Chombezo : Nilambe Humo Humo
Sehemu Ya Tano (5)
‘’Nitashukuru kupita kiasi!” Nikasema haraka nikiwaza hata kama Lady Jay dee ataniita mwanaume kama binti na Bushoke kuniita Mume bwege shauri yao! Nitafanyaje hali nimesha ulowanya?” Nikakubali.
Lakini kabla haya hayajafanyika inakubidi uanze taratibu za uchumba na kwa hili hatuna budi kwenda kupima afya zetu kwanza ili ulete barua ya posa wakati huo huo ukianza Driving School! Sawa mpenzi?!”
Nikasikia kama nimepigwa na nyundo kichwani! Ule msururu wa wanawake niliotembea nao toka Uwanja wa fisi, Songambele, Gobbah Sotele, Msangule, Msanga na vijiji vingine hamsini kidogo utanisalimisha kweli?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘’Mbona hivyo Ibra?” Shamsa akanigundua “Au hukuvaa kondomu vizuri? Si umeniambia ulihakikisha unajilinda?’’
‘’Ni kweli! Nikajibalaguza, sura yangu ikavaa tabasamu bandia.
“Nilikuwa makini mno!’’ Nikaongezea.
‘’Sasa mbona unaogopa?’’
‘’Siogopi nina hofu kidogo tu! Unajua tena kuna Saloon, Hospital, Ajali na kadhalika. Kote huko unaweza kuambukizwa!’’
“Jiamini Ibra!” Akasema kwa karaha, “Kumbuka kutojiamini huko ndio kumekufanya ufeli na kuharibu ndoto zako!’’
‘’Kwa… kwa… kwani nilazima sana kupima? Si ningeleta tu hiyo barua ya posa na … na …!” Uoga ulinisumbua. Wale wanawake wa kule fisi afadhali, lakini kule katika ngoma, thubutu! Nilitumia kondomu mara chache sana!
‘’Ni lazima Ibra!” Shamsa akanikata kalmia na kuendelea.
“Mimi na wewe tunataka kufunga pingu za maisha zitakazofunguliwa na kifo, tunataka kutengeneza familia bora yenye afya furaha na amani, tunataka kuanza kuyaona maisha katika mwanga bora, na hii inaanza na kujua afya zetu Ibra. Ujue mimi na wewe tumekutana VETA, huko nyuma kila mtu amekuwa na majangusho yake, na katika majangusho hayo, lolote laweza kuwa limetokea. Hapana Ibra, kupima ni lazima dia!”
Sikuwa na jinsi. Kwa kila hali nilikuwa nimeshikwa. Kadiri nilivyotaka kuruka viunzi ndivyo alivyonibana kwa hoja hata nikakosa la kusema. Mwishoe nikaamua, “Acha niende nikajue moja kama kusuka au kunyoa,
Nikamkubalia, akafurahi na kunipongeza kwa kunikumbatia.
Hatukwenda kupima mara moja tu, zilipita siku za kutosha mpaka tukahitimu na kutunukiwa. Baadae alinipeleka kwao na kunitambulisha kwa wazazi wake kuwa nilikuwa Boy friend wake,
Wazee wake walikuwa na uwezo kweli, yale mandhari na ile nyumba yao mpaka sasa sijaiona mfano wake. Tena walikuwa wakarimu kweli. Tukajadiliana nao sana kuhusu maisha na mafanikio.
Siku iliyofuata ndio tukaenda Angaza
Tulikutana na akina dada wazuri wakatupa ushauri wa kutosha wa Ukimwi. Wenyewe wanaita ushauri nasaha. Tuliposema tumeelewa, tukaingia ndani na kupimwa!
Kabla ya kupewa majibu, tukapewa ushauri nasaha mwingine! Ushauri wa kina. Tuliposema tuko tayari, tukapewa majibu yetu. Ikawa kitu na box!! Naam! Nilikuwa nimeathirika wakati Shamsa alikuwa amesalimika.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘’Shamsa hakuyaamini masikio yake ingawa mimi niliyatarajia hayo, akauliza mara mbili mbili kama daktari alikuwa amekosea au lah! Jibu alilopata lilikuwa lile lile! Akavunjika moyo vibaya,
Akageuka na kuniangalia kwa majonzi, machozi yakateleza juu ya mashavu yangu. Akanisogelea na kunifuta, bado yaliendelea kunitoka. Moyo ukinidhihaki kwamba huu ulikuwa mwisho wa kila kitu baina yangu na Shamsa, mwisho wa ahadi! Mwisho wa mikakati ya kuelekea katika nchi ya maziwa na asali! Kwanini machozi yasinitoke? Kwanini?!
Shamsa akaniinua taratibu, tukatoka nje huku nikiwa sina nguvu hata moja . Naam! Malipo ya ngono ni ukimwi.
Hatua chache kabla ya kutoka nje ya jengo hilo, nikashindwa kabisa kutembea! Nikauegemea ukingo wa nguzo, Shamsa akalitambua hilo, akajua ninahitaji faraja faraja ya kweli
‘’Taratibu akajivuta maungoni mwangu na kunikumbatia kwa nguvu huku maneno ya faraja yakimtoka ‘’Huu sio mwisho wa maisha Ibra!’’ akasema mara nyingi na kuongeza “Wapo watu waliokuwa na matatizo lukuki na bado wakafaulu, usife moyo…! ’’
Kana kwamba hiyo haitoshi, akaanza kunipapasa hapa na pale huku pia akiruhusu mikono yangu itembee katika kiuno chake na nyonga kwa ujumla.
Tukaendelea kuchezeana pale kwa muda huku kucha za vidole vyake zikitambaa katika shingo yangu na kunipa faraja iliyo pitiliza, kutahamaki mikono yangu ikarukia katika matiti yake, ‘
Akaguna.
Akaacha kunichezea shingoni na kurudi kunikumbatia kwa nguvu tena. Mikono yangu ikashindwa kufanya chochote maana ilibanwa barabara katikati ya kifua changu na cha Shamsa.
Nyuso zetu zilibakiza sentmita chache sana kukutana, wakati huu tulikuwa tukibadilishana pumzi. Hata mapigo ya mioyo yetu tuliweza kuyahisi. Kila mmoja aliyahisi ya mwenzake,
Nikafunua mdomo kumuomba anipe ulimi!
Akanielewa. Akasogea taratibu, ikiwa imebaki sentmita tatu hivi midomo yetu iungane na ndimi kusalimiana, Shamsa akashituka na kurudi nyuma ,
‘’I m so sorry Ibra, Samahani mpenzi! Akanong’ona akinikumbatia kwa nguvu.
‘’Najua!’’ nikasema kwa jazba ‘’Najua kama nimeathirika lakini kidogo tu!’’
‘’Haitawezekana Ibra! Unaweza kuniambukiza, kumbuka nina watu wanaonitegemea wazazi na ndugu zangu waliojikusuru na kunilipia kozi yangu yote ili nije kuwa msaada kwao . Niamini dear kama sio hilo ningekuruhusu tu unilambe humo humo mdomoni!’’
‘’Shamsa ajue mimi ni wa kufa tu kwa sasa nahitaji faraja, tafadhali mara moja tu ukimwi hauambukizwi kwa kunyonyana ndimi!’’
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘’Sio kweli Ibra, asilimia kadhaa ya virusi hivyo huishi kwenye mate pia!’’
‘’Kwa hiyo unananinyanyapaa Shamsa?” Nikafoka nikishindwa kuidhibiti akili yangu “Wote waninyanyapae, hata wewe Shamsa? Nani basi atakayenipa upendo! Nani atakaye nijali, nani atakayenifariji nani atakaye…Oooh! Mungu wangu mbona umeniacha?!!’’ Nililia kwa uchumgu msisimko wote ulioletwa na Shamsa ukitoweka.
‘’Hapana Ibra!” Alikuwa Shamsa kwa sauti thabiti, sauti yenye mamlaka, sauti inayobembeleza, kusihi na kushawishi. Sauti tamu ajabu! Akaendelea.
“Hapana mpenzi wangu! Hapana! Amini kwamba ninakupenda kwa dhati, ninakupenda ukweli wa kukupenda, tena ninakupenda kwa moyo wangu wote.
Na ili kulinda heshima yako sitaolewa wala kuwa na mpenzi mwingine maishani ila wewe tu, potelea mbali kama hatutafanya mapenzi daima nitaishi maisha ya kitawa mpaka hapo muumba atakaponichukua! Nakuahidi hilo na ninakuapia hii ni ahadi ya dhati kabisa toka moyoni hasa!”
Nikamtazama na kutabasamu, akanifuta machozi.
Nilijua hii ni kauli tu kama kauli zingine. Kauli za wanasiasa, kauli ya faraja, kauli kutoka kwa aliyesalimika, kwenda kwa aliyeathirika. Hata siku moja sikutaka kuyaamini kwamba atayatekeleza yote aliyonihubiria! Ili tu kunilindia heshima! Heshima gani niliyo nayo kwake? kwa thamani ipi? Kwa kipi cha ajabu nilichomfanyia hata anikumbuke hivyo?
‘’Nimempa nini hata ayafanye hayo eti tu kumlindia heshima mtu ambae miaka mitatu kama sio minne ijayo atakuwa chini ya ardhi futi saba huku tani kadha wa kadha za mchanga zikiwa tele juu yake.
Nikazipokea! Kumbe ningefanya nini? Na ili kutomvunja moyo nikamwambia, “Nitafurahi sana ikiwa utatimiza hayo uyanenayo!’’ Shamsa akaniangalia tena na kutabasamu.
‘’Tabasamu zuri ajabu akaniambia.
‘’Kwa uwezo wa mola Hakika nitayatimiza!’’
Akashuka ngazi kabla hatujajipakia kwenye taxi ya Sudi na kutokomea!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO.
SEMA LOLOTE KUHUSIANA NA SIMULIZI HII LEO...USIPITE KIMYA KIMYAAA....
0 comments:
Post a Comment