Chombezo : Safari
Sehemu Ya Tatu (3)
hali waweze kutoka kwenye janga hilo, basi walipo ona PAPA wakiwafata kwa kasi, nao walizidi kutafuta njia za kuwakwepa,
lakini PAPA hao walikuwa wanavutia harufu, kuwakimbia ilikuwa kazingumu sana, na ndipo binti alipofikiria jambo, akatumia
ishala kumpatia kijana MWAIPAMBA, nae aliafiki alichokuwa akikusudia binti huyo basi, nao walianza kupanda juu, huku
wakitizama juu, kuangalia kama kuna chombo chochote, kati ya vile walivyo kuwa wakisfiri navyo, watakapo ibukia ili iwe
vyepesi kuingia ndani nakunusulika na wadudu hawa, basi walizidi kutupa macho na kuona kitu kikiwa kina enda kwa kasi kidogo
juu yao, na ndipo walipoongeza kasi ili kuwai kile walicho kuwa wamekiona nakuzani ni chombo chao, basi walipiga maji
kwakasi kuelekea juu ya uso wa bahari, na walipo karibia tu! waliona ni PAPA, basi hofu iliwatanda, wakati huo yule PAPA
ndipo alipogeuka na kuwaona binti pamoja na kijana, wakiwa kwenye mshangao, na ndipo alipo wafata kwa speed, huku akiwa
kafungua mdomo wake, kwani ulikuwa na uwezo wa kuwala wote wawili.
BERALITA pamoja na kijana MWAIPAMBA walipoona hivyo hawakuwa na ujanja na kushikana mikono na kufumba macho, wasione wavyo
tafunwa, walikuwa wameshakata tamaha kabisa, baada ya kuona kabakisha hatua chache kufika walipo na kuanza kusali,kila mtu
sala anayaijuwa yeye, Wakati wakiendelea kusali huku wamefumba macho, walishangaa kuona PAPA huyo anachelewa sana
kuwafikia, na walipo fungua macho, walishuhudia yule PAPA aikwa amerushwa juu hukuakiwa ametapakaa damu, akionyesha kukatwa
na kitu kikali sana, YOROBI alishituliwa nabinti mmoja, mle kwenye jahadhi akimwambia atazame upande ule, ile kutazama
baharini, alishangazwa na alichokiona, PAPA mmoja alirushwaa juu, na kuchanjwa chanjwa, na vitu vyenye ncha kali sana, kwani
waliona alivyo kuwa akipiga piga mkia na bawa zake, YOROBI nae kuona hivyo, akajuwa kuna hali ya hatari ina wawinda,
alichukua siraha yake na kuiweka mkao wa vita, kwani hali alioiona hapo ilikuwa ya vita tu! na kuamini binti pamoja na
kijana MWAIPAMBA hawako nao tena, katika dunia hii ya tatu, yaani wameliwa na PAPA wa baharini.
Basi vijana wote walikaa mkao wa vita, ni kwaamri ya kiongozi wao, ali waambia wawe tayari kwalolote nao waliitika, sasa
waliweza kuwaona jinsi PAPA wa baharini walivyo chachamaa, wakajikusanya sehemu ile yenye damu ya mwenzao, lakini kitu cha
hajabu, walionekana kuzidi kushambuliwa na kitu kisichoonekana, machoni kwawakina YOROBI, hapo wote waka duwaa, nakushindwa
la kufanya, hakuna alie wafikilia wakina BERALITA maana waliamini wamesha kufa......... duh! wacha kwanza tuishie hapa mpaka
baadae, ila ukisha soma nijulish kwa comment na like ili tuone kama wakina MWAIPAMBA walitoka na roho zao, au ilikuwaje,
jibu uta lipata hapa hapa, kwa mkali wako
NO 10: Ndipo walipoanza jitiada za kuweka sawa vifaa vyao, na kujiimalisha kwaajili ya mapambano hayo, ambayo hawa
kuyatarajia, kwani pindi walipo pita njia hiI wakati wakuja, walikuta iko safi bira buguza yoyote.
Basi nae YOROBI aliamuru vijana kukaaa tayari, na alipoamlisha kwa mara ya.mwisho vijana walianza kupambana na hao
PAPA.waliokuwa wametapakaaa kote na ndipo vijana kutupa mishare na kila siraha, ilionekana itawazuru maadui zao (PAPA).
Hawakuamini kilichokuwa kikiendelea, kwani PAPA hao walionekana kuwa kama wametumwa, pengine walihisi ndivyo sivyo, lakini
mawazo yao yote yalikuwa hapo, pindi walivyoona mapambano yamekuwa na changamoto kali, walipokuwa wakiendelea na mapambano
hayo, waliona kwa mbali watu wakiwa wana piga maji, huku wakiomba msahada, walionekana wamechoka sana, ndipo YOROBI alipo
weka macho kwenye lenzi kali, na kuwaona binti BERALITA na kijana MWAIPAMBA wakiomba msaada, basi nae aliwaonyesha wenzie
waliokuwa nao pembeni yake, na kuamuru chombo kielekee mahali walipo, nao kuona hivyo vijana waliongeza kasi, ili kuwawai
wasije kuzulika na PAPA hao, jitiada zilionekana pale walipo wakaribia, nao waiongeza kupiga maji ili kufikia chombo, binti
BERALITA alionesha juhudi kali huku akimsaidia kijana MWAIPAMBA kumkokota, kwani kwa kile kichapo alicho mpa, kilikuwa cha
huakika, kilimlegeza sana nakumfanya achoke mapema, kwakweli alikuwa mwingi wa huruma na utu binti huyo, walifika mpaka
kwenye chombo walimokuwa wenza, lakini kabla kupanda kwenye chombo hicho, waligeuka wote wawili na kuutazama msitu wa PAPA waliokuwa wakiwakizidi kuangamizwa na kitu kisichoonekana, ndipo
binti BERALITA alipo toa pumzi ndefu kama ameshusha mzigo mzito, alitazama tena walipotoka na kuto amini kilicho tokea huku
wakiwa salama, tena bila hata majeraha mengi, sana maana aliye umia sana, alikuwa ni kijana MWAIPAMBA.
Basi nao waliingia ndani ya chombo, huku kwa mbali, wakianza kuona kiumbe flani wakiona, kikiwasurubisha wale PAPA, kila
mmoja wao kwenye chombo, alibaki akiwa na butwaa, kwani baada ya muda mchache, PAPA wote walionekana kutulia wakielea juu ya
bahari hiyo, wakiwa hawana uhai, huku wakiona maji yakiendelea kuchemka kuonyesha kuna kuvumbi bado kinaendelea, watu wote
wakatulia kusubiri kuona, kitu kitachoibukia pale, huku vjina wawili hawa BERALITA na MWAIPAMBA, wakipewa huduma ya kwanza,
watu hawawakiwa wame kodoa macho yao, waliona na kitu cha hajabu kwenye maji, kila mmoja alistuka... wameona nini, hapo ni
mwanzo wa safari je? huko mbele itakuwaje, endelea kuwepo hapa kwamkali wako Mbogo Edgar, ila husisahau kuni julisha ukama
ndelea kuwapa huduma huku waliendelea wakishanga, nini kinacho wamaliza wale PAPA, wote walitazama macho kuangalia nini kitatokea pale wanapoona mapambano, lakini hawakujua ni ya baina ya upande upi na upi, basi YOROBI alingoja na kukaa akionyesha umakini mkubwa, kwa hali aliyoiona ndani ya maji, huku akihisi kuna tukio litatokea, ambalo siyo lakawaida,Naam wote wakiwa wanatazama baharini mala wakaona, bahari ikiwa ime tulia na mizoga ya PAPA ikiwa ina elea juu ya uso wa bahari, kisha wakaanza kuona kiumbe kikiibuka toka ndani ya maji, kadri alivyo zidi kuibu ndivyo walivyo zidi kumwona izuri, alikuwa ni binadamu, tena ni wakike, huku akiwa ameshika siraha, mfano wa kisu kilicho jikunja mbele inaitwa mundu, (kuna makabila wanaita chikwakwa) uso wa mwana mke huyu ulionesha kuwa bado ni mwingi wa hasira, walipo mwangalia vizuri ndipo walipo gunduwa kuwa yule wanae mwona hakuwa bina damu ila ni samaki mtu, kwa kiswahili anaitwa NGUVA, kwa ENGLISH anaitwa MAILRMAID, hakuna ambae hakutambua kuwa yule ndie aliekuwa akipambana na wale PAPA, nakuwaokoa wakina BERALITA, binti Nguva alikuwa amesimama akiwatazama nakuwaonyesha ishala flani, ambazo wao hawakuzifahamu, kiukweli nnguva yule alikuwa na nia nzuri kwao na lengo lake ni kuwajulisha kuwa wasi pite kule wanako elekea, Ndipo alipoonekana akinyoosha mkono wake na kuwaonesha kuwa bado kazi ikiendelea, kwani PAPA walikuwa wengi, na alipokwisha kuwaonesha mara gafra PAPA.nao waliongezeka haraka sana, na kuwafanya vijana waliokuwa kwenye JAHAZI wakiongozwa na YOROBI, huku wakihofia sana juu ya kupoteza, uhai wao hapo kila mmoja akajipanga tayari kwa mapambano, pasipo kuogopa kufa au kuliwa na PAPA, hapo bkila mmoja akitumia silaha za jadi, wote walitumia zana zao mpaka zikawaishia. kasolo YOROBI ambae hakutumia bastola yake,
NGUVA huyo kumbe alikuwa akilinda haki za wanyonge, ambao hawakuwa na msaada baharini, sababu iliompelekea mpaka awasaidie watu awa hakutaka kuonakuona wakimwaga damu zao bila hatia yoyote, aliamua kutoa msahada huo, ukweli alifanya kazi kubwa sana, pindi alipokuwa akijitolea kuokoa umati huo.
Basi binti NGUVA alianza kupambana mno, akijitahidi kuwazuia PAPA wale wasiingie kwenye chombo, na kufanya mahafa, kwa watu waliokuwemo ndani ya chombo hicho. kweli tuna fanana nywele, lakini siyo hakili, wakati hayo yakiendelea, YOROBI alikuwa ametulia, akitafakari jambo juu ya yule Binti Nguva, uwezi amini alichokuwa akiwaza YOROBI, mawazo ya ke yalikuwa ni kumzibiti haraka sana BINTI NGUVA, akiamini kuwa atakapo maliza, kuwa angamiza wale PAPA ataamia kwao,...... unazani itakuwaje? nini kitatokea endapo YOROBI atafanya kitendo hicho cha kipuuzi, nijulishe kama umesoma
NO 12: Pindi alivyokuwa akiwaza hayo kijana YOROBI alijitoa ufahamu na kuanza kuikoki siraha yake na kuirudisha tena sehemu za kiuno chake, kiukweli wenzake hawakujuwa kama alitaka kufanya jambo ambalo halikupaswa, hata kufanya kwa mda huo, basi nae aliendelea kumkazia macho NGUVA huyo, ambae bado aliendelae kupambana na PAPA, huku matazamio yake yalikuwa ni kumpoteza kabisaaa NGUVA huyo. wakatihuo akiwa hajuwi hili wale NGUVA huyo aliendelea kusafisha bahari, huku akiwatembezea visu wale PAPA, basi alijitaidi sana kufanya hivyo huku malengo yake ni yake ni kuokoa jahazi la watu hao, nakuwaelekeza njia yakupita, kwani hakupenda kuona damu ya mtu ikimwagika maeneo hayo, alipo maliza na aligeuka kwenye jahazi walilokuwemo binti pamoja na kijana YOROBI, huku akitaka kuwaelekez njia yakupita, na kuwatakia safari njema.kwani kazi ilikuwa imekwisha aliyokuwa akiifanya, kuangamiza wote waliokuwemo eneo la bahari hiyo. PAPA wote walipotea kwa kichapo alicho wapa NGUVA huyo huku wengine wakikimbilia mbali, ili wasije kulika kwa kitu chochote, nao walitimkia mbali sana.
Ndipo kijana YOROBI kuona nguva akiwatazama, uoga ukamshika akijuwa kuwa zamu yao imewadia, hakutaka hata kupoteza mda, nae alitoa mguu wa kuku (bastora) nakuielekeza alipo binti NGUVA, ile kuona viele binti BERALITA, kitendo cha YOROBI kumuoneshea NGUVA huyo aliye angaikia uhai wao walipokuwa ndani ya maji, basi alitoka speed mahari alipokuwepo na kumfata alipokuwepo kijana YOROBI, kuzuia kitendo hicho, lakini mbio zake hazikuzuia kile alicho kusudia YOROBI, kwani alipokuwa akikimbia binti huyo na alipofika tu! alikuta kaisha fyatua risasi, ambayo ilienda moja kwa moja mpaka kwenye bega la NGUVA huyo, huku nae NGUVA alishangaa sana kwa kile kitendo alichofanya kijana YOROBI, kiukweli hakikumpendeza, alishikwa na gasira kali sana, akajiuliza "nawafanyia haya yote kwaajili yao, bado wana nitendea haya"
Basi binti BERALITA alipoona hivyo, alimsukuma kijana YOROBI pembeni na kumtazama sana NGUVA, kama ame dhurika kiasi gani, alimwona akipiga kelele kuashiria risasi ile imempata barabara. Binti BERARITA alimlaumu sana kijana YOROBI, kwa kitendo hicho huku kijana YOROBI, akijiona kafanya jambo la kishujaha, ndipo alipokaa chini akimsikiliza binti BERALITA akifoka sana juu ya tukio, yeye hakumjari zaidi aliwaimiza vijana wake wazidi ku piga makasia nakuinuwa tanga ili jahazi liongeze mwendo, haya sasa ni atuwa gani atachukuwa Binti Nguva? isome kisha nijulishe ili nikujuze kuamuzi alio chukuwa Binti
NO 13 : Vijana nao walifanya kile alicho sema kiongozi wao YOROBI, kwa kuchochea chombo kile na kuanza safari, huku binti BERALITA akimsihi YOROBI japo amwonyeshe yule binti NGUVA aliye
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment