Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

BWANA MIHAMALA - 3

  

Chombezo :  Bwana Mihamala 

Sehemu Ya Tatu (3)



Usikose sehemu ijayo kuijua hatma ya wawili hawa Shaibu na Judy......




Shaibu akiwa nyumbani kwa Judy , badala ya kuanza kazi yake wanaaza mambo mengine kabisa....Baadae Shaibu anarudi kwa Muki na kukuta ugomvi kwa sababu Muki ameshindwa kutoa hela ya umeme na maji....Shaibu anailipa....Baadae Shaibu na Judy wakakutana lengo likiwa ni Shaibu kutaka kujua historia ya maisha Judy.......


*Songa nayo hapa...*


Baada ya kukutana wakatafuta sehemu nzuri wakatulia na kuketi mahala. Salamu zikatangulia na masihara ya hapa na pale kisha Shaibu akazama kwenye lengo lake.


Shaibu alianza kama masihara vile lengo ni kutaka kumfanya Judy asijisikie vibaya na asijue kama alimwita hapo kwa lengo hilo.


Katika maisha hata kama upo na rafiki yako kuna baadhi ya maswali yanaweza yakaleta mgongano wa kimawazo au ugomvi, hivyo ni vyema ukachagua namna nzuri ya kuuliza swali.


"Alafu nimekumbuka kitu...wewe ushawahi kukaa Mwanza eeeh...."


Shaibu alimuuliza Judy kiudadisi..Judy akajibu,


"Mmmmh hapana....vipi kuna nini...?"


"Kuna mahala kama niliwahi kukuona hivi ndio nikadhani utakuwa wewe na utakuwa mtu wa kule ..."


"Aah sijawahi hata kwenda huko, mimi kwetu Iringa...."


"Kwa hiyo Dar ni kwa mume eti...."


"Yeah sina ndugu hapa Dar zaidi ya yule ninae kaa naye tu......"


"Na yule Mr Shamte ni mtu wa hukohuko Iringa?"


"Hapana yule kwao Tanga.."


Shaibu akatulia kidogo kisha akaguna,


..."Mmmmh..."


"Vipi mbona Mmmmh tena?"


Judy akauliza...


"Unajua kuna jambo halijakaa sawa kichwani mwangu najaribu kuangalia uhusiano wa maeneo haya mawili...Iringa na Tanga naona mbalimbali kweli...sasa najiuliza hapa mlikutana kutana vipi... (huku Shaibu akionesha sura ya mshangao na ya kimasihara hivi)"


Judy naye akatulia kidogo hivi huku akiwa anatingisha kichwa chake akiwa anaonekana kama ana majonzi kwa mbali hivi.


"Aah Shaibu...jinsi nilivyokutana naye ni kisa kingine kabisa...Naomba nikuambie siku nyingine tutakapokutana tena..."


Kwa sababu lengo lake lilikuwa hilo, Shaibu akang'ang'ania kujua na baadae Judy akaamua kumuhadithia jinsi ilivyokuwa.


"Shaibu kwanza kabisa ujue mimi nimemaliza bachelor pale Mlimani (udsm), nimesoma masuala ya Statistics 'takwimu'"


Huku mdomo ukiwa wazi, Shaibu akajikuta anasema...


"Aaah kumbe una bachelor? "


"Ndio nina shahada,ulidhani mi 'mbugila' eeh.... utulie sasa wewe si umetaka kujua...!! Utauliza baadae...!!"


"Aya poa nakusikiliza"


Shaibu akasema kisha akatulia vizuri na kumwangalia Judy akiwa ameshika kidevu chake.


"Basi ndio hivyo, baada ya kumaliza chuo, sikutaka kurudi nyumbani, nikaamua kubaki hapa hapa Dar kutafuta kazi........


ngoja nikujibu najua unatamani kujua kwanini sikutaka kurudi nyumbani Iringa...Huko nyumbani maisha ndio magumu kabisa, wazazi wangu wote walishafariki kwa ajali ya gari tangu nikiwa sekondari , nikawa naishi kwa Shangazi kijijini kabisa huko ila sikuwa napata sitahiki zote kama ilivyokuwa nipo na wazazi wangu, manyanyasho mengi yalikuwa juu yangu kwa hiyo nilijua kama ningeenda huko basi pengine nisingepata amani ya nafsi na kama ujuavyo sasa hivi ajira zimekuwa chache sana kwa hiyo ningekuwa mtu wa nyumbani tu....Nilijiaminisha kuwa hapa Dar ninaweza kupata kazi hivyo nikafanya maamuzi magumu ya kwenda kupanga chumba"


Judy akatulia kidogo , kisha baadae akaendelea....


"Sasa nilichotegemea sio nilichokutana nacho, niliangaika hapa Dar kutafuta kazi ofisi zote unazozijua wewe nilipeleka barua lakini hakuna hata sehemu niliyoitwa kufanya hata Interview tu...Pesa zangu za boom 'mkopo' ambazo nilikuwa nazo kidogo, zote ziliisha kwa nauli na pesa za kutolea copy za vyeti.


Pale nilipopanga, kodi ilivyoisha ikabidi nikakae kwa rafiki yangu wa hapahapa Dar anayeishi huko Tabata , huko nilikaa wiki tu , wazazi wake wakamwambia anifukuze maana nilikuwa naishi kwao bila msaada na hali ya maisha ni ngumu hivyo waliniona ni kama mzigo wa kinyesi ambao hauna faida zaidi zaidi utakutia harufu tu..........."


Ukatokea ukimya kidogo kisha Judy akasonga mbele..


"Rafiki yangu alikuwa ananipenda sana ila hakuwa na namna ya kufanya ikabidi awatii wazazi wake , mimi nikaondoka hapo kwao na begi langu mgongoni huku mkononi nikiwa na shilingi elfu 30 ambazo alinipa huyo rafiki yangu zinisaidie nauli ya kufika nyumbani....


Sikwenda nyumbani, nikatafuta guest ya bei rahisi mno ili walau nikae hapo hata kwa siku mbili tu, kwani niliamini mjini ndiko kazi ziliko."


Sasa Shaibu mikono yake yote miwili ikawa imeshika kidevu na kumwangalia kwa makini sana Judy ambapo mpaka wakati huo bado hakujua walikutana vipi na Mr Shamte.


Judy akaendelea kueleza,


"Siku ya pili nikiwa pale guest ambayo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya hela yangu, kuna kampuni fulani nilipeleka barua ndipo nilipokutana na Mr Shamte kwenye kampuni hiyo. Mr Shamte ndiye meneja pale, anahusika kila kitu, baada ya kukutana naye ofisini kwake ndipo aliponiweka wazi kila kitu ... .'binti mjini hapa hakuna kazi utakayopata bila hata wewe kutoa kitu, si unajua mkono tupu haulambwi??" Nakumbuka vizuri hiyo ndiyo kauli ya kwanza kuniambia Mr Shamte, huku nikidhani kuwa anataka hela ila akaniambia akinitajia hela sitaweza kumlipa, hakuhitaji kingine kwangu zaidi ya mwili wangu....."


Hapo sasa Shaibu akaitoa mikono kwenye kidevu kisha akainamisha kichwa chini na hofu ikaanza kumjia moyoni mwake. Alianza kuhisi hali ya hatari mbeleni mwake hasa afya yake, maana alijua watu kama hao (Mr Shamte) mara nyingi huwa wanawaambukiza makusudi watoto wadogo magonjwa, hasa ule ugonjwa dume ulioshindikana kwa miaka kupatikana tiba.


*Itaendelea*


Nasikia uchungu kuendelea kuandika , maana najaribu kufikiria kama ikiwa kweli anachofikiria Shaibu unadhani itakuwaje?????


Bado turudi kulekule kwa wasemavyo wahenga....


*Ukitaka kuruka agana na nyonga* *wala Usipime urefu wa kina cha maji kwa mguu*


_tuendelee kumuomba Mungu atuepushe na covid19 huku tukiendelea kuchukua tahadhali_





Judy na Shaibu wanakutana na Shaibu kuanza kumdadisi Judy ili kujua historia yake ya nyuma. Judy anaonekana kama anakataa hivi lakini baadae anakubali kufunguka yote aliyokutana nayo....anahadithia kuanzia mwanzo hadi kukutana na Mr Shamte.....


*Endelea hapa*


Judy alimuona Shaibu kama amefadhaika hivi , akaamua kutulia na kisha kumuuliza Shaibu kulikoni.


Shaibu ambaye kichwa chake kilikuwa kimeinamishwa chini alijibu kuwa hamna kitu na alimtaka aendelee tu.


Sauti aliyoitoa Shaibu ilikuwa ya kinyonge sana, haikuwa yenye kuchangamka hata Judy aligundua jambo hilo.


Baadae Judy akaendelea na story yake....


"Basi yule bosi 'Mr Shamte" baada ya kusema kuwa anahitaji mwili wangu , mimi mwanzo nilidhani kama masihara vile kwani umri wake na alichokiongea havikuhusiana kabisa.


Lakini Mr Shamte alikomaa na kukaza sura , nilipoendelea kukataa sikuamini kabisa kilichotokea, alinifukuza nje kabisa ya ofisi na huku akimwambia mlinzi hataki kuniona tena.


Nilitoka hapo ofisini na kurudi guest, nikiwa guest nikafikiria wapi pa kwenda lakini sikupaona nikaona bora nirudi tu kwa Mr Shamte nikaendane na masharti yake...... (huku machozi yanamtoka Judy)"


Ukimya kidogo ukatokea, Judy akaendelea......


"Kwa hiyo siku hiyohiyo baada ya kurudi ofisini, na kumwambia kuwa nimekubali, Mr Shamte alitabasamu palepale ofisini kwake huku akinishika shika kidevu changu, Hapo hapo nikapewa mkataba ambao ulinitaka mara moja kuanza kazi siku inayofuata, siku hiyo hiyo nililala naye hotelini. Nikamweleza shida zangu na asubuhi tu ya siku inayofuata alinitafutia nyumba na kunipangia nyumba nzima ndio ile uliyofika"


Shaibu akanyanyua kichwa chake kisha akamuuliza Judy,


"Sasa Judy kwanini ulikubali hayo yote? Si bora ungerudi nyumbani tu "


"Unajua wakati tunasoma pale chuoni kila mmoja wetu alikuwa na ndoto za kuwa na maisha bora baada ya kumaliza chuo, sasa kama nilivyosema nyumbani ni kijijini sana sidhani kama ningetoboa maisha kama ningeenda kule"


"Kwa hiyo sasa hivi umetoboa?"


"Sasa wewe huoni tu, namiliki gari hilo hapo, ninakaa kwenye bonge la nyumba tena peke yangu bila hata bugudha na mtu...."


"Je unayafurahia maisha unayoishi?"


"Hapana .....Si kivilee kwa sababu naishi na mtu ambaye sio chaguo langu sina amani naye hata kidogo....kuna mambo mengi nashindwa kuyafanya na hata nikiwa naye yaani hata sijisikii amani....Umasikini mbaya sana Shaibu"


"Basi bado hujatoboa Judy, kama maisha unayoishi yatakupa furaha hapo angalau unaweza kujisifu kuwa umefanikiwa kwa kiasi fulani ila kama kinyume chake wewe bado hujatoboa... lakini naomba nijue sasa mmefunga ndoa? "


Judy akajibu kuwa hawajafunga ndoa na suala la ndoa Mr Shamte hajawahi kulizungumzia hivyo wanaishi tu hivyohivyo.


Shaibu naye akampa background ya maisha yake. Judy akapata kutambua kuwa janga la ukosefu wa ajira nalo limemkumba bwana Shaibu.


Wakaendelea kupiga story za hapa na pale mpaka pale jua lilipoanza kuzama ndipo wakaamua kurudi nyumbani.


Wakiwa njiani, Shaibu akajaribu kumdodosa Judy kama anaweza kumsaidia kwa Mr Shamte apate ajira hata kama ni ya muda tu.


Siku zote tajiri hanuniwi, yaani pamoja na kuona kama Mr Shamte hana utu lakini bado Shaibu alitamani kupata msaada kutoka kwa Mr Shamte.


Judy akamwambia Shaibu kuwa ataenda kumsaidia , atajaribu kumshawishi Mr Shamte kama ataweza ampe kazi yeyote ofisini kwake.


Shaibu na Judy wakaachana, Shaibu akaenda kwa Muki kumpa story za Judy.


Shaibu alimweleza kila kitu rafiki yake Muki. Muki baada ya kuambiwa kila kitu akamalizia kwa kusema kimzaha mzaha...


"Mzee inabidi ukapime kwanza mambo mengine yatafuata...."


Shaibu akahamaki kimasihara,


"Kwa hiyo unataka kusema mimi nina ngoma au sio...."


"Aaah mzee mbona umeenda mbali sana, unajua pesa, kazi na hizi mali zoote hazina faida ikiwa kama afya zetu zinatishia uhai, maana ya kwenda kupima ni kuangalia tu afya, wewe si umeona mazingira yenyewe haya jinsi yalivyo....!?"


" aah baba kupima siendi , wewe fikiria umri huu uambiwe umeukwaa itakuwaje....Na mimi nina mashaka sana na yule mzee"


Muki akawa kama amekumbuka jambo hivi, akauliza swali kwa Shaibu.


"Hivi huyo mzee kabla hajakutana na Judy hakuwahi kuwa na familia? Na vipi hawajapata mtoto wakiwa na Judy?"


Shaibu huku akishika kichwa akasema,


"....aaah kweli hapo nimebugi mzee ....unajua nilisahau kabisa kumuuliza jambo hilo Judy na hata hivyo mimi nahisi hawana watoto maana nikienda kwao pale huwa nawaona wao tu na papo kimya sana...."


Wakajadiliana kuhusu jambo ambalo alilomwambia Judy na kutafutiwa kazi kwa Mr Shamte. Muki aliona kuna hatari inaweza kutokea endapo kama watakuwa wanakaa karibu na judy maana siku zote mapenzi hayafichiki, wanaweza wakajisahau hadi wakawa wanajionesha waziwazi na mwishowe Mr Shamte kuwashtukia mapema.


Lakini pamoja na hofu yote hiyo , hawakuwa na jinsi waliona bora tu waende kufanya kazi pengine wanaweza pata nafuu ya maisha. Ila wakajiapiza kuwa makini sana na Shaibu muhusika mwenyewe akamuahidi rafiki yake Muki kuwa kamwe hatahusika tena kimapenzi na Judy na atakaa naye mbali sana.


Baada ya kuagana hapo, Shaibu alipofika kwake akalikumbuka lile swali la Muki la kama Judy na Mr Shamte wamepata mtoto au la au kama Mr Shamte alikuwa na familia kabla hawajakutana au la. Shaibu anayakumbuka haya yote ili ajiridhishe nafsini mwake asiwe na hofu kwamba pengine amepewa ngoma na Judy.


Akaangalia saa akaona bado mapema hivyo bado Judy atakuwa hajafika kwake kwani walipoachana alisema atapitia kwa rafiki yake hivyo atakuwa yupo mbali na Mr Shamte, akanyanyua simu kumpigia Judy...


Simu iliita na kupokelewa na Mr Shamte.


*Itaendelea*


Je Shaibu atasema nini mbele ya Mr Shamte??? Au ndo maji yanataka kumwagika hapo mapema tu hata kabla hawajapata kazi?


Unadhani Shaibu ataenda kupima kweli?


Ikiwa kama atapima, unahisi majibu yatakuwaje?


Hebu tuendelee mpaka mwisho tujue hatma ya haya yote.......



Bwana miamala Shaibu anakutana na Judy, Judy anamweleza kila kitu cha nyuma hadi alipo kwa wakati huo. Shaibu anamuomba kitu Judy (amsaidie kupata kazi kutoka kwa Mr Shamte).....Kuna vitu vinamtia wasiwasi Shaibu anaamua kumpigia simu Judy ili amuulize lakini simu inapokelewa na Mr Shamte.....


Endelea sasa......


Kumbe wakati Shaibu anadhani Judy atakuwa yupo peke yake alikuwa anajidanganya, Judy alipofika nyumbani alimkuta teyari Mr Shamte amesharudi. Wakati Shaibu anapiga simu, Shamte na Judy walikuwa pamoja sebuleni. Na mbaya zaidi simu ya Judy alishika Mr Shamte wakati huo akiwa anakagua sms na call history zote za siku hiyo. Mr Shamte alikuwa na wivu uliopindukia kwa Judy, hakutaka kumpa nafasi yeyote ya kufanya chochote nje ya yeye mwenyewe.


Shaibu baada ya kuisikia sauti ya Mr Shamte alisita kidogo kujibu kwa haraka. Wakati simu inapigwa Judy aliona jina la Shaibu ili kuua jambo hilo kwa haraka , Judy akamwambia Mr Shamte akate simu.


Mr Shamte akamtii Judy, akakata simu. Judy akamuwahi Mr Shamte hata kabla hajasema kitu.


"......aaah unajua baby nilisahau kabisa kukuambia kuhusu huyu kijana....."


"Enhee kafanya nini huyu kijana?"


"Hivi unajua kama ana degree yule?"


"Degree. ...!!?"


"Yeah......"


"Enhee.....nipe maneno"


"Ile siku aliyokuja hapa ambayo ulimtuma alilia lia hapa akiomba msaada wa kazi yaani kaomba sana umpe kazi yeyote kasema hivyo...."


"Aaah sasa mbona hajasema siku zote hizi...Alafu kwanini akuambie wewe na asiniambie mwenyewe....?"


"Mimi nilimwambia akufuate wewe lakini akaogopa ....sasa naona hapo anapiga simu ndo anataka kuniulizia kama nilikuambia au la...."


Mr Shamte huku akilichezea tumbo lake kubwa lililotangulia mbele kama mlima, akasema,


"Daaah Asee huku tunakoelekea sijui itakuwaje...Vijana wanahangaika sana kutafuta ajira....pale ofisini hamna hata nafasi au sijui tumchomeke kule kitengo cha usafirishaji au wewe unasemaje....Au nimweke pale kitengo cha wageni na takwimu awe msaidizi wako ??"


"Wewe mwenyewe utaangalia akae wapi....!!"


"Aaah mke wangu.... mimi nakusikiliza wewe tu"


Judy huku akijichekesha chekesha na tabasamu kwa mbaaali akamwambia Mr Shamte hata akimweka awe msaidizi wake itafaa tu.


Mr Shamte hakuwa na kipingamizi chochote , akamwambia ampigie simu Shaibu na amwambie asubuhi tu aende ofisini kwake.


Judy akampigia simu Shaibu, Shaibu alipata mashaka sana kuipokea simu ya Judy kwani alidhani atakuwa Mr Shamte ndiye anayempigia.


Judy alipoona hapokei ikabidi amtumie sms alafu akapiga tena ndipo akapokea. Judy akamwambia kama walivyojadiri na Mr Shamte.


Habari zilikuwa njema sana kwa Shaibu.


Asubuhi ilipofika Shaibu alienda mahala alipoelekezwa. Alipokelewa na kupelekwa kwa Mr Shamte. Mr Shamte akampa maelezo ya kampuni bwana Shaibu huku akimdokeza na kazi yake ambayo anatakiwa kuitekeleza.


Shaibu akaanza kazi siku hiyohiyo huku kazi yake ya miamala akiiweka kando kidogo na kumrudishia mwenyewe ofisi. Maisha yalisonga mbele ila kwake Muki bado hali ilikuwa tete, sasa ilikuwa kazi ya Shaibu kumuomba Mr Shamte amsaidie na Muki.


Kwa sababu Shaibu alikuwa akiifanya kazi yake kikamilifu na kwa heshima yake na Muki pia akaitwa kwenye kampuni, akapewa kitengo.


Siku zilisonga mbele, angalau maisha yao (Shaibu na Muki) yalikuwa na uhakika wa kula na sehemu ya kulala. Maisha ya kazi yakaendelea vizuri hakukuwa na dosari yeyote.


Siku moja wafanyakazi wa kampuni wakiwa wanapiga tu story za hapa na pale. Shaibu na Muki wakiwepo, mfanyakazi mmoja akamgusia bosi wao Mr Shamte., na ndipo stori zikatiririka kama maji.


"Daaah Mr Shamte jamani balaa asee, hivi unajua yule mzee ana familia yake ? .....basi yule ana mke na ana watoto wakubwa sana lakini mambo yake mmmmmmh kama kijana wa wa leo vile...."


"Hapa ofisini wadada wote hawa unaowaona, kawamaliza wote hakuna hata mmoja ambaye ameruka, kwa usije ukaona demu hapa ukamuona mpya...utakwishaa"


"Enheee hata yule Judy kaingia kazini kwa mtindo huohuo , alitoa mzigo ndio akapewa kazi ila kwa hali ilivyo acha tu atambe bwana ...Yeye si ndo kashika mpini acha waumie wanaoshika makali"


"Mimi nawaambia yule mzee nahisi ana ngoma , si unakumbuka yule dada aliyekuwa Secretary wake ambaye kwa sasa marehemu.....basi yule alikufa na ngoma na mzee wetu hapa ndio alikuwa mzigo wake ule...."


"Aaaah noma mazee yaani siku hizi inabidi kuwa makini sana asee maana watu wa rika zetu ndo wanachukuliwa na wazee..."


"Sasa kama ndio hivyo si Judy naye atakuwa nao? Daaah huruma sana mtoto mbichi kabisa yule kashamwaribia maisha.....Ila tamaa zinawaponza hawa dada zetu za kutaka maisha bora kwa haraka..Kama asemavyo Trump 'No shortcut in life' kwamba hakuna kitonga lazima upambane ."


Wafanyakazi waliendelea kubwabwaja na kila mmoja kuongea lake kuhusiana na kampuni hiyo hasa Mr Shamte bila kujua kuwa maneno yao yalikuwa mwiba mkali kwa Shaibu.


Kipindi chote hicho, Muki na Shaibu walikuwa kimya kwani wao walikuwa wageni hivyo hawakuwa na story nyingi za kampuni. Walikaa kimya ili kupata dondoo za yale ambayo walikuwa hawayajui.


Habari za Mr Shamte zilifungua upya akaunti ya hofu na mashaka kwa Shaibu. Alianza kuhisi kama anaishiwa nguvu hivi. Akanyanyuka ili aende chooni, hata chooni kwenyewe hakufika, akaanguka njiani. Mtu pekee aliyeona tukio lile alikuwa ni Muki kwani tangu ananyanyuka alikuwa anamwangalia anaenda wapi, haraka akawaita wenzake , wakamchukua na kumpeleka hospitali.


Daktari alipomcheki aligundua kuwa alikuwa na pressure iliyochanganyika na hofu kubwa. Alitundikwa drip ya maji na kupatiwa matibabu mengine.


Masaa matatu mbele, Shaibu akapata nafuu. Wakati huo mbele yake kulikuwa na Mr Shamte, Judy pamoja na Muki. Shaibu alikuwa anamwangalia Judy kwa uchungu sana huku akiamini kuwa teyari ameyapata maradhi mabaya kutoka kwa Judy. Kuna wakati Mr Shamte alitoka nje kuongea na simu ndipo Shaibu alipopata nafasi ya kumwambia Judy kwa sauti ya unyonge ....


"Umeniua Judy...."


Wakati huo Muki alikuwa anamkonyeza Shaibu kuacha kuongea kwani Mr Shamte alikuwa anaingia.


Baadae Shamte na Judy wakaondoka, wakabaki Muki na Shaibu ndipo Muki akamshauri Shaibu akapime tu ili kuondoa hofu yake. Shaibu aliogopa sana ila baadae akakubali kwa shingo upande.


Wakaenda kwa daktari na wote wawili wakachukuliwa vipimo vya damu . Baada ya nusu saa wote wawili waliitwa kwa daktari, walikubaliana kupokea majibu kwa pamoja.


Daktari akaanza nasaha nyingi kama kawaida yao,ambapo nasaha hizo ndizo zikazidi kumtia hofu Shaibu ambaye alitamani kuondoka kabisa eneo hilo. Baadae Daktari akachukua karatasi ya majibu ili awasomee majibu yao.


*Itaendelea*


Nini kitajili kwenye chumba cha daktari? Ni majibu gani atayasoma?


Unadhani majibu atayapokea kweli Shaibu?


*Hofu huondoa uhai, hofu husababisha mambo mengi yasifanikiwe*





Judy anafanikiwa kumshawishi Mr Shamte na hatimaye Shaibu na Muki wanapata kazi kwenye kampuni yake.


Maisha ya kazi yanaendelea vyema, ila siku moja wafanyakazi wanaamua kupiga stori za hapa na pale na kumgusia bosi wao ambapo stori zao zinamtia hofu Shaibu hadi anpoteza nguvu na kuanguka.


Baadae Muki na Shaibu wanaamua kwenda kupima ili wajue afya zao hasa hasa Shaibu ambaye amepitia katika kipindi kigumu. Vipimo teyari na kazi imebaki kwa daktari kusema majibu.


*Sasa songa hapa....*


Daktari akauliza,


"Hapa Shaibu ni nani?"


Shaibu na Muki wakatazamana alafu wakakaa kimya. Daktari akauliza tena na hapo Muki akanyoosha kidole kwa Shaibu kuashiria ndiye yeye.


Baadae daktari akasema,


"Anyway naona kama bado mna wasiwasi, nianze na nani kutaja majibu yake kati yenu?"


Shaibu akanyoosha kidole kwa Muki na huku akisema "anza na huyu..."


Muki hakuwa na kipingamizi, akakubali aanze yeye. Daktari akayasoma majibu ya Muki.


Majibu yalionesha ni negative ( hakuwa na shida yeyote). Sasa daktari akamgeukia Shaibu ili na yeye amwambie majibu yake. Kabla hata hajaanza kusoma, teyari Shaibu mwili wake uliloa jasho kama kamwagiwa na maji. Mapigo ya moyo wake yalikuwa yanasikika kama mngurumo wa radi.


Shaibu akamwangalia Muki na kumwambia waondoke, majibu yake watayafuata siku nyingine. Wakati anasema hivyo teyari Shaibu alishanyanyuka juu kutoka kwenye kiti alichokaa.


Muki kuna neno alitaka kulisema ila teyari Shaibu alikuwa ameshatoka nje ya chumba cha daktari. Muki naye akatoka nje na wote wakaondoka bila kujua majibu ya Shaibu.


Walienda hadi nje ya hospitali ambapo pembeni yake palikuwa na mgahawa, wakaenda kuagiza maji , wakanywa , wakatulia kidogo baadae hali ya utulivu ikarejea kwa Shaibu, wakaamua kuondoka na kurejea makwao , hawakurudi tena kazini siku hiyo maana teyari muda ulikuwa umeshakwenda( muda wa kazi uliisha) hivyo wakarudi wanakoishi.


Usiku ule wa siku hiyo ulikuwa mrefu sana kwa Shaibu na hata kwa Judy. Shaibu bado alikuwa anafikiria stori za boss wake wakati Judy akifikiria ile kauli ya Shaibu kwamba anamuua. Judy akawa anajiuliza anamuua Shaibu kivipi? Aliwaza lakini hakupata majibu. Aliona majibu atayapata kwa Shaibu siku wakikutana.


Asubuhi ilifika na wote kila mmoja akawa anaendelea na majukumu yake ya kazi.


Wakiwa kazini , kila mmoja kwa wakati wake, Shaibu na Muki walipigiwa simu na wenye nyumba na kuambiwa kuwa gari la bomoa bomoa limeanza kubomoa nyumba ambazo zipo katika hifadhi ya barabara ili kupisha ujenzi wa barabara ya lami.


Nyumba hizo ziliwekwa alama ya X muda mrefu sana na serikali ilishawapa taarifa kuwa wanatakiwa waame ila wakapuuzia , waliona kama bado saaana na kama utani vile. Nchi nyingi za Afrika ndio kasumba yake hiyo, kwenye janga lolote lile huwa hawachukui taadhari mpaka waanze kuona madhara ndipo wanashtuka.


Taarifa zilikuwa mbaya sana kwao, ikabidi waende kwa meneja wao Mr Shamte kumwelezea suala ili ikiwezekana basi waende kwao kutoa hata vitu vyao. Mr Shamte akawaruhusu, wakati wanatoka Judy alikuwa anawaona, akaamua kuwafuata na kuwauliza mbona wanaondoka muda huo.


Shaibu akamweleza Judy kilichotokea. Moyo wa Judy ukasononeka sana lakini alipata faraja baada kuona kwa tatizo hilo basi kwake itakuwa fursa ya kukutana tena na Shaibu, kuna jambo lake aliwaza haraka haraka mara tu baada ya kuambiwa shida hiyo.


Shaibu na Muki wakaondoka na kila mmoja akafika anakoishi na hawakuwa wanaishi mbali mbali saana. Walipofika walikuta watu wakiangaika kutoa vitu vyao ndani.


Nao wakaingia kazini kuanza kutoa vitu vyao na kuviweka sehemu salama. Kwa sababu hawakuwa na vitu vingi basi haikuwa kazi ngumu sana kwao. Walimaliza kwa haraka tu.


Wakati Shaibu na Muki wanaondoka, Judy alienda ofisini kwa Mr Shamte. Judy aliingiza na mapenzi katika maongezi yao, sauti ya kimahaba ndiyo iliyotumika kuongea na Mr Shamte.


"Baby nimekutana na akina Shaibu hapo nje wanasema wanakokaa wamebomolewa nyumba zao ndo wanaenda kutoa vitu vyao ...Daah So sad....ila nawaonea huruma sana sijui wataenda wapi mchana huu maana ni ghafla sana, unaonaje tukienda kuwaweka kwenye kile chumba cha nje kwa muda tu alafu baadae wakipata sehemu wataondoka..."


Judy aliongea hivyo akichezea sharubu za Mr Shamte. Mr Shamte akatabasamu kisha akasema,


"Neno lako kwangu ni sheria, sina kipingamizi chochote tena itafaa sana maana nyumba ile ni kubwa sana alafu muda mwingi ulikuwa unakaa peke yako hivyo itakuwa fursa ya kuchangamsha nyumba...."


Mara baada ya kuongea hivyo tu, Mr Shamte akampigia simu dereva wa kampuni na akamwambia aende ofisini kwake mara moja.


Dereva bila hata kukawia akaingia ofisini kwa Mr Shamte, Mr Shamte akampa maelezo dereva,


"Chukua gari kubwa ya ofisi alafu utaongozana na huyu Judy ...Kuna sehemu mtachukua vitu alafu mtapeleka nyumbani kwa Judy, tafuta hapo nje vijana hata wawili tu mkasaidiane kubeba vitu hivyo"


Dereva hakuwa jibu lingine zaidi ya kusema "sawa mkuu" maana agizo la bosi ni sawa na amri au sheria ambayo inapaswa kufuatwa vinginevyo mkaidi ndiye itakuwa mwisho wa kazi yake.


Judy akatoka na dereva pamoja na vijana wawili kama alivyosema Mr Shamte, Walipofika karibu na mitaa anayoishi Shaibu Judy alimpigia simu Shaibu na kumwambia amfuate sehemu alipo maana yeye Judy aliisahau nyumba anayoishi Shaibu. Kwakuwa hapakuwa mbali , dakika tano zilitosha kuwafikia.


Judy akajifanya hahusiki kabisa, akamwambia Shaibu kuwa bosi wao ndio ametuma gari lichukue vyombo na wakakae nyumbani kwake kwa muda.


Shaibu akiwa anashangaa shangaa teyari Judy alishawaambia vijana wapakie vitu garini. Faster tu wakamaliza, wakatoka hapo wakaenda kwa Muki nako wakapakia vitu na kwenda kwa Judy moja kwa moja. Vitu vikashushwa na kuwekwa store maana nyumba hiyo ilikuwa na kila kitu hivyo hapo wakaoneshwa chumba tu ambacho ndani kilikuwa na kila kitu.


*Itaendelea*


Bado Majibu ya Shaibu hayajajulikana hadi sasa....


Bobomo bomoa inamfanya Shaibu akae karibu sana Judy.


Hebu fikiria kwanza watu hawa kuwa karibu kiasi hiki....Kweli watavumiliana hawa bila hata chochote kufanyika..??


Tutayajua mengi sehemu ijayo, usikose.


*Tatizo halikimbiwi, tatizo hutafutiwa ufumbuzi*,




Daktari anafanikiwa kumpa majibu yake Muki lakini kazi inakuwa ngumu kwa Shaibu, kutokana na hofu aliyokuwa juu ya majibu , Shaibu anaondoka bila hata kuyapokea majibu. Bomoa bomoa inawakumba akina Shaibu na Muki na Kwa mpango wa Judy ambaye yeye alikuwa na kusudi maalumu anaamua kumshawishi Mr Shamte ili Shaibu na Muki waamie nyumbani kwake ili tu yeye awe karibu na Shaibu. Shaibu na Muki wanaamia kwa Judy na kuanza maisha mapya.


*Sasa endelea hapa.....*


Siku ya kwanza Shaibu na Muki walifikia katika chumba cha nje (kilijitenga na nyumba yao kubwa ). Wote walilala chumba kimoja. Jambo hili Judy akaliona kwake halifai kwani bado atakuwa yupo mbali na Shaibu. Akazichanga karata zake vizuri, ili aumalize mchezo mapema sana.


Usiku wa siku ya pili yake, Judy aliutumia vyema kumshawishi Mr Shamte ili Shaibu aamie nyumba kubwa.


"Unajua baby mimi ninachoona hapa si vizuri kwa watu wazima kama wale waendelee kulala kitanda kimoja mimi naona kimaadili haijakaa poa na ukkzingatia hapa kuna vyumba vingi tu....."


Judy alisema akiwa amejilaza kifuani kwa Mr Shamte. Mr Shamte alipenda kumpa sana nafasi Judy katika maamuzi. Udhaifu mkubwa wa Mr Shamte ulikuwa katika wanawake, hasa wanawake 'vimada' yaani lolote aliloambiwa kwake alilitekeleza bila hata kujiuliza uliza.


Mr Shamte akiwa ametabasamu akamuuliza Judy,

"Kwa hiyo unasemaje sasa malaika wangu...hebu wewe sema unachokitaka....Nilishasema neno lako kwangu ni Sheria.....haa haa haa....."


Mr Shamte alimaliza kusema na huku akitoa kicheko cha watu wenye pesa ambacho huwa kinalazimishwa na huwa hakitoi sauti sana.


"Mimi naona bora mmoja aje kulala ndani huku au hata wote waje kulala humu lakini vyumba tofauti...."


"Kwa hiyo unataka nani aje kulala huku maana vijana hawa wasije wakaleta tamaa tamaa hapa si unajua siku nyingine huwa mimi nasafiri , nakaaga hadi wiki, mwezi sijarudi.....Au anyway kwa sababu teyari Shaibu ashaizoe nyumba hii basi mwambie aamie chumba hicho cha jirani na chetu"


Mr Shamte akajiingiza mwenyewe mtegoni, akanyoosha njia kwa Judy , Judy sasa akawa anatiririka tu mteremkoni. Judy akamwambia sawa haina Shida itafanyika kama alivyopendekeza.


Asubuhi na mapema tu wakati wanajiandaa kwenda kazini, Mr Shamte aliwapa maelezo akina Shaibu ili lengo baadae wakirudi basi kila mmoja afikie kwenye chumba chake.


Wakaenda kazini na baadae waliporejea, Shaibu akaonyeshwa chumba chake kipya.


Usiku wa siku hiyohiyo, wakiwa wanakula chakula Mr Shamte akapigiwa simu , simu ambayo ilionesha ni muhimu sana. Simu hiyo ilimtaka aondoke na kwenda huko.


Mr Shamte haraka haraka akawaaga na kuondoka. Hakuna aliyejua anaelekea wapi zaidi ya yeye mwenyewe.


Simu aliyopigiwa Mr Shamte ilitoka kwa mke wake ikiimtarifu kuwa mwanaye alikuwa anaumwa sana. Mr Shamte wakati wote huo ambao alikuwa anautumia akiwa na Judy kumbe alikuwa na familia yake. Jambo hili Judy hakulitambua kwani mara nyingi Mr Shamte alikuwa anashinda na Judy hivyo haikuwa rahisi hata kidogo kugundua jambo hilo.


Hata zile siku ambazo alikuwa anataka kwenda kwa mke wake, basi Mr Shamte alikuwa anaaga anaenda kufanya kazi zake za ofisi.


Baada ya kuondoka Mr Shamte huku nyuma sasa wakabaki Muki, Shaibu na Judy.


"Sijui bosi kapata simu gani asee maana ghafla tu anaondoka..."


Alianza Muki kuongea, na Shaibu naye akadakia,


"Labda tumuulize Judy mama mwenye nyumba....kulikoni(Shaibu alisema kimasihara?"


Judy akasema huku akimalizia kumeza wali ambao teyari alishauvunja vunja mdomoni,


"Heee jamani sisi wote tupo hapa na ameondoka tukiwa hapa wote....Mimi nitajuaje sasa....."


Shaibu akadakia,


"Ila mtu mkubwa yule itakuwa watu wa ofisini hao au mabosi wenzake wamemuita...."


"Aaah jamani eeeh mtu mzima yule mwenyewe anajua anachokifanya...."


Judy akadakia na kumaliza mjadala. Wakaendelea kula na walipomaliza wakaendelea kutazama Tv huku kukiwa na ukimya yaani hakukuwa na stori zozote zile zaidi ya kuelekeza macho yao kwenye TV.


Dakika kama 30 hivi mbele, Judy akapigiwa simu na Mr Shamte kisha akaambiwa kuwa hataweza kurudi kwa siku hiyo hivyo wataonana asubuhi.


"Aaah jamani Mr Shamte kasema hatarudi leo, kwa hiyo hadi kesho. Mimi nina usingizi sana ngoja nikalale....."


Judy aliongea kisha akasimama na kuwatakia usiku mwema kisha huyooo akaishia zake.


Muki akatia neno kwa Shaibu,


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog