Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

JIRANI TAM TAMUU - 3

   


Chombezo : Jirani Tam Tamuu 

Sehemu Ya: Tatu (3)


"Yes,"

"sawa sisi tunatoka basi,"

"sawa ila gari yangu imegoma kuwaka?. "

"Si ungeenda na juma au alitangulia kutoka?. "

Kabla hajajibu simu yangu iliita kuangalia alikuwa mke wangu,

"hellow wife, "

"gari ya kazi kwangu imepita nimepanda ili nisikusumbue kunipitisha ofisini, "

"sawa kwa hiyo ilikuwa imekuijia?."

"Hapana ilikuwa inatoka kwa dk Alex, mtaa wa nyuma hapa"

"sawa, "

nikiitika ila nikijiuliza eti gari ya Hospital imepita inatoka mtaa wa nyuma kwa dokta Alex? Inamaa hizi siku chache mitaa yote kaijuwa? Na huyo Dokta ni nani? Huyu mke vipi mbona kama ana wenge? Niliacha kuyawaza nikaendelea kuongea na shomy,

"hajanitangulia kutoka ile yule mwanaume hawezi kunipakia kwenye gari yake?. "

"Kwanini?"

"Sijui basi tu hataki?. "

"Twende basi nikupe rifti,"

"usihofu nitachukua tax, "

"why wakati mimi nipo?"

. "Wewe unaenda air port mimi naenda posta wapi na wapi vinakutana?."

"Nitakupeleka kwa kuwa najua thamani ya mwanamke, "

Alitabasamu akaniangalia akajibu

"haya twende,

Tuliianza safari ile natoka tu nikapigiwa simu, "

"seif wahi ofisini bosi anakuhitaji kwa ajiri ya mkutano wa dharula,

"sawa niko njiani mwambie dk40 nitakuwa hapo,"

"sawa, "

"vp unahitajika ofisini?. "

"Ndio nahitajika ila acha nikufikishe ofisini kwako, "

Niliendesha gari kwa spidi kari ili niwahi kufika posta niko kwenye mataa ya jagwani upande wa pili nililiona gari juma mme wa shomy ila nilipoangalia vizuri nilimuona Zahara akiwa ndani ya hilo gari pamoja na juma,

*mmh!! Naota au sioni vizuri?* nilijiuliza kichwani ila nilipata jibu kutoka machoni mataa yaliruhusu gari ya juma ikakata kushoto kuelekea mhimbili na mimi nikaunga nyuma ila shomy hakuusoma mchezo wala gari hakuiona, "shemeji mbona huku?"

"Nakwepa foreni ya faya,"

"mh!! Njia unazijua za mkato,, "

"sana tu, gari ya juma ilisimama nje ya super makert,


Endeleaaa...

Nilichofanya nilipitiliza nikasimama mbele kidogo nikashuka,

"shomy nisubili kidogo nakuja, "

"sawa"

Niliondoka nikaelekea kwenye hiyo super market nilipofika mlangoni niliwaona kupitia kwenye vioo wakicheka ?? ?? kwa fura niliumia sana ndani ya moyo nikalilia ??moyoni nikaona haina haja bora niondoke zangu,

Nilirudi kwenye gari nikaondoa gari kwa kasi shomy akaniangalia kwa jicho la mshangao,

"vp seif?"

"Kawaida tu, "

alinyamanza hakuuliza kitu kingine, kwani alijiuliza huenda nimeona kitu kilichonikasilisha nilipokwenda.

Nilikuwa najiuliza mambo mengi sana kwani niliwaza au zahara na juma walikuwa na mahusiano ya mda mrefu? Nilijiuliza ila hakukuwa na jibu nilibaki kufikilia kuwachunguza ili nipate ukweli wote,

Nilijikuta nafika posta nikamshusha shomy,

"Seif asante sana, "

"na wewe pia,"

"na mimi pia? "

"Ndio,"

"kwa lipi?"

"Kwa kunipa sapoti ya maongezi na kukubali kutia baraka katika gari yangu,, "

"sawa wahi basi maana si nilisikia unahitajika ofisini?, "

"ndio, basi kwaheli nitarudi kukuijia, nipe namba yako."

"mh!!. Nisikusumbue Seif, namba ni 0763*56 **4"

"wala hunisumbui,"

"Mh!!.. sawa basi utaniijia,"

"Ok. Kazi njema,"

"na wewe pia,"

***********

Niliachana na shomy nikawahi ofisini,

Nilifikia kwenye kikao cha bodi kujadili kupandisha bei ya usafilishaji,

"Seif mbona kimya tunataka mawazo yako wewe ndie master hapa"

"labda tumsikilize meneja masoko si ndie anayejuwa zaidi,"

"Seif hauko sawa hebu tuvunje kikao tutakutana kesho tena,"

Kikao kilivunjwa nikarudi ofisini ila mawazo yalikuwa kwa mke Wang nilijiuliza ukaribu wake na juma unatokea wapi alafu nikajiuliza kwanini alinidanganya kuwa anaenda na gari ya kazini wakati aliondoka na juma? Kwa uongo huo inaonesha ana uhusiano wa kimapenzi na juma,

Niliwaza ila nikapata hakiri ya kumpigia chande simu anifafanulie kwanini amemleta juma kupanga kwangu na anieleze juma ana uhusiano gani na mke wangu wote si madokta wanajuana,

"Hallow chunde habari yako? "

"Nzuri vipi swahiba,"

"poa ila nieleze juma na Zahara wana uhusiano gani?,"

"mh!!! Si kwa ajiri ya kazi tu, "

"acha ujinga chande nieleze ukweli,"

Chande alishangaa kumuita mjinga kwani alijuwa kuwa namheshimu sana,

"Seif unanitusi?. "

"Nieleze acha kuzunguuka bwana,,"

"Seif nimekwambia hawana uhusiano wowote,"

"Chande kuanzia leo usinisemeshe,"

"kwanini?"

"Sina kwanin' kwaheli,"

Like yako ndio italeta mwendelezo.

"Usikate simu nitakwambia"



Endelea nayo.

"Niambie sasa,,"

"Seif ama kweli una hasira ila kumbuka tulipotoka alafu ujue dhamani yangu kwako,"

"Hatuko kwenye ngonjera hapa nieleze kama hutaki achaa.."

"Sikia seif nikuwa juma na mkeo hawana mahusiano ila mwaka ulioisha juma alitakakumuoa Zahara lakini ikashindikana kwa kuwa Zahara alikuwa anakwenda India kusoma, alipokuwa india huku nyuma juma alipaanza mahusiano na msicha aliyekuwa nesi pale hospita na mahusiano yao yaliazaa matunda kwa kupata mtoto, zahara aliporejea alikutana hali hiyo na ndipo habari ya uchumba ikafia hapo na kudhibitishia kuwa hawakuwahi hata kufanya mapenzi wala hata busu haikuwepo,"

"Nashukuru sana kwa maelezo, "

nilikata simu,

Kumbe hapo nimepata jibu kwa hiyo watakuwa wamefufua mapenzi yao?

Niliwaza mengi yasiyokuwa na majibu kabisa ila moyo uliniambia vitendo vyao vitanipa majibu,

Nikiwa katika mawazo chande aliingia ofisini kwangu,

"Habari yako seif?."

"Nzuri,"

"Seif imebidi nije kuna nini tatizo kuhusu juma na Zahara?."

"Nikuulize swali? "

"Uliza, "

"hv juma ana tatizo la macho?."

"Hapana, "

"juma siku anahamia pale nilipomchunguza niliona anamkonyeza mke wangu,"

"mh!! Labda walikuwa wanataniana.."

"Matani kukonyeza mke wa mtu?"

"Hapo ndio tabu," "sikia na isitoshe zahara leo nilimuacha kwenye gari yangu nikaingia ndani ile niko ndani akanipigia simu kuwa ameona gari ya kazini kwao kwahiyo amepanda ameondoka, nikamwambia sawa kwakuwa tunaishi barabarani nikajua kweli kaiona ila nilichoshudia sasa ndicho kilichonitoa imani nilipokuwa kwenye mataa pale jangwani nilimuona akiwa na juma kwenye gari ya juma nikashituka sana nikawafuatilia nyuma nikaona wameingia suprmarket ya pale mtaa wa muhimbili hv mpaka hapo wewe chande kuhusu simulizi hii unaweza kuidadavua vipi kama wewe ndio mimi? "

"Mh!!!. Nashindwa niseme nini? "Siyo kwamba unashindwa useme nini ila wewe ndie mtuhumiwa wa kwanza kwa kuwa nakuhisi wewe ni dalali kwa mke wangu, "

chande alinikatisha akadakia,

"kwanini uniite dalali, "

"tena sikia chande wewe si dalali bali wewe ni kuadi wa mke wangu kwaku ulimuombea nyumba juma ili aweze kuwa karibu na mke wangu wafanye mambo yao, "

"Seif utakuwa unanihukum bule mimi,"

chande alitoa machozi huku kwa uchungu mpaka nikamuonea huruma nikakumbuka tulipotoka,

Enzi hizo miaka hiyo tukiwa watoto wadogo tena tukiwa hatuna wazazi tukiishi mwanza katika kituo cha tuliane cha watoto wa mitaani hali ilikuwa ngumu kupata chakula ilikuwa mtihani ila tulisaidiana kwa kila hali nilichonacho nilimpa alichokuwa nacho alinipa tulitembea pamoja kuomba omba mitaani aliyepata alimpa mwenzie ikafikia hatua chande akapata mfadhiri ulaya ila akakataa kwenda kwa kuhofia ataniacha mpweke ila nikatumia ujasiri kumwambia aende,

"chande wewe nenda ukipata na mimi nitakuwa nimepata, "

"siwezi kukuacha seif, "

"usipoondoka hutakuwa rafiki yangu tena maishani mwangu,"

Kauri hiyo ilifanya chande aondoke kwenda ulaya,

Nilipokumbuka hayo nilimsogelea chande huku machozi yakinitoka,

"Nisamehe chande,"

"nimekusamehe najua mke anauma kiasi gani,"

Tuliogea mengi hatimae tukaachana akarudi ofisini kwake,

Jioni nilimpigia simu mke wangu,

"Hallow wife?."

"Yes swty, "

"nitakuijia au? "

"Usisumbuke nitakuja na gari ya ofisini,"

"sawa,"

"Utatoka kazini saa ngapi?. "

"Saa 12,

"sawa,"

Nilinyamanza baada ya kufika saa kumi nilimpigia shomy, "vp mtoto wa kinyamwezi?"

"Poa za wewe? "

"Poa nakupitia njua mida ndio hii,"

"sawa,"

Nilienda posta nikamchukua tukaanza kurudi nyumbani ila nilipofika mitaa ya home nikamuona Zahara akiwa na juma wakishuka kwenye gari huku waneshikana mikono wakiingia ndani niliwaisha gari nikalipaki nje ya geti ili wasijue kama nimerudi, "mbona umepaki hapa? "Nisubili ndani ya gari nakuja, "

"poa,"

Niliwaza *ina maana zahura amefanya haya akijuwa nitachelewa kurudi kama kawaida? Sasa leo imekula kwake*

Itaendeleaaa.




Endeleaa....

Nilitoka nikazunguuka nyuma ili shomy asinione kama naenda nyumbani nilipofika getini nilifungua mlango mdogo nikaingia ndani ya geti nikanyata mpaka mlango wa sebuleni nikakuta umefungwa kwa nje,

Nilizunguuka dirashani nikaangalia nikaona wamekaa kwenye kiti kimoja wakiwa wanakunywa juice huku meno yote 32 yakiwa nje kwa vicheko,

Roho iliniuma ila sikuwa na jinsi nilichukua simu yangu nikawapiga picha kupitia dirishani nilisitaajabu nkaona jamaa anatoa cheni anamvisha mke wangu shingoni matukio yote niliyapiga picha, moyo ulilipuka pale nilipomuona juma anambusu shavuni mke wangu niliumia nakutoa chozi ?? japo halikuwa na wakulidhamini, *ningemuowa Nasra haya yote yasingekuwepo maana ndie alikuwa chaguo langu*

Sikuwa na jinsi nilirudi nilikotoka kwenye gari yangu, nikiwa njiani kuelekea nyumbani nilipita dukani nikachagua ka blauzi kazuri na kakiatu kazuri nikafungasha nikaenda nako kwenye gari

"Nimechelewa?. "

"Kawaida tu, "

"nimekuletea zawadi,"

"ooh!! Thx seif,"

Alitaka kufungua kuangalia kuna nini nikamwambia ?

"Utaangalizia nyumbani,"

"sawa asante sana moyo wangu umefurahi sana,"

"unafurahi zawadi yenyewe hujaiona je ikiwa mbaya?"

"kitendo cha kupewa zawadi kimenifurahisha sana,"

"sasa shomy naomba ushukie hapa maana huwezi juwa labda juma anaweza kuwepo nyumbani,"

"kwani kuna tatizo gani akiwepo? "

"Anaweza kujihisi vibaya,"

"hilo nalo neno seif japo mimi sina wasiwasi,"

"Atanifikilia vibaya mimi,"

"Basi sawa kwaheli tutaonana home,"

"Poa,"

************

Nilikuwa wa kwanza kufika nyumbani shomy kwa kuwa alikuwa kwa miguu alichelewa kidogo,

Nilipofika nyumbani nilikuta sebuleni hakuna mtu ila kwa kuwa mimi ni mpelelezi niliyefuzu FBI niliweza kusoma mchezo kuwa wametoka sebureni hawana hata dk2 kilichonijulisha ni pazia za mlangoni zilikuwa zikicheza na pia niliangalia walipokuwa wamekaa nikabaini kuwa wamenyanyuka hawana mda kwani sehem hiyo ilikuwa na joto la makalio.

Niliingia chumbani kwangu nikamkuta mke wangu akivua nguo ili kwenda kuoga nilipiga jicho shingoni nikahisi maumivu moyoni kutokana na ile cheni nikajiuliza nimuulize au nipotezee?.

"Habari yako mke wangu?"

"Nzuri vp za kazi?"

"Nzuri,"

Nilijitupa kitandani na simu yake ilikuwa kitandani mala sms ikaingia nikaishika kwa juu ya kioo ilionesha jina la juma yes atanieleza kuhusu hii sms nikapeleka mkono kwenye sehemu ya kuruhusu meseji ifunguke



Endelea.

Ile napeleka kidole kwenye batani tu akanikwapua simu,

"Umekuaje mke wangu?."

"Naona unataka kusoma sms zangu?."

"Wala nilitaka nikupokeze simu tu,"

"basi asante,"

"haya, lakini mke wangu hata nikisoma kuna ubaya gani? kuna kitu cha siri sana unachoficha nisijue "

"Sifichi chochote ila neno simu ya mkononi inabidi tulizingatie na kuliheshimu kwa kuwa sisi sote ni wasomi tuna elewa maana yake. "

"Sawa asante kwa elimu unafumbua macho leo nami nitaeneza elimu hiyo. "

Nilimuacha ili ajione yeye ni mshindi zaidi yangu,

Nilimuangalia alipokuwa anasoma ile sms uso wake ukapata tabasamu nilichoamuwa nilitoka nikaenda sebuleni nikamcheki juma yuko bize na simu nikajua yuko ana chat na mke wangu,

Na mimi nikashika simu nikaanza kuchat na mke wake.

*heloow dear?. Akajibu, *yes dear,

*vp zawadi umeifungua?. *ndio nimejipima kabisa yaani imenipendeza wewe acha tu,, *kweli?. *ndio, *uko wapi shomy?, *chumbani, *namuona jamaa anachart tu hapa sebuleni, *yuko ana chart na hawala zake kila siku yuko hivyo, *mimi mwenye mke wangu yuko kwenye wasap sijui ana chart na nani nikaona na mimi acha nichat na wewe?. *pole kwa hiyo hakupikii leo?. *sijui si unajua nyie wanawake mlivyo? *mh!!! Siyo wote bwana, *kama siyo wote wewe mbona humpikii mmeo?, *anajuwa kuwa leo sipiki, *kwanini?.

*sijisikii vizuri si unajua sisi wanawake tena tarehe hizi, *ok sawa nimekuelewa, *kwa hiyo utalala bila kula? *naona kabunda tu hapo sebuleni wakati nimemwambia nasikia njaa, *nipe dk10 narudi kwenye chat? " *sawa ,

***********

Nilikata simu nikatoka nje nikaelekea kwenye mgahawa mmoja uliopo jirani yetu.

"Nipe biriani na kuku rost, "

"sawa, "

Nilichukua msosi nikala baada ya kula nikamwambia mhudum.

"nifungie nyingine naondoka nayo"

, "sawa na yenyewe ni biriani kuku rost?"

"Ndio,"

Nilichukua nikapita dukani nikanunua pedi nikaweka kwenye mfuko nikaondoka.

Nilipofika ndani zilipita dakika tano nikamwambia Juma, "Nasikia Kama gari yako inapiga alam, "

Nilimwambia alitoka mbio mpaka nje na mimi nikapata upenyo nikakipimbia mbio mpaka chumbani kwake.

Shomy, alishituka maana hakutalajia kuniona pale, mshituko ule mpaka taulo yake ilidondoka, "seif nini tena?. "Chukua, nilimpa mfuko mimi nikachomoka ile natoka mlangoni nikakutana na juma."

Poleni kwa kuwa fupi nimekosa muda wa kuirefusha.

Like yako ndiyo inaleta mwendelezo.

Itaendelea...........



Endelea nayo.

Nilihisi nimekutana na juma kumbe ilikuwa pazia ya mlangoni mapigo ya moyo yalienda mbio, nilijuwa nimeisha,

Nilienda nikakaa kwenye sofa juma alipotoka chooni alinikuta nimekaa kwenye sofa.

"vp kaka? "

"Poa niaje?. "

"Shwari, "

Alikaa kwenye sofa akaanza kuchat hata hakuniambia Kama gari yake ilikuwa na tatizo gani, nilipoona hali hiyo nilienda chumbani nikakuta mke wangu naye ana chart, nilirudi sebuleni nikakuta jamaa yuko bize ana chart karoho kalikuwa kanauma ila nilijikaza mpaka nitakapoona mwisho wake,

Nilikaa kwenye sofa mala sms ikaingia.

*asante kwa kunijali dear, *mbona kawaida tu, *hapana seif nimependa kwa ulichofanya, "*sawa," *seif ulichonifanyia sitokuja kukisahau kamwe katika maisha yangu, "*mbona ni mambo madogo sana hayo," *kwangu ni makubwa sana umenijali kwa chakula, hadi pedi mme wangu kakaa hapo sebuleni tu, *labda ana chart na wagonjwa?, *kweli ni wagonjwa ila wa mapenzi, *vpi umekula?. *ndio nakula dear karibu, *asante endelea, *biriani ni tamu sana dear, *haijazidi chumvi?. *hapana iko sawa kabisa, *sawa kula kwanza tuta chart baadae, *seif nikwambie jambo?. *niambie shomy,

*ningependa tungekuwa tunakula wote huku tunapiga story, *mh!!! Sawa hata kesho j'mosi najua utatoka kazini mapema basi naomba uje pale air port tule chakula cha mchana pamoja,

*nitakuja kwakweli maana unanivutia seif hakika wewe ndie mme bora kwa mkeo, *hata wewe pia ni mke bora kwa anaejua ubora wako, *naona mmeo anakuja huko, *basi baadae hata biriani yangu nimeimaliza, *sawa,

Baada ya dk 3 nilimuona mke wangu naye anakuja sebuleni nilitulia simu ilikuwa pembeni.

"Mme wangu utakula nini nikupikie mayai na mkate?. "

"Nimeshiba asante,"

"Umeshiba nini?."

"Upepo,"

"upepo?."

"Ndio,"

"Mme wangu mbona hivyo,"

"sitaki maswali mengi fanya yako nitakula simu yako,"

"Utakula simu yangu kivipi?"

"Ungejua mimi ni mmeo ungefanya maandalizi mapema ya chakula uanze kupika mida hii nitakula saa ngapi?."

Wakati huo shomy alitoka chumbani akakuta marumbano yangu na mke

wangu.

"shomy: habari yako zahara?"

"Nzuri za kwako? "

"Nzuri,"

alipomaliza kusalimia alipitiliza jikoni.

"Mme wangu naomba unisamehe?."

"Naomba ufanye yako achana na mimi,"

"sawa asnte,"

aliondoka kwa hasira nikaona kuwa amebadilika angekuwa ana tii angenibembeleza.

Baada ya dk2 shomy alikuja sebureni akiwa ana haraka akaja mpaka nilipokuwa nimekaa.

"Seif chukua,"

alitoa juice ya pakiti kwenye taulo yake akanipa.

"Asante,"

alisogea pembeni akakaa kwenye sofa jingine.

"vp unaendeleaje?."

"Poa,"

sms iliingia kwenye simu yangu.

*seif tuchart,"

"poa,"

*vp juice tamu?."

*sana tena sana,,"

*sawa naenda kuoga,,"

*nije nikusugue?."

*mh!!!...."

*mh!!!!.. nini?."

**nisije kupigwa,"

*hamna wa kukupiga bana,"

*haya njoo ndio naenda hivyo,,"

*sawa tangulia,,"

*natangulia, leo naenda simu bafuni,"

*kwanini?."

*wasnipekua sms zangu,"

*kwani huzifuti?."

*nikiwa peke yangu nazipitia,"

*sawa umefika bafuni?."

*nimefika,"

*wakati unaondoka nilikuwa navutiwa kuangaliwa sebene lako,"

*seif una matatizo wewe hebu njoo,,"

*nakuja, "

Nilienda mpaka korido ya bafu nikamtumia sms kumbe mke wangu alikiwa nyuma.

*shomy fungua,"

*sawa,,,"

Kitasa kikacheza kuashilia nafunguliwa mlango.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog