Chombezo : Timbwili .... Timbwili
Sehemu Ya Nne (4)
NYUMBA ya nne kutoka kwenye saluni aliyoingia Mwajuma kulikuwa na kijigrosari. Baadhi ya wateja waliketi ndani, baadhi waliketi nje. Saad naye aliamua kuketi nje ili aweze kumwona Mwajuma pindi atakapotoka saluni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akaagiza soda na kuinywa taratibu, macho yake yakitalii kwa wateja wengine. Mara macho yakatua katika meza moja iliyokuwa na watu wawili. Watu hao nao wakamtazama. Wakatabasamu.
Saad akasimama na kuwafuata. Wakaunganika katika meza hiyo. Wakasalimiana na kuongea hili na lile huku vinywaji vikiendelea kunyweka.
Wale watu wawili ambao Saad aliwakuta, walikuwa ni mwanamume na mwanamke; Salum na Hadija. Wao walikuwa wakinywa bia. Katikati ya maongezi yao, Hadija aliuliza, “Vipi shem, mama Sauda ameshaanza
yale mafunzo ya ushonaji nguo?”
Mama Sauda ndiye Halima, aliyekuwa mkewe Saad.
Saad alifikiri kidogo kisha akajibu, “Kwa kweli, sijui.”
“Hujui?” Hadija aliuliza kwa mshangao.
“Ndiyo, sijui na wala sitaki kujua,” sauti ya Saad ilibainisha kuwa hakupendelea kuongea chochote kuhusu Halima.
Hata hivyo Hadija hakukoma. Aliendelea kudadisi, “Kwani imekuwaje?”
“Tumeachana!”
“Mmeachana?!” macho ya mshangao yalizidi kumtoka Hadija.
“Nd'o maana'ake.”
“Nilipata fununu kuhusu hilo,” Salum alichangia kwa sauti ya unyonge. Akaongeza, “Hata hivyo siwezi kukulaumu kwa hatua uliyochukua. Mama Sauda hajatulia. Inashangaza ulichelewa kuzijua nyendo zake, labda ungekwishamtema siku nyingi.”
“Ndilo kosa nililofanya,” Saad alikiri. “Tatizo langu nilitokea kumwamini sana. Hivyo sikuwa nazifuatilia nyendo zake hata kidogo. Yalikuwa ni makosa makubwa sana.”
Hadija alimtazama kwa macho ya huruma. Akatikisa kichwa, kisha akasema, “Saad, ni kweli lilikuwa ni kosa kubwa kumwamini Mama Sauda, lakini mimi naona kuwa ulifanya kosa kubwa zaidi kumwacha Mwajuma.
“Maskini Mwajuma! Nikikumbuka natamani hata kulia kwa kumhurumia. Mwajuma siyo tu kwamba alikupenda bali alikutukuza. Mtu hukai naye dakika mbili, kishakutaja. Kinywa chake kilijaa jina lako. Saad...Saad...! He! Yaani mwanamke alikupenda yule! Na ulipomtema hakuamini! Wiki nzima alishinda ndani; kula hali, na akila basi ni kidogo sana. Muda wote macho yalimwiva kwa ajili ya kulia. Mwajuma alikonda!”
Ukimya ukapita kwa sekunde kadhaa. Hatimaye Salum akauvunja kwa kuuliza, “Kwani Mwajuma mwenyewe yuko wapi siku hizi? Siku nyingi sijamwona. Au kishaolewa?”
“Yupo,” Hadija alijibu. “Siku hizi haonekani ovyoovyo. Akitoka kazini tu, nyumbani. Hatoki tena. Alimfuma mzee mmoja limbukeni, akampangia chumba Mwenbechai hii hii! Kamlipia kodi ya miaka mitatu mbele, na kamjazia mifenicha kibao ndani mwake. Mifenicha ya nguvu! Nakwambia ukifika kwa Mwajuma, utakubali mwenyewe.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Saad aliguna. Kwa mbali alionekana kusinyaa usoni. Akauliza, “Huyo mzee mwenyewe ni nani?”
“Nani anamjua?” Salum naye alimdaka kwa swali. Akacheka na kuongeza, “We' kaa tu ukijua kuwa kama unataka kumrudia Mwajuma, basi tayari una mpinzani kizito. Sasa Mwajuma ni maji marefu.”
Maneno hayo yalimfanya Hadija ahisi kuwa yatamchanganya zaidi Saad. Yatamfadhaisha. Hivyo akaamua kumtia moyo, afarijike.
Akamtazama kidogo Salum kisha akayarejesha kwa Saad.
“Aah, wapi! Samwel si mpinzani wa maana,” alisema kwa madaha na mikogo, akivikunja na kuvikunjua vidole vya mikono huku akiubinuabinua mdomo katika hali ya mtu asikiaye kinyaa.
Akaendelea, “Kwa yule mzee Samwel, Mwajuma ni demu wa pembeni tu, wala hata siyo nyumba ndogo kwake. Na kwa bahati mbaya Mwajuma ni Mwislamu, Samwel ni Mkristo. Mkristo haruhusiwi kuwa na wake wawili na kuendelea. Ni mke mmoja tu, na hakuna cha kupeana talaka. Ni kifo ndicho kinawatenganisha. Kwa hiyo haiwezekani Samwel akamwoa Mwajuma.”
Kwa mara nyingine ukimya ukajijengea himaya katika meza hiyo. Hadija akamtazama Saad na kumwona kama aliye mbali kimawazo.
“Vipi Saad, mbona kama vile hatuko pamoja? Umemkumbuka Mwajuma, nini?” Hadija alimuuliza.
Saad hakujibu, badala yake aliachia tabasamu hafifu na kuyatupia macho kwenye chupa yake yenye ujazo mdogo wa soda. Akaishika na kuipeleka kinywani ambako aligugumia mafunda kadhaa na kuirudisha mezani.
Alijitahidi kutowatazama Hadija na Salum lakini nafsi ilimkatalia. Alikuwa akisubiriwa kujibu swali aliloulizwa. Akauinua uso na kumtazama Hadija. Naam, alitaka asimithilishwe na mwanamke mshamba aogopaye macho ya mwanamume amtongozaye. Tabasamu likaendelea kuchanua usoni pake.
“Sema, Saad,” Hadija alimdaka. “Yaonekana Hadija bado yuko akilini mwako kwa sana, eti?”
“Ni kweli,” Saad alijibu. “Bado kabisa nampenda Mwajuma. Kinachonisikitisha ni kusikia kuwa ana mtu...”
“Us'konde,” Hadija alimkata kauli. “Ni'shakwambia huyo mzee s'o mtu permanent. Yupo yupo tu. We' sema, kama kweli unamtaka, niongee naye.”
“Namtaka kikweli-kweli,” Saad alisisitiza. “Hata leo...”
“Kwa leo itakuwa ngumu,” Hadija alimkata kauli. “Kwa vyovyote saa hizi atakuwa nyumbani kwake, mzee Samwel kamlalia mapajani.”
Saad aliachia kicheko. “Hayuko kwake, yuko jirani tu kutoka hapa.”
“Nini?” Hadija alimkazia macho.
“Yuko saluni ile pale,” Saad alisema akionyesha kwa kidole.
“We Saad, unaota?” Hadija hakuamini.
“Wala sioti. Nikwambiayo nd'o ukweli wenyewe.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kha! Kumbe mambo shwari!”
“Bado. Bado kabisa. Nimekutana naye leo kibahati-bahati tu, nikajipendekeza kwake, na kwa kuwa alikuwa na safari ya kuja hapo saluni nd'o nikalazimika kuandamana naye ili labda aniruhusu kujieleza.”
“Lakini tayari huo ni mwanzo mzuri, Saad,” Hadija alisema. “Kwa hiyo mmekubaliana umsubiri hapa?”
“Siyo hapa. Kasema tu nimsubiri mahala f'lani. Kama unavyojua, isingewezekana mimi mwanamume kukaa mle saluni.”
“Ok,” Hadija alitikisa kichwa akiashiria kuafiki. Kisha akaongeza, “N'na hamu ya kuonana naye, sema tu kwa kuwa sie tuna safari kidogo.”
“Ya wapi tena?”
“Harusini. Jirani yetu anafunga ndoa leo. Sherehe iko Travertine Hotel.”
“I see.”
Hadija na Salum wakaagiza tena bia moja, moja. Saad naye akaongeza soda moja. Mazungumzo yakaendelea, vicheko na mizaha vikitawala.
**********
MWAJUMA alipotoka saluni alikuwa kapendeza maradufu. Akatembea kidogo kisha akasita. Akaangaza macho huku na kule akimtafuta Saad. Akawaza, laiti angelikuwa na namba ya simu yake angempigia ili ajue yuko wapi.
Lakini mara wazo moja likamjia. Alitambua fika kuwa Saad ni mpenzi wa bia. Nyumba ya nne kutoka hapo kulikuwa na watu wengi walioketi nje. Chupa za vinywaji mbalimbali zilionekana juu ya meza zilizokuwa nje ya nyumba hiyo. Mwajuma hakuhitaji kuchukua dakika hata moja kubaini pale kulifanyika nini. Hisia zake zikalenga kuwa huenda na Saad atakuwa hapo. Akalisogelea eneo hilo.
Ni Hadija aliyetangulia kumwona. Kwa furaha akapaza sauti akiita, “Mwajuma! Mwajuma! Tuko hapa!”
Mwajuma alishtuka, akageukia ilikotoka sauti hiyo. Akamwona Hadija akiwa na Saad na Salum. Akawafuata. Mara Hadija akanyanyuka, wakakumbatiana. Salamu kwa huyu na yule zikatwaa nafasi kwa muda, sanjari na kuulizana habari za siku nyingi.
Hatimaye Mwajuma alimkazia macho Saad. “Leo imekuwaje, Saad?”
“Kwa vipi?”
“Leo umekuwa mtu wa kunywa soda?”
“Mara mojamoja.”
“Au mwenzetu nd'o u'shaokoka?”
Wakacheka.
“Muda bado,” hatimaye Saad alisema. “Siku hizi nimejiwekea nadhiri, sinywi bia kabla ya saa kumi na mbili jioni.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwajuma aliketi, kinywaji chake naye hakikutofautiana na vinywaji vya Hadija na Salum. Meza ikazidi kuchangamka, maongezi yakanoga. Hatimaye kijigiza kikaanza kuitawala anga.
Hadija akaitazama saa na kusema, “Moja na nusu. Sasa huu ni muda mwafaka.”
“Muda wa?” Mwajuma aliuliza.
“Wa kwenda harusini. Kwani hujui kuwa Ahmad anaoa?”
“Haa! Ni'shasahau. Lakini tangu jana ni'shapanga n'ende. Sasa leo nimekutana na huyu jamaa, kumbukumbu yote ikafutika.”
Kwa mara nyingine vicheko vikatawala vinywani mwa Hadija na Mwajuma, vicheko vya 'kishangingi-shangingi.'
“Kwa hiyo inakuwaje?” Hadija akamuuliza.
“Tungekwenda wote lakini...” Mwajuma alisita na kumkodolea macho Saad.
Hadija alielewa. Akamwahi, “Twendeni wote. Mimi na Salum, wewe na Saad. Au vipi, Saad?”
“Itakuwa ngumu,” Saad alijibu. “Sikualikwa, isitoshe sijavaa rasmi.”
“Acha hizo, Saad,” Salum alimdaka. “Kuvaa rasmi! Nani kati yetu kavaa rasmi? Sisi watoto wa town, bwana, nani asiyetujua?”
“Afu tena, sisi s'o watu wa kualikwa,” Hadija aliongeza. “Bwana harusi alishasema kuwa majirani wote ruksa kuingia. Tuwe na kadi, tusiwe nazo. Mimi na Salum tutaingia kama Mr. na Mrs. Na wewe na Mwajuma, hivyohivyo. Au?”
“Nd'o maana'ake,” Mwajuma alisema.
Saad hakuwa na nguvu ya kupambana na hoja hizo. Alimhitaji Mwajuma na Mwajuma mwenyewe anataka waende wote huko kwenye sherehe. Angekataa?
Robo saa baadaye walikuwa ndani ya teksi wakielekea Travertine Hotel.
KWA mara nyingine vicheko vikatawala vinywani mwa Hadija na Mwajuma, vicheko vya 'kishangingi-shangingi.'
“Kwa hiyo inakuwaje?” Hadija akamuuliza.
“Tungekwenda wote lakini...” Mwajuma alisita na kumkodolea macho Saad.
Hadija alielewa. Akamwahi, “Twendeni wote. Mimi na Salum, wewe na Saad. Au vipi, Saad?”
“Itakuwa ngumu,” Saad alijibu. “Sikualikwa, isitoshe sijavaa rasmi.”
“Acha hizo, Saad,” Salum alimdaka. “Kuvaa rasmi! Nani kati yetu kavaa rasmi? Sisi watoto wa town, bwana, nani asiyetujua?”
“Afu tena, sisi s'o watu wa kualikwa,” Hadija aliongeza. “Bwana harusi alishasema kuwa majirani wote ruksa kuingia. Tuwe na kadi, tusiwe nazo. Mimi na Salum tutaingia kama Mr. na Mrs. Na wewe na Mwajuma, hivyohivyo. Au?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nd'o maana'ake,” Mwajuma alisema.
Saad hakuwa na nguvu ya kupambana na hoja hizo. Alimhitaji Mwajuma na Mwajuma mwenyewe anataka waende wote huko kwenye sherehe. Angekataa?
Robo saa baadaye walikuwa ndani ya teksi wakielekea Travertine Hotel.
**********
SHEREHE ya harusi ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel, ilianza saa 12 jioni. Ilihudhuriwa na watu wengi, na wengi wao walikuwa ni wenye kujiweza kifedha. Muziki laini ulianza kutumbuiza ilipotimu saa 1.00.
Kama walivyotegemea, Salum, Hadija, Mwajuma na Saad walipofika getini walimkuta mtu aliyewafahamu.
“Karibuni,” walikaribishwa kwa heshima.
Wakaingia, Hadija kashikwa mkono na Salum hali kadhalika, Mwajuma na Saad. Huko ndani vinywaji vilisambazwa kwa kila mmoja. Hadija na wenzake walipopata viti walikaa na kuletewa vinywaji. Sasa Saad hakunywa soda, alichukua bia.
Mambo yalizidi kushamiri ukumbini humo. Watu walikunywa, watu walikula. Kwa ujumla ilikuwa ni sherehe iliyoonyesha bayana kuwa iliandaliwa, ikaandalika.
Kadri muda ulivyokwenda ndivyo ukumbi ulivyozidi kuchangamka. Ilipotimu saa 3:00 mshereheshaji alitangaza kwenye kipaza sauti: “Naam, waheshimiwa wazazi wa bwana na bibi harusi, sasa nd'o mambo yananoga. Ndugu maharusi, nadhani mko tayari kukesha, siyo? Na waalikwa wote mko tayari kukesha, eti?”
Vifijo, vigelegele na mayowe vikatanda hewani. Baadhi ya watu wakabwata, “Tunakesha...! Tunakesha...!”
“Asanteni,” mshereheshaji aliwapoza. “Asanteni sana. Sasa tunataka kila mtu afurahi. Kila mtu acheke, kila mtu alie kwa furaha, kila mtu aifurahie bia yake, na walaji wa nyama wazifaidi nyama zao. Na kuna wale ambao hawali nyama wala kunywa bia...”
Vicheko vikatanda ukumbini.
“Hao,” aliendelea, “hao tunaamini wana maradhi yao. Muziki. Tena kama si Rusha Roho basi ni Mduara.”
Sasa kelele za wanawake zikatanda ukumbini. Hawakuwa wakizomea, bali walishangilia na baadhi yao wakiropoka katika kusisitiza uharakishwaji wa muziki huo.
“Haya, Dj weka vitu!” hatimaye mshereheshaji aliamua kukata mzizi wa fitina.
Muziki ulianza kurindima. Dj aliweka kanda ya muziki wa miondoko ya Mduara. Watu wakajimwaga ukumbini.
“Tengeneza mduara...tengeneza mduara...mduara jamani...mduara...” mshereheshaji alibwata huku akizunguka huku na kule.
Wachezaji walimtii. Wakatengeneza duara, wakicheza taratibu, lakini katika hali ya kuyavutia macho ya watazamaji walioketi.
“Tukacheze,” Mwajuma alimwambia Saad.
“Kacheze wewe, mimi bado n'na kiu,” Saad alisema.
Wakatazamana, macho yao yakizungumza mapenzi yaliyo dhahiri kwa kila mmoja. Kila mmoja wao akatabasamu kidogo.
Saad alikuwa na sababu ya kukataa kutii ombi la Mwajuma. Aibu! Pamoja na utanashati wake, pamoja na elimu yake, na pamoja na ulimi wake kuwa mwepesi katika kuzungumza maneno yasiyowakwaza wasikilizaji, uchangamfu ukiwa umemtawala, bado alikuwa na kilo nyingi za soni moyoni mwake.
Miongoni mwa mambo yaliyomfanya ajisikie kujawa na aibu, ni kucheza muziki na mwanamke. Aliwapenda wanawake kwa kuwa tu walikuwa msitari wa mbele katika kujiremba. Katika kila wanawake kumi aliokutana nao, tisa au wanane walipendeza. Lakini siyo kwamba aliwatamani. La hasha. Alimtamani yule tu aliye naye karibu kwa uhusiano wa kimapenzi.
Huyu Mwajuma aliachana naye miaka miwili na miezi kadhaa iliyopita. Alikuwa na haki ya kumchukulia kuwa sasa Mwajuma ni 'mtu mpya,' mgeni machoni na mwilini mwake. Hivyo, hata pendekezo la kumtaka wakajiunge na 'mduara' katikati ya ukumbi lilikuwa ni gumu kutekelezeka.
Mwajuma hakukubali. Wengi wa waliokwenda kuutengeneza mduara walikuwa katika seti mbili, mwanamume na mwanamke, na hao walikuwa ni wale wenye uhusiano wa ndani zaidi kimapenzi. Yeye angekwenda peke yake?
Hakukubali. Akamtazama zaidi Saad na kumuuliza, “Unaogopa?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hataa. Niogope nini?”
“Sijui. Nakushangaa eti unadai una kiu. Kwa nini hukunywa bia kule Mwembechai?”
“Sababu ya kutokunywa kule Mwembechai nilishaisema tukiwa kulekule. Umesahau?”
Mwajuma hakujibu. Akaendelea kuwaangalia wachezaji. Kisha kwa unyonge alisema, “Haya, hebu cheki, wenzetu wa'shajiunga na mduara. Twende basi.”
Saad aliipeleka chupa kinywani. Akaigugumia bia kama maji. Alipoitua chini ilikuwa tupu. Akamtazama Mwajuma kama aulizaye swali.
“Kunywa, tutakunywa,” Mwajuma alisema huku akimshika mkono. “Twende tukacheze kwanza.”
Saad alilazimika kutii. Akanyanyuka na kumfuata Mwajuma kama kondoo.
Wakajimwaga katikati ya ukumbi.
**********
MUZIKI ulishakolea. Wachezaji mahiri na waliojituma walikuwa ni wanawake. Hao walicheza, wakacheza, wakizungusha viuno vyao kwa namna iliyowastaajabisha wageni wa fani hiyo. Mwanamke mmoja wa fani hiyo alipagawishwa na mdundo huo, akajitoa kwenye msitari, akaingia katikati. Hapo sasa akaamua kufanya yale aliyohitaji kuyafanya.
Awali alicheza wima, kisha akalala kifudifudi, mara kiubavu-ubavu, chali na kadhalika na kadhalika. Watu walicheka, wengine walishangilia huku wakimtuza pesa.
Saad na Mwajuma walikuwa wakikaribia kujiunga na mduara huo lakini mara Mwajuma alisita, akasema, “Tucheze hapahapa.”
Kama awali, Saad hakuwa na nguvu ya kupinga kauli ya Mwajuma. Akasimama na kuanza kucheza, uchanga wake katika taaluma ya uchezaji muziki ukiwa bayana machoni mwa Mwajuma hata kwa watazamaji wengine.
Katika kumlindia hadhi, Mwajuma aliamua kumkumbatia. Wakawa wakicheza taratibu. Lakini ni katika cheza yao hiyo ndipo Mwajuma alipogundua kuwa Saad hakuziweka fikra zake katika muziki huo. Kumbatia yake, papasapapasa yake na mengineyo ambayo Mwajuma aliyatarajia zilikuwa ni taswira halisi kuwa Saad alikuwa 'mhitaji' na alihitaji utekelezaji wa haraka.
Alichofanya Mwajuma ni kumvumilia kwa dakika chache kisha akamwambia, “Basi. Basi, tukakae. Tukanywe bia zetu.”
“Bado,” sauti ya mkwaruzo ilimtoka Saad, mikono yake ikiendelea kumng'ang'ania Mwajuma kiunoni.
“Inatosha, bwana,” Mwajuma alisisitiza huku akijing'atua na kurudi kitini.
Wakaendelea kunywa, wakanywa hadi wote 'wakachangamka.' Mara kwa mara Mwajuma hakuona haya kuitumia mikono yake kutalii maungoni mwa Saad kwa namna iliyowashangaza waliokuwa jirani nao.
Mara muziki ukakatika. Mduara wa wachezaji ukavunjika. Hadija na Salum wakarudi mezani hapo na kuwakuta wenzao wakiwa katika hali ambayo kwa yeyote mwenye akili timamu lazima angejenga imani kuwa Saad na Mwajuma ni wapenzi wakubwa.
“Twen'zetu,” Mwajuma alimnong'oneza Saad. “Twen'zetu kwangu tukafurahi. Leo nd'o siku yetu. Nani kama sisi?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“No! Tusubiri ukataji wa keki,” Saad alisema.
“Keki! Keki ya nini kwetu?” Mwajuma alimaka. “Kwani tukishuhudia ukataji keki nd'o itatusaidia nini, au tutafaidika na nini? Bwana'ee, twen'zetu. Kwanza mimi niko chini ya himaya ya mtu. Hilo unalijua!”
Saad hakujibu.
Dakika chache baadaye walikuwa wakilifuata gati kubwa la hoteli hiyo. Walipofika nje wakakodi teksi.
“Kigogo,” Saad alimwambia dereva huku akiingia ndani ya teksi hiyo.
“Kigogo ipi?”
“We twende tutakuelekeza huko mbele ya safari. Tuna haraka, sema bei yako.”
“Ni mpaka tutakapofika. Lakini siyo zaidi ya kumi, na haipungui tano.”
“Okay, twende.”
***********
SAA 6:15 usiku iliwakuta Mwajuma na Saad wakiwa kitandani, chumbani mwa Saad, ikiwa ni zaidi ya saa nzima tangu walipoingia. Mwajuma alikuwa kamlalia Saad kifuani, wakinong'ona maneno ya mahaba.
Mara Mwajuma akaitazama saa yake ya mkononi. Akaguna. “Saa sita!” hatimaye alisema na kuongeza, “Muda umekwenda, Saad. Inanipasa niondoke sasa.”
“Acha hizo, mpenzi,” Saad alisema huku akimpapasa mapaja. “Wasiwasi wa nini? Kwani lazima uende usiku huu?”
“Ndiyo! Ile nyumba haiko kwenye mazingira mazuri kwa mtu kuamua kulala nje. Chumba changu ni cha nje, wezi wanaweza kunifanyizia.”
Saad alitaka kutamka neno akasita. Mwajuma alinyanyuka haraka. Akavinyoosha viungo kwa uchovu. Naam, alihisi uchovu mwilini, na alikuwa na sababu ya kuwa na uchovu. Tangu walipoingia humo ndani, nguo zikawa ni kero tupu miilini mwao. Wakazivua.
Kilichofuata ni kile walichokihitaji, na walihakikisha wanazikonga nyoyo zao kwa pumzi zao, wakivitumia viungo vyao kwa namna iliyowapa burdani isiyoelezeka kwa vinywa vya kawaida. Lakini sasa Mwajuma alihitaji kurudi kwake. Akaharakisha kukusanya nguo zake avae.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment