Search This Blog

Monday, October 24, 2022

MH! MISSED CALL YA SHEMEJI - 5

 





    Chombezo : Mh! Missed Call Ya Shemeji

    Sehemu Ya Tano (5)



    Ummy aliiweka simu aliyotoka nayo ndani kwenye mapaja, akaipokea aliyoletewa na Salma ambayo ilikuwa ikipigwa na Aisha wakiwa wote pale.Ummy alihisi kuumbuka kwani simu aliyoletewa ndiyo aliyokuwa akichati na Aisha.



    Alijifanya anaipokea,  lakini akaikata huku akiendelea kuongea…

    “Haloo, niambie mama Eliza, hajambo Eliza? Sisi tupo bwana, tunaendelea na kazi tu, sijui wewe. Haya…sawa nimekuelewa mama Eliza.”



    Alipomaliza alimwangalia Aisha na kumuuliza…

    “Vipi, umempata?”

    “Mh! Mtu mwenyewe amekata simu bwana,” alisema Aisha huku akimwangalia Ummy kwa macho yenye kuomba msaada.



    “Atakuwa amekuona hapo nje akaingia mitini, si ajabu alitaka kutumia jina la benki yetu kufanya utapeli kwamba anafanyia hapa, sisi hatuna mfanyakazi huyo,” alisema Ummy.

    Baada ya kuongea hayo, ulipita ukimya mkubwa, hakuna aliyekuwa akiongea na mwenzake, si Aisha si Ummy. Walipomaliza vinywaji, Aisha aliaga kuondoka ambapo muda mrefu Ummy alitamani aondoke ili ajue moja.



    “Basi sawa, mimi naondoka Ummy.”

    “Sawa, lini upo nyumbani nije kukutembelea?”

    “Mmmh! Wikienda huwa sitokagi, karibu sana.”

    “Oke, basi nitakupigia kwanza kabla sijaja.”

    “Sawa.”



    Ummy akiwa anarudi ofisini alimpigia simu Beka…

    “Baby…”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yes baby,” aliitika Beka akiwa hajui hili wala lile…

    “Unajua mkeo leo alikuja ofisini kwangu…”

    “Mke wangu alikuja ofisini kwako?”

    “Ndiyo baby.”



    “Kufanya nini na umemjuaje kuwa ni yeye?”

    “Mh! We acha tu! Ni stori ndefu sana.”

    Ummy alimsimulia kila kitu Beka. Beka naye akaanza kuumiza kichwa kwamba, mkewe aliipata wapi namba ya simu ya Faidha. Pia Beka mwenyewe alikuwa hajui kama Faidha ana jina jingine la Ummy.

    “Mh! Labda alichukuwa namba yako kwenye simu yangu asubuhi.”

    “Labda, mimi nilishindwa kumuuliza namba yangu aliipata wapi!”



    * * *

    Aisha naye aliendelea kuumiza kichwa kuhusu huyo Faidha, kwamba ni kweli alikuwa akimtapeli kufanya kazi pale benki au yupo lakini kafichwa?

    Alipofika nyumbani jioni alikaa sebuleni, akachukuwa laptop yake na kuingia kwenye Facebook, akaandika jina Faidha.



    “Mh!” aliguna Aisha kwani picha iliyojitokeza hapo ni ya Ummy…

    “Mungu wangu, naona kweli au nipo usingizini naota?  Faidha ni Ummy?” alisema Aisha.

    Akaendelea kupekuwa Facebook hiyo ambapo pia Faidha alijiandika kwamba hana mume jambo ambalo Aisha alilikubali maana alimwambia anatoka na mume wa mtu, aliandika pia anafanya kazi kwenye benki hiyo.



    “Ni yeye,” alisema akikiri moyoni mwenyewe. Aliendelea kuangalia mambo mbalimbali kwenye Facebook hiyo ambapo alikutana na mambo yaliyompa ushahidi wa moja kwa moja kwamba, kweli yule ni Faidha ana uhusiano na mume wake, mfano alikutana na posti ya Ummy ikiwa imeandikwa hivi:

    “Kama unajitambua kuwa ni mke, mpe haki yake mumeo na mheshimu sana ukimtii kwa kila jambo, ukilegea hapo unaweza kunyang’anywa ukabaki na kilio kama akina f’lani.”

    Pia alikutana na posti nyingine ikiwa na maneno haya…



    “Ni aibu kweli, mke anamkatalia mumewe tendo la ndoa, akitoka nje mume watampapatikia, we ulie tu.”



    “Huyu ni yeye, haya maneno pia yamenilenga mimi, lazima,” alisema moyoni Aisha akiumia. Aliangalia juu kwa muda akifikiri cha kufanya, akapata wazo la kumpigia simu Ummy kumweleza uovu wake…

    “Haloo Ummy,” aliita Aisha baada ya Ummy kupokea…

    “Niambie Aisha, upo nyumbani?”



    “Nipo, Ummy namshukuru sana Mungu nimemjua Faidha ni nani!”

    “Ni nani?” Ummy aliuliza kwa haraka sana.

    “Si wewe.”

    “Mimi?”

    “Ni wewe ndiyo.”

    “Kivipi?”



    “Nipo Facebook hapa, naona picha yako, tena umeweka wazi unakofanyia kazi ndiyo hapo nilipokuja ukasema humjui, loo! Ummy, yaani unanichukulia mume hivihivi naona?”

    “Khaa! Aisha, mbona sikuelewi?”

    “Umeshanielewa, acha hizo bwana.”



    Ummy alichoona mbele yake ni kukata simu haraka sana kisha akaizima kabisa huku akisonya chini kwa chini lakini moyoni alisema...

    “Du! Nimeumbuka. Kweli picha ya kwenye Facebook imeniumbua, hilo halina ubishi hata kidogo. Sasa?” alikosa majibu.



    Kwa upande wake, Aisha baada ya kukatiwa simu na Ummy au Faidha, alimwandikia meseji…

    “Kata simu, kataa niliyosema lakini ukweli ni kwamba wewe Faidha unatembea na mume wangu, Beka.”

    Akaituma akisubiri idelive wakati wowote.



    * * *

    Faidha alichukuwa simu nyingine na kumpigia simu Beka…

    “Dear mambo yamemwagika huku…”

    “Yamemwagikaje?”

    “Mkeo si nilikwambia mpaka pale tulipoachana?”

    “Ndiyo. Imekuaje?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kanipigia sasa hivi, kasema amejua Feidha ni mimi, akanilaumu kwa nini namchukulia mume wake, wewe Beka. Da! Nimeumia sana darling ila nimejikaza tu. Yaani, nilipoona anazidi kuchanganya shutuma zake kwangu nikamkatia simu na kuizima kabisa.”



    “Daa! Kweli kimenuka, sasa?” alihoji Beka kwa sauti ya kukatakata.

    “Hata sijui mimi. Unajua alipokuja na kunitambua ni Ummy wakati anaondoka nikampa namba za simu ile nyingine maana aliniomba lakini mimi sikuchukua ya kwanza, alipopiga sikumjua ila sauti nikajua maana si nilitoka kuzungumza naye.”

    “Kwani we uko wapi?”

    “Nyumbani, njoo.”



    “Mh! Kwani hukumwambia unaishi naye jirani?”

    “Hilo sikumwambia na kama Mungu vile, unajua kabla mambo hayajaharibika tulikubaliana niende kwake wikiendi hii kumtembelea.”

    “Daa! Hapa Feidha nimechangayikiwa sana, yaani hata sijui nini kifanyike ili kumaliza hili soo.”

    “Baby, mbona sikuelewi?”

    “Kivipi?”



    “Kwani si tulisema tutaishi pamoja, sasa unaogopa nini mke kujua? Mimi nimeogopa kwa sababu kumbe tunajuana.”

    “Hebu niache kwanza dear, nitakwambia kitu baadaye lakini.



    ***

    Beka alifika nyumbani kwake gizagiza linaingia, akafikia sebuleni ambapo alikutana na laptop kwenye kochi, mkewe akiwa jikoni.Aliisogelea laptop hiyo baada ya kuona picha ya mwanamke juu akiwa katika mapozi. Alipoifikia, ilikuwa picha ya Feidha akiwa amepozi kwenye makochi sebuleni, nyumbani kwake.

    “Mh! Hatari,” alisema Beka moyo ukamlipuka lip!



    Aisha alitoka jikoni baada ya kusikia mlango unafunguliwa, alipomwona ni mume wake akarudi jikoni huku akimuuliza habari za kazi…

    “Poa tu,” Beka aliitika kwa mkato na kuzama chumbani. Moyoni alinuia kufanya jambo la tofauti.

    Baada ya kumaliza kupika, Aisha alimwita Beka kula lakini akakataa kwa kigezo kwamba ameshiba.

    “Mh! Umekula wapi?”

    “Hotelini.”



    “Umeanza lini?”

    “Siku yoyote ikitokea.”

    “Mh! Haya,” alisema Aisha na kutoka chumbani kwenda kula. Chakula hakikupanda kivile! Aliacha!



    Alikaa sebuleni akiangalia tivii, mwisho alihisi anapata tabu tu, akaenda chumbani kwa mumewe…

    “Beka,” aliita Aisha.

    “Nini?” Beka aliitika.

    “He! Ndiyo kuitika gani huko?”

    “Unataka kuongea na mimi au?” Alihoji Beka.

    “Ndiyo.”



    “Ongea basi.”

    “Nataka kuuliza.”

    “Uliza.”

    “Feidha au Ummy ndiyo nani?”

    “Ni mwanamke wangu nilipanga kumuoa awe mke wa pili maana dini inaniruhusu.”

    “Unasemaje Beka?”



    “Ina maana hujanisikia au?”

    “Kwa hiyo unataka kuoa mke wa pili?”

    “Ndiyo maana yake.”

    “Kisa nini?”



    “Kisa cha kufanya nini?”

    “Wewe kuoa mke wa pili?”

    “Si unakijua.”

    “Sikijui.”



    “Nataka mke ambaye hawezi kuamua kuninyima unyumba akiwa anajua mimi ni mume wake. Ndiyo kisa!”

    Aisha aliishiwa nguvu kwani ukweli uliobaki ndani ya moyo wake aliujua kwamba, ni kweli amekuwa akimnyima unyumba mume wake na hata katika kikao cha wazazi wake walionesha kukerwa sana na hilo.

    “Mimi nadhani badala ya kuoa mke wa pili, niandikie talaka yangu umuoe yeye awe mke wako mmoja ndani ya nyumba,” Aisha alitingisha kiberiti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Oke, kama limetoka moyoni mwako nafurahi sana, unaitaka saa hivi?”

    “Nini?”

    “Hiyo talaka.”

    “Hapa haachwi mtu nakwambia Beka.”

    “Kwani aliyesema anaacha mtu nani, si umetaka mwenyewe?”

    Aisha alitoka, akaenda kukaa sebuleni. Alianza kumtumia meseji za vitisho Feidha…

    “Kama lengo lako ni kuniondoa kwenye ndoa yangu, huwezi na utaondoka wewe.”

    Meseji ilideliva kwa Feidha, akajibiwa…



    “Mimi nadhani ungetengeneza kwako kwanza ndiyo unigeukie mimi. Mwenyewe nimeumia sana kuona nimetembea na mume wa rafiki yangu, ndiyo maana ulipokuja kazini nilikuyeyusha maana pale si sehemu salama kuzungumzia masuala binafsi, lakini sasa niko tayari.”

    “Umeanza lini na mume wangu?” aliuliza Aisha.

    “Hilo swali hata ukimuuliza yeye atakujibu, si amesharudi uko naye!”

    “Kwa hiyo unanijibu utumbo siyo Ummy?”



    “Umetaka mwenyewe Aisha. Ungekuwa mpole ukapewa ushirikiano, lakini meseji yako moja umenitumia kali sana. “Mume wako nampenda sana na siwezi kumwacha kwa sababu wewe ni mburula tu.”



    Aisha alihisi mwili kuishiwa nguvu, kila mahali alipahisi hajiwezi, akainama kuangalia chini kwa mawazo…

    “Hivi huyu mwanamke nimfanye nini lakini? Yaani Ummy huyuhuyu ninayemjua mimi anaweza kunipora bwana na kunitamkia kwa kujiamini?



    “Eti umeyataka mwenyewe Aisha. Ungekuwa mpole ukapewa ushirikiano, lakini meseji yako moja umenitumia kali sana. Mume wako nampenda sana na siwezi kumwacha kwa sababu wewe ni mburula…

    “Hivi ana akili kweli, niwe mpole kwa mume wangu? Haitawezekana na haitatokea kwanza.”

    * * *

    Kule kijijini dada wa Aisha alishaanza kuchakaa kwa maisha ya kijijini, siku moja alimpigia simu Beka na kumwomba shilingi elfu kumi tu apate kununua hata mafuta ya kujipaka mwilini maana alikuwa amepauka sana.



    Beka kwa ubinadamu maana alijieleza sana, alimtumia shilingi elfu hamsini huku akimwambia amemmisi sana…“Hata mimi nimekumisi sana baby wangu, daa! Lakini vipi nyumbani kwako, ni amani tu au?”

    “Hakuna cha amani, mdogo wako eti sana ndiyo ameyajua makosa yake, siku zote hakuwa anajua.”

    “Mvumilie tu. Sasa mimi nakuja lini huko baby?”



    “Nitakwambia, lakini je, wazazi watakuruhusu kuja Dar?”

    “Sitasema nakuja Dar.”

    “Utasema unakwenda wapi?”



    “Moshi kwa rafiki yangu anaitwa Bitte.”

    “Oke, basi wikiendi hii nitakutumia pesa uje, lakini utafikia wapi?”

    “Si gesti jamani! We unadhani nitafikia wapi kama si gesti?”

    “Sawa.”

    * * *

    Aisha alianza kuwa mpole kwa mumewe, hata alipochelewa kurudi hakumuuliza aliko wala atarudi saa ngapi! Na mumewe aliporejea alikutana na uso wa tabasamu kutoka kwa mkewe tofauti na zamani.

    Na kila siku, Aisha alimsihi mumewe kuachana na tabia yake ya nyuma ya kumnyima unyumba kwani amebadilika sasa na anajitambua.

    * * *

    Wikiendi ilifika, Beka alimtumia pesa shemeji yake kwani hata yeye kutoka moyoni alilimisi sana penzi la shemejiye huyo.



    Baada ya kupokea mshiko huo wa nauli, dada wa Aisha alimwambia mama yake kwamba anakwenda Moshi kwa Bitte.    “Muage baba yako si mimi,” alisema mama mtu. Akamfuata baba’ke…

    “Baba samahani, ninaomba ruhusa niende kwa Bitte, Moshi.”

    “Bitte gani?”



    “Yule rafiki yangu, mtoto wa mzee Telekamalombi.”

    “Ameolewa yule au bado?”



    Dada ake Aisha hakujua maana ya swali la baba yake, yeye akaamini kwamba akisema hajaolewa, baba yake atamsema anakwendaje kwa mtu asiye katika ndoa, akasema…

    “Ameolewa baba, ana familia yake kwa sasa.”

    “Basi hakuna kwenda.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alishtuka dada ake Aisha, iweje akataliwe kwenda wakati mtu ameshamwambia ana familia…

    “Wewe umeishi kwa mdogo wako, Dar yaliyotokea unayajua leo hii unataka kwenda kwenye ndoa nyingine ili ukaitibue siyo? Hakuna kwenda nimesema.”



    Aliingia chumbani na kuanza kulia sana akidai baba yake anamfuga kama mtoto. Alimtumia meseji Beka…

    “Baby, baba amekataa mimi kusafiri. Sina cha kufanya.”

    “Pole sana, vuta subira iko siku atakubali tu, usiwe na haraka.”

    * * *

    Siku hiyo, Aisha aliamka akiwa na hasira zilizopitiliza, aliamua kwenda kazini kwa Faidha ili kuzungumza naye kwa njia yoyote ile, iwe kwa ujeuri au busara pungufu lakini lengo akampe vidonge vyake…



    “Angekuwa mwanamke mwenye busara kichwani angeamua kuachana na mume wangu maana amejua kwamba kumbe mimi ndiye mke wa Beka, lakini yeye bado anamng’ang’ania, kwa nini?” alisema moyoni Aisha akiwa anatoka kwake.



    Alifika kazini hapo na kukutana na mlinzi yuleyule wa siku ya kwanza…

    “Samahani, naweza kuonana na Faidha?”

    “We si ndiyo ulikuja siku zile?”

    “Ndiyo mimi.”



    “Oke, ofisi yake si unaijua ilipo?”

    “Ndiyo.”

    “Oke, basi pita.”



    Aisha alipita kwenda ofisini kwa  Faidha huku akiziandaa hasira. Aliamua kumwadhiri mbele ya wafanyakazi wenzake wajue kwamba anaiba bwana wa mtu!

    Ile anazama ndani tu, anakutana na mumewe Beka naye anainuka kutoka kwenye kiti, mezani kwa Faidha…



    “Faidha, nimekufuata wewe, lakini bahati nzuri nimemkuta na mume wangu leo,” alisema Aisha kwa sauti iliyotulia kama hana wasiwasi…



    “Nimefanya nini? Hapa ni kazini kwangu ujue Aisha,” alisema Faidha akiwa amemtumbulia macho Aisha. Mumewe, Beka alikosa nguvu, alishindwa kusimama sawasawa, akakaa.



    “Unajua unafanya nini na mume wangu? We ni mtu wa kunichukulia bwana kweli Ummy. Unajifanya unaitwa Faidha, kumbe Ummy! Loo! Ukome naseema Ummy,” alipayuka Aisha mbele ya wafanyakazi wenzake





    Sasa ofisi ilikuwa kama sokoni, mzozo ulianzia hapo kwani Feidha naye hakuwa tayari kudhalilisha mbele ya wafanyakazi wenzake, tena wadogo kwake kicheo.

    Aliamua kujibizana na Aisha…

    “Kwani kosa langu mimi ni nini? Mumeo mwenyewe kaja kwangu na kusema unampimia unyumba kama mafuta ya kula, sasa je?”



    “Lini alikwambia kama si umbeya wako?”

    “Muulize mwenyewe.”

    “Si huyu hapa, lini alikwambia?”

    Watu waliokuwemo kwenye ofisi hiyo walijitoa kuweka hali sawa lakini mzozo uliendelea…

    “Kama ungekuwa mwanaume kweli si ungetafuta mume wako?” alisema Aisha kwa sauti iliyojaa kebehi…



    “Na wewe ungekuwa mke kweli si ungekuwa unammwagia unyumba mumeo, angehangaika nje kufanya nini? Loo! Hata sijui kama ulifanyiwa kitchen party wewe na kama ulifanyiwa ulikula fedha za shughuli tu,” alitema cheche Feidha.

    Meneja mkuu wa benki alitokea akiwa mbogo baada ya kunyetishiwa kuwa, ofisini kwa Feidha kuna timbwili zito…



    “Ni nini hapa?” aliuliza meneja huyo. Alipoona hajibiwi na Feidha wala Aisha, achilia mbali Beka ambaye ilibidi arudi kukaa kwenye kiti, aliwauliza akina Salma…

    “Eti kuna nini?”

    “Huyu dada kaja anasema eti Feidha kampora mume wake.”

    Meneja alihisi ni kitu kikubwa, mfanyakazi wake kudaiwa mambo kama hayo ni kuichafua taasisi, akatuliza hali ya hewa, akataka watu wengine watoke nje, akabaki yeye, Beka, Feidha na Aisha tu, akakaa…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Feidha, niambie ukweli. Huyu ni mume wa huyu dada?”

    “Ni kweli bosi.”

    “Kaka, ni kweli wewe mkeo ni huyu dada?”

    “Wote wake zangu.”

    “Ah! Sasa kama wote wake zako kwa nini huyu anamshutumu huyu kuwa amekupora wewe.”

    “Huyu ni wivu wake tu.”



    “Eti dada, unamtambua Feidha kama ni mke mwenzio?” alimuuliza Aisha sasa…

    “Mi nadhani dada jibu la mfanyakazi wako limetatua kila kitu, maana mwenyewe amekubali huyu ni mume wangu na hakusema yeye ni mke mwenzangu. Aliyeleta hayo mambo ni huyu mume wangu. Mimi nadhani nisimulie kidogo.”

    “Hebu simulia kidogo,” alisema maneja huyo ambaye ni mwanamke.

    Aisha aliweka wazi uhusiano wake na mume wake, alikoangukia ni wapi na anakotaka kwenda ni wapi.

    “Kwa hiyo ni kweli ulikuwa unamnyima unyumba mume wako?” aliuliza meneja.

    “Ni kweli.”



    “Mh! ulipata wapi hayo mawazo?”

    “Ya?”

    “Ya kumnyima unyumba mume wako!”

    Aisha alinyamaza hapo, hakuwa na jibu.

    “Kwa hiyo hata wewe unakubali kwamba ulifanya makosa?”

    “Nakubali dada.”



    “Oke, enhe? Feidha! Wewe ulipokutana na huyu bwana alikusimulia matatizo ya ndoa yake?”

    “Ndiyo, ndiyo maana nikampokea. Kwani hata mimi kama mwanamke nikiolewa siwezi kumnyima unyumba mume wangu,” alisema Feidha kwa sauti iliyoonesha kupata tumaini jipya!



    “Sasa licha ya hayo yote Feidha, je ilikuwa halali wewe umchukue mume wa mwenzako kisa amekusimulia kwamba ananyimwa unyumba?”

    “Si sahihi,” alijibu kwa kudakia Feidha.

    “Lakini anti, mbona mimi hunipi muda wa kuzungumza?” alihoji Beka akionesha kuwa na shauku ya kutaka kusema…

    “Sema.”



    “Ni hivi, mimi nimeamua kwa imani yangu kuwa na wake wawili, Feidha na Aisha. Hilo hata Aisha analijua, nilimwambia. Kama kosa ni mimi kusema kuhusu matatizo ya mke wangu ni kawaida. Kila ndoa duniani ukiuliza wanandoa, wana asili ya kukutana.

    “Kwa hiyo mimi nilikutana na Feidha nikamsimulia matatizo ya mke wangu. Lakini ikawa ndiyo asili au chanzo cha mimi kujuana na Feidha hadi kufikia hatua ya kuwa mke wangu.”



    Wakati Beka anazungumza hayo, kutoka moyoni, Feidha hakuwa anapenda kusikia neno uke wenza. Hilo alikuwa halipendi toka anasoma shule ya msingi, aliweka ahadi kwamba hatapenda kuwa mke mwenza. Iwe kuanza yeye au kukuta mke mwenzake.

    “Sasa kaka, kama kweli ulimwambia mkeo kuhusu uke wenza huoni kama hataki ndiyo maana amekuja juu?”



    “Atataka tu.”

    “Feidha,” aliita bosi huyo.”

    “Abee bosi.”

    “Unalijua suala la wewe kuwa mke wa pili?”

    “Kusema ukweli bosi ndiyo nalisikia, niliambiwa ataachana na mkewe, mimi nitachukua nafasi, lakini kama ni uke wenza, siko tayari.”



    Mjadala ulikuwa mzito, alichotaka meneja huyo ni kutuliza ule mzozo wa awali…

    “Sasa sikieni, wewe Aisha na mume wako nendeni zenu. Mkifika nyumbani jadilianeni kuhusu hilo la uke wenza, mkikubaliana sawa, mje mniambie mimi, niko tayari kumsimamia ndoa Feidha,” alisema meneja.

    Aisha na Beka walikubaliana, wakaondoka wote kwa wakati huohuo huku Beka akichukua business card ya mwanamke huyo kwa ajili ya mawasiliano.

    Baada ya wawili hao kuondoka, meneja akamgeukia Feidha…

    “Feidha.”



    “Ndiyo bosi wangu.”



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Unajua ni jambo la ajabu sana limetokea?”

    “Sijaelewa bosi.”“Mwanamke kuja kufanya fujo hapa kazini!”

    Faidha aliposikia hivyo alibaki amejiinamia tu kwa aibu kwani hata dhamira yake ilimwambia kilichotokea si cha kawaida.

    “Ni kweli bosi.”



    “Kama ni kweli itabidi uandike barua ya kujieleza kwa nini uongozi usikuadhibu?”

    “Samahani bosi.”“Mimi langu ni hilo tu,” alisema bosi huyo huku akitoka kwa hasira.

    Faidha alikaa na kujiinamia. Mawazo kibao kichwani yalimpata. Alianza kukasirika na yeye akiamini bila Aisha yasingetokea yale yote…



    “Dawa yake yule kumchukulia mume wake moja kwa moja sasa,” alisema moyoni Faidha akijiapisha kwa dhati.Akina Salma nao walirejea baada ya kumuona bosi wao ametoka…



    “Kwani dada Faidha vipi? Yule mwanamke ana akili timamu kweli?” walimuuliza…

    “Ah! Yule kachanganyikiwa, kabip akapigiwa sasa anatapatapa tu…yeye angedili na mumewe si kuja ofisini kwa watu.”



    “Ni kweli dada Faidha, sisi wenyewe tumemshangaa sana. Halafu hata wewe huna kosa kwani ulimuita aje hapa?”“Si ndiyo hapo sasa!”

    “Mh! Wanawake wengine bwana, ni wa ajabu sana,” alisema Salma…

    “Wa ajabu wa ajabu,” alimalizia Faidha.

    ***

    Beka na Aisha walifika nyumbani, kila mmoja alitaka kumsikia mwenzake anasema nini kuhusu lilitokea lakini Beka akaonekana kutosubiri, akaanza…

    “Mwezi ujao nafunga ndoa na Faidha.”

    “Si alisema pale hataki uke wenza, hukumsikia?”



    “Hatakuwa mke wenza, wewe nakupa talaka yako sasa hivi, sitaki ujinga mimi!”

    “Unipe talaka nimekukosea nini mimi?”

    “Hujui ee?” Basi subiri utajua tu.



    Haiwezekani uwe mwanamke wa fujo, hekima imekupitia pembeni wewe,” alifoka Beka, akaenda kununua karatasi dukani na kumwandikia talaka Aisha.

    Siku ya pili, Aisha alirudi kwa wazazi wake na kusimulia yaliyompata akaambulia kupewa pole nyingi. Alikaa kwao kwa mwezi mmoja akarudi mjini kuanza maisha yake mwenyewe, Beka akafunga ndoa na Faidha.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO.



0 comments:

Post a Comment

Blog