Search This Blog

Sunday, February 26, 2023

BWANA MIHAMALA - 2

  

Chombezo :  Bwana Mihamala 

Sehemu Ya Pili (2)


"Hapana sijakuaribia Judy , mimi sikujua kama una mume . Kama ningejua hata hapa tusingefika, lakini teyari maji yashamwagika tusijilazimishe kuzoa..tutazoa matope hapa...Mm nachokiona wewe lala hapahapa alafu kesho useme ulilala huko huko kwenye party ya rafiki yako ila ukienda sasa hivi mambo yataharibika zaidi....".


Shaibu alimbembeleza Judy huku akizidi kumpapasa mgongoni kimahaba. Judy alionesha tabasamu hafifu kwa mbaali kisha akamwambia Shaibu.


"Kulala hapa sawa inawezekana ila simu zake sijapokea wala sijajibu sms....unadhani itakuwaje ? Nitamwambia nini?...."


"....aaah hiyo ondoa shaka, wewe nenda kamwambie kuwa sherehe ilipopamba moto wote waliamua kuweka silence simu zao na wakaziacha chumbani kwa rafiki yake huyo....hivyo simu hukuwa nayo karibu....tena huku unampa meneno matam matam mbona ataelewa tu...."


Shaibu alimpa mbinu Judy na hakika Judy alionekana kuziamini mbinu hizo maana sura yake ilionesha tabasamu japo lilikuwa jembamba.


Wawili hao wakarudi kitandani na kuendelea na usingizi. Walilala mpaka asubuhi kisha asubuhi walipoamka pia walitoka pamoja.


Shaibu alishuka njiani na kwenda kwenye biashara yake huku Judy akiendelea na safari kuelekea nyumbani kwake.


******


Zilipita siku tatu bila hata wawili hao kuwasiliana. Shaibu hakujua kilichoendelea kwa Judy baada ya kufika kwao. Alitamani sana kujua lakini aliingiwa na hofu kumpigia simu Judy kwani alihisi pengine anaweza kuwa yupo na mume wake.


Ingawa alikuwa na hofu lakini bado nafsi yake ilikuwa na mshawasha wa kutaka kujua kilichoendelea na sio hivyo tu alianza kuukumbuka uzuri wa Judy.


Shaibu aliamua kwenda kwa rafiki yake anayeitwa Muki ili kumpa mchongo wa Judy. Alipofika kwa rafiki yake huyo akamweleza kila kitu kuhusu Judy kuanzia mwanzo hadi mwisho.


Muki alimsikiliza kwa makini bwana Shaibu na mwishowe akamtadharisha kuwa hapaswi kumtafuta hata kwa sekunde moja kwani teyari kosa alishalifanya hivyo hapaswi kufanya kosa tena.


Shaibu alipata ushauri huo kutoka kwa Muki lakini Shaibu ni kama alikuwa na kitu chake kichwani vile. Shaibu alidhani Muki atakubaliana naye na wote watakuwa kitu kimoja.


Shaibu alipoona hivyo akaamua kuagana na rafiki yake huyo kisha akarejea nyumbani.


Akiwa chumbani kwake bado Shaibu aliendelea kumkumbuka Judy na alitamani kusikia hata kwa sekunde moja tu sauti ya Judy ili ajirizishe kuwa yu salama.


Shaibu akaishika simu yake na kulitafuta jina la Judy. Alipoliona akatafakari atume sms au apige na kwa wakati huo majira yalionesha saa moja usiku.


Akaamua kutuma sms.


"Habari..."


Zikapita dakika kumi, sms haikujibiwa. Shaibu akajiuliza itakuwa tatizo gani limetokea au ndio kusema wapo pamoja na mume wake.


Wazo la mume ndio wazo ambalo Shaibu hakutaka kulipa nafasi. Akashika tena simu akatuma sms nyingine.


"Habari Judy...."


Zikapita dakika kumi zingine sms haikujibiwa.


Sasa Shaibu akasema liwalo na liwe akashika Simu akapiga .....


"Tiiiii......tiiiiii.....tiiiii.....tiiiii"

Simu iliita hadi ikakata, hakuna aliyepokea.


Shaibu akawaza kisha akajipa majibu mwenyewe kichwani mwake kuwa pengine namba zoote zilifutwa kwenye simu na mume wake hivyo Judy hakuijua namba yake. Akaamua kujitambulisha.


"Hello mimi Shaibu....tafadhari pokea simu"


Sms ikaenda na akapiga na simu lakini hakukuwa na majibu yoyote.


Shaibu akakata tamaa ya kumsikia tena Judy. Akaachana na simu kisha akaendelea kufanya mambo yake mengine hapo chumbani.


Baadae kidogo akajibiwa sms.


"Safi , upo wapi sasa hivi?"


Shaibu akatasamu alipoona sms kutoka kwa Judy. Akajibu harakaharaka.


"Nipo home hapa..."


"Vipi tunaweza kuonana muda huu?"


"Wewe tu mimi nipo tu om...."


Shaibu akajibu bila wasi huku akiwa amesahau kama anachati na mke wa mtu.


"Unajua ile mitaa mimi nimeisahau kabisa hivi mtaa gani vile?"


Shaibu akamwelekeza mtaa kwa ufasaha kabisa yaani hata mgeni huwezi kupotea. Kamwelekeza hadi nyumba anayoishi tena akampa hadi ramani ya chumba chake.


Shaibu sasa alifurahi sana akajiona shujaa. Akapanga vitu vizuri chumbani kwake teyari kwa kumsubiri Judy.


Dakika 40 mbele, mlango wa chumba chake uligongwa. Shaibu akatabasamu akajua teyari Judy amekuja. Haraka sana akasema,


"Ingia mlango haujafungwa...."


Mlango ukafunguliwa na wakaingia watu wawili wote wakiwa wamevaa baibui.


*itaendelea*


Hakuna aliyejua kilitokea nini Judy alipoenda kwa kwake....na sasa kuna watu wawili wameingia chumbani kwa Shaibu....je mmoja wapo ni Judy? Kama ni Judy kafika na nani?


Nini kitatokea hapo chumbani? Sehemu ijayo inatoa majibu usikose...


_Mwili hutoa mwitikio tofauti na ubongo, kuna wakati roho inasema hii sio sahihi lakini mwili husema ni sahihi_


Japo ngumu ila maamuzi yaliyofikiriwa katika bongo ni sahihi zaidi kuliko maamuzi yaliyofanywa na mwili.




Shaibu anapata mshawasha wa kutaka kujua kilichojiri kwake Judy baada ya kuachana naye. Maana zilipita siku tatu bila hata kujua nini kilijiri. Ingawa alikuwa na hofu, shaibu anaamua kumtafuta Judy na sms kutoka kwa Judy inakubali kukutana naye kwa siku hiyo. Mlango wa Shaibu unagongwa na Watu wawili wanaingia wakiwa wamevaa baibui......


*Endelea*


Shaibu akiwa amejilaza kitandani chali huku akiwa na uhakika wa aliyegonga mlango alikuwa Judy, alishtuka baada ya kuona wanaingia watu wawili tena wote wakiwa wamevaa buibui.


Shaibu akaamka kitandani na kusimama kisha katika hali ya kupaniki na mshangao akauliza,


"Akina nani nyinyi?"


"Tulia kijana...."


Sauti nzito kutoka kwa mmoja wa walioingia ndani alimjibu Shaibu. Sasa mapigo ya moyo wa Shaibu yakaanza kwenda kasi kama upepo wa baharini. Japo hakuiona sura ya aliyemjibu lakini teyari alijua atakuwa mwanaume.


"Hebu kaa kwanza kijana...."


Mtu mwingine kati ya wale wawili akakazia alichosema mwenzake. Shaibu akaanza kuhisi hali ya hatari , akasogea karibu na mlango ili akimbie , mmoja akawahi kuziba mlango na kusema kwa ukali sana,


"Kijana ukifanya mchezo, pumzi yako haina hata dakika 3 tatu mbele itakuwa teyari imeisha....Wewe tulia utusikilize sisi"


Sasa Shaibu akapata uthibitisho kuwa kweli watu hao hawakuja kwa wema bali shari.


"Nyinyi akina nani na mnataka nini?"


Shaibu aliuliza huku sura yake ikiwa inaonesha imejaa mashaka tele.


"Kijana bila shaka ushafahamu kuwa sisi ni wanaume japo tumevaa mavazi ya kike, leo tumekuja kwa heri , siku nyingine tutakuja kwa kinyume chake.....mkuu hebu endelea (mmoja akamaliza kusema na kumgeukia mwenzake"


"Sasa kijana leo sura zetu hautaziona ila kuna siku utaziona ukiwa utaenda kinyume na hili nitakalokuambia.....


Bila shaka unamfahamu vyema Judy...Judy ana mume ambaye ndiye mimi, nimegundua ukaribu wako na mke wangu...Mimi hata sitaki upoteze malengo yako maana nakuangalia nakuona bado ni kijana mdogo sana ambaye bado unastahili kuvuta pumzi hii ya Mungu, najua vijana wa sasa hivi mnajifanya mnajua sana lakini nakushauri usijaribu kuyakana maagizo yangu....kaa mbali sana na Judy atakupotezea malengo yako....I'm innocent but i'm a killer...over"


Shaibu alitaka kujitetea lakini akakatizwa na mmoja wapo.


"Kijana huu sio muda wa mdahalo kana kwamba tunatafuta mshundi vile, cha muhimu kuijua nafsi yako tu ifanye nini kati kufuata nililokuambia au kufuata nafsi yako inavyokutuma...ila ikikutuma kuendelea na Judy basi matokeo utayapata"


Mtu huyo akamaliza kuongea baadae akamgeukia mwenzake na kumwambia waondoke. Wakafungua mlango na kuishia zao.


Shaibu alibaki chumbani huku akiwa amechanganyikiwa sana . Akapata uhakika kuwa aliyekuwa anachati naye hakuwa Judy bali ni yule mume wako.


Mpaka dakika kumi zinapita bado mapigo ya moyo wa Shaibu yalikuwa yanaenda kasi sana. Akaamua kwenda kuoga maji ya baridi ili kupunguza pressure maana hata kijasho cheembamba kilianza kumtoka.


Alipomaliza kuoga alirudi chumbani na kuamua kulala, ingawa ilimchukua muda mrefu kupata usingizi ila baadae alipata usingizi.


Alikuja kushtuka asubuhi ambapo kama kawaida alienda kwenye shuguli zake za kila siku.


*******


Miezi mitatu ilikatika huku taratibu akiwa teyari kumbukumbu za Judy zikiwa zimetoka kichwani mwa Shaibu. Maana hawakuwa na mawasiliano ya aina yeyote baina yao na kama ilivyo desturi ya wasiowasiliana mara kwa mara huua ukaribu wao kwa haraka sana. Mawasiliano ndio chanzo pekee cha kudumisha upendo kwa watu wanaokaa mbalimbali.


Siku moja Shaibu akiwa katika biashara yake ya miamala yaani sehemu ambayo anaifanyia kazi, ilikuwa ni jumapili, alifika mtu mmoja hivi kama mteja umri wake ukiwa umeenda kidogo kwa makadirio anaweza kucheza kwenye miaka 45 hadi 50 (kijana anayeuacha ukijana).


Mtu huyo alikuja kama mteja kufanya muamala.


"Sasa kijana nina shida ya kumtumia mtu hela kama milioni moja hivi, nimezunguka sana hapa naona wengi wamesema hawana salio....vipi naweza kuipata?"


Shaibu hakuwa na kiasi hicho, ilikuwa pungufu zaidi ya laki nane hivyo yeye alikuwa na laki mbili tu. Mzee huyo akamwambia kuwa afanye utaratibu wa kutafuta kwa mawakala wenzake hadi itimie hiyo hela. Shaibu aliwasiliana na wale mawakala wa jirani yake lakini hakuweza kuipata kwa wakati huo.


Mteja huyo kwa sababu hakuwa na jinsi na mbaya zaidi ilikuwa jumapili siku ambayo benki huwa hazifunguliwi, akamuomba Shaibu azunguke zunguke hadi aipate maana ilikuwa muhimu sana wa yeye kuituma hela hiyo hela kwa siku hiyo. Shaibu alihaidiwa kupewa shilingi elfu ishirini kama angefanikiwa kupata salio hilo.


Shaibu alikubali kufanya hivyo kwani ilikuwa ni kiasi kikubwa sana kwake kwani hata hiyo biashara yake yenyewe haikuwa ikimwingizia kiasi hicho kwa siku. Hivyo Shaibu aliona kama fursa ya haraka.


Mtu huyo akamwachia namba yake Shaibu na kumwambia kuwa hakai mbali sana na eneo anapofanyia biashara Shaibu hivyo akifanikiwa kuipata atampigia simu alafu atafika mara moja kwa ajili ya kumpatia pesa na kuituma.


Shaibu akaanza kupambana kutafuta 'float' salio kwa mawakala wenzake. Mwenye elfu hamsini , laki nakadharika.


Alipambana hadi ikatimia milioni moja na kisha akampigia simu yule mtu. Yule mtu baada ya kupokea simu alimuomba sana Shaibu achukue bodaboda ili akachukue hela na namba.


Kwakuwa hapakuwa mbali sana, Shaibu akachukua boda boda na kufika eneo aliloambiwa ndani ya dakika tano tu.


Alipofika eneo hilo akampigia simu, kisha akapata maelezo ya nyumba ilivyo na alipoiona akaenda moja kwa moja na kuingia ndani ya uzio.


Alipofika mlangoni (mlango wa nyumba yenyewe) akagonga kisha mlango ukafunguliwa na yule mtu na akamkaribisha ndani.


Waliketi kwenye sofa saafi za ngozi, ndani mkiwa na ubaridi wa kiyoyozi. Samani zilizokuwepo ndani humo zilikuwa za kisasa kabisa. Hakika sebule lilipendeza sana!


"Sijui lini nitayafikia haya maisha"


Shaibu alijiwazia moyoni mwake.


"Kijana nashukuru sana kwa msaada wako maana nilishakwama kabisa asee, unajua bwana kuna watu wanataka wautume mzigo wangu wa samaki wapo huko kisiwani mwanza....sasa ilkuwa lazima nitume leo maana wale samaki ni wabichi wakikaa sana wanaharibika.....ngoja nimwite wife alete pesa alafu namba hii hapa tuma humu...."


Shaibu akaanza kufanya muamala wake. Akamaliza kuufanya kikamilifu. Mtu yule akamwita mke wake ili amletee hela.


Dakika moja tu mbele, manukato mazuri yalianza kunukia sebuleni hapo. Mwanamke mrembo mdogo hivi wa umri pengine anaweza kuwa hata mwanaye wa kumzaa mtu huyo aliingia sebuleni akitokea chumbani. Bila shaka ndiye alikuwa ni mke wa huyo jamaa.


"Mpe huo mzigo huyu kijana"


Mtu huyo alisema, na yule mwanamke akageuka kumpa Shaibu mzigo.


Macho yao yalipokutana, kila mmoja alitumbua jicho la mshangao kwa mwenzake. Yule mwanamke alikuwa ni Judy.


*Itaendelea*


Hapa ndipo huja ile kauli usijaribu kuyazuia mafuriko kwa mikono yatakusomba.....


Hatimaye wamekutana....Je ni kweli yule mtu alimsahau Shaibu au ulikuwa mpango wake tu wa kutaka kujua kama wanawasiliana baina yao?


*Hisia hazizuiliki*


Hebu tuone nini kitajili sehemu ijayo, usikose.



Sehemu iliyopita imeishia wakati ambapo Shaibu anakutana tena kwa mara nyingine baada ya muda mrefu kupita bila hata mawasiliano. Wanakutana wakiwa nyumbani kwa Judy anapoishi yeye na mume wake. Shaibu yeye alienda kufanya miamala tu ambapo aliitwa na mume wa Judy. Inawezekana Mume wa Judy alimsahau kabisa Shaibu kwani alimuona siku moja tu tena ikiwa usiku.


Sasa endelea hapa....


Judy akasita kidogo huku macho yake yakiwa kama hayaamini amini hivi. Shaibu yeye japo alishtuka kidogo ila hakutaka kujionesha moja kwa moja kuwa ameshtuka. Alijaribu kujizuia ili asionekane kwa mume wa Judy.


Judy aliganda kama dakika moja hivi bila kukabidhi hela kwa Shaibu kitu ambacho kikamfanya mume wake aingilie kati.


"Vipi mama...mpe hela kijana akaendelee na kazi zake maana nimemchelewesha sana....."


Judy hapo ndo akazinduka, akamkabidhi hela Shaibu . Baada ya kupokea hela Shaibu akasimama ili aondoke.


Mume wa Judy akamwambia Shaibu kuwa yeye anaitwa Mr Shamte na atakuwa anampigia mara kwa mara kama atakuwa akihitaji huduma ya miamala.


Shaibu akaaga na kuondoka zake.


Baada ya Shaibu kuondoka, Judy akaamuliza mume wake amempata wapi wakala huyo.


"Aaaah basi ushaanza wewe mambo madogo kuyakuza....nilimuona hapo nyuma karibu na ile sheli tupojazaga mafuta kwa yule mdada....."


Sasa hapo Judy akapata ushaidi wa sehemu ambayo anaifanyia kazi Shaibu. Maana kuna siku za nyuma aliwahi kwenda kazini kwake na hakumkuta. Kumbe Shaibu sehemu ile aliama na kuamia sehemu nyingine na hii ndio sababu pekee iliyomfanya Judy ashindwe kuwasiliana na Shaibu kwa kipindi chote hicho.


Judy akajiridhisha kuwa mume wake hakuwa anamjua Shaibu na hakumleta pale kwa lengo lingine zaidi ya lile aliloitiwa la kufanya miamala.


Moyo wa mwanadamu umeumbwa kwa nyama na ile mishipa inayopitisha damu, hivyo kuumia ni sehemu yake. Moyo wa Judy ukaanza kuwa na Shauku ya kutaka kukutana na Shaibu.


Akili yake haikutulia tena, kila alilofikiria liliishia kwenye jina la Shaibu. Siku moja aliwahi kurudi kazini kwake ili ampitie Shaibu na waweze kuongea.


Kwa bahati mbaya sana alipofika sehemu hiyo hakumkuta , palikuwa pamefungwa. Namba yake hakuwa nayo maana laini ambayo ilikuwa na namba ya Shaibu aliibadirisha mume wake na kumpa laini mpya.


Judy akaenda nyumbani na alipofika akili haikumtulia kabisa. Akawaza sana akaona bora aende anakoishi labda atamkuta.


Alienda ile mitaa lakini bahati mbaya iliyomkuta alisahau nyumba na hata alipojaribu kuulizia jina la Shaibu hakuna aliyeweza kumjua.


Judy akarudi nyumbani na kutulia. Baadae akapata wazo , akaona ampigie mume wake na amwambie kuwa shangazi yake wa Iringa amempigia simu anataka amtumie hela hivyo akamuomba ampigie simu wakala amwambie amtumie kwani yeye anajisikia vibaya hawezi kutoka nyumbani kwake.


Mr Shamte kwa kuwa aliona ni kawaida tu wala hakufikiria kingine chochote, akampigia simu Shaibu na akumtaka aende nyumbani kwake ili akatume hela.


Shaibu siku hiyo hakufungua ofisi yake, wakati anapigiwa simu alikuwa kwa rafiki yake Muki wakipiga soga za hapa na pale. Shaibu alijua kuwa Mr Shamte atakuwa yupo kwake na ndiye aliyemwita.


Shaibu akamuaga Muki ili aende kufanya muamala na uzuri ni kuwa alikuwa anatembea na simu zake za kazi hivyo safari yake ilianzia hapohapo kwa Muki. Wakati anaondoka Muki akamtadharisha Shaibu awe makini akiwa nyumbani kwa Mr Shamte kwani wanawake wakiwa wanataka kitu, chochote huweza kufanya ili mambo yao yakamilike.


Shaibu akaondoka na kwenda nyumbani kwa Mr Shamte.


Mr Shamte alimtaarifu Judy kuwa wakala anaenda hapo, kwa hiyo hata mlango ulivyogongwa hakushangaa sana alijua ndiye atakuwa Shaibu. Ni kweli alikuwa Shaibu aliyegonga mlango.


Shaibu alishtuka alipokaribishwa na Judy tena akiwa amevaa kigauni chepesi sana ambacho kilimchora vyema mwili wake.


Sebule lilikuwa tulivu sana, palionekana papo kimya na hapakuwa na bugdha yeyote ile.


Shaibu alivuta pumzi ndefu sana na kisha akaishusha , Judy akaufunga mlango na kumkaribisha Shaibu kwa tabasamu bashasha lenye kusisimua.


"Usiogope nipo mwenyewe tu, kuwa na amani...."


Judy alizidi kumchangamsha Shaibu na kuzidi kumtoa hofu.


"Wewe ni kijana mdogo sana....kama unahitaji kuendelea kuvuta pumzi hii ya Mungu basi achana na Judy..."


Maneno aliyoambiwa na mume wa Judy miezi kadhaa iliyopita yakawa yanajirudia rudia kichwani mwa Shaibu.


"Ni mimi ndiye niliyekuita, nimekumisi sana...nimekukumbuka sana Shaibu....Nimeshindwa kujizuia kabisa...."


Judy aliongea huku akizidi kumsogelea Shaibu ambaye alikuwa anaonekana kama mtu anayewaza jambo hivi.


"Lakini...."


"Lakini nini..."


Judy alimziba mdomo Shaibu ambaye alionekana kuna jambo alitaka kuongea.


Wakati huo teyari Judy alikuwa ameshamvamia Shaibu, sasa walikuwa karibu sana tena sana. Mashetani ya Judy yalishapanda na hayakuwa na mtu wa kuyatuliza wakati huo.


Shaibu akaonekana kama anataka kama hataki, alikuwa katikati ila kwa hakika si kazi rahisi kwa mwanaume yeyote ambaye yupo kamili achomoke kwenye mazingira hayo aliyoyaonesha Judy.


Shaibu akaacha uchovu,akaanza kuonesha ushirikiano kwa Judy. Biashara ya miamala ikawekwa kando hata yale maneno ya Mr Shamte yakapotea ghafla. Mahaba yakatawala kati ya wawili hao.


*Itaendelea*


Haya sasa mambo ndo hayo yashakuwa mambo.


Hivi kweli kila jambo lilishapangwa na Mungu na binadamu anatimiza tu???


Hili la Shaibu na Judy lilishapangwa au ni wao wawili ndio wamepanga?


Unadhani watafanya mambo yao bila kukutwa na Mr Shamte?


Usikose sehemu ijayo....kuna mengi ya kujifunza.





Judy anamkumbuka Shaibu ,anatamani akutane naye .Anafanya kila mbinu na hatimaye kweli anafanikiwa kumpata Shaibu. Shaibu ambaye bwana miamala hakujua kama ni mtego wa Judy...anakubali kwenda nyumbani kwa Judy kufanya muamala.....Muamala haufanyiki....mambo ya baishara yanawekwa kando....mahaba mazito yanatawala ndani ya nyumba ya Mr Shamte.


Endelea sasa.......


Mahaba ya hapa na pale yakaendelea. Walijiachia kabisa kama gari lililokatika break likiwa mteremkoni, kila mmoja nafsi yake ikasema ,


"Hakika hizi ndio raha za dunia...."


Walifanya kila walichoweza kufanya. Hata kuoga bwana Shaibu alioga hapo hapo, hata chakula cha mchana bwana Shaibu alikula hapohapo.


Kwa muda mfupi tu, Shaibu akili yake iliruka na kuona kama hayo ndio maisha yake yaani kama yeye ndio mwenye nyumba vile.


Wakiwa bado wapo sebuleni, huku wakiwa wanachekeshana hapa na pale , simu ya Judy iliita , alikuwa ni Mr Shamte alikuwa anamuulizia kama alifanikiwa kutuma ile hela. Kwa sauti ya mahaba sana Judy akamjibu Mr Shamte,


"Eeeh nimeshafanikiwa kutuma...tena yule kijana yupo sharp sana yaani alikuja faster, hakika anaijua vizuri biashara yake...."


"Yeah kweli malaika wangu, yule kijana yuko vizuri sana , mimi nilimuona alivyoitafuta ile miliona moja ya siku ile....Mungu amjalie afike mbali sana na aje kupata mke bora....."


Baada ya mazungumzo hayo wakaagana kisha simu ikakatwa.


"Angejuaa?? hahaa kazi kwake....wewe ndiye furaha yangu ya kweli (huku akimshikashika mikono Shaibu)"


Judy aliongea hivyo mara baada ya kumaliza kuongea na Mr Shamte.


Shaibu na Judy waliji-mwaya mwaya hadi ulipokaribia muda wa kurudi kazini ndipo Judy akamtaka Shaibu aondoke.


Shaibu akaondoka zake na kitita cha hela kama laki tatu hivi alizokabidhiwa na Judy, laki moja ikiwa kama hela aliyoituma na laki mbili amepewa tu za matumizi yake.


Shaibu alienda moja kwa moja kwa mshkaji wake , Muki. Alipofika tu akakuta ugomvi unaendelea hapo kati ya Muki na wapangaji wenzake.


"Wewe unakaa tu hapa...hulipi umeme wala nini...."


"Kama maisha yamekushinda rudi kijijini kwenu huko usije ukatupa corona hapa..."


"Hata maji wewe hulipi..."


"Yaani hata hela ya usafi wa chooni hatoi yeye anajua kunya tu....."


Wapangaji hao walitoa kila aina ya neno bovu kwa Muki. Muki hakuwa na cha kuwajibu kwani yote wayasemayo ilikuwa ni halali yao kwani ilipita miezi 3 hakulipa hela yeyoyte.


Maneno hayo yalimchoma sana moyoni Muki , hasa akikumbuka kuwa elimu yake ni kubwa sana kuliko hao wapangaji lakini mfukoni hamna kitu.


"Oya mwanangu shika hii kilo(laki moja) wape..."


Shaibu alimnong'onezea Muki.


Muki akajibu,


"Aaah mwana eeeh achana nao hao....hela zenyewe za watu hizo, usije ukaingia matatizoni alafu mambo yakaaribika kila sehemu...."


Muki alimjibu hivyo Shaibu kwani wakati ule kabla Shaibu hajaenda kwa Judy alimdokeza suala la yeye kudaiwa hapo na alimtaka Shaibu amkopeshe hela ili alipe lakini hakuwa nayo , alikuwa ana hela ya biashara tu tena sio yake. Kwa hiyo Muki akafikiri kuwa Shaibu anataka kutoa hela ya mtaji kumbe Shaibu alijaa pesa kutoka kwa Judy.


Shaibu akatoa shilingi laki moja na kumkabidhi Muki kisha akamwambia mambo mengine wataongea baadae ila awakabidhi kwanza mzigo wao. Muki akachukua ile na kisha akahesabu elfu sabini na akamkabidhi mtu anayepokea hela.


Baada ya hapo, Shaibu na Muki wakaingia chumbani.


Shaibu na muki walikuwa marafiki walioshibana sana, urafiki wao ulianzia wakiwa chuoni huko Mwanza katika chuo kikuu cha SAUT wakiwa mwaka wa kwanza tu.


Wote hawa walisoma Shahada ya elimu katika sanaa yaani bachelor of arts with education. Walipomaliza , pia wakakutana tena mtaani jijini Dar es salaam na wakawa wanatafuta wote ajira ila kwa sababu ajira kuwa finyu sana hawakuweza kupata. Kila walipoenda walikosa, hata ile nafasi ya kujitolea hawakuipata.


Ndipo wakaamua kufungua kituo cha masomo ya ziada "Tuition" .


Wakawa wanafundisha nyakati za jioni maana ndio muda ambao wanafunzi wanakuwa teyari washarudi nyumbani. Wanafunzi waliwapata ingawa hawakuwa wengi sana na changamoto nyingine iliwakumba ya kutopata malipo yao kwa wakati hivyo bado hali ya kuyamudu maisha haikuwa ya kuridhisha.


Mambo yaliwabadirikia kabisa janga la corona lilipoingia kwani hata ile tuition yao wakalazimika kuifunga kufuatia agizo la waziri mkuu la kuepusha misongamano. Hata kile kiasi kidogo wakawa hawakipati.


Shaibu yeye akawa anasimamia kwa muda biashara hiyo ya miamala ya ndugu yake, kwani kwa wakati huo ndugu yake alisafiri nje ya mkoa.


Shaibu akampa stori Muki jinsi mambo yalivyokuwa nyumbani kwa Judy na hadi zile hela alizopewa hadi akampa yeye ile laki moja.


Ingawa pesa hizo zilimsaidia Muki siku hiyo katika kutatua mzozo wake lakini hakusita kuonyesha mashaka juu ya hatari iliyopo mbele ya Shaibu. Kwa mazingira yaliyopo , Muki akamshauri Shaibu amchunguze sana Judy kwani pengine kuna jambo limejificha nyuma ya pazia hasa ukiangalia umri wa mume wake na wake ni tofauti kabisa tena wameachana mbali mbali sana. Muki akaendelea kumwambia yawezekana yule mwanamke amekuja kuharibu maisha ya Shaibu maana ikija kujulikana basi Shaibu atakuwa matatizoni sana, hivyo pamoja na kujua mambo kadhaa kuhusu Judy, Shaibu hana budi kuachana na Judy.


Shaibu alikubaliana na mawazo ya Muki, akapanga siku wakutane na Judy ili waongee na kufahamiana kabisa maana tangu wakutane hawakuwahi kuzungumza kuhusu maisha yao binafsi zaidi ya mahaba tu.


Siku kadhaa mbele yapita kama mwezi hivi walikutana Judy na Shaibu katika moja ya fukwe zilizopo pembezoni mwa bahari ya Hindi huko maeno ya kigamboni.


*Itaendelea.....*


Je kuna jambo gani limemfanya Judy akae na mume mwenye umri mkubwa kuliko umri wake?


Hivi mtu unayetaka kuachana naye unataka kuijua historia yake ili uifanyie nini??? We shaibu wewe......



ITAENDELEA

BWANA MIHAMALA - 1

 


IMEANDIKWA NA: DAMIANI CHIKAWE

*******************************************************

Chombezo :  Bwana Mihamala 

Sehemu Ya Kwanza (1)


Imeandikwa na *Mwl Damian Chikawe.*


Mvua ya rasha rasha ambayo haikutaka kuisha bado iliendelea kunyesha usiku ule na kusababisha mikusanyiko yote ya vijana kushindwa kuhudhuria kijiweni kama ilivyokuwa desturi yao ya kufanya hivo kila ifikapo majira ya saa moja usiku na kuendelea, licha ya mvua tu bado serikali imekataza mikusanyiko kwa kipindi hicho kwa sababu ya janga la corona. Shaibu ambaye alikuwa anafanya biashara za mihamala ya simu maeneo ya rangi tatu 'Mbagala rangi tatu' alikuwa mpekwe sana siku hiyo. Kwenye chumba chake hakukuwa na TV wala redio hivyo upweke kwake ulikuwa mkubwa mno. Mbaya zaidi hata umeme ulikatika siku hiyo hata ile simu yake kubwa ya kisasa 'smartphone' haikuwa na chaji. Maana angalau ingekuwa ina chaji ingeweza kumuweka bussy kidogo. Hakika bwana shaibu aliona usiku utakuwa mrefu sana. Katika chumba hicho Shaibu alikuwa anakaa peke yake, alikuwa bado hajaoa. Alichukua simu ili ampigie mmoja wa wapenzi wake ila akakumbuka kuwa hawapo karibu naye. Alikuwa na wapenzi wawili ambao wote kwa wakati huo walisafiri kwenda nje ya mkoa wa Dar es salaam kwa hofu ya janga hili baya la corona.


Shaibu alijilaza kitandani chali huku akitazama juu na asijue nini cha kufanya. Alijaribu kufungua game lililopo katika simu yake ndogo 'kiswaswadu' ambapo kulikuwa na game la nyoka. Hata hivyo haikumchukua muda akaachana nalo maana halikuwa na mvuto kabisa.


Akiwa bado anaendelea kuwaza na kuwazua ,kuna jambo lilimjia kichwani mwake. Akarudisha matukio ya mchana nyuma, akakumbuka wakati anahudumia wateja alikuja mteja mmoja mtoto wa kike . Alikuwa mrembo sana huyo msichana. Licha ya urembo wake , alikuwa mzuri sana. Alikuwa anavutia ukimtazama usoni au sehemu yeyote ya mwili wake. Shaibu alikumbuka mrembo huyo jinsi alivyokuwa anaongea kwa mapozi na huku akitabasamu kila mara.


Shaibu aliishia kutabasamu maana hakuwa na ujanja wa kuweza kumpata msichana huyo kwa wakati ambao alimkumbuka.


Katika kuwaza waza Shaibu alikumbuka jambo. Akachukua simu yake ya uwakala na akaanza kupekua mihamala yote aliyoifanya siku hiyo. Alikagua hadi akaukuta muhamala aliomfanyia mrembo ambaye alimkumbuka usiku huo.


Shaibu akatabasamu, kisha akachukua namba na kuingiza katika simu yake. Haraka haraka akampigia , simu iliita bila majibu. Akapiga tena bado mambo yalikuwa yale yale. Simu haikupokelewa. Mpaka nyakati hizo muda ulisomeka saa tatu kasoro dakika tano tu.


Shaibu akajisemea moyoni baada ya kuona simu haipokelewi


"Mmh au inawezekana akawa mke wa mtu yule, pengine wamelala sasa, mmmh lakini mbona mapema? Au pengine simu ameweka chaji? Au namba ngeni huwa hapokei? Mmmh nini shida sasa......"


Shaibu kila alichowaza hakupata majibu zaidi ya kuukumbuka tu urembo na uzuri wa mwanamke huyo. Alijaribu tena kupiga ila bado haikupokelewa. Matumaini yake ya kusikia sauti ya mrembo huyo ili angalau imliwaze kwa usiku huo yalianza kukatika.


Shaibu akaamka kitandani na kukaa tena kitako. Alienda maliwatoni kwa haja ndogo. Aliporudi alikutana na sms kutoka kwa mtu aliyempigia sana simu na hakupokea. Akaifungua na kukutana na ujumbe....


"Nani?"


Shaibu alivuta pumzi ndefu na kisha akaishusha chini. Akaingia haraka haraka uwanja wa meseji ili ajibu. Shaibu akaandika "Aaah umenisahau? au ushafuta namba yangu?"


Shaibu alianza kumwandikia kwa namna hiyo kana kwamba wanajuana vile ila ni mbinu zake tu.


Baada ya dakika moja ujumbe ukarudi

"wewe nani? Bila shaka utakuwa umekosea namba, mimi unanijua?"


Shaibu akajibu,

"Hapana sijakosea, wewe si

Irene?"

Shaibu alijaribu kutaja jina lake ili aone kuwa anamjua vizuri ,lengo likiwa ni kupata uraisi wa kuchati naye. Jina hilo alilipata kwenye muhamala uliobaki kwenye simu yake.


Ujumbe ukarudi

"hapana mimi si Irene, huyo ni mama yangu...."


Shaibu akashtuka na akapata jibu kuwa inawezekana wakati laini inasajiliwa alitumia kitambulisho cha mama yake. Akapoteza pointi ya kwanza Shaibu, akabakiwa na pointi mbili tu za kumfanya aendelee kuchati naye.


Shaibu akajikakamua..

."Sasa hapo mimi nimekosea nini? Nimeamua kuanza na jina la mama yako ili kumbukumbu zako zirudi nyuma na uweze kunikumbuka....naamini sasa ushanikumbuka, vipi naweza kukupigia tuongee? "


Ujumbe wala haukukawia kurudi kutoka kwa mtu aliyedhaniwa anaitwa Irene...


"Wewe huna lolote hilo jina utakuwa umeangalia kwenye usajili wa namba yangu....sasa sitaki nijue umepata wapi namba yangu wala nini sijui...wewe hunifahamu mimi na sitaki tena usumbufu wako....Nataka kupumzika sasa, usitume tena sms wala kunipigia"


Shaibu ikamfikia sms hiyo na mapigo ya moyo wake yakaenda kasi kama virusi vya corona. Akaiacha simu kitandani, akaishika tena na kuisoma sms hiyo. Wakati anafikiria zaidi akamkumbuka mwalimu wake wa saikoloji akiwa chuoni ambaye aliwaambia kuwa ..."hakuna kilima kisicho na kilele...,pata tabu kuupanda mlima ila ukifika kileleni utaserereka tu...."


Maneno haya yakamtia nguvu Shaibu , akaishika simu na kuingia tena uwanja wa meseji. Akaanza kuandika ili amtumie mrembo huyo.


Itaendelea........


*Akili za kuambiwa changanya na zako*


Wewe unatamani nini? Shaibu ampate huyo mdada au asubiri corona iishe na wapenzi wake warejee nyumbani?


*Upweke husababisha matatizo mengi sana, zipo namna mzuri za kudili na upweke, hvo kuwa makini pale unapohitaji kutafuta faraja la moyo ama tulizo la moyo*




Kijana anayeitwa Shaibu ambaye anafanya kazi ya miamala ya simu katika jiji la Dar es salaam anakutana na wakati mgumu wa upweke akiwa kwake nyakati za usiku. Hivo akaamua kufanya jambo ili aondoe upweke huo. Anapekua miamala aliyoifanya siku hiyo na kukutana na namba ya mrembo matata ambaye alifanya muamala katika ofisi yake.......


Je atafanikiwa kumtia nguvuni?


*Endelea....*


"Busara ni kumsikiliza mtu anasema nini hata kama hakikupendezi na uungwana ni kulitafakari lile akuambialo, haujajua hata nataka nikuambie nini lakini teyari umetoa maamuzi....ila poa naamini utanitafuta mwenyewe katika wakati ambao sitapatikana....si unakumbuka leo kuna sehemu umefanya muamala pale mbagala rangi 3?...."


Shaibu alijitutumua kwa kumkumbusha alichokifanya mchana ili angalau amfanye kuwa na 'Attention' juu ya amwambiacho.


Zilipita dakika kama thelathini hivi bila hata ujumbe huo kujibiwa. Shaibu alijigaragaza kitandani hadi akapitiwa na usingizi na kulala fofofo.


Kwa upande wa yule mwanamke, alijifikiria sana kuhusu jumbe alizokuwa anazipata kutoka kwa Shaibu. Aliwaza sana na baadae akajipa majibu mwenyewe kuwa yawezekana kuwa kweli kijana Shaibu atakuwa na jambo la kutaka kumwambia. Akaamua kuchukua simu yake na kumpigia Shaibu. Simu ya Shaibu iliita bila kupokelewa. Alipiga zaidi ya mara tatu lakini haikupokelewa. Shaibu alikuwa amelala fofofo hata muito wa simu hakuweza kuusikia. Dada huyo akahisi kuwa Shaibu amekasirika kwa sababu ya ujumbe wake wa mwisho wa kumtaka asimtafute tena.


Biti huyo moyo wake ukahudhunika sana, akaamua kumtumia ujumbe Shaibu,


"Samahani sana ..I'm very sorry, nilifikiri unaweza kuwa muhuni tu ndo maana nikajibu vile...Mimi naitwa Judy ,una shida gani?"


Ujumbe huo pia haukujibiwa. Hali hii ikamfanya Judy aendelee na program zake nyingine ila baadae naye akapitiwa na usingizi, akalala.


Shaibu alipoamka asubuhi na mapema kabisa , alienda maliwatoni kwa ajili ya kujiandaa ili aende kazini kwake. Baada ya kujiandaa akaishika simu yake , akakutana na sms pamoja missed calls. Akazifungua , alikuwa ni yule mrembo. Shaibu akashika kichwa na mdomo ukiwa wazi. Kisha akajilaumu kwa usingizi wake wa kama pono. Ilikuwa ni saa 12 kasoro kama dakika tano hivi asubuhi, palepale akaishika simu na kumpigia.


Simu iliita na kupokelewa kwa sauti yenye uchovu wa usingizi. Iliashiria wazi Judy bado alikuwa amelala. Shaibu alipoona hivyo ikabidi amwambie basi wataongea baadae akiwa ameamka.


Shaibu akaondoka na kwenda kazini kwake kama kawaida lakini huku akilini mwake akiwaza maneno mazuri ya kumwambia Judy pale watakapoongea vizuri.


Shaibu akiwa kazini kwake majira ya saa nne asubuhi simu yake iliita na jina lilikuwa ni Judy. Judy alimuuliza Shaibu lengo lake ni nini hadi akaamua kumtafuta. Shaibu alimwambia Judy ni vyema wakaonana ana kwa ana kwani si vyema kuongea kwenye simu. Judy alikubali ombi la Shaibu na wakapanga siku waonane.


Jumamosi ya wiki hiyo walikutana kwani ndio siku ambayo walipanga waonane. Shaibu alitupia pamba kali sana ambazo yeye mwenyewe alikuwa anaziamini akivaa basi hupendeza sana. Mtu wa kwanza kufika eneo la tukio alikuwa Shaibu hvyo wakati Judy anafika naye alipata kumuona tena vyema. Mapigo ya moyo wa Shaibu yalienda kasi sana baada ya kumuona Judy akiwa ana-drive gari yeye mwenyewe akifika sehemu hiyo. Mawazo yakampeleka mbali sana na kuamini kuwa Judy hakuwa type yake. Lakini alijikaza tu ,hadi wakakutana na kuanza kuongea.


Hata kabla hawajaendelea kuongea sana , Judy akamtadhaharisha Shaibu kuwa mazungumzo yasiwe marefu kwani hapaswi kuonekana sehemu kama hizo tena na mtu ambaye hausiani na ndugu zake. Mpaka muda huo Shaibu alikuwa hajui chochote kuhusu Judy na hata hofu ilimpata Shaibu. Kila alipojaribu kumwangalia Judy aliona ameachwa mbali sana hasa kiuwezo wa kifedha. Shaibu hakujua aanze wapi.


"Ongea basi haraka, mimi nataka niondoke, weekend leo bata linanisubiri....."


Judy aliongea kwa sauti ya madaha huku akitoa simu yake kwenye mkoba na kuanza kuichezea.


Kwa sauti ya hofu Shaibu alijikuta akimuuliza swali Judy...


"umenikumbuka?"


Judy alitikisa kishwa kuashiria kukataa hamkumbuki kabisa. Shaibu huku akijichekesha akamwambia kuwa yeye ni yule wakala ambaye siku kadhaa zilizopita alifanya muamala kwake.


Judy akadakia harakaharaka...


."kwa hiyo unasemaje? Nambie lengo lako ni nini?"


Shaibu akaanza kwa kujiuma jiuma maneno.


"Aaah kiukweli unajuaa....tangu siku ile....."


Judy akadakia hapo hapo

"Mbona kama huna cha kusema....?"


Wakati huohuo simu ya Judy ikaita , alivyoipokea akadanganya kuwa yupo kwenye party ya rafiki yake. Baada ya kukata simu, JUdy alionekana kuwa na hofu kubwa sana.Akamwambia Shaibu watoke eneo hilo na watafute eneo lingine la kujificha. Wakati huo wote Shaibu hakujua ile simu aliyopigiwa Judy ilitoka kwa nani na kwanini aliingiwa na hofu na kutaka watafute sehemu nyingine. Shaibu na Judy wakaingia ndani ya gari, gia ikaingizwa na kuondoka eneo hilo. Shaibu ndiye aliyekuwa anamwelekeza njia Judy. Pita hapa ....kunja hapo....ingia hapo.....Alafu nyoosha.....Hayo ndio baadhi ya maneno yaliyokuwa yanasikika ndani ya gari hilo kutoka kwa Shaibu. Shaibu alikuwa na akili zake kichwani, alikokuwa anamwelekeza nako anakujua yeye mwenyewe. Safari ilizidi kuchanja mbuga. Ndani ya gari hakukuwa na stori baina yao zaidi ya maelekezo tu ya wapi gari lipite kutoka kwa Shaibu.


*Itaendelea*


Kuna mengi ya kujifunza huko mbeleni......


Unajua Shaibu anampeleka wapi Judy? Je ni nani aliyempigia simu Judy? Kwanini hofu ilimpata Judy baada ya kupigiwa simu?


Majibu yanakuja sehemu inayofuata....usikose....




Shaibu na Judy wamefanikiwa kukutana lakini hakuna kilichoongeleka kwa sababu ya simu aliyopigiwa Judy kumtia hofu Judy . Shaibu na Judy wanaamua kutoka sehemu walipo na kwenda sehemu nyingine ambayo haitakuwa wazi ili wakajifiche. Muongoza njia ni Shaibu, na ndiye aliyejua anaelekea wapi. Judy hakujua kitu , akawa anafuata maelekezo ya Shaibu tu.


Songa nayo sasa.....


Walikatiza katiza mitaa kama mwendo wa dakika 30 hivi na mwishowe wakafika sehemu ambayo Shaibu akaamuru gari lisimame. Judy akasimamisha gari. Haikuchukua hata sekunde , Judy akashusha swali kwa Shaibu,


"Ndo wapi hapa....?"


Shaibu huku akionesha sura ya tabasamu, akamjibu hapo walipofika ndipo anapoishi.


"Aah sasa hapa tumekuja kufanya nini? Hebu tuondoke....."


Judy akadakia haraka haraka tena huku akiwasha gari na kuanza kurudi Riverse ili ageuze gari. Wakati hilo likiendelea , simu ya Judy iliita tena.


Judy akasimamisha gari, akalizima kabisa kisha akapokea simu. Kwa sababu ya utulivu wa eneo walilokuwepo Shaibu aliweza kuisikia vyema sauti ya aliyepiga simu.


"Nimeongea na rafiki zako wote wanasema haupo nao...wewe upo wapi?"


Sauti yenye ukali ilimuuliza Judy. Judy akaanza kubabaika kujibu. Alijitetea kuwa ni rafiki yake ambaye walisoma naye wakiwa chuo na walikutana wiki moja tu nyuma ndio wakabadirishana namba ndio maana hakumtambulisha rafiki huyo.


"Sasa kwanini umetoka haujaniaga? Huu ndio utaratibu wetu?"


Baada ya maelezo ya Judy , akaulizwa tena kwa ukali sana. Judy akajitetea tena kuwa alitoka ghafla na alipanga akifika huko atamtaarifu.


Sauti ya kushuka isiyokuwa ya ukali ikajibu...


"Sawa ila siku nyingine nitaarifu mapema....kuwa makini .....See you later"


Hapo simu ikakatwa na kisha Judy akashusha pumzi ndefu sana , kisha akasema huku akimwelekeza kidole Shaibu.


"Wewe unataka kunitia matatizoni"


Shaibu muda wote huo alikuwa hajui Judy anaongea na nani na kwanini anaonekana kuchanganyikiwa huku akimdanganya sehemu ambayo yupo.


"Vipi kwani ni nani ulikuwa unaongea naye?"


Shaibu alimuuliza Judy.


Judy huku akiupinda mdomo wake na kuonyesha sura ya kulipotezea swali aliloulizwa akasema.


"Aaah tuachane na haya....basi ongea hapahapa tukiwa garini ili niwahi kurudi nilikotoka..."


Shaibu akapiga muayo wa kujilazimisha kisha akamshawishi Judy akapaone anapokaa. Kwani kutoka walipo ni mbele tu ya gari yao yaani ukitazama mbele unaona nyumba. Ilikuwa ni nyumba ya wapangaji, haikuwa kubwa sana wala nzuri kivilee ilikuwa na vyumba vinne na kila chumba kilikuwa na mpangaji. Vyumba vyote walikaa mume na mke isipokuwa kwa Shaibu tu ndiye ambaye alikuwa bado hajaoa.


Judy hakuwa teyari kuingia ndani ila Shaibu alikuwa king'ang'anizi .


Hatimaye baadaye Judy akakubaliana na ombi la Shaibu. Wakalisogeza gari karibu na wakalipaki sehemu. Wakashuka wakaingia ndani.


Wapangaji wenzake ambao kwa wakati huo walibaki wanawake tu kwakuwa waume zao walikuwa kwenye miangaiko waliyatumbua macho yao wakimwangalia Shaibu akiwa na mrembo matata sana. Shaibu akawasalimia kisha akakatiza na kuzama ndani.


Akafungua chumba chake ambacho kilikuwa shagalabagala yaani ovyo ovyo hata kitanda hakikutandikwa na nguo zake nyingine zilikuwa chini ovyoovyo. Yaani kila kitu hakikuwa katika mpangilio.


Shaibu akamkaribisha mgeni wake , na wakati huohuo akaanza kutandika kitanda na kuokota nguo zilizokuwa chini na kuziweka vizuri.


Hakukuwa na kiti ndani ya chumba hicho zaidi ya kitanda na meza tu. Hivyo baada ya kutandika vizuri ndipo akamwambia Judy akae kitandani maana bado alikuwa amesimama.


"Nisamehe sana, si unajua naishi mwenyewe tu hapa kwa hiyo hata kupanga vitu vizuri naona uvivu sana, karibu sana..."


Muda wote huo Judy hakuongea kitu zaidi ya kuonesha sura ya mfadhaiko kisha akaketi kitandani.


Akaitoa simu yake kwenye mkoba na kuanza kuichezea tu. Shaibu alikuwa anamsoma tu Judy ambaye alikuwa kimya kabisa kwani tangu waingie ndani humo Judy hakuongea neno lolote.


Shaibu akatoka nje ya chumba kisha baada ya muda mfupi tu akarudi na maji kwenye chupa ya lita moja na nusu. Bila shaka aliyanunua dukani. Akachukua bilauri na kujaza maji kisha akamkaribisha Judy.


Judy akatingisha kichwa bila hata kusema lolote na akayachukua hayo maji. Hata hakuyanywa akayaweka kwenye meza na kuendelea na kuchezea simu.


Shaibu ndiye aliyekuwa anahangaika tu mara ashike hiki mara kile mara anamwongelesha stori Judy lakini Judy aliishia kutingisha kichwa tu.


Shaibu hakutaka kumwambia lolote Judy linalohusiana na mapenzi ingawa kichwani mwake hilo ndilo alilokuwa analiwaza. Shaibu aliamini kuwa kwakuwa amekubali kuingia ndani mwake basi hawezi kutoka salama.


Judy akawa kama anawaza kitu hivi, dakika moja mbele akanyanyuka kitandani alafu ghafla tu akasema,

"Asee kwa heri...tutaonana siku nyingine"


Akafungua mlango na kutoka nje kabisa. Akaingia garini . Shaibu hakuamini kama Judy angeweza kuondoka, ila alishuhudia gari likiwaka teyari kwa kuondoka. Shaibu akarudi chumbani na kujilaza kitandani huku akiangalia juu. Alijilaumu sana kwa ngoja ngoja zake ambazo ziliishia kumuumiza tumbo.


Hata kabla Judy haijaingia barabarani akiwa palepale alihisi maumivu ya tumbo ghafla labda pengine ni tumbo la hofu ya kuhofia mtu aliyepiga simu. Akalizima gari na kurudi tena chumbani kwa Shaibu. Shaibu alisikia mlango unagongwa, akafungua na kumuona Judy akiwa kashika tumbo ,


"Nioneshe choo"

Judy alisema.


Haraka, Shaibu akampeleka chooni. Baada ya dakika tano, Judy akarudi chumbani kwa Shaibu.


"Nasikia maumivu ya tumbo naomba , nijilaze kidogo baada ya muda nitaondoka..."


Hilo ombi halikuwa na kipingamizi kwa Shaibu, ni kama Kagere kaachiwa kipa tu alafu unamuuliza utafunga gori?


Judy akajilaza kitandani kifudifudi huku akiwa ameshika tumbo lake. Aliugulia mwishowe palepale alipitiwa na usingizi.


Shaibu alikuwa anamtazama Judy kwa uchu mkubwa hasa kwa jinsi alivyojilaza na kuyaacha makalio yakiwa juu kama mama mwenye ujauzito.


Shaibu Alipoona Judy amelala akachukua simu ya Judy na bahati ilioje haikuwa na Nywira 'password'. Cha kwanza kuangalia 'Call history' ili amuone yule aliyepiga simu ni nani.


Alishtuka sana baada ya kuona jina la mtu huyo aliyekuwa anampigia na kumuuliza yuko wapi. Akaangalia na sms zake walizokuwa na wanachati huko nako alibaki mdomo wazi. Alivyofika kwenye upande wa picha , picha nazo zilimshtua sana. Shaibu akabaki anaguna tu 'mmmmh'

Wakati huohuo Judy akajitingisha tingisha kuashiria anaamka.


*Itaendelea....*


Shaibu kapata penalty ndani ya dakika za lala salama....Je unadhani atapaisha au ataweka wavuni?


Ni kweli Judy alikuwa anaugua tumbo au kaamua tu kurudi tena kwa Shaibu? ?


Kuna jambo amegundua Shaibu kwenye simu ya Judy.....ambalo linaonesha sio jema mpaka linamfanya agune .....Ni jambo gani? Ameona jina gani ? Unadhani shaibu na Judy wapo sehemu salama?


Tuwe pamoja sehemu ijayo....ili tujue hatma ya wawili hawa.....


Mabaharia naona mnaona kama Shaibu anazingua vileeee.....????????


*Itaendelea*




teyari Shaibu amefanikiwa kumuonesha Judy nyumbani kwake...Kuna jambo lipo kichwani mwa Shaibu ambalo amepanga kulifanya kwa Judy.....Shaibu anagundua kitu kutoka kwenye simu ya Judy, Kuugua tumbo kumefanya Judy aendelee kubaki chumbani kwa Shaibu jambo ambalo ni kama ushindi kwa Shaibu....


*Songa nayo hapa....*


Shaibu alimuona Judy akijitingisha akajua atakuwa anataka kuamka hivyo akarudisha simu harakaharaka mahala alipoitoa na kutulia pembeni.


Judy akaamka na akaketi kwenye kitanda huku akionesha yu mchovu sana. Alimuomba maji ya kunywa Shaibu na kupatiwa kisha akayanywa.


Shaibu alionesha kujali kwa kumpa pole Judy na kisha kumuuliza kitu gani hasa kilikuwa kinamsibu. Judy alieleza kuwa hakujua tatizo nini ila alisikia tu maumivu ya ghafla kwenye tumbo lake hasa maeneo ya chini ya kitovu.


Judy alimuaga tena Shaibu kwa ajili ya kuondoka kwani teyari muda ulikuwa umeenda sana na teyari mishale ya saa ilikuwa ikisomeka saa tisa ikienda saa kumi jioni.


Judy akasimama na kumuomba Shaibu amfungulie mlango ili aondoke. Shaibu akashika kitasa cha mlango na kuufungua, hatua moja tu ndio aliyoinyanyua Judy, akahisi kizunguzungu....Mikono yake ikatua mabegani mwa Shaibu ili kupata balance ya kusimama maana alitaka kuanguka.


Shaibu akaufunga mlango. Akageuka upande wa nyuma na kumshika mabegani Judy huku akimpa pole na kumwambia inatakiwa aendelee kupumzika na hakuwa na sababu ya kuondoka kwa wakati huo.


Mikono ya Judy ilikuwa mabegani kwa Shaibu na mikono ya Shaibu ilitalii mabegani mwa Judy. Dakika moja ya ukimya ilipita wote wakiwa wanatazamana na hakuna aliyetoa sauti.


Shaibu akaishusha mikono yake hadi kiunoni mwa Judy kisha akamrudisha kitandani na kumketisha juu ya kitanda. Bado ukimya uliendelea kutawala miongoni mwao. Ni vitendo tu ndivyo vilikuwa vinafanyika.


Miili ya binadamu inapokaribiana hasa yenye jinsia tofauti huwa inatoa mwitikio ambao sio lazima mdomo useme. Hakuna aliyemwambia mwenzake afanye hiki au kile kwa wakati huo.


Wote miili yao ilitoa mwitikio, walijikuta wote wawili wakiwa juu ya kitanda. Teyari nguo zao walizokuwa wamevaa zilikuwa zimezagaa ndani ya chumba hicho. Walibaki watupu kama azaliwavyo kitoto kichanga. Uwanja ulionekana mdogo kwani kila mchezaji alitaka kujionesha anajua kuuchezea mpira kuliko mpinzani wake.


Kwenye uwanja huo, kulikuwa na wachezaji wawili tu, kipa pamoja mshambuliaji. Kipa alijitahidi sana kuokoa michomo mikali kutoka mshambuliaji , ilikuwa ni piga nikupige. Pambano round ya kwanza lilimalizika kwa mshambuliaji kuachia shuti kali la kiufundi lililoingia moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa akiwa hoi amelala chali.


Judy alionekana wazi kuufurahia mchezo, yawezekana ilikuwa surprise kwake. Sura yake ilitoa majibu tosha kuwa ame-enjoy kwani ilionesha kutabasamu.


Sasa wote walikuwa marafiki, hawakuogopana tena.Walichekeshana hapo kitandani hata yule Judy akasahau wazo la kwenda kwake.


Baada ya muda kupita Sura zikaambiana kuwa mapunziko yamekwisha, timu ziingie uwanjani tena kuendelea na mtanange. Mtanange uliendelea ,sasa kwakuwa walishasomana vyema kwenye mchezo wa kwanza basi hapo wakaonana kama vitoto vya bata vile. Vikawa vinaogelea juu ya bahari huku vikio sauti za furaha.


Mchezo ulienda vyema, kila mmoja aliridhika na matokeo aliyoyapata hakuna aliyemlaumu refa wala kiwanja kibovu.


Mpaka wakati huo teyari giza lilianza kuingia, majira yalisomeka saa 12 ikieleka saa moja moja hivi usiku. Judy na Shaibu wote wakaingia mariwatoni kwenda kuoga. Kama ungekuwa unawaona wakati wanaingia chooni basi ungedhani ni mume na mke lakini haikuwa hivyo.


Walipomaliza kuoga ikabidi watoke kwenda kutafuta chakula nje ya nyumba kwani Shaibu alikuwa hapiki hivyo hapakuwa hata na vyombo vya kupikia chakula.


Kwa muda mfupi tu walianza kuzoeana. Hata wakati wanakula chakula kuna muda walikuwa wanalishana.


Walipomaliza kula wakarejea tena kwa Shaibu. Sasa wakati mishale ya saa ilisomeka saa mbili usiku na dakika zake. Judy alisahau kabisa kama alihitajika kurudi kwake, naye akajiona wa hapohapo. Shaibu kwake yeye hata hakumkumbusha suala la kwenda kwake kwani kwake yeye ni kama fursa.


Uwanja uliwapendeza kila wakiutazama. Waswahili wanasema palipo na moshi ndipo panapowaka moto. Nyoyo zao zikawaambia waende tena uwanjani kuucheza mchezo. Walianza na kupasha misuli' walifanya mazoezi meepesi mepesi' ili kuiweka miili yao teyari kwa mchezo.


Wakaingia uwanjani na kuucheza mchezo vyema. Walipomaliza hapo hapo usingizi uliwachukua wote wawili, wakalala fofofo.


Baadae sana, usiku wa manane , Shaibu aliamshwa na kelele za simu ambayo ilikuwa inaita wakati huo. Ilikuwa simu ya Judy, Judy alikuwa bado amelala pengine alikuwa anachanja mbuga na ndoto wakati huo. Shaibu akashuka kitandani na kuishika simu ya Judy.


Kama kawaida jina lilikuwa lilelile la mwanzo. Jina hilo lilisomeka....


"My hubby"


Shaibu akabonyeza kibatani cha kuweka ukimya 'silence' , simu ikaita hadi ikakata. Ikapigwa tena , pia ikawa vilevile.


Shaibu alipoangalia call history alikutana na missed calls kama 10 hivi zote zikiwa za huyo huyo My hubby. Alipoingia kwenye sms huko nako zilijaa sms zake.


"My dear...."


"Mbona hadi sasa hujarudi?"


"Uko wapi Judy. ...?"


"Nini kimekupata mke wangu?"


"Mbona haupokei simu wala haujibu sms zangu"


"Tadhali sana kama watu wamekuteka ....basi niambieni mnataka niwape nini ili mke wangu arudi....nampenda sana na sipo teyari kumpoteza kwa namna yeyote ile ....."


Shaibu akaangalia sms zote kisha akatabasamu huku akijisemea kuwa mwanaume mwenzake amepatikana siku hiyo.


Ingawa alijiambia hivyo ila sms ya mwisho ilimtisha sana , akaona jinsi mume wake anavyompenda Judy..Roho ya utu ikamwingia, akaamua kumwamsha Judy. Alipoamka akamwambia kuwa simu yake ilikuwa inaita. Judy alipoangalia alikuta ni mume wake, akachanganyikiwa sana na alipoangalia saa ilikuwa teyari usiku mwingi sana.


"Mamaa nimekwisha jamani....."


Judy alijikuta akitoa sauti huku akiendelea kukagua sms za mme wake. Shaibu kwake hakuwa na pressure sana kwani teyari alishajua ni mke wa mtu hata kabla hawajafanya lolote kwa wakati ule mchana Judy akiwa amelala wakati tumbo linamuuma aliona namba ya mtu huyo ambaye alihisi moja kwa moja atakuwa mume wake.


Judy akatoka kitandani haraka na kuvaa nguo zake , baada ya hapo akataka atoke nje ili aondoke. Ila sauti ya Shaibu ndiyo ikamfanya asimame kumsikiliza.


"Subiri kwanza kabla hujaondoka kuna jambo nataka nikuambie....."

Shaibu alisema.


*itaendelea....*


Mke wa mtu na mpenzi wa mtu wamekutana....teyari wameshajuana vyema.


Hivi kosa lilikuwa la nani hapa????


Usikose sehemu ijayo kujua Shaibu atamwambia nini Judy usiku huo, je nini kitatokea ilikiwa Judy ataenda kwa mume wake usiku huo? Vipi mume wake aliyeahidi kumlinda kwa gharama yeyote akimjua bwana miamala Shaibu?


Ni balaaa ,yapo mengi ya kujifunza mbeleni huko.


Cha msingi....


*kabla hujatenda, fikiria matokeo.....*





Shaibu na Judy wameingia kwenye ulimwengu ambao pengine mmoja wapo hakuutarajia hasa Judy ila ukaribu wao ndio ukawafanya wafikie huko walikofika. Judy anajisahau chumbani kwa Shaibu mpaka anashtuka teyari muda ulikuwa umeenda sana yaani ilikuwa usiku wa manane.....Anaona bora aondoke muda huohuo ila Shaibu anamwita na kutaka kumwambia kitu....


*Sasa endelea hapa...*


Judy akasimama huku mkono wake mmoja ukiwa umeshika kitasa cha mlango. Shaibu akasema,


"Ngoja kwanza hebu utulie, mbona unakurupuka ? Una shida gani? "


Shaibu akajifanya hafahamu chochote, akamchota akili Judy.


"Naomba uniache ,tutaongea siku nyungine...."


Judy aliongea kisha akaanza kunyonga kitasa cha mlango. Shaibu akamsogelea Judy na kumshika mkono kisha akamleta kifuani pake huku akimuuliza nini kimemsibu na nani aliyekuwa anampigia simu kwa sauti ya upole na yenye kunyenyekea sana, sauti ambayo hata ukiwa umepaniki basi nawe utarudi na kushusha hasira zako.


Judy naye kwa upole akajibu,


"Huyu ni mume wangu, yaani sikutegemea kama tutafikia huku, umeniharibia Shaibu...."



ITAENDELEA

Wednesday, November 2, 2022

NI SHIIDA! - 5

 





    Chombezo : Ni Shiida!

    Sehemu Ya Tano (5)





    ?Baba Juliana? Haiwezekani hata kidogo kuuvunja mlango, haiwezekani?



    Mama Juliana alishindwa kumdhibiti baba Latifa. Akaamua aache baba Latifa auvunje kisha wakaingia ndani na kufikia sebuleni moja kwa moja huku wakimsubiri Juliana.

    ***

    ?Sweet! Sweet! Embu amka!? alisikika Bitungu akimwamsha Juliana. Juliana ambaye usingizi ulikuwa umemchukua baada ya kupigishwa gwaride la kufa mtu.

    ?Hee! Kwani saa ngapi sasa hivi??



    ?Saa tatu kasoro usiku, ujue tumepitiwa na usingizi halafu mlio nilioutegesha kwenye simu kumbe nilikosea kurekebisha muda!?

    ?Unasemaje Bitu!?

    ?Simu sweet!?



    ?Simu eeh! Umenifanyia makusudi Bitungu mpenzi wangu, ona sasa na funguo za nyumbani ninazo, mama hawezi kunielewa!??Funguo! Ina maana umeondoka na funguo za nyumbani kwenu? Lakini si atakuwa nazo nyingine!?

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ?Wee humjui tu mama yangu, siku moja utamuona! Mama aliniachia nyumba na miye nikajifanya mbishi kwa ajili ya mapenzi yako, nikafunga na kuja na ufunguo, hizo hapo kwenye kimkoba changu.?



    Juliana aliongea kimtego huku Bitungu asijue mama yupi anayezungumziwa. Aliinama chini kisha akakiinua kichwa na kuangaza kwenye kile kimkoba na kuanza kuuangalia ufunguo wa nyumbani kwao. Akahamia kwenye simu ambapo aliichukua na kukutana na missed call zaidi ya nne zote zikiwa zimetoka kwa mama yake.



    ?Nimekwisha mimi, nimekwisha leo!?

    ?Umekwisha kwa kipi???Ona sasa! Kumbe alikuwa akinitafuta kwenye simu!?

    ?Fanya basi uvae, uende fasta!?



    Juliana hakutaka cha kusikiliza tena, hata kuingia bafuni kujimwagia maji aliona ni kazi kubwa zaidi ya kuchukua nguo zake na kuvaa haraka-haraka, akaitumbukiza ile simu kwenye kimkoba chake kisha akatoka nduki bila hata ya kumuaga Bitungu vizuri.



    Mpaka inafika saa nne na nusu Juliana alikuwa nje ya nyumba yao. Taa zote za ndani zilikuwa zimewashwa na hakuelewa vizuri imekuwaje wakati funguo anazo.

    ?Au mama alikumbuka kuchukua funguo zake??



    Alijiongelesha Juliana huku akipiga hatua mdogomdogo kuelekea mlango wa mbele. Akiwa katika mwendo wa kunyata, wazo likamjia. Wazo la kuelekea dirishani kwa wazazi wake na kusikilizia kujua kinachoendelea. Alipofika kimya kilikuwa kimetanda na wala taa hazikuwa zimewashwa hivyo akabadili wazo na kuelekea sebuleni moja kwa moja. Kabla hajafika kwa mbali akasikia sauti za wazazi wake wakiteta!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ?Hadi sasa, hakuna cha huyo Juliana wako wala nani? Kwa hiyo mlitaka kunilaza nje hadi sasa hivi, kama nisingepata wazo la kumchukua baba Latifa avunje ingekuwaje??

    ?Baba Juliana jamani si yameshakwisha!?



    ?Hayawezi kuisha hadi nijue Juliana yupo wapi hadi sasa hivi? Na utakuwa unajua hutaki kuniambia tu!?

    ?Najua chochote nitakachokwambia bado utaniona muongo tu, subiri labda akija!?



    Juliana alizidi kuogopa. Alitamani arudi zake Bagamoyo akajichimbie na Bitungu waliendeleze gwaride kuliko kuingia ndani ambapo aliona kumeshachafuka. Akili yake ilizidi kuchemka huku mkono wake mmoja ukiwa umekishikilia kitasa cha mlango tayari kwa kukifungua.



    ?Juliana?? aliita baba Juliana kwa hasira baada ya kuhisi kitasa cha mlango kimetikisika.

    Je baba Juliana atamfanyaje Juliana?

    Juliana atasema ukweli alipokuwa?





    Juliana alisita kufungua kile kitasa, akabaki ameduwaa huku mkono akiurudisha.

    "Nani unayefungua mlango kama siyo Juliana?" alisikika baba Juliana.

    "Mh! Baba Juliana?, hata mlango haujafunguliwa unafikiria Juliana tu!"

    "Ndiyo! Sa we' unafikiri atakuwa nani?"



    "Sidhani kama atakuwa Juliana, embu ngoja nikafungue."

    Mama Juliana aliinuka na kusogea hadi mlangoni kisha akafungua ule mlango na kukutana uso kwa uso na Juliana. Juliana aliyeonyesha kutetemeka asijue la kufanya.

    "Haya ulikuwa wapi?"

    "Mama nil..."



    Kabla Juliana hajaanza kujitetea, baba Juliana naye aliinuka kwenye kochi na kuwafuata pale mlangoni.

    "Pumbavu wee ingia ndani mwenyewe!"

    "Baba ndiyo naingia lakini...."

    "Lakini nini? Nimesema ingia..."



    Juliana aliingia huku wazazi wake wakiwa nyuma yake. Aliongoza moja kwa moja hadi kwenye kochi kisha akaketi huku akishikashika vidole vyake vya mikononi.

    "Niambie ulikuwa wapi na kwa nini uliondoka na funguo?" alianza kuhoji mama Juliana kwa ukali.

    "Mama niliondoka na marafiki zangu walikuja kun..."

    "Kimya! Ishia hapo hapo! Na ufunguo ukauacha wapi?"

    "Nilijua nitawahi kurudi."



    Juliana akiwa katika kujitetea. Yale majibu yalimkera sana baba yake. Alichokifanya aliongoza chumbani kwake moja kwa moja na kurudi akiwa na mkanda wa suruali kisha akataka kumvaa Juliana.

    "Nipishe mama Juliana! Nipishe nimuadhibu mpumbavu huyu."



    Roho ya huruma ilianza kumuingia mama Juliana. Akajikuta amemkumbatia Juliana ili aepukane na kipigo cha mkanda kutoka kwa baba yake. Akiwa bado katika kumkumbatia mama Juliana akahisi kitu puani mwake. Harufu kali ya ‘pafyumu' kutoka kwa Juliana ikamuingia puani, akamwachia Juliana kwa hasira.



    "Muadhibu, mpige tu pumbavu huyu!"

    Baba Juliana alimvaa Juliana na kuanza kumpiga mfululizo. Juliana alijitahidi kujifunika kwa mkoba wake lakini kichapo kilikuwa kikimuingia vilivyo.

    "Baba nisamehe, sitorudia tena! Nisamehe!"



    Baada ya kumpiga kwa muda, baba Juliana aliutupa ule mkanda pembeni.

    "Haya nenda chumbani huko."



    Muda wote mama Juliana alikuwa amepigwa na butwaa. Kuanzia Juliana anapigwa hadi anamaliza kupigwa bado alikuwa hajielewielewi, ile harufu ya pafyumu aliyoisikia kwa Juliana ilimpagawisha.

    "Ina maana alikuwa kwa Bitu wangu?" aliwaza na kuwazua lakini bado hakupata jibu.

    "Bitu kumbe msaliti kwangu? Kujitoa kote kule mpaka Bagamoyo ananisaliti bado?" Akili ya mama Juliana bado ilikuwa haipo sawa.



    "Na wewe vipi?" alihoji baba Juliana baada ya kumuona mama Juliana amezubaa mwenyewe.

    "Hapana mume wangu, namfikiria huyu mtoto kwa jinsi alivyobadilika, yaani Juliana wa kutujia usiku namna hii?"

    "Wee si ndo uliyemdekeza, na huu ni mchezo wenu wa kurudi muda huu wala hakuna cha kujitetea hapo."

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hapana mume wangu."

    "Na huyo mtoto ana bahati naumwa la sivyo ningemuua leo."

    Baba Juliana bado alikuwa katika hasira. Aliondoka pale sebuleni na kuelekea chumbani kwake huku akimuacha mama Juliana peke yake pale sebuleni.

    Alichokifanya mama Juliana ni kukaa kwa muda kwenye kochi kisha akaichukua simu yake na kuanza kutuma meseji kwa Bitungu.



    "Mambo baby wangu! Nilifika salama, nakuwaza sana hadi nakosa raha!"

    Akaituma na baada ya muda, Bitungu akaijibu.



    "Hata mimi Sweet wangu, siwezi kuisahau mechi ya leo. Si unakumbuka hata uwanja tuliochezea, yaani hapa nimejilaza hoi sijiwezi natamani ungekuwepo ungenikandakanda kwa maji ya vuguvugu."

    Mama Juliana aliisoma meseji hiyo na kuiangalia mara mbilimbili kwa hasira za juu. Akajiongeza kuwa huenda Bitungu amechoka zaidi kwa kukutana na Juliana japokuwa hakuwa na hakika zaidi ya kuifananisha harufu ya pafyumu. Akamwandikia tena Bitungu meseji.



    "Baby wangu hivi ile pafyumu yako inaitwaje tena? Maana nimeipenda harufu yake nataka kesho nikainunue ili nikiwa naitumia niwe nakukumbuka."

    Mama Juliana alikuwa mjanja wa maneno, aliweza kuyaungaunga na kumdanganya Bitungu. Akaingia kwenye mstari na kumjibu.



    "Waaaaooh! Sweet wangu, ina maana leo hii umeisahau? ile inaitwa UDV."

    Meseji ikamfikia mama Juliana. Ikamuuma sana baada ya kujua ni UDV ambayo harufu yake ni ile aliyoisikia kwa Juliana. Alichotaka kujua ni kupata uhakika wa jina la pafyumu. Aliondoka pale sebuleni na kuongoza moja kwa moja hadi chumbani kwa Juliana. Akamkuta amejitupa kitandani huku akiendelea kulia kwa uchungu.



    "Wee Juliana? Embu acha uchuro wako hapa!"

    Aliongea mama Juliana huku akifuata mkoba ule wa Juliana na kuanza kupekua ndani yake. Jicho lake likagongana na kichupa cha pafyumu. Pafyumu iliyokuwa ikimuumiza kichwa. Pafyumu ya UDV.

    "Wee Juliana! Juliana?"





    Aliita mama Juliana kwa ukali.

    Ndiyo kwanza Juliana aligeukia upande wa pili huku akiendelea kulia kwa maumivu, maumivu yale ya kipigo kutoka kwa baba yake. Ilibidi Mama Juliana atumie nguvu za mikono na kumvuta kwa nguvu.

    ?Mama niacheee!!?



    ?Si nakuita we mwanaizaya! Kumbe ulikuwa ukinisikia hutaki kuitikia, si ndiyo??

    ?Hapana mama, sijiskii vizuri mwili wote unaniuma!?

    ?Hata kama unakuuma, ujue Juliana!?



    Mama Juliana akapunguza sauti na kuifanya isikike kwa chini ili mumewe asije akasikia kinachoendelea. Lengo lake ni kumuweka Juliana kwenye kumi na nane ajibu kila kitu kuhusiana na ile pafyumu aliyoitoa kwenye mkoba wake. Pafyumu ya UDV.

    ?Nakusikia mama!?



    Juliana alijiweka vizuri. Hakuwa amebadili nguo tangu ametoka Bagamoyo alipokuwa na Bitungu. Alishusha miguu yake kwenye kitanda kisha akakaa.

    ?Nakusikia mama.?



    ?Mwanangu hivi kwa nini unapenda kufanya kitu kwa makusudi? Si nilikwambia usitoke??

    ?Ndiyo mama ila walikuja marafiki za...?

    ?Hivi mara ngapi haohao marafiki zako wanakupotosha we bado unafuatana nao. Kwa nini wewe usiwapotoshe mpaka wao ndiyo wakufanyie hivyo. Halafu mwanangu mpendwa unajua kabisa baba yako ana hasira.

    ?Najua mama.?



    ?Kama unajua kwa nini sasa mwanangu unakosea!?

    ?Nisamehe mama!?

    ?Mimi nilishakusamehe hata kabla baba yako hajakuchapa na mkanda. Ila mwanangu naomba uniambie mimi kama mama yako.?

    ?Nakusikia mama.?

    ?Una mpenzi??



    Juliana alionyesha kushtuka. Alisogea kwenye kile kitanda. Woga ulimshika kwa muda huku macho akiyatoa.

    ?Hapana mama, bado najitunza!?

    ?Kweli unajitunza mwanangu Juliana??



    ?Ndiyo mama wala usiwe na wasiwasi na mimi!?

    ?Sasa mwanangu usiku wote huu tangu mchana ulikuwa wapi??

    ?Marafiki mama...?



    ?Haya hilo tuliache, mwanangu hii pafyumu nani aliyekununulia??

    Juliana alishtuka kwa mara ya pili. Aliona sasa huenda mama yake alimuona kipindi kile Bagamoyo akiwa katika kupanda bajaji katika ile gesti alipokuwa na Bitungu. Mama Juliana alimuonyeshea Juliana ile pafyumu.



    ?Mama hiyo niliinunua mwenyewe!?

    ?Wapi? Na nani alikupa pesa??

    ?Nilijibanabana mama.?



    ?Hii ni pafyumu ya kiume mwanangu na wewe haikufai.?

    ?Nimekuelewa mama ila miye niliipenda harufu yake...?



    Wakiwa katika majibizano, bila hata ya hodi mara baba Juliana akawavamia. Baba Juliana aliyekuwa ameshikilia simu mbili, moja yake moja ya mke wake. Kitendo cha kuingia akamkuta mama Juliana akiwa bado ameishikilia ile pafyumu huku akiwa amemnyooshea Juliana.



    ?Ina maana huyo mpuuzi bado hajalala siyo??

    ?Jamani! Nina maongezi naye kidogo ila atalala tu.?

    ?Na hiyo pafyumu uliyoshika ndiyo maongezi yanaingia vizuri siyo??

    ?Hapana mume wangu.?



    ?Embu leta, leta!?

    Baba Juliana akaiwahi ile pafyumu na kumpokonya mkewe. Akawa ameshagundua kuwa ni ya kiume.

    ?Haya mnaweza kunieleza hii ya nani??

    Wote kimya...

    ?Si naongea na wewe mama Juliana??

    ?Mume wangu embu basi punguza hizo hasira.?



    ?Msinichanganye? Ni nani anayetumia pafyumu ya kiume kati yako na Juliana??

    Juliana aliendelea kutetemeka. Alijihisi kojo kumtoka kwani tayari kitumbua kilikuwa kimedondoka katikati ya mchanga, aliona ni bora alivyogundua mama yake kuwa ni ya kiume kuliko alivyogundua baba yake.



    Alikuwa katika kusitasita huku akitaka kusema ukweli wote kuhusu uhusiano wake na mama yake pamoja na Bitungu ili litakalotokea litokee.

    ?Hiyo pafyumu alin...?



    Kwa haraka mama Juliana alichezwa na machale. Akamuwahi Juliana kabla hajamalizia kuongea.

    ?Mume wangu hii hapa nimeipata huko kwenye vikoba nasikia ni nzuri kwa mabinti hasa mtoto wetu huyu, ndiyo nikawa nimemletea kama atapendezwa na harufu yake nimuachie.



    ?Unasemaje mama Juliana? Ina maana ushaniona mtoto siyo? Haya sawa umemletea mwanetu safi! Embu nielekeze ni wapi wanapouza pafyumu ikiwa robo??



    Kabla mama Juliana hajajibu, simu ikaita. Baba Juliana akaangalia mkononi na kugundua ni simu ya mama Juliana ndiyo ilikuwa ikiita huku jina likiandikwa Bitu. Akaichukua na kuipokea kisha akakaa kimya bila kuongea.

    ***

    Muda wote Bitungu alikuwa hana raha. Aliwaza sana maneno aliyoambiwa mara ya mwisho na mama Juliana. Maneno juu ya pafyumu. Akili zote zilimuhama na kuona huenda anajuana na Juliana.

    ?Haiwezekani? Lakini kwa nini aniulize habari za pafyumu??



    Alijiuliza Bitungu na kujijibu mwenyewe kisha akainuka pale kitandani na kuelekea kwenye meza ambapo aliiweka ile pafyumu yake ya UDV. Alipofika hakuona chochote.

    ?Ina maana kuna mchezo nafanyiwa au? Sasa itakuwa wapi??



    Bitungu aliendelea kujiuliza mwenyewe. Alichokifanya aliichukua simu yake na kuanza kupiga namba ya mama Juliana. Iliita bila kupokelewa hadi ikakata, akajaribu kupiga kwa mara nyingine tena ikapokelewa.

    ?Mpenzi wangu mbona hupokei simu yangu? Embu niambie pafyumu yangu ya UDV uliichukua?







    Bitungu aliendelea kufloo lakini bado upande wa pili hakujibiwa kitu chochote zaidi ya kimya kutanda. Alichokifanya aliikata simu na kuipiga kwa mara ya pili. Napo ikapokelewa tena na kumfanya atabasamu.





    "Sweet wangu nitakuchukia? Embu niambie kama nimekuudhi nisamehe jamani bado nakupenda na sitaki kukupoteza hata kidogo!"



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bitungu aliendelea kuchanika maneno ya kimahaba bila hata kujua kinachoendelea upande wa pili. Safari hii aliipoza zaidi sauti yake huku akiwa amejilaza juu ya kitanda cha gesti na kuendelea kutoa sauti ya kubembeleza.





    Akiwa katika kubembeleza bila kujibiwa mara akasikia makelele ya majibizano kati ya mume na mke yakiendelea. Akainuka harakaharaka pale kitandani akiwa hajiamini kwa kinachoendelea. Akaisogeza tena simu yake sikioni na kuendelea kusikia majibizano yale.





    ***Ugomvi uliendelea kuwa mkali kati ya baba Juliana na mkewe. Simu iliyopigwa na maneno yaliyokuwa yakiongelewa yalizidisha hasira za baba Juliana. Alijiangalia mara mbilimbili mwili wake ulivyotota kwa jasho na meno yakiumana kisha akamgeukia mkewe huku akimkazia macho na vidole akimnyooshea.





    "Nikisema nianze kukutandika kama mtoto wako huyo nitakuwa nimekosea?"

    "Kwani nimekosa nini mume wangu?""Si simu! Unajifanya hujui kinachoendelea?"

    "Imefanyaje? Kwani we huwa hupigiwi simu na watu waliokosea namba?"





    "Mama Juliana? Hivi ni mtoto gani utamdanganya kwa hiki kinachoendelea kwenye simu?"

    "Mume wangu, leo unaonekana kuwa na hasira sana. Hiyo namba kubaliana na mimi kuwa imekosewa na imekuja kwa bahati mbaya.""Nakujisevu imejisevu kwa bahati mbaya siyo!"





    "Kwani imejisevuje mume wangu si namba tu imetokea!"

    "Batu sijui Bitu! Si umeandika wewe hapa unajifanya hujui siyo?"

    Baba Juliana alimsogezea kwa ukaribu mama Juliana na kuanza kumwonyesha jina la Bitu kwenye ile simu yake. Simu haikuwa imekatwa hali iliyomfanya mama Juliana ashtuke na kutaka kuikata lakini baba Juliana akamuwahi na kuusogeza mkono wake pembeni.





    "Unataka kufanyaje? Si umesema amekosea! Sasa kuanzia sasa hii namba nakula nayo sahani moja ama zangu ama zake pumbavu!""Msimamo wangu uko palepale mume wangu, siwezi kukusaliti hata siku moja na hiyo namba imekosewa.





    Kama ukichukua maamuzi mabaya shauri yako wala usinishirikishe!"

    "Nitaelewa tu msaliti ama siyo msaliti ngoja nilifanyie kazi. Kukuachia uhuru na mtoto wako mnautumia vibaya!""Amua utakavyofanya na ukweli utaujua maana nakwambia sijui lolote unaendelea kukazania, amua tu!"





    Iliimbidi mama Juliana azuge kuwa amekasirika ili baba Juliana aamini lakini wapi! Ndiyo kwanza baba Juliana aliondoka chumbani mule na kumuacha Juliana na mama yake wakiwa kwenye butwaa. Vita ikaanza upya kwa Juliana na mama yake.





    "Halafu wewe mshenzi wewe? Kwanza una bahati sana baba yako kasahau kuhusu pafyumu hii. Haya niambie ukweli umeitoa wapi hii pafyumu ya kiume?""Mama si nilishakwambia kuwa nilijibanabana nikanunua!""Unasemaje? Ukanunua siyo?"





    Hasira za mama Juliana zilimwishia Juliana. Tayari alishajiona amempoteza Bitungu kwa jinsi mumewe alivyoondoka kwa hasira akiwa na simu yake mbaya zaidi aliposema atakula nayo sahani moja kuhakikisha anamjua na kumpata. Alimshika Juliana kwa nguvu kisha akamwachia."Nakupa nusu saa, naenda chumbani huko alipo baba yako, nikirudi nataka uiniambie ukweli wote hii pafyumu umeitoa wapi?"





    Kitendo cha mama Juliana kuondoka huku nyuma kamwacha Juliana na maswali ya sintofahamu. Cha kwanza mama yake alivyojichanganya kwenye jina la Bitu lililokuwa kwenye simu ya mama yake na pili ni kumjibu mama yake juu ya ile pafyumu alipoitoa.





    "Nitamweleza pafyumu ya Bitungu akinipiga namwambia baba ukweli wote hadi nilivyomshuhudia gesti kule Bagamoyo kama kukosa tukose wote tu."Juliana alijiongelea na kujijibu mwenyewe. Aliiweka ile pafyumu pembeni kisha akajipindua pale kitandani na kuanza kuutafuta usingizi akiwa na maswali kibao kichwani.

    ***

    Muda wote Bitungu alibaki na bumbuwazi asijue lipi la kufanya. Maneno ya mwisho aliyoyasikia kwenye simu yalimpagawisha zaidi. "Ina maana atakula sahani moja na mimi? Hapana mimi kidume kwanza atakuwa ni hawara wake tu."





    "Lakini bado picha haijanijia! Kweli sweet wangu ndiyo aniingize kwenye matatizo? Na kwa nini simu alimpa mume aipokee kama kweli ananipenda?"Alichokifanya Bitungu ni kutoka moja kwa moja hadi bafuni na kuoga kwa mara nyingine kisha akavaa nguo na kulipia mule gesti na kuondoka.





    "Kama anajijua ni mke wa mtu basi na mimi ni mume wa mtu, naenda kuusema ukweli wote kwa huyo mumewe anayetaka kula sahani moja na mimi."







    Hakujali giza lililokuwa limefunika. Muda wa saa nne za usiku wala haukumtisha ndiyo kwanza alielekea moja kwa moja hadi kituo cha daladala ambapo napo alikuta patupu. Daladala nyingi zilikuwa zimeshakwenda kupaki lakini hilo halikumuuza kichwa Bitungu.





    ?Haiwezekani nikaingia matatizoni eti kisa mwanamke!?

    Alijiongelea mwenyewe Bitungu huku akisubiri usafiri wa daladala. Hadi nusu saa inakatika bado hakukuwa na dalili zozote za kutokea kwa daladala zaidi ya Bitungu kuendelea kujiegesha kwenye eneo maalum la kukaa abiria.





    ?Lakini? Hivi kwa nini nisirudi kulala halafu asubuhi nikadamkia huko? Hapana ila nisubiri kwanza tu.?

    Bado akili ya Bitungu haikuwa imekaa sawa. Baada ya kukaa kwa muda moyo wake ukaingiwa na furaha. Furaha baada ya kuiona daladala ikiingia kituoni hapo ikitokea katikati ya jiji la Dar.

    ?Haipakizi tena hii, inaenda kulala.?





    Aliongea kondakta wa ile daladala baada ya Bitungu kupitisha mguu wake akitaka kuingia ndani.

    ?Kama haipakizi sawa nitaenda kulala hukohuko inapolala.?





    ?Mwana mbona husikii! Hii inalala hapo pembeni mpaka asubuhi saa kumi na mbili ndiyo inahamsha tena.?

    ?Lakini nyie makonda mnajifanyaga wajanja sana, mnasema haipakizi halafu baada ya muda inapakiza tuwaeleweje??



    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliongea Bitungu kwa jazba. Lengo lake akilini lilikuwa ni kutoka tu maeneo yale ya Bagamoyo hata kama atafika mjini usiku mnene ingekuwa sawa tu ili mradi atoe dukuduku lake kwa baba Juliana.





    Ile daladala ilipomaliza kushusha ilijisogeza hadi pembeni na kupaki. Bitungu alinyong?onyea ikambidi akubaliane na ukweli kuwa muda ule alikuwa amechelewa. Alichokifanya ni kurudi mpaka kwenye ile gesti kwa mara ya pili na kuchukua chumba kingine kwa lengo la kudamkia asubuhi na mapema kwa mama Juliana akauseme ukweli kwa mumewe.

    ***

    Hadi asubuhi kunakucha, si mama Juliana wala baba Juliana ama Juliana aliyekuwa ameamka. Wote walikuwa wamepitiwa na usingizi. Haikuwa kawaida ya baba Juliana kupitiwa na usingizi kiasi kile ila ilimtokea kwa kuwa alikuwa bado hajisikii vizuri kiafya.





    Juliana alikuwa mtu wa kwanza kushtuka chumbani kwake. Alitoka hadi sebuleni ambapo saa yao ya ukutani ilimuonyesha kuwa tayari ilikuwa imetimia saa mbili za asubuhi. Kumbukumbu za kichapo cha jana yake usiku bado zilimtawala akilini. Kikubwa kilichomuuma zaidi ni kuendelea kuchanganywa kimapenzi na Bitungu. Aliiwasha simu yake na kumpigia Bitungu.





    ?Bitungu mpenzi!?

    ?Niambie sweet, vipi mzima jamani!?

    ?Bitu miye naumwa na nataka uje unione nyumbani??

    ?Unaumwa? Nini tatizo??





    ?Bitu naumwa kwa kukuwaza wewe, unaniweka kwenye wakati mgumu wakati unajua fika kuwa nakupenda!??Sijakuelewa? Nakuweka katika wakati mgumu kivipi wakati wajua fika bado nipo huku Bagamoyo na wafanyakazi wenzangu na huku semina iliyonileta itaisha baada ya wiki.?

    ?Nikuulize kitu bebi??





    ?Nakusikiliza uliza tu??

    ?Unanipenda kabisa kutoka moyoni au unanitamani embu niambie ukweli bebi wangu, samahani lakini!?

    ?Hapana sweet kama ningekuwa nakutamani mbona ningeshaachana na wewe siku nyingi tangu nilipomaliza shida zangu kwa mara ya mwisho.?





    ?Nafurahi kusikia hivyo lakini kuna jambo moja linanitatiza kweli.?

    ?Lipi hilo na mbona leo umeamka na maswali hivyo mpenzi wangu??

    ?Yote hiyo kwa sababu nakupenda, nakuwaza kila muda na sipendi kukupoteza hata siku moja.?

    ?Hata miye sipendi nikuache, haya niambie kinachokutatiza kipi hasa??





    ?Bebi niambie ukweli wako kabisa maana siku nikigundua nitaumia sana! Niambie ukweli umeoa ama hujaoa???Ningeoa mke si ungemuona? Uko peke yako mpenzi wangu na ndiyo maana hata tunavyokutana huwa sina wasiwasi wowote.?

    ?Kweli bebi wangu??





    Juliana alimtega Bitungu kwa makusudi, lengo lake ni kummbana atambue kuwa anashiriki mapenzi na familia moja yaani yeye na mama yake. Kila alipokuwa akitaka kumwambia ukweli alikuwa akisita na kumfanya aongee mengine. Mateso aliyoyapata jana yake usiku yalikuwa yamesababishwa na Bitungu huyohuyo kwa kiasi kikubwa.





    Moyo wake Juliana ulishamwambia kuwa aachie ngazi. Amwachie mama yake aendeleze mapenzi yao. Juliana alijikaza kwa muda akakaa kimya kisha akaikata ile simu aliyokuwa akiongea na Bitungu. Baada ya kuikata akaamua kutuma meseji ya hasira na ya mwisho kwa Bitungu.





    ?Naomba unielewe kwa makini! Kuanzia sasa sitakuita tena mpenzi, bebi wala honey. Mapenzi ya mimi na wewe Bitungu naomba yaishie hapa leo hii. Nilikupenda Bitungu lakini ukweli nilioujua ndiyo umenifanya kuchukua maamuzi haya magumu, ukweli wa wewe kuto....?



    ...Likishaondoka zake tu nitakwambia Bitu wangu wala usiwe na shaka!"

    "Haya bebi wangu, nakupenda! Wewe ndo kila kitu moyoni mwangu.."





    ILIPOISHIA

    ...Likishaondoka zake tu nitakwambia Bitu wangu wala usiwe na shaka!"

    "Haya bebi wangu, nakupenda! Wewe ndo kila kitu moyoni mwangu.."

    SEREBUKA NAYO SASA...



    Baba Juliana aliisoma meseji ile aliyoituma Bitungu kwa hasira kali. Akaizima kabisa simu ile na kuiweka pembeni kisha akainamisha kichwa chake chini na kujikaza kiume. Moyoni alikosa raha, hakuwa na amani tena.



    "Hivi mama Juliana wa kunifanyia hivi? Kitu gani ambacho simridhishi mwanamke huyu?"

    Alijiongelea na kujijibu mwenyewe. Aliamua kutoka nje ya ofisi lengo likiwa kwenda kupata hewa zaidi. Kile kiyoyozi kilichokuwa kimefungwa ofisini kwake alikiona hakitoi hewa yoyote.

    ***

    Siku nzima mama Juliana alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, kila muda alikuwa akimuita Juliana bila kumwambia chochote. Wakiwa wametulia jikoni mara simu ya Juliana ikaita.

    "Haloo!"



    "Mama yako yupo wapi?"

    "Niko naye hapa!"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Nipe niongee naye."

    Bado hasira za maneno kutoka kwa Bitungu aliyokuwa ametumiana naye kwa njia ya meseji hazikuwa zimemuisha.



    "Mama! Simu yako, baba anataka kuongea na wewe!"

    "Haloo!""Nisikilize kwa makini mama Juliana! Nina jambo zuri nataka kukwambia mke wangu!"

    "Nakusikia mume wangu!""Nitachelewa kurudi leo lakini ikifika saa moja nitakuhitaji uje sehemu sawa?"

    "Haya niambie ni wapi?"



    "Kuna sehemu nitakuelekeza baadaye tukishaambiwa rasmi hapa ofisini kwani bosi wetu ametushtukiza kuwa leo mke wake amewasili mchana na jioni tutajumuika naye katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.""Haya utaniambia mume wangu ngoja niandae nguo ya kuvaa kabisa!"



    Baba Juliana akawa ameshacheza na akili ya mkewe. Akaikata simu kwa makogo huku akiamini mtego wake utanasa kwa asilimia zote. Akamtumia na meseji ya msisitizo.

    "Usisahau kunibebea na koti langu la suti nililisahau!"

    "Haya, umesema saa moja!"

    "Ndiyo?"



    "Sasa simu yangu unayo nitakujaje mume wangu?"

    "Tumia simu hiihii ya Juliana!"

    "Haya baadaye basi!"

    "Sawa usisahau mke wangu uwepo wako ni muhimu sana kwa siku ya leo.

    ***

    Ilipofika saa kumi na mbili baba Juliana alikuwa bado kazini. Malengo yake ni kuwakutanisha Bitungu pamoja na mama Juliana ili aujue ukweli. Hakuwa ameiwasha ile simu ya mama Juliana tangu mara ya mwisho wamalize kutumiana meseji.



    Kitendo cha kuwasha tu simu ya mama Juliana aliyokuwa nayo, meseji mfululizo zikaanza kuingia, zote zikiwa ni lawama kutoka kwa Bitungu."Sweet, kwa nini unanifanyia hivi? Mbona unanizimia simu lakini muda wote nakutafuta?"



    Baba Juliana akamjibu meseji karibia zote.

    "Sorry bebi wangu jamani, huku kwetu umeme ulikatika na hapa nilipo ndiyo kwanza simu nachati na wewe huku ikiwa kwenye chaji.



    "Haya muda si umeshafika jamani fanya basi tukutane mwenzio nina hamu na wewe kweli!"

    "Tena una bahati nimeshatoka Bagamoyo tangu saa saba za mchana, nipo maeneo ya Tegeta."
"Huko unafuata nini bwana njoo tukutane baa ya Sweet Mama hapa karibia na Sinza Mori kuna gesti moja nzuri sana."



    "Basi nipe nusu saa sweet wangu."

    Bitungu alikuwa na pupa. Hakutaka kuambiwa chochote, meseji kutoka kwa baba Juliana kwa kutumia simu ya mama Juliana zilimchanganya. Asilimia zote alijua anachati na mama Juliana.

    Shangwe zilimtawala baba Juliana na kujiona zoezi lake linaenda kukamilika ndani ya muda mchache. Tayari alikuwa ameshamteka akili Bitungu na kumsubiria ajilete tu.



    "Nimeshafika sweet wangu uko wapi?"

    "Nitachelewa bebi ila chukua chumba kabisa kisha niambie namba ngapi nitakuja moja kwa moja."

    Muda wote baba Juliana alikuwa eneo la nje ya Baa ya Sweet Mama akimsubiri Bitungu. Bitungu alifika na kuchukua chumba namba 32 kisha akatuma meseji.

    "Nimeshafika! Nipo chumba namba 32."



    "Haya bebi wangu nipo maeneo hayahaya nikute mlango wazi huko!"

    Mama Juliana naye alikuwa amewasili. Alikuwa ameongozana na Juliana lakini alipofika alishikwa na mshangao baada ya kumkuta mumewe akiwa amekaa mwenyewe huku kukiwa hakuna dalili yoyote ya sherehe.



    "Juliana amefuata nini hapa?"

    "Mume wangu si umeniambia sherehe nikaona bora tuwe wote!"

    "Ok, sasa tunaelekea kwenye chumba namba 32 kwenye sherehe yenyewe."



    Hofu kubwa ilianza kumjaa mama Juliana. Mapokezi hakukuwa na mhudumu hivyo wakaongoza moja kwa moja wote watatu huku akisitasita lakini baba Juliana alikuwa nyuma yake akimsukuma.

    "Sherehe ipo humu ndani ingia!"

    Baba Juliana akamsukuma mkewe, akafungua kitasa na kuingia huku akibaki nje ya mlango na Juliana.

    "Sweet wangu!"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Haraka Bitungu akamuwahi mama Juliana.

    "Nani?"Kabla Bitungu hajamalizia, baba Juliana akiwa na Juliana wakaingia chumbani. Bitungu akashangaa zaidi."Bitungu?"



    Juliana uzalendo ukamshinda akasimulia yote kuhusu Bitungu alivyowachanganya na mama yake huku mama Juliana akibaki hajielewielewi.



    "Nimejua yote kuanzia mwanzo kisha wewe mama kuanzia leo mimi na wewe ndiyo basi baki na huyo mpumbavu wako. Meseji zote hizi hapa kama ushahidi kwa ndugu zako."



    ************************MWISHOOOOOO*******************?


    .

NI SHIIDA! - 4

 






Chombezo : Ni Shiida!

Sehemu Ya Nne (4)





"Ina maana Mama Zai ndiyo alikuwa amepiga?"

"Sijui mama, wala sikuangalia jina!"



Alichokifanya mama Juliana ni kuangalia sehemu ambazo simu ile imepokelewa na kugundua kuwa alifanyiwa mchezo na Juliana. Mchezo wa kukatiwa simu ya Bitungu.

"Kwa nini umekata simu yangu!"



"Hapana mama iliita yenyewe na kukatika!"

"Ina maana miye mjinga sijui simu? si nakuuuliza?"

"Kweli mama!"



Mama Juliana aliiweka pembeni ya bafu simu ile na kumfukuza Juliana arudi chumbani aendelee na kazi ya usafi.

Juliana alijirudia zake ndani akiwa amejiongeza vya kutosha, alishaelewa picha kamili juu ya kitakachotokea mbeleni. Alichoamua ni kwenda kuchukua simu yake na kumpigia Bitungu.

"Haloo!"



"Yes baby! Nimekumisi upo wapi sasa hivi?"

"Nipo maeneo ya mbali kidogo!"

"Si uniambie tu hata kama mbali, mbali mbinguni bwana"

"Sweet niko Bagamoyo lakini kesho nategemea kurudi!"

"Bagamoyo? Umeenda lini?"



"Embu subiri kwanza kuna simu ya bosi wangu inaingia, ntakupigia."

Aliongea Bitungu kisha akamkatia simu Juliana. Juliana aliishiwa pozi, penzi la Bitungu lilishamkolea, alijifariji na kuona kuwa huenda ni kweli Bitungu atakuwa amepigiwa simu na bosi wake. Akiwa bado anatafakari kuhusu Bitungu kwa mbali akasikia sauti ya mama yake ikiongea na simu. Hatua kwa hatua akasogelea hadi eneo la sebuleni ambapo mama yake alikuwa na kanga moja tu ametoka kuoga huku akiongea na simu.



"Niambie moja nijue nikukute wapi?"

"Utakuja moja kwa moja hadi gesti ya Tupendane ipo mtaa wa Mchopanga huku Bagamoyo,"

"Kwa nini mpenzi wangu umeamua kwenda mbali huko! Embu njoo mjini bwana!"



"Hukuhuku ndiyo safi na kuna amani kuliko huko kuwa na hofu kibao, kwanza dakika 40 tu umeshafika!"

"Haya ngoja nivae haraka nakuja, nilivyo na hamu asikwambie mtu na leo nataka mechi ya kikubwa, sitaki mechi za mchangani za kuishia nusu saa."

"Kwa hilo usijali, miye ndiye Bitungu!"



"Haya mpenzi nipe saa moja nitakuwa nimeshafika hapo."

Maneno ya Mama Juliana aliyokuwa akiongea kwenye simu yalimuumiza sana Juliana, alijinyong'onyea huku akiwa bado amejificha kwa kujibanza kwenye ukuta wa sebuleni kwao, mama Juliana hakutambua kama Juliana ameyasikia yote aliyoongea kwenye simu.



Alichokifanya Juliana ni kukimbia chumbani kwake na kujiandaa tayari kwa kumfuatilia mama yake hadi atakapoelekea, lengo lake kubwa lilikuwa ni kuhakikisha anamtenganisha Bitungu na mama yake.

"Juliana!"

"Abee mama!"



"Natoka ila nitawahi kurudi mwanangu, nimeitwa sehemu kuna mwenzetu anatakiwa kufanyiwa kicheni pati hivyo nimeitwa kushirikiana nao katika kuandaa."

"Sawa mama!"



"Nakuona unameremeta tu, sitaki utoke na wala sichelewi narudi mchana huuhuu nikukute!"

"Sawa mama!"

Aliitikia Juliana huku akiwa ameshapendeza bila mama yake kujua kuwa wapo safari moja huko aendapo.



http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



Kitendo cha mama Juliana kutoka kuelekea kupanda bodaboda hadi kituo cha Mwenge ndipo akapande daladala za kwenda Bagamoyo, huku nyuma Juliana alizuga kwa dakika chache na kuufunga mlango kisha akampigia simu Bitungu.

"Haloo"

"Ndiyo sweet!"



"Mbona hukunipigia tena ulipomaliza kuongea na bosi wako!"

Juliana alimtega Bitungu makusudi.

"Ohh! Sorry Sweet, nilijisahau hata hivyo simu yangu inaelekea kuisha chaji muda si mrefu itakatika na huku nilipo hakuna umeme!"

"Jamani! Hata Jenereta hamna baby!

"Ndiyo..."



Kabla Bitungu hajamalizia kuongea akaikata simu na kuizima kwa makusudi, alijua ameshamdanganya Juliana na wala hawezi kujua lolote. Alijiweka sawa akimsubiri mama Juliana. Aliamini baada ya muda ataiwasha simu na kumuelekeza alipo.



Kwa upande wa mama Juliana presha ilikuwa juu, alionyesha kuchanganyikiwa. Alishafika kituoni Mwenge na kumpigia simu Bitungu ikawa haipatikani, akashindwa afanye nini.

"Ndiyo nini ananifanyia! Kama alikuwa hataki kuonana na mimi leo si angeniambia?"

Alijisemea mama Juliana huku hasira zikimzidi, hakuonyesha kukata tamaa kwa sababu maji alishaamua kuyavulia nguo, alichokifanya aliendelea kupiga simu ya Bitungu mara mbilimbili huku ikiwa haipatikani, mara ikaita.



"Haloo!"

"Tushaonana watoto sasa!" Aliuliza mama Juliana kwa jazba.

"Hapana chaji mpenzi, vipi umefika wapi?"

"Nipo kituoni Mwenge, tena una bahati nilikuwa nataka kurudi nyumbani nikalale!"

"Ahhaa!! Usinifanyie hivyo mpenzi utaniua panda daladala uje!"

"Nishuke wapi!"



"Shuka Bagamoyo mwisho, nitakuja kukuchukua stendi, halafu tuelekee hadi eneo ilipo gesti."

Maneno yale yalimpa faraja moyoni mama Juliana, aliona anapendwa kuliko hata mume wake anavyompenda, mwili wake ulikuwa umepatwa na mshtuko kama wa radi na Bitungu tu ndiyo alikuwa fundi wa kurekebisha mshtuko huo. Haikuchukua muda mama Juliana akawa ameshaingia kwenye daladala ya kuelekea Bagamoyo.



Wakati mama Juliana akiwa ndani ya daladala, Juliana naye alikuwa tayari ameshauona mchezo mzima pale kituoni, alikodi bodaboda ya kumpeleka hadi Bagamoyo.

"Hakikisha daladala ile pale mbele yetu haituachi hata chembe!"

Juliana alimwamuru dereva bodaboda.



Kila kituo daladala ilipokuwa ikisimama, dereva bodaboda alikuwa akisimama kwa nyuma yao kidogo. Baada ya mwendo wa zaidi ya nusu saa hatimaye wakaingia Bagamoyo.

"Tusimame hapahapa!" Juliana alimuamuru dereva.



Mahesabu ya Juliana yalikuwa sahihi, alishuhudia mama yake akishuka kwenye daladala moja kwa moja na kufuatwa na Bitungu ambapo walikumbatiana kisha wakaingia kwenye bajaji na kuchomoka.

"Tuwafuate, mpaka nitajua mwisho wake, haiwezekani nifanyiwe mchezo mchafu huku nashuhudia!"

Aliongea Juliana huku dereva bodaboda akiendelea kuwafuatilia bila kujua kama anayemfuatilia Juliana ni mama yake mzazi.



Baada ya mwendo mfupi, ile bajaji ikawa imeshasimama, mama Juliana alitoka sambamba na Bitungu na kuelekea katika gesti ya Tupendane.

"Nimerudi tena!!"



Aliongea Bitungu, akimwambia mhudumu wa mapokezi katika ile gesti huku akielekea kwenye chumba alichopangiwa na kufikia moja kwa moja kwenye kitanda.

"Mpenzi nilikwambia huku kumetulia!"

"Kweli, lakiniii..."



"Lakini nini tena!! Umeshaanza kulalamika!"

"Hapana Bitungu, itabidi tufanye haraka nirudi si unajua huku ni mbali!"

"Najua!"



Mama Juliana alivua nguo zake na kufungua kimkoba alichokuwa nacho na kutoa khanga na kuivaa, kisha akatingisha mwili wake kwa makusudi mbele ya Bitungu aliyekuwa akimtolea macho.

"Twende basi tukaoge mpenzi!"

"Mhh, unajua wewe ni mzuri asikwambie mtu! Utamu ulionao ni zaidi ya kitu chochote!"

Aliongea Bitungu huku akivua suruali yake na kuchukua taulo la gesti na kumshika Mama Juliana hadi bafuni kwenda kuogeshana.



Muda wote Juliana alikuwa yupo nje ya gesti ya Tupendane, presha kwake ilikuwa kubwa, hakujielewa ni njia gani atatumia kujua chumba walichokuwa Bitungu na mama yake mule ndani.

"Kuna vyumba!"



Aliongea Juliana akimwambia mhudumu yule wa mapokezi.

"Ndiyo, unataka single au double?"



"Kwanza shilingi ngapi? Na ingekuwa vizuri kwanza niweze kuviona na ukubwa wake!"

Aliongea Juliana huku akijijua kabisa hakuwa na uwezo wa kulipia chumba kutokana na pesa kidogo aliyokuwa amebeba. Yule mhudumu wa mapokezi alimwelekeza chumba kimoja baada ya kingine huku akikiruka kile chumba ambacho yupo Bitungu na mama yake.

"Mbona vingine hunionyeshi?"

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ukiona hivyo ujue vina watu ndani yake."

"Kwani?? Yule mama aliyeingia humu ndani na kijana mmoja hivi kama dakika kumi zilizopita kaingia chumba gani?"



Juliana alimuuliza yule mhudumu kimitego.

"Chumba hiki hapa tulichokiacha!"



Alijibiwa Juliana huku akili yote ikimuhama, akaachana na yule mhudumu na kuelekea chumba alichokuwa ameelekezwa, moja kwa moja akaufungua mlango wa kile chumba, haukuwa umefungwa hivyo akaingia moja kwa moja na kuzama ndani.

"Lakini huko si nimekwambia kuna watu!"

"Hata kama!! Nawafahamu ngoja niwasalimie kwanza!"





Aliongea Juliana huku akiwa ameshaingia ndani na kumuacha mhudumu nje akiwa mdomo wazi. Kitendo cha kuingia kwenye kile chumba alikikuta kitupu, macho ya Juliana yaligongana na nguo za mama yake sambamba na mkoba uliokuwa kitandani pale, hakujiamini mara mbilimbili kama alikuwa ni mama yake.



"Lazima watakuwa wameingia kuoga tu!"

Alijiongelea Juliana huku akipiga hatua kuelekea kwenye bafu ambalo lilikuwa ndani mulemule. Alipokaribia katika mlango wa lile bafu aligundua kuwa haukuwa umefungwa, hivyo akausukuma kidogo na kuchungulia kwa jicho moja. Alimshuhudia mama yake akiwa anamsugua mgongo Bitungu, Bitungu naye akimsugua mama Juliana huku wakifurahia kwa kupigana mabusu.



Baada ya kusuguana kwa muda wakajimwagia maji kuondoa mapovu kisha Bitungu akataka kufanya mambo mulemule bafuni...

"Mhh sasa naona mechi yetu kama tukaihamishie kule kwenye uwanja mkubwa maana nahisi huu si uwanja mzuri..."



"Kwani una nini sweet!"

"Wee huoni, vichuguu kila kona, hata mashuti unayopiga nashindwa kuyadaka vizuri!"

"Ni kweli sweet lakini ngoja kwanza nikijikwaa tu ndiyo tuh..."

"Ukijikwaa nini, sitaki kusubiri mpaka ujikwae, miye nainuka bwana!"

"Hapana Sweet subiri kwanza!"



Muda wote Juliana alikuwa akiwapiga jicho kupitia kaupenyo kadogo kwenye mlango, mzuka ulionekana kumpanda hata lile wazo la kutaka kuwafumania likakaukia kwenye ubongo wake kwa muda mfupi.

"Inamaana Bitungu ndiyo mchezo wake enhh!, kwangu miye anajifanya kunibania kwa mama anampa vyote!"



Aliendelea kujisemea Juliana huku akiwa bado kauinamia mlango.

Ndani ya muda mchache Bitungu na mama Juliana walikuwa katika mapumziko ya mechi yao, mama Juliana alikuwa hoi hajiwezi huku Bitungu akishughulika kwa kumvalisha khanga yake.

"Vaa basi jezi yako, tukapumzikie kule!"

"Baby!"



"Nambie!"

"Usinivalishe hiyo khanga kwanza!"

"Kwa nini?"

"Hivi umeniroga ama nini?"

"Kwani vipi sweet?"



"Yaani haiwezekani hata mechi ya kwenye uwanja mbovu uwe unaijulia kiasi hiki!"

"Nilishakwambia miye fundi wa mipira iliyokufa, kiwanja chochote unachokitaka tunaweza kucheza na nikatoka na ushindi tena ule wa kishindo." Aliongea Bitungu kwa kujisifu.



Maneno yale yalipata kusafiri hadi kwenye ubongo wa Juliana, akayanasa kwa hasira ya hali ya juu sambamba na macho yakimkakamaa.

"Bitungu... Bitunguuuu?"



Juliana alijikuta akitoa sauti ya ukali akilitaja jina la Bitungu kwa sauti ya juu, moyoni mwake alishakubaliana na lolote litokee. Alichokifanya kabla Bitungu na mama Juliana hawajatoka mle bafuni, alifungua kitasa cha mlango ule na kutaka kuingia ndani.

"Unafanyaje chumba hiki?"



Sauti nene na kali ya kiume ilimhoji Juliana. Juliana akageuka na kuisikia sauti ile inapotokea, kisura hakuweza kumfahamu zaidi ya kuambulia kumjua yule mhudumu wa mapokezi aliyekuwa amefuatana naye.



"Nilimwambia chumba hicho kina watu akasema anafahamiana nao," alijitetea yule mhudumu wa mapokezi akimuelezea yule kaka mbele ya Juliana.

"Dada hivi unajua utaratibu katika gesti hii?"

"Jamani si nilishawaambia kuwa nawafahamu?"



"Hata kama unawafahamu ndiyo uwachungulie tena wakiwa bafuni?"

"Haya tusubiri watoke muone kama hawanijui!" Aliongea Juliana kwa kujiamini lakini yule mkaka hakutaka kabisa kuaminiana naye, alichokifanya alimshika Juliana mkono na kumtoa katika kile chumba.

"Nimesema sitoki, hata mfanyaje mpaka wa huku bafuni wanione?"

Aliongea Juliana kwa kujiamini.



"Utatoka tu! Wee nani mpaka usitoke na kwanza hivi umelipia hata chumba humu ndani?"

"Sijalipia lakini sitoki!"

Juliana alitolewa kwa nguvu huku akiburutwa mpaka kwenye korido ya mule ndani ya gesti.



***

Wakati yote hayo yakiendelea si Bitungu wala mama Juliana aliyekuwa anajua kinachoendelea. Ndiyo kwanza mama Juliana alikubali kuendelea na kipindi cha pili baada ya kuchanganywa na mechi iliyopigwa kipindi cha kwanza japokuwa uwanja ulikuwa mbovu.

"Bitu mpenzi!"



"Niambie sweet!"

"Nasikia kuna makelele kweli nje na sauti ya dada kama analia kwa mbali?"

"Achana nao wanaweza wakawa watu wamefumaniana hao lakini kwa hapa, hapana! Sidhani kama kuna mambo hayo!"

"Nina wasiwasi Bitu!"

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Achana nao kwanza hayatuhusu tumekuja kula raha zetu hapa na siyo kufuatilia mambo ya watu."

Aliongea Bitungu huku akimvalisha mama Juliana ile khanga yake. Walikuwa tayari wameshatosheka kwa mechi kali mbili. Kitendo cha kutoka bafuni na kuelekea kitandani ile sauti iliyokuwa ikilia ndiyo kwanza ikazidi.



"Bitu, wacha nikaone anayelia mbona sauti kama ya mwanangu!"

"Mwanako? Afuate nini huku? Embu jifute tuagize chakula tupumzike kidogo urudi hayo mambo mengine waachie hukohuko hayatuhusu."

"Bitu kwangu miye nahisi kama yananihusu."







"Hayakuhusu sweet wangu embu nisikilize basi!"

"Bitu?"

"Nakusikia!"

"Kwa kuwa nakupenda! Nimeamua siendi tena!"

"Sawasawa, ndiyo maana nakupenda sweet wangu!"

Mama Juliana aliamua kutii amri mbele ya Bitungu japokuwa kelele alizokuwa akizisikia kwa mbali zilimaanisha. Alitoa mafuta yaliyokuwepo kwenye mkoba wake na kuanza kujipaka kisha akampaka na Bitungu.



"Haya mpenzi kwa sasa tupumzike."

"Lakini..."

"Lakini nini tena!"

"Hapana itabidi nirudi tu sasa hivi kwani kulala nitachelewa jamani na si unajua kuna mwanangu nimemuacha."



"Najua, wee tulale, nitatega mlio wa kutuamsha hapa kwenye simu baada ya nusu saa ndo utaondoka."

"Sawa mpenzi!"

Aliitikia mama Juliana huku akiachana na dera alilokuwa anataka kuvaa, aliendelea kuishikiza khanga yake kifuani kisha wakavutana na Bitungu hadi wakajikuta wamelala kitandani huku Bitungu akiwa juu yake na baada ya muda kidogo usingizi ukawapitia.

***

Bado Juliana alikuwa katika machungu makubwa, machungu ya kushuhudia mama yake akicheza mechi ya nguvu na Bitungu, tena mechi ya mchangani bila viatu. Bitungu aliyekuwa amemuamini lakini kumbe alikuwa akimficha siku zote.



Kwa muda huu Juliana alikuwa ameshindwa kabisa nguvu na wale wahudumu wa ile Gesti ya Tupendane. Alikuwa amejikalia zake nje ya ile gesti akitafakari huku pembeni yake akiwa na dereva bodaboda.



"Turudi tu nyumbani!" aliongea dereva bodaboda akimwambia Juliana.

"Hapana, siwezi ni bora uniache!"

"Nikuache?"

"Ndiyo niache hujaelewa nini?"

"Hasira zako hukohuko, haya nipe changu nirudi zangu?"

"Sh. Ngapi?"



"Unajifanya hujui bei tuliyokuwa tumeongea? Nipe elfu 10 zangu."

Juliana alikuwa ameshajipanga kwa kiasi hicho cha pesa. Pesa ambazo alikuwa akiwekeza nyumbani kwao kidogokidogo. Alifungua kipochi chake kidogo kilichokuwa na zaidi ya shilingi elfu 50 kisha akachomoa noti ya elfu 10 na kumpatia na kuondoka zake.



Macho, mwili viliashiria Juliana kukata tamaa ya kitu flani, hakuwa Juliana wa kawaida kutokana na kitu kilichomtokea. Alijiapiza na moyo wake asiondoke mpaka amshuhudie mama yake akitoka pale nje na Bitungu."Lazima Bitungu achague moja leo, kati yangu na mama nani anastahili kuwa naye!"

Alijikuta akijisemea mwenyewe Juliana huku akikazia macho eneo la mbele ya ile gesti kwa kila aliyekuwa akitoka ama kuingia.



Baada ya kukaa nje kwa zaidi ya nusu saa, giza lilianza kuomba njia. Juliana wala hakutetemeka kurudi kwani mtu aliyemhofia kama akichelewa kurudi alikuwa ni mama yake na siyo baba yake anayechelewaga kurudi nyumbani.



Hatimaye mama Juliana akatoka akiwa ameongozana na Bitungu. Bitungu aliyekuwa amevalia bukta na tisheti ya bluu huku mkono mmoja ukiwa kiunoni mwa mama Juliana.



Hasira kwa Juliana zilikuwa zaidi ya simba jike mwenye njaa kali. Alitamani kwenda kuwasambaratisha lakini moyo wake uligeuka na kuwa mzito kwa kuona kama mapenzi yake na Bitungu yanaweza kuelekea ukingoni. Macho yake yalibaki njia panda yakiwaangalia tu. Baada ya muda alishuhudia bajaj ikifika eneo hilo kisha mama Juliana akampiga busu Bitungu la kumuaga.

"Bitungu! Bitungu! Bitungu!"



Juliana uzalendo ulimshinda na kujikuta akilitaja jina la Bitungu kwa sauti ya juu. Ndo kwanza Bitungu akawa kama hajasikia zaidi ya kuiachia ile Bajaj ikiondoka na mama Juliana. Juliana alichokifanya ni kumsogelea Bitungu karibu.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Umefuata nini huku? Na nani kakwambia nipo eneo hili?"

"Unanigombeza au unaniambia?"

"Nakuuliza nani kakwambia nipo huku?"

"Uliniambia mwenyewe kwenye simu!"

"Kuwa?"



"Kuwa upo Bagamoyo kikazi!"

"Ndiyo nipo kikazi na hapa wafanyakazi wenzangu wengine wapo ndani!"

"Hata miye naona maana kuna mfanyakazi mwingine wa kike nimemuona umetoka naye na kumuangushia mabusu kisha akaondoka na bajaj!"

"Unasemaje Juliana?"



"Mfanyakazi mwenzenu wa kike nimemuona tena mnashikana hadi viuno?"

"Acha kunikosea mpenzi hebu kwanza twende tukakae kwanza pale tupate japo kinywaji!"

"Hapana nataka twende ndani!"

"Ndani kuna wafanyakazi wenzangu."



"Ndiyo vizuri ukawatambulishe kwangu au vibaya?" Juliana alikuwa akicheza na akili ya Bitungu kwa makusudi. Alikuwa ameshaujua mchezo mzima hadi chumba walichokuwa wakicheza mechi ya mchangani.

"Haya twende lakini..."



"Hakuna lakini Bitungu miye ndiye mpenzi wako wa pekee hao wengine si wafanyakazi wenzako?"

"Ndiyo!"

Kitendo cha Bitungu kuongozana na Juliana hadi chumbani, Juliana alimuwahi na kumsukuma hadi kitandani na kuanza kumshambulia kwa mabusu kadhaa. Wakiwa katika mahaba mazito mara simu ya Bitungu ikaita...







Kabla Bitungu hajaipokea ile simu, Juliana akawa ameiwahi na kuishika huku akitaka kubonyeza kitufe cha kupokelea.?Nooo! Nipe simu yangu mpenzi!?

?Hapana sikupi mpaka nijue anayekupigia.?



?Sasa sweet tumefikia huko! Najua tu watakuwa ni wafanyakazi wenzangu tu, nipe pliiz!?

?Hata kama!?

?Nipe basi!?



?Nimekwambia sitaki, embu kwanza.?

Juliana alikuwa wa kwanza kujua aliyekuwa akipiga simu ile ya Bitungu. Jina ambalo lilikuwa limeseviwa katika ile simu lilikuwa limemshtua vilivyo. Alichokifanya ni kuangalia tena ile namba mara mbilimbili na kugundua kuwa ni mama yake ndiye aliyekuwa akipiga, akaikata kisha akampa Bitungu.

?Shika lisimu lako!?



Harakaharaka Bitungu aliichukua na kuangalia aliyekuwa akipiga lakini kabla hajapokea ikawa tayari imeshakatika. Hasira zikamshika baada ya kugundua aliyepiga ni mama Juliana, akabaki akimtolea macho Juliana kwa hasira.

?Umeridhika sasa!?

?Kwa kipi hasa??



?Si umekata simu ya mfanyakazi mwenzangu!?

?Mfanyakazi mwenzako??

?Ndiyo! Unajua alichokuwa akitaka kuniambia??

?Ujue mpenzi sipendi kabisa nikuudhi na hata wewe uniudhi.?

?Kumbe unajua hilo! Kwa nini uniudhi??

?Nisamehe basi!?



?Haya nimekusamehe, tupumzike basi!?

?Bitu...?

?Niambie!?

?Mi sitaki kupumzika bwana! Natamani nikukumbatie muda wote tu!?

?Najua mpenzi lakini leo tulikuwa na kikao cha muda mrefu, hapa nilipo nimechoka sana mgongo kwa kuinama kuandika. Acha tupumzike kwanza na hata akili yangu haijakaa sawa...

?Hivi kweli Bitu unanipenda??

?Ndiyo kwani vipi??



?Hapana mtu unayempenda huwezi kumwambia hivi!?

?Lakini...

?Lakini nini??

Wakiwa katika maongezi huku Bitungu akiwa hana dalili ya kucheza mechi ya aina yoyote kutokana na uchovu aliokuwa ameupata baada ya kumaliza kucheza mechi ngumu ya mchangani na mama Juliana. Kila akijaribu kujiweka vizuri ndiyo kwanza alikuwa akichokozwa na Juliana.



?Ujue Bitu... nahitajika kurudi nyumbani na hii yote nimekuja kwa ajili yako kwa nini unifanyie hivi... kwa nini uutese moyo wangu jamani, nielewe mpenzi...?

?Sweet, nakuomba kesho uje nitakuwa free kabisa!?

?Basi hata mara moja nirudi nyumbani inatosha!?

?Mara moja nini??

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

?Mara moja umuagize mwanajeshi wako afanye mashambulizi.?

Bitungu aliendelea kuwa mgumu hali iliyomfanya Juliana aendelee kuumia zaidi kila akikumbuka alivyokuwa akishuhudia mechi kati ya Bitungu na mama yake.



Mechi waliyokuwa wakiichezea mchangani tena wakiwa na jezi. Baada ya kusumbuana kwa muda, Bitu aliamua kumkubalia Juliana ambapo alimuweka sawa na kuanza kufanya mashambulizi ya kupima uwezo wake wa kulicheza gwaride kabla hajavua rasmi magwanda na kuingia vitani.

***

Usiku ulizidi kuingia. Hadi inafika saa mbili za usiku si mama Juliana wala Juliana waliokuwa wamefika. Siku hiyo baba Juliana alijuta kurudi mapema kwani tangu saa kumi na mbili za jioni alikuwa nyumbani akiwasubiri. Homa aliyokuwa akiisikia ilimfanya kuachana na pombe siku hiyo na kuwahi kurudi ambapo alikuta milango yote ya nyumbani kwake ikiwa imefungwa. Hatimaye mama Juliana akatokea na kumkuta mumewe akiwa amekaa kibarazani kwa hasira.



?Umetoka wapi sasa hivi??

?Baba Juliana ndiyo salam kweli hiyo??

?Sitaki salam, kunigandisha muda wote na simu umezima ndiyo nini??

?Simu imezima??

?Ndiyo! Umeamua kunizimia simu siyo??

?Hapana sijazima simu, siyo hii hapa iko on??

?Sipendi upumbavu mama Juliana, haya nifungulie mlango.?



?Kwani umefungwa? Nilimuacha Juliana, au atakuwa ndani amepitiwa na usingizi??

?Angekuwa amelala tangu saa kumi na mbili si angenifungulia, nimegonga mpaka nimechoka. Ujue msiniletee ujinga!?



?Hapana mume wangu, miye funguo zangu za akiba zote niliziacha nikijua nimemuacha Juliana na nilimwambia kuwa asitoke narudi naelekea kwenye vikoba.?



?Leo mtaniambia vizuri mlikuwa wapi, haiwezakani mnifanyie ujinga wa namna hii kwa kunigandisha, kumbe siku zote ninazochelewaga kurudi nyumbani mnajiachia namna hii siyo??

?Hapana mume wangu!?

?Hapana nini??



Mama Juliana alijitahidi kudanganya lakini ndiyo kwanza baba Juliana alizidisha ukali. Hakutaka kusikia lolote zaidi ya kufunguliwa kwanza mlango halafu aelezwe ukweli juu ya Juliana alipo. Woga ulishaanza kumshika huku akitetemeka mwili asijue afanye nini ili mlango ufunguke, akili ya haraka aliichukua simu yake na kutaka kutoka eneo lile.



?Embu ngoja niiulizie hapa jirani kwa mama Latifa,?

?Uulizie nini wakati kote nimeshaulizia wamesema hakuna ufunguo na mtu wa mwisho kuonwa akitoka alikuwa Juliana.?



Mama Juliana aliishiwa pozi, ujanja wote wa maneno ulikuwa umeshamwishia, alishindwa kujiongeza zaidi ya kuamua liwalo na liwe. Aliichukua simu yake na kuanza kumpigia Juliana kwa papara huku akiiweka loud spika ili wote wajue eneo alipo.





Mikono yake ilionyesha wazi kutetemeka hasa maeneo ya vidoleni, muda wote baba Juliana alikuwa pembeni yake akimuangalia tu. Simu iliita mpaka ikakata yenyewe, akajaribu zaidi ya mara mbili lakini bado haikupokelewa.



?Sasa atakuwa ameenda wapi Juliana huyu??

?Hayo maswali usiniulize mimi, ninachotaka kwanza mlango ufunguliwe kisha ndo mnijibu vizuri kwa nini mnaondoka tena na funguo zote!?

?Jamani baba Juliana! Si nilishakwambia funguo zangu zipo ndani!?

?Fungua sasa!?

?Nitafunguaje??



Baba Juliana bado alikuwa na hasira kali. Alichokifanya ni kujisogeza kwenye ukuta na kutaka kukaa kwa mara nyingine, kabla hajakaa wazo likamjia. Akajiongeza!

?Naenda kumuita baba Latifa!?

?Wa nini??



?Aje aubomoe tu huu mlango!?

?Halafu ukishabomolewa??

?Tunaingia, anaurudishia!?



?Jamani baba Juliana embu kuwa mvumilivu basi hata kidogo, Juliana kama ametoka si atakuja kuliko kuanza kumuita baba Latifa aje avunje.?

?Ndo nishasema sasa!?

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baba Juliana hakutaka kusikia lolote zaidi ya kunyanyuka na kuongoza moja kwa moja mpaka kwa baba Latifa ambapo alimkuta na baada ya dakika chache alirudi naye kwake akiwa na vifaa vyote vya kubomolea mlango.



?Fanya uwezavyo, uvunje tu tuweze kuingia halafu utaurudishia!?

?Haina shida bosi!?

?Hapana baba Latifa, Hapana usiuvunje!?

?Wee mwanamke! Embu muache baba Latifa auvunje huo mlango.?

?Baba Juliana kwa nini hutaki kunisikiliza mkeo!?



?Mimi si ndo baba Juliana, baba mwenye nyumba? Haya fundi vunja nimesema na kama pesa nakulipa mimi wala si huyu mwanamke??







ITAENDELEA

Blog