Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

BWANA MIHAMALA - 4

  

Chombezo :  Bwana Mihamala 

Sehemu Ya Nne (4)


"Mwanangu kuwa makini sana ujue sasa hivi upo karibu sana na shetani, yaani hapo lolote laweza tokea, komaa baba vinginevyo utaaribu mambo mapemaa"


"....Aaah hamna mwanangu siwezi jichanganya kwa lolote....".


Kumbe wakati wanaongea hivyo , Judy alikuwa amejibanza sehemu fulani, hakuwa ameenda chumbani moja kwa moja kama alivyoaga. Kwa hiyo mazungumzo yao aliyanasa vyema.


Katika maisha ukiwa unapigana vita bila kujua adui yako hasa ni nani basi ni ngumu sana kushinda vita hiyo. Ndicho kilichomkuta bwana Shaibu, mara kwa mara amekuwa dhaifu sana kwa Judy na hata bila yeye mwenyewe kujijua kwanini inatokea hivyo.


Ukishamjua adui yako teyari umeshashinda nusu ya vita, Judy aliposikia mazungumzo yao akaenda zake chumbani , akabadili nguo na kuvaa kigauni chake cheepesi mno ambacho kwa kule Ulaya huitwa 'Night dress' , kigauni hicho kilionesha moja kwa moja maumbile yake.


Baada ya hapo akarudi hadi ilipo main switch ya umeme akaweka off (akazima) na nyumba nzima ikazima umeme, alafu akajibanza sehemu kuwasubiri akina Shaibu watafanya nini na lengo lake kubwa alitaka Muki akalale chumbani kwake na yeye aucheze mchezo wake alioupanga usiku huo.


Akina Shaibu wakadhani Tannesco wamekata umeme wakajiamsha kwa kujimulikia na simu zao. Muki akaaga na kutoka nje kwenda kulala chumbani kwake. Mlango ukafungwa na Shaibu kisha akawa anaelekea chumbani , kabla hata hajafika akagongana na Judy ambaye alijipeleka mbele kwa Shaibu kwa makusudi.


Shaibu aliposhtuka na kumuulika tochi ya simu yake alikuwa ni Judy.


"Aaah sorry Sikukuona...."


Shaibu alijitetea na Judy yeye hata hakujibu samahani hiyo na akasema itakuwa hitilafu tu ya umeme imetokea hivyo akamwambia Shaibu wakajaribu kuwasha main switch kama itakubali.


Wakafanya hivyo, umeme ukawaka. Ulipowaka umeme ndani kukawa na mwanga ambapo sasa waliweza kuonana vyema.


Shaibu akataka kujitia ugumu wala hakumwangalia sana Judy, akamuaga na kuishia zake chumbani.


Katika maisha usiombe ukutane na mwanamke anayehitaji jambo lake litimie, atakunasa tu!


Judy akarudi zake chumbani ;akakaa kama dakika kumi hivi kisha akaenda mlangoni kwa Shaibu na kugonga wakati huo akijifanya anaongea na simu.


"Huyu hapa namwamusha , usikate simu nampa sasa hivi..."


Judy alijifanya kuna mtu anamwitaji Shaibu, Shaibu aliposikia hivyo alitoka chumbani harakaharaka akiwa na kibukta chake kidogo dogo maana alikuwa teyari yupo kitandani. Shaibu aliamini moja kwa moja ni simu kutoka kwa Mr Shamte ndo maana alikurupuka kwa haraka sana.


*Itaendelea*


Furaha ya kweli hutokana na amani ya moyo, Unaweza ukaigiza mapenzi ya uongo ila kamwe huwezi kuzificha hisia. Kila mmoja anahitaji furaha,ndio maana asilimia 80 ya matendo ya binadamu huwa ni kwa ajili ya kuikamilisha ama kuitafuta furaha yake.


Je Judy atafanikiwa lengo lake? Shaibu atajizuia kweli?


Tuendelee kuona mwisho wa haya yote itakuwaje....


Mwaandishi wa mkasa huu anaamini katika Mungu. ...Ila naomba niache swali hili kwenu wasomaji waaminio katika Mungu kama mwandishi


*"Hivi ni kweli hapa duniani kila kinachoendelea kimepangwa na Mungu na binadamu hutekeleza tu?"*



Tulipoishia.....


Shaibu na Muki wanaanza maisha mapya nyumbani kwa Judy...Judy hatulii ,anafanya kila mbinu ili amtie nguvuni Shaibu. Usiku mmoja, Shaibu anabaki na Judy huku Muki akiwa chumbani kwake na Mr Shamte akiwa hayupo.


Judy anahakikisha Shaibu hakwepi mshale wake, anamdanganya kuna simu yake , Shaibu anatoka chumbani kwake na kuja kwa Judy....


Endelea hapa....


Shaibu alivyotoka tu, alimuona Judy akiwa hana simu wala chochote mwilini mwake. Yaani mwili wake ulikuwa kama alivyozaliwa, hakuwa na nguo yeyote. Shaibu akafanya kama anasita hivi, akajikuta anauliza kwa kigugumizi.


"Si...si..simu iko wapi?"


Judy wakati huo alikuwa anamsogelea Shaibu. Shaibu akataka kurudi ndani ila Judy teyari alishamvamia Shaibu na huku akimwambia...


"Shaibu bado tu hujazijua hisia zangu kwako...? Kila ninalofanya ni kwa sababu yako...Wewe ndiye furaha yangu"


Shaibu akazidi kuingiwa na kigugumizi hata maneno yake hayakutoka vizuri.


"La...a..ki..ni akitu....ku...ta Mr Sha..."


Hata ile Mr Shamte hakuimaliza kuisema, Judy akajivuta na akamvuta na Shaibu wote wakawa wapo chumbani kwa Shaibu. Kwa wakati huo, ni mdomo tu ndio ambao Shaibu aliweza kuutumia kukataa lakini mwili wake wote ulitamalaki na ulikuwa na shauku ya kufuata maagizo ya Judy.


Siku zote mkate hata ukiwa mgumu vipi, hauwezi kushindana na chai, ukiuchonywa tu basi hulegea na kugawanyika vipande vipande. Shaibu hakuweza kujizuia tena, alifyata mkia kwa mapigo ya Judy. Chumba kikatumika kuwa uwanja wa mapambano, mapambano ambayo hayatoi damu wala kuumizwa mtu.


Shaibu na Judy walilala pamoja hadi asubuhi huku moyo wa Judy ukiwa na furaha na amani sana. Hakuwahi kupata furaha hata siku moja akiwa analala na Mr Shamte.


Judy akawaza mbali sana akatamani kama kila siku ingekuwa hivyo. Shaibu pia alifurahi lakini haikuipa nafasi kubwa furaha yake kwani Judy alikuwa mtu wa Mr Shamte na yeye alikuwa kama mwizi tu.


Siku tatu mfululizo, Mr Shamte hakulala pale kwa Judy walikuwa wanakutana kazini tu na hii ni kwa sababu bado alikuwa anatatua changamoto iliyojitokeza katika familia yake. Hivyo basi siku hizo tatu, Shaibu aliamia kabisa chumbani kwa Judy. Wakawa kama wenye nyumba vile.


Wakati haya yote yanaendelea Muki alikuwa hajui kitu. Shaibu hakutaka kumwambia Muki kwani alijua Muki hawezi kuwa upande.


Siku ya nne Mr Shamte alirudi kwa Judy na ilikuwa jumamosi siku ambayo huwa hawaendi kazini.


Wakati anarudi Muki alikuwa yupo sebuleni peke yake anachezea simu yake, wakasalimiana. Judy na Shaibu hawakuwepo.


Mr Shamte alienda moja kwa moja chumbani kwake huko nako hakumkuta Judy. Akarudi tena sebuleni na kumuuliza Muki.


Muki naye hakuwa anajua lakini mda mchache tu uliopita wametoka kunywa chai wote wakiwa hapo sebuleni. Muki kwa kuwa alijiziuka kuchezea simu ,hakuwa makini sana kuangalia wameenda wapi.


Mr Shamte akaamua kumpigia simu Judy, simu iliita palepale sebuleni kumbe aliacha kwenye sofa.


Shaibu na Judy walikuwa wapo chumbani kwa Shaibu wakiendelea kufanya mambo yao, walifanya hivyo kwani Judy alishapewa taarifa na Mr Shamte kuwa atarudi siku hiyo hivyo wakaona baadae hawatapata muda wa kufanya mambo yao. Walivyotoka sebuleni, walitoka kila mmoja kwa style yake ambayo Muki hakuweza kuielewa.


Muki na Mr Shamte

wakiwa bado wapo sebuleni, Muki akawaza mbali sana na akagundua kuna dalili za wawili hao kuwa pamoja. Mawazo ya Muki yalimpeleka moja kwa moja kuwa watakuwa wapo chumbani kwa Shaibu, maana hakukumbuka kama kuna mtu alitoka nje.


Muki akaamua kulicheza game, baadae akawa kama mtu aliyekumbuka kitu vile., akasimama huku akionesha sura ya ucheshi akasema,


".......aaah bosi nishakumbuka kitu, itakuwa wameenda sokoni maana nilimsikia Judy akisema kuwa ataenda sokoni kununua kuku..."


"Mmmh mwanamke anapenda kuku huyu...."


Mr Shamte alimjibu Muki na kisha akaenda chumbani kwake.


Muki akampigia simu Shaibu faster , Shaibu alipokea , kwa sauti ya chini sana ,Muki alisema...


"Mko wapi nyinyi, Mr Shamte kaingia hapa na yupo chumbani, asee kama mpo wote rudini haraka....."


Shaibu hata hakujibu, aliitupa simu kitandani. Wakavaa nguo zao haraka haraka ili watoke nje ya chumba.


Muki hakuwa ameikata simu yake hivyo alikuwa anasikia wakati wakinong'onezeana ....


"Judy...Shamte karudi, tutoke faster.."


Dakika moja mbele Judy na Shaibu wakaingia sebuleni, sasa hapo hapakuwa na kificho tena kwa Muki . Muki alielewa kila kinachoendelea baina yao.


Muki yeye kawaambia tu kuwa Mr Shamte amerudi na amendanganya kuwa wameenda sokoni.


"Sasa itakuwaje akiniuliza vitu nilivyonunua ...."


Judy alijikuta akiuliza huku mikono ikiwa kiunoni.


Shaibu alikuwa kama amepaniki hivi yeye alikuwa anamsisitiza tu Judy asiongee kwa sauti kubwa. Muki yeye pekee ndiye aliyekuwa mtulivu kwa wakati huo, akamwambia Judy aende chumbani kwake na akamwambie kuwa alivyotoka alisahu kubeba hela.


Wazo la Muki likapitishwa, Judy akaenda chumbani kwake haraka ambapo alimkuta Mr Shamte na tumbo lake kubwa amekaa huku ameishika boxer ambayo alikuwa anaikagua.


"......ooooh baby..."


Mr Shamte alimkaribisha Judy ambaye bado alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa. Hata kabla hawajasalimiana, Mr Shamte akasema tena....


"..hii boxer ni ya nani...?"


Huku akijichekesha na kumkaribia zaidi Mr Shamte, Judy akajitetea kuwa ile ni boxer yake kwamba huwa anavaaga akiwa amevaa nguo laini ili zisimuoneshe makalio yake. Mr Shamte akaingia kingi, akatulia.


Mr Shamte macho yake yakatua kichwani kwa Judy na kukuta nywele zake zimetimka timka kama manyoya ya tausi wa ikulu. Akauliza...


"Vipi mama nywele mbona zimekaa vibaya sana....ndo unaenda sokoni hivi kweli?"


"Aaah si unajua baby haraka haraka hiyo....ulivyonitaarifu kuwa utakuja leo ndio nikaamua nifanye haraka haraka nikuandalie chakula kizurii mme wangu....lakini hata hivyo yaani nimetoka hapa kumbe nilisahau kubeba hela bwana...."


Mr Shamte akajaa mazima kwenye ndoo ya uongo wa Judy, akamuamini .


"Sasa nipe vitu basi masuala ya sokoni achana nayo kwanza..."


Mr Shamte alisema na kuanza kumpapasa Judy. Judy alikuwa kwenye 'off mood' kabisa..hakuwa na hisia naye tena Mr Shamte. Judy akamwambia Mr Shamte waatafanya baadae.


Kwa mara ya kwanza Mr Shamte alinyimwa unyumba na Judy, hapo awali alikuwa kila akimwitaji basi hupata papo hapo. Siku hiyo Mr Shamte alishangaa ila ikabidi akubaliane naye tu.


Usiku ukafika kila mmoja akaelekea anakolala. Shaibu alianza kuingiwa na wivu alipoona Judy anaenda kulala na Mr Shamte , akawa anawaza jinsi watakavyolala na kitakachoendelea.


Judy yeye ndo hakutulia kabisa mawazo yake yalikuwa kwa Shaibu. Mr Shamte aligundua utofauti mkubwa kwa Judy maana kila alipojaribu kumpapasa , Judy hakuonesha ushirikiano wowote. Mpaka inafika asubuhi, Mr Shamte aliambulia patupu!


Mr Shamte alimwita Shaibu asubuhi wakati Judy akiwa jikoni anaanda kifungua kinywa na akamuuliza swali...


"Hivi hizi siku ambazo sijakuwepo hapa hakuna kidume aliyekuwa anakuja kuja hapa kweli?"


"Hapana bosi sijawahi kuona mtu wa hivyo.."


"Au usiku mama yenu(judy) hakuwa anatoka kweli?"


"Aaah sijawahi kumuona labda kama usiku sana wakati nimelala...."


Shaibu alijibu huku akiwa na wasiwasi mkubwa baadae akijitoa uoga akauliza kwanini anauliza hivyo. Mr Shamte akamjibu....


"Yaani kuna mambo nimeshangaa sana jana...ngoja nikuambie tu wewe kwa sababu mwanaume mwenzangu hata kama umri wako mdogo...kwanza nimekuta boxer ya kiume na mbaya zaidi jana yote sijamgusa yaani alikuwa hataki...."


Maneno ya Mr Shamte yakamtia nguvu Shaibu na kuamini kuwa Judy hakufanya lolote jana yake na alipata wivu wa bure tu.


Mr Shamte hakuishia hapo siku moja aliamua kumtafuta fundi wa cctv camera na akaenda kuiweka kwenye nyumba hiyo kwa siri bila kujua mtu yeyote ili ajue kama kuna mtu anakuja kwa Judy. Kwa hiyo kuanzia siku hiyo kila tukio lilikuwa linarekodiwa.


*Itaendelea*


Mr Shamte kapata ufumbuzi sasa kila kitu kitakuwa kinarekodiwa...tunaweza kusema huo ndo mwisho wa Shaibu ? Au ndo sterling hafi?


*Unaweza kumlazimisha ng'ombe kwenda mtoni ila huwezi kumlazimisha kunywa maji*


Jirinde na Corona, endelea kunawa mikono na kuepuka misongamano isiyo ya lazima.




Mapenzi ya Shaibu na Judy yamepamba moto katika nyumba ya Mr Shamte. Almanusra wakamatwe na Mr Shamte baada ya kurejea nyumbani lakini Muki anawaokoa. Mr Shamte anapata wasiwasi juu ya penzi lake kwa Judy, kwa sababu ya uwezo wake wa kifedha anaamua kuweka kamera za cctv kwa lengo la kurekodi kila kinachoondelea nyumbani ili ambaini mtu ambaye ana muaribia furaha yake.


Endelea ......


Mr Shamte baada ya kuhakikisha kila kitu kipo sawa, akaamua kuandaa mtego ili kuwanasawa wabaya wake. Kama kawaida ili kutoa nafasi ya mtego kufanya vizuri basi ukitega kaa pembeni ikiwezekana usionekane kabisa maeneo ya mtego ila hakikisha mtego upo vizuri. MR shamte ili apate kitoweo chake vizuri akajifanya anasafiri kwenda Kenya na atakaa huko siku tatu ndipo atarudi.


Wakati anawaaga nyoyo za Shaibu na Judy zilikongeka kwa furaha huku zikitamani apunguze maneno ya kuwaaga ili aondoke na mambo yaanze hapo hapo. Maana mara baada ya kusema kuwa anaondoka tu, macho ya Judy yalitua kwenye macho ya Shaibu, walipoonana tu wakakonyezana kwa furaha.


Mr Shamte akaondoka zake huku kila kitu kikiwa kimewekwa vyema na kwa usiri mkubwa ambapo mtu wa kawaida hawezi kuona labda uambiwe na aliyeweka au labda uwe unatoka shirika la kijasusi la kimarekani (FBI).


Kwa sababu Muki ndiye aliyeenda kufunga geti la nyumba mara baada ya Mr Shamte kuondoka, Shaibu na Judy wakalianzisha muda huohuo. Wakaingia zao chumbani, wakaendeleza mtanange wao waliouzoea.


Muki aliporejea hakuwakuta sebuleni , teyari akajua washaanza michezo yao. Muki akajisemea moyoni mwake,


"Ama kweli mapenzi yaliyojengeka ndani moyo, hata kwa mtutu wa bunduki hauwezi kuyaondoa...Never never...Yaani hata geti halijafungwa vizuri hawa jamaa teyari mmmmh balaaa"


Muki akatulia zake kwenye sofa na huku akiendelea kuchezea simu yake.


Shaibu na Judy wakatoka baadae sana kuja sebuleni na kumkuta Muki akiwa anaangalia Tv sebuleni . Kwa kuwa Muki waliona anajua kinachoendelea, Shaibu na Judy walijionesha waziwazi kwa Muki.


"Sasa ndugu zangu hata dakika haijapita teyari mmeshaliamsha.....daah aloo nyie wanangu sio poa kabisa...."


Muki aliongea kimzaha mzaha huku akijichekesha kile kicheko cha kinafiki. Wakapiga piga stori za hapa na pale hadi siku ikapita.


Zile siku tatu zilipita huku kukiwa na mapenzi mubashara kati ya wawili hao. Yaani walijiachia haswaa hata Muki naye aliizoea hali hadi akafikia hatua anamwita shemeji Judy. Kuna wakati hata jambo la kutisha likiwa linaonekana kila mara basi huwa la kawaida.


Ndio maana wahenga husema ukitaka kuwa wa tofauti basi hakikisha hauzoeleki na unafanya mambo ya tofauti tofauti.


Mr Shamte alirudi baada ya siku nne. Hakuwa na haraka sana, siku aliyorudi akina Judy walikuwa wapo kazini. Akachukua tape ambayo ilikuwa inarekodi matukio ya nyumba nzima. Akaiweka katika laptop yake na kuiwasha ili aone kilichojiri.


Mr Shamte aliona kila kitu, alishika kichwa huku akisema,


"daaah kumbe kweli kikulacho........"


Mr Shamte alisikia uchungu mkubwa sana, aliona fadhila zake zote ni kama alikuwa anatwanga maji kwenye kinu vile. Pengine mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu....Maumivu aliyopata siku hiyo yalimfanya amkumbuke mke wake akiwa analia lia kila mara pale ambapo huwa harudi kwake. Alianza kuona ni kweli mke wake ameyapitia maumivu makubwa sana kutokana na matendo yake. Roho ya huruma ikamjia lakini akajikakamua na kuendelea na hili la Judy na Shaibu.


"Mr Shamte mimi ni mtu mzima sitakiwi kujiliza wala kuumia kiasi hichi, nachotakiwa kufanya kwa sasa ni kuhakikisha tu anayeharibu furaha yangu na yeye furaha yake inapotea....,lazima nimpoteze...lazima"


Mr Shamte alijipiga piga kifuani huku akisimama na kuelekea chumbani kisha akachukua begi lake pamoja na laptop na kuodoka moja kwa moja hadi kwa rafiki yake mzee mmoja hivi wa kifipa ambaye yeye alikuwa anaishi peke yake kwa miaka mingi sana na hii ilitokana baada ya kumfanyia mauaji mke wake.


Kwa kifupi mzee huyo alikuwa mwanajeshi, kuna wakati alikuwa ameenda kozi fulani huko nje ya nchi ila siku aliyorudi kwake alimkuta mkewe akiwa yupo na mwanaume mwingine tena kwenye kitanda chake. Yule mzee aliwapiga risasi wote wawili hapohapo , baadae alionekana ameua bila kukusudia hivyo hakutiwa hatiani.


Kwa hiyo tangu siku hiyo alimuona kila mwanamke kama mnyama kwake , alichokiamini yeye sio watu wa kukaa nao ndani. Akawa anachukua wanawake anawatumia kisha anawalipa na kuwafukuza. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yake kwa kipindi takribani miaka kumi hivi.


Mr Shamte na Mzee huyo walishibana sana na mara kwa mara walikuwa wanashauriana mambo kadhaa ya maisha yao. Kwa hiyo hata hilo la akina Judy akamwambia kila kitu tena kwa kuweka na video yake kabisa.


Mzee huyo akacheka sana kisha akasema,


"Mr Shamte....Mr Shamte....hadi leo na umri huo bado unaumia kuhusu mwanamke? Unapoteza muda mzee mwenzangu....ukiendelea kuwafuatilia hao watakuumiza kichwa sana...hao ni wa kuwatumia tu basi...."


Mr Shamte akamwangalia mzee mwenzake huyo kisha akamuuliza sasa afanyaje kitu gani. Mzee huyo alimjibu Mr Shamte kwa kumuonesha ishara kwa kutumia mkono wake ambao aliupitisha shingoni mwake yaani kuashiria atenganishe kichwa na kiwiliwili cha mtu (aue).


Wakashauriana sana na wakaona kama Mr Shamte atawaua kwa kuwapiga risasi wote wawili basi inawezekana akatiwa nguvuni na serikali ukizingatia Judy sio mke wake wa ndoa na hata hivyo kuua ni kosa la kisheria.


Walichokiona wote wawili ni kuwatafuta vijana wa kazi, wamteke Shaibu alafu wakamtese sana alafu baadae wamuue.


Mipango ikasukwa siku hiyo , Mr Shamte hakutaka kulaza damu kabisa na kwa sababu alikuwa na hela basi kila kitu kilitimia kama ujuavyo pesa yaweza kuamisha hata milima, Shaibu akapatikana siku hiyohiyo baada ya kudanganywa kuwa yeye pamoja na Muki wanaitwa na Mr Shamte katika moja ya sehemu ambazo Mr Shamte alikuwa anapenda kutembelea, kwa sababu ilikuwa jioni giza likiwa ndio linaingia ingia hivi Shaibu na Muki hawakuweza kuona vizuri wanapelekwa wapi. Usiku kwa usiku walipelekwa kusikojulikana. Walianza kupata hofu baada ya kuona safari yenyewe hawafiki na huku gari likiwa linaenda kasi sana, kiasi kwamba hata ukipiga kelele huwezi kusikika.


Wakati huo huo Mr Shamte alialika vijana watatu wa kiume walioshiba shiba vizuri na kuwaficha nyumbani kwake huku Judy akiwa hajui hili wala lile.


ITAENDELEA


Mr Shamte kaujua ukweli na teyari kawanasa akina Shaibu.


Je Muki na Shaibu watafanywa nini? Au ndo watauwawa kama alivyotaka Mr Shamte?


Wale vijeba walioalikwa na Mr Shamte nyumbani kwa Judy wanataka kufanya kazi gani? Na ni akina nani hao?


*Moyo wa mtu Kichaka*


Tuendelee kumtegemea Mungu kwa kila jambo hata hili la corona litapita



Mr Shamte baada ya kupata hofu ya kusalitiwa anaamua kufanya maamuzi ya kuweka kamera na kurekodi kila kitu, hatimaye anaujua ukweli wote. Anapata wazo baada ya kushauriana na mzee mwenzake. Shaibu na Muki wanatekwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kusikojulikana. Wakati huohuo , Judy akiwa hajui chochote kinachoendelea, Mr Shamte anawaalika vijeba walioshiba shiba na kuwaficha nyumbani kwake.....


Sasa endelea hapa.....


Judy akiwa haelewi chochote, yeye na Mr Shamte wakiwa sebuleni kwao alishangaa kuona mpaka giza linaanza kuingia akina Muki na Shaibu bado hawajarudi kutoka kazini maana mara nyingi yeye Judy huwa wa kwanza kutoka kazini.


"Leo kutakuwa na kazi nyingi sana au sijui usafiri unasumbuaa....?"


Judy alijisemea huku akimtazama Mr Shamte kuashiria anamshirikisha pia swali hilo. Mr Shamte kwa kujiamini akajibu,


"....Aaah vijana wale, wana sehemu nyingi za kupitia ....si unajua damu inachemka bwana......."


"Hata kama ndio hivyo ila haijawahi kutokea kama hii ya leo...."


"....Vipi mke wangu mbona una mashaka sana kwani hata wasiporudi leo wewe utapata hasara gani? Kama wangekuwa na tatizo si wangesema bana....hebu acha habari za hao watu"


Mr Shamte alifura sana na akaonesha amehamaki kwelikweli. Judy akanywea, akatulia na kuacha kabisa habari hizo maana kwa jinsi alivyofokewa basi kama angeendelea kusema habari za kina Shaibu angeweza kusababisha matatizo.


Judy alipika chakula na kula pamoja na Mr Shamte huku kingine kikiwekwa kwenye poti kwa ajili ya akina Shaibu.


Walipomaliza kula, Mr Shamte akahakikisha kila kitu kipo sawa , nyumba yote ilifungwa vioo ili kupunguza sauti kupenya kutoka ndani kwenda nje, Judy alishangaa sana siku hiyo kumuona Mr Shamte akifunga vioo wakati haikuwa kawaida yake, lakini kwa sababu ndiye mtu wake hilo hakulipa nafasi sana, akatulia na kumwangalia Mr Shamte alivyokuwa anaangaika na tumbo lake kubwa.


Baadae Mr Shamte akasema,


"Leo nataka nikupe zawadi nzuri sana ambayo utaikumbuka maisha yako yotee.."


"Mmh zawadi gani hiyo baby?"


"Usiwe na papara utaipata muda mchache ujao"


Mr Shamte baada ya kusema hivyo akamwambia Judy amsubiri kama dakika tano hivi alafu baada ya hapo atamuonesha zawadi yake.


Mr Shamte akatoka sebuleni. Judy alikuwa na shauku kubwa sana ya kutaka kujua zawadi yake kutoka kwa Mr Shamte. Alijaribu kuwaza ni zawadi ya namna gani lakini hakupata majibu. Kwa sababu Mr Shamte alikuwa safarini Kenya , basi Judy akafikiria hiyo zawadi basi itakuwa inatoka Kenya.


Baada ya dakika sita , Mr Shamte akarudi sebuleni na kumwambia Judy amfuate akamuoneshe zawadi yake. Judy akamfuata Mr Shamte lakini akashangaa, akaona hawaingii katika chumba chao wanacholala badala yake walienda moja kwa moja hadi katika chumba kingine tu ambacho kilikuwa hakitumiki.


Mr Shamte akamwambia Judy afumbe macho alafu atamwambia afumbue ndipo atakapoiona zawadi yake.


Judy alipata hofu kwa mbaali lakini kwa sababu aliamini kuwa amemteka Mr Shamte hivyo hawezi kumfanyia lolote baya. Judy akafuatisha kama alivyoambiwa, akafumba macho.


Mr Shamte akamshika mkono Judy na kumwongoza Judy hadi wakaingia katika chumba hicho. Walipoingia tu , Mr Shamte akasema,


"Sasa mrembo wangu unayenitii kiunafiki, usiyependa kuona unaendelea kuishi, unayefanya vitu vya hatari vionekane vya rahisi, usiyejua uchungu wa pesa za mtu....fumbua macho yako uione zawadi yako nzuri kutoka kwa Mr Shamte, mzee kijana wa mjini, nisiyekuwa na huruma pale ninapochezewa...."


Judy akafumbua macho yake huku akiwa na mashaka tele maana maneno ya Mr Shamte yalimtia hofu sana. Alishtuka sana baada ya kuona mambo yaliyopo mbeleni mwake.


Aliwaona wale vijana watatu ambao Mr Shamte aliwaweka kwa siri bila Judy kujua. Vijana hao wote walikuwa hawana nguo, walikuwa kama walivyozaliwa. Judy akataka kukimbia ila hakuweza hata kugeuka nyuma, teyari alikuwa mikononi mwa kijana mmoja wapo.


Wakati huo Mr Shamte alikuwa anacheka kwa dharau na kwa kukejeli. Judy akaanza kupiga kelele lakini kelele zake ziliishia katika chumba hichohicho yaani hazikuwa tofauti na machozi ya samaki ambayo huishia baharini tu..


Walipoona anazidi kuwa msumbufu wakachukua plaster na wakambandika mdomoni, hapo sasa hata ile sauti nyembamba haikutoka.


Mr Shamte akaenda kukaa katika kiti kilichopo ndani humo. Baadae akasema,


"Unahisi nini Judy? Hata sijakuambia zawadi yako unaanza kupiga kelele....kumbe unajua ulichofanya ??"


Judy akawa anatamani kuongea ila mdomo ulizibwa hivyo hakuweza kuitoa sauti.


"Hebu sikiliza wewe binti ilitakiwa utambue mapema katika hii dunia msaada wowote ule uwe unatoka kwa ndugu au kwa mtu baki, mara zote huwa na lengo maalumu yaani mtu anaweza kukupa msaada lakini baadae atahitaji kitu kutoka kwako , unaweza usitambue moja kwa moja lakini huo ndio ukweli.."


Mr Shamte akanyanyuka kwenye kiti kisha akamsogelea Judy, akamwinua kidevu chake, akaendelea kusema,


"Mimi nilikupa msaada kwa lengo niwe na wewe na hilo hata wewe unalijua, pengine jambo ambalo haulijui mimi nimeitelekeza familia yangu kwa ajili yako , wanangu wanapata shida kwa ajili yako, sasa imekuwaje tena penzi langu analionja bwana mdogo huyu...Yaani mnavyojiamini chumba changu ndicho kikawa chenu bila hata uoga basi angalau mngekuwa na heshima kidogo , mngeenda hata huko magesti mkafanya mambo yenu....Ila kwa sababu wewe ni mjinga haya yote wewe ukayaona hayana maana na mimi ukaniona kama furushi la kinyesi..."


Mr Shamte akarudi tena kwenye kiti chake na akaketi. Akawaambia wale vijana wamvue nguo Judy. Judy kavuliwa nguo zake zote na kubaki mtupu na huku wale vijana ambao walikuwa hawana nguo wakianza kupata shida hata ile milingoti ya bendera ikaanza kunyooka ikiwa teyari kwa kupandishwa bendera maana umbo la Judy lilikuwa ni la ushawishi mkubwa sana.


Mr Shamte kwa kejeli akasema,


"Aya mrembo....thamani yako ipo wapi sasa ? Nini hasa unachojiringia? Elimu yako iko wapi?

, Nyie mnaojiita wasomi mnapenda mambo makubwa ambayo hamna uwezo nao, tamaa zako zimekuponza....na leo ndio utajua kuwa kuna umuhimu mkubwa kuvuka barabara kwa kutumia zebra na sio kuvuka vuka tu kila sehemu..."


Baadae Mr Shamte akasema tena,


"Kwakuwa unapenda kufanya mapenzi na wanaume wengi basi hawa hapa nimekuletea...mimi si nilikuwa sitoshi kwako hadi ukamtafuta yule kijana basi hawa hapa labda watakutosha"


Baada ya hapo Mr Shamte akatoa amri kwa vijana wafanye kazi yao.


Vijana wakaanza kuichangamkia fursa maana hata wao walikuwa wanaona kuchelewa kupewa amri ya kuanza kazi yao iliyowaleta.


Kama ilivyo kukata tamaa ikiwa bado pumzi unayo haifai, Judy naye hakuwa mchovu akaanza kujitetea huku Mr Shamte akiwa anatazama na kuonyesha tabasamu kwa mbaali.


*Itaendelea*


Bila shaka lengo la Mr Shamte tushalijua, Je Judy ataweza kujitetea kweli na akatoka salama chumbani humo?


Vipi kule upande wa pili, Muki na Shaibu kimewapata nini au wako wapi?


*Kupata kwa haraka kuna gharama zake mbeleni, tuendelee kutafuta kwa haki huku tukimtegemea Mungu*




Mr Shamte anaanda mpango kabambe wa kutaka kumkomesha Judy kwa sababu alimsaliti, anawaanda vijana shupavu kwa ajili ya kumshughulikia Judy.


Kabla hajawaruhusu kuanza kumshughulikia Mr Shamte anaaza na kumkumbusha Judy alikomtoa. Na baadae anawaruhusu vijana waanze kazi.


Endelea hapa....


Judy akalalama na huku akijaribu kujitetea lakini hakuweza kujitoa mikononi mwa vijana hao ambao hawakuonesha sura za kutabasamu hata kwa sekunde moja. Alijitetea hadi akaishiwa nguvu ya kurusha hata mkono. Alilegea, akawa hana tena ujanja mbele ya vijana wenye roho ya ukatili ambayo haikuwa na hata chembe ya ubinadamu, ni unyama mtupu ndio ulioendelea chumbani humo.


Mr Shamte hakutaka hata kumpa nafasi moja ya kumsikiliza Judy, aliona pengine kufanya hivyo inaweza ikarudisha nyuma lengo lake alilokusudia. Ukiamua kufanya jambo lifanye kikamilifu usifanye nusunusu, ndio msimamo ambao alikuwa nao Mr Shamte kwa wakati huo.


Mr Shamte alibaki kwenye kiti chake huku akiwa anashuhudia ukatili ambao alikuwa anafanyiwa Judy. Wale vijana walichangamkia fursa kwelikweli. Ilikuwa ni vurugu, anaingia huyu ,anakuja mwingine na mwingine. Walibadirishana hivyo hivyo tena huku mwingine akiingia mlango wa mbele ya nyumba na mwingine akiingia kupitia mlango wa nyuma wa nyumba.


Judy alionekana kuanza kupoteza fahamu, hata macho yake yalisinzia , hayakuweza kuona mbele tena. Vijana hawakumwacha mapema, waliendelea kushughulika.


Chumba kilitapakaa damu, kinyesi na mkojo yaani unaweza ukadhani machinjioni. Hapo sasa Mr Shamte akawaambia waache, vijana wakamuacha Judy kisha wakakaa pembeni.


Mr Shamte akamsogelea Judy , akaona hawezi hata kuongea na teyari alikuwa amezimia. Mr Shamte akawaambia vijana wamchukue na kumpakia kwenye gari kisha safari ikaanza mara moja usiku huohuo.

Gari ikaendeshwa mkukumkuku , mwendo wa kama lisaa limoja hivi, walifika walikokuwa wanaenda. Maeneo hayo yalikuwa nje kidogo mwa mji wa Dar es salaam, palikuwa tulivu sana, gari likapaki. Sehemu yenyewe haikuwa na nyumba hata moja zaidi ya miti tu iliyoonekana mbeleni mwao.


Mr Shamte akashuka garini na wale vijana pia, baadae kidogo kama dakika mbili hivi wakaja vijana wawili na kuwapokea akina Mr Shamte kisha wakamshusha na Judy ambaye bado alikuwa amekata pumzi na huku akiwa hana nguo hata moja. Wakatembea kama dakika tatu hivi wakafika sehemu ambayo wapo watu wengine. Walikuwa akina Muki na Shaibu pamoja watesi wao.


Shaibu na Muki walishtuka baada ya kuona kuna watu wengine wanakuja, kwa sababu ya giza hawakuwatambua mapema watu hao.


Walipofika walipo akina Shaibu , tochi za simu zao zikawashwa, Shaibu na Muki walimuona vyema Mr Shamte, hapo sasa wakashtuka na kujua teyari mambo yote yamepangwa na Mr Shamte, hawakuwa na namna nyingine zaidi ya kusubiri matokeo tu.


Mr Shamte akamsogelea karibu Shaibu ambaye wakati huo alikuwa amefungwa mikono kwa nyuma. Akamshika shingoni kwa nguvu alafu akasema,


"Wewe ndo unaniharibia nyumba yangu..... Sasa wewe si unajifanya mwamba na hauogopi kabisa wake wa watu ngoja nikuoneshe leo kuwa kuna miamba mingine huwa haipasuki hata kwa bomu...."


Shaibu akajitetea huku akijifanya hajui chochote anachokisema,


"Bosi nimefanya kitu gani mimi? Sijaharibu nyumba yako ....."


Mr Shamte akawaambia wamsogeze karibu Judy , vijana wakamnyanyua Judy na kumpeleka karibu na Shaibu, wakamulika tochi.


Shaibu akashtuka tena baada ya kumuona Judy akiwa hajielewi tena akiwa yu uchi. Mr Shamte akasema,


"Nadhani sasa umeelewa kinachoendelea hapa....si umemuona huyu kahaba mwenzako? Mlidhani sitajua? Mimi sichezewi, nilitafuta pesa kwa tabu sana sasa huu ulikuwa muda wangu wa kutumia alafu unakuja kijana mdogo kabisa kuniharibia furaha yangu....hahaa (kicheko cha kulazimisha) "


"Nisamehe mkuu , Judy ndio alinilazimisha"


Shaibu alisema huku akionesha hofu katika sura yake. Mr Shamte akampiga kibao Shaibu, alafu akasema,


"Kila mtu wakati anatenda jambo lolote lile nafsi yake huwa inajua hilo jambo kama ni jema au baya.....Naamini hata nafsi yako ni shahidi ,itakuwa ilikuambia kuwa unachofanya unakosea ila ukijifanya wewe ndio wewe....ulitakiwa uyafikirie matokeo kwanza kabla hata hujaanza mchezo...."


Shaibu alitaka aongee tena ila Mr Shamte akamkatiza kwa kuendelea kusema yeye....


"Msamaha hausaidii kwa sababu hauwezi kurejesha heshima yangu kwa sasa, sasa hivi kuna jambo moja tu mbeleni, na wewe upate mateso na ulipie gharama za mateso yangu , hebu muangalie mwenzako alivyo (huku akimulika tochi katika mwili wa Judy ambao ulitapakaa damu na harufu ya kinyesi) na wewe pia utakuwa hivi muda sio mrefu"


Shaibu alijutia moyoni mwake kwanini alikutana na Judy. Shaibu akakumbuka hata wale wapenzi wake wawili aliwaambia asiwe na mawasiliano naye , yaani alishaachana nao wote. Aliijutia nafsi yake lakini hakuwa na uwezo wa kuiokoa.


Muki wakati wote huo alikuwa anatazama tu kinachoendelea huku akiilaumu bomobomoa kwani ndiyo iliyomfanya awe karibu na Judy na mwishowe balaa limewakuta.


Mr Shamte akamgeukia Muki na kumwambia,


"Wewe naye nakujumuisha pamoja na hawa kwa sababu bila shaka naamini kuwa ulikuwa unajua kinachoendelea ila kosa lako ni kutoniambia na kama ujuavyo ukiwaona watu wanafanya maovu na wewe ukawaacha bila kuwaambia basi wewe nawe unakuwa sehemu ya maovu hayo...."


Muki alipoona mambo yanaelekea kuwa mabaya zaidi alipiga hesabu akaona bora ajiokoe mwenyewe kwa kukimbia, kuna wakati fulani mahala ulipo huwa ni pazuri kuliko pale unapokombilia ndio maana kuna msemo wa kiingereza usemao,


'sometime it is better to stay where you are rather than to move on'..


, Muki akaanza kujitenga taratibu , akafyatuka kama risasi , akakimbia lakini kwa sababu alikuwa amefungwa kamba mikononi mwake kinyumenyume hakuweza kufika mbali walimkamata na hapo hapo Mr Shamte akaamuru vijana wake wamalize kona. Vijana hao wakamkaba kooni Muki ,Muki akaanza kurusha rusha miguu kwa kukosa pumzi. Vijana wakazidisha kibano mpaka pale Muki alipoiacha dunia na kuelekea katika makazi mengine kabisa ambayo kwake yataenda kuwa mapya. Walipoona ametulia , vijana wakamuacha na wakamsogeza kwenye kichaka na kumtupa.


"Malizeni na huyu, tuondoke...."


Mr Shamte aliongea huku akionesha kidole kwa Shaibu kwamba na yeye auwawe kisha waishie zao.


Vijana wa kazi wakamshika Shaibu na wakamnyanyua wakaanza kumpiga ngumi za tumboni na wengine wakimkaba kooni.


*Itaendelea....*


Muki teyari pumzi zake zimeisha, hatujui kama Judy ataamka tena au naye teyari habari zake zimeisha.....


Shaibu naye yupo hatua za mwisho kupelekwa kuzimu....


Hivi ni kweli Mr Shamte yuko sahihi kwa kile anachokifanya???


Kuna matukio mengine ni Mungu tu atakayekuokoa, kila binadamu huwa amezaliwa kwa kusudi maalumu hata upitie magumu kiasi gani bado utasimama imara tena ili kusudi lako litimie hapa duniani.


Usikose sehemu ijayo kesho muda kama huu kuijua hatma ya hayo yanayoendelea.




Judy anashughulikiwa na vijana kwa nguvu zao zote na mwishowe Judy anapoteza fahamu ambapo haijulikani kama ataamka tena au la., Muki wakati akijaribu kujiokoa kutoka kwa watekaji anakamatwa na kukabwa shingoni hadi umauti unamkuta. Baadae vijana hao wanaanza kumpiga Shaibu ili wamuue.


Songa hapa sasa.....


Vijana walimpiga sana Shaibu hadi akapoteza nguvu. Akalegea lege lege, viungo vyake havikuwa na ushirikiano tena. Wakamwangalia machoni, macho yake yalifumba. Wakaona wameshamaliza kazi, wakamchukua na yeye kisha wakamtupa kichakani. Wakarudi alipo Judy, naye wakamkagua kagua wakaona amekata pumzi na hawezi kuamka tena, wakamchukua na yeye wakamtupa kichakani waliko wenzake.


Baada ya hapo Mr Shamte na vijana wake walijiridhisha mambo yote yamekaa sawa. Wakapanda katika magari yao na kuishia zao.


Mr Shamte na vijana wake usiku huo walienda katika moja pub kubwa sana, wakanywa na baadae Mr Shamte akawapa mzigo wao wa fedha kisha kila mmoja akaelekea anakokujua.


Mr Shamte akarudi hadi pale alipokuwa anakaa Judy. Akaingia zake bafuni kuoga, alipotoka akachukua tena laptop yake ili aangalie kitu gani hasa Judy alikuwa anapenda kutoka kwa Shaibu hadi akakubali kufanya ujinga katika nyumba yake.


Aliangalia kwa utaratibu matukio yote yaliyokuwa yanafanyika. Alibaini Judy alikuwa na furaha sana akiwa na Shaibu kuliko hata alipokuwa yupo na yeye. Na hapa ndipo akagundua kuwa furaha hailazimishwi, furaha huja pale ambapo mtu anafanya anachokipenda na moyo wenyewe utasema tu hata kwa ishara kuwa unafurahia kile unachokifanya.


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog