Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

BWANA MIHAMALA - 1

 


IMEANDIKWA NA: DAMIANI CHIKAWE

*******************************************************

Chombezo :  Bwana Mihamala 

Sehemu Ya Kwanza (1)


Imeandikwa na *Mwl Damian Chikawe.*


Mvua ya rasha rasha ambayo haikutaka kuisha bado iliendelea kunyesha usiku ule na kusababisha mikusanyiko yote ya vijana kushindwa kuhudhuria kijiweni kama ilivyokuwa desturi yao ya kufanya hivo kila ifikapo majira ya saa moja usiku na kuendelea, licha ya mvua tu bado serikali imekataza mikusanyiko kwa kipindi hicho kwa sababu ya janga la corona. Shaibu ambaye alikuwa anafanya biashara za mihamala ya simu maeneo ya rangi tatu 'Mbagala rangi tatu' alikuwa mpekwe sana siku hiyo. Kwenye chumba chake hakukuwa na TV wala redio hivyo upweke kwake ulikuwa mkubwa mno. Mbaya zaidi hata umeme ulikatika siku hiyo hata ile simu yake kubwa ya kisasa 'smartphone' haikuwa na chaji. Maana angalau ingekuwa ina chaji ingeweza kumuweka bussy kidogo. Hakika bwana shaibu aliona usiku utakuwa mrefu sana. Katika chumba hicho Shaibu alikuwa anakaa peke yake, alikuwa bado hajaoa. Alichukua simu ili ampigie mmoja wa wapenzi wake ila akakumbuka kuwa hawapo karibu naye. Alikuwa na wapenzi wawili ambao wote kwa wakati huo walisafiri kwenda nje ya mkoa wa Dar es salaam kwa hofu ya janga hili baya la corona.


Shaibu alijilaza kitandani chali huku akitazama juu na asijue nini cha kufanya. Alijaribu kufungua game lililopo katika simu yake ndogo 'kiswaswadu' ambapo kulikuwa na game la nyoka. Hata hivyo haikumchukua muda akaachana nalo maana halikuwa na mvuto kabisa.


Akiwa bado anaendelea kuwaza na kuwazua ,kuna jambo lilimjia kichwani mwake. Akarudisha matukio ya mchana nyuma, akakumbuka wakati anahudumia wateja alikuja mteja mmoja mtoto wa kike . Alikuwa mrembo sana huyo msichana. Licha ya urembo wake , alikuwa mzuri sana. Alikuwa anavutia ukimtazama usoni au sehemu yeyote ya mwili wake. Shaibu alikumbuka mrembo huyo jinsi alivyokuwa anaongea kwa mapozi na huku akitabasamu kila mara.


Shaibu aliishia kutabasamu maana hakuwa na ujanja wa kuweza kumpata msichana huyo kwa wakati ambao alimkumbuka.


Katika kuwaza waza Shaibu alikumbuka jambo. Akachukua simu yake ya uwakala na akaanza kupekua mihamala yote aliyoifanya siku hiyo. Alikagua hadi akaukuta muhamala aliomfanyia mrembo ambaye alimkumbuka usiku huo.


Shaibu akatabasamu, kisha akachukua namba na kuingiza katika simu yake. Haraka haraka akampigia , simu iliita bila majibu. Akapiga tena bado mambo yalikuwa yale yale. Simu haikupokelewa. Mpaka nyakati hizo muda ulisomeka saa tatu kasoro dakika tano tu.


Shaibu akajisemea moyoni baada ya kuona simu haipokelewi


"Mmh au inawezekana akawa mke wa mtu yule, pengine wamelala sasa, mmmh lakini mbona mapema? Au pengine simu ameweka chaji? Au namba ngeni huwa hapokei? Mmmh nini shida sasa......"


Shaibu kila alichowaza hakupata majibu zaidi ya kuukumbuka tu urembo na uzuri wa mwanamke huyo. Alijaribu tena kupiga ila bado haikupokelewa. Matumaini yake ya kusikia sauti ya mrembo huyo ili angalau imliwaze kwa usiku huo yalianza kukatika.


Shaibu akaamka kitandani na kukaa tena kitako. Alienda maliwatoni kwa haja ndogo. Aliporudi alikutana na sms kutoka kwa mtu aliyempigia sana simu na hakupokea. Akaifungua na kukutana na ujumbe....


"Nani?"


Shaibu alivuta pumzi ndefu na kisha akaishusha chini. Akaingia haraka haraka uwanja wa meseji ili ajibu. Shaibu akaandika "Aaah umenisahau? au ushafuta namba yangu?"


Shaibu alianza kumwandikia kwa namna hiyo kana kwamba wanajuana vile ila ni mbinu zake tu.


Baada ya dakika moja ujumbe ukarudi

"wewe nani? Bila shaka utakuwa umekosea namba, mimi unanijua?"


Shaibu akajibu,

"Hapana sijakosea, wewe si

Irene?"

Shaibu alijaribu kutaja jina lake ili aone kuwa anamjua vizuri ,lengo likiwa ni kupata uraisi wa kuchati naye. Jina hilo alilipata kwenye muhamala uliobaki kwenye simu yake.


Ujumbe ukarudi

"hapana mimi si Irene, huyo ni mama yangu...."


Shaibu akashtuka na akapata jibu kuwa inawezekana wakati laini inasajiliwa alitumia kitambulisho cha mama yake. Akapoteza pointi ya kwanza Shaibu, akabakiwa na pointi mbili tu za kumfanya aendelee kuchati naye.


Shaibu akajikakamua..

."Sasa hapo mimi nimekosea nini? Nimeamua kuanza na jina la mama yako ili kumbukumbu zako zirudi nyuma na uweze kunikumbuka....naamini sasa ushanikumbuka, vipi naweza kukupigia tuongee? "


Ujumbe wala haukukawia kurudi kutoka kwa mtu aliyedhaniwa anaitwa Irene...


"Wewe huna lolote hilo jina utakuwa umeangalia kwenye usajili wa namba yangu....sasa sitaki nijue umepata wapi namba yangu wala nini sijui...wewe hunifahamu mimi na sitaki tena usumbufu wako....Nataka kupumzika sasa, usitume tena sms wala kunipigia"


Shaibu ikamfikia sms hiyo na mapigo ya moyo wake yakaenda kasi kama virusi vya corona. Akaiacha simu kitandani, akaishika tena na kuisoma sms hiyo. Wakati anafikiria zaidi akamkumbuka mwalimu wake wa saikoloji akiwa chuoni ambaye aliwaambia kuwa ..."hakuna kilima kisicho na kilele...,pata tabu kuupanda mlima ila ukifika kileleni utaserereka tu...."


Maneno haya yakamtia nguvu Shaibu , akaishika simu na kuingia tena uwanja wa meseji. Akaanza kuandika ili amtumie mrembo huyo.


Itaendelea........


*Akili za kuambiwa changanya na zako*


Wewe unatamani nini? Shaibu ampate huyo mdada au asubiri corona iishe na wapenzi wake warejee nyumbani?


*Upweke husababisha matatizo mengi sana, zipo namna mzuri za kudili na upweke, hvo kuwa makini pale unapohitaji kutafuta faraja la moyo ama tulizo la moyo*




Kijana anayeitwa Shaibu ambaye anafanya kazi ya miamala ya simu katika jiji la Dar es salaam anakutana na wakati mgumu wa upweke akiwa kwake nyakati za usiku. Hivo akaamua kufanya jambo ili aondoe upweke huo. Anapekua miamala aliyoifanya siku hiyo na kukutana na namba ya mrembo matata ambaye alifanya muamala katika ofisi yake.......


Je atafanikiwa kumtia nguvuni?


*Endelea....*


"Busara ni kumsikiliza mtu anasema nini hata kama hakikupendezi na uungwana ni kulitafakari lile akuambialo, haujajua hata nataka nikuambie nini lakini teyari umetoa maamuzi....ila poa naamini utanitafuta mwenyewe katika wakati ambao sitapatikana....si unakumbuka leo kuna sehemu umefanya muamala pale mbagala rangi 3?...."


Shaibu alijitutumua kwa kumkumbusha alichokifanya mchana ili angalau amfanye kuwa na 'Attention' juu ya amwambiacho.


Zilipita dakika kama thelathini hivi bila hata ujumbe huo kujibiwa. Shaibu alijigaragaza kitandani hadi akapitiwa na usingizi na kulala fofofo.


Kwa upande wa yule mwanamke, alijifikiria sana kuhusu jumbe alizokuwa anazipata kutoka kwa Shaibu. Aliwaza sana na baadae akajipa majibu mwenyewe kuwa yawezekana kuwa kweli kijana Shaibu atakuwa na jambo la kutaka kumwambia. Akaamua kuchukua simu yake na kumpigia Shaibu. Simu ya Shaibu iliita bila kupokelewa. Alipiga zaidi ya mara tatu lakini haikupokelewa. Shaibu alikuwa amelala fofofo hata muito wa simu hakuweza kuusikia. Dada huyo akahisi kuwa Shaibu amekasirika kwa sababu ya ujumbe wake wa mwisho wa kumtaka asimtafute tena.


Biti huyo moyo wake ukahudhunika sana, akaamua kumtumia ujumbe Shaibu,


"Samahani sana ..I'm very sorry, nilifikiri unaweza kuwa muhuni tu ndo maana nikajibu vile...Mimi naitwa Judy ,una shida gani?"


Ujumbe huo pia haukujibiwa. Hali hii ikamfanya Judy aendelee na program zake nyingine ila baadae naye akapitiwa na usingizi, akalala.


Shaibu alipoamka asubuhi na mapema kabisa , alienda maliwatoni kwa ajili ya kujiandaa ili aende kazini kwake. Baada ya kujiandaa akaishika simu yake , akakutana na sms pamoja missed calls. Akazifungua , alikuwa ni yule mrembo. Shaibu akashika kichwa na mdomo ukiwa wazi. Kisha akajilaumu kwa usingizi wake wa kama pono. Ilikuwa ni saa 12 kasoro kama dakika tano hivi asubuhi, palepale akaishika simu na kumpigia.


Simu iliita na kupokelewa kwa sauti yenye uchovu wa usingizi. Iliashiria wazi Judy bado alikuwa amelala. Shaibu alipoona hivyo ikabidi amwambie basi wataongea baadae akiwa ameamka.


Shaibu akaondoka na kwenda kazini kwake kama kawaida lakini huku akilini mwake akiwaza maneno mazuri ya kumwambia Judy pale watakapoongea vizuri.


Shaibu akiwa kazini kwake majira ya saa nne asubuhi simu yake iliita na jina lilikuwa ni Judy. Judy alimuuliza Shaibu lengo lake ni nini hadi akaamua kumtafuta. Shaibu alimwambia Judy ni vyema wakaonana ana kwa ana kwani si vyema kuongea kwenye simu. Judy alikubali ombi la Shaibu na wakapanga siku waonane.


Jumamosi ya wiki hiyo walikutana kwani ndio siku ambayo walipanga waonane. Shaibu alitupia pamba kali sana ambazo yeye mwenyewe alikuwa anaziamini akivaa basi hupendeza sana. Mtu wa kwanza kufika eneo la tukio alikuwa Shaibu hvyo wakati Judy anafika naye alipata kumuona tena vyema. Mapigo ya moyo wa Shaibu yalienda kasi sana baada ya kumuona Judy akiwa ana-drive gari yeye mwenyewe akifika sehemu hiyo. Mawazo yakampeleka mbali sana na kuamini kuwa Judy hakuwa type yake. Lakini alijikaza tu ,hadi wakakutana na kuanza kuongea.


Hata kabla hawajaendelea kuongea sana , Judy akamtadhaharisha Shaibu kuwa mazungumzo yasiwe marefu kwani hapaswi kuonekana sehemu kama hizo tena na mtu ambaye hausiani na ndugu zake. Mpaka muda huo Shaibu alikuwa hajui chochote kuhusu Judy na hata hofu ilimpata Shaibu. Kila alipojaribu kumwangalia Judy aliona ameachwa mbali sana hasa kiuwezo wa kifedha. Shaibu hakujua aanze wapi.


"Ongea basi haraka, mimi nataka niondoke, weekend leo bata linanisubiri....."


Judy aliongea kwa sauti ya madaha huku akitoa simu yake kwenye mkoba na kuanza kuichezea.


Kwa sauti ya hofu Shaibu alijikuta akimuuliza swali Judy...


"umenikumbuka?"


Judy alitikisa kishwa kuashiria kukataa hamkumbuki kabisa. Shaibu huku akijichekesha akamwambia kuwa yeye ni yule wakala ambaye siku kadhaa zilizopita alifanya muamala kwake.


Judy akadakia harakaharaka...


."kwa hiyo unasemaje? Nambie lengo lako ni nini?"


Shaibu akaanza kwa kujiuma jiuma maneno.


"Aaah kiukweli unajuaa....tangu siku ile....."


Judy akadakia hapo hapo

"Mbona kama huna cha kusema....?"


Wakati huohuo simu ya Judy ikaita , alivyoipokea akadanganya kuwa yupo kwenye party ya rafiki yake. Baada ya kukata simu, JUdy alionekana kuwa na hofu kubwa sana.Akamwambia Shaibu watoke eneo hilo na watafute eneo lingine la kujificha. Wakati huo wote Shaibu hakujua ile simu aliyopigiwa Judy ilitoka kwa nani na kwanini aliingiwa na hofu na kutaka watafute sehemu nyingine. Shaibu na Judy wakaingia ndani ya gari, gia ikaingizwa na kuondoka eneo hilo. Shaibu ndiye aliyekuwa anamwelekeza njia Judy. Pita hapa ....kunja hapo....ingia hapo.....Alafu nyoosha.....Hayo ndio baadhi ya maneno yaliyokuwa yanasikika ndani ya gari hilo kutoka kwa Shaibu. Shaibu alikuwa na akili zake kichwani, alikokuwa anamwelekeza nako anakujua yeye mwenyewe. Safari ilizidi kuchanja mbuga. Ndani ya gari hakukuwa na stori baina yao zaidi ya maelekezo tu ya wapi gari lipite kutoka kwa Shaibu.


*Itaendelea*


Kuna mengi ya kujifunza huko mbeleni......


Unajua Shaibu anampeleka wapi Judy? Je ni nani aliyempigia simu Judy? Kwanini hofu ilimpata Judy baada ya kupigiwa simu?


Majibu yanakuja sehemu inayofuata....usikose....




Shaibu na Judy wamefanikiwa kukutana lakini hakuna kilichoongeleka kwa sababu ya simu aliyopigiwa Judy kumtia hofu Judy . Shaibu na Judy wanaamua kutoka sehemu walipo na kwenda sehemu nyingine ambayo haitakuwa wazi ili wakajifiche. Muongoza njia ni Shaibu, na ndiye aliyejua anaelekea wapi. Judy hakujua kitu , akawa anafuata maelekezo ya Shaibu tu.


Songa nayo sasa.....


Walikatiza katiza mitaa kama mwendo wa dakika 30 hivi na mwishowe wakafika sehemu ambayo Shaibu akaamuru gari lisimame. Judy akasimamisha gari. Haikuchukua hata sekunde , Judy akashusha swali kwa Shaibu,


"Ndo wapi hapa....?"


Shaibu huku akionesha sura ya tabasamu, akamjibu hapo walipofika ndipo anapoishi.


"Aah sasa hapa tumekuja kufanya nini? Hebu tuondoke....."


Judy akadakia haraka haraka tena huku akiwasha gari na kuanza kurudi Riverse ili ageuze gari. Wakati hilo likiendelea , simu ya Judy iliita tena.


Judy akasimamisha gari, akalizima kabisa kisha akapokea simu. Kwa sababu ya utulivu wa eneo walilokuwepo Shaibu aliweza kuisikia vyema sauti ya aliyepiga simu.


"Nimeongea na rafiki zako wote wanasema haupo nao...wewe upo wapi?"


Sauti yenye ukali ilimuuliza Judy. Judy akaanza kubabaika kujibu. Alijitetea kuwa ni rafiki yake ambaye walisoma naye wakiwa chuo na walikutana wiki moja tu nyuma ndio wakabadirishana namba ndio maana hakumtambulisha rafiki huyo.


"Sasa kwanini umetoka haujaniaga? Huu ndio utaratibu wetu?"


Baada ya maelezo ya Judy , akaulizwa tena kwa ukali sana. Judy akajitetea tena kuwa alitoka ghafla na alipanga akifika huko atamtaarifu.


Sauti ya kushuka isiyokuwa ya ukali ikajibu...


"Sawa ila siku nyingine nitaarifu mapema....kuwa makini .....See you later"


Hapo simu ikakatwa na kisha Judy akashusha pumzi ndefu sana , kisha akasema huku akimwelekeza kidole Shaibu.


"Wewe unataka kunitia matatizoni"


Shaibu muda wote huo alikuwa hajui Judy anaongea na nani na kwanini anaonekana kuchanganyikiwa huku akimdanganya sehemu ambayo yupo.


"Vipi kwani ni nani ulikuwa unaongea naye?"


Shaibu alimuuliza Judy.


Judy huku akiupinda mdomo wake na kuonyesha sura ya kulipotezea swali aliloulizwa akasema.


"Aaah tuachane na haya....basi ongea hapahapa tukiwa garini ili niwahi kurudi nilikotoka..."


Shaibu akapiga muayo wa kujilazimisha kisha akamshawishi Judy akapaone anapokaa. Kwani kutoka walipo ni mbele tu ya gari yao yaani ukitazama mbele unaona nyumba. Ilikuwa ni nyumba ya wapangaji, haikuwa kubwa sana wala nzuri kivilee ilikuwa na vyumba vinne na kila chumba kilikuwa na mpangaji. Vyumba vyote walikaa mume na mke isipokuwa kwa Shaibu tu ndiye ambaye alikuwa bado hajaoa.


Judy hakuwa teyari kuingia ndani ila Shaibu alikuwa king'ang'anizi .


Hatimaye baadaye Judy akakubaliana na ombi la Shaibu. Wakalisogeza gari karibu na wakalipaki sehemu. Wakashuka wakaingia ndani.


Wapangaji wenzake ambao kwa wakati huo walibaki wanawake tu kwakuwa waume zao walikuwa kwenye miangaiko waliyatumbua macho yao wakimwangalia Shaibu akiwa na mrembo matata sana. Shaibu akawasalimia kisha akakatiza na kuzama ndani.


Akafungua chumba chake ambacho kilikuwa shagalabagala yaani ovyo ovyo hata kitanda hakikutandikwa na nguo zake nyingine zilikuwa chini ovyoovyo. Yaani kila kitu hakikuwa katika mpangilio.


Shaibu akamkaribisha mgeni wake , na wakati huohuo akaanza kutandika kitanda na kuokota nguo zilizokuwa chini na kuziweka vizuri.


Hakukuwa na kiti ndani ya chumba hicho zaidi ya kitanda na meza tu. Hivyo baada ya kutandika vizuri ndipo akamwambia Judy akae kitandani maana bado alikuwa amesimama.


"Nisamehe sana, si unajua naishi mwenyewe tu hapa kwa hiyo hata kupanga vitu vizuri naona uvivu sana, karibu sana..."


Muda wote huo Judy hakuongea kitu zaidi ya kuonesha sura ya mfadhaiko kisha akaketi kitandani.


Akaitoa simu yake kwenye mkoba na kuanza kuichezea tu. Shaibu alikuwa anamsoma tu Judy ambaye alikuwa kimya kabisa kwani tangu waingie ndani humo Judy hakuongea neno lolote.


Shaibu akatoka nje ya chumba kisha baada ya muda mfupi tu akarudi na maji kwenye chupa ya lita moja na nusu. Bila shaka aliyanunua dukani. Akachukua bilauri na kujaza maji kisha akamkaribisha Judy.


Judy akatingisha kichwa bila hata kusema lolote na akayachukua hayo maji. Hata hakuyanywa akayaweka kwenye meza na kuendelea na kuchezea simu.


Shaibu ndiye aliyekuwa anahangaika tu mara ashike hiki mara kile mara anamwongelesha stori Judy lakini Judy aliishia kutingisha kichwa tu.


Shaibu hakutaka kumwambia lolote Judy linalohusiana na mapenzi ingawa kichwani mwake hilo ndilo alilokuwa analiwaza. Shaibu aliamini kuwa kwakuwa amekubali kuingia ndani mwake basi hawezi kutoka salama.


Judy akawa kama anawaza kitu hivi, dakika moja mbele akanyanyuka kitandani alafu ghafla tu akasema,

"Asee kwa heri...tutaonana siku nyingine"


Akafungua mlango na kutoka nje kabisa. Akaingia garini . Shaibu hakuamini kama Judy angeweza kuondoka, ila alishuhudia gari likiwaka teyari kwa kuondoka. Shaibu akarudi chumbani na kujilaza kitandani huku akiangalia juu. Alijilaumu sana kwa ngoja ngoja zake ambazo ziliishia kumuumiza tumbo.


Hata kabla Judy haijaingia barabarani akiwa palepale alihisi maumivu ya tumbo ghafla labda pengine ni tumbo la hofu ya kuhofia mtu aliyepiga simu. Akalizima gari na kurudi tena chumbani kwa Shaibu. Shaibu alisikia mlango unagongwa, akafungua na kumuona Judy akiwa kashika tumbo ,


"Nioneshe choo"

Judy alisema.


Haraka, Shaibu akampeleka chooni. Baada ya dakika tano, Judy akarudi chumbani kwa Shaibu.


"Nasikia maumivu ya tumbo naomba , nijilaze kidogo baada ya muda nitaondoka..."


Hilo ombi halikuwa na kipingamizi kwa Shaibu, ni kama Kagere kaachiwa kipa tu alafu unamuuliza utafunga gori?


Judy akajilaza kitandani kifudifudi huku akiwa ameshika tumbo lake. Aliugulia mwishowe palepale alipitiwa na usingizi.


Shaibu alikuwa anamtazama Judy kwa uchu mkubwa hasa kwa jinsi alivyojilaza na kuyaacha makalio yakiwa juu kama mama mwenye ujauzito.


Shaibu Alipoona Judy amelala akachukua simu ya Judy na bahati ilioje haikuwa na Nywira 'password'. Cha kwanza kuangalia 'Call history' ili amuone yule aliyepiga simu ni nani.


Alishtuka sana baada ya kuona jina la mtu huyo aliyekuwa anampigia na kumuuliza yuko wapi. Akaangalia na sms zake walizokuwa na wanachati huko nako alibaki mdomo wazi. Alivyofika kwenye upande wa picha , picha nazo zilimshtua sana. Shaibu akabaki anaguna tu 'mmmmh'

Wakati huohuo Judy akajitingisha tingisha kuashiria anaamka.


*Itaendelea....*


Shaibu kapata penalty ndani ya dakika za lala salama....Je unadhani atapaisha au ataweka wavuni?


Ni kweli Judy alikuwa anaugua tumbo au kaamua tu kurudi tena kwa Shaibu? ?


Kuna jambo amegundua Shaibu kwenye simu ya Judy.....ambalo linaonesha sio jema mpaka linamfanya agune .....Ni jambo gani? Ameona jina gani ? Unadhani shaibu na Judy wapo sehemu salama?


Tuwe pamoja sehemu ijayo....ili tujue hatma ya wawili hawa.....


Mabaharia naona mnaona kama Shaibu anazingua vileeee.....????????


*Itaendelea*




teyari Shaibu amefanikiwa kumuonesha Judy nyumbani kwake...Kuna jambo lipo kichwani mwa Shaibu ambalo amepanga kulifanya kwa Judy.....Shaibu anagundua kitu kutoka kwenye simu ya Judy, Kuugua tumbo kumefanya Judy aendelee kubaki chumbani kwa Shaibu jambo ambalo ni kama ushindi kwa Shaibu....


*Songa nayo hapa....*


Shaibu alimuona Judy akijitingisha akajua atakuwa anataka kuamka hivyo akarudisha simu harakaharaka mahala alipoitoa na kutulia pembeni.


Judy akaamka na akaketi kwenye kitanda huku akionesha yu mchovu sana. Alimuomba maji ya kunywa Shaibu na kupatiwa kisha akayanywa.


Shaibu alionesha kujali kwa kumpa pole Judy na kisha kumuuliza kitu gani hasa kilikuwa kinamsibu. Judy alieleza kuwa hakujua tatizo nini ila alisikia tu maumivu ya ghafla kwenye tumbo lake hasa maeneo ya chini ya kitovu.


Judy alimuaga tena Shaibu kwa ajili ya kuondoka kwani teyari muda ulikuwa umeenda sana na teyari mishale ya saa ilikuwa ikisomeka saa tisa ikienda saa kumi jioni.


Judy akasimama na kumuomba Shaibu amfungulie mlango ili aondoke. Shaibu akashika kitasa cha mlango na kuufungua, hatua moja tu ndio aliyoinyanyua Judy, akahisi kizunguzungu....Mikono yake ikatua mabegani mwa Shaibu ili kupata balance ya kusimama maana alitaka kuanguka.


Shaibu akaufunga mlango. Akageuka upande wa nyuma na kumshika mabegani Judy huku akimpa pole na kumwambia inatakiwa aendelee kupumzika na hakuwa na sababu ya kuondoka kwa wakati huo.


Mikono ya Judy ilikuwa mabegani kwa Shaibu na mikono ya Shaibu ilitalii mabegani mwa Judy. Dakika moja ya ukimya ilipita wote wakiwa wanatazamana na hakuna aliyetoa sauti.


Shaibu akaishusha mikono yake hadi kiunoni mwa Judy kisha akamrudisha kitandani na kumketisha juu ya kitanda. Bado ukimya uliendelea kutawala miongoni mwao. Ni vitendo tu ndivyo vilikuwa vinafanyika.


Miili ya binadamu inapokaribiana hasa yenye jinsia tofauti huwa inatoa mwitikio ambao sio lazima mdomo useme. Hakuna aliyemwambia mwenzake afanye hiki au kile kwa wakati huo.


Wote miili yao ilitoa mwitikio, walijikuta wote wawili wakiwa juu ya kitanda. Teyari nguo zao walizokuwa wamevaa zilikuwa zimezagaa ndani ya chumba hicho. Walibaki watupu kama azaliwavyo kitoto kichanga. Uwanja ulionekana mdogo kwani kila mchezaji alitaka kujionesha anajua kuuchezea mpira kuliko mpinzani wake.


Kwenye uwanja huo, kulikuwa na wachezaji wawili tu, kipa pamoja mshambuliaji. Kipa alijitahidi sana kuokoa michomo mikali kutoka mshambuliaji , ilikuwa ni piga nikupige. Pambano round ya kwanza lilimalizika kwa mshambuliaji kuachia shuti kali la kiufundi lililoingia moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa akiwa hoi amelala chali.


Judy alionekana wazi kuufurahia mchezo, yawezekana ilikuwa surprise kwake. Sura yake ilitoa majibu tosha kuwa ame-enjoy kwani ilionesha kutabasamu.


Sasa wote walikuwa marafiki, hawakuogopana tena.Walichekeshana hapo kitandani hata yule Judy akasahau wazo la kwenda kwake.


Baada ya muda kupita Sura zikaambiana kuwa mapunziko yamekwisha, timu ziingie uwanjani tena kuendelea na mtanange. Mtanange uliendelea ,sasa kwakuwa walishasomana vyema kwenye mchezo wa kwanza basi hapo wakaonana kama vitoto vya bata vile. Vikawa vinaogelea juu ya bahari huku vikio sauti za furaha.


Mchezo ulienda vyema, kila mmoja aliridhika na matokeo aliyoyapata hakuna aliyemlaumu refa wala kiwanja kibovu.


Mpaka wakati huo teyari giza lilianza kuingia, majira yalisomeka saa 12 ikieleka saa moja moja hivi usiku. Judy na Shaibu wote wakaingia mariwatoni kwenda kuoga. Kama ungekuwa unawaona wakati wanaingia chooni basi ungedhani ni mume na mke lakini haikuwa hivyo.


Walipomaliza kuoga ikabidi watoke kwenda kutafuta chakula nje ya nyumba kwani Shaibu alikuwa hapiki hivyo hapakuwa hata na vyombo vya kupikia chakula.


Kwa muda mfupi tu walianza kuzoeana. Hata wakati wanakula chakula kuna muda walikuwa wanalishana.


Walipomaliza kula wakarejea tena kwa Shaibu. Sasa wakati mishale ya saa ilisomeka saa mbili usiku na dakika zake. Judy alisahau kabisa kama alihitajika kurudi kwake, naye akajiona wa hapohapo. Shaibu kwake yeye hata hakumkumbusha suala la kwenda kwake kwani kwake yeye ni kama fursa.


Uwanja uliwapendeza kila wakiutazama. Waswahili wanasema palipo na moshi ndipo panapowaka moto. Nyoyo zao zikawaambia waende tena uwanjani kuucheza mchezo. Walianza na kupasha misuli' walifanya mazoezi meepesi mepesi' ili kuiweka miili yao teyari kwa mchezo.


Wakaingia uwanjani na kuucheza mchezo vyema. Walipomaliza hapo hapo usingizi uliwachukua wote wawili, wakalala fofofo.


Baadae sana, usiku wa manane , Shaibu aliamshwa na kelele za simu ambayo ilikuwa inaita wakati huo. Ilikuwa simu ya Judy, Judy alikuwa bado amelala pengine alikuwa anachanja mbuga na ndoto wakati huo. Shaibu akashuka kitandani na kuishika simu ya Judy.


Kama kawaida jina lilikuwa lilelile la mwanzo. Jina hilo lilisomeka....


"My hubby"


Shaibu akabonyeza kibatani cha kuweka ukimya 'silence' , simu ikaita hadi ikakata. Ikapigwa tena , pia ikawa vilevile.


Shaibu alipoangalia call history alikutana na missed calls kama 10 hivi zote zikiwa za huyo huyo My hubby. Alipoingia kwenye sms huko nako zilijaa sms zake.


"My dear...."


"Mbona hadi sasa hujarudi?"


"Uko wapi Judy. ...?"


"Nini kimekupata mke wangu?"


"Mbona haupokei simu wala haujibu sms zangu"


"Tadhali sana kama watu wamekuteka ....basi niambieni mnataka niwape nini ili mke wangu arudi....nampenda sana na sipo teyari kumpoteza kwa namna yeyote ile ....."


Shaibu akaangalia sms zote kisha akatabasamu huku akijisemea kuwa mwanaume mwenzake amepatikana siku hiyo.


Ingawa alijiambia hivyo ila sms ya mwisho ilimtisha sana , akaona jinsi mume wake anavyompenda Judy..Roho ya utu ikamwingia, akaamua kumwamsha Judy. Alipoamka akamwambia kuwa simu yake ilikuwa inaita. Judy alipoangalia alikuta ni mume wake, akachanganyikiwa sana na alipoangalia saa ilikuwa teyari usiku mwingi sana.


"Mamaa nimekwisha jamani....."


Judy alijikuta akitoa sauti huku akiendelea kukagua sms za mme wake. Shaibu kwake hakuwa na pressure sana kwani teyari alishajua ni mke wa mtu hata kabla hawajafanya lolote kwa wakati ule mchana Judy akiwa amelala wakati tumbo linamuuma aliona namba ya mtu huyo ambaye alihisi moja kwa moja atakuwa mume wake.


Judy akatoka kitandani haraka na kuvaa nguo zake , baada ya hapo akataka atoke nje ili aondoke. Ila sauti ya Shaibu ndiyo ikamfanya asimame kumsikiliza.


"Subiri kwanza kabla hujaondoka kuna jambo nataka nikuambie....."

Shaibu alisema.


*itaendelea....*


Mke wa mtu na mpenzi wa mtu wamekutana....teyari wameshajuana vyema.


Hivi kosa lilikuwa la nani hapa????


Usikose sehemu ijayo kujua Shaibu atamwambia nini Judy usiku huo, je nini kitatokea ilikiwa Judy ataenda kwa mume wake usiku huo? Vipi mume wake aliyeahidi kumlinda kwa gharama yeyote akimjua bwana miamala Shaibu?


Ni balaaa ,yapo mengi ya kujifunza mbeleni huko.


Cha msingi....


*kabla hujatenda, fikiria matokeo.....*





Shaibu na Judy wameingia kwenye ulimwengu ambao pengine mmoja wapo hakuutarajia hasa Judy ila ukaribu wao ndio ukawafanya wafikie huko walikofika. Judy anajisahau chumbani kwa Shaibu mpaka anashtuka teyari muda ulikuwa umeenda sana yaani ilikuwa usiku wa manane.....Anaona bora aondoke muda huohuo ila Shaibu anamwita na kutaka kumwambia kitu....


*Sasa endelea hapa...*


Judy akasimama huku mkono wake mmoja ukiwa umeshika kitasa cha mlango. Shaibu akasema,


"Ngoja kwanza hebu utulie, mbona unakurupuka ? Una shida gani? "


Shaibu akajifanya hafahamu chochote, akamchota akili Judy.


"Naomba uniache ,tutaongea siku nyungine...."


Judy aliongea kisha akaanza kunyonga kitasa cha mlango. Shaibu akamsogelea Judy na kumshika mkono kisha akamleta kifuani pake huku akimuuliza nini kimemsibu na nani aliyekuwa anampigia simu kwa sauti ya upole na yenye kunyenyekea sana, sauti ambayo hata ukiwa umepaniki basi nawe utarudi na kushusha hasira zako.


Judy naye kwa upole akajibu,


"Huyu ni mume wangu, yaani sikutegemea kama tutafikia huku, umeniharibia Shaibu...."



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog