Chombezo : Tattoo
Sehemu Ya Nne (4)
ILIPOISHIA
Siku ziliendelea kukatika, Annabel alizidi kumpenda zaidi mtu ambaye wala hakuwa na mapenzi yoyote yale moyoni mwake juu yake. Huku moyo wake ukiendelea kujilazimisha kumpenda Annabel, hapo ndipo alipompata msichana aliyeona kwamba alistahili kuwa mpenzi wake, huyu alikuwa Pamela.
SASA ENDELEA...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Annabel hakujua kitu chochote kile, hakujua kama mtu ambaye alikuwa akimpenda kwa mapenzi ya dhati alikuwa katika mapenzi na msichana mwingine. Kila siku alijitahidi kumuoneshea Jonathan mapenzi ya dhati lakini mvulana huyo hakuwa na shida naye.
Tattoo yenye jina la Jonathan aliyojichora kifuani mwake ilikuwa ni alama moja muhimu ya kumuoneshea mvulana huyo kwamba alikuwa akimpenda kupita kawaida. Wavulana waliokuwa wakimtaka Annabel kimapenzi hawakuwa na nafasi tena, msichana huyo mrembo tayari alikuwa amechukuliwa na mvulana mwingine.
Annabel hakusitisha malezi yake kwa Jonathan, kila siku alikuwa akiendelea kumhudumia lakini akili ya mvulana huyo haikuwa kwake kabisa. Bado Jonathan aliendelea kumtumia msichana huyo kama chemchemi yake ya kuchota fedha kitu ambacho alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
Siku ya kwanza ambayo Jonathan alimwambia Pamela kwamba alikuwa akimpenda, msichana huyo mwenye shepu kubwa na macho yaliyolegea hakuwa na kipingamizi japokuwa alifahamu fika kwamba mvulana huyo alikuwa katika uhusiano na msichana kutoka katika shule ya wasichana ya Kisutu, Annabel.
“Simtaki, si mzuri kama wewe,” alisema Jonathan, muda huo alikuwa na Pamela huku akijaribu kurusha ndoano yake.
“Acha kunitania Jonathan, Annabel utamfananisha na kinyago mimi?” aliuliza Pamela huku akitoa tabasamu pana lililoendelea kummaliza Jonathan.
“Nani Kinyago? Wewe? Hapana, u mrembo mno na si kama yeye. Hebu mwangalie Annabel halafu jiangalie na wewe, hakufikii hata robo,” alisema Jonathan.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Maneno yaliyojaa sifa ambayo alikuwa akiambiwa yakaonekana kumfurahisha Pamela, kila alipokuwa akijiangalia, kweli alijijengea sifa na kujiona kuwa msichana mrembo zaidi ya alivyokuwa Annabel.
Hakuwa na pingamizi, sifa zile alizopewa zikamfanya kumpenda Jonathan kwa kuona kwamba kila siku angeendelea kuzisikia masikioni mwake kutoka kwa mvulana huyo.
Mahusiano ya siri baina ya watu hao yakaanza rasmi, hiyo ikawa furaha kwa Jonathan ambaye kila alipokuwa akimwangalia Pamela, alionekana msichana mrembo asiyekuwa na dosari hata kidogo.
Kwa sababu moyo wake ulikuwa umekwishajiwekea kwamba alikuwa akitaka kumlia Annabel fedha ake tu, hakumuonyesha mabadiliko yoyote yale, alijifanya anampenda huku moyoni mwake akimzomea.
Moyo ulitunza siri ambayo kamwe Annabel hakuwa akiifahamu kabisa. Kila alipokuwa akibusiwa, alijihisi kuwa katika ulimwengu mwingine kabisa wenye raha ambao ulimfanya kusisimka. Hakujua kwamba kila kitu kilichokuwa kikitokea kilikuwa unafiki mkubwa.
“Unanipenda?” aliuliza Annabel huku akimwangalia Jonathan usoni.
“Ninakupenda malaika wangu, ninakufananisha na ua zuri litoalo harufu nzuri na yenye kunukia huku mimi nikiwa nyuki mwenye uchu wa kukufuata kwa ajili ya kuchukua vitu muhimu kwa ajili ya kutengeneza asali yangu,” alisema Jonathan.
“Nakupenda pia mpenzi,” alisema Annabel.
“Huwa ninajiuliza, umeumbwa wakati gani, ni mchana au usiku? Kama ni mchana, natumaini Mungu aliacha kazi zake zote kwa ajili ya kukuumba wewe, na kama alikuumba usiku, natumaini alikesha kwa ajili yako tu,” Jonathan alisema maneno yaliyomfanya Annabel kujisikia vizuri, hakujua kama Jonathan alikuwa muigizaji mzuri zaidi ya JB.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Huwa ninajiuliza, umeumbwa wakati gani, ni mchana au usiku? Kama ni mchana, natumaini Mungu aliacha kazi zake zote kwa ajili ya kukuumba wewe na kama alikuumba usiku, natumaini alikesha kwa ajili ya kukuumba wewe tu”
Jonathan alisema maneno yaliyomfanya Annabel kujisikia vizuri, hakujua kama Jonathan alikuwa muigizaji mzuri zaidi ya JB.
Mapenzi yalimsumbua Annabel, kila wakati akawa mtu wa mawazo tu, mapenzi ambayo alimpa Jonathan yalikuwa ni ya juu ambayo aliamini kwamba yangeendelea kumpagawisha mvulana huyo.
Jonathan hakuwa na muda, mapenzi yote aliyokuwa akionyeshewa na Annabel yalionekana si kitu, msichana ambaye alikuwa akimpenda kwa wakati huo alikuwa Pamela tu.
Kila siku ilikuwa ni lazima akae na Pamela na kupiga naye stori, kila alipokuwa akimwangalia msichana huyo, alichanganyikiwa, alimuona kama malaika kwani uzuri wake mbele ya macho yake ulikuwa hauna mfano.
Kila kitu kilichoendelea kilikuwa siri kubwa, hakutaka Annabel apate taarifa juu ya kile kilichokuwa kikiendelea. Msichana huyo bado alikuwa mtaji, kila alipokuwa na tatizo lililohitaji fedha, alikuwa akilimaliza kwa haraka sana.
Alipendwa lakini upendo aliopewa aliuona hauna thamani kabisa. Annabel alikuwa kama chizi, kila siku ilikuwa ni lazima kuwasiliana na Jonathan ambaye kwa kumsikiliza tu, usingeweza kujua kama hakuwa na mapenzi ya dhati kwa msichana huyo.
“Hivi siwezi kumwambia aachane na mimi?” alijiuliza Jonathan.
Hakutaka kumuacha Annabel kwani aliamini kwamba kitendo cha kumuacha msichana huyo kingemfanya kukosa kila kitu alichokuwa amekitegemea kabla, hivyo alitakiwa kuendelea kumuoneshea unafiki.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kila alipokuwa akiulizwa kuhusu Pamela, Jonathan alikuwa akificha, hakutaka kuweka wazi kwa wanafunzi wenzake kwani alijua kwamba endapo angewaambia ukweli basi taarifa zingeweza kumfikia Annabel na hivyo kukosa kila kitu.
“Nataka tutoke mtoko wa usiku,” alisema Annabel huku akiwa kifuani mwa Jonathan chumbani mwa mvulana huyo.
“Lini?”
“Leo usiku. Ninatamani sana kuwa karibu nawe,” alisema Annabel kwa sauti ya chini iliyokuwa nyororo kwa kuamini kwamba ingeweza kumsisimua Jonathan.
“Sawa, hakuna tatizo,” alisema Jonathan.
Siku hiyo, Annabel hakutaka kulala nyumbani usiku. Alijua fika kwamba alikuwa ‘mtoto wa geti’ lakini haikuwa sababu ya kulala nyumbani kila siku wakati alikuwa akitaka kujivinjari na Jonathan.
Usiku ulipoingia, Annabel akajiandaa tayari kutoroka kwenda kuonana na Jonathan usiku huo.
Alichokifanya ni kujiandaa kwa kuvaa nguo zilizokuwa na mvuto huku akijipulizia manukato ya bei mbaya yaliyokuwa yakinukia harufu nzuri. Alipomaliza, akatoka nje huku akifunga mlango wa chumba chake kwa nje na kuondoka na ufunguo wake.
“Nataka kwenda sehemu,” Annabel alimwambia mlinzi.
“Usiku huu?”
“Ndiyo. Ila ninataka iwe siri, wazazi wamelala na nina uhakika hawatafahamu, kama utaniruhusu, elfu hamsini hizi hapa, nitarudi saa saba usiku,” alisema Annabel huku akitoa noti tano za elfu kumi.
“Mmh! Aliguna mlinzi huku uso wake ukiwa umetawaliwa na tamaa ya fedha zile.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mmh!” aliguna mlinzi huku uso wake ukiwa umetawaliwa na tamaa ya fedha zile kwani kila alipokuwa akizitazama, moyo wake uligawanyika, mwingine ulimwambia azichukue, mwingine ulimwambia aziache.
Usiku huo, Annabel hakutaka kubaki ndani ya nyumba yao, naye alitaka kutoka mtoko wa usiku na Jonathan. Japokuwa hiyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza lakini hakuonekana kujali, kitu pekee alichokuwa akikitaka ni kuonana na Jonathan tu.
Alimwangalia mlinzi, macho yalimtoka, aliziangalia noti zile za shilingi elfu kumi huku nafsi yake ikimwambia kwamba lingekuwa jambo la kijinga kuziacha na wakati aliishi kwa kutegemea mshahara mdogo.
Japokuwa kiasi kile kikubwa cha fedha alikuwa akikitamani lakini fedha hizo zilikuja na masharti mazito kwamba azichukue na kumuacha Annabel aondoke ndani ya nyumba hiyo, tena usiku kama huo.
Kichwa chake kikaanza kujifikiria mara mbilimbili huku akikipa kazi ya kuamua uamuzi aliotakiwa kuuchukua mahali hapo. Tamaa ya fedha ilikuwa imemkamata lakini kila alipokuwa akifikiria hatari yake, alikosa nguvu.
“Hizi fedha za wema kweli?” aliuliza mlinzi.
“Ni za wema kabisa. Nataka uniruhusu niondoke, nitarudi baada ya masaa machache,” alisema Annabel.
“Sawa, mzee wako hawezi kujua?”
“Hawezi, nimeufunga mlango kwa ufunguo. Kama hautomwambia, hawezi kufahamu kwamba sipo ndani ya chumba changu,” alisema Annabel.
“Sawa. Zilete, ila usichelewe,” alisema mlinzi huku akizichukua fedha zile.
“Hakuna tatizo, nitawahi kurudi.”
Mlinzi akafungua geti dogo na Annabel kutoka. Alitembea harakaharaka kuelekea sehemu zilipokuwa Bajaj. Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi, alikuwa akitaka kufika mapema huko alipoahidiana na Jonathan.
Alipofika katika eneo hilo, akaifuata Bajaj moja na kuingia na safari ya kuelekea katika ufukwe wa Coco ikanza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Njiani, Annabel alikuwa akijitahidi kuwasiliana na Jonathan na kumwambia kwamba tayari alikuwa njiani kuelekea katika ufukwe huo, sehemu waliyokuwa wamekubaliana.
“Hakuna tatizo, nitafika muda si mrefu,” alisikika Jonathan.
Mara baada ya kufika, Annabel akateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea sehemu iliyokuwa na viti vingi huku watu wengi wakiwa mahali hapo, wengi wao walikuwa wapenzi.
Annabel akatulia katika moja ya viti vilivyokuwa mahali hapo, akachukua simu yake na kumtaarifu Jonathan kwamba alikwishafika katika eneo hilo, ndani ya nusu saa, naye Jonathan alikuwa mahali hapo.
Muonekano wake haukuwa wa Jonathan, haukuwa wa kawaida. Alizoea kumuona Jonathan mwenye furaha tele huku uso wake ukionesha tabasamu kila wakati.
Siku hiyo, ndani ya usiku huo, Jonathan alionekana tofauti kabisa, alikuwa kama mtu aliyelazimishwa kufika mahali hapo. Hali hiyo ikamtisha zaidi Annabel kwa kuona kwamba kulikuwa na kitu
kimetokea, hakuongea kitu, akanyamaza kuona ni kitu gani
kingeendelea.
Jonathan alijiona kuchoka, kila siku alijitahidi kumuoneshea mapenzi ya dhati Annabel na wakati ukweli kutoka moyoni, hakuwa akimpenda msichana huyo. Unafiki wake ukaonekana kufika ukingoni, siku hiyo alitaka kumwambia Annabel ukweli juu ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
Alichoka kuishi kama mfungwa, alitaka kuwa huru kufurahia maisha yake na msichana Pamela ambaye alikuwa amejitoa kwa ajili yake na ndiye msichana pekee aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwake.
Annabel alionekana king’ang’anizi, hakumpenda hata kidogo, aliona kwamba ilikuwa bora kuendelea kuishi maisha ya kimasikini kuliko kuwa mtumwa kwa kujifunga kwa msichana huyo asiyekuwa na mapenzi naye.
“Mbona upo hivyo?” aliuliza Annabel.
“Nipo vipi?”
“Umebadilika, unaonekana hauna raha, tatizo nini mpenzi?” aliuliza Annabel.
Jonathan hakutaka kuongea kitu, alitulia kwa muda na kuanza kumwangalia Annabel. Moyo wake ulitaka amani na uhuru, kumwambia Annabel ukweli juu ya moyo wake ungemfanya kuwa huru kama zamani.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika upande mwingine, alikuwa akimuonea huruma msichana huyo ambaye alijitoa kwa asilimia mia moja kuwa naye. Hakujua ni kitu gani kingetokea mara baada ya kumwambia kwamba hakuwa akimpenda kama alivyokuwa akifikiria.
“Jonathan, niambie mpenzi tatizo linalokusibu, unapokuwa hivyo, sijisikii amani moyoni, niambie tatizo nini,” alisema Annabel.
Jonathan hakusema kitu chochote kile, bado kichwa chake kiliendelea kuwa na mawazo mengi juu ya kile alichotakiwa kuzungumza mahali pale. Kila alipokuwa akimwangalia Annabel, hakuwa na msisimko wowote wa mapenzi moyoni mwake.
Annabel bado alitaka kufahamu ukweli, hali aliyokuwa nayo mpenzi wake ilimuogopesha, alitegemea kwamba usiku huo ungekuwa moja wa usiku wenye furaha kwa kukaa pamoja na mpenzi wake lakini mwisho wa siku, mwanzoni kabisa, huzuni ikaanza kuchukua nafasi.
“Kuna jambo muhimu ningependa kuongea nawe,” alisema Jonathan, Annabel akazidi kuwa na wasiwasi.
“Jambo gani mpenzi? Mbona unanitia wasiwasi?” aliuliza Annabel.
“Najua unanipenda, najua unanithamini, najua umenifanya kuwa muhimu moyoni mwako, lakini.....” Jonathan alisema na kukaa kimya ghafla.
“Niambie, niambie Jonathan, tatizo nini?”
“Nimejaribu kwa kiasi kikubwa sana kuwa kama wewe lakini mwisho wa siku nimeshindwa kabisa. Nilijitahidi kukupenda kama ulivyokuwa ukinipenda, nikashindwa kabisa, nikatamani kukujali kama unavyonijali, nikashindwa kabisa. Annabel, kila nilipojitahidi kufanya kama unifanyiavyo, nimeshindwa kabisa,” alisema Jonathan.
“Unamaanisha nini?” aliuliza Annabel, machozi yakaanza kumbubujika.
“Naomba uniache na maisha yangu,” alisema Jonathan na kuinuka, akaanza kuondoka mahali hapo. Annabel akahisi kuzimiazimia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment