Chombezo : Nilambe Humo Humo
Sehemu Ya Tatu (3)
Wengine ndugu zao wa kiume walikuwa wamewadhulumu mali za urithi walioachiwa na wazazi wao, wengine walikuwa yatima walioondokewa na wazazi wao na kukosa mtu wa kuwaangalia! Wengine walikuwa wametupwa na wazazi wao baada ya kuzaliwa wengine… wengine!
Basi ilimradi kulikuwa na mlolongo wa matatizo ambayo kwa hakika yalichusha na kuudhi.
Hofu ya ukimwi je?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walikuwa nayo lakini wangefanyaje? Waliona bora waishi kwa furaha leo kwa kuwa hata kesho wasipokufa kwa ukimwi kama watajitunza, basi watakufa kwa njaa, umasikini na adha zingine kadha wa kadha.
Ugunduzi huu ukanifanya nisiwatizame kwa jicho baya tena, bali nikawaona kama wahanga fulani hivi!
Nikajitengenezea utaratibu mzuri wa kwenda pale na kuhudumiwa mara nne kwa wiki! ulikuwa utaratibu nilioupenda na kuufuatisha kama ibada, utaratibu mtamu kweli, mtamu haswaa.
* * *
Asubuhi kulipokucha, Akimu allikuja kunigongea, nikainuka na kufungua mlango.
‘’Mambo?’’ Akanisalimu akiingia ndani.
“Poa!’’
‘’Vipi mbona hivi, leo huendi?”
‘’Wapi?” Nikamuuliza kwa wasi wasi kidogo.
‘’Mara hii umesahau kuwa juzi tulikubaliana kwamba leo tutakuwa na round discussion kuhusu Utambuzi wa Short na mitihani ya mwisho inayokuja?
“My God!’’ Nikaguta. Nilishasahau kabisa, ukweli leo sikujisikia kujadili chochote mwenyewe nilikuwa nataka masaa yaende mbio jioni niende zangu uwanja wa miutamu.
‘’Sorry Akimu!’’ Nikamwambia Akimu “Sitaweza kuja katika discussion leo nataka nifue then nipumzike kabla sijajisomea kisha nitakwenda mahala!’’
‘’Lakini tulikubaliana utakuja!’’
“Ndio hivyo tena!’’
‘’Basi itakubidi umueleze Shamsa kabisa maana binti yule asipokuona hasomi sawa sawa!’’ Nikatabasamu “Nitamwambia!’’ nikajibu.
Wakati anataka kujibu akakiona kitabu cha gwiji wa riwaya nchini marehemu Eddie Ganzel ’Kijasho chembamba’, vile anavyopenda riwaya za Ganzel akainuka na kukitwaa.
Alipokiinua tu kadi za mapenzi, zenye picha nzuri na maua ya kuvutia pamoja na barua za mapenzi zikaonekana chini yake, akaniuliza maswali machache kuhusu nilikokipata kitabu kile, halafu akauliza
‘’Hivi haya maua na hizi kadi bado tu hujazipeleka kwa Shamsa?’’
“Bado!’’
Akimu akanitumbulia macho kwa mshangao!
Alikuwa na haki ya kushangaa, alikuwa nayo. Mosi ni
yeye aliyekuwa mwandani wangu, alifahamu vingi na mengi kunihusu, pili alikuwa shuhuda wa macho wa namna nilivyoathirika kwa kumpenda binti yule.
Na ni yeye aliyetoa ushauri wa kumpelekea zana hizo na kama vile haitoshi alikuwa amenisindikiza kuzinunua, kubuni maneno mazuri yaletayo faraja na kuyaandika juu ya kadi hizo, tena alikuwa amenitaka kumpelekea haraka iwezekanavyo ili kama kuna lolote tulijadili kwa pamoja.
Na sasa ulikuwa umepita mwezi na kidogo toka tulipoziandaa
“Kwanini hujazipeleka? Ibra usiniambie ulikosa ujasiri, maana nilikwambia wewe ukishindwa kumkabidhi nipe mimi nitamkabidhi!’’ Akatua kwa kila hali alikuwa na hasira, mimi nikatabasamu na kumjibu.
‘’Nimeona haina haja Akimu!’’
‘’Eti?!’’
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘’Enh! Hanisumbui tena nimesha muweka chini ya himaya yangu!’’ ikawa zamu yake kunitazama kwa mshangao, nusu akitabasamu nusu akitaka kushangilia.
‘’ Ina maana umeisha… umeisha….! Mungu wangu, mbona siamini!’’
‘’Sijafanya nae mapenzi wala hajanikubali niwe mpenzi wake! Ila nimemdhibiti, hanisumbui tena! Maelezo yangu yakazidi kumchanganya Akimu. Akanisaili tena.
‘’Unamaana gani Ibra?’’
‘’Nina maana kuwa kuna mahala ninapoupoza moyo wangu kwa maji baridi, maji ya ya mapenzi, maji ya uzima!’’
“Inamaana umepata mpenzi mpya unayempenda kuliko Shamsa?”
“Sijasema simpendi Shamsa!’’ Nikasema kwa karaha “Nikingali nampenda na nitaendelea kumpenda maisha yangu yote!”
‘’Basi nyoosha Kiswahili Ibra, hata hao wahenga misemo na mithali zao zilieleweka kwa urahisi!’’
“Nitakwambia!” Nikamwambia huku tabasamu likiwa limeupamba mdomo wangu “Nitakwambia rafiki yangu, tena nitakwambia ukweli mtupu naomba tu uniwie radhi kwa kukuficha!”
Nikakaa vizuri na kumueleza ugunduzi wangu wa kule Fisi. Nilimueleza kwa tuo pasipo kuacha hata tukio moja. Nilipo maliza Akimu alikuwa ameshika kichwa kama aliyepoteza kitu cha thamani sana!
‘’Ni kweli unielezayo Ibra?” Sasa machozi yalikuwa yakimlenga
‘’Ni kweli kabisa!’’
‘’Umepotea rafiki yangu, tena umepotea vibaya sana. Sio watu wale ni balaa!’’
‘’Tatizo lao liko wapi Akimu? Kama nilivyo kwambia nimewastadi vya kutosha kabla ya kuamua kuwa nao chanda na pete.
‘’Hawako salama wale! Kila mwaka wanakufa! Na wanakufa na idadi kubwa sana ya watu! Hii ni kwa vile wanafanya mapenzi na watu wengi sana, wengine hutembea mpaka na wanaume elfu sita na mia sita kwa mwaka hadi elfu saba na mia mbili.
Ni washenzi wa tabia wasio na utu walioamua pesa iwe yao kwa kila hali, ukiwa na pesa unaweza kumwambia akuuzie hata utumbo wake na akakuuzia! Zaidi na zaidi ni wabaya wazee na wasiovutia kwa chochote! Ndio maana nasema umepotea!”
Akiwa na jazba Akimu alitumia zaidi ya robo saa kuwaponda makwini wa fisi. Alipomaliza ndipo nami nilipoanza kum’bishia. Tulibishana sana na mwisho wa siku ikawa imeamuliwa mimi na yeye twende uwanja wa fisi wote akajionee, nae akasisitiza mimi nikajionee, tukaondoka mchana huo huo!
Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia uwanja wa fisi mchana. Eh! zaidi ya maajabu yalikuwa yakinisubiri
Wanawake karibuni wote waliokuwa wakiuza miili yao walikuwa watu wazima hasa, wazima kweli, umri umekwenda mno. Sura zao zilikuwa tisho jingine. Mbali ya kuwa zimekomaa kwa namna ya kuchusha, huo mkorogo waliojimwagia sikuwahi hata kuufikiria. Mkorogo hadi mapajani! Mkorogo hadi miguuni, hadi katika matiti!
‘’Niliwezaje kufanya mapenzi na watu hawa?” nikajiuliza nikitikisa kichwa kwa masikitiko. Nikajuta. Akimu akanikokota tukarudi chuoni nikiwa nimenyongea.
‘’Kwanini uliamua kuja huku Ibra?” Akanisaili kwa upole baadae.
‘’Msongo rafiki yangu! Mhemko! Nilihemkwa na kutamani ngono kupita kitu chochote! Nikaona huku ndio pa’ kuponea! Laiti ningelijua…,” Nikalia kimya kimya. Akimu akinifariji.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa shinikizo lake niliweza kushiriki katika Round discussion ingawa nilipooza Kama ugali uliokosa moto wa kuuivisha sawa sawa. Shamsa alikuwepo na alifurahi kuniona, nikamtaka radhi kuwa sikuwa nikijisikia vizuri.
Mpaka tunamaliza majadiliano yetu sikuwa nimechangia lolote!
* * *
‘’Kanini umenileta huku Akimu? Nikamuuliza tukitembea kutoka sokoni, tulikuwa Songambele, kijiji kimoja kilichoko mkoani pwani ndani kabisa wenyewe walikuwa wamekibatiza jina la Gobba , ingawa jina lake la asili lilikuwa Songambele Sotele.
Kilikuwa kijiji ambacho Akimu alisomea elimu yake ya sekondari kabla hajafaulu vizuri, akakataa kuendelea na masomo ya juu na kuja kusomea umeme pale VETA. Hili lilijiri kwa kuwa Baba yake alikuwa fundi umeme aliyefanikiwa sana kimaisha kupitia kazi hiyo.
“Nimegundua rafiki yangu u’mhanga wa starehe! Starehe ya mapenzi. Huku utaburudika utastahali na kuneemeka vya kutosha. Na uzuri wanawake wa huku hawatokitoki hovyo nje ya vijiji vyao kwahiyo ni salama kwa kiasi kikubwa!”
Akanijibu. Angejua nilivyojiapiza kutofanya tena mapenzi tangu ulipojiri ule ugunduzi wa yaliyopo Uwanja wa fisi, wala asingejisumbua! Moyoni mwangu alibakia Shamsa pekee na vile tulibakiza miezi sita tuhitimu, nilijua nitamtamkia wakati huo na kitakachofuatia ni ndoa mara moja.
Nikiendelea kutembea, niliendelea kukiperuzi kijiji hiki cha Gobbah kuona kama kingeweza kunifariji. Hakikuwa na chochote cha kujivunia! Mifugo michache yenye siha na afya ya wastani, wakazi ambao mwonekano wao uliashiria umasikini uliotukuka na ardhi kubwa yenye rutuba ambayo haikuwa imelimwa, vilikuwa baadhi ya vitu vilivyoipamba Songambele Sotele a.k.a Gobbah.
Jioni tulikuwa baharini, tuliogelea na kufurahi pamoja na wenyeji wa eneo hilo ambao walikuwa na ukarimu unaovutia. Halafu tukaelekea mpirani. Usiku tulikuwa kwenye vijiwe vya kahawa ambapo tulipiga soga mpaka usiku ulipokomaa, tukaenda kulala.
Siku mbili zilizofuatia tuliishi katika mtindo huu.
Wakati nimeanza kuchoshwa na maisha haya katika siku ya tatu na nikiwa tayari kumwambia Akimu turudi Dar es salaam; ndipo lilipotokea lile ambalo ni miongoni mwa mambo matatu muhimu yalinifanya nishike peni na karatasi na kuandika mkasa wangu huu ambao Uncle Wamaywa ameamua kuuita chombezo.
‘’Jiandae Ibra,’’ Akimu Aliniambia kwa bashasha. ‘’Leo kuna ngoma! Watoto aina kwa aina wanakusanyika toka kata nzima. Hii hakuna kulala ni kutimbwirika hadi majogoo!”
Nikamtazama nisimuelewe! Ngoma ni miongoni mwa vitu ambavyo sikuwa na hobi navyo, Nikamuuliza taratibu hali nikiwa nimemkazia macho. ‘’Najua unajua kwamba mimi sipendi ngoma!”
‘’Najua sana, lakini hii tunaita ngoma kimazoea! Jina lake hasa ni mnanda!”
“Mnanda?!”
‘’Ndiyo!”
‘’Mnanda ni nini na Ngoma ni nini?!”
‘’Yanini tuandikie mate il-hali wino upo? mnanda unaanza saa kumi na mbili jioni na sasa ni saa kumi jioni subiria masaa mawili tu utapata majibu timilifu, majibu ya vitendo! Jiandae tu!”
Maswali yalikuwa mengi kichwani, lakini kila nilipomuuliza Akimu jibu lake lilikuwa moja tu. ‘’Jiandae, jiandae!’’
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikajiandaa.
Kweli, jioni tukakusanyika mnandani watu aina na aina wakijisogeza na kumsherehekea binti huyu anayeolewa. Wasichana na niseme wanawake walikuwa wamejikwatua vilivyo na walikuwa wakijituma hasa pale dimbani.
Nikashangaa kwa kuwa sikuwa nimewaona kabla. Akimu akinijulisha kuwa nisingeweza kuwaona kwa kuwa ule ni mkusanyiko wa watu kutoka kata nzima na pengine tarafa.
‘’Mambo zaidi utayaona usiku!’’ akahitimisha wakati nikianza kusisimkwa! Ule uchezaji wao ulivutia kwa hakika, ulikuwa uchezaji ambao ungekulazimisha kuangalia huku mwili ukipatwa na joto ghafla.
Wachezaji walio wengi walikuwa akina mama ambao walikuwa na kanga mbili tu, moja kifuani na nyingine kiunoni. Ile ya kiunoni ilikunjwa kiustadi ikaweza kufunika matiti na tumbo kwa kiasi kidogo.
Ile ya kiunoni ilifungwa kinamna kiasi cha kuweza kuonyesha shanga za kutosha zilizosheheni pale kiunoni. Wachezaji walijenga duara kwa mirindimo yao na katikati ya duara hilo kulikuwa na meza iliyojengwa mfano wa jukwaa na kuwekwa nguzo katikati yake.
Kadiri ngoma ilivyokuwa ikinoga, ndivyo mwanamke mmoja alivyochepuka kutoka katika mduara na kuiparamia ile stage ya meza, akainama na kuishikilia ile nguzo kama nyenzo ya kumfanya asianguke!
Hapa tena atayabinua makalio yake ambayo hayakuwa na kitu ndani zaidi ya ile khanga iliyofungwa chini kidogo ya shanga. Halafu angeanza kuzungusha kiuno katika namna ambayo usingetamani aache.
Mwingine midadi ilipomzidia kabla mwenzie hajashuka basi angeinama tu na kumwaga vitu, atamwaga vitu kweli kweli. Mara mbili ngoma ilizimwa, mpiga ngoma akasikilizwa.
Ni katika wakati huu nilipogundua kuwa Akimu hayupo! Unadhani nilimtafuta? Thubutu, ule uchezaji ulishanikamata na kunifanya mateka kabisaa! Akimu nitamtafuta baadae! Nilijiambia nikiendelea kuufuatilia muziki ule wa asili.
Naam huu ulikuwa mduara orijino wa Segere au ‘mnanda’ kama ilivyozoeleka. Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho walikuwa wakizunguka kwa pozi huku wakizungusha viuno vyao taratibu kwa ustadi mkubwa.
Mirindimo ya ngoma sambamba na kiuno cha mwanamama mmoja kilichokuwa kikizunguka vitamu vikayafanya macho yangu yamuandame! Yakamwandama kila alipokwenda.
Halafu ngoma ikazimwa.
Yule mwanamama ambae wakati huo alikuwa ameshagundua kuwa nilikuwa nikimtazama akanitupia jicho na kuachia tabasamu. Ngoma ikapigwa upya na kurindima kwa robo saa hivi. Ilipozimwa tena na moto ulio kuwa ukitoa mwanga pekee hapo uwanjani nao ukazimwa!
Kabla mshangao wangu haujaisha, nikajikuta ninashikwa mkono na kuvutwa kuelekea migombani. Nikaweka mgomo kiasi, lakini nilipogundua kuwa kwamba jimama lililokuwa likizungusha kiuno vitamu ndilo lililokuwa likinivuta, nikatabasamu na kulifuata mithili ya mwanakondoo.
Kisha macho yangu yakazoea giza.
Huko Migombani nikashangaa kukuta seti mbilimbili za watu wakiwa wameng’ang’aniana huku wakitoa milio ya ajabu ajabu! Nilipo watazama vizuri, nikataharuki! Walikuwa wakifanya mapenzi!
Nikatolewa ndani ya taharuki na jimama lililokuwa likinivuta ambalo nalo lilikuwa tayari likinishinikiza tufanye mapenzi! Vile nilivyokuwa na ukata wa mwanamke, vile ambavyo jimama yule alikuwa amenihamasisha vya kutosha sikujivunga mwanaume! Nikampa kitu na box!
Tukaneng’eneka kisawa sawa.
‘’Ngoma ilipoanza kupigwa tena ishara ya kuwaita watu warejee ngomani, mimi na yule jimama hatukurudi. Tulikuwa tumeianza ngwe ya pili. Ngwe ambayo ilikuwa na urefu usiochusha wala kuudhi, urefu mtamu.
Ufundi wote aliouonyesha katika ngoma sasa aliuonyesha mbele yangu juu ya nyonga yangu. Nilifaidi hasa, nilifaidi mno! Nilifaidi ukweli wa kufaidi. Mpaka tunafika tamati na kumwaga mizigo yetu ya kuni pale, kila mmoja wetu alikuwa ameridhika.
‘’Ahsante anti!’’ Nikamshukuru
‘’Asante nawe! U’ngangari na unayaweza kwa hakika!’’ akajibu yule jimama.
‘’Sikushindi wewe!’’
‘’Ahsante’’
Ukimya mfupi ukapita
‘’Unaitwa nani?”
‘’Havijawa! Havijawa Mawimbe! Na wewe?’’
‘’Ibra! Ibrahim Semkee Kinara! Ni mgeni hapa nimetokea Dar es salaam!”
‘’Najua kama umetokea Dar!’’
‘’Eeh?”
‘’Ndiyo!’’
“Umejuaje?’’
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
‘’Pale ulipofikia yupo anti Hidaya, Hidaya ametujuza kila kitu kuwahusu, kuwa mmekuja huku kuburudisha mioyo akili na mawazo! Na manta hofu Ibrahim, hapa hamtaburudisha mioyo tu, bali na miili pia!‘’ Akanambia, nikabaki hoi.
Nikamuuliza maswali kadhaa kuhusu mnanda, akanieleza mengi ambayo sikuyajua, mengi mno!. Nilipoagana nae tukawa tumeachiana namba za simu.
Kesho yake tulipoonana na Akimu nyumbani kila mtu alikuwa na kitu cha kumuhadithia mwenzake. Nae yalimkuta kama yangu! Tulikaa Gobbah kwa siku kadhaa halafu tukarejea Dar.
Ambacho Akimu hakukijua ni kuwa mie niliendelea kuwasiliana na Havijawa na nikawa mgeni wa Gobah kila baada ya siku kadhaa. Minanda nikaizoea, nikawa mzaramo hasa.
Vile Havijawa alikuwa akijuana na wale wapiga ngoma ambao walikuwa wakimpa ratiba ya kazi. Wiki hii tutapiga kijiji X, mwezi ujao tutamtoa na kumfunda mwali kijiji Y!
Ngoma zote nikawa nahudhuria! Mara nyingi nikiwa na Havijawa.
* * *
‘’Leo jioni kuna ngoma!” Sauti nyembamba niliyoifahamu fika ikapenya masikioni mwangu. Nikasisimkwa furaha ikinitawala nusu nusu.
‘’Unasema?’’ Nikauliza tena.
‘’Nasema hivi…,” akarudia kwa msisitizo tunaoweza kuuita wa herufi kubwa “Leo kuna ngoma, nyumbani kwetu!’’
‘’Eti?!’’
‘’We bwana ni kiziwi au kitu gani? Leo kuna ngoma bwana! ‘mnanda!’ nyumbani kwetu!’’
‘’Kwa hiyo nije?’’
‘’Unauliza majibu? Njoo!’’
Nikaenda. Niliyoyakuta yalinitoa jasho! Havijawa alikuwa amenipokea vizuri japokuwa hakutaka kuwa karibu na mimi, kila niliposema nimsogelee aliongea na mimi kwa mkato mkato tu kabla ya kunitaka radhi na kutoweka!
Una nini leo? Nilikuwa nimekumbuka kumuuliza hivi kwenye sms kupitia simu ya mkononi mara kadhaa, pasipo kupata majibu. Ngoma ilipozimwa kwa mara ya kwanza na watu kwenda kupoza makoo mie nilibakia mpweke nikitandikwa na baridi.
Ilipozimwa mara ya pili hali kadhalika.
Mara ya tatu nikiwa nimeanza kupandwa na ghadhabu ndipo yule mpiga ngoma mmoja ambae nilikuwa nimekaa karibu naye na ambae alianza kuwa rafiki yangu aliponiambia kitu kilichoniogopesha kama sio kunitisha. Hii ilikuwa baada ya yeye kuniuliza, nami kumtajia Havijawa.
“Kaka bora utafute mwanamke haraka sana!’’
‘’Mmh hilo nalijua, ndio maana namsubiria Havijawa’’
‘’Huyo hakufai kwa sasa hivi huyo ni moto!’’
Nikashtuka na kumuuliza kwa pupa ‘’Una maana gani?!”
‘’Havijawa ni mke wa mtu!’’
‘’Eti?” Nikasikia nanga zinapaa.
‘’Enhe na mwenyewe keshajua kuwa kuna doezi linalomuibia mali zake ambalo ni lilevi la ngoma ingawa sio lizaramo! Kwa taarifa yako Ngoma hii ni mtego! Mnasubiriwa wewe na Havijawa tu mwende mkaneng’eneke mkamatwe wewe ugeuzwe asusa, baadae mshikaki ili liwe fundisho kwa wengine, ndio maana nakwambia tafuta mwanamke mwingine!’’
Yakaniingia! Nikaweza kuunganisha moja na moja na kupata mbili, baadae kama mpelelezi niliyefundwa vyema, nikafanya mbili na mbili na kupata nne. Havijawa alijua huu ni mtego na hakutaka kunitosa ndio maana akawa mbali.
Akashindwa hata kujibu meseji zangu. Sikujua yuko wapi kwa sasa na sikujua yuko katika hali gani. May be yuko katika kibano kilichopatiliza, na kama hivyo ndivyo basi hata simu yangu kuendelea kuwa hewani ni kosa, nikaizima.
Nikamdodosa rafiki yangu mila na taratibu za pale nae akanifahamisha kuwa adhabu ya ugoni ni kifo. Nikazidi kuogopa ngoma ikiendelea yule bwana akazidi kuwa rafiki yangu.
Ilipozimwa kwa mara ya nne na ya mwisho, Havijawa akatokea! Hakuwa na furaha na bashasha kama ilivyo ada yake. Sura yake ilisawijika na kupoteza nuru, yaelekea alikuwa akilia kwa muda mefu.
Nikijua mtego ndio unakaribia kufyatuka, sikumgusa!
Badala yake nilikwapua mwanamke mwingine nikatokomea nae migombani na kwenda kuneng’eneka nae, Nikamuacha Havijawa pale pale uwanjani. Mwanamke niliyemchukua hakuwa haba, alikuwa bora kwa kila hali.
Nikamuuliza kama ameolewa akasema bado, nikamuomba niwe mgeni wake kwa siku hiyo akakubali. Sikurudi uwanjani nikaenda kulala kwa mwanamke huyu mpya.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**Ni mambo juu ya mambo katika NILAMBE HUMOHUMO……..nini kitajiri…….HAVIJAWA!!!!!!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment