Chombezo : Aah Shemeji ... Achaaa !
Sehemu Ya Nne (4)
BAADA ya mwaka mmoja kupita. Ilikuwa imebaki takriban miezi mitatu ili Aisha aweze kuhitimu masomo yake lakini haikuwa rahisi kumaliza.
“Haloo!” Ilisikika sauti ya Aisha ikitoka kwa unyonge akimpigia simu shemejiye.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Haloo!Mpenzi mzima wewe?”
“Mimi ni mzima wa afya lakini mwingi wa mawazo.”
“Mwingi wa mawazo ?Mawazo gani tena dear mbona unanishtua?Hebu nieleze.”
“Mimi sizioni siku zangu, hivyo inanipa wasiwasi.”
“Sasa wewe unafikiri ni nini?”
“Ninajihisi kuwa ni mjamzito.”
“Mjamzito, nani kakupa?”
“Heee!Shemeji umeshaanza kunikana mapema yote hii?”
“Hapana dear ila sikutegemea kutokea kitu kama hicho. Basi itabidi Jumapili nikija twende hospitali ili tupate uhakika zaidi.”
“Sawa hakuna shida.”
“Haya dear mchana mwema.”
Baada ya kupata taarifa hizo Bw. Abdul hakuwa na raha tena alikuwa ni mwingi wa mawazo. Aliwaza kuwa ikiwa mkewe atabaini suala hili itakuwaje.
Bw. Abdul alijua wazi kuwa mkewe ni mkali pia ana hasira endapo akijua suala hili huenda hata akamuua mdogo wake. Hivyo alifikiri kuwa waende hospitali ili Aisha akatoe mimba.
Hata hivyo Bw. Abdul alikuwa na mawazo kinzani kwani yapata miaka saba sasa tangu wafunge ndoa na Nasra lakini hawakubarikiwa kupata mtoto. Hivyo kwa upande huu suala la Aisha kutoa mimba hakuona kuwa na maana. Bw. Abdul alisumbuliwa na mawazo hayo usiku na mchana, hakuwa na raha. Hali hii ilimtia wasiwasi mkewe kwani haikuwa kawaida.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nasra hakuweza kulifumbia macho suala hili hivyo alimkabili mumewe na kutaka kujua kinachomsibu lakini Bw. Abdul hakutaka kumweleza ukweli mkewe.
Ilikuwa siku ya Jumapili asubuhi Bw. Abdul aliamka na kujiandaa mapema mithili ya mtu anayewahi kazini. Saa moja kamili Bw. Abdul aliwasha gari na kuelekea Mikocheni katika chuo anachosoma Aisha. Njiani Bw. Abdul hakupisha gari, baiskeli, mkokoteni wala mtu kwani alihisi kuwa anachelewa kufika.
Dakika chache zilipita mara alijikuta yuko getini. Alipiga honi kisha taratibu alishuka ndani ya gari na kulielekea geti lililokuwa mbele yake. Mlinzi alifungua geti na kumsikiliza. Mlinzi alipojua kuwa Bw. Abdul anamhitaji Aisha alikwenda kumwombea ruhusa kwa matroni. Alipewa ruhusa na kuambiwa kuwa asichelewe kurudi. Mlinzi alimwandikia kibali cha kutoka nje ya geti.
Njiani Bw. Abdul alimuuliza Aisha maswali ya hapa na pale lakini Aisha alionekana kuwa na mawazo mengi . Muda mfupi waliwasili katika hospitali moja ya binafsi iliyojulikana kwa juina la Tayma. Walifika mapokezi na kuomba kuonana na daktari. Chumba namba mbili ndicho kilichokuwa cha daktari ambacho aliamuriwa kuingia.
“Habari za kazi daktari,” sauti ya Bw. Abdul alisikika.
“Njema tu za njumbani.”
“Nzuri kiasi nimemleta huyu binti naomba umfanyie vipimo vya UPT(Urine Pregnant Test).”
Daktari alichukua vifaa vilivyohitajika kwa ajili ya kufanyia vipimo. Kisha akampa Aisha chupa ndogo kwa ajili ya kuwekea haja ndogo. Aisha aliipokea ile chupa na kuelekea chooni. Alipofika alikuwa akitetemeka hadi kujihisi kama hakuwa na haja ndogo. Alijitahidi kujikamua hatimaye alipata ingawa ni kiasi kidogo sana.
“Nimepata kidogo sana daktari.”
“Kinatosha hiko, kipimo hiki hakihitaji kiasi kingi, haya weka juu ya meza kisha kasubiri hapo nje kwenye benchi.
Aisha alifanya kama alivyoagizwa kisha alitoka nje. Muda kidogo kupita daktari aliwaita.
“Majibu yenu yapo tayari sijui mupo tayari nikupatieni.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Twambie tu daktari.”
“Majibu yanaonyesha ‘ positive.’
“Heeeee!”
“Vipimo ndiyo vinaonyesha hivyo mzee siyo mimi.” Kaeni hapo nje kidogo mpumzike kisha kama kuna la zaidi mtaingia tena baadaye.”
Pale nje walishauriana mambo mbalimbali ingawa Aisha alikuwa akibubujikwa na machozi.Bw. Abdul alimwahidi Aisha kumlinda na kumtunza mpaka atakapojifungua bila ya dada yake kujua. Pia alimwahidi kuwa atampangia nyumba.
Waliingia ndani kwa daktari na kumuaga kisha wakaingia ndani ya gari na kuelekea kwenye fukwe moja ya bahari ili kupoteza mawazo. Huko walistarehe na kusahau kabisa matatizo yanayowakabili. Walikimbizana wakacheza na kufurahi kama watoto wadogo.
Bw. Abdul alipoangalia saa aligundua kuwa ni saa kumi na mbili jioni wakati muda wa mwisho kwa wanafunzi kurudi chuoni ni saa kumi jioni. Hivyo Bw. Abdul aliagana na Aisha kisha walielekea mahali walipoegesha gari na kuingia kwa haraka. Bw. Abdul aliwasha gari na kuendesha kwa mwendo wa kasi. Wakati wakiwa njiani Aisha alijikuta akiwa na mawazo upya na kuanza kulia, alisahau raha zote alizozipata kule ufukweni. Machozi yalimtiririka lakini Bw. Abdul hakwisha kumbembeleza. Walifika getini majira ya saa moja hivi lakini mlinzi alikataa kumruhusu Aisha kuingia ndani Bw. Abdul alimbembeleza na kumpa kitu kidogo.
Mlinzi hakuendelea tena kugoma kwa kuwa ameshapewa hela ya chai. Alimruhusu kuingia ndani ya geti kisha wakaagana na Bw. Abdul.
*****
Ilikuwa siku ya Jumatatu asubuhi ambapo mwalimu mmoja alimwona Aisha akitapika katika viunga vya chuo ndipo alipomwita na kumuuliza kama alikuwa amaumwa. Aisha alimwambia kuwa anasumbuliwa na malaria lakini ameshapata dawa.
Kwa kuwa mwalimu yule alikuwa wa kike tayari alishagundua kinachomsumbua Aisha. Siku iliyofuatia mwalimu aliwaita walimu wenzake na kuwaeleza aliyoyafahamu juu ya Aisha. Walimu walikubaliana wamwite Aisha kisha wampime ili kujua kama ni mjamzito.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya masomo walimu walimwita Aisha na kumuuliza kama alikuwa ni mgonjwa. Aisha alijibu kama alivyomjibu mwalimu wa kwanza kuwa yeye alikuwa akisumbuliwa na malaria. Walimu walichukua chupa na kumpa ili akaweke haja ndogo kama alivyofanya kwa daktari. Aisha alishtuka kwa kuwa alijua wazi kuwa mambo yote yatakuwa hadharani. Alitoka nje kuelekea chooni ndipo alipomwona Suzan, alimwita kwa kumkonyeza.
Suzan hakusita kwenda .
“ Vipi shost mbona huku saa hizi kulikoni?”
“Shost yaliyonikuta ni mazito lakini ngoja nikueleze kwa kuwa wewe ni rafiki yangu.”
“Mmmm! Mbona wanitisha shost.”
“Shost mimi ni mjamzito lakini nimepanga kuficha nisijulikane kwa kuwa umebaki muda mchache tumalize masomo lakini walimu si ndo’ wamenigundua wamenipa chupa hii niwapatie haja ndogo ili wanifanyie vipimo. Hata hivyo naona Mungu yu pamoja nami ndiyo maana amenikutanisha na wewe sasa.”
“Mmm! Shost hayo ni makubwa.”
‘Ni makubwa ndiyo lakini kumbuka kuwa na mimi si mtoto mdogo pia ni mjanja kuliko wao waliojifanya wamenikamata.”
“Sasa sikiliza naomba unipatie wewe haja yako ili niwapelekee.”
“Poa haina shida.”
Suzan alichukua ile chupa na kuelekea chooni. Baada ya dakika mbili hivi alitoka na kumkabidhi Aisha ile chupa. Huku ofisini walimu walimsubiri Aisha kwa muda mrefu bila ya kutokea ndipo mwalimu mmoja alipoamua kwenda kumfuatilia. Kabla hajafika mbali alikutana na Aisha akiwa anarudi huku ameshika chupa mkononi.
“Mbona umechelewa hivyo?”
Nimechelewa kupata haja.”
“Haya peleka .”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aisha alipeleka akiwa na matumaini kuwa amewakomoa kwani hawatagundua kuwa ni mjamzito. Suzan alikubali kufanyahivyo kwakuwaalijiamini kuwa hawezi kuwamjamzito kwani ni siku moja t undo amewahi kufanya mapenzi. Baada ya kufanya vipimo majibu yalionyesha kuwa ni mjamzito. Aisha hakuamini kabisa lakini hakuwa na la kufanya, alifikiri kuwa ni bora angemwomba mtu mwingine kumpatia haja kuliko Suzan. Aisha aliandikiwa barua ya kufukuzwa chuo.
Aisha alimweleza Suzan juu ya majibu yake pamoja na barua ya kufukuzwa chuo. Suzan alishikwa na butwaa hakuamini kama naye ni mjamzito.
“Aisha tafadhari nakuomba unifichiesiri yangu iliwalimu wasigundue kuwanami ni mjamzito.”
“Siwezi kukuchomea utambi shost, kuwa na amani.”
Aisha alimpigia simu shemejiye akamweleza kisha kumtaka aende akamchukue. Bw. Abdul aliingiwa na woga aliwaza kuwa pengine watu wote walishagundua uhusiano wake na Aisha hivyo alimtaka Aisha achukue teksi na kuelekea mahali ambapo yeye atakuwepo.
Aisha baada kupaki mizigo yake yote alifanya kama alivyoagizwa. Muda mchache Aisha alifika pale na kukuta Bw. Abdul amepaki gari lake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment