu, nikamshikilia mpaka alipotulia, nikamsaidia kulala vizuri pale juu ya sofa. Haukupita muda akapitiwa na usingizi mzito. Hiyo ndiyo ilikuwa ponapona yangu kwani sasa nilikuwa na nafasi ya kutatua utata juu ya yale makufuli.

    Harakaharaka nilimrudisha mkuu wa kaya kwenye himaya yake, nikasogea pale kwenye begi la laptop, nikalitoa lile kufuli la Madam Bella, yakatoka yote mawili pamoja na lile la Salma. Kwa jinsi yalivyokuwa yakifanana, nilipata wakati mgumu wa kuyatenganisha, baadaye nikapata wazo la kupima ukubwa.

    Kimwili Madam Bella alikuwa mkubwa kwa kila kitu kwa Salma, kwa hiyo ‘nikajiongeza’ kwamba lazima lile kubwa ndiyo litakuwa la kwake, nikajiridhisha pia kwa harufu ya manukato!

    Baada ya kumaliza zoezi hilo, nilijiweka sawa, nikabeba laptop na kwenda kufungua mlango. Kama nilivyofanya mwanzo, nilitoka na kufunga mlango kwa nje kisha nikaingiza funguo kupitia chini ya mlango lakini wakati nikiinama kuingiza funguo hiyo, nilisikia kitu kama kimenichoma kwenye mgongo wangu, yakafuatia maumivu makali kwelikweli ambayo hata siwezi kuyaelezea.

    Nilijikaza na kuondoka nikiwa na laptop yangu, nikaenda ofisini kwangu kimyakimya na baada ya kuweka laptop, nilienda ‘washroom’ kujiswafi kuondoa ushahidi lakini mgongo ulikuwa unaniuma kwelikweli. Nikarudi ofisini kwangu na kwenda kukaa huku nikijisikilizia maumivu.

    Muda mfupi baadaye, Salma alinifuata, akanikuta nimekaa kichovu huku nikiwa naichezea laptop yangu.

    “Vipi baby!”

    Alisema huku akija mwilini mzimamzima na kunikumbatia, akanibusu!

    “Mh! Mbona kama unanukia harufu ya pafyumu ya bosi,” aliniuliza swali ambalo sikulitegemea, nikamdanganya kwamba kuna kazi nilikuwa namuelekeza bosi kwenye laptop kwa hiyo muda muda mwingi tulikaa karibu na kugusana, akashusha pumzi ndefu akionekana kuukubali uongo wangu.

    “Umeona ulichonifanyia?” alisema huku akipandisha juu sketi yake laini aliyokuwa ameivaa, macho yangu yakatua kwenye kiota cha ndege tetere kilichokuwa na mvuto wa aina yake machoni.

    “Umeondoka na ‘naniliu’ yangu, unaona mwenzio nimebaki hivi hata kutoka nje nilikuwa naogopa,” alisema kwa aibu za kikekile huku akinisogelea vilevile, ikabidi nivunge kwani mgongo ulikuwa unaniuma kwelikweli, nikanyoosha mkono na kutoa kufuli lake kwenye begi la laptop, nikataka kumpa lakini akaniambia eti ananipa adhabu ya kulirudisha mahali pake.

    “Please Salma, mwenzio naumwa ujue, nitakufa uju...” kabla hata sijamalizia kauli yangu, tayari alikuwa ameshanivaa mwilini, akapitisha mikono yake ndani ya shati nililokua nimevaa na kushika kifua changu kwa ustadi wa hali ya juu, nikahisi kama nimepigwa na shoti ya umeme.

    “Kwa ni..ni..ni una..ni..cho..ko..za,” nilisema kwa sauti ya kugugumia, akawa ananitazama kwa uchu, mdomo wake ukajaa mate kama mtu aliyeona kipande cha ndimu.

    Alichokifanya, alinisogezea kopo langu la Redbull ambalo nilikuwa nimekunywa nusu! Akaninywesha ile iliyobaki mpaka ikaisha. Akanipokonya lile kufuli lake na kulitupa chini, nikajua kazi ipo.

    Aliilegeza ile sketi yake upande wa kiunoni, alipoiachia ilidondoka mpaka chini, nikawa namtazama utafikiri ndiyo mara yangu ya kwanza kumuona. Hata sijui alifunga mlango saa ngapi, akaja kunikumbatia kwa hisia za hali ya juu huku mapigo ya moyo wake yakienda mbio na pumzi zikimtoka bila mpangilio.

    Ni kweli nilikuwa najisikia maumivu makali ya mgongo na sarakasi nilizozifanya muda huo zilikuwa zimenimaliza kabisa nguvu lakini sikuweza kuvumilia majaribu aliyokuwa ananifanyia Salma.

    Hata kama ningesema navunga, mkuu wa kaya kama kawaida yake, kiherehere chake kilimfanya ashindwe kutulia sehemu yake, Salma naye akatumia fursa hiyo kutimiza lengo lake, akamchomoa pangoni na bila ajizi, alimuelekeza sehemu anayotakiwa kuwepo muda huo, akamsindikiza kwa mbwembwe za hali ya juu zilizonifanya niwe kama nimepandwa na mashetani.

    Unajua wasichokijua watu wengi ni kwamba japokuwa wanawake wanaweza kuonekana sawa kwa macho ya nje, ukweli ni kwamba kila mmoja yuko tofauti kabisa na mwingine. Japokuwa nilikuwa nimetoka kuliamsha dude kwa Madam Bella, Salma na yeye alikuwa tofauti kabisa.

    Cha ajabu ni kwamba hata yale maumivu ya mgongo sijui hata yaliishia wapi, ikawa ni piga nikupige katika lango la timu pinzani, yeye alileta ujuzi wake na mimi nikawa nampelekea ‘machejo’ yangu, kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele ndivyo ushirikiano kati ya akili na mwili ulivyokuwa unapungua, ikafika mahali nikawa hata sielewi niko wapi na nafanya nini.

    Ninachokumbuka ni kwamba Salma alijifunga goli la kushtukiza na mimi nikapachika lingine lililotingisha nyavu zake, kisha nikadondoka kama mzigo, giza nene likatanda kwenye upeo wa macho yangu.





    Sikuelewa tena kilichokuwa kinaendelea, baadaye nikaanza kusikia sauti kwa mbali, watu wawili walikuwa wakijadiliana, mmoja akimuuliza maswali na mwingine akijibu.

    “Huyu ni nani yako?”

    “Ni mume wangu.”

    “Mh! Mume wako?”

    “Ndiyo.”

    “Nini kimetokea?”

    “Kuanzia asubuhi alikuwa analalamika kwamba mwili unaishiwa na nguvu, ghafla tukashangaa amedondoka chini na kupoteza fahamu.”

    “Hebu tusubirini nje.”

    “Hebu mtundikieni dripu kwanza kwa sababu inaonesha ana upungufu mkubwa wa maji,” nilimsikia yule mwanaume akisema, nikaanza kuvuta picha kwamba lazima nitakuwa hospitali. Nilijaribu kufumbua macho mara kadhaa lakini nilikuwa nashindwa, kila kiungo katika mwili wangu kilikuwa ni kama kimekufa ganzi.

    Basi nilisikia kama mkono wangu ukifutwafutwa na kitu chenye ubaridi, kisha nikasikia sindano ikiingia mishipani. Nilitamani kufumbua macho lakini sikuweza kwa hiyo ikabidi nitulie tu.

    Baada ya kama dakika ishirini hivi, nilijaribu tena kufumbua macho, safari hii nilifanikiwa. Nilichokuwa nakihisi ndicho kilichotokea, kweli nilikuwa nimelazwa kwenye kitanda kilichotandikwa mashuka meupe huku dripu ikiwa inatiririka kwa kasi kuingia mishipani mwangu.

    Nilijikakamua na kugeuka pembeni, nikaona kuna vitanda vingine kibao huku kukiwa na wagonjwa, nikageuka upande mwingine nako nikaona hivyohivyo, ni kweli nilikuwa hospitali.

    “Dokta! Amezinduka,” nilisikia sauti ya nesi akimuita daktari. Kumbe kulikuwa na nesi amekaa pembeni ya kitanda changu upande wa miguuni akifuatilia kila kitu nilichokuwa nakifanya. Muda mfupi baadaye, kitanda changu kilikuwa kimezungukwa na daktari na manesi kadhaa.

    “Unajisikiaje kijana.”

    “Najisikia vizuri ila kichwa kinanigonga, hapa ni wapi na nimefikaje?”

    “Hapa ni hospitali, umeletwa baada ya kudondoka na kupoteza fahamu,” alisema daktari huku akinipimapima kwa kutumia kifaa maalum, nikashangaa anawaambia wale manesi watupishe ana jambo la kuzungumza na mimi.

    “Kijana umeoa?”

    “Hapana dokta, kwa nini?”

    “Kuna mama mmoja kati ya wanawake waliokuleta anasema yeye ni mkeo, ili nikikutazama mwili wako na umri wako naona kama hamuendani naye kabisa.”

    “Dokta, kwani kushauri mambo ya mahusiano ya kimapenzi ya wagonjwa wako nayo ni miongoni mwa kazi zako?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nilimuuliza kijeuri maana niliona anaanza kuniingia mwilini.”

    “Siyo hivyo kijana, inaonekana wewe huumwi chochote kwa sababu tumekupima vipimo vyote lakini kuna kitu mimi nataka kuzungumza na wewe kama mwanaume mwenzangu,” alisema dokta kwa sauti ya chini kidogo huku akitazama huku na kule kuhakikisha kama hakuna mtu anayetusikia.

    “Hivi huwa unafanya mapenzi mara ngapi kwa kutwa nzima na unakutana na wanawake wangapi kwa siku?”

    “Swali gani hilo dokta?” nilimjibu huku nikigeukia pembeni. Nilijua na yeye anataka kuanza kuleta za kuleta kama yule daktari wa Mwananyamala.

    “Dalili zote ulizonazo zinaonesha kwamba wewe unafanya ngono sana, hata ulipofikishwa hapa nilipokuchunguza kwa makini niligundua kwamba kuna uwezekano mkubwa ukawa umepoteza fahamu wakati wa tendo, kweli si kweli,” alisema yule daktari huku akinilazimisha nimgeukie.

    Sikumjibu kitu, akaendelea kunieleza kwamba kutokana na tabia yangu hiyo, majimaji kwenye viungio vya mifupa (joints) kama kwenye magoti, kwenye mabega, kwenye kiuno na sehemu nyingine zenye viungio yalikuwa yamekauka.

    Aliniambia pia kwamba nilikuwa na upungufu mkubwa wa maji na damu ambavyo vyote ni kwa sababu ya kuushughulisha sana mwili kwa kufanya mapenzi. Aliniambia kitaalamu, kufanya tendo la ndoa, unapopiga mshindo mmoja, nguvu inayotumika ni sawa na kutembea kwa miguu kwa kilometa kibao.

    “Hapana dokta, naona sasa unaleta stori za vijiweni,” nilimkatisha kwa sababu vijiweni huwa kuna stori nyingi za aina hiyo, mwingine anakwambia kupiga mshindo mmoja ni sawa na kutembea 3 kwa miguu, mwingine anakwambia ni sawasawa na kilometa saba na kadhalika.

    Kama ungefuata stori hizo za vijiweni, maana yake ni kwamba kwa muda wa wiki moja tu mimi ningekuwa nimeshapita Morogoro na sasa naitafuta Dodoma kwa miguu kwa sababu nilikuwa nimefanya sana, tena kwa wanawake tofautitofauti.

    “Sawa, zinaweza kuwa ni stori za vijiweni lakini hoja ya msingi unayotakiwa kuijua hapa, ni kwamba unapofanya tendo la ndoa, nguvu unayotumia kwa kila mshindo ni kubwa sana kwa hiyo unapofanya hovyohovyo siyo kwamba unaonesha uhodari wako, bali unaumaliza kabisa mwili wako.

    “Tazama ulivyokonda, kiuno kimebaki kama nyigu, hujionei huruma?”

    “Hizo sasa dharau dokta, kama unaweza kunitibu wewe nitibu lakini siyo kunisimanga kwa sababu hata kiapo cha kidaktari sidhani kama kinakufundisha kumsimanga mgonjwa.”

    “Yapo magonjwa ambayo mtu unaweza kumuonea huruma mgonjwa, lakini siyo mambo ya kishenzi kama yako, angalia dripu inavyoingia kwa kasi kwenye mwili wako, umekaukiwa kabisa maji. Unawaona hawa wagonjwa wengine, kila mmoja anaumwa sana lakini hakuna aliyejitakia kama wewe.

    “Lile limama kubwa namna ile eti linasema wewe ndiyo mume wake, si lazima litakuwa linakutumikisha kingono? Acha uboya wewe,” alisema daktari huku akiondoka, akionesha kukasirika.

    Hii ilikuwa mara ya pili sasa nakutana na suala kama hilo, mara ya kwanza ilikuwa ni kule Mwananyamala na yule daktari baada ya kunisemea mbovu, nilihisi ni kwa sababu ya wivu kwani nilikuwa na Khazija, lakini huyu naye ambaye kiumri alikuwa mkubwa kidogo, naye alikuwa akizungumza maneno yaleyale.

    Niliona sasa kuna haja kweli ya kuyafanyia kazi yale waliyoniambia kwa sababu ilionesha kabisa kwamba nikiendelea na mchezo huo, siku zangu zinahesabika. Dakika chache baadaye yule daktari alirudi tena pale kitandani kwangu, akaendelea kunichana wakati mwingine akitumia maneno ya kuudhi.

    “Wewe bado ni kijana mdogo sana, kwa nini usitafute mwanamke mnayelingana naye, ukafuata taratibu zote zinazotakiwa ili awe mkeo halali badala yake una kazi ya kuparamia watu wazima?”

    “Dokta, hebu naomba uniache tafadhali, nimekusikia.”

    “Wewe jifanye kichwa ngumu, siku nyingine ukiletwa hapa hata kama unakaribia kupoteza maisha, tutakuacha maana inaonekana wewe mwenyewe hujijali.”

    “Tusifike huko dokta, unajua mimi ni kama ndugu yako,” nilijirudi baada ya daktari kuanza kutoa maneno makali, alionesha kweli kukasirishwa na kilichotokea.

    Nilipoonesha kukubali makosa, na yeye alipunguza jazba na kuniambia madhara ya kiafya ya kufanya ngono hovyo na watu tofautitofauti, huku akinionya kwamba ukiachilia mbali mateso niliyokuwa nayapata, naweza pia kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwemo Ukimwi.

    Alinipa elimu kubwa sana ambayo siyo kwamba sikuwa naijua kwa sababu hata yule daktari wa Mwananyamala alishanieleza, moyoni nikajiapiza kwamba nitafanya kila kinachowezekana ili kuondokana na hatari iliyokuwa mbele yangu.

    Basi niliendelea kupewa matibabu pale na muda wa kuona wagonjwa ulipofika, kizaazaa kikubwa kiliibuka wodini kwani ukiachilia mbali Madam Bella ambaye ndiye aliyenileta pale hospitali, lakini pia alikuwepo Salma ambaye ndiye aliyenizimisha, alikuwepo Khazija wangu ambaye alishapewa taarifa lakini naye alikuja na mama mwenye nyumba, Ruqaiya naye sijui alipewa taarifa na nani kwani naye alikuja akiwa na mapochopocho kibao kwa ajili ya mgonjwa, sambamba na Nancy, ambaye sijui aliambiwa na nani.

    Nikawa nimezungukwa pale kitandani na wanawake zangu wote, ambao kila mmoja alikuwa ameleta chakula na kila mmoja alikuwa anataka wenzake wamtambue kwamba yeye ndiye mpenzi wangu.







    Nilichokifanya, niliamua kutengeneza bonge la ‘script’ kama wasanii wa Bongo Muvi kwa sababu nilijua muda wowote kinaweza kunuka.

    Nikajifanya kama najisikia maumivu makali sana, nikamuagiza Ruqaiya akamuite daktari, akaweka kikapu chake chini na kutoka mbiombio kuelekea kule kwenye ofisi ya nikamuagiza Khazija akaninunulie maji ya moto nje, nikamuagiza pia mama mwenye nyumba akanitafutie dawa ya kupunguza maumivu.

    Niliwachanganya wote kwa makusudi kwa sababu sikutaka waendelee kukaa pamoja nikiamini lazima kuna jambo baya litatokea na kuwa skendo pale hospitalini. Kweli dili lilitiki, wote wakasambaratika na kuniacha peke yangu pale kitandani.

    Muda mfupi baadaye, Khazija alirudi akiwa ameongozana na yule daktari aliyekuwa akinitibu, akaniinamia kwani nilikuwa naugulia kwelikweli.

    “Unajisikiaje?”

    “Dokta, wewe ni mwanaume mwenzangu, naomba unisaidie tafadhali.”

    “Dada, hebu naomba utupishe kidogo,” alisema dokta akimwambia Khazija, kweli akatii na kusogea pembeni maana nilivyokuwa nazungumza naye, nilikuwa nataka mtu mwingine yeyote asijue kinachoendelea.

    “Hawa wanawake wote ni wanawake zangu.”

    “Unasema?”

    “Ndiyo dokta, sasa hapa wanaweza kusababisha matatizo zaidi.”

    “Mkeo halali kati ya hawa ni yupi?”

    “Yule aliyekuja kukuita ndiyo mimi nina malengo naye, wale wengine si unaona kwanza wengine ni watu wazima?”

    “Unawezaje kuwa na wanawake wakubwa na wengi kiasi hiki?”

    “Dokta nisaidie.”

    “Nakusaidia nini sasa?”

    “Naomba uwazuie wasiingie tena wodini na kama wakiingia, waje mmojammoja, ikiwezekana waambie kabisa kwamba umenipima na kunikuta na Virusi vya Ukimwi,” nilisema, akashtuka na kunitazama:

    “Umechanganyikiwa nini kijana?”

    “Hapana dokta, nisaidie.”

    “Miiko ya kidaktari hairuhusu kabisa kufanya hicho unachokitaka, tafadhali tusiharibiane kazi.”

    “Dokta! Dokta,” nilisema huku machozi yakianza kunilengalenga. Alinitazama kwa huruma kwani kiukweli nilikuwa na hali mbaya, ukiachana na sekeseke hilo la wanawake hao, bado afya yangu haikuwa nzuri kabisa na nilihitaji msaada.

    “Siwezi kuwazuia kuja kukuona kwa muda huu kwa sababu ni muda wa kutazama wagonjwa, ninachoweza kukifanya ni kuzuga hapa kama naendelea kukuhudumia mpaka muda wa kuona wagonjwa utakapoisha,” alisema, nikatingisha kichwa kukubaliana naye.

    Basi alijifanya kama ananipimapima huku na kule, mara arekebishe dripu, mara anipime mapigo ya moyo, ilimradi tu aonekane yupo bize.

    Wale niliowazuga, wote tayari walikuwa wamesharejea, huyu akiwa na chupa ya maji, mwingine akiwa na vocha, na mwingine akiwa na matunda, basi na mimi nikawa nazidi kugugumia kama naumia sana.

    “Inabidi nikuhamishie wodi ya private, utaweza kulipia?”

    “Nina bima kubwa dokta, we nihamishe tu dokta,” nilimwambia. Kweli akawaita manesi na kuwaelekeza kunihamisha harakaharaka, na mimi nikawa nazidi kujilegeza ili hali yangu ionekane kuwa mbaya.

    “Samahani, nyie ni ndugu wa huyu mgonjwa?” nilimsikia yule daktari akiwauliza, wote wakajibu harakaharaka huku kila mmoja akimsogelea mwilini ili ionekane yeye ndiyo yupo karibu na mimi.

    “Kwa nini hamumsimamii mgonjwa anywe dawa zake za kurefusha maisha mnasababisha anazidiwa kama hivi?”

    “Mungu wangu?” wote walisema kwa pamoja utafikiri walioambizana, daktari akaanza kuwasema kwamba wao ni ndugu gani wasiojali afya yangu kiasi cha kushindwa kunisimamia ninywe vidonge vyangu vya ARV?

    “Dokta, kwani vidonge vya ARV si wanakunywa wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi?”

    “Ndiyo! Kwani nyie hamna taarifa kwamba huyu ndugu yenu ni mwathirika? Eti, au hukuwaambia ndugu zako?” Dokta aligeuka na kuniuliza, muda huo tayari manesi wakiwa wameshaanza kukisukuma kitanda changu kuelekea wodi ya wagonjwa binafsi.

    Moyoni nilitamani kucheka kwa jinsi walivyopatwa na mshtuko kusikia maneno hayo kwa sababu ni kweli wote walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mimi na hakuna hata mmoja kati yao ambaye tulifanya mapenzi kwa kutumia kinga.

    Nadhani moyoni mwao kila mmoja akawa anajisemea ‘nimeshaambukizwa ngoma’. Sikuwajali kwa sababu moyoni nilikuwa najua kwamba nafanya hivyo kwa sababu gani.

    “Nani mke wa huyu mgonjwa kati yenu?” dokta aliuliza huku akitembea harakaharaka kunifuata kule nilikokuwa napelekwa. Sikuwa mbali kwa hiyo niliweza kusikia kila kilichokuwa kikizungumzwa, nikaona wote wakikwepa kwa kasi swali hilo.

    “Mimi ndiyo mkewe,” alisema Khazija, sijui alipata wapi ujasiri huo lakini nadhani ni kwa sababu na yeye alishapima, tena siku chache zilizopita kwa hiyo alikuwa na uhakika kwamba mimi na yeye tupo salama.

    “Basi wewe mkewe ndiye utakayeruhusiwa kuingia humu wodini, wengine jamani naomba mnisubiri nimhudumie mgonjwa naona virusi vyake vimechachamaa,” alisema daktari, akafunga mlango kwa ndani.

    Kiukweli nilikuwa najizuia sana kucheka japokuwa nilikuwa naumwa, Ukimwi usikieni tu lakini kiukweli unatisha sana. Basi hata sijui kila mmoja aliondoka saa ngapi lakini daktari alipokuja kutoka, hakuna aliyekuwepo pale nje ya wodi niliyokuwa nimelazwa.

    “Jamani mume wangu, mbona hujipendi kiasi hicho? Yaani hawa wote ni wanawake zako?”

    “Hapana, walikuwa wanawake zangu zamani, tena kwa nyakati tofauti, sina taimu nao tena.”

    “Muongo mkubwa wewe, hawa wengine mbona nawafahamu kabisa na nimewafahamia kwako?” Khazija alianza kulalama tena. Ikabidi nimpe ‘option’ moja muhimu, nikamwambia nikipona nataka tuhame kabisa mji, ikiwezekana twende Arusha au kwao Zanzibar, tubadilishe namba za simu na kukata mawasiliano kabisa ili tuanze maisha mapya.

    Alifurahi sana na akanihakikishia kwamba wazazi wake wanao uwezo mkubwa wa kutusaidia kama tukiamua kwenda kuishi Zanzibar, ila akanisisitiza ni lazima nimuoe tuwe mume na mke kama tulivyokubaliana.

    Basi niliendelea kutibiwa na baadaye nikapata ahueni, tukaruhusiwa kurudi nyumbani lakini kwa sababu maalum, tulienda kulala hotelini na Khazija. Usiku huo tukanunua laini nyingine za simu na kabla sijatoa ile laini yangu inayofahamika, niliwatumia meseji wote kuwaaga kwa sababu sikuwa naachana nao kwa ubaya.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nikawaambia wasiwe na wasiwasi kwa sababu mimi sina Ukimwi kama daktari alivyosema, nikawataka kila mmoja kwa wakati wake aende hospitali kuhakikisha ila nikawaambia kwamba nimeamua kuoa na kutulia kwa hiyo nahama mji. Nikazima simu muda huohuo na kutoa laini, nikaivunjavunja na kuweka ile nyingine.

    Kesho yake asubuhi tulienda mpaka bandarini, tukakwea boti na safari ya kuelekea Zanzibar na Khazija ikaanza. Miezi michache baadaye, afya yangu ikiwa imeimarika kabisa, nikiwa pia nimepata ajira kama mtaalamu wa teknolojia ya mawasiliano kwenye hoteli iliyokuwa inamilikiwa na baba yake Khazija, nilifunga rasmi ndoa na Khazija na kuwa mke wangu wa halali na huo ukawa mwisho wa tabia yangu ya ukivuruge.





    Mwisho. .

0 comments:

Post a Comment

Blog