Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

UPEPO WA KISULISULI - 5

    


Chombezo : Upepo Wa Kisulisuli 

Sehemu Ya: Tano (5)


"Sultan?"

Nilishangaa kuona Nancy akishangaa kwa kunitolea mimacho huku akiziba mdomo.


ENDELEA..............


"Haa mbona unauliza Nancy?"


"Si kuuliza tu bali na kushangaa pia, haiwezekani unipigie simu kisha usipatikane tena na leo hii unatokeza ukiwa na hali hii? Mungu wangu Sultan umekumbwa na nini? Niambie nijue."

Nancy aliongea maneno haya kwa uchungu mkubwa huku machozi yakimtoka na kila aliyekuwa akiingia dukani kwake alimshangaa lakini yeye hakujali kitu.


Mimi mwenyewe nilijisikia vibaya sana kwa machozi ya Nancy nikajikuta natokwa na machozi na baada ya kukumbuka yaliyonikuta nilitokwa zaidi na machozi nilitamani niliye zaidi lakini ndo hivyo pale nilikuwa kwenye mapito ya watu.

Nancy alikuja kutaka kunikumbatia lakini mimi nilirudi nyuma kutokana na nilivyokuwa nilihisi nitampa mikosi Nancy.


"Mbona unarudi nyuma Sultan ndo kusema hunitaki siyo?"

Nancy aliuliza.


"Hapana Nancy najiona mchafu mbele yako japo nimeoga lakini bado najiona nanuka mwili mzima na sistahili kuwa karibu yako."


"Kama ni hivyo ulikuja kufanya nini kwangu Sultan?"


"Nilikukumbuka Nancy na nilitamani kabla pumzi yangu haijakata walau wewe ambaye ni mtu wangu wa karibu upate kujua kilichopata siku kadhaa nyuma."


"Ulikutwa na nini sasa?"


"Naomba tusiongelee hapa Nancy tutafute sehemu salama kisha nitakusimulia kila kitu."


"Poa basi nisubiri niache utaratibu mzuri kwa mfanyakazi wangu dukani."


"Sawa nakusubiri Nancy."


Aliniacha na kuingia dukani kama alivyosema kuwa anataka aache mazingira mazuri ya kazi, na baada ya hapo alitoka na kunionesha ishara ya kumfuata kule alikokuwa na mimi bila ajizi nilitii amri na kumfuata.

Tuliingia kwenye kigari chake aina Suzuki New Model. Na safari ilianza.


"Sultan nimeona tuelekee kwangu ambako ni sehemu salama na tulivu sana."


"Sawa tu."


"Hapo katikati mambo yaliniendea kombo kidogo kutokana na kuumwa na pia mawazo juu yako mpaka nikaamua kubadilisha mfumo wa maisha yangu ikiwa ni pamoja na kuuza baadhi ya vitu vyangu yakiwemo magari yangu yote na hii ilikuwa tu ni kukusahau wewe Sultan lakini ilikuwa ni kazi bure kwani ikawa kama vile ndiyo nimeweka sura yako kwenye kioo cha miwani yangu kila siku nilikuwa siishi kukuwaza mpenzi na mpaka kuna siku nilirudi kule getoni kwako nikiamini naweza kukuona tena. Hata maagizo yako sikuwahi yatimiza ya kubeba vitu vyako."


"Pole sana Nancy, kwa hiyo unataka kuniambia kuwa bado viko kule kule?"


"Haina haja tena ya vitu hivyo mimi ninachojali ni wewe kuwa hapa tena mpenzi."


Muda huo tayari tulikuwa nje ya geti la nyumbani kwake na alipiga honi kumpa ishara ya kufungua geti. Huwezi amini baada ya geti kufunguliwa Casto alikuwa mlangoni akimpa ishara bosi wake ya kupitisha gari, baada ya kushuka tu alikuja mpaka pale nilipokuwa.


"Hivi nakufananisha au ni wewe Sultan?"


"Casto wala hujakosea mimi ndiye mwenyewe."


Nilipomjibu alitamani kuuliza swali lakini ndo hivyo aliishia kuniangalia kwa macho ya huruma wakati Nancy aliponitaka tuingie ndani.


"Karibu ndani mpenzi wangu Sultan."


"Asante sana mpenzi."


"Kabla ya yote naomba uoge na ubadili nguo zako najua nguo zangu zitakutosha tu kwa kuwa mimi na wewe hatutofautiani sana saizi zetu."


"Nashukuru sana mpenzi sina cha kukupa ila yavumilie matatizo yangu."


"Si muda wake hayo, ingia bafuni upate maji."


Niliongoza bafuni kuoga, nilioga na kisha niliingia chumbani kwa Nancy na kumkuta Nancy akiwa ameniandalia nguo za kubadilisha. Na baada ya hapo alinitaka tuelekee saluni kwa ajili ya kutengeneza muonekano wangu wa sura.

Tulitoka na kumuacha Casto sisi tukaelekea mjini.

Baada ya kufika tuliingia kwenye saluni moja hivi ya kiume na humo nilifanyiwa matengenezo ya nywele na sura yangu kwa ujumla.


"Wao na sasa wewe ndiye Sultan ninayemfahamu."


Nancy alinibusu na kunikumbatia mbele ya watu waliokuwamo mle saluni.


"Asante Nancy kwa kila kitu na sas


a najiona mtu mbele ya watu."


"Wala usijali mpenzi ni wajibu wangu kuyafanya yote haya kwa nimpendaye na nitafanya zaidi na zaidi."


Alitoa hela na kumlipa kinyozi kisha tulitoka na kuelekea dukani kufanya manunuzi ya nguo zangu si unajua tena ndo nilikuwa naanza upya life yangu.

Tulinunua nguo, viatu na vitu vingine muhimu vya kwangu.


" Unaonaje kabla ya kuelekea nyumbani twende maeneo ya airport kwa mtu mmoja ambaye ndiye aliyeniokota."


"Wala haina shida kabisa, tunaweza kwenda tu."


Basi safari yetu ilianza kuelekea airport kwa mwenyekiti ili nikamuage na kumshukuru kwa wema wake alionifanyia mimi.


"Hodi, hodi, wenyewe hodiii."


"Karibu pita ndani."


"Asante shemeji, Sultan hapa."


Alikuja na kutufungulia mlango na mara baada ya kutuona hakuamini.


"Hee Sultan umerudi, mbona umechelewa kiasi hicho? Umesababisha mpaka kaka yako kaenda mjini kukutafuta."


"Hakuwa na haja ya kunitafuta maana mimi ni mwenyeji zaidi hapa mjini."


"Sawa lakini wasiwasi ni muhimu kwa binadamu."


"Okey, ila nisingepotea shemeji."


"Sawa, naona una ugeni."


"Ni kweli kabisa hujakosea shemeji, huyu anaitwa Nancy ni mpenzi wangu na si mpenzi tu bali ni mchumba wangu ambaye muda wowote nategemea kumuweka ndani."


"Aisee hongera sana, nafurahi kusikia hivyo. Karibu sana Nancy sisi ndiyo tuliomuokota mpenzi wako akiwa hajitambui kabisa sijui kakusimulia?"


"Hapana bado, ndiyo tulikuwa tu shopping na baada ya kurejea nyumbani ndo yangefuata hayo ya alikokuwa."


"Shemeji tuachane na hayo kwanza kilicholeta zaidi ni kuja kukushukuruni kwa mema mlionifanyia sina cha kuwalipa ila Mungu ndiye atawalipa. Akija mwenyekiti nitaomba uniagie."


"Kwa hiyo ndiyo umekuja kuaga? Si ungeendelea kuishi hapa hapa Sultan tulishaanza kukuzoea japo ni siku moja tu tumeishi pamoja."


"Tunaomba tu uturuhusu maana hata mimi mpenzi wake nilikuwa na hamu naye sana hasa kwa sababu katokea iweje niishi naye mbali?"


"Ni kweli kabisa Nancy, kikubwa tu sisi tunaondoka na niwahakikishie kuwa nitaendelea kuwatembelea ninyi ni ndugu zangu shemeji."


"Haya shemeji mtembee salama na Mungu akawasimamie kwa kila mtakachokuwa mnakifanya maishani mwenu."


"Kwamba ndo safari Sultan?"

Mwenyekiti aliingilia mazungumzo yetu baada ya kuingia.


"Ndiyo mwenyekiti nimempata mwenyeji wangu nikaona nije kuwashukuru na kisha kuwaaga ndugu zangu."


"Sultan naye bwana eti mwenyeji wake si useme mchumba wako tu.

Mke wa mwenyekiti aliongea na kuwafanya Nancy na Sultan kutazamana na kucheka.


Ni kitu gani kitaendelea?

Usikose katika sehemu inayofuata ya ishirini na saba.




Waliaga na kuondoka zao maeneo hayo ya airport. Walikuwa wenye furaha sana muda wote hasa Nancy ambaye hakutarajia kukutana tena na Sultan Uwezo mara baada ya kukwaruzana.


"Hivi ni kwanini nimekuwa teja wa penzi lako Sultan?"

Nancy alinitupia swali.


"Hata mimi najishangaa kama wewe tu ni kwanini nimekuwa teja wa penzi lako, lakini nahisi jibu ni moja tu sisi ni mateja wa mapenzi ila si kwa wengine bali panzi letu."


Nilipomjibu hivyo acha tu bwana nilipigwa handwave kiss' matata sana. Sijui ni nini lakini hapa ndiyo nilianza kuuona uzuri wa Nancy namna alivyoumbika kuanzia jicho mpaka simalizii msije nivizia tena mkaniteka na kuniulia mbali ili mumbebe mazima Nancy wangu. Tulifika nyumbani na kwa kuwa tulimissiana sana kitu cha kwanza ilikuwa ni kwenda chumbani kupima uwezo wa uwanja wa fundi seremala kama unaweza kumudu pambano kwa muda mrefu na ukizingatia hapa katikati palipita kimya na hivyo kila mmoja wetu hapa alikuwa na hamu na mwenzake wenyewe wenye kiswahili chao huita Ugwadu sijui mwenzangu huitaje vyovyote vile ila tu ni kwamba vita ya miili yetu ilikuwa kubwa sana.


"Baby nilikumiss sana."

Yalikuwa ni maneno ya Nancy mara baada ya game kutamatika.


"Hata mimi nilikumiss sana mpenzi wangu acha tu."


"Kwanza nieleze ulikuwa wapi mpaka kuwa kwenye muonekano ule kama kizee cha miaka sabini?"

Alinitumia swali mpenzi wangu hakutaka kunipa hata sekunde moja.


"Sawa naanzaje kutokukusimulia wewe mboni ya jicho langu?

Ilivyokuwa mara baada ya kufika stendi, nilikutana na mke wa Johnson rafiki yangu tuliongea mengi lakini lililonishangaza muda ule wa majira ya jioni pale stendi ni kipi alikuwa anakifanya, lakini baada ya kumuuliza kilichomfikisha pale aliniambia anarudi kwao kwani kachoshwa na vitendo vya mumewe Johnson."


"Vitendo gani hivyo mume wangu."


"Inasikitisha sana mpenzi wangu, niliambiwa kuwa rafiki yangu kipenzi wa muda mrefu Johnson na shemeji yake Mooren ambaye ni rafiki wa mke wake wanatoka na shombe shombe moja hivi la Kiarabu."


"Mbona sikuelewi Sultan, punguza mashairi yako nenda kwenye pointi bwana."


"Nancy kuwa mpole utaelewa tu, katika maisha yangu yote ya kufahamiana na Johnson sikuwahi jua kuwa ni shoga tena shoga maarufu ambalo wateja wake walikuwa ni vigogo tu au watoto wa vigogo na watu maarufu."


"Mungu wangu mbona hafanani hata kidogo kwa muonekano wake Johnson?"


"Ndiyo hivyo Nancy, na mbaya zaidi aliamua kuoa ili kutimiza matakwa ya mwajiri wake tu kwani ilikuwa ili uendelee na kazi kwenye ofisi ile ilikuwa ni lazima uoe ili kuwa mfanyakazi makini hivyo Johnson akajikuta analazimika kuoa na katika hili alipongezwa na wafanyakazi wenzake na kupewa mazawadi kemkem kumbe nyuma ya pazia Johnson ni shoga."


"Lakini mpenzi wangu nasikia kuna baadhi yao wameoa na wanafamilia zao zenye afya tele."


"Inawezekana ila si kwa Johnson yeye alikuwa hawezi hata kusearch network hivyo yeye na mke wake walikuwa wanalala mzungu wa nne. Na mbaya kuliko yote ni Johnson kushirikiana na rafiki yake Evetha mke wake Mooren kumuhudumia kimapenzi mume mmoja hili lilimkwaza sana Evetha na kuamua kuondoka jijini Mbeya ili kuepukana na aibu kuu ambayo ingeikumba familia hiyo."


"Duniani kuna mambo ninyi?"


"Lakini Mungu hamfichi mnafiki hata siku moja kwani kwani mara baada ya Johnson kubaini siri yake imenifikia kuwa yuko hotelini akimpa uroda aka utamu mume wake huyo naweza sema hivyo, aliamua kuchukua maamuzi mazito ya kunywa sumu ambayo ilipelekea umauti wake na wakati tuko hospital kujaribu kuokoa uhai wake ndipo nilimuona yule mwanaume anayetoka naye na aliposikia kuwa Johnson hatunaye aliamua kukimbia na ndipo nilipomfuatilia kwa nyuma."


"Jamani Johnson alijiua, eeh nini kilifuata baada ya hapo?"


"Nilikumkuta yule mshenzi nikamueleza ninafahamu kila kitu kumuhusu yeye na marehemu Johnso


n hivyo asijidanganye kukimbia na nina ushahidi wa picha na video. Aliposikia hivyo ilibidi awe mpole na kuahidi kunipa shilingi milioni tano kasoro laki mbili kwamba keshi shilingi milioni nne na laki nane na baada ya kumchimba mkwara wa nguvu aliniandikia check ya shilingi milioni hamsini ili nisisambaze uchafu wake mtandaoni kwa kuwa baba yake ni mtumishi wa MUNGU. Nilikubali na ndipo nilipokupigia simu kwamba tuonane lengo likiwa ni kuja kukukabidhi fedha na ile check ndipo nirudi kuendelea na taratibu za maziko ya Johnson kwani hata safari ya Tabora niliona imeyeyuka tayari. Kumbe nilikuwa nimechelewa kwani wakati ndiyo nikiwa maeneo ya Makunguru nikija Soweto ndipo nilipotekwa na watu wake yule shombe shombe."


"Walikuteka?"


"Ndiyo mpenzi."


"Mungu wangu, ndiyo maana nilipiga simu siku ile wapi kumbe ulikuwa mikononi mwa watu wabaya?"


"Ndiyo mpenzi, na hapo ndipo walipokwenda kunifungia wapi maana nakumbuka tu zile siku za mwanzo ambazo nilimuona na yule Shombe Shombe alipokuja niliteswa sana ile check na hela walichukua."


"Kwani toka urudi una muda gani?"


"Leo ni siku ya pili tu na penyewe nilikutwa nimetupwa kwenye ule uwanja wa ndege wa zamani na mwenyekiti na watu wake ndipo waliokoa."


"Unajua ni muda gani umepita Sultan?"


"Ndiyo kinachonichanganya hapa ni hicho tu."


"Ni miezi miwili imepita toka unipigie simu na wewe unasema ulitekwa siku ile ile maana yake ni kwamba ulishikiliwa mateka kwa zaidi ya mwezi mmoja."


"Ndiyo maana!!"


"Ndiyo maana nini?"


"Wakati mwenyekiti ananipeleka kwake njiani nilimuona Mooren lakini hakunifahamu japo alinitazama sana kama vile ananifananisha."


"Kwa ulivyokuwa umechakaa ni nani angekufahamu mimi mwenyewe ilinichukua muda kukufahamu, kikubwa mpenzi wangu ni kumshukuru Mungu kuwa hawajakufanyia kitu mbaya kwa kuingilia mambo yao vingine tumuachie Mungu."


"Asante sana Nancy kwanza kwa kunipokea na pili kuyabeba madhaifu yangu yote na ni nakuahidi kuwa kuanzia sasa narudi kwenye kazi yangu ya uandishi wa hadithi na pia nakwenda kuwa mume wako iwapo utakubali hili."


"Unauliza? Hata muda huu niko tayari kuwa mke wako Sultan."


"Kama ni hivyo inatakiwa tufanye taratibu zote za kifamilia na kiimani kisha?"


"Kufurahiiii." Nancy alijibu kwa sauti ya juu.

Tulikumbatiana wenyewe kwa muda na huku kila mmoja akitokwa na machozi ya furaha na kisha tulioga na kutoka nje ambapo tulimkuta Casto akiendelea na shughuli zake za maua.


"Casto." Nancy alimwita.


"Naaam bosi."


"Kuanzia leo mtambue aliye mbele yako kama bosi wako namaanisha kuwa yeye ndiye Sultan halisi wa maisha yangu na mimi ni malkia wake."


"Waoooo, kila siku nilikuwa nawaombea mkutane na kusameheana na kuanzisha familia."

Casto aliongea hayo akiwa katukumbatia wote na ukumbuke kuwa huyu dogo alinikubali toka siku ya kwanza.


"Kwa hiyo bosi kuanzia sasa hadithi zitapikwa hapa hapa."


"Kama kawaida na nitakufundisha pia na wewe."


"Mhhh nitawezea wapi mimi mlugaluga."


"Utaweza tu Casto."


Tuliendelea na mazungumzo ya hapa na pale wakati huo Nancy alikuwa jikoni kuandaa kifungua kinywa.

Na baada ya kupata kifungua kinywa tuliondoka nyumbani pale na kuelekea nyumbani kwa akina Mwamvua kufuata vitu vyangu kwani sikuwa tayari kuviacha vitu vyangu hasa laptop yangu pamoja na kuharibika lakini ilikuwa na vitu vingi vinavyohusu uandishi wangu.


"Karibuni wageni."

Mwamvua alitukaribisha mara baada ya kushuka kwenye gari.


"Asante Mwamvua, habari ya siku."


"Ni nzuri japo si sana."


"Kwanini?"


"Mama yangu Chaukorofi alikamatwa na pombe kali ya gongo akiwa rafiki yake na hivyo hivi tunavyoongea wana wiki moja toka wahukumiwe kifungo cha miezi mitatu jela."

Mwamvua huyu aliyekuwa anaongea haya kwanza nilimshangaa sana kwa namna ambavyo alikuwa mtulivu tofauti na yule ninayemfahamu.


" Pole sana Mwamvua kwa yote yaliyowakuta najua Mungu atamsaidia na atatoka akiwa salama kabisa."

Nancy alimtia moyo Mwamvua kwa haya yaliyowatokea.


"Asante dada, na pia naomba msamaha wako Sultan kwa yote ambayo tulikufanyia huko nyuma."


"Mwamvua nilishawasamehe kitambo sana na ndiyo maana leo niko hapa kuchukua vitu vyan


gu na kama nisingewasamehe nisingerudi kamwe."


"Sasa kama umetusamehe kwanini unaondoka? Si ungebaki tuendelee kuishi hapa kama zamani."


"Usinielewe vibaya Mwamvua, ningeendelea kuishi hapa lakini huyu niliyenaye hapa anaitwa Nancy si mgeni kwako ndiye mke wangu."


"Haaa umeoa Sultan?"


"Nimeoa Mwamvua."


"Hongera sana Sultan Uwezo kwa maamuzi uliyofikia kwani ile siku umefurumushwa na mama nilikuwazia mengi sana inawezekana Mungu alisikia maombi yangu."

Maneno ya Mwamvua yalimtoa machozi Nancy kwa sababu siku hii anaikumbuka vizuri sana sababu ndiyo siku ambayo ilisababisha tutengane mimi na yeye.

Nilimtuliza Nancy na kisha nilimuomba funguo Mwamvua ili tutoe vitu ndani, ililetwa na kisha kwa kushirikiana naye tulitoa vitu vichache kama nguo na laptop tu vingine vyote nilimkabidhi Mwamvua kama zawadi yao na vile vile Nancy alitoa noti za shilingi elfu kumi ishirini yaani laki mbili na kumpa Mwamvua kama kumtia moyo kutokana na magumu anayopitia na kisha tuliaga na kuondoka zetu.


"Yaani baby huwezi amini Mwamvua huyu aliyekuwa anaongea kwa upole ndiye alikuwa mcharuko hatari kama mama yake kipindi cha nyuma."


"Maisha yanakwenda kasi sana na watu wanabadilika kulingana na nyakati my love"


"Ni kweli kabisa love kwa hili na amini."


"Tupitie Mwanjelwa nikakuoneshe kijiwe chako."


"Kijiwe cha kufanya nini?"


"Tukifika ndiyo uniulize."


"OK." Safari iliendelea na kweli tulifika Mwanjelwa ndani ya soko kuu tuliingia na kupaki usafiri wetu kisha tulipanda ngazi mpaka ghorofa ya pili na kuingia kwenye chumba namba 0001 ambacho mlangoni kulisomeka SULTAN UWEZO (Hadithi na Simulizi) OFFICE

Tuliingia na kukutana na bonge la ofisi likiwa limesheheni kila kifaa kinachotakiwa katika kazi ya uandishi na kukiwa na picha kubwa ukutani yangu na Nancy hakika ilikuwa bonge la surprise kwangu.


"Hii ndiyo ofisi yako mpya kabisa ya kazi."


"Baby niseme nini kwako mimi zaidi ya asante." Niliongea hayo na kumbeba juu juu Nancy wangu mtu ambaye amejitolea kuirudisha heshima yangu ambayo ilipotea muda mrefu.


"Wala usijali baby, huu ni mwanzo tu nitafanya kila kitu kwa ajili yako na njoo huku nikuoneshe ofisi nyingine."


Tulitoka nje na kuingia kwenye chumba kingine ambacho kilikuwa kinafanya kazi ila tu juu ya mlango kulikuwa na tambaa kubwa lisilo na maandishi. Tukaingia ndani.


" Habarini wadogo zangu."


"Salama madam za nyumbani."


"Kutaneni na mtu wa kuitwa Sultan Uwezo."


"Sultan Uwezo yupi dada?"


"Huyo huyo mnayemfahamu."


"Mungu wangu, huyu ndiyo mwandishi wa hadithi?"


"Hujakosea ndiye mimi mwenyewe Sultan Uwezo mwandishi wa hadithi zenye maudhui mbalimbali."


"Yaani siamini macho yangu, kaka mimi ni shabiki yako mkubwa wa hadithi zako hasa ile ya Safari ya Yatima ila tu nashangaa haiendelei."


Mmoja wa wafanyakazi aliuliza swali lakini halikujibiwa kwani Nancy alikatisha.


"Tusikilizane, Sultan Uwezo kwa sasa ndiye bosi wetu hapa NANCY UWEZO PHOTO POINT na kwa kusema hivyo naomba tutoke nje na Sultan utatutolea hicho kitambaa."


Nancy aliongea hayo kunitambulisha tukiwa nje ya ile studio na kisha nilikivuta kile kitambaa na kufanya maandishi yale yasomeke wazi kabisa ambayo ni NANCY UWEZO PHOTO POINT.


" Baby hii ni studio yetu ya picha pamoja na kutengeneza kava mbalimbali za vitabu, majarida na CDS na wewe ndiye bosi wetu karibu sana."


Kwanza huwezi amini nililia japo si kwa sauti bali nilijikuta tu machozi yananitoka kwa furaha nilimkumbatia Nancy na kumshukuru sana kwa zawadi alizonipa.


"Nancy nakushukuru sana kwa kila kitu kikubwa tu naomba niwaeleze kuwa bado Nancy ataendelea kuwa bosi wa ofisi hii na mimi nibaki kwanza kuiweka sawa ofisi yangu hiyo ambayo haijaanza na sasa hata wapenzi wa kazi zangu hawatapata ugumu kunifikia kirahisi."


Baada ya kila kitu kuwa sawa tuliwaaga wafanyakazi pale studio tukafunga na ofisi yangu kisha tukashuka zetu ngazi na tukiwa tunaikaribia gari nilimuona Moreen akiwa na yule mshenzi aliye niteka.


" Sultan upo, ulipotelea wapi mbona mazishini hukufika?"

Mooren alinipiga maswali mfululizo na wakati huo yule Shombe shombe wake alijidai kama anaongea na simu na kupotea zake.


"Mooren bado hujaacha mchezo yako michafu tu."


"Siwezi acha kwani niliianza toka niko skuli ya upili na huyu ndiye aliyenifundisha hivyo kwa sababu yake kuwa kufanya hivyo kutapelekea hata nikiolewa mume wangu atanikuta mpya kutokana na kutogusa njia halisi kumbe ilikuwa ni kujidanganya kwani kwa sasa nimekubuhu hela ndiyo hakimu wangu."


"Pole sana Mooren, ila kama ulivyouliza kwanini sikumzika Johnson ni kwamba uliyenaye ndiye aliyesababisha nisimzike kwani aliniteka kwa muda wa mwezi miwili hivyo sidhani kama nitaona hata kaburi lake."

Mooren alipogeuka nyuma ili amuulize jamaa yake kama ni kweli hakuona mtu.


" Unasema kweli Sultan, na ulitekwa kwa kosa gani? "


" Hilo utamuuliza yeye maana hata mimi hakuniambia."


"Na huyu ni nani Sultan?"


"Huyu anaitwa Nancy ambaye ndiye mke wangu mtarajiwa."


Mooren kusikia hivyo aliachia msonyo mrefu na kuondoka zake na kutuacha sisi tukitazamana na Nancy kisha tukaingia garini na kuondoka zetu kwani Nancy alijua stori nzima ya Mooren aliyoambiwa na Johnson.


** MWISHO *


MPENZI MSOMAJI NIKUSHUKURU SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI KUANZIA MWANZO MPAKA MWISHO WA HADITHI HII YA UPEPO WA KISULISULI.

MWISHO WA SIMULIZI HII NI MWANZO WA SIMULIZI NYINGINE.


0 comments:

Post a Comment

Blog