Chombezo : Dunga Dunga
Sehemu Ya Tatu (3)
“Hata ya rafiki yako wa karibu?”
“Sina rafiki wa karibu zaidi ya mama yangu”
“Sawa. Naomba nikupe yagu. Kama uktokea kupata muda, naomba japo uniambie usiku mwema....lunch njema na hata asubuhi njema” Nilimwambia.
Akabaki akitabasamu.
ANGALIZO: Mnaosoma msipite kimya kimya. Ukimaliza kusoma kama umeipenda sema lolote kwani huo ndiyo ujira wangu wala sihitaji pesa yako ili niendelee kuweka hapa. Mtaji pekee ni Comment yako, Share na Like ambapo itasaidia watu wengi kuweza kuisoma.
Unajua nini kilitokea?
Hebu bashiri, niambie unahisi nini kitatokea?
Kwa kasi ya ajabu nikaondoka mhali hapo na kukifuata kiduka kilichokuwa pemben yetu na kisha kuomba karatasi pamoja na kalamu. Judith alikuwa akinisubiri mahali pale alipokuwa. Niliporudi, nikaanza kuiandika namba yangu ya simu na kisha kumgawia.
“Tutaonana” Aliniambia na kisha kuondoka mahali pale. Nilibaki nikiendelea kumwangalia tu, vijana wote ambao walikuwa wakituangalia wakabaki wakinishangaa hawakuamini kama kweli nilipata nafasi ya kuongea na Judith na kisha kutangulizana nae.
“Taratibu ndio mwendo. Mimi ndiye simba mwenda pole bwana” Nilijisifia na kuondoka mahali hapo huku Judith akiwa amekwishaingia getini.
*****
Kila siku nilikuwa nikimfikiria Judith, akili yangu haikuwa ikitulia, Judith alikuwa akinipelekesha kupita kawaida. Katika siku zote, siku hizo ndizo ambazo nilikuwa makini sana na simu yangu. Nilikuwa nikiisubiria simu ya Judith kupita kawaida.
Kila simu yangu ilipokuwa ikiita, nilikuwa nikifikiria kuwa ni Judith na nilikuwa nikitegemea kuiona namba ngeni simuni mwangu. Nilichoka na kukasirika kila nilipokuwa nikiangalia kioo cha simu yangu na kuziona namba hizo kuwa si ngeni simuni mwangu.
Siku zilikatika wala namba ya Judith haikuingia simuni mwangu. Sikutaka kukubali, kila siku nilikuwa nikielekea katika mtaa wao huku lengo langu likiwa ni kuonana na Judith na kumuuliza sababu za kutokunipigia simu na wakati namba yangu alikuwa nayo.
Kumuona Judith halikuwa jambo rahisi, alionekana kuwa mgumu sana kupatikana mtaani. Vijana wa mtaa ule wa Mapipa bado walikuwa wakiniona kwamba mimi ni miongoni mwa watu waliokuwa na bahati sana. Kitendo cha kuongea na Judith kilionekana kuwashtua.
“Unasemaje?” Ezekiel aliniuliza huku akionekana kushtuka.
“Ndio hivyo. Niliongea nae na nikampa namba ya simu” Nilimwambia.
“Amekupigia?”
“Bado. Tena naombea hivyo hivyo aendelee kuchelewa” Nilimwambia Ezekiel.
“Kwa nini?”
“Nitamlalamikia katika hali ambayo hata yeye mwenyewe atanionea huruma” Nilimwambia Ezekiel ambaye akabaki akicheka tu.
“Wewe mkali. Nimeamini kwamba wewe mkali” Aliniambia.
Bado nilikuwa nikiendelea kumfuatilia Judith mtaani kwao lakini bado hakuonekana. Nilikuwa sina raha kabisa, Judith akaonekana kuanza kuuteka moyo wangu kupita kawaida. Siku bado zilikuwa zikiendelea kwenda mbele, Judith hakuonekana machoni mwangu na wala simu yake haikuingia simuni mwangu.
Naikumbuka siku hii. Nilikuwa nimetoka kucheza mpira. Uchovu mwingi ulikuwa umenipata kiasi ambacho baada ya kuoga nikaamua kutulia kitandan huku nikiangalia televisheni. Simu yangu ambayo ilikuwa pembeni kabisa ya kitanda ikaanza kuita.
Niliiangalia simu ile, nilionekana kukasirika, sikutaka kabisa kupokea simu katika wakati huo. Kwa kutotaka kelele nikaunyoosha mkono wangu na kuivutia kwangu. Macho yangu yakaelekea katika kioo cha simu, namba ilikuwa ngeni simuni mwangu. Kwa haraka haraka nikaipeleka sikioni.
“Halloooo....!!” Sauti ya kike ilisikika simuni.
Niliuhisi mwili wangu ukipigwa na ganzi, sikutegemea kupokea simu kwa wakati ile kutoka kwa msichana ambaye sauti yake ilikuwa ikivutia namna ile. Jina la Judih likaanza kujiandika kichwani mwangu, kwa mbali nikaanza kutabasamu huku ule uchovu ukionekana kunitoka.
“Hallooo...!” Niliitikia huku tabasamu likionekana usoni mwangu.
“Naomba unisamehe kwa kuchelewa kukupigia” Judith aliniambia.
Kichwani mwangu sikuona sababu yoyote ya msichana mrembo kama Judith kunimba msamaha, nilina kwamba alikuwa na sababu zote za kuchelewa kunipigia simu kutkana na urembo wake.
“Usijali. Kawaida tu japokuwa ulinifanya kutokujisikia fresh” Nilimwambia.
“Nafahamu na ndio maana nimekuomba msamaha. Nyumbani wananibania sana yaani hata sipati muda wa kutoka nje” Aliniambia.
“Urembo wako ndio unasababisha yote hayo Judith. Kama ungekuwa msichana wa kawaida....nafikiri wala usingezuiliwa kutoka nje” Nilimwambia Judith ambaye nilikisikia kicheko chake cha chini.
“Usinidanganye”
“Kweli Judith. U msichana mrembo sana, nafikiri kama sitoweza kukuaminisha hili, moyo wayo wangu ungesikia hukumu” Nilimwambia.
“Ila si mrembo kama msichana wako”
“Msichana wangu! Msichana yupi?”
“Huyo uliye nae”
“Yupi?”
“Kwa hiyo unataka kunidanganya kwamba hauna msichana?”
“Nitamtoa wapi? Bado sijamuona msichana wa kuwa nami” Nilimdanganya kama kawaida yangu.
“Aahahah...unanidanganya”
“Huo ndio ukweli Judy. Nahitaji msichana aliyetulia kama ulivyo. Sitaki kuchukua msichana atakayenifanya nijute” Niliendelea kumdanganya.
Kama umeipenda na unataka nikutumie simulizi hii WhatsApp, nitumie ujumbe WhatsApp kwenda 0712988278 andika "DUNGA DUNGA." Nitakutumia sasa hivi kwa bei ya ofa.
ANGALIZO: Mnaosoma msipite kimya kimya. Ukimaliza kusoma kama umeipenda sema lolote kwani huo ndiyo ujira wangu wala sihitaji pesa yako ili niendelee kuweka hapa. Mtaji pekee ni Comment yako, Share na Like ambapo itasaidia watu wengi kuweza kuisoma.
Unajua nini kilitokea?
Hebu bashiri, niambie unahisi nini kitatokea?
“Sawa. Tafuta, unaweza kumpata”
“Natarajia kumpata. Niko kwenye harakati za kumwambia ukweli”
“Safi sana. Nani huyo? Unaweza kunionyeshea ili nimjue wifi yangu?”
“Sawa. Unataka lini nikuonyeshee?” Nilimuuliza.
“Hata kesho”
“Utapata muda wa kuonana nami?”
“Nafikiri”
“Utaaga vipi nyumbani?”
“Niachie mimi ila ningependa uniambie utakuwa wapi na wifi yangu huyo”
“Kama itawezekana njoo Manchester Bar”
“Bar?” Aliniuliza huku akionekana kushtuka.
“Ndio”
“Sijazoea kuingia bar”
“Sawa. Basi njoo katika frmu zile za kutengeneza mikate katika msikiti wa Kichangani”
“Saa ngapi?”
“Muda wowote ule”
“Sawa. Basi tufanye saa nane. Nafikiri nitapitia huko nikitoka kumtembelea shangazi”
“Sawa. Utanikuta”
“Ila uwe nae mahali hapo”
“Sawa. Nitamwambia. Ila hii ndio simu yako?”
“Hapana. Hii ni simu ya mama. Usijaribu kupiga hata simu moja” Aliniambia.
“Sawa” Niliitikia.
“Usiku mwema”
“Na wewe pia mrembo” Nilimwambia, akatoa kicheko cha chini na kisha kukata simu.
Nilishusha pumzi ndefu, sikuamini kama kazi ingekuwa rahisi namna ile. Ni kweli nilikuwa nimetembea na wasichana wengi sana na kama ningeamua kumuonyeshea wifi zake, angechoka. Nilipanga kwamba sikutaka kumuonyesa msichana yeyote yule.
Sababu kubwa ya kumwambia tuonane katika fremu za msikiti wa Kichangani ni kwa sababu kutoka mahali hapo mpaka nyumbani wala hakukuwa mbali. Nilitaka kumpeleka nyumbani ambako huko kila kitu kingefanyika na hata kuitoa bikira yake ningeitoa bila ya wasiwasi wowote ule.
Nilibaki nikitabasamu, kwa hatua ambayo nilikuwa nimeifikia ilinifanya kujiona kwamba mimi ndio kidume na wala hakukuwa na ksa lolote la kunipa jina la DUNGADUNGA. Niliendana sana na jina hili japokuwa wazazi walikuwa wamenipa jina zuri la Gideon.
Nikaamua kumpigia simu Ezekiel na kumwambia kile ambacho kilikuwa kimeendelea. Ezekiel hakuonekana kuamini, aliniuliza maswali mengi juu ya Judith ambayo yote nilimjibu kwa ufasaha mkubwa. Nikakata simu na kujilaza kitandani huku nikiisubiria siku ya kesho. Hebu jifikiri....Judith atatokaje kwangu.
*****
Usiku kwangu ulionekana kuwa mkubwa kuliko siku nyingine zote. Kila wakati nilikuwa nikimfikiria Judith ambaye kwa kiasi kikubwa sana alikuwa ameiteka akili yangu. Nilijilaza kitandani huku macho yangu yakiangalia darini, niliona muda ukienda taratibu sana.
Usingizi kwangu ukawa mgumu kupatikana. Nilijitahidi kujigeuza geuza katika kila upande lakini wala usingizi hakupatikana kabisa. Nikanyanyuka kitandani na kukaa kitako. Nikaichukua simu yake na kuanza kupekua majina. Nilipofika katika jina la Judith, nikatulia kwa muda huku nikiliangalia.
Nilibaki nikiwa na furaha, kuliona jina la Judith kulinifurahisha kupita kawaida. Jina lake lilikuwa zuri na hata yeye mwenyewe aikuwa mzuri pia. Nilibaki nikiliangalia jina lile zaidi na zaidi, nikaiweka simu pembeni na kulala.
Wala sikumbuki usingizi ulinipata muda gani, lakini nilipokuja kushtuka tayari ilikuwa saa mbili asubuhi. Kwa kuwa katika kipindi hiki kilikuwa kipindi cha likizo, nikaelekea bafuni, nikajimwagia maji na kisha kuanza kunywa chai.
Katika kipindi chote hicho nilikuwa nikiendelea kumfikiria Judith ambaye bado hakutaka kabisa kutoka akilini mwangu. Macho yangu wala hayakutoka katika saa yangu ya mkononi, mara kwa maa nilikuwa nikiiangalia mishare ya saa ile ambayo kwa siku ile ilikuwa ikienda taratibu kuliko kitu chochote kile.
Nikaanza kufanya usafi wa chumba changu pamoja na vitu mbalimbali, hiyo yote ilikuwa ni kutaka kuufanya muda uende kwa haraka. Nilimpenda sana Judith katika kipindi hicho, nilitaka kufanya nae mapenzi ambayo ndio ilionekana kuwa kiu yangu kubwa.
Neno ‘bikira’ likaanza kujengeka kichwani mwangu. Nikakumbuka kwamba pamoja na uzuri wake wote lakini Judith alikuwa na kitu kingine acha kujivunia, hiki kilikuwa bikira. Nilitamani sana kuitoa bikira yake ambayo ilionekana kuwa ngumu sana kutolewa na vijana ambao walikuwa wakiishi mtaani kwao.
Kila nilipokuwa nikiifikiria, nilibaki nikifurahia tu.
Muda ulizidi kwenda mpaka kufikia saa nane kasoro, muda ambao nikatoka na kuelekea katika femu za msikiti wa Kichangani. Wala sikukaa muda mrefu, kwa mbali Judith akaanza kuonekana machoni mwangu. Akili ilicanganyikiwa zaidi, uzuri wa Judith uinifanya kumkodolea macho huku nikionekana kutokuamini.
Si mimi tu nilikuwa nikimwangalia kwa kuvutiwa nae bali hata vijana wengine nao walikuwa wakimwangalia huku nyuso zao zikionyesha kuwa na mshangao wa kuuthaminisha uzuri wa Judith. Akaendelea kupiga hatua mpaka mahali pale ambako nilikuwa nimesimama.
“Umefika muda mwingi?” aliniulizas mara baada ya salamu.
“Hapana. Kama dakika tano zilizopita” Nilimwambia.
“Oooohh..! Pole kwa kunisubiria muda mrefu namna hiyo,” aliniambia huku akinionyeshea tabasamu ambalo lilinifanya kuchanganyikiwa.
“Asante. Usijali” Nilimwambia.
Sikutaka tuendelee kukaa mahali hapo, nikaanza kumwambia kwamba kwa wakati huo ulikuwa muda muafaka wa yeye kufika katika nyumba ambayo nilikuwa nikiishi. Japokuwa tulikuwa tumekubaliana siku iiyopita lakini kwa kipidi hicho akaanza kuonekana mgumu.
“Hapana. Tunaweza kwenda hata katika mghahawa wowote ule” Aliniambia.
“Mbona unataka kuunyong’onyeza moyo wangu?” Nilimuuliza.
“Kivipi?”
“Nimekusubiri kwa takribani masaa ishirini na nne, nimeandaa chakula nyumbani kwa ajili yako, halafu unaniambia kwamba hautaki kuja nyumbani. Kweli unanitendea haki hapo?” Nilimuuliza japokuwa hakukuwa na chakula chochote nilichokiandaa.
“Umeandaa chakula?”
“Ndiyo.”
“Kwa ajili yangu tu?”
“Ndiyo.”
“Inaelekea umejiandaa sana”
“Hapana. Ila nimejaribu kukuonyeshea ni kwa jinsi gani nauheshimu ugeni wako” Nilimwambia.
Kama unataka kuisoma simulizi hii yote WhatsApp nicheki kwenda namba 0712988278. Nitakutumia kwa bei nafuu.
Angalizo: Mnaosoma msipite kimya kimya bila kusema lolote. Ukimaliza kusoma toa maoni yako, Like pamoja na Share ili simulizi hii isomwe na wengi.
Unajua nini kilitokea?
Hebu bashiri, niambie nini kitatokea?
Judith hakuonekana kubisha tena, tayari nikamuona akianza kuelekea kibra. Nikaushika mkono wake na kisha kuanza kutembea. Ingawa kwa wakati huo nilikuwa nikiongea nae lakini kichwa changu kilikuwa kikiwaza mapenzi, hasa bikira ambayo alikuwa nayo.
Tulitumia dakika tano tukafika nyumbani, katika chumba changu ambacho wala hakikuwa na kiti zaidi ya kindana, kabati la nguo, televisheni na vitu vingine. Akabaki akikiangalia chumba kile huku akionekana kushangaa.
“Ila sitokaa sana. Nitakaa nusu saa tu” Aliniambia.
“Usijali. Hata ukitaka kukaa dakika tano, ruksa” nilimwambia kwani nilijua kwa vyovyote vile atakaa zaidi ya masaa mawili.
Nilichokifanya ni kuchukua albamu yangu, albamu tofauti kabisa na ile ya wachana mbalimbali na kisha kumgawia. Kila picha ambayo alikuwa akiifungua, nilikuwa peke yangu au nulikuwa nimepiga na ndugu zangu wa kiume.
“Hata wifi yangu haujamuweka. Roho mbaya hiyo” Aliniambia.
“Sikuwahi kumwambia kunipa picha zake” Nilimwambia.
Sikutaka kuendelea kukaa chumbani hapo, nikamuaga na kisha kwenda kununua chipsi, chakula ambacho niliamini kilikuwa kikipendwa na idadi kubwa ya wasichana. Niliporudi, nikauweka mfuko wa chipsi zie pembeni.
“Mbona ulisema kwamba chakula kipo?”
“Nilikudanganya tu. Niko peke yangu humu, nitawezaje kupika? Sijui kupika, labda ungenisaidia” Nilimwambia.
Mara baada kula, tukakaa kitandani na kuanza kupiga stori. Tulipiga stori nyingi, tukaanza kugusana katika miguso ambayo ilionekana kumchanya. Alibaki akiniangalia usoni na baada ya muda fulani akayaamisha macho yake na uanza kuuangalia kiganja cha mkono wangu ambacho kilikuwa kikikigusa kiganja chake. Macho yake yalionekana kutaka kuongea kitu fulani lakini sikujua sababu iliyompelekea kutokuongea chochote kile. Baada ya sekunde kadhaa, nikaanza kupanda juu zaidi na kuanza kuugusa gusa mkono wake. Bado alikuwa kimya, ukimya ambao ulinifanya niendelee zaidi na zaidi mpaka kufika kifuani mwake. Tamaa kali ya kufanya mapenzi ikanipanda katika kasi ambayo niliishangaa sana. Kifua chake kilikuwa kikinichanganya kupita kawaida. Kilikuwa kile kile ambacho wengi wetu hasa wapenda mapenzi tulikuwa tukikiita cha saa sita. Kabla sijafanya kitu chochote kile, nikayarudisha macho yangu usoni mwake. Alianza kubadilika na kuwa katika hali ya kimahaba zaidi. Sikuongea kitu chochote kile kwani tayari macho yake yalikuwa yakiniambia ‘Fanya chochote utakacho’ ****
Nilifanya mapenzi na wanawake wengi tena waliokuwa na figa mbalimbali lakini kwa Judith alionekana kuwa tofauti kabisa. Kila nilipokuwa nikikipitisha kiganja changu katika mwili wake, pumzi nzito za mahaba zilikuwa zikisikika kutoka kwake.
Nilichoamua kukifanya kwa wakati huo ni kuwa makini, kwa sababu nilikuwa na uhakika wa asilimia mia moja kwamba Judith alikuwa bikira, nilijiona kuwa na uhitaji wa kufanya mambo taratibu
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment