Chombezo : Mh! Missed Call Ya Shemeji
Sehemu Ya Nne (4)
Eti ni kweli?” alihoji baba mtu uso ukiwa umekunjamana…
Aisha aliinamia chini. Aliwaza ajibu nini, ni kweli au si kweli?
“Nakuuliza wewe Aisha. Na kama ukisema si kweli nampigia simu mumeo naye aje hapa ili nimsikie yeye anasemaje,” alikuja juu baba huyo.
“Ni kweli baba, lakini naomba samahani sana kwa hilo.”
“Ni kweli kwamba?” mama mtu alidakia sasa…
“Namnyimaga unyumba mume wangu.”
“Kabisa kabisa… na unadiriki kusema ni kweli bila aibu Aisha?” alizidi kushangaa mama mtu.
“Enhe, endelea wewe,” sasa hapo baba mtu alielekeza kwa dada mtu aendelee kusema…
“Kutokana na hali hiyo wazazi wangu hasa ikizingatiwa kwamba na mimi nilikuwepo pale bila mwanaume, ubinadamu ukanipata. Kwangu nilihisi kumwonea huruma shemeji yangu kwani ni kijana bado…”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Uliwahi kumwonya mdogo wako kuhusu tabia hiyo na madhara yake?” aliuliza baba.
“Niliwahi ndiyo. Nilimsema akasema nimwachie na maisha yake.”
“Eti ni kweli Aisha aliwahi kukuonya?”
“Ni kweli.”
“Ni kweli ulimjibu akuachie na maisha yako?”
“Ndiyo.”
“Haa! Kwanza hiyo tabia nani kakufundisha mwanangu Aisha. Mumeo unamnyima unyumba na wewe ndiyo mke, unataka iweje? Aisha unataka sisi wazazi tuseme siri zetu kwenu nyie watoto siyo?” Baba mtu alifoka.
Mama naye akadakia kwa hasira hasa alipokumbuka kwamba aliumwa ghafla…
“Mimi sijawahi hata siku moja kumwambia baba yenu sitaki, hata siku moja. Wewe Aisha umepatia wapi hiyo nguvu mwanangu?”
Dada mtu alimfuata mama yake kwa magoti na kumshika miguu akimwomba asiendelee kusema maneno hayo kwao kama watoto…
“Mama chondechonde, hayo maneno ni laana kwetu mama, usiyaseme.”
“Si ndiyo mnataka!”
Baba mtu alisimama akaingia ndani, chumbani…
“Haya, baba yenu kama hivi ameondoka. Haya yote shauri yenu. Sijui mkoje?” alipomaliza kusema hayo naye akasimama na kuondoka kumfuata mume wake.
Nje walibaki Aisha na dada yake. Walikuwa kimya, hakuna aliyejua nini kifuatie. Ikawa haijajulikani nani anazibeba lawama zote sasa.
Aisha alimwangalia dada yake, akasimama na kuingia ndani. Dada mtu alibaki kwa muda hapo akiwaza, akaenda mbali kidogo na nyumba akapiga simu kwa Beka. Simu hiyo ilipokelewa haraka sana na Beka…
“Haloo…”
“Haloo, mambo shemeji?”
“Poa, vipi huko?”
“Huku poa tu. Mwenzangu nikwambie kitu…”
“Niambie shemeji.”
“Si nimembwaga mkeo huku, kalowa kama katembea kwenye mvua, we acha tu.”
“Ilikuwaje?”
“Kwenye kikao, nikasema yote kisa cha yeye kukunyima unyumba, wazazi wakashtuka sana tena sana. Wakamuuliza alifundishwa na nani kumwambia mume sitaki?”
“Acha bwana…”
“Eee, baba amekasirika hadi akatoka kikaoni, mama naye akaondoka. Hivi hapa nipo nje naongea na wewe.”
“Da! Safi sana shemeji, sikujua kama ungeweza kutumia engo hiyo ya kuninyima unyumba.”
“Wee, unanijua unanisikia! Na mimi nikasema nitumie engo hiyohiyo.”
“Safi sana, nitakutafutia zawadi mama.”
“Nitaipataje?”
“Kwani hurudi?”
“Mh! sidhani, we unaamini naweza kuruhusiwa kuja Dar kwa Aisha? Labda nije kivyangu.”
“Basi siku ukija kivyako nitakuwekea zawadi yako,” alisema Beka.
“Baadaye shemeji, naona mlango unafunguliwa, sijui nani anatoka, nitakupigia,” alisema dada mtu na kukata simu.
Aliyetoka ni mama mtu…
“We huingii ndani kulala?” aliuliza mama.
“Naingia mama.”
Mama akatoka nje kabisa akamwambia kwa sauti ya chini…
“Baba yako amesema ulichofanya si kizuri, lakini alichofanya mdogo wako kwa mumewe ni kibaya sana. Amekasirishwa sana na mdogo wako. Amesema anaweza kusababisha ndoa kuvunjika na yeye hataki kusikia hivyo.”
Kwa mbali dada mtu huyo akaanza kuwaza kuhusu ndoa yake maana tangu amepigwa chini na mumewe hakuwaambia wazazi wake…
“Mimi mama sijafanya kwa nia mbaya.”
“Hapana, ulipoona shemejiyo kakwambia hivyo na umemshauri mdogo wako hataki, ungetuletea habari sisi.”
“Nisamehe mimi mama.”
Mara mlango ukafunguliwa, Aisha akatoka huku akimwaga machozi
Nini wewe?” aliuliza mama mtu huyo.
“Mama mimi nasafiri usiku huuhuu.”
“Kwenda wapi?”
“Kurudi kwangu.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nini kimetokea, mbona unalia?”
“Nimekumbuka mengi mama. Ni kweli nilikuwa nakosea kumkatalia unyumba mume wangu…amekuwa akinisema sana kuhusu hilo sikuwa namsikia, sasa najuta mama.”
“Huwezi kupata gari muda huu! Nadhani unajua.”
“Hata malori nitapanda mama.”
Mara, baba mtu naye akatoka baada ya kumsikia Aisha akitangaza kuondoka usiku huohuo kurudi kwa mume wake, Dar es Salaam…
“Kama amelijua kosa lake na kuamua aende sawa tu, nenda. Ukipata gari wasalimie, ukikosa rudi ulale kesho uondoke,” alisema baba mtu huyo huku akirudi ndani. Sauti yake haikuonesha uzembe wakati wa kuzungumza.
***
Asubuhi Aisha aliwaaga wazazi wake kurudi Dar kwa mume wake baada ya jana yake kukosa usafiri.
“Sisi wazazi wako Aisha tunakutaka ukaishi kwa mumeo ukijua yeye ndiye kichwa cha nyumbani kwako. Kama utataka kujifanya mko sawa hamtafika mbali, ukweli tunakwambia.”
“Sawa mama, mimi nimeelewa lakini pia naamini mnajua nilivyotendewa na dada yangu,” alisema Aisha huku akimwangalia dada yake kwa jicho baya!
“Tunajua, hilo tuachie sisi tutajua jinsi ya kufanya, wewe nenda salama na uwe na amani. Yote yatoe moyoni mwako ili uishi kwa amani.”
***
Ilikuwa jioni baada ya Aisha kuondoka, baba yao alipokuwa amerudi kutoka kwenye mihangaiko yao, alimwita mkewe na kumwambia wamuweke chini dada wa Aisha na kumuuliza kuna nini nyumbani kwake mpaka akaenda Dar kuishi kwa mdogo wake yakatokea ya kutokea…
“Tumekuita hapa Ime, tunataka kujua na wewe nyumbani kwako kuna nini mpaka ukaenda kuishi kwa mdogo wako Dar es Salaam?” aliuliza baba mtu kwa sauti isiyotaka utani wale kucheleweshewa majibu…
“Mimi nimeachika!”
“Umeachika! Ime, unasema kweli unanitania?” alidakia mama mtu huku akikaa sawasawa.
“Nimeachika mama,” alisema dada mtu huyo huku akianza kulia.
“Nyamaza! Umeachika kwa sababu gani?” baba mtu alikuja juu…
“Mume wangu alisema amechoka tu kuishi na mimi, akanipa nauli niondoke.”
“Siyo kweli, mimi si mtoto wa kunidanganya Ime,” alikataa baba mtu. Mama naye akasema…
“Au ulifanya umapepe wako huko?”
“Hapana mama.”
Baba mtu huyo alichukua simu yake na kumpigia mkwewe lakini huku naye akishangaa kwamba kama ni kweli kwa nini mkwewe huyo hajamwambia?
“Hujambo baba?”
“Sijambo baba shikamoo?”
“Marhaba, mzima?”
“Mimi mzima kiasi, habari za hapo nyumbani?”
“Njema. Tumeona kimya, nikasema ngoja nikupigie.”
“Nipo baba.”
“Sasa eti huyu mwenzako alipatwa na nini? Maana kaja hapa tunamuuliza kwa mumeo vipi anasema umemwacha.”
“Baba kwani hajawapa barua yangu?”
“Barua! Wala hajatupa, ulimpa barua?”
“Nilimpa barua yenye maelezo ya kutosha kabisa, akasema anaanzia Dar kwa Aisha halafu anakuja huko. Nikajua ni kweli, jana tu nikasikia kaharibu Dar, nikashangaa kugundua kumbe alikuwa bado Dar muda wote huo.”
“Mh! Baba mimi nashukuru sana. Kwa sababu umesema kuna barua ngoja nimwambie anipe niisome kwanza halafu nitawasiliana na wewe baba.”
“Sawa baba.”
Baba mtu alimgeukia binti yake…
“Eti barua yangu iko wapi?”
“Ilipotea baba.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mzee huyo alisimama na kumfuata mwanaye ili amchape makofi, lakini mama mtu akajitahidi kumzuia asifanye hivyo.
“Mjinga sana huyu mtoto. Kenge mkubwa kasoro mkia wewe. Unataka kutufanya sisi watoto wadogo? Barua haikupotea bali umeipoteza wewe makusudi ili tusijue kilichoandikwa ndani yake, mimi nampigia mumeo aniambie kisa,” alisema baba huyo kwa sauti yenye ukali.
***
Aisha alifika nyumbani kwake lakini hakumkuta mume wake, Beka. Akachukua funguo mahali na kuzama ndani bila kumwambia kwamba amerudi.
Beka siku hiyo alikuwa kwa demu wake mpya ambaye alianza kuwa na uhusiano naye siku mbili kabla ya fumanizi lake na shemejiye. Kwa hiyo alikuwa nyumbani kwa demu huyo ambapo si mbali sana kutokea kwake.
“Baby, kwa hiyo ni kweli kabisa mkeo anaweza kukunyima unyumba?”
“Si anaweza, ananinyimaga sana tu.”
“Daa! Anakosea sweet,” alisema demu huyo anayeitwa Faidha huku akimlalia kifuani Beka na kumkumbatia kwa staili ya mahaba mazito.
“Basi kwangu umefika, hata akikunyima mwaka mzima, mimi nipo dear,” alisema Faidha huku akifungu vifungo vya shati la Beka.
*****
Beka alikuwa akipumua kwa nguvu, kila alipokuwa akimwangalia demu wake mpya, Faidha alivyokuwa akifungua vifungo vya shati lake, akabaki akitweta tu.
“Yule mwanamke alinikera sana,” alisema Beka.
“Achana naye bwana, hajui jinsi ya kumuhendo mwanaume, ngoja nimuonyeshe,” alisema Faidha, alijua fika kwamba alikuwa mwizi, hivyo alitaka kufanya vitu kwa nguvu zote ili aweze kumchukua Beka jumla.
Kwa sababu alisoma alama zote za nyakati hasa kile kilichokuwa kikitaka kutokea mahali hapo, Beka akachukua simu yake na kuizima kabisa, hakutaka kusumbuliwa kwani aliona muda mchache baadaye angekuwa bize.
“Una kifua kizuri, yaani nashangaa alikuachaje miezi yote hiyo jamani, hana hata huruma,” alisema Faidha.“We acha tu, hebu endelea kwanza, yule mjinga sitaki hata kumsikia.”
Faidha alitumia ujuzi wake wote, mara aukandekande mgongo wa Beka, mara ampeleke huku na kule, yaani kila kitu alichokuwa akikifanya mahali hapo kilikuwa ni kumfanya Beka amuone kuwa bora zaidi, alijua kwamba yeye ni mwizi, hivyo alihakikisha kwamba wizi wake unafanikiwa.
* * *
Aisha alitulia chumbani, kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, alikuwa akijuta juu ya kile alichokuwa amekifanya cha kumnyima unyumba mume wake kwa muda mrefu.
“Mimi mwanamke kwa nini nimefanya vile? Hivi kama ningefanyiwa mimi ingekuwaje?” alijiuliza Aisha.
Wakati huo, hakujua kwamba mume wake alikuwa kwa demu wake mpya baada ya kuona kwamba mke wake huyo alikuwa akimletea mapozi. Aisha aliendelea kumsubiri mume wake arudi ili akae naye chini na kuyazungumza.
“Kwanza yupo wapi? Mbona anachelewa hivyo? Au kapata demu mwingine?” alijiuliza Aisha lakini hakutaka kukubaliana na mawazo yake, alijua kwamba mumewe ni mwaminifu sana japokuwa alimsaliti kwa dada yake, Ime.
***
Baba Aisha hakutaka kukubali, alijua kwamba Ime alipoteza barua ile kwa ajili ya kupoteza ushahidi juu ya kile kilichokuwa kimeandikwa, hivyo alitaka kumpigia mume wa Ime ili amwambie ukweli.
“Niambie baba.”
“Huyu mkeo kapoteza barua, hebu niambie ilikuwaje.”
“Unaona baba, nilijua tu hataifikisha, huyo mwanamke mpumbavu sana.”
“
Hebu niambie ilikuwaje.”
“Ime si mwaminifu kabisaaa, yaani japokuwa nilimuoa, alikuwa akitoka nje ya ndoa bila mimi kujua.”
“Unasema kweli?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo, wewe si umeona hata ule ujinga alioufanya kwa mdogo wake, umekuwa gumzo jiji zima.”
“Aiseeee, yaani kumbe ndiyo aliyokuwa akiyafanya?”
“Ndiyo baba. Wakati mwingine anachelewa kurudi, nimemfumania mara kibao tu, akawa ananipiga saundi kwamba alikuwa kwa marafiki zake.”
“Kumbeeeee.”
“Ndiyo, huyo hafai kuwa mke wangu. Na ndiyo maana hata hiyo barua hakutaka kuileta kwenu.”
“Sawa, tutaongea zaidi.”
Baba Aisha akakata simu na kuanza kumwangalia Ime, kwa jinsi alivyoonekana tu, alikuwa na hasira tele.
* * *
Mlango ukafunguliwa, Beka akaingia chumbani, macho yake hayakuonyesha mshtuko wala tabasamu, kitendo alichofanyiwa na mke wake, Aisha kilimuuma, sasa alikuwa amefika hapo wayamalize.
“Karibu mume wangu.”
“Asante,” alisema Beka huku akikaa kitandani, bado alionekana kuwa na kitu moyoni.
“Naomba unisamehe.”
“Nikusamehe! Umefanya nini?”
Aisha akanyamaza kwa muda.
“Nilikuwa nakunyima unyumba.”
“Kwa hiyo leo ndiyo umeamua kuniomba msamaha baada ya kugundua kwamba lile lilikuwa kosa?”
“Hapana, siyo hivyo, naomba unisamehe tu.”
Aisha akaona hiyo haitoshi, alichokifanya ni kumsogelea Beka na kuanza kumshikashika mgongoni, Beka mwenyewe wala hakutaka kushoboka, kila kitu alikimalizia kwa demu mpya, Faidha.
“Sawa, tutaangalia.”
“
Jamani, sasa tutaangalia nini baby?”
Beka hakutaka kuongea sana, kile alichokisema kilitosha kabisa, akasimama na kulifuata kabati, akavua nguo, akavaa nyingine na kutulia kitandani.
“Naomba unisamehe mpenzi.”
“Mbona yameshakwisha, si umeamua kurudi, yameshakwisha kitambo tu.”
“Sawa. Nashukuru.”
Wala Beka hakuwa na mawazo na huyo mke wake, kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Faidha tu, kwake, kipya kilikuwa kinyemi, hivyo demu huyo alionekana kuwa na nguvu kuliko Aisha.
***
“
Haya sasa endelea kutudanganya, yote yashawekwa kweupeeeee, nimeshayajua,” alisema baba Aisha huku akimwangalia Ime.
“Amesemaje?” aliuliza mama.
“Kumbe alikuwa akimsaliti mwenzake, hakuwa akitulia, keshazoea ule mchezo na ndiyo maana akaenda kuurudia hata kwa shemeji yake, yaani hata aibu haoni.”
“Nisameheni,” alisema Ime huku akijitahidi kuyatafuta machozi.
“Wewe si umejifanya mjanja kupoteza barua, kiko wapi sasa, tumeshajua ujinga wako. Unapata mume wa kuishi naye, unafanya ujinga, hujui kama kuolea dili.”
“Nisameheni.”
“Kwani umetukosea sisi? Nenda kamwambie mumeo kwamba ulimkosea.”
* * *
Mapenzi ya Faidha yalimchanganya Beka, japokuwa alimpiga kalenda mke wake kwamba angemwambia kama alimsamehe au la, lakini bado naye alikuwa na mchepuko wake uliokuwa ukimliwaza.
Beka akabadilika kabisa, akawa anakaa sana kwa mchepuko wake Faidha huku wakati mwingine akilala hukohuko kwa kisingizio cha kazi nyingi.
Aisha akavumilia, hakuwa na jinsi, hakuweza kuondoka nyumbani hapo, ila pamoja na yote hayo, makosa yalikuwa kwake, alilikoroga weee, sasa alitakiwa kulinywa.
“Jamani mume wangu unanitesa.”
“Nakutesa?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/--
“Ndiyo. Kila siku unachelewa kurudi.”
“Kazi zimekuwa nyingi mno.”
“Sasa mbona hauniambiagi?”
Beka hakutaka kuendelea kujibu maswali zaidi kwani yalimchosha. Alikuwa radhi kukaa kimya na kuanza kuufikiria mchepuko wake kuliko kumjibu Aisha ambaye kwake alionekana muuaji, miezi miwili hadi mitatu bila unyumba, ilikuwa ni shiiiiiida.
Mwezi mmoja ulikatika tangu Aisha aliporejea kwake kutoka kijijini kwao na kutaka yaishe kwa mumewe lakini mumewe alishakolea kwa Feidha…
“Hivi, huyu mwanamke anayemsumbua mume wangu yukoje kwanza? Anaweza kufanana na mimi au kachangudoa tu?” alijiuliza Aisha na kuamua kufanya mkakati wa kumjua.Siku moja mumewe akiwa anaoga, yeye aliichukua simu yake kwa siri na kuanza kusoma meseji akiamini kuwa, atakutana na meseji ambayo itamjulisha kwamba ni ya mwanamke wa Beka…
“Oyaa! Leo vipi, wapi? Mi nikitoka job nakwenda Migomigo kwenye ile baa ya jana.”
Meseji hiyo aliipuuza Aisha, akajua ni ya mwanaume…
“Bro vipi ule mzigo, nikuletee lini sasa?”
Meseji hiyo pia aliipuuza Aisha, akaona ni walewale. Aliendelea kuskroo mpaka akakutana na meseji yenye namba iliyoseviwa kwa jina la ‘Material’ akahisi ni yenyewe baada ya kusikiasikia maneno kutoka kwa wanaume yakisema ‘wife material.’ Akaifungua…
“Sweet, ile suti uliyosema nimeipata kwenye duka moja mjini, ni shilingi laki mbili na nusu, nimekununulia hivyohivyo maana napenda sana siku moja uvae tukiwa wote.”
Aisha alishusha pumzi kwa nguvu, akavuta picha na kumwona mwanamke huyo mbele yake, kwamba ni mzuri kuliko yeye na pia ana kazi nzuri kuliko yake…
“Mpaka amemnunulia mume wangu suti ya laki mbili ina maana yuko vizuri? Mh! Sasa nitamwonaje?” alijiuliza Aisha akapata wazo, akachukua ile namba ya simu na kuisevu kwenye simu yake, akaiandika;
NIKIKUKAMATA!
Beka alipotoka kuoga alimkuta mkewe amebadilika sura lakini hakumuuliza kitu kwani alishaamua kutowasiliana naye kwa undani.
Alijiandaa, akaondoka zake kwenda kazini. Nyuma, Aisha alituma pesa kupitia namba za simu alizochukua kwenye simu ya mumewe, akaambiwa athibitishe anakotuma pesa kabla ya kuingiza password ambapo lilitokea jina la Faidha…
“Mh! Jina zuri lakini,” alisema moyoni, akamtumia meseji akisema…
“Mambo Feidha?”
Feidha hakuijibu meseji hiyo, ndani ya nusu saa, akapiga simu. Aisha akahangaika apokee au la! Mwishowe akakaa kimya mpaka simu ikakata, ikaingia meseji ikiuliza…
“Samahani nani mwenzangu? Nilipoteza simu.”
“Mimi naitwa Suzy, nataka kukutana na wewe Feidha.”
“Samahani sana Suzy, Suzy wa wapi na kukutana kuhusu nini anti yangu? Samahani lakini.”
Aisha alianza kupata picha ya aina ya mtu anayechati naye kwamba, kwanza si mshari, mstaarabu na mwenye akili zake timamu…
“Suzy wa Kinondoni, nilipewa namba yako na dada mmoja anaitwa Jane, akaniambia unaweza kunisaidia jambo.”
Kutoka moyoni mwake, Feidha alikuwa ana rafiki anaitwa Jane, akampigia kwanza simu ikawa haipo hewani. Alitaka kumuuliza ili ajue kama kuna ukweli kuhusu madai ya Suzy huyo feki.
“Oke. Uko wapi Suzy?”
“Nipo Posta kwa sasa.”
“Na mimi nipo kazini hukuhuku Posta, nafanyia CRDB Makao Makuu hapa, njoo.”
“Mh!” aliguna Aisha baada ya kusoma meseji hiyo, akajiuliza.
“CRDB Makao Makuu, anafagia ofisi, anahudumia wateja au bosi? Lakini kufagia ofisi asingeweza kumnunulia mume wangu suti, atakuwa ana nafasi fulani hivi.”
“Oke, nakuja. Nikifika nikuulizie nani?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Feidha aliishangaa sana meseji hiyo kwani wakati anaanza kumuuliza alisema mambo Feidha iweje aseme akifika amuulize kwa jina gani?
“Ulizia Feidha tu.”
Aisha alijua amechemka kwenye hilo, akaumia sana. Alichanganya miguu hadi benki hiyo na kumuulizia Feidha..
Mhudumu alimuuliza kama ana ahadi naye…
“Ndiyo.”
Alipelekwa kwenye ofisi ya Feidha ambako kulikuwa na wadada watatu…
“Haa, Ummy…” alishangaa Aisha…
“Haa, Aisha ni wewe?” alisema msichana huyo akiwa amesimama kumlaki Aisha. Walikumbatiana kwa furaha yote.
“Karibu ukae Aisha,” Aisha alikaribishwa kisha huyo Ummy akamgeukia mhudumu …
“Anti, halafu kuna mgeni wangu akija mwambie anisubiri hapo kwenye benchi.”
“Sawa bosi.”
Aisha alibaki na mawazo ya kasi kichwani mwake …
“Enhe, za siku Ummy?”
“Poa tu. Karibu sana.”
“Asante.”
Wasichana wengine wawili walikuwa wazuri sana, lakini aliyempokea Aisha, yaani Ummy alikuwa mzuri zaidi kuliko wote. Aisha aliamini kwamba katika wasichana wale wawili mmoja wao ni Feidha.
“Niambie, umejuaje niko hapa?” aliuliza Ummy…
“Ummy wala sijajua kama wewe uko hapa, mi nimemfuata anti mmoja,” alisema Aisha akiwa amemsogelea Ummy kwa karibu sana…
“Nani?”
“Kwani hao kuna nani na nani?”
“Mmoja anaitwa Salma, mwingine Magreth.”
Mh! Kweli? Basi niliyemfuata mimi hapa hayupo,” alisema Aisha akiwaangalia wale akina dada, yaani Salma na Magreth.
“We kwani umemfuata nani?” aliuliza kwa shauku Ummy…
“Hebu twende nje nikakwambie,” alisema Aisha huku akimwangalia Ummy kwa macho ya kutaka kujua atafanyaje baada ya kumwambia waende nje.
Ummy alisimama, wakatoka huku akiwaaga wenzake…
“Jamani niko mgahawani na mgeni wangu.”
“Sawa,” alisema Salma.
Baada ya kuondoka, Magreth alianzisha mazungumzo…
“Unajua nimeshangaa sana!”
“Umeshangazwa na nini?”
“Kumbe Faidha anaitwa Ummy?”
“Ee, kweli bwana, hata mimi nilishangaa pia.”
“Haya majina haya, usikute Faidha Ally ni mtu mwingine kabisa, ila Ummy kaliibukia jina lake kwenye cheti cha chuo.”
“Hilo mbona lipo sana tu.”
“Teh! Teh! Teh! Teh! The,” walicheka na kuendelea na shughuli zao.
* * *
“Aisha naona unapendeza tu mwenzangu!” alisema Ummy wakiwa wameshatoka nje.
“Wewe je? Mi nilidhani mzungu bwana, kumbe mbantu halisi…”
Walicheka wote huku wakiwa wanaingia kwenye mgahawa mmoja jirani.
Mhudumu alifika, akawasikiliza. Alipoondoka, Ummy akashtuka kwa simu yake kuita…
“Sorry Aisha, napokea simu mara moja.”
“Oke.”
“Haloo baby…poaaa…niko sawa sijui wewe baby wangu! Vipi mamaa hajambo? Bado anaendelea na mambo yake yale? Ha! Ha! Ha! Nipo job…oke…oke sweet..eee…jamani B…oke baadaye,” alimaliza Ummy, akamgeukia Aisha ambaye alionekana anataka kusema neno…
“Naona unaongea na shemeji!”
“Mwenzangu, lazima kubembeleza ndoa kwanza, si unajua tena.”
“Kwani ulishafunga ndoa Ummy?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nifunge wapi? Wanaume wenyewe hawanioni, nimejikuta nimeangukia kwenye ndoa ya mume wa mtu.”
“Kweli Ummy?”
“Sasa n’tafanyaje Aisha?”
“Mh! Kazi unayo, ungekuwa wewe vipi?” aliuliza Aisha huku akimkodolea macho mwenzake…
“Ningekuwa vipi kivipi?”
“Mume wako akichukuliwa na mwanamke mwingine?”
“Weee! Ningeua mtu Aisha. Mimi nilivyo na wivu, sijui ingekuwaje hakyamungu.”
“Kumbe mkuki kwa nguruwe siyo? Basi uache na wewe kuiba waume za watu”
“Tatizo si mimi, ila mwanaume mwenyewe ana bifu na mke wake ndiyo maana nimeibuka mimi kumpa faraja. Lakini anyway, tuyaache hayo shoga yangu, lete habari,” alisema Ummy huku akionekana kuwa siriasi sasa kwa kumsikiliza Aisha…
“Ummy, mimi nina matatizo, kuna mwanamke ameingilia ndoa yangu, anafanya kazi hapa benki…” alianza kusema Aisha…
“Benki hii?”
“Ndiyo, benki hii. Nimeongea naye akaniambia yuko kazini ndiyo nikaja.”
“Kama ni kweli na amekuona si atakuwa amekimbia!”
“Si rahisi maana nimetumia mbinu nyingine.”
“Anaitwa nani?”
“Anaitwa Faidha.”
“Faidha?” aliuliza kwa mshutuko Ummy…
“Ndiyo, unamjua?”
Ummy alinyamaza kimya kwa muda kwani yeye ndiye Faidha mwenyewe.
Ummy aliingia chuo akitumia jina la Faidha Ally na ndilo aliloajiriwa nalo kwenye benki hiyo. Hata pale Aisha alipoingia ofisini na kumlaki kwa kumwita jina la Ummy, wenzake, Salma na Magreth walishtuka, wakagundua kumbe Faidha ana jina lingine…
“Kwani vipi Ummy, unamjua?” aliuliza Aisha…
“Hapana, simjui, huyo mume wako anaitwa nani?”
“Beka.”
“Mh! Ni mumeo kabisa?”
“Ee, kwani vipi Ummy, unamjua huyo Faidha?”
“Simjui,” alisema Ummy akionekana kukosa raha kabisa.
“Ngoja nikuoneshe namba zake za simu, huenda ukamjua,” alisema Aisha huku akibofyabofya simu yake. Hilo halikumsumbua Ummy kwani alijua jina lake aliloandikishia kwenye usajili wa laini anayoitumia ni kwa jina la Ummy.
“Namba yake hii hapa,” alisema Aisha akimwonesha namba hiyo Ummy.
“Oke…oke! Sasa atakuwa nani?” aliuliza Ummy, akaongeza…
“Mi tangu nimeanza kazi humu ndani huu mwaka wa pili sasa sijawahi kumsikia mtu anaitwa Faidha.”
Aisha alishangaa unyonge wa ghafla wa Ummy. Aliamini hayupo sawa kama alivyomkuta kwani uso wake ulionesha waziwazi kwamba ana kitu moyoni mwake.
Aisha, bila kumwambia Ummy aliipiga ile simu ikaita. Aliiweka sikioni huku akisema…
“Nampigia.”
Ummy alitaka kushtuka lakini akakumbuka kwamba simu yake aliiacha mezani kwake ndani kwa hiyo hakuna mtu ambaye angepokea.
“Hapokei?” aliuliza Ummy kwa sauti ya chini kidogo kwani bado alikuwa hana raha.
“Hapokei,” alijibu Aisha, akapiga tena…
Mara Salma alitokea akiwa kasi ameshika simu ya Ummy…
“Simu yako inaita bosi,” alisema Salma huku akimkabidhi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment