Chombezo : Upepo Wa Kisulisuli
Sehemu Ya: Nne (4)
Sikumjibu chochote zaidi ya kumuonesha ishara kwenye simu naye ni kama alibaini tatizo ikabidi aichukue na kuifungua kwenye meseji aliusoma ujumbe ule na pale pale nikamuona akiiachia simu na kuibeba mikono yake kichwani nikajua kazi imefika hivyo kwa kujikongoja hivyo hivyo nikamkumbatia na kumnong'oneza kitu sikioni mwake nikamshika kiuno na kuondoka naye eneo hilo la stendi kwani kwa tulichokiona kwenye meseji hatukuwa na jeuri ya kuendelea na safari kwani pamoja na kilichotokea nyuma wao walikuwa bado ni watu wetu. Tulichukua Bajaj na kuelekea hospital ya Rufaa Mbeya wenyewe wanaitambua kama HOSPITALI YA KANDA na baada ya kufika moja kwa moja kwa kupitia geti la dharura tuliingia ndani na kuelekea kule tulikoelekezwa. Tulipofika tulikutana na Mooren akiwa kainamisha kichwa chini kwa aibu ya michezo yao michafu, Evetha alimfuata na kumuuliza hali ya Johnson ikoje lakini kabla Mooren hajajibu chochote daktari alitoka na kuonekana kama kuna mtu anamtafuta na mara akamvuta pembeni Mooren kuna jambo waliteta kisha Mooren alituacha na kumfuata mtu mmoja aliyekuwa anaongea na simu na wote wakaja msobe msobe lakini yule mtu alivyotufikia alituangalia sana kwa zamu kisha akazama zake ndani.
"Mbona hapa kama sielewi elewi hivi kuna nini?"
Nilimuuliza Evetha.
"Huyo ndiyo bwana yao niliyekueleza jana."
Evetha alinijibu kwa kuninong'oneza sikioni.
"Sasa hapa unafikiriaje kuhusu tulivyotazamwa na hili jamaa?"
"Mimi mwenyewe nina wasiwasi kwa kuwa hili jamaa shughuli zake hapa mjini hazifahamiki lakini lina mpunga wa hatari."
"Mimi naona tuondoke tukajifiche sehemu ambayo Mooren na lile jamaa wasiweze kutuona."
Nikweli tuliondoka eneo lile maana mpaka muda huo hakuna taarifa yoyote ya Johnson kama yu hai au la maana kwa mujibu wa meseji ya Mooren ni kuwa mara baada ya kujua siri yake imevuja kuwa yeye ni shoga Johnson aliamua kunywa sumu ambayo aliifuata dukani baada ya kutoka hotelini pale kupakuliwa.
"Angalia kule Sultan."
Evetha alinitaka niangalie kule chini kwani muda huo sisi tulikuwa kwa juu karibu na geti la kutokea kwenye parking ya magari.
"Naona Johnson ameshatuacha angalia namna wanavyolia Mooren na mume wake pale na mwili ndo ule unaingizwa mochwari."
"Hata kama alikuwa shoga lakini alikuwa ni mume wangu wa machoni mwa watu, ucheshi wake tu sitamsahau Johnson."
Evetha alimwaga machozi yasiyo na ujazo ilibidi nichukue jukumu la kumtuliza maana niliona dalili za sauti kupaa na ilibidi nimsisitiza ajikaze.
" Niache nimlilie mume wangu Johnson."
Evetha alinisisitiza na kunisukumia pembeni na kutoka mbio kuelekea kule waliko wakina Mooren, sikuwa na jinsi zaidi ya kujificha pale kushuhudia kinachoendelea.
"Washenzi ninyi ndiyo chanzo cha mume wangu kujiua na ninawahakikishia kuwa nitawafanyia kitu ambacho hamji sahau maishani mwenu."
Mapovu ya Evetha yalipelekea yule fala kutoka eneo lile kama anaongea na simu na hapo ndipo nilipogundua ni lioga halina chochote hivyo nilishuka kutoka nilipokuwa na kumfuata kwa nyuma.
" Oya vipi unakwenda wapi sasa si mke wako kafariki? "
" Brother punguza uzito wa maneno yule si mke wangu mbona ni kidume kama wewe."
Alivyojibu vile alianza kuongeza mwendo ili anikimbie, hilo nililiona hivyo nikajiongeza mwenyewe. Nilimsogelea na kuwa naye sambamba.
" Ukiinua tu unyayo wako napiga kelele za mwizi hivyo kwa usalama wako mwenyewe tembea taratibu kwa kufuata maelekezo yangu, sawa!"
"Sawa kaka nimekuelewa."
Alijibu jamaa huyo, kwa namna alivyojibu nilijikuta nacheka kimoyo moyo nikifikiria namna ambavyo sisimizi kamdhibiti
paka.
"Brother ee naomba uniachie nitakupa chochote unachotaka maana mimi baba yangu ni kiongozi mkubwa wa kanisa so akijua kuwa mimi nacheza michezo hii hawezi kuniacha salama."
"Alaa kumbe, sasa nisikilize kwa makini hapa tulipo ni mguu kwa mguu mpaka kwenu nikaongee na wazazi wako tofauti na hapo nihitaji kiasi cha fedha muda huu."
"Niambie kiasi gani brother sasa hivi nikupe."
"Unafurahia unafikiri ni ya kitoto, kwanza hapa nilipo nina picha na video zote za michezo yako na wale vikaragosi wenzako na ili ubaki salama nahitaji kiasi cha shilingi milioni hamsini keshi bila hata sifuri kupungua."
"Aaahh kaka utaniua sasa kiasi hicho ni kikubwa sana kwangu nipunguzie kidogo."
"Okay tufanye hivi ndugu yangu, mimi nimekuachia bure kabisa sihitaji hata kumi yako unaweza kwenda tu."
"Sijamaanisha hivyo kaka mbona unasema hivyo sasa."
"Si umeona ni kiasi kikubwa sana kwako huwezi kulipa basi nenda tu halafu mimi nitajua video na picha hizi zitamfikiaje baba yako kabla ya kuziweka sokoni najua kupitia hizi nakuwa mtu mwingine kabisa."
"Kaka tufanye hivi leo nitatoa milioni thelathini kisha kiasi kilichobaki kesho mchana kutakuwa tayari na business card yangu hii hapa."
"Haina haja hapa nina namba zako zaidi ya nne tayari fanya masuala fasta nikabidhi check ya kiasi hicho muda huu na pia nikabidhi cash nje ya makubaliano kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kushughulikia msiba."
"Sawa kaka hiyo ipo hapa hapa hii hapa ihesabu na twende kwenye gari nikakuandikie check."
Nilihakiki kiasi kile baada ya kuhesabu na kuikuta imepungua kama laki mbili kwani ilikuwa milioni nne na laki nane,sikujali niliweka kitu mfukoni nikaongozana naye mpaka kwenye gari akapanda na kuandika check wakati akiwa ndani ya gari alinitaka na mimi nipande nikagoma akinigeuza kisusio? Nikampa ishara ya yeye kuendelea, alipomaliza alinikabidhi kisha nikampa ishara ya kuondoka. Aliponipa mgongo tu nikaita bodaboda na kuishia zangu na safari ikawa ndani ya Hotel moja iliyoko maeneo ya Soweto. Na kwa kuwa nilikuwa na simu ya Evetha niliitumia kumpigia simu Nancy.
"Haloo nani?"
"Ni Sultan hapa."
"Nani, Sultan uko wapi niambie nikufuate sasa hivi mpenzi wangu."
"Niko hapa KING'S HOTEL maeneo ya Soweto."
"OK, okay usiondoke nakuja sasa hivi baby."
Nancy alijibu kitu ambacho kilinifanya nibaki mdomo wazi kwa sababu ni Nancy huyu huyu ambaye siku za hivi karibuni alinivimbia kiasi kwamba hata mfanyakazi wa nyumbani kwake alimtimua kisa mimi 'why' leo? Sikuwa na jibu la moja moja.
" Brother naomba niache hapa hapa."
"Si uliniambia nikupeleke Soweto sasa mbona njiani?"
Dereva bodaboda aliuliza.
"Kaka kwani tatizo lako nini kama ni buku zako nakulipa haya mengine yaache kwa mhusika."
Niliona anataka kuingilia tawala binafsi nikamtolea uvivu.
"Samahani ndugu yangu nimekosa."
Aliomba radhi baada ya kugundua amevuka mipaka.
"Amani mtu wangu."
Nilitelemka maeneo ya Makunguru na kumlipa chake yule bodaboda na kushika njia taratibu kuelekea Soweto huku nikiwaza iwapo Nancy atafika pale King's na kunikosa kwa uongo wangu si nitamkosa moja kwa moja. Lakini nikajipa moyo kuwa atanitafuta hewani. Nikiwa natembea nikiwa nimejikunyata kwa baridi kali lililokuwa linapuliza bila breki mara simu iliingia, nikatoa na kuangalia mpigaji ni nani nikahisi anaweza kuwa ni Nancy lakini kuja kuiangalia ilikuwa ni namba ngeni kabisa ilibidi niipokee hivyo hivyo.
"Sultan umefanya nini sasa?"
Hakuwa mwingine bali alikuwa ni Evetha sikujua alimaanisha nini kwa swali lake.
"Sijakuelewa Evetha kwa swali lako."
"Hujanielewa si ndiyo?"
"Ndiyo."
"Okay sawa, uko wapi muda huu?"
"Niko mbali kidogo na hapo."
"Yaani wewe ni wa kufanya ulichofanya? Johnson ni rafiki yako achilia mbali kwa yale aliyokuwa akiyafanya lakini bado alikuwa bado rafiki yako kama siyo mimi niliyekung'ata sikio bado ungekuwa naye sambamba. Kwanini umetutelekeza hapa Hospitali?"
"Unajua nini Evetha?"
"Sijui kitu."
"Naomba usipaniki, nilikuja mara moja huku mjini kutafuta nguo ya kumsitiri marehemu namaanisha Sanda."
Nilimpiga kamba maridadi Evetha.
"Si ungesema ilikuwaje ukaondoka kimya kimya? Sijapenda ulichofanya Sultan."
"Nisamehe mtu wangu nilichanganyikiwa tu."
"Sasa usije huku hospitali tumetoka tumeelekea kwake tayari kwa majadiliano na ndugu zake namna mazishi yatakavyofanyika."
"Sawa sawa Evetha nitakuwa hapo muda si mrefu."
Nilikata simu ya Evetha na kuiweka mfukoni na wakati namaliza tu kuiweka sawa simu mfukoni mara wanatokea watu nisiowafahamu bila kuongea chochote walinishika na kunivutia kwenye gari yao aina ya Alteza nyeusi iliyokuwa mbele yetu na baada ya hapo iliondoka kwa mwendo wa kasi na kuelekea kusikojulikana. Sura zilizokuwa mle ndani zilikuwa ngumu hizo utafikiri ni wale wapigania Uhuru Msumbiji. Walinifunga kitambaa usoni nisione ninakoelekea.
"Jamani mbona mnanifanyia hivi nimewakosea nini?"
"Tulia wewe Mjusi utajua mbele ya safari, hauoni raha kupata lifti ya bure kabisa hii?"
Aliongea mmoja wao ambaye sura yake ukiiangalia utafikiri hakuzaliwa na binadamu kwani hata ukitaka nikusimulie ilivyo lazima nitachemsha kwa namna ilivyo.
"Lakini mimi sikuwaomba lifti na pia lifti gani hii ya kufungana fungana mikamba?"
"Unaongea sana ee."
Nilistukia nimepigwa ngumi nzito ya kwenye paji la uso na kupelekea kuangukia siti maana pale nyuma nilikuwa mimi na aliyenipa konde na dereva tu.
"Endelea kuongea Kimburu wewe."
Maneno haya niliyasikia kwa mbali sana huku nuru ikiyaacha macho yangu na kusababisha giza nene ambalo lilipelekea kupoteza fahamu zangu.
Nilikuja zinduliwa na maji ya baridi ambayo nilimwagiwa na lile jitu lenye sura mbaya.
" Unakata moto wakati sisi bado hatujalipwa nyambafu."
Aliongea hivyo na kunisindikiza na kofi zito la shavuni kisha likaondoka zake.
Japo nilikuwa na maumivu makali lakini nilijitahidi kuyakagua mazingira yale kwamba yaweza kuwa ni ya wapi lakini sikuweza kuyatambua. Ni harufu tu mbaya ya kichumba ambacho nilifungiwa ilikuwa mbaya sana kiasi kwamba kama wewe ni mjamzito nafikiri ungekuwa unao
mba msaada wa ndimu kila wakati na mbaya zaidi ilikuwa ni pembeni kidogo ulikuwa unapita mfereji wa maji ambayo bila shaka ulitokea kwenye choo ikiwa ni mikojo ndiyo ilikuwa ikitiririka hapo. Nikiwa naendelea kula harufu ya mle ndani, mara mlango ulifunguliwa na likaingia lile jitu na kunikabidhi simu.
"Ongea na watu wako hao haraka."
Niliipokea simu na kuiweka sikioni ili kumsikiliza aliyepiga ambaye alikuwa ni Nancy.
"Baby mbona hapa King's haupo, uliamua kunidanganya siyo?"
Sikuweza mjibu chochote Nancy na kwa kuwa yule mtekaji alikuwa nje nilichofanya ni kumtumia ujumbe mfupi tu.
"BABY NIMETEKWA NA HAPA SIFAHAMU NILIPO, NAOMBA MSAADA WAKO NA USIIJIBU HII SMS."
"Wewe Kimburu bado tu na Ole wako ufanye janja janja humo ndani."
Sura mbaya alinichimba mkwara.
"Asante hii hapa simu nimemaliza."
Nilimkabidhi simu na kisha nilimuuliza sababu ya kutekwa kwangu, lakini alinijibu kuwa hata yeye hajui lolote kwani kazi waliyopewa na bosi wao ni kuifuatilia na kunishika tu kujua sababu si kazi yao.
Nilivyojaribu kuvuta kumbukumbu za kutosha nikajua hapa hakuna mwingine zaidi ya yule mshenzi niliyempiga milioni tano kasoro laki mbili. Sababu wengine kama wakina mama Mwamvua wasingeweza fanya hivi nilivyofanyiwa kwani wao shida yao ni mapenzi tu na hapa ndipo nilipoyakumbuka maneno ya Evetha kuwa hawa watu wanaofanya mapenzi ya jinsi moja siku zote wana mitandao mikubwa sana na ni hatari sana. Na hapo ndipo nilipojikagua mfukoni kuangalia kitita changu cha fedha pamoja na ile hundi sikuwa na chochote walikuwa tayari walikuwa wameshachukua na hapo ndipo nilipojiridhisha ni yeye aliyeniteka.
"Mtoe nje mpenda kutaka vya watu huyo."
Niisikia sauti ya yule yule jamaa ikinitaka nitolewe nje.
Walikuja wale walioniteka na kuufungua mlango kisha wakanitoa nje na kunipiga minyororo mikononi na miguuni.
"Mfungeni kwenye mti ule pale nimfunze adabu mwanaharamu huyu."
Aliongea yule bosi wao ambaye kutokana na taarifa ya Evetha na niliyoyaona pale Rufaa huyu ndiye aliyekuwa akitoka kwa wakati mmoja na Johnson na Mooren. Na hapa nilianza kumuomba Mungu aniepushe na adhabu ya kuliwa tigo na hili jamaa na watu wake.
Baada ya kufungwa alikuja karibu yangu na kuanza kunishambulia kwa mijeledi ya nguvu, alinichapa sana kila sehemu ya mwili wangu, maumivu niliyokuwa nayasikia yalikuwa makali sana nililia nikiamini nitaonewa huruma lakini wapi ikawa kama ndiyo namwambia ongeza spidi ya kuchapa. Nilichapwa sana mpaka nguo zangu ziligeuka manyapu nyapu zikiwa zimechanika chanika huku zikiwa zimepambwa na damu.
"Una bahati sana hawa jamaa waliokuteka wamesema tusikuoe kwa kipindi hiki utakacho kuwa hapa."
Niliposikia maneno hayo ya kuolewa niliusikia mwili ukiishiwa nguvu. Nikajikuta natokwa na maneno.
"Naomba nisamehe kwa kila kilichotokea ndugu yangu."
"Nyoooko, wewe si ulisema ni mbabe na unataka hela zangu kutokana na kile ninachokifanya."
"Kaka zile zilikuwa ni njaa tu wala si kingine."
"Ili uepukane na dhahama hii ni wewe kunikabidhi video ulizosema unazo."
"Kaka ningezitoa wapi mimi hizo, ile ilikuwa janja ya kukutia presha tu ili utoe mkwanja."
Nilijikuta nagongwa na kitu kizito kichwani tena na kupelekea kupoteza fahamu.
Nilikuja kupata fahamu nikiwa katikati ya kundi la watu ndani ya uwanja wa zamani wa ndege.
"Mwenyekiti amezinduka tayari."
Nilimsikia mmoja akitoa taarifa kwa mtu aliyeitwa mwenyekiti kuwa nimezinduka. Na mtu huyo ambaye ndiye mwenyekiti alikuja na kupiga magoti pale chini nilipo.
"Habari yako kijana."
"Samahani naomba maji ya kunywa."
"Wewe Bi Habiba hetu tuletee maji ya kunywa ya shilingi elfu moja"
Mwenyekiti aliagiza niletewe maji kunywa.
"Hebu mfungueni hiyo minyororo aliyofungwa, akinywa maji mpelekeni pale kwangu akapate maji maana si kwa hali hiyo aliyonayo inatisha sijui kakutana na nini maana ni sura ngeni kabisa katika eneo letu."
Mwenyekiti ambaye nahisi ndiye kiongozi wa eneo hili la Airport alikuwa akitoa maagizo kwa wachini wake.
" Lakini mwenyekiti haya si yakuyaonea huruma ni kuyachoma moto tu."
"Hapana angekuwa ni jambazi au vyovyote vile angekuwa alishauawa na waliomtelekeza hapa."
Mwenyekiti alipingana na wazo la mmoja wa wajumbe wake.
"Basi mwenyekiti tutafanya kama ulivyoagiza."
Alikubaliana na wenzake.
Na muda huo maji yaliletwa pale nikapewa nikanywa na kisha walinifungua ile minyororo na kisha walinipeleka nyumbani kwa mwenyekiti na tukiwa njiani kuelekea nyumbani kwa mwenyekiti kuna mtu tulipishana naye njiani na alionekana kuniangalia sana kama ananifahamu hivi ila mimi nilimfahamu nilitamani kumsemesha lakini nikaona niachane naye.
"Nancy ina maana mimi ni kichaa kweli usinifanyie hivyo mimi si kichaa ni Sultan yule yule?"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment