Chombezo : Bwana Mihamala
Sehemu Ya Pili (2)
"Hapana sijakuaribia Judy , mimi sikujua kama una mume . Kama ningejua hata hapa tusingefika, lakini teyari maji yashamwagika tusijilazimishe kuzoa..tutazoa matope hapa...Mm nachokiona wewe lala hapahapa alafu kesho useme ulilala huko huko kwenye party ya rafiki yako ila ukienda sasa hivi mambo yataharibika zaidi....".
Shaibu alimbembeleza Judy huku akizidi kumpapasa mgongoni kimahaba. Judy alionesha tabasamu hafifu kwa mbaali kisha akamwambia Shaibu.
"Kulala hapa sawa inawezekana ila simu zake sijapokea wala sijajibu sms....unadhani itakuwaje ? Nitamwambia nini?...."
"....aaah hiyo ondoa shaka, wewe nenda kamwambie kuwa sherehe ilipopamba moto wote waliamua kuweka silence simu zao na wakaziacha chumbani kwa rafiki yake huyo....hivyo simu hukuwa nayo karibu....tena huku unampa meneno matam matam mbona ataelewa tu...."
Shaibu alimpa mbinu Judy na hakika Judy alionekana kuziamini mbinu hizo maana sura yake ilionesha tabasamu japo lilikuwa jembamba.
Wawili hao wakarudi kitandani na kuendelea na usingizi. Walilala mpaka asubuhi kisha asubuhi walipoamka pia walitoka pamoja.
Shaibu alishuka njiani na kwenda kwenye biashara yake huku Judy akiendelea na safari kuelekea nyumbani kwake.
******
Zilipita siku tatu bila hata wawili hao kuwasiliana. Shaibu hakujua kilichoendelea kwa Judy baada ya kufika kwao. Alitamani sana kujua lakini aliingiwa na hofu kumpigia simu Judy kwani alihisi pengine anaweza kuwa yupo na mume wake.
Ingawa alikuwa na hofu lakini bado nafsi yake ilikuwa na mshawasha wa kutaka kujua kilichoendelea na sio hivyo tu alianza kuukumbuka uzuri wa Judy.
Shaibu aliamua kwenda kwa rafiki yake anayeitwa Muki ili kumpa mchongo wa Judy. Alipofika kwa rafiki yake huyo akamweleza kila kitu kuhusu Judy kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Muki alimsikiliza kwa makini bwana Shaibu na mwishowe akamtadharisha kuwa hapaswi kumtafuta hata kwa sekunde moja kwani teyari kosa alishalifanya hivyo hapaswi kufanya kosa tena.
Shaibu alipata ushauri huo kutoka kwa Muki lakini Shaibu ni kama alikuwa na kitu chake kichwani vile. Shaibu alidhani Muki atakubaliana naye na wote watakuwa kitu kimoja.
Shaibu alipoona hivyo akaamua kuagana na rafiki yake huyo kisha akarejea nyumbani.
Akiwa chumbani kwake bado Shaibu aliendelea kumkumbuka Judy na alitamani kusikia hata kwa sekunde moja tu sauti ya Judy ili ajirizishe kuwa yu salama.
Shaibu akaishika simu yake na kulitafuta jina la Judy. Alipoliona akatafakari atume sms au apige na kwa wakati huo majira yalionesha saa moja usiku.
Akaamua kutuma sms.
"Habari..."
Zikapita dakika kumi, sms haikujibiwa. Shaibu akajiuliza itakuwa tatizo gani limetokea au ndio kusema wapo pamoja na mume wake.
Wazo la mume ndio wazo ambalo Shaibu hakutaka kulipa nafasi. Akashika tena simu akatuma sms nyingine.
"Habari Judy...."
Zikapita dakika kumi zingine sms haikujibiwa.
Sasa Shaibu akasema liwalo na liwe akashika Simu akapiga .....
"Tiiiii......tiiiiii.....tiiiii.....tiiiii"
Simu iliita hadi ikakata, hakuna aliyepokea.
Shaibu akawaza kisha akajipa majibu mwenyewe kichwani mwake kuwa pengine namba zoote zilifutwa kwenye simu na mume wake hivyo Judy hakuijua namba yake. Akaamua kujitambulisha.
"Hello mimi Shaibu....tafadhari pokea simu"
Sms ikaenda na akapiga na simu lakini hakukuwa na majibu yoyote.
Shaibu akakata tamaa ya kumsikia tena Judy. Akaachana na simu kisha akaendelea kufanya mambo yake mengine hapo chumbani.
Baadae kidogo akajibiwa sms.
"Safi , upo wapi sasa hivi?"
Shaibu akatasamu alipoona sms kutoka kwa Judy. Akajibu harakaharaka.
"Nipo home hapa..."
"Vipi tunaweza kuonana muda huu?"
"Wewe tu mimi nipo tu om...."
Shaibu akajibu bila wasi huku akiwa amesahau kama anachati na mke wa mtu.
"Unajua ile mitaa mimi nimeisahau kabisa hivi mtaa gani vile?"
Shaibu akamwelekeza mtaa kwa ufasaha kabisa yaani hata mgeni huwezi kupotea. Kamwelekeza hadi nyumba anayoishi tena akampa hadi ramani ya chumba chake.
Shaibu sasa alifurahi sana akajiona shujaa. Akapanga vitu vizuri chumbani kwake teyari kwa kumsubiri Judy.
Dakika 40 mbele, mlango wa chumba chake uligongwa. Shaibu akatabasamu akajua teyari Judy amekuja. Haraka sana akasema,
"Ingia mlango haujafungwa...."
Mlango ukafunguliwa na wakaingia watu wawili wote wakiwa wamevaa baibui.
*itaendelea*
Hakuna aliyejua kilitokea nini Judy alipoenda kwa kwake....na sasa kuna watu wawili wameingia chumbani kwa Shaibu....je mmoja wapo ni Judy? Kama ni Judy kafika na nani?
Nini kitatokea hapo chumbani? Sehemu ijayo inatoa majibu usikose...
_Mwili hutoa mwitikio tofauti na ubongo, kuna wakati roho inasema hii sio sahihi lakini mwili husema ni sahihi_
Japo ngumu ila maamuzi yaliyofikiriwa katika bongo ni sahihi zaidi kuliko maamuzi yaliyofanywa na mwili.
Shaibu anapata mshawasha wa kutaka kujua kilichojiri kwake Judy baada ya kuachana naye. Maana zilipita siku tatu bila hata kujua nini kilijiri. Ingawa alikuwa na hofu, shaibu anaamua kumtafuta Judy na sms kutoka kwa Judy inakubali kukutana naye kwa siku hiyo. Mlango wa Shaibu unagongwa na Watu wawili wanaingia wakiwa wamevaa baibui......
*Endelea*
Shaibu akiwa amejilaza kitandani chali huku akiwa na uhakika wa aliyegonga mlango alikuwa Judy, alishtuka baada ya kuona wanaingia watu wawili tena wote wakiwa wamevaa buibui.
Shaibu akaamka kitandani na kusimama kisha katika hali ya kupaniki na mshangao akauliza,
"Akina nani nyinyi?"
"Tulia kijana...."
Sauti nzito kutoka kwa mmoja wa walioingia ndani alimjibu Shaibu. Sasa mapigo ya moyo wa Shaibu yakaanza kwenda kasi kama upepo wa baharini. Japo hakuiona sura ya aliyemjibu lakini teyari alijua atakuwa mwanaume.
"Hebu kaa kwanza kijana...."
Mtu mwingine kati ya wale wawili akakazia alichosema mwenzake. Shaibu akaanza kuhisi hali ya hatari , akasogea karibu na mlango ili akimbie , mmoja akawahi kuziba mlango na kusema kwa ukali sana,
"Kijana ukifanya mchezo, pumzi yako haina hata dakika 3 tatu mbele itakuwa teyari imeisha....Wewe tulia utusikilize sisi"
Sasa Shaibu akapata uthibitisho kuwa kweli watu hao hawakuja kwa wema bali shari.
"Nyinyi akina nani na mnataka nini?"
Shaibu aliuliza huku sura yake ikiwa inaonesha imejaa mashaka tele.
"Kijana bila shaka ushafahamu kuwa sisi ni wanaume japo tumevaa mavazi ya kike, leo tumekuja kwa heri , siku nyingine tutakuja kwa kinyume chake.....mkuu hebu endelea (mmoja akamaliza kusema na kumgeukia mwenzake"
"Sasa kijana leo sura zetu hautaziona ila kuna siku utaziona ukiwa utaenda kinyume na hili nitakalokuambia.....
Bila shaka unamfahamu vyema Judy...Judy ana mume ambaye ndiye mimi, nimegundua ukaribu wako na mke wangu...Mimi hata sitaki upoteze malengo yako maana nakuangalia nakuona bado ni kijana mdogo sana ambaye bado unastahili kuvuta pumzi hii ya Mungu, najua vijana wa sasa hivi mnajifanya mnajua sana lakini nakushauri usijaribu kuyakana maagizo yangu....kaa mbali sana na Judy atakupotezea malengo yako....I'm innocent but i'm a killer...over"
Shaibu alitaka kujitetea lakini akakatizwa na mmoja wapo.
"Kijana huu sio muda wa mdahalo kana kwamba tunatafuta mshundi vile, cha muhimu kuijua nafsi yako tu ifanye nini kati kufuata nililokuambia au kufuata nafsi yako inavyokutuma...ila ikikutuma kuendelea na Judy basi matokeo utayapata"
Mtu huyo akamaliza kuongea baadae akamgeukia mwenzake na kumwambia waondoke. Wakafungua mlango na kuishia zao.
Shaibu alibaki chumbani huku akiwa amechanganyikiwa sana . Akapata uhakika kuwa aliyekuwa anachati naye hakuwa Judy bali ni yule mume wako.
Mpaka dakika kumi zinapita bado mapigo ya moyo wa Shaibu yalikuwa yanaenda kasi sana. Akaamua kwenda kuoga maji ya baridi ili kupunguza pressure maana hata kijasho cheembamba kilianza kumtoka.
Alipomaliza kuoga alirudi chumbani na kuamua kulala, ingawa ilimchukua muda mrefu kupata usingizi ila baadae alipata usingizi.
Alikuja kushtuka asubuhi ambapo kama kawaida alienda kwenye shuguli zake za kila siku.
*******
Miezi mitatu ilikatika huku taratibu akiwa teyari kumbukumbu za Judy zikiwa zimetoka kichwani mwa Shaibu. Maana hawakuwa na mawasiliano ya aina yeyote baina yao na kama ilivyo desturi ya wasiowasiliana mara kwa mara huua ukaribu wao kwa haraka sana. Mawasiliano ndio chanzo pekee cha kudumisha upendo kwa watu wanaokaa mbalimbali.
Siku moja Shaibu akiwa katika biashara yake ya miamala yaani sehemu ambayo anaifanyia kazi, ilikuwa ni jumapili, alifika mtu mmoja hivi kama mteja umri wake ukiwa umeenda kidogo kwa makadirio anaweza kucheza kwenye miaka 45 hadi 50 (kijana anayeuacha ukijana).
Mtu huyo alikuja kama mteja kufanya muamala.
"Sasa kijana nina shida ya kumtumia mtu hela kama milioni moja hivi, nimezunguka sana hapa naona wengi wamesema hawana salio....vipi naweza kuipata?"
Shaibu hakuwa na kiasi hicho, ilikuwa pungufu zaidi ya laki nane hivyo yeye alikuwa na laki mbili tu. Mzee huyo akamwambia kuwa afanye utaratibu wa kutafuta kwa mawakala wenzake hadi itimie hiyo hela. Shaibu aliwasiliana na wale mawakala wa jirani yake lakini hakuweza kuipata kwa wakati huo.
Mteja huyo kwa sababu hakuwa na jinsi na mbaya zaidi ilikuwa jumapili siku ambayo benki huwa hazifunguliwi, akamuomba Shaibu azunguke zunguke hadi aipate maana ilikuwa muhimu sana wa yeye kuituma hela hiyo hela kwa siku hiyo. Shaibu alihaidiwa kupewa shilingi elfu ishirini kama angefanikiwa kupata salio hilo.
Shaibu alikubali kufanya hivyo kwani ilikuwa ni kiasi kikubwa sana kwake kwani hata hiyo biashara yake yenyewe haikuwa ikimwingizia kiasi hicho kwa siku. Hivyo Shaibu aliona kama fursa ya haraka.
Mtu huyo akamwachia namba yake Shaibu na kumwambia kuwa hakai mbali sana na eneo anapofanyia biashara Shaibu hivyo akifanikiwa kuipata atampigia simu alafu atafika mara moja kwa ajili ya kumpatia pesa na kuituma.
Shaibu akaanza kupambana kutafuta 'float' salio kwa mawakala wenzake. Mwenye elfu hamsini , laki nakadharika.
Alipambana hadi ikatimia milioni moja na kisha akampigia simu yule mtu. Yule mtu baada ya kupokea simu alimuomba sana Shaibu achukue bodaboda ili akachukue hela na namba.
Kwakuwa hapakuwa mbali sana, Shaibu akachukua boda boda na kufika eneo aliloambiwa ndani ya dakika tano tu.
Alipofika eneo hilo akampigia simu, kisha akapata maelezo ya nyumba ilivyo na alipoiona akaenda moja kwa moja na kuingia ndani ya uzio.
Alipofika mlangoni (mlango wa nyumba yenyewe) akagonga kisha mlango ukafunguliwa na yule mtu na akamkaribisha ndani.
Waliketi kwenye sofa saafi za ngozi, ndani mkiwa na ubaridi wa kiyoyozi. Samani zilizokuwepo ndani humo zilikuwa za kisasa kabisa. Hakika sebule lilipendeza sana!
"Sijui lini nitayafikia haya maisha"
Shaibu alijiwazia moyoni mwake.
"Kijana nashukuru sana kwa msaada wako maana nilishakwama kabisa asee, unajua bwana kuna watu wanataka wautume mzigo wangu wa samaki wapo huko kisiwani mwanza....sasa ilkuwa lazima nitume leo maana wale samaki ni wabichi wakikaa sana wanaharibika.....ngoja nimwite wife alete pesa alafu namba hii hapa tuma humu...."
Shaibu akaanza kufanya muamala wake. Akamaliza kuufanya kikamilifu. Mtu yule akamwita mke wake ili amletee hela.
Dakika moja tu mbele, manukato mazuri yalianza kunukia sebuleni hapo. Mwanamke mrembo mdogo hivi wa umri pengine anaweza kuwa hata mwanaye wa kumzaa mtu huyo aliingia sebuleni akitokea chumbani. Bila shaka ndiye alikuwa ni mke wa huyo jamaa.
"Mpe huo mzigo huyu kijana"
Mtu huyo alisema, na yule mwanamke akageuka kumpa Shaibu mzigo.
Macho yao yalipokutana, kila mmoja alitumbua jicho la mshangao kwa mwenzake. Yule mwanamke alikuwa ni Judy.
*Itaendelea*
Hapa ndipo huja ile kauli usijaribu kuyazuia mafuriko kwa mikono yatakusomba.....
Hatimaye wamekutana....Je ni kweli yule mtu alimsahau Shaibu au ulikuwa mpango wake tu wa kutaka kujua kama wanawasiliana baina yao?
*Hisia hazizuiliki*
Hebu tuone nini kitajili sehemu ijayo, usikose.
Sehemu iliyopita imeishia wakati ambapo Shaibu anakutana tena kwa mara nyingine baada ya muda mrefu kupita bila hata mawasiliano. Wanakutana wakiwa nyumbani kwa Judy anapoishi yeye na mume wake. Shaibu yeye alienda kufanya miamala tu ambapo aliitwa na mume wa Judy. Inawezekana Mume wa Judy alimsahau kabisa Shaibu kwani alimuona siku moja tu tena ikiwa usiku.
Sasa endelea hapa....
Judy akasita kidogo huku macho yake yakiwa kama hayaamini amini hivi. Shaibu yeye japo alishtuka kidogo ila hakutaka kujionesha moja kwa moja kuwa ameshtuka. Alijaribu kujizuia ili asionekane kwa mume wa Judy.
Judy aliganda kama dakika moja hivi bila kukabidhi hela kwa Shaibu kitu ambacho kikamfanya mume wake aingilie kati.
"Vipi mama...mpe hela kijana akaendelee na kazi zake maana nimemchelewesha sana....."
Judy hapo ndo akazinduka, akamkabidhi hela Shaibu . Baada ya kupokea hela Shaibu akasimama ili aondoke.
Mume wa Judy akamwambia Shaibu kuwa yeye anaitwa Mr Shamte na atakuwa anampigia mara kwa mara kama atakuwa akihitaji huduma ya miamala.
Shaibu akaaga na kuondoka zake.
Baada ya Shaibu kuondoka, Judy akaamuliza mume wake amempata wapi wakala huyo.
"Aaaah basi ushaanza wewe mambo madogo kuyakuza....nilimuona hapo nyuma karibu na ile sheli tupojazaga mafuta kwa yule mdada....."
Sasa hapo Judy akapata ushaidi wa sehemu ambayo anaifanyia kazi Shaibu. Maana kuna siku za nyuma aliwahi kwenda kazini kwake na hakumkuta. Kumbe Shaibu sehemu ile aliama na kuamia sehemu nyingine na hii ndio sababu pekee iliyomfanya Judy ashindwe kuwasiliana na Shaibu kwa kipindi chote hicho.
Judy akajiridhisha kuwa mume wake hakuwa anamjua Shaibu na hakumleta pale kwa lengo lingine zaidi ya lile aliloitiwa la kufanya miamala.
Moyo wa mwanadamu umeumbwa kwa nyama na ile mishipa inayopitisha damu, hivyo kuumia ni sehemu yake. Moyo wa Judy ukaanza kuwa na Shauku ya kutaka kukutana na Shaibu.
Akili yake haikutulia tena, kila alilofikiria liliishia kwenye jina la Shaibu. Siku moja aliwahi kurudi kazini kwake ili ampitie Shaibu na waweze kuongea.
Kwa bahati mbaya sana alipofika sehemu hiyo hakumkuta , palikuwa pamefungwa. Namba yake hakuwa nayo maana laini ambayo ilikuwa na namba ya Shaibu aliibadirisha mume wake na kumpa laini mpya.
Judy akaenda nyumbani na alipofika akili haikumtulia kabisa. Akawaza sana akaona bora aende anakoishi labda atamkuta.
Alienda ile mitaa lakini bahati mbaya iliyomkuta alisahau nyumba na hata alipojaribu kuulizia jina la Shaibu hakuna aliyeweza kumjua.
Judy akarudi nyumbani na kutulia. Baadae akapata wazo , akaona ampigie mume wake na amwambie kuwa shangazi yake wa Iringa amempigia simu anataka amtumie hela hivyo akamuomba ampigie simu wakala amwambie amtumie kwani yeye anajisikia vibaya hawezi kutoka nyumbani kwake.
Mr Shamte kwa kuwa aliona ni kawaida tu wala hakufikiria kingine chochote, akampigia simu Shaibu na akumtaka aende nyumbani kwake ili akatume hela.
Shaibu siku hiyo hakufungua ofisi yake, wakati anapigiwa simu alikuwa kwa rafiki yake Muki wakipiga soga za hapa na pale. Shaibu alijua kuwa Mr Shamte atakuwa yupo kwake na ndiye aliyemwita.
Shaibu akamuaga Muki ili aende kufanya muamala na uzuri ni kuwa alikuwa anatembea na simu zake za kazi hivyo safari yake ilianzia hapohapo kwa Muki. Wakati anaondoka Muki akamtadharisha Shaibu awe makini akiwa nyumbani kwa Mr Shamte kwani wanawake wakiwa wanataka kitu, chochote huweza kufanya ili mambo yao yakamilike.
Shaibu akaondoka na kwenda nyumbani kwa Mr Shamte.
Mr Shamte alimtaarifu Judy kuwa wakala anaenda hapo, kwa hiyo hata mlango ulivyogongwa hakushangaa sana alijua ndiye atakuwa Shaibu. Ni kweli alikuwa Shaibu aliyegonga mlango.
Shaibu alishtuka alipokaribishwa na Judy tena akiwa amevaa kigauni chepesi sana ambacho kilimchora vyema mwili wake.
Sebule lilikuwa tulivu sana, palionekana papo kimya na hapakuwa na bugdha yeyote ile.
Shaibu alivuta pumzi ndefu sana na kisha akaishusha , Judy akaufunga mlango na kumkaribisha Shaibu kwa tabasamu bashasha lenye kusisimua.
"Usiogope nipo mwenyewe tu, kuwa na amani...."
Judy alizidi kumchangamsha Shaibu na kuzidi kumtoa hofu.
"Wewe ni kijana mdogo sana....kama unahitaji kuendelea kuvuta pumzi hii ya Mungu basi achana na Judy..."
Maneno aliyoambiwa na mume wa Judy miezi kadhaa iliyopita yakawa yanajirudia rudia kichwani mwa Shaibu.
"Ni mimi ndiye niliyekuita, nimekumisi sana...nimekukumbuka sana Shaibu....Nimeshindwa kujizuia kabisa...."
Judy aliongea huku akizidi kumsogelea Shaibu ambaye alikuwa anaonekana kama mtu anayewaza jambo hivi.
"Lakini...."
"Lakini nini..."
Judy alimziba mdomo Shaibu ambaye alionekana kuna jambo alitaka kuongea.
Wakati huo teyari Judy alikuwa ameshamvamia Shaibu, sasa walikuwa karibu sana tena sana. Mashetani ya Judy yalishapanda na hayakuwa na mtu wa kuyatuliza wakati huo.
Shaibu akaonekana kama anataka kama hataki, alikuwa katikati ila kwa hakika si kazi rahisi kwa mwanaume yeyote ambaye yupo kamili achomoke kwenye mazingira hayo aliyoyaonesha Judy.
Shaibu akaacha uchovu,akaanza kuonesha ushirikiano kwa Judy. Biashara ya miamala ikawekwa kando hata yale maneno ya Mr Shamte yakapotea ghafla. Mahaba yakatawala kati ya wawili hao.
*Itaendelea*
Haya sasa mambo ndo hayo yashakuwa mambo.
Hivi kweli kila jambo lilishapangwa na Mungu na binadamu anatimiza tu???
Hili la Shaibu na Judy lilishapangwa au ni wao wawili ndio wamepanga?
Unadhani watafanya mambo yao bila kukutwa na Mr Shamte?
Usikose sehemu ijayo....kuna mengi ya kujifunza.
Judy anamkumbuka Shaibu ,anatamani akutane naye .Anafanya kila mbinu na hatimaye kweli anafanikiwa kumpata Shaibu. Shaibu ambaye bwana miamala hakujua kama ni mtego wa Judy...anakubali kwenda nyumbani kwa Judy kufanya muamala.....Muamala haufanyiki....mambo ya baishara yanawekwa kando....mahaba mazito yanatawala ndani ya nyumba ya Mr Shamte.
Endelea sasa.......
Mahaba ya hapa na pale yakaendelea. Walijiachia kabisa kama gari lililokatika break likiwa mteremkoni, kila mmoja nafsi yake ikasema ,
"Hakika hizi ndio raha za dunia...."
Walifanya kila walichoweza kufanya. Hata kuoga bwana Shaibu alioga hapo hapo, hata chakula cha mchana bwana Shaibu alikula hapohapo.
Kwa muda mfupi tu, Shaibu akili yake iliruka na kuona kama hayo ndio maisha yake yaani kama yeye ndio mwenye nyumba vile.
Wakiwa bado wapo sebuleni, huku wakiwa wanachekeshana hapa na pale , simu ya Judy iliita , alikuwa ni Mr Shamte alikuwa anamuulizia kama alifanikiwa kutuma ile hela. Kwa sauti ya mahaba sana Judy akamjibu Mr Shamte,
"Eeeh nimeshafanikiwa kutuma...tena yule kijana yupo sharp sana yaani alikuja faster, hakika anaijua vizuri biashara yake...."
"Yeah kweli malaika wangu, yule kijana yuko vizuri sana , mimi nilimuona alivyoitafuta ile miliona moja ya siku ile....Mungu amjalie afike mbali sana na aje kupata mke bora....."
Baada ya mazungumzo hayo wakaagana kisha simu ikakatwa.
"Angejuaa?? hahaa kazi kwake....wewe ndiye furaha yangu ya kweli (huku akimshikashika mikono Shaibu)"
Judy aliongea hivyo mara baada ya kumaliza kuongea na Mr Shamte.
Shaibu na Judy waliji-mwaya mwaya hadi ulipokaribia muda wa kurudi kazini ndipo Judy akamtaka Shaibu aondoke.
Shaibu akaondoka zake na kitita cha hela kama laki tatu hivi alizokabidhiwa na Judy, laki moja ikiwa kama hela aliyoituma na laki mbili amepewa tu za matumizi yake.
Shaibu alienda moja kwa moja kwa mshkaji wake , Muki. Alipofika tu akakuta ugomvi unaendelea hapo kati ya Muki na wapangaji wenzake.
"Wewe unakaa tu hapa...hulipi umeme wala nini...."
"Kama maisha yamekushinda rudi kijijini kwenu huko usije ukatupa corona hapa..."
"Hata maji wewe hulipi..."
"Yaani hata hela ya usafi wa chooni hatoi yeye anajua kunya tu....."
Wapangaji hao walitoa kila aina ya neno bovu kwa Muki. Muki hakuwa na cha kuwajibu kwani yote wayasemayo ilikuwa ni halali yao kwani ilipita miezi 3 hakulipa hela yeyoyte.
Maneno hayo yalimchoma sana moyoni Muki , hasa akikumbuka kuwa elimu yake ni kubwa sana kuliko hao wapangaji lakini mfukoni hamna kitu.
"Oya mwanangu shika hii kilo(laki moja) wape..."
Shaibu alimnong'onezea Muki.
Muki akajibu,
"Aaah mwana eeeh achana nao hao....hela zenyewe za watu hizo, usije ukaingia matatizoni alafu mambo yakaaribika kila sehemu...."
Muki alimjibu hivyo Shaibu kwani wakati ule kabla Shaibu hajaenda kwa Judy alimdokeza suala la yeye kudaiwa hapo na alimtaka Shaibu amkopeshe hela ili alipe lakini hakuwa nayo , alikuwa ana hela ya biashara tu tena sio yake. Kwa hiyo Muki akafikiri kuwa Shaibu anataka kutoa hela ya mtaji kumbe Shaibu alijaa pesa kutoka kwa Judy.
Shaibu akatoa shilingi laki moja na kumkabidhi Muki kisha akamwambia mambo mengine wataongea baadae ila awakabidhi kwanza mzigo wao. Muki akachukua ile na kisha akahesabu elfu sabini na akamkabidhi mtu anayepokea hela.
Baada ya hapo, Shaibu na Muki wakaingia chumbani.
Shaibu na muki walikuwa marafiki walioshibana sana, urafiki wao ulianzia wakiwa chuoni huko Mwanza katika chuo kikuu cha SAUT wakiwa mwaka wa kwanza tu.
Wote hawa walisoma Shahada ya elimu katika sanaa yaani bachelor of arts with education. Walipomaliza , pia wakakutana tena mtaani jijini Dar es salaam na wakawa wanatafuta wote ajira ila kwa sababu ajira kuwa finyu sana hawakuweza kupata. Kila walipoenda walikosa, hata ile nafasi ya kujitolea hawakuipata.
Ndipo wakaamua kufungua kituo cha masomo ya ziada "Tuition" .
Wakawa wanafundisha nyakati za jioni maana ndio muda ambao wanafunzi wanakuwa teyari washarudi nyumbani. Wanafunzi waliwapata ingawa hawakuwa wengi sana na changamoto nyingine iliwakumba ya kutopata malipo yao kwa wakati hivyo bado hali ya kuyamudu maisha haikuwa ya kuridhisha.
Mambo yaliwabadirikia kabisa janga la corona lilipoingia kwani hata ile tuition yao wakalazimika kuifunga kufuatia agizo la waziri mkuu la kuepusha misongamano. Hata kile kiasi kidogo wakawa hawakipati.
Shaibu yeye akawa anasimamia kwa muda biashara hiyo ya miamala ya ndugu yake, kwani kwa wakati huo ndugu yake alisafiri nje ya mkoa.
Shaibu akampa stori Muki jinsi mambo yalivyokuwa nyumbani kwa Judy na hadi zile hela alizopewa hadi akampa yeye ile laki moja.
Ingawa pesa hizo zilimsaidia Muki siku hiyo katika kutatua mzozo wake lakini hakusita kuonyesha mashaka juu ya hatari iliyopo mbele ya Shaibu. Kwa mazingira yaliyopo , Muki akamshauri Shaibu amchunguze sana Judy kwani pengine kuna jambo limejificha nyuma ya pazia hasa ukiangalia umri wa mume wake na wake ni tofauti kabisa tena wameachana mbali mbali sana. Muki akaendelea kumwambia yawezekana yule mwanamke amekuja kuharibu maisha ya Shaibu maana ikija kujulikana basi Shaibu atakuwa matatizoni sana, hivyo pamoja na kujua mambo kadhaa kuhusu Judy, Shaibu hana budi kuachana na Judy.
Shaibu alikubaliana na mawazo ya Muki, akapanga siku wakutane na Judy ili waongee na kufahamiana kabisa maana tangu wakutane hawakuwahi kuzungumza kuhusu maisha yao binafsi zaidi ya mahaba tu.
Siku kadhaa mbele yapita kama mwezi hivi walikutana Judy na Shaibu katika moja ya fukwe zilizopo pembezoni mwa bahari ya Hindi huko maeno ya kigamboni.
*Itaendelea.....*
Je kuna jambo gani limemfanya Judy akae na mume mwenye umri mkubwa kuliko umri wake?
Hivi mtu unayetaka kuachana naye unataka kuijua historia yake ili uifanyie nini??? We shaibu wewe......
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment