Chombezo: Vitilivyogo ( Papa na Muhogo )
Sehemu Ya Tano (5)
“Siyo hivyo Shaka, mara nyingi ninapokuwa na wewe huwa anajua nipo wapi hunipitia na kunisindikiza nyumbani, kwa vile ni shoga yangu humuamini kuwa nimepitia kwao.”
“Bado sijakuelewa, inaonekana hii ndiyo tabia yenu?”
“Tabia gani tena baby mbona najuta kulizua.”
“Siyo kulizua nafahamu kabisa mtindo huu haukuanza leo kwa vile sikukuta msichana.”
“Mungu wangu, yaani umefika huko?”
“Mimi nani yako?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mume wangu.”
“Kwa nini huniambii ukweli?”
“Baby haki ya nani, kuna siku unakumbuka tuliachana saa nne usiku niliporudi nyumbani niligombezwa sana na kuonekana nimeanza umalaya. Nilimueleza siku ya pili Diana ambaye ndiye aliyenifundisha mbinu za yeye kuja kunitembelea na mimi kwenda kwao ili nikikutana na wewe nipate nafasi ya kujitetea. Akiwa hayupo huwa nawahi mwenyewe unafahamu bali unataka kunionea tu.”
Stella alijitetea mpaka machozi yalimtoka kwa kuhofia kumpoteza, Shaka aliingiwa na huruma na kuamini anayosema mpenzi wake.
“Basi mpenzi yamekwisha.”
“Shaka nakupenda sana amini sina mwanaume yeyote zaidi yako.”
“Nimekuelewa mpenzi.”
“Basi nipe haki yangu.”
“Tutachelewa baby.”
“Nikiwa na wewe hata nikipigwa nyumbani siogopi.”
“Kwa sasa ni saa ngapi?”
“Saa mbili usiku.”
“Basi tumalizie baby.”
Waliingia kilingeni Shaka aliendelea kugawa dozi kama hana akili nzuri maufundi aliyofundishwa na Betty, Stella alichanganyikiwa na kumlazimisha Shaka walale pale hotelini.
“Hapana baby sasa ni saa tatu na nusu tuwahi nyumbani.”
“Shaka unanipenda?”
“Tena sana.”
“Basi naomba leo tulale kwa mara ya kwanza.”
“Hapana kitamu huliwa kwa hamu pia ukila na kipofu usimshike mkono.”
“Nimekuelewa,lakini naomba kwa leo tu baby.”
“Unawaheshimu wazazi wako?”
“Ndiyo.”
“Unapenda penzi letu liendelee?”
“Tena tuwe mke mume na mke tuzae na watoto.”
“Basi nyanyuka tukaoge tuwahi nyumbani.”
“Mmh! Sawa babu nakubali kwa vile nakuamini kwa asilimi elfu moja.”
Walikubaliana kwenda kuoga kisha walitoka muda ulikuwa saa nne za usiku, Stella alimteremsha Shaka kwao na yeye kurudi kwao bila kujua atawaeleza nini wazazi wake.
Shaka akiwa hoi alielekea kwao, kutokana na uchovu alipanga akifika ndani tu anabadili nguo na kujitupia kitandani bila kuwasha taa. Alitembea kwa kujivuta akielekea nyumbani. Alipofika alisogea mlangoni ili aingie ndani, alipogusa mlango ili azungushe kitasa kufungua mlango aliguswa kwa nyuma na kumfanya ashtuke.
Alipogeuka alishtuka kuonana uso kwa macho na Betty.
“Ha! Betty?”
“Ndiyo mimi,” Betty alisema kwa sauti ya upole.
“Mbona saa hizi unatoka wapi?”
“Shaka nikuulize mimi au wewe?”
“Betty mimi ndiye natakiwa kujibiwa kwa vile nimeuliza,” Shaka aliweka kibesi.
“Shaka huwezi kuamini leo nimekuwa sichezi mbali na kwenu toka saa mbili, kila nikiuliza wanasema hujarudi.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ha! Umemuuliza nani?”
“Wote, huwezi kuamini leo nimeingia chumbani kwako kwa mara ya kwanza ili kupata uhakika, nilijua mdogo wako alikuwa akinidanganya kuwa hujafika.”
“Mmh! Karibu.”
“Shaka ulikuwa wapi mpenzi wangu?”
“Mpirani.”
“Mbona mmechelewa kurudi?”
“Gari lilituharibikia njiani.”
“Lakini si nilikukataza kwenda?” Betty alimuuliza.
“Huwezi kuamini mechi zote walizocheza sikwenda, leo mwalimu alinitishia kuniadhibu ndiyo nikaenda.”
“Si utakuwa umechoka sana mpenzi wangu?” Betty alikuwa mpole.
“Wee acha tu, kuna kipindi tulilisukuma gari kwa umbali mrefu, ukichanganya na mechi hapa nipo hoi,” Shaka alitengeneza mazingira ya kumkwepa Betty kwani alikuwa amechoka sana.
“Kwa hiyo Shaka?”
“Kama mambo yetu! Utanisamehe, nipo hoi.”
“Shaka usinitanie, una siku gani hujanipa raha zangu, leo Shaka punda afe lakini lazima mzigo ufike.”
“Mpenzi huenda nisikuridhishe, kwa nini isiwe kesho ili nikupe kitu kamili?”
“Shaka utani huo njaa ya leo haiwezi kushiba kwa ahadi ya kesho.”
“Naogopa kukuudhi mpenzi.”
“Huwezi Shaka nitajua jinsi gani ya kufika safari yangu kwa msaada wako.”
“Mmh! Sawa, lakini sijala.”
Shaka hakuwa na jinsi kumchomoka Betty ambaye alikuwa na ugwadu wa muda mrefu. Betty naye hakutaka kupoteza muda waliondoka na Shaka hadi kwenye baa na kumnunulia chipsi mayai na nusu kuku, kisha waliondoka hadi kwake.
Walipofika kwanza alimpelekea Shaka maji ya moto bafuni kuoga kisha alimuandalia chakula mezani ili akitoka kuoga apate chakula na kopo la Red Bull kwa ajili ya kurudisha nguvu zilizopotea. Shaka akiwa bafuni alijiuliza maswali mengi juu ya kukabiliana na Betty, mwanamke mwenye ugwadu kama mfungwa.
Kwa vile alikuwa amemdanganya alipanga muziki utapozimikia basi ndiyo utakuwa mwisho wa burudani, kwani hatakuwa na lawama kutokana na kujihami mapema. Alijiuliza mwisho wake nini kutembea na wanawake wote wale kila mmoja akikutana naye anataka dozi kamili.
Betty naye hali ilikuwa mbaya kutokana na kukosa kipande cha muhogo wa Jang’ombe ambao kila alipougegeda lazima aliulamba mwiko. Siku alizomkosa Shaka na kwenda kwa mpenzi wake alirudi na upele wake kutokana na mkunaji kukosa kucha na mwenye kucha alikuwa anaumwa.
Shaka alitoka bafuni akiwa na upande wa kanga, Betty alichukua upande mwingine na kumfuta mwili mzima. Kisha alimsogeza kwenye chips yai kuku.
“Mpenzi wangu kunywa kwanza hii Red Bull ili irudishe nguvu, kisha ule upande nguvu angalau unipatia mguu wa jini uwe wa kukidhi haja. Kama utaniongeza mbili za mkwezi nitafurahi zaidi. Haki ya nani nitakupa zawadi kubwa.”
“Nitajitahidi mpenzi.”
“Basi kula mi naenda kuoga.”
Betty alisaula palepale na kuelekea bafuni bila kitu mwilini huku akichezesha vilima viwili vya nyuma ambavyo vilikuwa laini kama mchicha pori. Alifanya vile kumshtua Shaka kwa kuamini hata kama amechoka akiona umbile tamu kama ile lazima atarudi mchezoni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shaka naye alimsindikiza kwa macho huku akajishangaa kuweza kupata utamu wa mwanamke kama yule anayemilikiwa na mwanaume mwenye fedha tofauti na yeye kula chakula cha shikamoo. Japokuwa alikuwa amechoka lakini alijiapiza akimkosa sana basi mbili za mkwezi za haja.
Wasiwasi wake ukabakia kwenye kuchoka sana na kushindwa siku ya pili kwenda shule. Lakini aliamini hakumtendea haki Betty mpenzi wake kwa kumdanganya mtu aliyemfanya aonekane machoni kwa watu. Alipanga kupigana kufa na kupona kuhakikisha anapata zawadi aliyoahidiwa na Betty.
Betty akiwa bafuni kila alipojishika kwa bibi alihisi kama ameota upele unaohitaji kukunwa na Shaka. Alipanga hata kama Shaka atachoka mapema lakini atatumia mtindo wa mti wa kufulia nazi ambao kazi yake kusimama nazi kupigwa juu yake na nazi hutoka vizuri tayari kwa kupasuliwa na kukunwa.
Betty alitoka bafuni kama alivyoingia bila kitu mwilini na kurudi kwa Shaka aliyeshambulia msosi kama fisi mwenye njaa aliyevamia bucha. Muziki aliokutana nayo kwa Stella japokuwa ulimchosha ulikuwa wa kitoto ila kazi ilikuwa kwa Betty mama shughuli na shughuli yake lazima ushughulike kisawasawa.
Betty baada ya kukaa pembeni ya Shaka, alivuta upande wa khanga na kuwa saresare maua. Mchezo ulianzia palepale mezani Shaka hakuwa na haraka alianza kwa ulaji wa mboga saba kugusa kila bakuli na kumfanya Betty ambaye tayari mchicha ulikuwa umekolea nazi kuangukia banda la kuku na kupasua yai moja. Betty aliona Shaka chenga nyingi wakati hakabwi na mtu zaidi ya kuusukumia mpira wavuni.
“Shaka punguza chenga nifunge goli bhana, mwenzio maji yamechemka zamani tia mchele uache sufulia lifuate mwiko.”
Siku zote mfungaji mzuri akilaumiwa husahihisha makosa yake kwa kupeleka mpira wavuni na kuwafanya watazamaji walipuke na mayowe ya kufurahia goli na kusahau lawama.
Taratibu Shaka ambaye alikuwa ameanza kuwa mzoefu wa bahari aliingiza chombo majini na kuanza kupiga kasia taratibu kama mamba mzee kwenye mto. Betty dakika ya kwanza tu baada ya konga mbili tatu alikurupuka golini na kupishana na mpira na kumfanya apige kelele.
“Shakaaa, unaona..unaona mambo si ndiyo haya.”
Mtu mzima alikuwa akiokota yai lililopasuka kwenye banda la kuku, kama bondia alikuwa amekutana na ngumi asiyoitegemea na kumpeleka chini. Alinyanyuka harakaharaka na kufuta gloves mchezo ukaendelea.
Kwa vile Shaka alikuwa ametoka kutumika wazungu walikuwa mbali, kila alipowaita walikuja taratibu ikabidi Betty afungue bomba kwa kupasua madafu mengi, kitu kilichomfanya achoke sana.
Alishangaa Shaka kuwa na nguvu za ajabu kwa kuweza kumliza kilio mara nyingi bila kuonesha naye kamwaga hata tripu moja.
“Shaka hujafika hata mara moja?” Betty aliuliza kwa sauti ya muhemo kutokana na kuchoka sana.
“Bado.”
“Mmh! Ni Red Bull tu au umetumika?” alishtuka.
“Walaa, uchovu wa mpira na kinywaji ulichonipa kimefanya niwe na nguvu kama faru.”
“Mmh! Leo nimepatikana mtoto wa kike.”
“Tuache?”
“Hapana, mpaka ufike na wewe.”
Betty aliamini kwa mtindo ule atakesha, alikaa mkao wa kibao cha mbuzi mkuno wa nazi. Huku akitweta alimwambia Shaka:
“We tulia niachie kazi hii.”
Shaka alikaa kama alivyoelekezwa na kumuacha mtoto wa kike akiiacha nyonga ifanye kazi yake, kifuu kilijizungusha kwenye meno ya mbuzi. Shaka alijikuta akikutana na kitu kipya kabisa ambacho kilimfanya awahi kupasua yai la bata mzinga. Kwa vile Betty alikuwa mzoefu baada ya Shaka kutua mzigo alimpa pole.
“Pole na safari mpenzi,” Betty alimshukuru Shaka kwa kumtoa jasho la chini ambalo wanaume wengi walishindwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Asante,” Shaka naye alijibu huku akihisi uchovu wa ajabu kwa kusikia kizunguzungu.
Wote wawili walikuwa wamechoka sana, usingizi ukawapitia bila kujijua.
***
Betty alikuwa wa kwanza kuamka, alipojaribu kunyanyuka mwili ulikuwa umechoka sana kama alikuwa akiangusha mbuyu kwa kisu cha kukunja. Alipoangalia saa ya kwenye simu ilimuonesha ni saa kumi na moja alfajiri. Alishtuka kwa kujua ulikuwa muda muafaka kwa Shaka kuamka kwenda kujiandaa kwenda shule. Alimuangalia alikuwa amejilaza akiwa hoi kama mtu aliyekuwa akifua vyuma.
“Shaka,” alimwita huku akimtikisa.
“Mmh!”
“Amka kumekucha wahi kwenu ili ujiandae kwenda shule.”
“Leo siendi.”
“He! Leo hakuna shule?” Betty alishtuka.
“Ipo.”
“Sasa kwa nini huendi.”
“Nimechoka sana kazi uliyonipa jana si ya kitoto.”
“Sasa itakuwaje nyumbani kwenu watasemaje?”
“Wacha nilale kidogo ili baadaye nikalale nyumbani.”
“Hapana Shaka, japokuwa nimechoka naomba nikusindikize kwenu kwani sasa hivi ni saa kumi na moja.”
Shaka alinyanyuka kitandani huku mwili ukiwa umechoka sana, Betty alimsindikiza bafuni kuoga kisha alimsindikiza mpaka kwao. Wakati Betty akimsindikiza Shaka, shoga yake Edna alikuwa akitoka kumsindikiza mumewe aliyekuwa na sindano za masaa lakini hakutaka kumshtua.
Moyoni aliumia kwa kujua kama Betty amefanikiwa kulala na Shaka mpaka asubuhi basi atakuwa amepata raha kamili, utamu thabiti toka kwa kijana mdogo mwenye uwezo kama wa nyati. Moyoni alijilaumu kuolewa mapema, lakini alijipanga kuhakikisha siku moja analala na Shaka mpaka asubuhi.
Shaka baada ya kufikishwa kwao alimgongea mdogo wake baada ya kuingia alifikia kitandani na kuutwanga usingizi wa haja. Asubuhi alipoamshwa kwenda shule alisingizia ugonjwa, siku ile aliamka saa sita mchana. Hakuwa yeye tu aliyepigika hata Betty naye alikuwa hoi.
Baada ya kurudi kumsindikiza Shaka alipofika kitandani naye usingizi mzito ulimpitia. Majira ya saa nne asubuhi shoga yake Edna alitaka kupata umbeya, alikwenda kwa shoga yake. Alipofika alikuta mlango umerudishwa aliingia ndani na kuita lakini hakujibiwa, alikwenda chumbani na kumkuta Betty amelala usingizi mzito akiwa hajitambui.
Mlalo aliolala ulikuwa unaonesha jinsi gani alivyokuwa amechoka, alikuwa amejitandaza kitanda kizima huku akikoroma. Edna alijikuta akimuonea wivu shoga yake na kujiuliza siku gani na yeye anapata kipigo kile cha pweza. Aliamini akimuamsha atakuwa sawa na kuzuia chafya kwani alitakiwa kuachwa alale ili hamu zake zimuishe aamke mwenyewe.
Alimuacha bila kumwamsha na kurudi kwake huku akiwa na mawazo mengi juu ya uwezo wa Shaka. Kilichomshangaza kuwa na uwezo japokuwa hakuwa mtaalamu sana wa kitandani lakini nguvu zake zilimfanya mwanamke kulia kilio cha mvua ya machozi.
Siku hiyo Betty aliamka saa nane mchana, kutokana na kuwa na njaa kali, kuoga aliona anachelewa alijifunga vitenge na kukimbilia kwenye baa ya karibu na kuagiza mchemsho na kuteremshia na pombe kali. Edna aliyekuwa anapita karibu na baa ile alishangaa kumuona shoga yake mchana ule akipata kinywaji huku akionekana hajatulia.
Alimfuata na kumsalimia.
“Shoga vipi mbona upo hivyo?”
“Mmh! Shoga wee acha tu, Shaka jana kidogo aniue.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kivipi?”
“Toka nivunje ungo jana kidogo roho iachane na mwili kwa utamu usioisha hamu.”
“Kwa nini?” Edna alishtuka na kukaa kitako macho yamemtoka pima kama aliyeona samaki wakivuliwa kwenye lami.
“Shoga si ya kuzungumza hapa ngoja nimalize kinywaji twende nyumbani, yule mtoto lazima atakuwa amechanjia. Jana nilimwaga mpaka tenki likakauka mtoto ndo kwanza anakuja. Huwezi amini njaa niliyokuwa naisikia, kuoga niliona nachelewa.”
“Mmh! Shoga inatosha utanimalizia nyumbani.”
Betty alimaliza kinywaji chake haraka na kulipa kisha waliongozana kurudi nyumbani. Edna alikuwa na shauku ya kujua kitu gani Shaka alichomfanyia mpaka akasababisha tenki kuvunja mpaka likakauka.
***
Majanga hayakuwa kwa Shaka na Betty tu, Stella asubuhi ilipofika kitanda kilikuwa kitamu kama nini, alijishauri mara mbilimbili juu ya kwenda shule. Alijikuta akiamua kupumzika kwani mtanange wa jana usiku ulikuwa wa kufa mtu na kumfanya achoke sana. Alikubaliana na maneno ya Diana kuwa Shaka haonjwi mara moja akakuisha hamu.
Aliamua siku ile kulala nyumbani na kusingizia kwa mama yake anaumwa tumbo baada ya kwenda kumuamsha. Diana alimpitia rafiki yake kama kawaida, alipofika alipokelewa na mama yake.
“Shikamoo mama.”
“Marahaba Diana.”
“Vipi shosti wangu ameshatoka?”
“Hapana, leo anaumwa.”
“Nini tena mama?”
“Tumbo, anasema limemuanza toka usiku.”
“Ngoja nikamuone ili niwahi shule.”
Diana alikwenda moja kwa moja chumbani kwa Stella, alimkuta amepitiwa usingizi. Alimsogelea kitandani na kumtikisa huku akimwita.
“Stella... Stella.”
“Abee,” Stella aliitika huku akigeuka kumtazama Diana.
“Vipi?”
“Mbona hivyo tatizo nini?”
“Mmh! Wee acha tutazungumza jioni ukirudi, nimechoka sana.”
“Nini Tena?”
“Mmh! Shaka temea chini.”
“Ndio ukanifanya nini kunigandisha nikaliwa na mbu.”
“Shoga yangu nisamehe, sasa hivi utachukua elfu kumi juu ya meza, lakini jioni nitakulipa fidia, naomba ukamwambie dereva akuwahishe shule.”
“Mmh! Hongera mwaya.”
Diana aliondoka huku roho ikimuuma kwa kitendo cha kugandishwa wakati mwenzake akila raha ambazo kwake alikuwa amezikosa kwa muda mrefu. Lakini moyoni alifarijika kwa kuamini siku ile utawala ungekuwa wake kutokana na Stella kutoenda shule na yeye kuwa na Shaka na jioni ya siku ile naye angepata raha alizosikosa kwa muda mrefu.
Baada ya kumueleza dereva maagizo ya Stella, alimchukua na kumuwahisha shule mara moja.
Lakini alipofika shule alijikuta akikosa raha na kuiona siku ile mbaya baada ya kumkosa Shaka aliyetegemea kumkuta shuleni. Kwa vile shule ilimtumbukia nyongo naye alisingizia ugonjwa na kurudi nyumbani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
Siku ya pili Shaka na Stella wote walikuja shule kama waliambizana. Diana alijikuta kwenye wakati mgumu. Shida yake kubwa ilikuwa kuzungumza na Shaka kwa nafasi bila Stella kuona. Alimvizia Shaka alipokwenda msalani alimfuata ili kumuuliza. Walisubiri wakati anatoka msalani ndipo alipomsimamisha na kumuuliza:
“Shaka vipi, mbona unanitesa?” Diana alilalamika.
“Kivipi?”
“Mbona sikuelewi?”
“Kivipi?”
“Ina maana na mimi sina hamu na wewe?”
“Tatizo nini?”
“Yaani naona kila siku wewe na Stella, mimi lini jamani?”
“Stella ndiye mwenye mali.”
“Shaka nionee huruma nami nina hamu na wewe.”
“Basi kesho.”
“Jamani kesho mbali kwa nini isiwe leo? Shaka nionee huruma yaani nina hamu kama mjamzito na embe mbichi kila nikikuona mate ya uchu yananijaa mdomoni.”
“Ngoja niangalie mambo yatakavyokuwa.”
“Shaka au hunipendi? Mapenzi niliyokupa hukuyapenda?”
“Hujui jinsi gani nilivyo na usongo na wewe, niache kazi hiyo nitakujulisha hata leo jioni.”
“Yaani nitafurahi ile mba...”
“Diana, Stella huyo,” Shaka alimshtua Diana baada ya kumuona Stella akija kwa mbali.
“Mungu wangu, sijui atajua?” Diana alisema kwa sauti ya chini.
“Wewe niachie wala usioneshe wasiwasi wowote.”
“Sawa.”
Baada ya muda Stella alifika na kusimama pembeni yao. Aliwaangalia wote usoni na kumuuliza Diana.
“Diana unazungumza nini na mpenzi wangu?”
“Jamani kuna ubaya gani kuzungumza na shemeji yangu?”
“Stella tatizo nini?” Shaka aliingilia kati mazungumzo.
“Kwani huyu nani yako?”
“Shemeji yangu.”
“Sehemu hii mnazungumza nini wawili?”
“Huyu si shoga yako?”
“Ndiyo, lakini simuamini.”
“Kwa hiyo nikitaka kumtuma kwako nisimtume.”
“Mtume, lakini si kusimama muda wote huo.”
“Sawa mama.”
“Haya nimekuja mwenyewe niambie.”
“Nilikuwa namwambia jioni ukitoka unisubiri,” Shaka alitengeneza uongo.
“Yaani hata mimi nilikuwa na hamu na wewe, japokuwa juzi ulinipa kipigo cha pweza, leo ilikuwa lazima nikuambie ukanizimue. Kila ninapokuona mate ya uchu yananijaa mdomoni lakini leo baba taratibu kesho nije shule.”
“Wewe tu mama, ndiyo maana nilikuwa namtuma Diana aje akutaarifu mapema ili ujiandae usiseme nimekushtukiza.”
“Mimi na wewe hata ukiniamsha usiku wa manane huniishi hamu.”
“Basi mi’ natangulia darasani.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Shaka alirudi darasani na kuwaacha Stella na Diana wakienda msalani. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na haja ya kujisaidia bali waliingia msalani kutimiza wajibu.
Stella alishtuka baada ya kutoweka kwa Shaka na Diana kwa pamoja darasani, siku zote hakumuamini shoga yake kutokana na kauli tata.
Alijikuta akiingiwa na wasiwasi kitu kilichomfanya atoke darasani na kuanza kumtafuta Shaka. Bahati aliwaona kwa mbali karibu na msalani wamesimama wakizungumza.
Mtoto wa kike presha ilimpanda na kwenda kama mbogo. Lakini majibu ya Shaka ya kumtaka jioni ilimfurahisha kwani ndicho kitu alichokitaka jioni ya siku ile baada ya kipigo cha juzi yake.
Diana roho ilimuuma baada ya nafasi yake ya kupunguza mateso kuchukuliwa tena na Stella. Alimshangaa Shaka kubadili kitu walichokipanga kwa jioni ya siku ile. Lakini bado alijipanga kuzungumza na Shaka kabla muda wa kutoka shule.
Shaka naye aliamini njia aliyotumia ndiyo iliyosaidia bila hivyo Stella angewasha moto kwa vile hakuwa na simile anapopandisha hasira. Alipanga kuonana na Diana siku inayofuata.
Jioni ilipofika Shaka aliondoka na Stella kwenda kula raha na kumuacha Diana akikasirika kwa kupinda mdomo kama pindo la jamvi bovu. Hata Stella alipomuomba amsindikize alikataa kwa kusingizia kuwa Sam mpenzi wake ametuma ujumbe amsubiri. Stella alikodi gari na kuondoka wawili na mpenzi wake Shaka bila kujua kaharibu mpango wa watu.
Lakini Shaka kabla ya kuondoka alimpa Diana ujumbe wa siri uliosema: Usiumie kesho zamu yako nitazimaliza hamu zako zote. Ujumbe ule ulimfanya Diana atabasamu kidogo.
Siku ile mchezo ulikuwa wa kawaida na kuwafanya wote wawahi nyumbani.
***
Siku ya pili wote walikuja shuleni kama kawaida kitu kilichozidi kumuudhi Diana ambaye alitegemea shoga yake kupata kipigo cha pweza mkaidi na kumfanya asije shule.
Kwa vile siku ile Stella alikuja shule Diana ilibidi awe mbali na Shaka, lakini alikuwa katika wakati mgumu wa kumfikia Shaka bila Stella kujua. Muda wa mapumziko kama kawaida Stella alikuwa karibu na Shaka muda wote kama kawaida yake hakutaka kumpa nafasi baada ya kuugundua utamu wake.
Kipindi cha mapumziko, muda wote alikuwa karibu hakutaka msichana yeyote ajipendekeze, kitu kilichofanya kila msichana shuleni kumwita Shaka shemeji.
Wakiwa wamekaa kwenye bustani ya shule wakipata vinywaji, Diana alikuwa akihangaika kama kuku anayetaka kutaga kufikisha ujumbe kwa Shaka japokuwa kuna wakati alimkonyeza na Shaka kuishia kutabasamu tu. Shida yake kubwa ilikuwa kumfikishia Shaka ujumbe kuhusiana na ahadi yao ya kukutana siku ile jioni ya siku ile kama walivyokubaliana jana yake.
Alipoona muda wa kurudi darasani unakaribia, alijifanya anakwenda msalani, alipofika aliandika ujumbe kwenye karatasi: Sasa leo itakuwaje? Si unajua zamu yangu.
Baada ya kuandika alirudi na kukaa pembeni yao. Alimtegea Stella anatazama pembeni, akakirusha kile kikaratasi ambacho kilidondoka pembeni lakini Shaka alishindwa kukichukua, alitegea wakiondoka akiokote ajue nini kimeandikwa katika kile kikaratasi.
Kengele ilipolia wakati Stella akinyanyuka alikiona kile kikaratasi na kukifungua, Diana na Shaka wote walishtuka lakini waliondoka bila kuangalia nyuma kusubiri.
Stella alikifungua na kukisoma hakukielewa alikitupa na kumfuata Diana aliyekuwa ameshusha pumzi nzito baada ya kuona kile kikaratasi kimetupwa na Stella kuelekea alipokuwa bila kuonyesha amegundua kitu kwenye kile kikaratasi.
“Shaka mpenzi,” Stella alimwita Shaka.
“Niambie.”
“Jana nimeinjoi sana mapenzi yaani nimelala swaafi, leo nataka tena maana hamu zangu bado zipo juu kila nikikuona, ikiwezekana wiki hii yote uwe unanipa mbili za mkwezi au mguu wa jini.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hakuna tatizo baby,” Shaka alijibu huku akimtazama Diana aliyekuwa amevimba kwa hasira.
Walielekea darasani, walipofika Shaka alitoka kujifanya anakwenda msalani ili arudi kukichukua kile kikaratasi. Alichepua mwendo haraka kuwahi eneo kilichopo kikaratasi na kukichukua. Stella alitoka darasani kuelekea ofisini alishangaa kumuona Shaka akitokea kwenye eneo walilokuwa wamekaa.
Alijiuliza Shaka pale alifuata nini, alijikuta machale yakimcheza na kurudi eneo lile ambapo Shaka alikuwa ameshaondoka na kuingia darasani. Kilichomshtua Stella ni kukikosa kikaratasi kile, aliachana nacho kwani aliamini huenda ni wasiwasi wake tu.
Shaka alipofika darasani alikifungua kile kikaratasi kwa siri na kukutana na ujumbe wa Diana wa kumtaka kuwa naye kwa siku ile. Alijiuliza atafanyaje kumkwepa Stella ambaye alikuwa na hati miliki ya kummiliki na tayari alikuwa amemkubalia wakati huohuo Diana alikuwa akijua ndiyo siku yake.
Lakini aliamini kama hatamdanganya basi atamtoroka na kwenda kumpa raha Diana kwani naye alikuwa na manjonjo yake ndani ya kumi na nane ambayo aliyamisi.
Wakati Shaka akiwaza yale Diana kwenye dawati alikuwa katika wakati mgumu baada ya shoga yake kurudi alipokidondoshea kipande cha karatasi.
Wasiwasi wake ulikuwa kuulizwa na Stella lakini baada ya kurudi hakuonesha wasiwasi wowote. Naye alikaa kimya kuogopa kujiingiza mwenyewe kwenye mtego.
Akiwa kwenye dawati lake muda mwingi aliwaza jinsi ya kupata jibu la Shaka ili ajue moja atapata au atakosa.
Wakati akiwaza yale Stella aliitumwa kupeleka madaftari ofisini, alipotoka nje ya darasa alichepua haraka mpaka kwa Shaka aliyekuwa ameinama akisoma daftari.
“Shaka vipi?” alimuuliza kwa sauti ya chini.
“Poa.”
“Ujumbe umeupata?”
“Ndiyo.”
“Kwa hiyo?”
“Kawa kawa.”
“Shaka muongo!”
“Kweli.”
“Na Stella.”
“Kazi hiyo niachie mimi, wee kaa mkao wa kula.”
“Poa.”
Diana alirudi haraka kwenye dawati lake kabla ya Stella hajarudi.
***
Diana baada ya kupata uhakika wa kuwa na Shaka jioni ya siku ile alipanga kutoka mapema kwa kisingizio cha ugonjwa wa tumbo. Alitengeneza uongo kwa shoga yake ili akiondoka asiwe na wasiwasi.
“Stella nasikia tumbo linaniuma,” Diana alisingizia ugonjwa.
“Limeanza saa ngapi?”
“Mmh! Muda lakini sasa hivi nasikia kama kuendesha.”
“Kwani usiku umekula nini?”
“Chipsi mayai.”
“Basi yatakuwa mafuta tu.”
“Wacha niwahi msalani.”
“Shoga nenda peke yako, sikusindikizi,” Stella alijifanya kuchoka.
“Haya shoga wala nisikusumbue, si unajua matatizo ya kuendesha kazi yangu nitakuwa kama konda wa daladala kwenda na kurudi kila dakika.”
“Pole shoga, siku nyingine uwe makini na machipsi yenu.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Diana hakujibu alijifanya kukimbilia msalani, alifurahi mpango wake kwenda kama ulivyopangwa. Baada ya kwenda kama mara tatu Stella aliamini shoga yake ni mgonjwa kweli.
“Shoga tumbo leo silielewi bora nikapumzike.”
“Kapumzike shoga yangu.”
Diana aliondoka na kicheko moyoni huku akimng’ong’a shoga yake ambaye aliamini shoga yake kweli anasumbuliwa na tumbo. Diana baada ya kuondoka alikwenda zake kwenye nyumba ya wageni waliyokwenda siku ya kwanza kula raha zao huku akijipanga kumpiku shoga yake kwa machejo ya kwenye sita kwa sita.
***
Muda wa kutoka shule, Shaka alikwenda hadi kwa Stella ambaye alijua atamkuta wapi. Alipofika alijifanya mwenye wasiwasi mwingi.
“Shaka vipi mbona kama haupo sawa?” Stella alimuuliza huku akishika glasi ya juisi.
“Wakati nakuja nimekutana na mwalimu John kanieleza kuwa baba alikuja na kutoa maagizo nikitoka shule nisipite popote, mama anataka kunituma.”
“Mmh! Sasa itakuwaje?”
“Yaani nimechanganyikiwa najuta kupitia eneo la ofisini,” Shaka alijifanya kujilaumu.
“Siyo mbaya basi tufanye kesho.”
“Hakuna tatizo.”
“Basi kunywa juisi uwahi nyumbani,” Stella alimbembeleza Shaka anywe juisi.
Shaka alikunywa juisi harakaharaka kama mtu mwenye haraka ya kweli, Stella alimpa fedha ya kukodi teksi awahi kwao.
“Basi mpenzi wangu wahi nyumbani msalimie mama mkwe.”
Stella alimpa shilingi elfu ishirini ya nauli.
“Mpenzi itakusaidia kwa nauli.”
“Asante,” Shaka aliipokea na kutoa pochi mfukoni ili aweke fedha aliyopewa.
Kumbe wakati anatoa pochi karatasi ya ujumbe wa Diana ilidondoka bila kujua, Stella aliimana kuiokota. Wakati ananyanyuka Shaka naye alikuwa akigeuka kwa haraka alikitupia kwenye begi la madaftari na kutulia. Shaka aliagana na Stella na kuwahi kwenye miadi yake na Diana aliyetangulia machinjioni.
Baada ya Shaka kuondoka, Stella alikitafuta kile kikaratasi lakini hakukiona, alipanga atakwenda kukitafutia nyumbani. Kwa vile shoga yake aliondoka anaumwa aliamua kupitia kwao kumjulia hali. Alikwenda hadi nyumbani kwao na Diana lakini alielezwa hajaonekana toka alipotoka asubuhi alipokwenda shule.
Kwa vile alikuwa akimjua vizuri shoga yake alijua alikwenda kwa mwanaume tu. Aliamua kurudi kwao bila kuwaeleza lolote juu ya taarifa za kuumwa kwa shoga yake kuogopa kumchongea. Akiwa njiani kwenda kwao alimshangaa shoga yake kuwa msiri kiasi kile kushindwa kumwambia anakwenda wapi.
Alipofika nyumbani baada ya shughuli zake alikumbuka kuna kikaratasi alichoangusha Shaka na kukitupia kwenye mfuko wa madaftari. Alijikuta akipandwa na shauku kutaka kujua kikaratasi kile kina nini.
Aliuchukua mfuko wa madaftari na kumimina madaftari yote kitandani na kuanza kutafuta kwa kupekua ukurasa mmojammoja kwa umakini na kushangaa kukikuta kwenye kitabu cha hadithi.
Kabla ya kurudisha vitu vyake ndani ya begi alikifungua kile kikaratasi, alishtuka kukiona kile kikaratasi na ujumbe ambao aliuona asubuhi na kuudharau. Kilichomshtua kukikuta kwa Shaka aliyerudi sehemu alipokitupia, wazo la haraka lilimjulisha kuna siri nzito kati ya Shaka na Diana na kuona kabisa shoga yake alikuwa akimzunguka.
Alijilaumu kuchelewa kukisoma kile kikaratasi kwani lazima angewafumania, aliamini kabisa Diana hakuwa akiumwa bali kumtoroka ili akamzunguke na kura raha zake. Hata taarifa za Shaka kuitwa nyumbani aliamini hazikuwa za kweli bali uongo uliotengenezwa ili waende wakakutane.
Stella alijikuta akikosa raha kabisa usiku ukawa mbaya sana kwake na kupanga kumtia adabu shoga yake hata ukiwezekana kuuvunja kabisa kwa vile hakuwa mtu sahihi kuwa naye. Kama vile tu anamchukulia
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mpenzi wake vipi akiolewa anaweza kumchukulia hata mumewe.
Siku hiyo alilala kwa shida sana huku akiomba siku ya pili ifike haraka ili akamtie adabu shoga yake mnafiki. Wasiwasi wake wa siku za nyuma aliamini kuwa Diana anatembea na Shaka ulikuwa na ukweli japo Shaka alimbana kutokana na yeye kuonekana ndiye aliyeuza siri ya utamu wake, hivyo kumfanya shoga yake aingie kichwakichwa.
Lakini aliapa kesho yake moto atakaomuwashia Diana hakutakuwa na wa kuuzima, akajiapiza kuwa tayari kwa lolote hata kufukuzwa shule lakini lazima amtie adabu shoga yake anayemlamba kisogo pamoja na msaada mkubwa wa kimaisha anaompa lakini hakuridhika na kumchukulia mpenzi wake.
***
Siku ya pili kama kawaida Stella alikwenda shuleni akiwa na shauku ya kuonana na shoga yake amueleze ukweli jana alikwenda wapi. Hata hamu ya masomo hakuwa nayo zaidi ya kutaka kupata ukweli ya mambo yaliyotokea jana. Diana naye siku ile alijitahidi kumchangamkia shoga yake baada ya kujua jana kama mali zake ziliibwa:
“Jamani shoga pole,” Diana alimpa pole Stella iliyomshtua.
“Pole ya nini shoga?” Stella alishtuka.
“Nilisikia jana ulikuja nyumbani kunitazama ukanikosa.”
“Wewe si umeondoka ukiwa unaumwa?”
“Ndiyo shoga.”
“Uliniaga unakwenda wapi?”
“Nyumbani.”
“Sasa mbona hukurudi nyumbani?”
“Sikuweza kurudi nyumbani kwa kuogopa kuboreka home kwa muda mrefu.”
“Ulikwenda wapi?”
“Kwa shemeji yako.”
“Nani?”
“Jamani kuna mwingine zaidi ya Bonny, nilipofika nilikunywa dawa na kujilaza mpaka jioni aliporudi shemeji yako akanirudisha nyumbani.”
“Mmh! Sawa, unaendeleaje?”
“Niko poa.”
“Mmh! Sawa.”
Stella alijikuta akibakia njia panda na kujiuliza ule ujumbe katika karatasi Shaka aliandikiwa na nani japokuwa mwandiko ulikuwa kama wa Diana. Alijikuta akirudi nyuma kwanza ili kufanya uchunguzi wa kina. Baada ya Diana kuruka kimanga Stella alipanga kumbana Shaka kuhusiana na kile kikaratasi alichokidondosha.
Aliamini kama atamuuliza swali jepesi atalipangua lakini kama atapeleka tuhuma za moja kwa moja lazima atamchanganya na kujua ukweli. Siku hiyo hata hamu ya masomo hakuwa nayo alitaka kujua nani aliingiza mkono kwenye mzinga wake na kulamba asali yake tamu kwa Shaka.
Alipanga kuonana na Shaka mapumziko huku aliapa moyoni kumshikisha adabu yeyote akayemjua kumchukua mpenzi wake na kuwa radhi hata kufukuzwa shule lakini amshikishe adabu. Shaka naye akiwa darasani hakujua kipi kinaendelea wala kukikumbuka kikaratasi alichopewa na Diana kama kimo mfukoni au kimepotea.
Stella alimtoka Diana amwite Shaka kwenye darasa lililokuwa halina wanafunzi, Shaka alikwenda bila wasiwasi bila kujua anaitiwa nini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali ya shuleni ilikuwa ya kawaida kila mwanafunzi alisimama popote kwani walimu walikuwa wamefuata mshahara benki. Alipoingia darasani alimkuta Stella ametulia darasani peke yake,
“Niambie mpenzi?” Shaka alijifanya kuchangamka.
“Poa,” Stella alijibu kwa sauti ya unyonge kitu kilichomshtua Shaka.
“ Shaka sasa hivi umekuwa si muaminifu.”
“Una ushahidi kwa hayo uyasemayo?”
“Ninao Shaka.. ninao,” Stella alijikuta akidondosha chozi mbele ya Shaka.
“Ushahidi gani?”
“Shaka nitakupa leo jioni.”
“Ushahidi wa nini?”
“We si unabisha utauona.”
“Haya tusubiri hiyo jioni.”
“Kwa hiyo leo itakuwaje?”
“Stella naomba leo unisamehe kwa vile nilipata mualiko wa shangazi nilishindwa kukataa,” Shaka alitengeneza uongo kwa vile jioni ya siku ile alikuwa na kazi na Betty.
“Sasa mbona hukumtuma mtu kunieleza kuwa amepata mwaliko?”
“Hilo ndilo kosa langu.”
“Au Shaka umeshanichoka maana kila kukicha vituko haviishi.”
“Stella unakwenda wapi huko, lini nimekufanyia hivi?”
“Unajua Shaka! Ila mi sitaki kusema,” Stella alisema huku akifuta machozi.
“Basi mpenzi nisamehe nakuahidi sitakuumiza tena.”
“Sawa Shaka nitafanyaje nami nakupenda wewe nifanyie vituko lakini mwisho wa siku utajua mwenye mapenzi ya kweli ni mmoja tu, mimi Stella wengine wote wezi na matapeli.”
“Nimekuelewa mpenzi wangu lakini wasiwasi wako tu, mimi ni wako peke yako.”
“Shaka naomba unyamaze usinichefue.”
“Haya mama nimenyamaza.”
“Jioni ya leo nina kazi na wewe, tena nataka maelezo ya kina bila hivyo leo nitamtwanga mtu, siwezi kuliwa kisogo huku najiona.”
“Stella mbona kila dakika huishi lawama.”
“Utasema hivyo lakini leo jioni utaujua ukweli.”
“Haya mama jioni tutajua mbivu na mbichi.”
“Baby nimeshikika ngoja niwahi msalani.”
“Poa, ukitoka huko urudi hapa.”
Shaka alikwenda msalani, wakati anarudi alikutana na Diana naye anatoka msalani.
“Mambo mpenzi?”
“Poa.”
“Jana umenipa burudani ya kufa mtu.”
“Aah! Kawaida tu.”
Kumbe wakati wakizungumza Stella aliwaona kwa mbali na kuja kasi alipokaribia Shaka alikuwa wa kwanza kumuona.”
“Stella huyo.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yupo wapi?” Diana alipogeuka alikutana na uso wa Stella uliojaa shari, Stella alikuja na kazi moja kumtia adabu shoga yake baada ya kuona akilamba asali yake kwa siri na kumgeuza babu jinga inama ufikiri mali yako inaliwa.
Stella aliyekuwa na hasira alikwenda moja kwa moja kumvaa Diana, kitu kilichomfanya ashtuke na kuhoji.
“Stella vipi?”
“Diana kwa nini unanizunguka?”
“Mimi?” Diana alijifanya kushangaa.
“Unafanya nini msalani na Shaka?” Stella alimuuliza kwa sauti ya juu.
“Jamani mbona makubwa, imeanza lini?” Diana alijifanya kushtuka.
“Stella leo umekuwaje?” Shaka naye aliungana na Diana kushtuka huku akitaka kumtenganisha na Diana.
“Niache nimshikishe adabu,” Stella alitumia nguvu kumkunja Diana.
“Stella hapa ni shule mambo hayo hayafai tutafukuzwa shule,” Shaka alimtahadharisha Stella.
“Acha nikufuzwe lakini nimshikishe adabu.”
“Leo una tatizo gani, kusimama na Stella nimeanza leo? Umemtuma kwangu mara ngapi? Muda si mrefu ulimtuma kwangu, umenitanguliza naye sehemu mara ngapi?” Shaka alijifanya kuja juu.
“Shaka mnanila akili,” Stella alilalamika huku akiangua kilio.
“Naomba unisikilize,” Shaka alimbembeleza Stella aliyekuwa amepandwa na hasira.
“Utaniambia nini Shaka wakati nina ushahidi?”
“Ushahidi gani Stella?”
“Najua mtaumbuka siamini kama Diana angenilamba kisogo,” Stella aliendelea kulalamika huku akitokwa machozi.
“Stella jamani, Shaka ni shemeji yangu kuna kosa gani kusimama naye kwani limeanza leo?” Diana alijitetea.
“Jamani hebu tuwe wastaarabu, kama kuna tatizo tutazungumza jioni baada ya masomo.”
“Edna una bahati leo ningefukuzwa shule kwa ajili yako,” Stella alimwambia shoga yake kwa hasira.
“Jamani tusambae mkuu wa shule anakuja huku,” Shaka aliwashtua walipogeuka walimuona mkuu wa shule akielekea upande ule.
Shaka na Stella walielekea msalani na Diana alirudi darasani akiwa na maswali lukuki sababu ya Stella kumbadilikia ikiwa asubuhi walikuwa wakicheka pia hata kusimama na Shaka haikuchukua hata dakika mbili kusema aliwaona kwa muda mrefu akajua wanatongozana.
Hali ya shoga yake kipenzi kumkunja shati huku akiwa amekasirika na kuwa tayari kwa lolote. Alijikuta akiwa na maswali juu ya kukutana jana yake kwa siri na Shaka huku ikiwa hakuna mtu aliyewaona kwani kila mmoja alikwenda kivyake kwa hilo aliamini hujui lolote huenda ni wasiwasi wake tu lakini hakuwa anajua lolote juu ya kukutana na Shaka jana yake.
Kutokana na kuwa na mawazo mengi alijikuta amepita darasa mpaka alipoitwa na mwanafunzi mwenzake ndipo aliposhtuka na kurudi darasani mwake. Muda wote alikuwa ajiuliza jioni itakuwaje kikao chake na shoga yake kipenzi aliyegeuka mbogo na kutaka kumpa kipigo cha mbwa mwizi.
Alijiuliza huo ushahidi anaotaka kuutoa ni upi? Picha? Alikataa na kuamini hajawahi kupiga picha na Shaka pia hata kukutana kwao mazingira hayakuwa rahisi kuwatilia mashaka na mtu. Alijipa moyo kusubiri jioni ifike ili atoe ushahidi unaoonesha yeye na Shaka ni wapenzi.
Shaka na Stella wakiwa wanaelekea msalani Stella alimwita Shaka.
“Shaka.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unasemaje?”
“Ukitoka msalani nisubiri.”
“Poa.”
Shaka aliingilia msalani akiwa anajindaa kujibu maswali ya Stella huku akijipanga kupinga shutuma zote atakazoambiwa. Alipotoka msalani alimsubiri pembeni ya choo baada ya muda Stella alitoka na kumsogelea.
“Vipi baby?” Shaka alimuwahi Stella.
“Shaka nimekukosea nini?”
“Kivipi baby?”
“Shaka unadiriki kunizunguka kwa shoga yangu?” Stella alianza tena kulia.
“Stella nimekueleza toka zamani maneno ya watu yatatugombanisha.”
“Si maneno ya watu bali nina ushahidi kumbe jana hukwenda kwenu ulikuwa na Diana.”
“Si kweli, jana nimewahi nyumbani na kutumwa na mama mjini kwenda kumnunulia matunda ya juisi.”
“Sasa jana Diana alienda wapi?”
”Stella hilo swali la kuniuliza mimi?”
“Sasa nimuulize nani?”
“Kwa hiyo mambo ya Stella ushindwe kujua shoga yake nijue mimi hiki si kioja?” Shaka alijifanya kushangaa.
“Si kioja bali unajua kila kitu Shaka,” Stella alianza kulia.
“Stella mambo gani tena haya mpenzi?”
“Shaka kwa nini huridhiki na mimi?”
“Kivipi baby.”
“Mwalimu wewe wanafunzi wewe, kwa nini lakini?”
“Tatizo lako kila mwanafunzi wa kike nikimchekea unajua mpenzi wangu.”
“Sawa ukweli jioni utajulikana.”
“Hakuna tatizo japo naamini sina kosa.”
“Sawa Shaka,” waliongozana mpaka darasani bila kusemezana huku Stella akifuta machozi.
“Usilie baby,” Shaka alimsogelea na kumnong’oneza sikioni.
“Kwa mtindo huu nitaendelea kulia na mwisho nitakunywa sumu.”
“Stellaaa maneno gani hayo!”
“Wewe si unaona raha kunitesa.”
“Basi jioni tutazungumza.”
“Shaka,” sauti ya mwalimu Rose iliwashtua na kufanya wageuke.
“Mnafanya nini?”
“Wewe unataka tufanye nini?” Stella alimjibu mwalimu kwa hasira.
“Stella usimjibu hivyo mwalimu,” Shaka alimzuia.
“Nisimjibu yeye nani? umbeya tu unamsumbua.”
“Stella unamwambia nani?” mwalimu Rose alimuuliza.
“Kwani hapa nazungumza na kima?”
“Stella, Stellaaa!” mwalimu Rose alisema huku akimfuata Stella alipokuwa amesimama.
“Mwalimu acha bwana,” Shaka alimuwahi mwalimu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Shaka mwache aje nimwoneshe malaya mkubwa.”
“Mimi malaya?” mwalimu Rose alijitahidi kutoka katika mikono ya Shaka iliyokuwa imemshikilia madhubuti.
“Shaka mwachiee, ukimshika unampa kichwa.”
Bahati nzuri mwalimu Monika alifika kuamua ugomvi ule.
“Jamani mbona aibu kuna nini tena mwalimu na mwanafunzi?”
“Si huyu mtoto.”
“Mimi si mtoto kama unavyofikiria mi mkubwa mwenzako,” Stella alijibu kwa maneno ya nyodo.
“Stella kwa nini lakini, kama hunisikilizi tusijuane,” Shaka alichimba mkwara.
“Nimekusikia Shaka lakini mwambie na mwalimu aache kunifuatafuata mimi si mke mwenzie.”
“Nini?” mwalimu Rose aliyekuwa amepandwa na hasira alitaka kujitoa kwenye mikono ya mwalimu Monika amfuate.
“Mwacheee aje malaya mkubwa umekosa walimu wenzio unafuata wanafunzi.”
“Jamani hebu mwalimu tuondoke wanafunzi wameanza kujaa,” mwalimu Monika alimshika mwenzie na kumpeleka nyuma ya shule kukimbia mkusanyiko wa wanafunzi walioanza kujaa. Naye Shaka alimchukua Stella aliyekuwa akilia kwa hasira na kumtoa eneo la tukio.
Stella pamoja na watu kuondoka alikuwa bado na hasira na kujikuta akishindwa kuzuia hasira zake na kuendelea kulia. Shaka alimfuata na kumbembeleza:
“Stella mambo gani haya?”
“Mambo gani wakati unafurahi.”
“Mi nimefanya nini tena jamani?”
“Hujui? Bila wewe ningetukanana na shoga yangu na mwalimu?”
“Stella hutaki kunisikiliza ungenisikiliza yote haya yasingetokea.”
“Shaka sina moyo wa chuma nina moyo wa nyama naumizwa na matendo yako.”
“Lakini lini ulinikamata na mwanamke?”
“Shaka najua mambo yako mengi jioni utajua nakufahamu vipi?”
“Naomba ujizuie na hasira unakoelekea kubaya, tunaweza kufukuzwa shule.”
“Kwa hili nipo tayari kufukuzwa shule, ina maana wamekuona baada ya kuwa na mimi, kabla yangu wao walikuwa wapi? Huyo Diana mshenzi mkubwa si ndiye alikuwa ananinanga kuwa natembea na mtu asiye hadhi yangu leo ndiyo umekua hadhi yao?”
“Lakini Stella, Diana sina uhusiano naye ni shemeji yangu tu.”
“Narudia tena kukueleza kukuvulia nguo si kwamba sina akili, nina akili zangu timamu kwa vile mapenzi hayana cheo bali kupata kiupacho furaha moyo wako.”
“Ni kweli lakini kuhusu wote unaonifikiria vibaya ni mazoea tu wala sina uhusiano nao wa karibu.”
“Shaka kwa nini umekuwa malaya wa kiume?”
“Stella utanionea bure, heri niache shule maana nina wasiwasi wa kukuharibia muda uliobakia.”
“Shaka tatizo si kuacha shule bali kujiheshimu, wewe si mtoto mdogo usiyejua zuri na baya lipi linafurahisha na lipi linaumiza.”
“Najua unaumia, lakini bado unajiumiza mwenyewe kujiingiza katika mateso ya kujitakia.”
“Shaka unadiriki kusema hivyo? Sawa..sawa jioni ndo utajua najitesa au unanitesa.”
“Sawa, jioni si itafika? Nimekueleza muda mrefu ukifuata ya watu tutatengana huku tunapendana.”
“Si kutengana bali kumkomesha mmoja katika hao wadokozi ili liwe onyo kwa wengine, kwani wanaume wamekwisha mpaka wakufuate wewe?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Basi Stella tutazunguza jioni.”
Stella alikwenda kwenye bomba na kunawa uso kisha alirudi zake darasani, Edna alipata nafuu baada ya kuona shoga yake kama kachanganyikiwa kugombana ovyo na kuamini huenda siku ile aliamka vibaya.
Stella akiwa mwingi wa hasira alichukua kitabu chake na kutulia kwenye dawati lake akisoma bila kuelewa kilichokuwa kimeandikwa. Taratibu hasira zake zilianza kushuka na kujikuta akitabasamu baada ya kukumbuka kitu.
Shaka naye alirudi darasani akiwa na msimamo wake wa kutokukubali kuwa ana uhusiano na Edna kwa kujua Stella hajui lolote zaidi ya kubahatisha na jioni angeweza kutoa ushahidi wa maneno ambayo hayana nguvu kwa vile kukutana kwao kulikuwa kwa siri sana.
Kwa hiyo hakuwa na wasiwasi wowote kuhusiana na tuhuma za kutembea na Edna na kujua jioni Stella angeona aibu.
***
Stella aliisubiri jioni kwa hamu, ilipotimu alimuagiza Edna kama kawaida atangulie na Shaka japokuwa moyo ulikuwa ukimuuma lakini aliamini siku ile ndiyo shoga yake angemjua yeye ni nani. Shaka akiwa ametangulia na Edna walipata muda wa kubadilishana mawazo kabla hajafika.
“Shaka mbona Stella anajiamini hivyo ana ushahidi gani?” Edna aliuliza.
“Hana ushahidi wowote zaidi ya kushuku, wewe na mimi ni kukataa kwa nguvu zote.”
“Mmh! Kile kikaratasi nilichokuwa kipo wapi?”
“Nilikitupa.”
“Ulikitupia wapi?”
“Nakumbuka kilikuwa mfukoni naweza kuwa kimefuliwa kwenye kaptula.”
“Msiwe mlikwenda kwenye mambo yebu akakiona ikiwa kimbembe,” Edna alimtaadhalisha Shaka.
“Walaa wasiwasi wako, kuhusu kile kikaratasi ondoa hofu kabisa.”
Wakiwa katika ya mazungumzo walikatisha mazungumzo baada ya kumuona Stella akija kwa mbele. Walipofika walikaa mkao wa kumsikiliza, ilikuwa tofauti alikuja na tabasamu tofauti na walivyofikiria patachimbika, alipofika aliwauliza:
“Jamani vinywaji vipi?”
“Tulikuwa tunakusubiri wewe.”
“Agizeni basi.”
Waliagiza na kuanza kunywa kukiwa kimetawaliwa na kimya, Stella alikuwa wa kwanza kumwita mpenzi wake.
“Shaka.”
“Naam.”
“Huyu ni nani yako?” alimuonesha Edna.
“Semeji yangu.”
“Kwa nani?”
“Kwako.”
“Vizuri, na Edna unamfahamu vipi Shaka?”
“Namfahamu kama mwanafunzi mwenzangu pia shemeji yangu.”
“Shemeji yako kivipi?”
“Kupitia kwako.”
“Vizuri, unamfahamu vipi Shaka zaidi?”
“Kumfahamu zaidi kivipi?” swali lilimchanganya kidogo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Unavyomfahamu nje ya ushemeji?”
“Simjui vyovyote nje ya ushemeji kupitia kwako.”
“Eti Shaka?”
“Eti kuhusu nini?”
“Kufahamiana na Edna, ni ushemeji tu au kuna zaidi?”
“Ni shemeji tu.”
“Sasa sikilizeni, huenda mnaniona kama mtoto mdogo mnaweza kunila akili.”
“Kivipi?” Shaka aliuliza.
Stella hakusema kitu alichukua mkoba wa shule na kufungua zipu kisha alitoa kikaratasi na kukisoma kwanza kisha alimpa Edna aliyekipokea alipokitupia jicho moyo ulimpasuka baada ya kukuta ujumbe aliomtumia Shaka upo mikononi mwa shoga yake. Stella aliuona mshtuko wa Edna baada ya kusoma ule ujumbe.
Baada ya ukisoma alitulia wakati huo Shaka tayari aliishagundua nini kimetokea, wakati huo Stella alitembeza macho kwa kila mmoja kumuangalia amepokeaje taarifa ile. Alimuona shoga yake akishusha pumzi nzito kuonesha alishtushwa na ujumbe ule aliomtumia Shaka uliosema: Sasa leo itakuwaje? Si unajua zamu yangu..
“Mpe na Shaka,” Stella alisema kwa sauti ya kistaarabu.
Edna akiwa ametota kama mwanga aliyekamatwa mchana alimpa Shaka kikaratasi kile. Shaka baada ya kukipokea alitulia kusikiliza Stella anataka kusema nini baada ya ushahidi ule.
“Nina imani ujumbe ulioandikwa mmeuona?”
“Ndiyo,” alijibu Shaka, Edna midomo ilikuwa mizito.
“Hebu nielezeni hiki kikaratasi kaandika nani na kilikuwa kinaenda kwa nani?”
Kabla hajapata jibu simu ya Stella iliita alipoangalia ilikuwa inatoka kwa mama yake, alisogea mbali kidogo na kina Edna ili azungumze na mama yake ile ikuwapa nafasi ya kulaumiana.
“Shaka sasa umefanya nini?” Edna alikuwa wa kwanza kuuliza.
“Yaani siamini naona kama mazingaombwe.”
“Mazingaombwe wapi, wakati umefanya makusudi.”
“Nifanye makusudi ili iweje?”
“Ili unigombanishe na Stella.”
“Huwezi kuamini kikaratasi nilikuwa nacho mfukoni nashangaa Stella amekipataje?” Shaka naye alishangaa.
“Ulikaa nacho cha nini, ulishajua kila kitu kwa nini uliendelea kuwa nacho?” Edna aliendelea kumlaumu Shaka.
“Bahati mbaya.”
“Sasa tumelikoroga sijui itakuwaje?”
“Ataamua atakavyo hamtishi mtu,” Shaka alisema kwa kujiamini.
“Kwako hutishiki lakini kwangu msala mzito na wewe ndiye umeniponza,” Edna aliendelea kumlaumu Shaka.
“Umejiponza mwenye bado una mapenzi ya kizamani ya kuandikiana barua ungekuja hata kwa wakati wako si ningekuelewa,” Shaka alijitetea.
“Kwa hiyo umeamua kunikomoa siyo?” Edna alizidi kumlaumu Shaka.
“Edna kuwa muelewa kama ningeamua kukukomoa nisingemdanganya Stella na kukubali mwaliko wako.”
“Sasa tutafanyaje?”
“Wewe ikane hii karatasi kwa nguvu zote, mimi nitaikubali na kumtafuta msichana yeyote kumbambikia lakini kwako nitakuruka.”
“Fanya hivyo la sivyo hali ni tete.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walinyamaza baada ya kumuona Stella amesogea karibu, alipofika alisimama kusubiri kupewa jibu la kuhusu kile kikaratasi. Shaka na Edna walibakia kimya wakimtazama. Stella baada ya kutembeza macho kwa wote aliwauliza:
“Jamani mbona mnageuka mabubu naomba jibu langu?”
“Sasa tukujibu nini?” Shaka aliuliza.
“Hamna jibu siyo?” aliuliza huku amewakazia macho.
“Kwangu sina jibu labda Edna,” Shaka alijifanya kujitoa.
“Eti Edna ujumbe huu ulikuwa unamwandikia nani?”
Edna kabla ya kujibu alikifungua tena kile kikaratasi na kukisoma upya kama kigeni machoni mwake. Baada ya kukirudia zaidi ya mara kumi alinyanyua mdomo wake na kusema:
“Kwa kweli sijui lolote.”
“Huu mwandiko wa nani?”
“Siujui,” Edna aliukana mwandiko wake.
“Eti Shaka kikaratasi hiki kakuandikia nani?” Stella alimgeukia Shaka.
“Mi sikijui,” Shaka alijifanya naye kuruka futi mia sita.
“Sasa mimi nimekitoa wapi?”
“Mi nitajuaje, tukuulize wewe?” Shaka alijifanya kumgeuzia kibao Stella.
“Edna wewe ni shoga yangu mkubwa, nimekufanya kama ndugu yangu katika shida na raha, siamini kama unaweza kunifanya hivi. Siku ile tukiwa break niliokota kikaratasi hiki ambacho sikukitilia maanani, wakati nakwenda darasani mnilimuona Shaka anarudi eneo lile kitu kile kilinishtua sana juu ya kile kikaratasi, lakini niliporudi sikukikuta.
“ Japo nilikuwa na wasiwasi na Shaka bila kuelewa kile kikaratasi kinamaanisha nini, baada ya kukikosa nilipuuza yale mawazo japo sikuwaza kama utakuwa shoga yangu kipenzi. Lakini siku ile nilipokipata kikaratasi hiki kwa Shaka na kukichunguza nilishtuka kuona mwandiko wa Edna moyo uliniuma sana.
“Pia hata uondokaji wenu ambao mwanzo niliona wa kawaida nilipata jibu la hiki kikaratasi kukikuta kwa Shaka na mwandiko wako. Pia hata jioni nilipokuja kwenu kukujulia hali sikukuta na kesho yake ulikuwa hujambo kabisa...Shaka kwa nini unanisaliti?” Stella alimgeukia Shaka.
“Kikaratasi hicho umekitoa wapi?” Shaka alijifanya hakijui.
“Kwako.”
“Umekitoaje?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Shaka wewe si mtoto wa kiniuliza maswali ya chekechea, leo umetoka kunigombanisha na mwalimu Rose kwa ajili ya umalaya wako. Wakati huohuo unanisaliti na shoga yangu kipenzi?” Stella alimjia juu Shaka.
Mara simu ya Edna iliita alipotaka kwenda kupokelea pembeni Stella alimzuia.
“Pokelea hapahapa hutoki bila kunieleza sababu ya kunigeuka, wewe si ndiye uliyekuwa kimbelekimbele cha kutaka mi na Shaka tuachane kwa vile Shaka ni mtoto mdogo kuwa naye nilikuwa najiaibisha?”
“Sawa ngoja basi nipokee dada ananipigia”
”Pokea,” Stella alijibu huku amekunja uso na kumsimamia mbele kama jini la kutumwa.
Edna aliona maji yamefika shingoni baada ya kila kitu kuwa wazi kama vazi la kahaba. Huku kijasho cha kuumbuka kikimtoka alipokea simu ya dada yake
MWISHO
0 comments:
Post a Comment