Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

BEPARI TIMOTH - 5

   


Chombezo : Bepari Timoth

Sehemu Ya: Tano (5)


naye alimkumbuka kijana beko, alikuwa ni mtoto wa rafiki yake mkubwa ambae kwa

sasa ni malehemu, basi waliingia ndani nakumusimulia kila kitu kinachoendelea

kule kijijini kwao. kwaufupi nikwamba, chief matomondo ndie alikuwa kiongozi

wa kijiji chao hapo mwanzo, baada ya kijiji kuvamiwa bepari Timoth, akiuwa

viongozi akiwemo na baba yake Timoth, yeye alikimbia akiwa na jeshi lake,

alikaa porini kwa mda mrefu. Huku naye kwa muda huo, alikuwa anapanga njama za

kuvamia kijiji hicho nakukikomboa, sasa alipofika beko alipa njia zote za

kuvamia kijiji hicho, kwa kuwa beko aliishi kwa mda mrefu sana kijijini hapo

akiwa mateka, alimpa mbinu nyingisana za kuvamia. Ndipo jitihada na mipango ya

kwenda kukikomboa kijiji chao, ilikuwa ikipamba moto basi vijana walifanya

mazeozi makali sana, huku chief matomondo na Kijana Beko ndiyo waliokuwa

kakiongoza mazoezi hayo. Zilipita siku kazaa za maandalizi hayo makali, siku

ya siku walianza safari ya kwenda kukikomboa kijiji chao, basi walitumia mda

mrefu sana, mpaka wakaanza kukiona kijiji cha bepari Timoth, ilikuwa usiku

sana, ndipo wakapanda kwenye kilima huku wakiwa makini sana, ndipo Beko

akawapa mbinu za kuingia kwenye kijiji kile, basi Chief matomondo akaamulu

vijana wake, akiwagawa kwamakundi, bahazi wapite mbele na wengne nyuma ya ile

ngome, huku Beko na Chief matomondo wakipeana majukumu ya kukiteka kile

kijiji... je watafanikiwa, itakuwaje kwa wakina Tausi, ukimaliza kusoma

nijulishe kwa like au comment yako kisha




No32: kama walivyo elekezwa na Beko, ndivyo vijana wa Chief Matomondo walivyo

Fanya, basi walifanikiwa kuingia ndani yakijiji, licha ya mapambano kuwa

makali baina ya kikundi cha Chief matomondo na bepari Timoth.lakini vijana

waliokuwa pamoja na Beko walijitahidi sana, Kiukweli vijana wa Chief matomondo

walikuwa wameimalika kikamilifu, licha ya vijana wa bepari Timoth, walizidiwa

nguvu. Huku mapigano yakiendelea vijana wa Chief matomondo walikuwa wakisonga

mbele, bila kuludi nyuma,huku wakialibu na kuchoma moto sehemu muhimu za

bepari timoth, hali ilivyo endelea kuwa upande wa timoth ilibidi waludi nyuma,

hivyo basi, wakina beko walikomboa kipande kikubwa cha eneo lile. wakati huo

pia kijana Beko aliangaika kila kona, akimtafuta Tausi bila mafanikio yoyote,

ndipo alopoonana na Kijana yule, aliye kuwa akichunga lile fahari, lililo

pelekea majerui kwa malkia shadya, (nazani umekumbuka) ndipo Beko akamuuliza

yule Kijana naye alimwelekeza huku akisema "nimemwona akikimbia, huku na yule

mama wa mfalme, (akimaanisha shadya) lakini kama wana fukuzwa na timoth " bila

ya kupoteza mda, Beko alitoka mbio akifwata njia, aliyo elekezwa na yule

Kijana, huku njia nzima, akipambana na wapinzani wake, aliokutana nao, kwenye

mapambano hayo, Kijana Beko hakuwa na utani na maadui .... UNAZANI BEKO ATAWAI

KUYANUSURU MAISHA YA MPENZI WAKE, NINI KITATOKEA BEPARI AKIWAI KUWAKAMATA,




No 33 :Jitiada za Beko kumtafuta Tausi azikuzaa matunda,licha ya kupita

chocholo zote anazo zifahamu, lakini Kijana huyo akukata tamaa, hiyo ilikuwa

desturi yake daima kukata tamaha kwake ni mwiko. Kumbe Tausi aliposikia vita

vimeanza akajua tu! kuwa jembe lake Beko karudi kukomboa kijiji chao, mida

hiyo mtiti unaanza, Tausi alikuwa na shadya maeneo ya kulia chakula,

akimuhudumia huku wakipiga story, maana baada yakugundua kuwa Beko alikuwa

mpenzi waTausi, alijutia nafsi yake, na urafikiwao ukawa waukweli, siyo wa

malkia na mtumwa, baada yakusikia kelele nje walichungulia na kuona mapigano

yamepamba moto, ndipo Tausi alimshika mkono mwenzake wakaanza kutafuta mahari

pa usalama zaidi. Huku vita vikiendelea bepari Timothy alichanganyikiwa kwa

kuona vijana wake wanavyo uawa. Bepari Timothy aliimalisha ulinzi alipokuwa na

kujificha kwa uwoga zaidi ndani ya jumba lake, nadipo alipo mwona Tausi

anapita na bi, Shadya akaamua kuwafwatilia, maana alikuwa na uakika kuwa

muusika wauvamizi ule ni kijana mtukutu Beko, upande mwingine mfalme yule

aliye toka UK aliona hali ni ngumu na kutokomea pasipo jurikana, akiwa na

walinzi wake, huku akimwacha mkewe shadya. Basi vita ilishika kasi kwa mda

mrefu huku Chief matomondo, akiakikisha vijana wake wanaondoka wakiwa kufua

mbele. Beko na wapiganaji wenzake waliakikisha wanapambana na wanajeshi wa

Timoth pekee huku wakiwaacha watu wote wasio na hatia, Timoth naye aliendelea

kuwafwatilia kwa ukaribu wale wakina Tausi, pasipo wao kujuwa, kwa sasa hapa

pana tosha wakati una jiandaa kupata story nyingine endelea ku like na ku



No34:Timoth naye aliendelea kuwafwatilia kwa ukaribu wale wakina Tausi, pasipo wao kujuwa, shadya na Tausi wao waliendelea

kukimbia, Beko alizidi kukimbia huku na huku akimsaka Tausi, maana aliamini lazima Timoth, akiwakamata atamfanyia kitu

kibaya, hapo hapo ikwa ina mjia picha ya sikuile alipo nusulika, kunyongwa,basi loho ilimuuma sana, akapndwa na hasira, pipa

zima, akaongeza speed, kwakimbilia, wakati huo baada ya kuona mumewake amemtelekeza mke wa Bepari Timoth, akaona akibaki

mwenye pale nyumbani yata mkuta majanga, maana wavamizi lazima watavamia pale, ambapo ndiyo makazi ya Timoth, na wakimkuta,

lazima atafidia maovu ya mumewake, akatoka nje na kutazama pande zote, akaona wavamizi hawakuwa na mpango na wakina mama

wala watoto,akaona siyo mba akikimbai kweny shamba la miwa akajifiche huko mpaka asubuhi, ndipo ajuwe lakufanya, maana

atakama wavamizi hawawadhuru, wakina mama kamayeye, lakini yeye ni tofauti, maana ni mke wa adui yao, timoth naye alikuwa

amesha wakalibia kabisa wakina Tausi, ambao walikuwa wana kimbilia kwenye mashmba yamiwa, na muda wote alikuwa na basola

yake, huku mke wa timoth aliendelea kukimbilia kwenye shamba la miwa, lakini kwambali alimwona mmewake akiwa kimbiza

wanawake wawili, kutoka na giza hakuweza kuwatambua, nao walikuwa wakielekea kwenye mashamba ya miwa, . Bila ya kujua Tausi

na shadya walijitaidi kukimbia ili wajifiche kwenye miwa, ndipo walipo kodwa macho yao na kumwona bepari Timoth karibu yao,

hofu ikamjia kweli alishituka sana kwani alikuwa mjamzito huku mimba ilikuwa tayari imekomaa kwaajili ya mtoto kuzaliwa.

Bepari Timoth alinyoosha mkono wake uku ukiwa na mguu wa kuku (bastola) ili bidi Tausi awempole kwani alikuwa anamjuwa

vizuri, mtu huyu bepari Timoth, ni katiri sana linaweza kumuua papo hapo. Upande mwingine Beko alijitaidi sana kumtafuta

Tausi ila akumwona ndipo alipochukua jukumu la kuingia kila nyumba ili amtafute mpenzi wake Tausi,wakati anafanya zoezi la

nymba kwa nyumba, malakasikia mlio wa risasi, ukitokea upande wa mashamba ya miwa, hapo hapo aktoka mbio kufwata mlio wa

risasi ulipo tokea, Duu! unazani hiyo risasi imetuwa kwa nani? ebu somakwaza hii kisha










No 35 : bepari Timoth alikuwa amepiga risasi moja juu,ilikuwa tishia wana Tausi, nakuwalazimisha watulie, na aliakikisha akuna atakaye mtoroka, ili yeye apate njia rahisi ya kumuua Beko mpenziwake Tausi. Basi aliwachukua wawili hao nakutoka nao mbali kidogo na eneo la vita, akiingia ndani zaidi ya shamba la miwa, wakati bepari Timoth akitoka nao, mkewe naye aliona kwa mbali akitokomea na shadya na Tausi, kumbuka naye mke wa bepari Timoth alikuwa amechoshwa na ukatiri aliokuwanao mumewe, basi naye aliwafata nyuma nyuma kwa kuibia, ili ajue niwapi anawapeleka. hapo Tausi na Shadya hawakuwa na ujanja, waliongoza kama mbuzi anaekwenda kutolewa kafara, maana Timoth alikuwa na bastora mkononi. hukunako kwenye mapigano Ushirikiano wa wanakijiji wapale na vijana wa Chief matomondo, kiongozi wao wazamani, ulikuwa ni nzuri sana, maana wanakijiji nao, walichoshwa na ukatiri ulikuwa ukiendeshwa na bepari Timoth, kwenye kijiji chao, walizamiria wakimwondosha kabisa wakiamini watakuwa huru. Beko alipokuwa anapita mbio mbio kuelekea kwenye mashamba ya miwa, wanakijiji walimshangilia sana wakimtia moyo kwa vifijo na ndelemo, huku akipambana vilivyo, kwa style ya mapigo na mwendo, ili kuakikisha masaria ya uchafu wa bepari Timoth hayatakuwepo, wakatimingine aliuliza wanakijiji, nao walimwelekeza njia aliopita bepari Timoth, naye alizifata ili kuakikisha mpenzi wake Tausi yuko salama. Bepari Timoth alipofika ndani kidogo ya shamba la miwa, kama alikuwa amepandwa na mashetani, ukatiri wake ukampanda ghafla na kutaka kuwaua wanawake hawa, maana aliamini kuwa, haya mapinduzi yana letwa na mtu wao Beko, akaona jambo zuri, nikuwa twanga risasi, naye atokomee porini, hapo akainua bastola yake, akiwaelekezea wanawake hawa wawili, ambao walikuwa wanatetemeka vibaya mno, wakijuwa mwisho wao umewadia,wakati Timoth akijiweka sawa kummaliza Shadya ambae, alikwa ameshikilia Tausi, Ndipo mke wa bepari Timoth, ambae alikuwa akifwatilia mchezo mzima, alipoona kuwa akifanya mchezo mumewake ata wamaliza wale wote, hapo alichukua kipande cha muwa mkubwa uliokuwa umedondoka maeneo yale, naye kwa tahadhari kubwa alisoge kwakunyata, kisha kwa nguvu zakezote aliinua ule muwa nakuuvuta nyuma , kama mtu anaye cheza mpila wa gofu,hapo Timoth kwakidole chake cha pili baada gumba, aliminya kifyetulio (trriger), "paaaah!" mlio ambao ulimfikia tena Beko, lakini sasa kwaukaribu zaidi, akaongeza mwendo, kuwai eneo la tukio,..... haya wadau sijuwi kama risasi hii imemwacha mtu salama, ebu soma hii kisha nijulishe kwa like na comment kisha tuendeleee, ili leo tumalizane na Bepari Timoth, tumsome



No36: Risasi ile ilimpata Tausi kwenye bega lake la kushoto, nakupoteza fahamu kutokanana maumivu makali sana aliyoyapata, kwani risasi ilipitakaribu na mfupa wa bega, nalengo la bepari Timoth alikusudia kupiga kwenye moyo wa Tausi, sasa Tausi wakati ikipigwa ile risasi yeye alijitaidi kuikwepa, lakini hakufanikiwa, risasi siyo mpra wa rede, ndipo ilipo mpata maeneo hayo ya bega lake. kuna msemo usemao, kama siku zako zimefika, ndiyo zimefika tu! hakuna ata sekunde za kukopa, lakini kwa binti Tausi zilikuwa bado azijafika, na mungu alifanya yake, mke wa Tomoth, alisita kwanza kutokana nakuogopa ul mlio wa risasi, lakini sasa akona, hasichelewe, akuvuta tena muwa kitendo bila kuchelewa, akausukuma kwa kasi ya kilomite buku, kwa saa, na uzito wa tani moja, muwa huo ulituwa sawia nyuma ya kichwa, karibu na maeneo ya shingoni, hapo kama gunia lisilo na uhai bepari timoth alienda chini"puuu!" akifwatiwa na muwa mwingine wa kichwa, uliosababisha kuvunjika kabisa muwa wenyewe, nakumpatia usalama wake Timoth ambae alikuwa amesha katamoto (amezimia). kwa muda hule Beko kwambali aliona tukio la timoth kupigwa na muwa, kitucha kushangaza alikuwa ni mkewake mwenye ,ndie alie mtandika, alipo kalibia zaidi alimwonkama Tausi yuko chini, kwa nguvu zote bila kuchoka alikimbia upesi na kufika mahari, akamwangalia mkewake, ambae alikuwa amekata moto, huku damu ikimvuja kwafujo kifuwani..... haya jamani leo ni weka kitu toa kitu, soma hii nijulishe kama tayri, ili tuendelee, lengo tuimalize kisha tuanze na kitu cha ISABELAH, nahiyo ni hapa hapa



No37 ambae alikuwa amekata moto, huku damu ikimvuja kwafujo kifuwani , Beko huku akilia kwauchungu akijuwa amesha mpoteza mkewake, maana alijuwa Tausi wake kaisha poteza maisha, alimsika na kumtazama mkewake, lakini akagundua kuwa mapigo yamoyo yalikuwa yapga kwambali, ndipo alipo agiza kijana mmoja, amletee dawa za kienyeji ili ampatie huduma ya kwanza Tausi, wakati akitoa huduma ya kwanza, ndipo alipo alipowaamulu vijana wamuondoe bepari Timoth, wampeleke chini ya mti aliowaelekeza kwenye uwanja wa damu, bila kuchelewa vijana walimwondoa pale alipokuwa amelala, ambapo na sasa alikuwa anajiwa nafahamu, akashuhudia vijana wakimburuza, nakuelekea hasipo kujuwa, huku jitihada za kuokoa maisha ya Tausi zilianza Mara moja bila ya kupoteza mda. Miongoni mwa wale vijana kunakijana mmoja alikuwa hodari, kutumia mitishamba na kuponesha watu kama Tausi. Ndipo alipo itwa Mara moja, akaja nakuanza kumtibu Tausi, wakati akiendelea kutibiwa Tausi alishituka kidogo na kufumbua macho ndani ya dakika chache, kisha aka funba tena akionyesha hakuwa nanguvu za kutosha, kitendo hicho kiliashiria kwamba, Tausi bado ajafa. Chief matomondo alifika naye maeneo Yale, na vijana wake wachache wakawachukua wale wanawake, iliwakawaifazi vizuri, yani shadya na mke wa Timoth, huku wakimbeba Tausi na wote kwapamoja wakaelekea kwenye mapango ya karibu na ile ngome basi walifanya hivyo, na Tausi aliendelea kupata nafuu. Basi Beko baada ya kujilizisha kuwa ,mkewake yupo katika hali nzuri, akajiunga nawenzake, kwenda kupambana tena, ilikumalizia malizia masalia ya vijana wa bepari Timoth........ hapo sasa tuendelee kuwa pamoja ili tumalizie mkasa huu wa BEPARI TIMOTH, tuanze



No38: Beko alirudi vitani huku akimwachia maagizo Chief matomondo ateuwe vijana wampeleke Tausi kwa mganga wa kienyeji basi Chief alifanya hivyo ili kuokoa maisha ya binti Tausi. Vijana wa Chief matomondo walimfikisha Tausi KWA mganga huyo na kuanza matibabu haraka. Vita haikuwa ya kitoto maana bepari Timothy alikuwa na majeshi mengi sana, vita ilikuwa kama ya maji maji vile watu awakulala. kwa upande mwingine shadya na maria mke wa bepari timoth wajibanza pangoni wakiwa wanashuhudia jinsi gani mapambano hayo yakipamba moto huku wakiona majeshi ya bepari Timoth yakikimbia ovyo ovyo! na kukosa mwelekeo wengine walitimukia porini na wengina walijifanya vichwa ngumu, eti mpaka tone la mwisho, walipigana wakiambulia kifo, maana jeshi la Chief matomondo lilikuwa limejipanga kikamilifu.Shadya na Maria, walitulia pale huku wakimsifu kijana Beko kuwa kijana mwenye moyo wa upende na mwenye utu, ilifika mda kijiji kilikuwa kimeturia, kikiashiria vita vimekwisha. Takilibani msaa kumi vita vilikuwa vinapigwa, mpaka ikafika tamati, kilicho fwata waka chaguliwa vijana sita, wakamchukua Timoth nakuongosana na Beko, kisha waka elekea kwenye zizi la ng'ombe, nakumfunga kamba Timoth mikono na mi guu, kisha wakalfungia kwenye lile fahari lenye vurugu, kisha waka lifungulia na kuli chpa pa fimbo, nalo likaanza kutimua mbio laiki mbuluza timoth, ng'ombo huyo alizunguka kijiji kizima, na kil watu walipo mwona wali mlushia mawe nalo lika zidi kutimua mbio, nakuzidi kumwazibu bepari timoth, ambae alikuwa anahacha alama za damu kila anapopita ..... naam tunakaribia kufika mwisho wa story hii




No39: kijiji kilikuuwa kimya kwa mda huku kikiashiria vita vimekwisha, nusu saa baadae, wanakijiji walipiga kilele za shangwe, wakiamini uhuru wa kijiji chao umetimia. Wanakijiji waliwashangilia mashujaa wao beko pamoja na Chief matomondo, kwa kuwa mstari wa mbele kupigana kufa na kupona mpaka mwisho. Beko alikwenda ambako Tausi alipokuwepo kwa mganga wa kienyeji, na kukuta hari yake iko vizuri. Tausi alipomwona Beko alilia sana kwani hakujuwa kuwa Beko ameichukuliaje kuhusu ile mimba, huku akiwaza hayo beko alimchukua Tausi na kumpeleka mahari alipokuwa ameandaa kwaajili ya kuishi yeye na familia yao. nipale alipokuwa anakaa Bepari timoth, ambae sasa alikuwa amekata roho, na kwenda kutupwa kwenye mto wamamba, Walifika huku na beko akamwandalia maji ya kuoga Tausi akamwogesha, ukuchukulia kuwa Tausi bado alikuwa haja rudiwa nanguvu sawa sawa, alipo maliza waliketi pamoja huku wakipiga story mbili tatu ndipo Tausi alipo mweleza ukweli Beko kuhusu ile mimba, na beko akamwelewa mkewake, nahakuwa nakipingamizi chochote, siku zikapita amani ikatawala maisha yao, muda ulifika na Tausi alijifungua mtoto wakiume, aliyekuwa akimfanana sana na bepari Timoth, licha ya yote yaliyo tokea, beko alimwona kama mwanae tu. Beko alifanya mipango ya kuwasaidia shadya na maria mke wa bepari Timoth kuondoka kwenye kijiji kile, basi mipango ilikwenda sawa na shadya aliludi kwao UK pia maria mke wa bepari Timoth, aliondoka na kurudi kwao. Basi wanakijiji walimteuwa beko kuwa kiongozi wao, kwani alikuwa mstari wa mbele kwaajili ya kuleta uhuru kwenye kijiji hicho, lakini Beko hakuwa tayari kuongoza kijiji hicho, hivyo alimkabizi madaraka Chief matomondo, kuwa kiongozi wa kijiji chao, kwani licha ya kuwa yeye aliwai kuwa kiongozi wa kijiji hicho,pia naye alikuwa mstari wa mbele katika mapinduzi, basi wanakijiji awakupinga maamuzi ya Beko, ndipo Chief matomondo akawa kiongozi wao. Miaka ikapita ndipo beko naye akapata mtoto kwa Tausi. Beko alikuwa tajiri sana pale kijijini, alikuwa akisaidiana na Chief matomondo kukiongoza kijiji hicho, ndipo maneno ya Beko yakatimia kuwa lazima atakipigania kijiji chake, na sasa kijiji kina tawaliwa na AMANI UPENDO NA FURAHA, MPAKA KUFIKIA HAPO WADAU TUMEFIKIA MWISHO WA SIMULIZI HII YA MICHORO, ILIYO KUJIA KWA ISANI YA KENDY TOKA AFRICA YA KATI, JIANDAE KWA STORY YA ISABELAH ITAKAYOANZA HIVI PUNDE...NASHUKURU SANA KWAKUWA PAMOJA NA MIMI MWANZO MPAKA MWISHO 



MWISHO


0 comments:

Post a Comment

Blog