Search This Blog

Monday, October 24, 2022

AAH...SHEMEJI...AACHAAA...! - 3

 





    Chombezo : Aah Shemeji ... Achaaa !

    Sehemu Ya Tatu (3)



    ***** ***** *****

    “AENDE zake huko kama haupo wenzio wala,nami ntazoea taratibu ye amewezaje mpaka mi nishindwe. Waswahili wanasema hakuna cha peke yako hususan hapa mjini.

    “Ukitaka kuhakikisha kama umeshaanza kuzoea turudie tena utagundua kuwa makelele uliyokuwa ukipiga mwanzo hayatakuwapo tena.”

    “Hee!Shida ya kunigeuza kizazi, hapa nilipo miguu haina ushirikiano.”

    “Nakutania tu dear.”

    Bw. Abdul aliingiza mkono ndani ya suruali yake aliyoivaa na kutoa kitita cha laki mbili kisha akamkabidhi Aisha.

    “Asante sana mpenzi.” Aisha alisema kwa furaha baada ya kukabidhiwa fedha.

    Walikumbatiana na kukubaliana kukutana siku nyingine.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******

    Ilikuwa ni siku ya Jumatatu tulivu majira ya saa 10 jioni. Aisha na Anita walikutanakatika bustani iliyokuwa kando ya nyumba ya kina Aisha wakibadilishana mawazo na kupashana umbea.

    “Shoga basi ngoja nkwambie.”

    “Mmmmh! Nambie shoga yangu.”

    “Shoga jana si ndo tukatoka na shemeji.”

    “Mlienda wapi tena.”

    “Kwenye ile Hoteli ya Sandiego.”

    “Mmmh! Lete uhondo shoga.”

    “Basi bwana kitu nilichokutana nacho huko ni aibu hata kuhadithia.Mechi tuliicheza karibu saa nzima, hiyo mashine sasa sijawahi ona.Hapa nilipo miguu haifanyi kazi, nikisimama nahisi kudondoka.”

    “Aisee!Pole sana best.”

    “Asante ila maumivu sikuona kitu ukilinganisha na mshiko alionidakisha.Mshiko wa maana, kitu mbili.”

    “Elfu ishirini?”

    “Mmmm! Shoga elfu ishirini ndo mshiko wa kuusifia kiasi hicho?”

    “Kitu laki mbili.Hizo elfu ishirini labda akampe mkewe.”

    “Unasema kweli?Kama ndiyo hivyo inakubidi umkamate kisawasawa.”

    Waliendelea na stori zao za umbea huku wakicheka na kufurahi. Anita alimshauri shoga yake kuwa makini ili dada yake asije akagundua. Pia alimshauri kumheshimu na kutokuonyesha dalili yoyote pindi wanapokuwa nyumbani.



    Bw. Abdul alikolea kwa penzi adimu alilolipata kwa Aisha, hivyo alitaka kuwa na uhuru zaidi ili aweze kufaidi raha za dunia. Ndipo alipoamua kumpeleka Aisha katika chuo cha utalii kilichopo eneo la Mikocheni. Wazo hilo halikuwa gumu kulifanikisha kwani Nasra alimpenda sana Aisha pia alipenda sana maendeleo yake ya kimasomo.

    Aisha alifurahi sana kusikia kuwa anataka kupelekwa katika chuo cha utalii. Ni miaka miwili sasa imepita tangu Aisha ahitimu kidato cha sita katika Shule ya sekondari Ifunda iliyopo Iringa. Aisha alishindwa kujiunga na chuo kikuu kutokana na kupata alama ndogo katika matokeo yake. Aisha hakuwa tayari kurudia mtihani . Miezi michache baada ya matokeo hayo Aisha alichukuliwa na mama mmoja kwenda kuuza duka la vipodozi, kabla ya dada yake kuja kumchukua ili wakaishi wote jijini Dar es Salaam.

    Aisha ni mtoto wa pili katika familia ya Mzee Dambala. Familia yao ilikuwa na hali duni kiuchumi ila baada ya Nasra kuolewa na Bw. Abdul maisha yao yalianza kubadilika kwani Mzee Dambala alifungua duka la vyakula. Aisha alisomeshwa pia walikuwa wakitumiwa pesa za matumizi kwa kila mwezi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ******

    Aisha aliripoti chuoni kama ilivyo kawaida katika chuo hicho kulikuwa na utaratibu wa kutembelea wanafunzi kila siku ya Jumapili. Ndugu pekee wa Aisha aliyetambuliwa na chuo ni Bw. Abdul. Nasra hakuandikishwa kama ndugu wa karibu kwani siku ambayo Aisha aliripoti kwa mara ya kwanza chuoni Nasra alikuwa akisumbuliwa na Malaria hivyo hakuweza kumsindikiza mdogo wake.

    Hivyo basi Nasra hakuweza kwenda peke yake kumtembelea Aisha hadi aende na mumewe.

    Bw. Abdul aliitumia fursa hiyo kwa kila Jumapili kwenda kumchukua Aisha na kisha kwenda kujirusha sehemu mbalimbali za starehe.

    Aisha na shemejiye hawakukosekana katika kumbi ambayo kunakuwa na bendi inayotumbuiza. Mapenzi yalishamiri hadi Bw. Abdul kufikia hatua akamsahau mkewe huku akiwa bize na Aisha . Katika siku za wiki Bw. Abdul aliipenda siku ya Jumapili ambayo hukutana na Aisha. Huwa akimuaga mkewe kuwa anakwenda kazini lakini haikuwa hivyo kwani huwa anakwenda kumchukua Aisha. Bw. Abdul hakutaka kupoteza siku hata moja bila ya kujirusha na Aisha. Hivyo hakuona sababu ya kwenda na Nasra wala kumuaga kuwa anakwenda huko.



    ******

    Nasra aliendelea na maisha yake kama kawaida huku akufikiri kuwa endapo mdogo wake akimaliza chuo na kufanya vizuri katika masomo yake basi anaweza kupata kazi mzuri kisha wote wakashirikiana kuwatunza wazazi wao.

    Asubuhi Nasra akiwa anafagia maeneo yaliyozunguka nyumba yao. Mara alitokea jirani yake aliyejulikana kwa jina la mama Sada.

    “Habari za asubuhi.”

    “Nzuri tu mama Sada habari za kwako.”

    “Nzuri tu, mbona siku hizi yule mdogo wako simwoni, yu wapi?”

    “Nani Aisha, amekwenda kusoma chuo.”

    “Chuo cha nini.”

    “Chuo cha utalii.”

    “Ndiyo muda wote huo hata likizo hakuna.”

    “Huwa wana ratiba ya kutembelewa kwa kila Jumapili lakini mimi sikujiandikisha kama ndugu wa karibu hivyo siruhusiwi kwenda mpaka niwe na mume wangu, yeye ndo amejiandikisha. Naye siku hizi yuko bize sana hadi Jumapili huwa anakwenda kazini hivyo humtumia pesa kutumia tigo pesa.”

    “Ama kweli kikulacho ki nguoni mwako, hivyo huna habari kuwa Aisha anatembea na mumeo na kila Jumapili huwa anakwenda kumchukua na kwenda kujirusha sehemu mbalimbali za jiji.”

    “Hivi we mwanamke una akili kweli, waswahili bwana wakimwona mtoto wa mtu anaendelea vizuri na masomo, wanamwonea wivu na wewe si umpeleke yule mwanao Anita.”

    “Kama mimi sina akili sawa, ila usipoziba ufa utajenga ukuta , kwa heri.”

    Mama Sada aliaga na kuelekea nyumbani kwake taratibu. Kumbe mama Sada hakuwahi hata siku moja kuwakuta Aisha na shemejiye ila taarifa hizi alizipata kutoka kwa mtoto wake wa kwanza aliyeitwa Anita, ambaye ni rafiki wa Aisha.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa kipindi chote ambacho Aisha alikuwa chuo hakwisha kuwasiliana na Anita na kumpa habari zake zote kuhusu maendeleo ya uhusiano kati yake na shemejiye. Anita alikuwa na wivu kutokana na Aisha kupelekwa chuo kwani naye alitamani kupata fursa kama ile ila hakuipata kutokana na familia yake kuwa na hali duni kiuchumi. Hivyo aliamua kusambaza habari za Aisha kwa watu mbalimbali akijua kuwa zikifika kwa dada yake Aisha basi atamchukia mdogo wake na kumrudisha kijijini lakini haikuwa hivyo.

    ******

    Baada ya mwaka mmoja kupita. Ilikuwa imebaki takriban miezi mitatu ili Aisha aweze kuhitimu masomo yake lakini haikuwa rahisi kumaliza.

    “Haloo!” Ilisikika sauti ya Aisha ikitoka kwa unyonge akimpigia simu shemejiye.

    “Haloo!Mpenzi mzima wewe?”

    “Mimi ni mzima wa afya lakini mwingi wa mawazo.”

    “Mwingi wa mawazo ?Mawazo gani tena dear mbona unanishtua?Hebu nieleze.”

    “Mimi sizioni ziku zangu, hivyo inanipa wasiwasi.”

    “Sasa wewe unafikiri ni nini?”

    “Ninajihisi kuwa ni mjamzito.”

    “Mjamzito, nani kakupa?”

    “Heee!Shemeji umeshaanza kunikana mapema yote hii?”

    “Hapana dear ila sikutegemea kutokea kitu kama hicho. Basi itabidi Jumapili nikija twende hospitali ili tupate uhakika zaidi.”

    “Sawa hakuna shida.”

    “Haya dear mchana mwema.”

    Baada ya kupata taarifa hizo Bw. Abdul hakuwa na raha tena alikuwa ni mwingi wa mawazo. Aliwaza kuwa ikiwa mkewe atabaini suala hili itakuwaje.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog