Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

UPEPO WA KISULISULI - 1

  

IMEANDIKWA NA: SULTAN UWEZO

*****************************************

Chombezo : Upepo Wa Kisulisuli 

Sehemu Ya: Kwanza (1)


“Kwa hiyo unataka kuniambia nini Sultan?”

“Natakiwa muda huu niondoke nikaonane na meneja wangu tuipitie hii ofa tuone kama ina maslahi

kwetu.”

“Sawa utakwenda tu, muda huu subiri msosi kwanza unaandaliwa.”

“Chakula nakula muda wowote niutakao hapa Mimi ni kwangu, kwa leo acha niwahi.”

“Mmhh haya bwana umeamua usile pishi la Shemeji yako, Sweetieee.” Aliita

“Bee hon

Ey.”

“Mgeni anaenda huku.”

“Baby mwambie tunaandaa Chakulaaa!”

“Ana haraka kuna sehemu kaitwa eti.”

“Shem chakula tupike.”

“Siku nyingine nitakula.” Yaani hata kutaja neno Shemeji mdomo ulikuwa mzito hebu fikiria

nilivyoshambuliwa vile halafu nikae nao mezani kula chakula? Hasa hasa huyo anayeitwa Mooren

kwangu ni kama mafia fulani hivi. Nilibeba kibegi changu na kutoka nje, Johnson naye alitoka na

kuchukua gari yake na kunisindikiza mjini.

“Lakini janja hujafanya poa kuondoka wakati chakula kinaandaliwa.”“Johnson hebu tuziache hizi stori sababu hata nikisema niendelee kufafanua jambo hili huwezi nielewa

ila kuna muda utanielewa tu.”

“Kivipi?”

“Baada ya hili dili kukaa Sawa.”

Nilimjibu kwa kumkwepa lakini mimi nilikuwa namaanisha wale walio kwake ndiyo sababu ya Mimi

kuondoka kwake ila sikutaka kumueleza chochote mpaka pale ambapo wao watakapomweleza mkasa

ule uliotokea kwenye daladala. Tulifika mjini nikaagana naye na kushuka zangu na kuelekea kona moja

hivi kutuliza akili kwa kuangalia sinema then baada ya hapo nielekee nyumbani.

Nikiwa nazama zangu ndani ya jumba hili la SINEMA mara mlio wa kuashiria ujumbe mfupi kuingia

ukalia. Niliitoa simu yangu mfukoni na kufungua na kuangalia nani kanitumia ujumbe, niliufungua lakini

ni ujumbe ambao ulitumwa bila jina na ulisomeka hivi ;-

“MAMBO SULTAN, SASA MBO…..” Mara simu ilizima kabla sijamaliza kuusoma ujumbe huo ambao

mtumaji sikumtambua kutokana na kuingia bila jina.

Kitendo cha simu kuzima kiliniudhi sana kwamba kwanini haikuzima kabla sijaanza kuisoma meseji ile.

Lakini wazo jingine likaniijia kwamba niufungue mfuniko wa simu ili niicheki betri kama ina tatizo

kwanini haitunzi moto. Niliifungua na baada ya kuiangalia nikabaini kuwa betri ile imeanza kuvimba.

“Shiit!” Nilijisemea mwenyewe.

Hapo hapo safari ya kuingia kusinemeka ikafa pale pale nikaufunga mfuniko ule wa simu na kushika njia

kuelekea dukani. Niliingia duka moja hivi ambalo halikuwa mbali sana na pale nilipokuwa nikaingia na

kukuta msongamano wa wateja na nikaunga wenyewe wanasema tela. Nikaifuata meza moja hivi na

kumkuta mhudumu mmojawapo wa wale wa mle dukani.

“Mambo Anti.”

“Poa, karibu nikuhudumie.”“Asante, unaweza ukawa na betri ya hii simu.” Nikaitoa mfukoni na kumuonesha.

“Hii simu ni aina gani?” Aliuliza yule mhudumu.

“Inaitwa TSD old model.”

“Mbona sijawahi iiona simu ya aina hii?”

“Ni toleo ambalo halikudumu sana sokoni hivyo wamiliki tuko wachache.”

“Mhh!” Aliguna.

“Kwa hiyo siwezi kupata hiyo betri?” Nilimuuliza.

“Dada eti tuna betri za simu kama hii?” Alimuuliza bosi wake.

“Ni aina gani ya simu hiyo?”

Ni TSD old model.

“Mhh, hata new model hatuna hapa.”

“Kaka yangu si umesikia mwenyewe?”

“Nimesikia.”

“Haaa jamani Sultan Uwezo huyoo mambo!” Alitokea dada mmoja na kunichangamkia pale.

“Poa, kwema dada yangu?” Na mimi nilimchangamkia japo sikumfahamu.“Naitwa Shadya ni msomaji mkubwa wa stori zako na huwa sikubali kupitwa na kila sehemu.”

Alijitambulisha.

“Aisee, nafurahi sana kukutana na shabiki wangu kama wewe.”

“Na mimi pia Sultan.”

Aliniomba tupige picha ya kumbukumbu maana ni kama hakutarajia kukutana na Mimi pale dukani,

tulipiga za kutosha na mrembo Shadya.

“Vipi ulikuja kununua jiko jingine la kutupikia vigongo vya moto ee!” Aliuliza Shadya.

“Hapana, nilikuja kununua betri ya kisimu changu lakini nimekosa.”

“Ni simu gani hiyo ambayo unakosa betri yake?”

“Ni TSD, hii hapa!” Nikamuonesha.

“Sultan unaanzaje kumiliki simu ambayo spea zake hazipatikani?”

“Sikujua kama hakuna spea zake eti.”

“Ok, niandikie namba yako hapa.” Alinikabidhi simu yake.

Niliipokea na kumuandikia namba yangu kisha nikamuaga. Wakati natoka nikaitwa na yule msimamizi

wa lile duka.

“We kaka uliyekuwa unaulizia betri!”Niligeuka kumuangalia aliyeniita. Nikakutana na ishara ya mkono kunitaka niende pale alipo. Nilimfuata

pale mezani kumsikiliza alichoniitia.

“Chukua business kadi yangu tutawasiliana inawezekana tukaulizia kule tunakochukua mzigo na tukaleta

na wewe acha yako .” Alifafanua.

“Ok..!” Niliichukua na kumuachia yangu na kwa kuwa sikuwa na business card ilibidi nimuandikie.

Kisha niliagana naye na kutoka zangu kuelekea kituo cha daladala. Baada ya dakika kadhaa nikawa

nyumbani na moja kwa moja nikaitoa ile simu na kuiweka kwenye umeme huku nikiwa nina hamu ya

kutaka kuimalizia ile meseji. Nilichukua ndoo ya maji na kuelekea bafuni kupata maji ili kutoa uchovu.

Nilimaliza na kurejea chumbani kwangu nikafanya haraka kujikausha na kwa kuwa kulikuwa na kijoto

kwa mbali sikutaka kupaka mafuta nilibadili nguo na kuifuata laptop yangu na kuiwasha. Iliwaka na moja

kwa moja nikafungua Facebook na kupitia yaliyojiri lakini macho yangu yakaganda kwenye ukurasa wa

mrembo ambaye Facebook anajiita “katoto” maana nilikutana na picha moja ambayo tulipiga na Shadya

pale dukani huku Kukiwa na maneno yaliyosomeka “LEO ILIKUWA SIKU NZURI KWANGU KUKUTANA NA

HUYU KIUMBE.” Nilicheka sana baada ya kuifuatilia profile yake Katoto na kubaini ndiye Shadya. Na

ikabidi nipitie comments za wadau pale chini.

Kiboko yako : Jamani mwambie na Mimi nataka picha naye.

Konki : Sultan umemuacha salama huyo mshenzi.

Katoto :Halafu wewe Konki nani mshenzi.

Kitoyo : Bora hukukutana na mimi ungejuta wewe.

Kiboko yao :Hovyooo Kitoyo huna chochote.

Basi nilizisoma zile comments zilikuwa ni nyingi kwa kweli hakika nilifurahi sana kuona kuwa mashabiki

zangu wako pamoja nami muda wote. Niliachana na Facebook na kuifuata simu yangu ambayo kwa

muda huo ilikuwa tayari imeshiba moto kidogo. Nikaiwasha ili nione kilichomo. Ilipowaka tu.??????


 Ilipowaka tu sms iliingia nyingine "HI UWEZO! NAHITAJI KUKUTANA NA WEWE UKIWA NA MUDA." sms hii nayo haikuwa na jina la mtumaji nikaiiangalia ile namba kisha nikaitoa ile kadi niliyopewa na yule mwenye duka na kufananisha na kugundua ni yeye. Nikaijibu ile meseji na kisha nikaifungua ile ya mwanzo nikaimalizia "....... MBONA ULIONDOKA BILA KULA CHAKULA?" By Mooren.

Aagh nikaipotezea ile meseji ya Mooren lakini ghafla ikaingia nyingine.

"NAOMBA NISAMEHE KWA AMBACHO KILITOKEA KWENYE DALADALA NAJUA UMECHUKIA NA NDIYO MAANA HUJIBU SMS ZANGU." Mooren akiendelea kulilia msamaha. Nikiwa nafikiria nimjibu nini huyu kiumbe Mara mlango ukafunguliwa na macho yangu kodo kwa huyu aliyeingia........




Niliamka asubuhi na mapema nikachukua mswaki wangu na maji yangu nikatoka nje kuswaki, kubwa ilikuwa ni maandalizi ya kukutana na Mooren mapema ili kwenye mishale ya alasiri hivi nikakutane na yule dada wa duka. Nikiwa naendelea kuswaki mara kaja mjumbe wa mtaa.

"Bora nimekukuta mwanangu!"

"Karibu mama!"

"Asante sana, mama Mwamvua yupo?"

"Bila shaka yupo, nikamuamshe?"

"Hapana, wewe utamfikishia ujumbe wangu."

"Ndiyo nakusikiliza mama yangu."

"Leo ni jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya usafi hivyo utamwambia kuwa mnatakiwa kufanya usafi wa eneo lenu, Sawa mwanangu!"

 "Sawa mama."

Nikawaza sijui nimuulize mimi nahusika vipi ilhali ni mpangaji tu lakini nikaona niachane naye niendelee na yangu. Baada ya kuswaki nikaona kilichobaki nioge fasta kabla mama Mwamvua hajaamka nisepe zangu maana dalili za dili zangu kubaunsi nilianza kuziona. Niliingia ndani na kuchukua maji ili nioge haraka lakini kabla sijatoka aliingia ndani bila hodi Mwamvua kama kawaida akiwa na kanga tu na mbaya zaidi alipoingia aliufunga mlango na funguo akaitoa, moja kwa akaongoza mpaka kitandani kwangu na kujitupa.

"Mwamvua hivi mzima kweli wewe?" Nilimuuliza

"Kwani unanionaje?"

"Nahisi una Jini Mahaba wewe!"

"Ni kweli haujakosea na si moja ninayo mengi tu. Una swali jingine labda." Alijibu huku akitoa kanga yake na kuitupa chini na kubaki kama alivyozaliwa.

"Wazazi wako wana hasara."

"Inawezekana, ila kilichonileta leo hapa kitandani kwako ni kimoja tu Sultan."

"Acha ngonjera zako nipe funguo nikaoge mimi."

"Njoo uchukue hii hapa." akiwa kaishikilia mkononi.

"Nilimfuata pale kitandani ili niichukue funguo."  Ebwana ee nilifanya kosa kubwa sana kumsogelea Mwamvua Kwani badala ya kuchukua funguo, alinivuta na kujikuta uso kwa sura na Mwamvua nikiwa bado namtazama huyu bibie mwenye pepo alinishika shingoni na kunivuta zaidi kwake, nilishangaa tu kuna kitu kinanitekenya sikioni mwangu huku ikiambatana na mhemo mkali kama wa panya anayepuliza baada ya kukung'ata.

Mhhh Mwamvua aliyokuwa akiyafanya kwangu wala hayaendani na umri wake.

Akaona haitoshi si akanipiga kabali ya miguu nikawa sina jinsi, hata watangulizi wetu walinena mtoto akililia wembe mpe. Niliamua kujibu mashambulizi kwa kasi niliivamia shingo yake na kuanza kuifanyia mambo wee Mwamvua aliruka kule nikagundua jini lake limekaa shingoni nilimsogeza tena lakini yeye akahamia kulicheki chimbio kama lina Uwezo wa kuchimba shimo vizuri, alilikagua na kuanza kulisafisha kwa ulimi wake. Nilisahau kila kitu nilichokuwa nimekipanga na kwa kuwa alikuwa amegeuka akiulekeza mpododo wake kichwani kwangu nikaona isiwe shida nikaanza kupiga deki kwa staili ya aina yake iliyopelekea afyatue shuti lake lililokuwa na spidi kali nikaona nitakaua Kamwamvua hivyo nikakaweka 'mbuzi kagoma' vurugu zote za Mwamvua ziliisha kwa mishuti niliyokuwa namsukumizia dakika chache tu alikuwa pembeni hajitambui. Nilitoka zangu kuoga niliporudi nilimkuta ndo anajifunga kanga yake.

"Sultan wewe hatari."

"Kwanini?"

"Si kwa dozi yako iliyonifanya nikate moto ghafla."

"Si ndo ulitaka hivyo."

"Lakini siyo kwamba umeshinda nilikuacha niusome mchezo wako na hivyo usiku najibu mashambulizi na ndo utanijua vizuri Mwamvua mie."

"Hivi Mwamvua unanitakia mema hapa kwenu?"

"Kuhusu nini?"

"Si ni mambo hivi haufikirii siku nikikutwa nini kitatokea?"

"Acha uoga wewe Mimi huwa sikurupuki tu, mama kaenda kijijini kwa bibi toka jana jioni hivyo kwa siku hizo ambazo hatakuwepo nichakaze utakavyo."

"Na hao wakina Mangi huko mtaani itakuwaje?"

"Kwa hiyo ile siku nilivyokwambia vile Kuhusu Mangi wa dukani uliniamini ile ilikuwa gia ili usinidharau kuwa mimi mdogo."

"Nenda bwana nataka kutoka mimi na mjumbe alikuja kasema mfanye usafi."

"Sasa si tufanye wote bwana." Aliongea hayo akinifuata nikajua huyu anataka kunizoea nikamuwahi na kumshika mkono na kumtoa nje.

"Kwa hiyo unanifukuza?"

"Ulichokitaka si umekipata tayari?"

"Sijatosheka bado, wanasema mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na kushoto na wewe umenipiga kulia nataka nikugeuzie na kulia."

Duu sikuamini kile kilichozungumzwa na Mwamvua kwani bado binti mdogo sana lakini tayari alishapita kwenye Barbara ya njia mbili na sikumjibu kitu nikabana mlango na kuondoka zangu.

" Mbona unaondoka sasa au hujanisikia? "

" Nikirudi nitakupa kila unachokihitaji mtoto."

"Hayo ndiyo maneno Sultan wangu mwenye Uwezo wake." Alijibu hivyo aliingia ndani akanipa nafasi na mimi kuondoka zangu.

Nilitembea haraka kuelekea stendi ya daladala tayari kwenda kukutana na Mooren ambaye muda huo alikuwa amenitext kuwa nitamkuta AFRICAN PEAK HOTEL. Lakini nikawa bado nafikiria vituko vya Mwamvua pale nyumbani na suluhisho nililolipata ni kuhama pale uswahilini bila shaka itakuwa salama yangu maana tofauti na hapo Mwamvua atanifikisha sehemu ambayo sikuwahi ifikiria maishani mwangu.

"Naomba nikimbize AFRICAN PEAK HOTEL mara moja."

"Buku mbili tu kaka."

"Nitakupa buku jero."

"Ongeza kaka mafuta yamepanda bei na sehemu yenyewe ni mbali."

"Haya basi nitajazia niwahishe."

Niliona isiwe tatizo kwani mimi nilikuwa na haraka zangu hivyo kwa muda huo sikuhitaji kipingamizi chochote na ndiyo maana nilichukua bodaboda ili nitumie muda mfupi.

Tuliwasili nikampa chake dereva yule nikazama zangu ndani, nikatoa simu na kumpigia Mooren.

"Pande zipi?"

"Umefika?"

"Yap."

"Okey kama uko hapo kwenye lango la kuingilia angalia kulia kwako kuna miamvuli mingi ufuate wa Bluu."

Niligeuka na kuiona hiyo miamvuli nikachanganya miguu kuelekea upande ule, kumbe yeye alikuwa tayari kaniona. Akanyosha mkono juu kutoa ishara ya kuniita.

Niliongoza mpaka pale alipokuwa ameketi.

" Hi, " Alinifuata na kunikumbatia.

" Hi too." Nilimjibu baada ya kujitoa na kuniashiria nikae.

"Sultan Uwezo."

"Naam."

"Tafadhali karibuni niwahudumie." Mhudumu wa pale alikatisha mazungumzo yetu.

Tulitazamana usoni na Mooren kisha nikamwambia aagize chochote.

"Unanipa nafasi ya kuchagua?"

"Ndiyo chagua."

"Sawa, Tafadhali tuletee kitimoto nusu kilo na ndizi mbili."

"Ok Sawa."

"Lakini pia mletee naye juisi kama hii ya parachichi."

"Asante kwa kunichagulia."

"Mimi ndiyo nikushukuru wewe Sultan."

"Kivipi."

"Unajua vizuri yale ambayo yalitokea siku kadhaa nyuma."

"Inawezekana ilikuwa njia ya Mimi na wewe kukutana."

Tulicheka na kugonga kwani kama ilivyotokea siku ile kwa mitusi ya Mooren na kila aina ya dharau ambayo alinifanyia

kwa mtu mwingine nafikiri hata salamu ingekuwa ndoto kila mmoja njia yake lakini kwetu imekuwa tofauti baada ya yote hayo leo tumekutana. 

"Mooren wewe mbabe!"

"Hebu tuachane na hizo mambo sitaki nikumbuke maana zilininyima raha na kila wakati nilikuwa nikikumbuka tu machozi yalinitoka sana."

(akifuta machozi)

"Mooren yote yamepita tugange ya mbele sasa."

"Ni kweli lakini sijui kwani nilifanya vile kwa mtu ambaye pamoja na maneno yangu mabovu lakini hakuacha kuomba msamaha." (aliendelea kulia)

Nikaona nimuache alie kwanza mpaka uchungu utakao ndani kabisa uishe ndipo stori ziendelee.

"Karibuni." Mhudumu alitukaribisha Meza ilikuwa imesheheni.

"Asante kaka."

Niliinuka na kumfuata Mooren nikatoa kitambaa changu na kumfuta machozi yaliyokuwa yakiendelea kuloanisha mashavu yake.

"Mooren."

"Abee."

"Chakula kiko mbele yetu."

"Asante."

"Sultan! Umenisamehe kweli?"

"Kwa lipi Mooren, wewe ndiyo ulitakiwa kunisamehe mimi kwa tendo ambalo nililifanya."

"Jibu kwanza, Umenisamehe?"

"Ndi..........."

"Ndiyooooo." 

Kabla sijamalizia neno langu mara Johnson alidakia kutoka nyuma yangu akiwa na mrembo wake. Kumbe walikuja wote na walikuwa mwamvuli mwingine ambao sikuweza kuwatambua si unajua tena eneo lenye watu wengi.


Yaani sikuamini macho yangu baada ya kubaini kuwa Johnson na Mpenzi wake Evetha walikuwa pale hotelini ila walikaa mbali kidogo na sisi. Nilimtazama Mooren kwa jicho la swali lakini naye alinyanyua mabega na mikono kuonesha hajui chochote.

"Mpaka ujiulizeeee mwenyeeewe wakati jibu ni jepesi tu NDIYOO NIMEKUSAMEHE'" Akiwa kabana pua.

Ilibidi wote tuachie cheko la pamoja.

"Mooren mbona uliniambia uko peke yako?"

"Ulitaka nifichue siri za jeshi!"

"Sultan huwezi amini toka ile siku umetoka pale maskani tulikuwa na kazi ya kumbembeleza mtu hapa." Johnson alieleza. 

"Mmhh shemeji, mtu gani si useme tu kuwa ni mimi! Japo na chumvi kidogo imezidi."

"Sinaga kinyongo na mtu mimi Johnson unanifahamu vizuri." Nilijimwambafai mwenyewe.

"True boy!" Johnson alijazia.

"Jamani na mimi nina mengi ya kuongea na 'the man himself' Sultan but tule kwanza maana naona minyoo inabishana tumboni."

Evetha aliongea yake na yeye. 

"Hata mimi bado sijamalizana naye." Mooren alitia uzito.

"Mhudumu mara moja!" Johnson alimwita Mhudumu.

"Abee kaka!" Sauti ya kimwana iligonga masikioni mwa Johnson akajikuta anamtolea macho kuanzia kichwani na kuweka kituo kichuguuni.

"Muone ulivyotoa macho mwanaume wewe huoni hata aibu!" Kiwivu kilimpata Evetha.

"Aagh baby, kwanini umefika huko? Nilikuwa namfananisha na dada mmoja hivi."

"Huna lolote unajishaua tu shemeji umedakwa kweupeee!" Mooren aliongeza hasira za Evetha.

"Dada naomba uende tu, na hapa hakiliki kitu na tuondokeni." Evetha aliwasha moto.

Mimi nilibaki nawashangaa tu hawa watu maana ni dakika chache tu tulikuwa happy na sasa ndani ya hotel ya AFRICAN PEAK HOTEL upepo ulibadili mvumo.

"Mbona mmeganda au sijaeleweka nirudie." Evetha aliuliza tena.

"Baby ndo nini sasa unafanya hapa? Rafiki yako ndo kwanza kaja kumalizana na ma' boy Sul na hawajafikia muafaka na wewe mwenyewe ni shahidi sasa tukiondoka huoni tutakuwa tumewakatili." Johnson aliona amwage mashairi.

"Nimesema tuondokeni na kama hamtaki semeni niwaache peke yenu." Aliendelea kupigilia msumari kuonesha kuwa hatanii katika hili.

"Griii Griii griiiiiiiiii griiiiiii"

Mara kisimu changu kiliita. Nilicheki mpigaji ni nani? Nikaona alama ya doti nikagundua huyo si mwingine ni dada wa duka maana ndivyo nilivyomsevu. Nikawaomba samahani kidogo nikawaacha na kusogea pembeni.

"Habari." Nilimsabahi.

"Nambie mkali wa simulizi?"

Alitania.

"Sina neno dada yangu pole na majukumu!"

"Asante, vipi upande wako."

"Wapi sijafanya chochote si unajua tena daftari langu la kuandikia hadithi limepata hitilafu." Nilimueleza.

"Aisee pole Sana Sultan kwa hilo ila nina imani kuna siku litakwisha hilo."

"Sijui."

"Ndiyo hivyo niamini mimi."

"Inawezekana, Mungu mkubwa."

"Wapi muda huu kijana." Aliuliza.

"Niko sehemu moja hivi nimetulia naangalia tu movie."

"Sasa ni hivi, namalizia kufunga hapa dukani si unajua leo jumamosi tunafunga saa Sita mchana hivyo jitahidi unikute hapa nakusubiri."

"Dakika sifuri nitakuwa hapo dada."

"Usiharibu ratiba yangu Uwezo?"

"Bila shaka."

Nilikata simu na kurudi pale na kukuta watu wako wima wima wananisubiri mimi. Nilifika na kumtupia swali Evetha.

"Shemeji ndo kusema hutengui msimamo wako?"

"Nimemaliza haya si matangazo ya vifo." Alijibu huku akipiga miguu yake chini na kufanya chuguu lake ambalo halijakaliwa sana na mchwa kutikisika.

"Evetha majibu gani hayo unayatoa kwa Sultan? Anakosa gani kwako?"

Badala ya kujibu alishika njia na kuondoka zake na kutuacha tunatizamana wenyewe.

"We Evetha, Evetha nisubiri." Mooren aliita huku akimkimbilia na alipofika hatua kadhaa mbele aligeuza na kurudi tena.

"Sultan msamehe bure rafiki yangu kwa alichokujibu." Aliongea na kunisogelea kisha alinikiss na kuondoka mbio.

Mwanaume mimacho hiyoo kwa Johnson naye alibetua tu midomo yake na kuondoka kuwafuata wakina Evetha. Nilimpa ishara ya kidole sikioni kwamba nitampigia.

" Oya vipi wewe twenzetu." Johnson aliniita.

"Nitakucheki mishale mishale kuna kona naingia."

"Mooren ataelewa?"

"Kwanini asielewe."

"Basi poa."

Nilitoka na kuwafuata pale nje walipokuwa wamepaki gari nikawaaga. Lakini Mooren alikuwa kajiinamia tu kitini kana kwamba kuna kitu anakifanya kumbe alikuwa analia.

"Mwamba twende zetu si unacheki Mooren hana furaha Kabisa."

"Nitamcheki hewani."

Nikaona kama wananichelewesha tu nikaondoka zangu na kuingia kwenye tax iliyokuwa nje ya Hotel hiyo. Najua watakuwa waliulizana kwanini nichukue tax wakati gari wanayo? Jibu ni jepesi tu yaani nipande kisha waning'ang'anie na kuharibu ratiba yangu, isingewezekana hata chembe.

"Wapi kaka." Dereva Tax aliuliza.

"Nipeleke mtaa wa Juakali pale kwenye duka kubwa la simu za jumla na reja reja."

"Duka la LULU PHONES AND ACCESSORIES?" Aliuliza.

"Kitu kama hicho brother sikusoma jina la duka.

Tulifika pale nilivyolicheki lile duka Lilikuwa ni lenyewe kama alivyosema dereva Taxi. Nilimlipa chake nikashuka na kuelekea upande ule.

Nilifika lakini lilikuwa tayari limefungwa, niliangaza huku na kule sikuona mtu. Nikajua tayari nimeyakoroga na mtu kaondoka.

Niliondoka pale lakini ghafla gari ndogo aina ya Braves (black) ilisimama na vioo vilishushwa na nilipoangalia ndani nilipewa ishara ya kuingia basi nilifungua mlango wa gari hiyo na kuzama ndani.

"Mbona umechelewa hivyo?"

"Si unajua tena uswazi kwetu lazima uweke mambo Sawa kabla ya kuondoka."

"OK, tunaelekea kwangu sawa."

"Wewe tu dada yangu."

"Naitwa Nancy Thompson."

"Na lile jina la LULU je?"

"LULU ni jina la marehemu mama yangu aliyefariki nikiwa nazaliwa hivyo sikubahatika kumuona hata sura yake hivyo Nikaona wacha nimuenzi kwa kulitumia kama utambulisho wa biashara zangu."

"Pole Sana dada Nancy."

"Asante bwana ndo hivyo akifuta machozi."

"Mimi nilijua ni jina lako au la mtoto wako."

"Sultan bwana acha hizo, mimi sina mtoto wala mume."

"Acha uongo sister, kwa urembo huo uwe hujaolewa?"

"Ndo hivyo kwani ajabu?"

"Shemeji hajaamua kukuweka ndani kaona mle mema ya dunia kwanza."

"Mmhh shemeji yako gani, sina bwana unajua nini?"

"Sijui."

"Kwanza jina lako halisi ni lipi?"

"Naitwa Sultan Uwezo."

"Nilijua la utani, hongera kwa hadithi nzuri unazotunga."

"Asan....! Kabla sijamalizia gari lilifungwa breki za ghafla na kisha Nancy akateremka fasta.



Alishuka haraka na kuelekea mbele sikujua kulikoni, alipofika ya gari aliinama na baada ya dakika kadhaa alirudi na kukanyaga mafuta safari ikaendelea mbele.

"Mbona ulifunga breki ghafla na kushuka?" Nilidadisi.

"Kawaida tu, kuna mlio fulani niliusikia nikahisi kuna kitu nimekanyaga."

"Umekiona ulichokikanyaga?"

"Hamna nilisikia vibaya si unajua magari haya tunaendesha masikio yako nje."

Mara gari ilisimama nje ya geti jeusi na Nancy akapiga honi, kwa tendo nikajua tumefika mwisho wa safari yetu.

Geti lilifunguliwa na gari iliingia na kwenda kupaki moja kwa moja kwenye sehemu yake ambayo ilikuwa na turubai la blue. Alishuka na Kuja kunifungulia mlango, niliteremka na yeye akalock milango ya gari na kuja upande niliokuwa mimi.

"Sultan karibu sana, hapa ndipo ninapoishi."

"Asante sana, una jumba zuri sana."

"Mbona ya kawaida tu Sultan."

Alifungua mlango na kunikaribisha ndani, na mimi kwa mwendo wa ugeni niliingia ndani na kukutana na bonge la sebule ambayo ilikuwa imepambwa na picha kubwa ya Nancy. Hakika hii sebule ilikuwa imesheheni na kujitosheleza sana kwani ukiachana na picha hiyo kulikuwa na skrini kubwa aina ya LG iliyopambwa na stend holder' ya rangi nyeusi hakika ilivutia. Nancy alirudi baada ya kubadili nguo akiwa katupia kikaptura cha rangi ya kaki na kit-shirt cha rangi nyeupe ukiunganisha na rangi yake acha tu Nancy ni mrembo.

"Sultan kwenye friji kuna kila aina ya kimiminika unaweza nenda chagua kinachokufaa." Alinikaribisha akiwa na glasi ya maji mkononi.

"Asante." Nilijibu na kuinuka na kuliendea friji na kuibuka na 'melon juice' juisi ya tikiti na kuja kutulia nayo.

"Unapendelea juisi ya tikiti?"

"Naipenda sana hata lenyewe."

"Mbona lipo, ngoja nikuandalie." Aliinuka na kuifuata friza yake mwenyewe mwendo wake sasa da kikaptura kilichojichimbia kwenye mfereji wa suez kwa nyuma acha tu. Hakika Nancy alistahili kuitwa majina yote unayoyafahamu ya mwanamke mrembo, ukimuangalia chuguu lake na mwendo wake ndiyo lilikuwa linatikisika hilo kama limeniona naliangalia.

"We Casto njoo." Nancy alimwita kijana wake wa kazi za nje.

"Naam dada."

"Mbona umebana nje, hata salamu tu hakuna?"

"Nilikuwa namalizia kwanza kupanda maua kwenye garden ile mpya."

"Sawa Casto lakini kujuliana hali ndo utamaduni wetu bwana."

"Nisamehe dada nilipitiwa tu."

"Ok, siku nyingine usirudie tena."

"Sitarudia."

"Nimekusamehe, halafu Mbona matunda hujaweka humu?"

"Leo umeniotea nilipanga kwenye saa kumi hivi ndo nikanunue ukizingatia yaliyopita niliyamaliza mwenyewe."

"Shida yako maneno mengi kama muuza karanga, haya kaendelee na kazi yako ila kabla msalimu mgeni kwanza."

"Habari ya mchana kaka!"

"Salama, za majukumu?"

"Tunapambana kama hivi."

"Huyu ndiyo Sultan Uw...." Kabla Nancy hajamaliza alikatishwa na Casto.

"Usiniambie ndiyo huyu Sultan Uwezo?"

"Dada acha utani anawezaje kuwa yeye?"

"Kwanini brother, Mimi ndiyo Sultan Uwezo mtunzi wa simulizi mbalimbali kwenye Mitandao ya kijamii."

"Kama zali nimekutana na mtu ambaye nimekuwa nikisoma simulizi zake hasa moja hivi iliitwa FAKE BUSINESS hukuimalizaga kwanini?" Casto aliuliza.

"Niliachana nayo baada ya kukutana na changamoto mbalimbali za kimaisha lakini nimerudi tena."

"Casto, Casto kamalizie kazi zako bwana si nimetoka kusema hapa mtu gani hauishiwi maneno."

"Muache akate kiu yake kwangu."

"Kaka utaniandikia namba yako kwenye simu yangu hii." Aliniachia simu yake na kutoka nje.

Nancy alikuwa bize na laptop yake pale kitini sijui alikuwa akiperuzi kitu gani? Mara aliniita nisogee pale alipokuwa.

"Hivi huyu Tausi haujamtokea kweli?"

"Kwanini umeuliza hivyo?"

"Maana mtoto mashallah kajaliwa kila kitu hapa hebu mcheki na pia kila stori lazima akomenti."

"Huyo ni bonge la shabiki yangu lakini hatuna uhusiano wowote ule."

"Nilikuona siku ile pale dukani na yule msichana mara waooo."

Huwezi amini lakini ndo hivyo mshumaa ulizimwa kitendo cha kusema waoo mdomo wake una sumaku vile, nilijikuta nashambuliwa midomo yangu mhh nami sikuwa mchovu nilijibu mashambulizi pale sofani. Tulibadilishana mate mpaka basi hapo nikaona nimpandishe tempa yake nikaupeleka mkono wangu mgongoni kwake na kuanza kucheza nao staili ya nyemvua nyemvua aka washa washa acha Mbona alipagawa mtoto wa watu.

"Paaaaa.......!"

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog