Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

JIRANI TAM TAMUU - 1

  

IMEANDIKWA NA: SEIF JABU

*****************************************

Chombezo : Jirani Tam Tamuu 

Sehemu Ya: Kwanza (1)


Kawaida mjini ni mipango na kila mtu anaishi mjini kwa mahesabu yake anayoona yako sahihi,,


Nilipotimiza miaka 19 nilitamani kuoa kwa kuwa niliamini ili kupata mafanikio zaidi ni lazima niowe ila msichana niliyewazia kumuoa alikuwa ni binti mwenye elimu yake ili niweze kumpatia japo kamtaji afanye biashara au nimtaftie kazi ya kufanya,


Katika maisha yangu ya ubachela nilikuwa nilikuwa naishi na rafiki yangu anayeitwa Chande, chande alikuwa ni msomi mkubwa kwani alikuwa ni dokta katika hospital ya mhimbili na pia alikuwa ni mtumishi katika hospital ya Agakan alikuwa ni dokta pekee wa moyo Tanzania nzima kwa hiyo taifa lilimhitaji sana serikari ilimkumbatia sana kwa kumpa mshahara mzuri na malupu lupu yasiyokuwa na idadi kifupi alikuwa ni mtu mhimu sana katika idara ya afya,


Alikuwa ni mtu asieyeweza kukamatwa na polisi hata itokee amefanya kosa gani,


Katika suala langu la kuowa nilimuomba ushauri,,


**************


"Chande mimi nafikiria kuoa,"


"Unataka kuoa lini?."


"Mda wowote nikipata binti ninaye mpenda,"


"Ina maana hata mchumba huna?"


"Sina,"


"Sasa unataka kuoa jiwe au mto?"


"Nilikuwa nahitaji ushauri wako katika hili suala,"


"Ushauri wa namna gani seif?"


"Nahitaji mke msomi ili niweze kujipanua kimawazo na kipato kwa ujumla,"


"Kwa hiyo unahitaji shuga mamy la kukuhudumia."


"Siyo hivyo ninahitaji msichana msomi mwenye miaka 18-20, kwa kuwa najua naweza kumpa biashara akafanya na pia kama hawezi biashara basi naweza mtafutia kazi."


"Seif una mawazo mazuri sana ila kumpata msichana msomi siyo kwamba utakuwa umepata msichana mwenye tabia njema hilo ulitambua?."


"Nalitambua hilo suala ila nina imani nitamlekebisha,"


"Sawa kama unalifaham hilo kwa hiyo nikusaidie vp?"


"Unajua ukikaa na uwa ridi na wewe utanukia tu,"


"Una maana gani?."


"Na maana kuwa nikiwa na wewe msomi hakika nitampata msomi mzuri mwenye tabia nzuri pia."


"Seif usiwe nashaka na hilo mimi nitarikamilisha tu wewe jiandae mimi nina safari ya zanzibar kwa hiyo tutaambatana wote' kule kuna msichana nitakuonesha amehitimu chuo mwaka huu,"


"Sawa nitashukuru kwa hilo,"


************


Siku hazigandi hatimae tulianza safari ya zanzibar mimi na chande,


"Seif huyo binti anaitwa Zahara ni shombe shombe wa kialabu amehitimu udokta na anatarajia kufanya kazi katika hospital ya mhimbili,"


"Mh!!!..!!.. shombe shombe baby,"


"Unaenda kuoa kwa warabu bwana seif,"


"Mungu ajalie tu nifanikishe,"


"Utafanikisha tumuombe mungu,"


Tulingia zanzibar tukawa tumefikia kwa shangazi yake na chande.


"Seif mtoto yuko nyumba hiyo ya pili"


"Mh!!..!!.. ni geti kali?"


"Ndio baba yake ni mzito hapa zanzibar,"


"Tutaingia kwao lini?"


"Ni Sasa hv jiandae twende hakuna muda wa kupoteza."


Nilijianda vizuri sana nikavaa nguo nayojuwa inanitoa vizuri kisha nikamtaka chande twende.


"Chande twende tayari normalize"


Nilitoka na chande mpaka nyumba ya pili kwenda kujionea mtoto shombe shombe Zahara tuligonga hodi tukakalibishwa.


"Dokta chande karibu sana,"


"Asante jamani za siku nyingi?"


"Nzuri tunamshukuru mungu,"


"Naona umetuletea na mgeni karibu mgeni?."


"Asante,"


"Habari yako mgeni?."


"Nzuri vp nyie hapa nyumbani?."


"Sisi ni wazima wa afya,"


"Nashukuru kisikia hivyo,"


"Dakika mbili nakuja,"


"Sawaa,"


"Chande huyu ndiye yeye nini?."


"Tulia wewe siyo huyo huyo ni nasira ni mtoto wa nje wa huyu mzee hapa wanamfanya kama mfanyakazi,"


"Jamani ni kazuri alafu kachangamfu,"


"Umeanza ujinga wako?."


"Si ninasifia tu kizuri kisifie bwana,"


Gafla alitokea binti mrefu mwenye shepu nzuri akatoa salam.


"Asalam aleykum?."


"Waleymumsalam mzima?"


"Mimi mzima karibuni sana,"


"Asante,"


"Dokta chande za siku nyingi?"


"Nzuri ukaondoka dar es salaam bila kuniaga?."


"Ilikuwa ni gafla tusameheane,"


"Sawa huyu ni rafiki yangu anaitwa Seif anafanya kazi air port dar es salam, Seif huyo ni zahara ni rafiki ila ni kama ndugu,"


Zahara alinyanyuka akanipa mkono.


"Nashukuru kukufaham karibu sana jisikie uko nyumbani,"


"Asante na mimi pia nimefurahi kukufaham karibu dar es salaam kwetu,"


"Asante siku nikija nitakutembelea,"


"Karibu sana,"


Tuliendelea na maongezi ya hapa na pale gafla mlango ukasukumwa na alieingia hakuwa mwingine alikuwa baba na mama wa zahara.


"Asalam aleykum Benjamin?."


"Waley kumsalam Hatujambo shikamoni,"


"Marhaba, chande za miaka?"


"Nzuri baba za siku?.."


"Tunashukuru sisi ni wazima,"


Maongezi yalianza upya hatimae tukaaga na tukaondoka kurudi nyumbani kwa shangazi.


"Vp seif umemuanaje mtoto?."


"Ni mzuri ila sijapendezwa na tabia yake?."


"Kivipi tena seif?."


"Aliniboa pale alipomuita nasra, :wewe mpuuzi"


:abe dada,"


:waletee wageni juice,"


"Niko nayiandaa,"


:ina maana hakuna juice iliyotayari."


:ndio,"


:huo ujinga wako ndio nisioupenda ina maana juice wakati inaisha hukuona?."


:niliona ila kazi zilikuwa nyingi,,"


"Nitokee hapa kawaletee juice ya pakiti chukua pesa,"


"Kwa hiyo seif hilo ndilo lililokukera,"


"Ndio kwani wewe unaona ni sawa?."


"Yale ni maisha yao achana nayo wewe cha kuangalia ni mchumba tu na elimu yake kama ulivyo niambia,"


"Kwa tabia ile sijui kama ataishi na ndugu zangu kwa amani,"


"Sasa seif wewe unaowa mke kwa ajiri ya familia au kwa ajirii yako?."


"Kwa ajiri yangu na familia,"


"Seif acha utoto kwa hiyo umeghairi kuoa?."


"Sijagairi ila naona bora nimuowe Nasra,"


"Acha ujinga wewe nasra hajasoma yule kaishia form four na hana dira yoyote ya maisha,,"


"Nitamuowa hivyo hivyo kwani uwezo wa kumsomesha ninao,,"


"Poa, kwasababu hakuna anayejuwa kilichotupeleka pale andika barua nitampa mjomba na wazee wawili wataiwasilisha kwa wenye,"


"Poa tena naandika sasa hv,"


"Poa, andika."


**************


Niliandika barua na chande naye akaenda kumuweka sawa mjomba wake ili wanipelekee barua.


Baada ya masaa kadhaa mambo yalienda vizuri nikawakabidhi barua wazee na mjomba wakaipeleka,,


************

Tumekuja na ujumbe mzee Basity na ujumbe wenyewe ndio huu hapa,,


Mzee alimuita mkewe ndipo wakafungua bahasha ile ili kujua kilichomo walikutana na laki tano ikiwa nabarua ya uchumba,,


"Sawa tumeisoma tumeilewa basi ngoja tuifanyie kazi nyie njooni hapa kesho kutwa adhuhuri kuchukua majibu,,


"Sawa tuombeane heli,"


*************


Mambo yaliendelea kuwa mazuri familia ya Nasra ilitoa majibu.


"Bwana sisi tumekubali kumuoza binti yetu kwenu"


"Tunashukuru kwa majibu mazuri,"


Mahali jumla na vikolombezo vya hapa na pale walitutoza mil.5,


Nilifanya juu chini nikalipa mil.5, kesh bila kubakiza hata kumi,,

Tarehe ya harusi ilipangwa ya karibu kwa kuwa mimi nilikuwa nahitajika kurudi kazini na nilitaka kurudi nikiwa na mke.


************

Nyuma ya pazia, mama zahara na mwanae,,

"Mama: una habari nasra kaposwa?"


"Zahara: hapana,"


"Karetewa posa na harusi ni tarehe 27/7/2015,"


"Aliyeleta posa ni nani?."


"Yule rafiki yake chande,"


"Aliyekuja nae hapa siku ile?"


"Ndio,"


"Mama fanya juu chini mimi ndie niolewe na yule kijana,"


"Heee wee nitaanzia wapi nasra mwenyewe kaisha ambiwa kakubali na istoshe baba yako analifaham hili swala,"


"Weee mama wa wapi? Wambie kumbe yule kijana alichapia majina posa alikuwa ameitoa kwa ajiri ya Zahara na siyo nasra umwambie kamtuma chande,"


"Mh!!!.. ngoja sasa hv nimuone baba yako huko sebuleni nijaribu,"


"Usijaribu wewe sema bila uoga,"


"Sawa ila je siku ya harusi akikukata kuwa siyo wewe?."


"Hayo niachie mimi,"


*********************************


Mama zahara alielekekea sebureni kuongea na mume wake ili aone kama itawezekana kubadili ndoa mwanaye ndiye aolewe, ila kabla ya kuongea na mume wake kwanza waliongea na kupanga mambo mengine ya siri.


"mme naona umepumzika?."


"Ndio si unajua leo nilikuwa na kazi nyingi sana mke wangu?."


"Pole mme wangu,"


"asante mke wangu, "


"kuna taarifa zimeletwa hapa na chande,"


"taarifa gani tena mke wangu ni nzuri au mbaya?."


"Ni mbaya ila upande mwingine ni

Nzuri,"


"ni taarifa gani hizo?."


"Ni kwamba seif alichanganya majina katika barua yake, yeye alikuwa amemlenga Zahara ila akajikuta anaandika Nasira,"


"mh!!.. kwa hiyo?. "


"Kwa hiyo Zahara ndie muolewaji,"


"Nasra atazipokea vp hizi taarifa mbona ni balaa hili,"


"balaa gani itabidi akubaliane na matokeo tu,"


"mh!!. Itabidi nimpigie chande nimuombe amsihii seif,"


"amsihi nini tumeisha yaongea na Zahara amekubali na seif amepokea taalifa hizo tayari,"


"kwanini mmefanya hiv lakini bila kunishirikisha?."


"Hata ungeshirikishwa ungeamuwa nini muoaji ndiye anaechagua,"


"sawa basi yameisha muandaeni Zahara japo inaniuma,"


"kinachokuuma ni nini sasa hawo wote si wanao?."


"Ndio lakini jua kuwa Nasra tayari alianza kufundwa na taarifa zimezagaa kwa watu wa familia na marafiki,,"


"hilo siyo tatizo kama nyota yake ni ya chooni huwezi kuisafisha ikawa ya dhahabu,"


************


Taarifa zimfikia Nasra siyo siri aliumia sana kwani alijuwa kuolewa kwake atakuwa ameondokana na mateso ya hiyo familia ila imekuwa ndivyo sivyo kwake,


*nilijuwa naolewa naenda kuanza maisha yangu ila imeshindikana, ni bora nichukue maamuzi magumu maana hii ni aibu ndugu na jamaa walijuwa naolewa ila imeshindikana inanibidi niamuwe maamuzi magumu nikitoka kwa huyu kugwi sitoonekana tena pale kwenye ule mji, nimeteseka vya kutosha watu wa familia moja wananibagua kama hawanijui wamesitisha masomo yangu wananipiga kama ngoma na baguliwa mpaka kwenye vyombo chombo nacholia mimi wenye hawakitumii pedi hawaninunulii msichana mzima natumia matambala? Baba yangu anamiliki boti tatu mabasi zaidi ya mia nyumba zaidi ya hamsimi alafu nalala chini bila hata godoro kweli?*


Nasra alisikitika sana hapo aliahidi kuchukua maamuzi magumu sikujua anaenda kuchukua maamuzi gani tutajua mbele ya safari,,


*********************************


Harakati za harusi ziliendelea siku yenyewe ikazidi kusogea hatimae siku yenyewe ikafika,


"Seif siku yenyewe ndiyo hii imefika unaenda kuchukua mwali wako vipi unajisikiaje?"


"Najisikia vizuri ila vp kuhusu ile nyumba Juma kaisha ilipia?"


"Kaisha lipia na leo anapeleka vitu ndani na pia nimeongea na Amina atakusaidia kupamba kwa hiyo utafika nakulala na chombo chako,"


"mh!! Nyumba yenyewe niliyohamia siyijui wala nini kwa hiyo nitakuwa na mimi ni mgeni,"


"Acha hizo seif ile nyumba mpya ya mzee shengoma pale magomeni huijui?."


"Naijuwa mbona ile nyumba kubwa sana,,"


"ile mtakuwa wapangaji wawili ila wa pili hajapatikana yule mzee amesema wewe ndie utakaye tafta mpangaji wa pili,"


"Kwanini?."


"Anasema ukimtafta wewe yeye hatapata malalamiko yoyote,"


"kwa hiyo na kodi nitakuwa napokea mimi?. "


"Ndio kwani situmemlipa kodi ya nyumba nzima,, "kumbe ile laki tano ni ya nyumba nzima?."


"Ndio,"


Tulijadili makazi maana ilibidi mimi kuwapa kazi marafiki zangu wa dar es salaam wanitaftie nyumba ya kuishi,,


Mda ulifika pilika pilika za harusi zilikuwa zikiendelea vizuri sana na mda ulipofika tulielekea kwao na bibi harusi kuchukua mke ila kuna sehemu ilinichanganya pale shehe alipokuwa akifungisha ndoa,"


"Seif jabu uko tayari kumuoa Zahara,"


alipofika kwenye hilo jina niligeuka pembeni yangu nikamuangalia Chande ila chande naye niliona ameshangaa kusikia lile jina ila akaniambia kwa ishara kuwa niitike,"


Nilikubaliana na yote ila baada ya kumaliza nilimgeukia Chande,"


"Chande kulikoni?."


"Na mimi sielewi?."


"Ngoja tutayajua kwao huko huko,,"


Tulifika kwao na Zahara shamla shamla zilikuwa zikiendelea furaha ilikuwa imetawala na kila mtu aliyekuwepo pale alionesha jino kuashiria amefurahia kile kitendo kinachoendelea pale,


Baada ya kutulia kidogo nilipelekwa kwenye chumba alichomo bibi harusi ili kuhakikisha kama ndiye mlengwa au siyo,"


Niliingia ndani ya chumba nikamkuta mwali akiwa amekaa kitandani ila cha kushangaza alikuwa peke yake bila mpambe hata mimi nilipoingia niliambiwa niwe peke yangu ina maana nilikuwa mimi na bibi harusi tu jambo ambalo siyo utaratibu.


"Habari yako mke wangu?."

ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog