Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

PENZI LA BINTI NGUVA (2) - 1

    

IMEANDIKWA NA: EDGAR MBOGO

*******************************************************

Chombezo :  Penzi La Binti Nguva (2) 

Sehemu Ya Kwanza (1)



Aya mdau ule wakati ulio kuwa una usubiri kwa hamu ndio ume wadia, katika utangulizi tume mwona jinsi binti matata, Fadhira

binti nguva alivyo hatari kwa vijana wadoezi wa kitumbua chake, ebu basi tuungane na mimi msimulizi wako Mbogo Edgar katika

kisa hiki kingine tena cha kusisimua, mkasa unaazia siku moja jioni mida ya saa kumi na moja jioni, ni mwezi mmoja tu! toka

Fadhira alipo mfanyia kitu mbaya Kijana Kanyika, huku kijijini kila mmoja akiongea lakwake, juu ya kupotea kwa kijana huyu,

ambae sifa yake ya ubakaji ilijulikana sana pale kijijini, wapo waliosema Kanyika amemia kijiji cha pili yaani mandepwende,

wapo waliosema ameenda mjini kutafuta maisha, wengine walisema ameenda polini kupasua mbao, kiukweli kijijini pale ofu ya

ubakaji ilipungua maana wakina mama walishindwa atakuwaachia watoto wadogo wakike wacheze wenyewe, wakiofia Kanyika asije

akawapitia, mida hii ya jioni binti Fadhira alionekana akikatiza kwenye mitaa ya kijiji cha Matimila akilejea njia ambayo

siku zote utumia wakati wakuja, kwamaana hiyo ni kama alikuwa anarudi kwao, ambako vijana wengi walitamani kupajuwa ili

waweze kumpata liulahisi kwa gia ya kuoa, Fadhira akiwa na ungo wake ulio jaandizi kichwani na kisu chake kikali cha mkunjo

(chikwakwa) mkononi alitembea taratibu akikatiza eneo lililo changamka sana la kijiji hiki, ambalo lilitumika kama soko, kwa

walio muona walizani kuwa binti huyu anatembea kwa madaa, akifanya makusudi kutikisa kamsambwanda kake ka wastani, maana

ukimwona anavyotenbea unge tamani asisogee, yani afanye kama wanavyo fanya askari wanapoambwa chapa mguu, watu walimtazama

kwa macho ya usuda huku vijana wachache wakikosa uvumilivu na kumchokoza "dada ume jaliwa" lakini yeye akuwajari zaidi

alitembea taratibu kuelekea nje ya mji, usawa wa mto matimila, Fadhira binti Nguva alitembea huku akiwaza jinsi alivyo

chelewa, maana uwa anapenda sana kurudi mapema kuogopa binadamu wasije kumdhuru, asa baada ya tukio la sikuile kuviziwa na

Kanyika, japo kwa wanao mfahamu binti huyu angeweza ata kukiangamiza kijiji kizima kwa mkono wake, lakini hakutaaka

kuendelea kuwa umiza binadamu, nahii ni kutokana na kuanza kumpenda kijana mmoja ambae atajina lake bado alikuwa

ajalifahamu, licha yakuwa aliwai kumwona malambili mfurulizo, siku nyingi zilizo pita , lakini bado aliendelea kumkumbuka

kijana huyu, japo ajamwona mda mrefu sasa lakini sura yake ilimjia usoni, akakumbuka siku ya kwanza kumwona, yule kijana

alikuwa anakuja mbele yake akionekana mwenye mawazo mengi sana kichwani, yeye Fadhira alikuwa amebeba ndizi zake na mkononi

ame beba kisu chake kama kawaida, kiukweli alitokea kuvutiwa na kijana yule, ambae alionekana kuwa ni mtulivu sana, lakini

wakati wana pishana kwa bahati mbaya waka pigana kikumbo cha vibega, na kisu cha fadhira kikadondoka, "samahani sana dada

yangu, samahani sijuwi mawazo yangu yalikuwa wapi, yani sikukuona kabisa" alisema yule kijana huku akiinama na kuokota kile

kisu mkunjo, na kumkabidhi fadhira mkononi, wakati anamkabidhi ndipo fadhira aka mwona yule kijana akimtazama usoni, na

kumshangaa kwa uzuri wake alionao, haya mdau inaonyesha Binti Nguva amedata kwa kijana binadamu, itakuwaje? minaona nikupe offer mdau, chakufanya usizime data nakuletea sehemu ya pili baada ya kuona like na comment zakutosha, kwenye hii sehemu ya kwanza si

unajuwa vitu vya weekend, pia usikose sehemu




(soma kwanza sehemu ya kwanza)

wakati wana pishana kwa bahati mbaya waka pigana kikumbo cha vibega, na kisu cha fadhira kikadondoka, "samahani sana dada yangu, samahani sijuwi mawazo yangu yalikuwa wapi, yani sikukuona kabisa" alisema yule kijana huku akiinama na kuokota kile kisu mkunjo, na kumkabidhi fadhira mkononi, wakati anamkabidhi ndipo fadhira aka mwona yule kijana akimtazama usoni, na kumshangaa kwa uzuri wake alionao, ndiyo Fadhira alijijuwa kuwa yeye mzuri, kwa mshangao ule fadhira alitegemea kusikia akitongozwa, lakini kitu cha hajabu, yule kijana aliinuka na kuondoka zake huku Fadhira akisahau kusema asante, na mala ya pili alipishana nae akiwa na binti mmoja mdogo sana alie fanana na kijana yule aikuwa siri kuwa ni binti yake, fadira aliwaza hayo pasipo kujuwa kuwa anaye muwazia yupo nyuma yake akimfwata, wakati anawaza hayo Fadhira alikuwa amna katiza kwenye sehemu moja ya kuuzia pombe, ambayo vijana kwa wazee utumia kwa kunywa pombe, mahali hapo uwa anapitaga kwa masimango sana, asa muda kama huu wajioni, ambapo walevi wanakuwa wamejaa maali pale ndo maana uwa hapendi kuchelewaga kupita mahali pale, "karibu mrembo" aliongea jamaa moja kibonge cha mtu, ambae alikuwa ame kaa akinywa pombe huku chupa kazaa zikiwa chini yake, Fadhira akampuuza "unajiona mzuri sana we malaya, ebu ipeleke wakaikanyage huko" aliongea yule mlevi baada yakuona hajajibiwa kitu na Fadhira, ambae wao wanamuita dada muuza ndizi, kauli hiyo ilimchefua sana Fadhira, ambae alitamani amfwate yule jamaa na kumchana chana kwa kisu chake mkunjo, "huna lolote, kwanza demu mwenyewe mchafutu" yani nikama yule jamaa alikuwa ame mpania Fadhira aliendelea kushusha matusi kwenda kwa binti Nguva, nakumjaza hasira, asa kutokana na walevi wengine kucheka kwa dhaarau, lakini binti huyu alijizibiti hasira zake, nakuendelea kutembea kwa mwendo wake hule hule, ujuwe sifa ni kitu kibaya sana, kuona yule binti yupo kimya hapo yule kijana anae julikana kwa jina la kizito, aliinuka na kumfwata Fadhira ambae alisikia vishindo nya kufuatwa na yule jamaa, akakiandaa kisu chake tayari kumwaga damu ya mtu, ok! mdau unazani nini kitamtokea mlevi huyu bwana kizito?, basi





kwa binti Nguva, nakumjaza hasira, asa kutokana na walevi wengine kucheka kwa dhaarau, lakini binti huyu alijizibiti hasira

zake, nakuendelea kutembea kwa mwendo wake hule hule, ujuwe sifa ni kitu kibaya sana, kuona yule binti yupo kimya hapo yule

kijana anae julikana kwa jina la kizito, aliinuka na kumfwata Fadhira ambae alisikia vishindo nya kufuatwa na yule jamaa,

akakiandaa kisu chake tayari kumwaga damu ya mtu, "ebu simama hapa, uwezi kukatiza bulebule wakati watu tunaitaji vitu kama

hivi" aliongea yule mlevi, wenzake wakimshangilia, huku akisogeza mkono wake kwa begani kwa binti Nguva, ili kumkamata na

kumfanyia vurugu, pasipo kujuwa kunakisu kina ngoja afanye ujina wake, lakini bahati ya bwana Kizito, ilikuwa nzuri, maana

kabla haja mgusa yule binti Nguva, akastuka akidakwa mkono namtu mwingine alie tokea nyuma yake, "mwache huyo mwanake wewe"

ilisikika sauti nzito ya kiume, anabahati huyu mshenzi" alijisemea binti Nguva Fadhira, akigeuka kumtazama alieingilia ugovi

ule, naam Fadhira alikodoa macho kwakuto kuamini anacho kishuhudia, **** kumbe toka anatokea kule sokoni, alikuwa

anafwatiliwa na kijana mmoja anae julikana kwa jina la James Komba wengi walimjuwa kama mjukuu wa Komba, kutokana na wazazi

wake kuishi mjini, na yeye kulelewa na babu yake mzee Komba, tokea akiwa na miaka mitano, kijana huyu ambae alikuwa anaishi

pale kijijini nyumba moja na binti yake Rehema, siku zot alikuwa mpole na mwenye hekima kwa watu wengine, alikaa mda mrefu

sana bila mke, ni baada ya mwanamke alie kuwa nae yaani mama Rehema, kutoloka kijijini na mwanamume mwingine, ambae alikuja

pale kijijini kununua mazao, nakumwacha Rehema akiwa na mwaka mmoja tu!, kutokana na tukio ilo kijana huyu akutamani tena

mwanamke, alidumu hivyo mpaka Rehema alipotimiza miaka sita, ndipo alipo mwona kwamala ya kwanza mwanamke mmoja mrembo sana,

ambae alikuwa anajiusisha na bihashara ya kuuza ndizi, alishindwa kumsemesha mapema kwasababu hakutaka kuupa kazi ya ziada

moyo wake, pia alitoka kupigana nane kikumbo kwa bahati mbaya, akajisemea kuwa endapo atamwona tena atamwambia la moyoni,

mala ya pili alipo mwona alishindwa tena sababu alikuwa na mwanae Rehema, sasa leo wakati anatoka safari yake ya mjini

ambako alienda kupeleka bidhaa za majiko,ambayo utengeneza yeye mwenyewe, na kununua maitaji ya nymbani, ufanyahivyo kwa

sababu ya kukwepa gharama za pale kijijini, alimwona yule dada muuza ndizi, akiwa anatoka nje ya mji akishika uelekeo wa

mandepwende, njia inayo pita pembeni ya mto matimila, akaamua bola amfwate ikiwezekana amsindikize huku akitoa yake

yamoyoni,sasa wakati anaendelea kumfwata, ndipo alipo waona vijana wenzake, ambao nimahalufu sana pale kijijini kwamatendo

maovu, tena akamwona Kizito akienda kumfanyia fujo yule dada muuza ndizi, nipo alipoamua kununua ugovi, "niache bwana

unaniumiza" alilalamika Kizoto huku wenzake wakishangaa wasijuwe wamsaidiaje, kutokana na kuzidiwa na majukumu ya kitaifa

leo naomba niishie hapa ila kesho mapema sana



sababu ya kukwepa gharama za pale kijijini, alimwona yule dada muuza ndizi, akiwa anatoka nje ya mji akishika uelekeo wa

mandepwende, njia inayo pita pembeni ya mto matimila, akaamua bola amfwate ikiwezekana amsindikize huku akitoa yake

yamoyoni,sasa wakati anaendelea kumfwata, ndipo alipo waona vijana wenzake, ambao nimahalufu sana pale kijijini kwamatendo

maovu, tena akamwona Kizito akienda kumfanyia fujo yule dada muuza ndizi, nipo alipoamua kununua ugovi, "niache bwana

unaniumiza" alilalamika Kizoto huku wenzake wakishangaa wasijuwe wamsaidiaje, maana kijana Jamsi Komba alionekana mbabe sana

tena mwenye mwili wa kimazoezi, Fadhira akiwa ame duwaa kwakumwona kijana alietokea kumpenda sana, akimzibiti yule mlevi kwa

kumminya mkono wake na yule jamaa akilalamika kwa maumivu anayo yasikia, binti Nguva alitabasamu kidogo na kupotezea maana

hakutaka kuonyesha uzaifu wake, "niachie we bwege, hoya nyie njooni mnisaidie" bwana Kizito alipiga kelele za kuomba msaada,

yule binti alitembea mbele kidogo karibu na mwanzo wa shamba kubwa la midizi na kusimama, akiangaliza jinsi kijana James

Komba alivyo mminya yule mlevi, "hoya Jamesi mwachie huyo mshkaji bwana, kwanza malaya mwenye ata umjuwi" aliongea mlevi

mwingine, kauli iliyo mkela sana Fadhira binti Nguva, "kama hamnijuwi mnanichokozea nini?" aliongea kimoyo moyo binti Nguva,


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog