Chombezo : Jirani Tam Tamuu
Sehemu Ya: Tano (5)
Endeleaa....
Gafla mke wangu alitokea nyuma ila hisia zangu zilinisaidi kutambua kuwa kuna mtu anakuja nikawa nimetoa mdomo wangu kwa shomy nikajifanya kama namtolea mdudu,
"Tulia nikutolee huyu mdudu shomy,
Shomy alikuwa ni msichana mwenye uelewa mkubwa sana aliposiki nimebadili mada akajua kuna jambo ma yeye akaendana na hali halisi,
"Ataniuma jamani mtoe,,
Mke alikuwa anajua hatujamuona kumbe nilitilumia hisia kufaham uwepo wake mke wangu alitoa salam,
"Habari zenu jamani?.
"Nzuri vp mzima?.
Zahara alimjibu ila mimi nilimchunia,
"Nzuri tu shomy vipi za kwako?
"Nzuri ila naona kuna kamdudu kalitaka kuniuma,
"Pole,
Waliendelea kuongea mimi nikaingia chumbani nikakaa kimya,
Mke wangu naye aliingia chumbani,
"Mme wangu mbona umenikasilikia?.
"Nieleze ulikuwa wapi mpaka sasa hv?.
"Mme wangu ndio unaniuliza kwa hasira hivyo?
Kabla sijamjibu nilisikia sauti ya juma sebureni nikajua atakuwa amekuja naye hapo hasira zikazidi,
"Sitaki ngonjera sema ulikuwa wapi?
"Lakini mbona hivyo?.
"Mpumbafu jibu nilichokuuliza?..
Niliongea kwa sauti ya juu nikamtia na kofii la nguvu moja,,
"Mmee wangu unanipigaaa...
Aliongea huku akilia kwa uchungu,
"Kimya sema ulikuwa wapi pumba wewee,,
"Nilikuwa kazini,,
"Mpaka mida hii??..
"Ndio,,
"Mshenzi wewe ipo siku yako nitakutia mikononi,,
Nilimuachia nikapanda kitandani nikiwa kitandani sms ilingia kutoka kwa shomy,
"Seif please acha kumpiga mkeo,,
"Kaniboa sana,,
"Kakuboa nini?.
"Mpaka sasa hv ndio anarudi nyumbani toka asubuhi,,
"Mbona mimi umenirudisha sasa hvi na bwege langu halijanipiga?
"Wewe ni wewe mkeo wangu ni mke wangu,,
"Mh!!!.. naona una hasira kwaheli,
Tuliacha kuchart,
Nililala mida ya saa tano na nusu mke wangu akaniamusha nikale chakula,,
"Mme wangu karibu chakula,,
"Achana na mimi bwege wewe,,
"Jamani hata chakula mme wangu,
Nilimkatisha kuongea kwa kumfokea,,
"Toka usinipigie kelele pumbafu wewe..
Aliogopa akarudi sebuleni akiwa mpole kama barafu,,
Asubuhi kulikucha nikaenda mitaaa ya mwenge kumtafta Nasra nione kama nitampata,
Niluzunguuka vibanda vyote vya mama ntilie hatimae nikapata nafuu nikampata anayemjua,
"Yupo msubili anafanya kibarua hapa,,
"Sawa asante,
Nilikaribishwa ndani nikakaa kumsubili..
Itaendelea...
Endeleaa...
Nilikaa ndani kumsubili Nasra sema ukweli nilikuwa na hamu ya kumuona Nasra kwani moyo wangu ulikuwa umemchagua kuwa naye,
Nilika kama dk16 nikasikia nje jina la Nasra likitajwa,
"Nasra una mgeni wako yuko ndani ana kusubili,,
"Mgeni wangu mimi?
"Ndio, "ni nani?.
"Yumo ndani si ukamuangalie..
Mahojiano hayo yalinidhihilishia kuwa Nasra wa kipindi hicho zanzibar ndio yule yule hajabadilika maana hakuamini kama anaweza kuwa na mgeni,
Nasra aliingia ndani akanisogelea bila kuniangalia usoni akaniuliza,
"Unasemaje maana huu ni mda wa kazi na istoshe huwa sipendelei maongezi na watu napenda kufanya kazi zangu nikimaliza nipumzike nifikilie maisha ya kesho,,
"Nasra Nasra...
Aliposikia sauti yangu alikuwa kama amepigwa shoti ya umeme akanigeukia na kuniangalia,,
Hakuamini kuniona pale aliniangalia kwa tahamaki kisha akasimama akaniangalia usoni akasimama na kutaka kuondoka,,
"Nasra namba unisamehe naomba kuongea na wewe..
"Seif ulinitia aibu ya mwaka,,
"Naomba unisikilize nasra,,
"Seif kwa sasa niko kazini niko nasambaza chakula kwa wateja,,
"Kwani mko wangapi hapa kwa kuhudumia?.
"Tuko wawili..
"Twende nikuombee kwa bos,
"Seif utanihalibia kazi yangu,,
Nilitoka naye nje nikmuomuaga yule mama mwenye hotel,,
"Mama namchukua huyu ndungu yangu hatarudi tena hapa,,
"Eeeh!! Kwanini?
Nasra alishangaa ile kauri ila akanyamanza,
"Sasa mbona sina hapa pesa yakumlipa kwa sasa?
"Hiyo usijari mama,,
"Sawa safari njema,,
"Haya kwaheli,,
Nilimuingiza kwenye gari nasma tukaianza safari mda wote Nasra alikuwa kimya,
"Nasra wewe ndie ulikiwa chaguo langu niliyekuchagua ila hila za pale kwenu wakanibadilishia mke wakanipa yule ndugu yako,
"Niliyajuwa hayo ndugu yangu alinisimulia,,
"Pole kwa matatizo nasra,
Niliisha poa,
Nilimpeleka mpaka maeneo ya sinza nikamchukulia chumba hotel nzuri ya garama,
"Ingia ukaoge uje,,
Baada ya kuoga tulishuka sehem ya kula tukala chakula huku tunapiga story mbali mbali baada ya kula nikampeleka duka la nguo za kisasa nikamnunulia nguo za bei kali baada ya hapo nikampeleka saloon kubwa yenye hadhi kubwa wakamlemba nikamnunulia mahitaji yote ya kujipodoa siyo siri Nasma alingaa alipendeza na uzuri wake ukaonekana kumbe Nasra alikuwa mzuri kuliko hata zahara,,
Mida ya saa kumi na moja nilirudi nyumbani nikakuta Zahara hayupo nikamuuliza shomy,
"Vp zahara katoka saa ngapi?
"Mida hii,
"Alikwambia ameenda wapi?.
"Amesema ana shift ya usiku kazini,
"Ok, vp mme wako yupo?.
"Hayupo nae kaingia kazini shift ya usiku,
"Sawa,
Nilitika nikaingia chumbani nikajua hakuna cha shift ya usiku atakuwa na juma,,
Itaendelea....
Endelea.......
Nilijiegesha huku nikifikiliya cha kufanya,
*ningejua walipo ningewatokea ili niwabambe vizuri nimpe taraka yake mbwa huyu*
Nilishitushwa na hodi iliyosikika mlango w chumbani kwangu,
"Karibu,,
"Asante, "ingia basi,
Aliingia shomy akakaa kitandani kwangu,,
"Seif leo umeshinda wapi?
"Nilikuwa kwa jamaa zangu na marafiki zangu,,
"Toka asubuhi?.
"Ndio,
"Seif naomba nikueleze kitu kimoja,
"Kitu gani?
"Naona sitokuwa namtendea haki mme wangu kuendelea kutumika na wewe kimapenzi,
"Kwa hiyo?.
"Naomba tuachane kila mmoja afanye yake abaki na familia yake,
"Sawa haina shida itakuwa vizuri,
Maneno ya shomy hayakuniuma ila yaliongeza furaha moyoni mwangu kwani nilikuwa nikiwaza kila siku itakuwaje kuhusu Nasra kama nitaendelea kuwa kimapenzi na shomy na nilijua huenda mawazo ya shomy nikuachika ili nimuowe na hilo nililijuwa fika kuwa litatokea, ila maneno yake niliona amenilahisishia,
"Seif mimi natoka,
"Sawa,,
Shomy alitoka nikamsindikiza na macho mpaka alipoishilia nje,
Kumbe mawazo ya shomy yalikuwa chanya hebu sikia mawazo yake,
*seif akija leo natikisa kiberiti namwambia tuachane ili karoho kamuume anibembeleze nipate nafasi ya kumwambia kuwa nataka niachike aniowe hata nikiwa nyumba ndogo sawa tu*
Shomy angejitambua na kinitambua asingewaza huo ujinga nazani alisahau ule usemi usemao kuwa KATA MTI PANDA MTI
alijidanganya sana kwani na mimi nilikuwa na mawazo yangu tofauti na alivyofikiria,
Ilipotimu mida ya saa kumi na mbili nilitoka nikawaza kwenda kwa Nasra nimpange maneno ili aweze kukubaliana na mimi nimuowe,
Nilitoka nje ya chumba changu nilipofika sebureni nilikutana na shomy akiwa amekaa sebureni nilipita tu bila kusema chochote akanisemesha,
"Seif seif...
"Naam,, "unaenda wapi?..
"Naenda kuzurula,
"Twende wote?
"Hapana we si mke wa mtu?
Alikosa cha kujibu nikatoka nikaenda zangu,
Nilifika alipokuwa Nasra hotelin tukawa tunaongea mawili matatu,
"Nasra twende tukakae sehem iliyotulia tuongee mawili matatu,
"Sawa,
Tulitoka tukaenda hotel moja iko kuduchi karibia na bahari ya india maji yalikuwa karibu sana tulikaa tukasgiza vinywaji huku tunasubili mda wa kula tuagize chakula,
Nilimweleza A mpaka B nasra kuhusu kumuowa akawa anasta akiogopa kuvunja ndoa ya ndugu yake,,
Tukiwa katika maongezi nilimuona jamaa yangu mmoja tunayefamiana sana,
"Seif mambo vp?
"Poa,, "za siku mbili tatu?
"Nzuri,
"Vipi ndio unaenda home?
"Ndio familia iko kwenye gari,
"Basi poa mimi bado nipo,
"Poa ila shemeji nimemuona kule mbona mko mbali mbali?
"Tuna kakikao kidogo kwa hiyo tunasubiliana tuko wengi,
"Ahaa poa basi naenda,
"Poa umesema yuko wapi?.
"Pale kwenye deli la cocacola,
"Aah!! Poa atanikuta hapa,
"Poa,
"Nassra unaona umalaya wa ndugu kaaga anaenda kazini kazini ndio hapa?.
"Twende nikamfuate asiniletee upuuzi wake,,
Itaendeleaa....
Endelea....
Nilinyanyuka nikaeleke alipokuwa amekaa Nasra nilimkuta amekaa na juma nikasimama mbele yao kama dk2 nawaangalia dokta juma akakosa cha kuongea akabaki ameinamisha uso chini,
"Zahara hapa ndio kazini?.
"Hapana,
"Unafanya nini hapa?.
"Nimekuja kula chakula,
Mh!! Yaani unatoka mhimbili mpala kunduchi kuja kula cuakula?
""Ndio mme wangu,
Nilimuangalia kwa jicho kali nikachukua tishu nikaandika taraka,
NIMEKUPA TARAKA LEO TAR 03/08/2015 KWA KUKUFUMA UKIWA NA MWANAUME USIKU SEHEM YA STAREHE BILA RIDHAA YANGU.
NI mimi mmeo SEIF JABU..
"chukua taraka yako na leo usirudi kwangu na leo naowa,,
"Mme wangu naomba radhi kwa hili,
"Kwaheli,,
Niliondoka nikiwa na Nasra tukaingia kwenye gari nikawasha gari nikaondoka mpaka kwa rafiki yangu chande nikaingia kwake nasra nikamuacha kwenye gari,
"Chande nimekuja hapa nina shida na leo nataka niitatue,
"Shida gani?
"Nataka kuowa,
"Nini seif,
"Nazani una masikio mazima naomba twende,
"Sasa seif,,,...,,
"Kama hutaki usinifuate,,
Kwa upendo aliokuwa nao chande juu yangu alinifuata nyuma masikini ya mungu alisahau hata kama amevaa taulo akaingia kwenye gari tukaondoka Nasra alishangaa ile hali ya mtu kuingia kwenye gari na amevaa taulo,,
"Nasra tutafunga ndoa leo leo nawapigia wafungishaji tutawakuta nyumbani,
"Seif mbona maamuzi ya haraka hivyo?
Chande naye akachangia mada,
"Eti seif mbona maamuzi yamekuwa ya haraka sana,
"Nasra anajua kila kitu,
Chande alishituka kusikia nasra,
"Ina maana huyo mbele ni nasra?
"Ndio,
"Nasra za siku?.
"Nzuri,,
Hapo nilimpigia sheikh wa kufungisha ndoa,
"Shehe tukutane nyumbani kama sms ilivyokufikia,
"Sawa, kwa hiyo ndoa leo,
"Ndio ndoa ni saa yoyote nitakayofika,,
"Kwa hiyo sisi utatukuta kwako?
"Ndio,
Nilikata simu nasra akadakia,
"Ila seif kwanini tusingeshauriana kwanza?.
"Wewe ndie ulikuwa chaguo langu kwa hiyo nilipokuonea ndio hapo hapo ndoa,
Nilipofika tu getini na gari ya juma akiwa na Zahara walifika..
Endelea......
Tulifikia kwa pamoja nyumbani,
Niliingiza gari mpaka ndani ya geti nikatelemka
nikiwa na Nasra na chande tukaingia ndani
nilikuta mashsikh wameisha fika wako ndani
wananisubili mimi tu,
Shomy naye alikuwa kwenye sofa akiwa
anaangalia tv tulipoingia alishanga kumuona
chande akiwa na taulo na mimi niko haile haile,,
"Shomy: haaa jamani vipi tena mbona hivyo?
Kabla hajajibiwa alishangaa kuona mmewe na
mke wangu wakiingia huku mke wangu akiwa
analia,
"Shomy: heee!!... jamani kulikoni mbona sielewi?.
Nilimjibu,,
"Utaelewa tu,,
Niliingia ndani nikaenda nikaleta kitezo nikaweka
hapo,
"Mashehe mnaubani?.
"Ndio tunao,
"Haya tuanze kazi iliyowaleta,
"Sheikh: bibi harusi yuko wapi?.
"Huyu hapa, nasra sogea hapa,
Alikosa namna ikabidi asogee,,
"Sheikh: shahidi wa bibi harusi yuko wapi?.
"Hayupo wewe fungisha tu mimi na yeye
tumerdhiana,,
"Sheria haisemi hivyo,
"Wewe chande mbona umezuba zuba tu hebu
kaa hapa uwe shahidi wa nasra,
Chande alisogea akiwa na kataulo kake,,
"Sheikh: sasa mbona si waelewi?
"Usicho elewa nini sasa hapa au umepewa
rushwa mbona unaanza kuleta vikwazo?.
"Siyo vikwazo sasa huyu jamaa (chande) kavaaje
kweli?.
Nilimuangalia chande nikagundua kavaa taulo,
"Hivi chande zinakutosha?
"Nini?
"Hakili,
"Nimefanyaje?
"Nenda chumbani kwangu uvae suruali,
Chande alijiangalia hakuamini macho yake
yalichokiona,,
Alikimbia chumbani akavaa suriali na yenyewe
akaigeuza akarudi kwenye mkeka,
"Sheikh: huyu anaitwa nani?.
"Anaitwa chande,,
"Na msichana,
"Anaitwa Nasra,
Hapo chacha wakati wote huo mke wangu
hakuwa anafaham kama huyo anayeolewa ni
Nasra ndugu yake kwa baba,
"Seif sikubali huweza kumuoa Nasra,
"Kwanin?.
"Sikubali sikubali..
Fujo zikianza mda wote juma alikuwa akiangalia
zoezi linavyokwenda,
Vurugu zilizidi nikamuwasha makofi mawi ya
nguvu zahara ili atulie,
"Sheikh endelea..
"Bwana chande umekubali kumuoza nasra kwa
seif kwa mahali ya sh 500000?.
"Ndi...oo..
Kabla sheikh hajaendelea shomy akasimamisha
shuguli,,
"Shomy: sheikh subili hapo hapo,,
"Shomy: seif sikubali nina.....
Endelea...
"Shomy: seif sikubali nina ujauzito wako....
Nyumba nzima ilishituka kwani kila mmoja alijua shomy ni mke wa juma,
Sheikh alisimama,
"Seif kwaheri siwezi kufungishisha hii ndoa mpaka utakapojipanga,
Sheikh na watu wake waliondoka nikabaki na msala wa shomy,
"Seif: unasemaje shomy?.
"Nina mimba yako,
Kichwa kiligonga mala mia zaidi nikajiuliza kwanini shomy aonge mbele ya watu?. Tena mmewe akiwepo,
Juma aligeuka akaangaliana mkewe kisha akamuuliza,
"Shomy una mimba ya seif? "Ndio,
"Kwa hiyo ulinisaliti mke wangu?.
"Nisamehe mme wangu,
Niliingilia kati,
"Juma wewe ndie uliyeanza kutoka na mke wangu kabla mimi sijatoka na mkeo kwa hiyo umsamehe mkeo,,
"Seif nakubali ila juwa kuwa mimi sijadhini na mkeo ila wewe umefanya mapenzi na mke wangu roho inaniuma sana,
"Nitaamini vp hujatembea naye?.
Mke wangu aliingia kati,
"Mme sikuwahi kuzini nje ya ndoa yangu wala sikuwahi kuzini kabla ya ya ndoa yangu nazani unajua uliniowa nikiwa na bikira yangu,,
"Mke wangu nini kilikukumba wewe mpaka ukawa karibu na juma?.
"Mme wangu nisamehe sema ukweli nilijuwa kuwa kwa kuwa sikuwa chaguo lako basi utakuja niacha kwa sababu niliona unaanza kubadilika mala kunifokea mala kukata kula chakula changu hiyo hali ndio iliyonifanya nitafte faraja nje ila nimegundua wewe ni mwanaume bora kwangu kwa kuwa nimeelewa mimi ndie niliye kosea na pia juma nilikuwa nafahamiana naye toka zamani na aliwahi kunichumbia kwa kipindi cha nyuma kwa hiyo nilijikuta nataka kurudisha mapenzi kwake ila nimeliona kosa langu nililiofanya kwako nisamehe seif naomba unisamehe mpenzi wangu,,
Nilikaa kimya nikamsikiliza mke wangu maneno yake niliona yana ukweli mtupu ila sikuweza kukubali mbele ya watu ili nisijeonekana mimi ni mkosaji,
"Nimekuelewa ila sitaki kulazimisha akiri yangu kukupenda,,
"Shomy: seif unaniweka upande gani mimi?
Swali la shomy lilinichanganya sana nikashindwa nionge nini?.
Endeleaa.....
Nilikosa cha kumjibu shomy nikabaki natoa macho nisijue nifanye nini?
Juma aliingia chumbani akapakia nguo zake akatoka kwa ajiri ya kuondoka,
"Seif: juma unaenda wapi?
"Sina changu hapa seif acha nikaanze upya nitapata mwanamke mwingine maana siwezi kuishi na mke mwenye mimba ya mtu mwingine,,
"Sote tulikosea juma ulimtamani mke wangu na mimi nikamtamani wa kwako kwa hiyo cha kufanya mchukue huyu mke wangu nendeni mtaowana huko huko,,
"Zahara: mimi najua kuwa wewe seif ni mme wangu kwa hiyo kunikabithi mtu niende naye ni sawa na kunibaka maana sijarithia,,
"Uliyomfanyia Nasra nazani unayatambua kwa sipendi kuwapa watu faida maana itakugarimu kwa hiyo bora uende tu,,
Nilishika mfukoni nikatoa noti tano za elfu kumi nikampa Nasra nikamwambia,
"Nenda uchukue tax ukapumzike nitakuja kukuona kesho,
"Sawa,
Nasra aliondoka zake na mimi nikabaki na msala wangu,
"Juma mambo yameharibika na aliyeanza ni wewe ulianza kumchombeza mke wangu siku ya kwanza ulipoingia katika hii nyumba kwani ulianza kumkonyeza pale siku ya kwanza nikanoki siku iliyofuata ukaenda naye kazini kwa kutumia gari yako alafu mke wangu akanidanganya kuwa eti aliondoka na gari ya kazini nilipoona hali hiyo nikatumia msemo mmoja na kuufanyiya kazi unaosema kuwa mla vya wenzie na vyake huliwa basi hapo ndipo niliponyemelelea tunda lako na kutumia udhaifu wako wa kuwa karibu na mke wangu kumnasa mkeo,
Kuna kipindi ulichart na mke wangu sana kwenye wasap mpaka akasahau kunipikia mimi mmewe nilipoona hivyo nikaamuwa na mimi kuchart ma mkeo na kweli nilifanikiwa kwani nilimfariji pale alipohitaji faraja,
"Seif nimekuelewa mkeo kipindi kilichopita nilitaka kumuowa ila akasafiri kuelekea India aliporudi alikuta nimezaa na binti mmoja ni nesi hospitalini kwetu hapo akabadili maamuzi na alipoenda kwao zanzibar akanitumia ujumbe kuwa anaolewa nikaridhi kinafiki tu basi na mimi ndio nikaamuwa kumuowa shomy ila bahati mbaya akapata maradhi yaliyosababisha nisishiriki naye kimapenzi mpaka sasa,
"Zahara: seif please nisamehe,,
Nilimuangalia usoni alionesha sura ya upole nikaingiwa na huruma,,
Itaendeleaaa.....
ila moyo wangu haukuwa tayari kumsamehe,
"Zahara nakuonea huruma ila siko tayari kuishi na wewe tena,,
Zahara aligara gara kama mtoto kwenye sakafu huku akinishika miguu na kuendelea kuomba radhi,
"Side ningekuwa malaya ningelikuwa nimeisha zini nje ya ndoa ila nilikutunzia heshima yako mme wangu,
Maneno yale yalizidi kuniumiza nikamuangalia mke wangu nikaona ni kweli nafsi yangu ikawa inaniambia kuwa kama wewe umezini mpaka kumpa shamira mimba kwanini usimsamehe aliyekutunzia heshima,
Nilimuangalia mke wangu nikaona bora nimsamehe ila kutamka kutoka mdomoni ikawa kazi,
"Shamira: side msamehe mkeo kweli anakupenda angalia kifua kilivyo jaa machozi kisha ujiulize nani mkosaji zaidi ya mwenzie kati yako na yeye?.
Maneno ya shamira yalizidi kuuchoma moyo wangu kama mkuki unavyochoma,
"Charles: side msamehe mke wako samehe saba mala sabini kwani wewe umemkosea mungu mangapi? Umefanya uzinzi mala ngapi?
Rudisha moyo msamehe mkeo side,
Chande naye aligongelea msumali palepale,
"Juma: side msamehe mkeo angekuwa msichana asiye na tabia njema ningekuwa tayari nimemvua chupi ila kwa kuwa anajiheshimu sikuweza kufanikisha ukimuacha huyu msichana utakuwa umeacha dhahabu na huenda ikaokotwa na na mtu asiyejuwa dhamani yake Side msamehe mkeo,
Maneno ya mme wa shamira yalikuwa kama nyundo iliyokuwa na uzito mkubwa,
Nilimuangalia shamira nikamuangalia Zahara nikamkumbuka Nasra kichwa nikahisi kinapasuka kwa ajiri ya mawazo,
"Side: najiwazia kuhusu shamira maana ana mimba yangu tayari, sasa ataileaje na mimi ndie niliyempa hiyo mimba?.
"Zahara : side kuhusu hii mimba isikusumbue nitailea mwenyewe,
Nilimuangalia juma juma aliponiangalia akachukua begi lake akaanza kupiga hatua za kuondoka huku akisema,
"Kwaherini jamani..,,..
Juma aliondoka hivyo,
"Charles: side nyie jadilini watatu naona mtafikia mwafaka mzuri acha na mimi niende,
"Side : charles muafaka tutapata njoo tuongee,,
Mimi na Charles tulitoka pembeni kidogo kuteta jambo LA kufanya
"Charles wewe ni rafiki yangu sasa sikia nenda Rombo hotel kaongee na Nasra vizuri mpaka akubari kuolewa na wewe mwambie mpigie side umwambie hutaki kuolewa naye,
"Side hebu subiri yaani unamaanisha nasra nimuowe mimi?
"Ndio maana sipendi yule mtoto ateseke,
"Hiyo itakuwa ngumu,
"Kwanini charles hebu fanya hivyo kama unataka ndoa yangu iendelee,
"Nitajaribu,,..,,
"Sawa nenda,,
Nilirudi sebuleni nikaendelea na kikao,
"Zahara ukitaka kuishi ma mimi lazima ukubari uwepo wa shamira hapa kama mke mwenziyo maana hana mme mpaka sasa,
"Sawa mme wangu hata tukiwa watatu mimi moyo wangu utaridhia maana nakupenda wewe ila ukumbuke kuwa Nasra naye anakupenda na kudhibitisha hilo nikuwa alijaribu kujiua pale aliposikia kuwa hataolewa na wewe na sifichi huenda akawa anakupenda kuliko hata mimi na shamira tunavyokupenda,
"Hayo niachie mimi kama unakubali hivyo kuwa na uke wenza basi sawa,,
Tulimaliza makubaliano yote pale kuwa shamira atatambulika ni mke wangu kuanzia siku hiyo,
"Sawa kila mmoja aende chumbani kwake nitapanga zamu,
Zahara aliingia chumbani akatoka na mfuko wa keki akatenga keki mezani akatukaribisha mimi na shamira,
"Karibuni keki,
"Asante,
Nilichukua kipande kikubwa nikawaaga,
"Endeleeni nakuja,
Niliondoka na keki nikaweka kwenye gari kisha nikaondoka ili nimuwahi Charles asimtongoze Nasra kwani moyo unaniambia nimfanye mke wa tatu
Mpaka hapo ilikuwa ni saa tisa za usiku nilitoka mbio mpaka Rombo Hotel nilipofika nilikuta Charles hajafika nikasema kimoyo moyo \imekula kwako nikuachie mtoto mzuri kama huyu.
"Twende nyumbani Nasra,
"Kuna nini?
"Kuna maongezi unatakiwa ushiriki,
"Maongezi gani?.
"Twende utayajuwa huko,,
"Sawa,
Niliondoka naye ile tunafika chini nikakutana na Charles na yeye anakuja kwa nasra jicho alilikodowa akashindwa kuelewa nini kinaendelea,,
"Vp side?..
"Poa,
"Charles twende zetu ingia kwenye gari,
Charles aliingia kwenye gari tukaanza safari ya kurudi nyumbani..
nilipoingia ndani nilishangaa kumuona shamira akiwa sakafuni akitoa mapovu mdomoni nilimkimbilia nikabaini yuko kwenye hali ya kukata roho,
Nilipogeuka upande wa pili na zahara ilikuwa hivyo nilichofanya niliwakimbiza hospital kuona kama nitaokoa maisha yao,
Tulipofika hospitali hiyo saa 10:45 alfajiri walianza kupewa matibabu ila ilipotimu saa kumi na moja kamili nilichungulia kujua ni kinaendelea huko ndani ila nilitahamaki kuona mgonjwa mmoja kati ya shamira au zahara amefunikwa shuka nyeupe mpaka juu kichwani ikiashira kuwa tayari mmoja wapo ameaga dunia nililia kwa uchungu mkubwa Nasra akaanza kunibembeleza pamoja na Charles,,
Saa kumi na mbili dokta alitoka chumba cha wagonjwa mahututi ili kuniambia maendeo ya wagojwa wangu,
"Poleni sana na vilevile hongereni kwa kuwahi kuwaleta wagonjwa hospital ila ni kwamba mmoja amefariki dunia naye ni shamira,
Nilipopata majibu hayo mwili uliishiwa nguvu nikadondoka chini nikapelekwa hodini nikapewa huduma ya kwanza kufika saa tano nilipata faham nikakuta Nasra yuko pembeni yangu machozi yakimtoka kwa wingi,
"Nasra vipi?.
"Safi,
"Charles yuko wapi tutoe taarifa za msiba wa A,
"Side, Charles amesindikiza msiba,
"Nasra naumia sana najihisi vibaya ila upande mwingine nashukuru mungu kwa kupona mke wangu Zahara maana nampenda sana mke wangu japo nilimuowa bila kumsudia nampenda sana mke wangu vipi hali yake?.
"Anaendelea vizuri..
Nasra alijibu kwa kwikwi ya kilio,
"Usirie nasra nakuvyokupenda nikikuona unalia naumia sana sipendi nikuone na uzuni..
"Sawa,
"Nasra nipeleke nikamuone Zahara,
"Side pumzika kwanza,,
Nilikaa kimya nikapitiwa na usingizi niliposhituka ilikuwa saa kumi kasoro,
Nilishangaa kumuona shamira mbele yangu nikahisi huenda ni mzimu wake nikamuuliza Nasra,
"Nasra unamuona shamira?
"Ndio,,
"Si walisema amekufa?
"Hapana hakufa,
"Ila?..
"Seif Zahara ndie aliyekufa dokta alichanganya majina,
"Unasemaje??...
Nilihisi kuchanganyikiwa nikaona maruweluwe nikasema hapana haiwezekani nilinyanyuka kitandani nikatoa dripu mkononi,
"Maiti yake iko wapi?.
"Wazazi wamekuja wakakodi ndege wakaipeleka ZANZIBAR kwenda kuizika na wanazika leo,
Nilitoa simu mfukoni nijalibu kupiga air port ofisini kwangu,
"Hallow kuna ndege ya zanzibar?.
"Ndio ila ina dakika tano itapaa,
"Izuiyeni nakuja nikatie tiketi tatu,,
"Sawa,,
Nilimpigia na Charles,
"Chande uko wapi?.
"Nyumbani,
"Acha ushenzi hauko ZANZIBAR?
"Niko ZANZIBAR.
"Wanazika saa ngapi?
"Saa kumi na nusu,
"Wambie wanisubili wasinizikie mke wangu,,
"Nitaanzia wapi?.
"Mpe simu baba mkwe,,
Akampa,,
"Baba mke wangu asizikwe kama mimi sipo,,
"Kwa sheria gani?.
"Wewe umemchukua hapa kwa sheria gani?.
"Usinieleze upuuzi side nina uchungu na mwanangu,
"Uchungu hata mimi ninao ni mke wangu tena yuko chini ya himaya yangu wewe unamchukua kama nani?
"Hayo ni yko na jeneza ndio linaondoka hivyo,
"Sawa,
Nilikata simu nikagairi hata kwenda msibani maana tayari wameenda kuzika,
Niliwaza nikateseka na mawazo hatimae baada ya miezi miwili niliwaowa Nasra na shamira tukaanza maisha mapya,,
Nasra na shamira walielewana utazani siyo wake wenza,,
Msababishaji wa kifo cha zahara aligundulika kuwa ni Juma akakamatwa akahukumiwa miaka 5 jera eti aliuwa bila kukusudia yote hayo mpaka kuhukumiwa hivyo ilitokana na kaka yake ambaye ni Mwanasheria kumsimamia kesi yake,
Baada ya miaka tano alitoka jera akakuta nina watoto watatu mkewe amenizalia wawili na Nasra mmoja,
Roho ilimuuma sana ila alinitafta na kuja kuniomba radhi na kunieleza kwanini alifanya vile,
Maisha ya wake wawli yaliendelea na wakaelewana na kila mmoja aliendelea na kazi yake mafanikio tukayapata utajiri ukaingia kwa kushirkiana na wake zangu wote wawili,,
The End
Mwisho ..
0 comments:
Post a Comment