Search This Blog

Monday, October 24, 2022

TIMBWILI...TIMBWILI - 5

 





    Chombezo : Timbwili .... Timbwili

    Sehemu Ya Tano (5)



    SAA 6:15 usiku iliwakuta Mwajuma na Saad wakiwa kitandani, chumbani mwa Saad, ikiwa ni zaidi ya saa nzima tangu walipoingia. Mwajuma alikuwa kamlalia Saad kifuani, wakinong'ona maneno ya mahaba.



    Mara Mwajuma akaitazama saa yake ya mkononi. Akaguna. “Saa sita!” hatimaye alisema na kuongeza, “Muda umekwenda, Saad. Inanipasa niondoke sasa.”



    “Acha hizo, mpenzi,” Saad alisema huku akimpapasa mapaja. “Wasiwasi wa nini? Kwani lazima uende usiku huu?”



    “Ndiyo! Ile nyumba haiko kwenye mazingira mazuri kwa mtu kuamua kulala nje. Chumba changu ni cha nje, wezi wanaweza kunifanyizia.”



    Saad alitaka kutamka neno akasita. Mwajuma alinyanyuka haraka. Akavinyoosha viungo kwa uchovu. Naam, alihisi uchovu mwilini, na alikuwa na sababu ya kuwa na uchovu. Tangu walipoingia humo ndani, nguo zikawa ni kero tupu miilini mwao.



    Wakazivua.



    Kilichofuata ni kile walichokihitaji, na walihakikisha wanazikonga nyoyo zao kwa pumzi zao, wakivitumia viungo vyao kwa namna iliyowapa burdani isiyoelezeka kwa vinywa vya kawaida. Lakini sasa Mwajuma alihitaji kurudi kwake. Akaharakisha kukusanya nguo zake avae.



    Akiwa katika zoezi la kuvaa, alimtazama kidogo Saad na kumuuliza,

    “Saad, unakumbuka wakati ule uliwahi kun'ambia unanipenda?”



    “Nakumbuka vizuri, mpenzi. Na hadi sasa bado nakupenda.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ya kweli hayo?”



    “Sikutanii, Mwajuma.”



    “Sawa, sikatai. Lakini ilikuwaje usinioe mimi na badala yake ukamwoa Halima?”

    Kimya.



    “Kwa nini hukunioa mimi?”



    “Tuachane na Halima. Nataka kumsahau kichwani mwangu.”

    Mwajuma akacheka kidogo. Hatimaye akasema, “Okay, sasa uko huru. Je, na mimi ningekuwa huru ungenioa?”



    Saad alikubali kwa kutikisa kichwa.



    “Hujanijibu. Kutikisa kichwa siyo jibu.”



    Wakacheka.



    “Ningekuoa, mpenzi. Kwa kweli namwonea wivu huyo mtu wako.”



    “Kwa hiyo, tuseme, mathalani mimi na mzee Samwel tukivunja uhusiano wetu, utanioa?” Mwajuma alizidi kumbana Saad.



    “Naam,” Saad alijibu kwa msisitizo. “Yaani niko tayari hata leo. Nakupenda Mwajuma. Kwa kweli nilikosea sana kumchukua yule hayawani.”



    Maneno hayo yalitoka moyoni mwa Saad. Alimpenda sana Mwajuma, pendo la dhati. Na kwa ujumla Mwajuma alikuwa na mvuto uliostahili kumfanya apendwe, mvuto uliopelekea hata mzee Samwel amtimizie mahitaji yake mengi, makubwa kwa madogo.



    Mwajuma alikuwa mweusi, weusi wake ukiwa ni ule wa kutakata. Ngozi yake ilikuwa nyororo ambayo ukiigusa huteleza kama samaki aina ya kambare na huchubuka kwa urahisi pindi ipatapo msuguano kidogo.



    Takriban kila sehemu ya mwili wake kuanzia umbile la uso, urefu wa mikono na miguu, kucha za vidole vya mikono na miguu na kwingineko, kulitia ashiki na msisimko na kuashiria mapenzi.



    Rehe ya mwili wake ilikuwa kivutio kingine, huwa kama ya jasho la majani ya mlimao. Alijaaliwa matiti yenye ukubwa wa wastani, mazito na yenye chuchu nyeusi tii. Mapaja yake hugusana kwa ndani na yamebinuka kwa nje na kupinda kwa ndani karibu na kiuno, na yamebinuka tena na kupinda kwa ndani karibu na magoti.



    Makalio yake ni makubwa na teketeke, akitembea huwa yakitikisika kwa namna iliyoyavuta macho ya wanawake na wanaume, kila mmoja kwa hisia zake.



    Naam, huyo ndiye Mwajuma, ambaye akilini mwa Saad, alikuwa ni mwanamke pekee aliyeweza kupata sifa mbili muhimu kati ya tatu ambazo mwanafalsafa mmoja aliwahi kudai kuwa ni vigumu kwa mwanamke yeyote duniani kufanikiwa kuwa nazo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwanafalsafa huyo maarufu duniani alidai kuwa, mwanamke bora sana ni yule aliye mrembo sana hadharani, pili; hodari sana jikoni, na tatu; malaya sana chumbani.



    Kwa Saad, Mwajuma alikuwa na sifa mbili; mrembo sana hadharani na malaya sana chumbani. Kwa hapo alikiri kuwa ni mwanamke awezaye kuiteka hata akili ya mcha Mungu aliye thabiti.



    Ni kwa mapenzi hayo makubwa kwake, Saad alimtaka Mwajuma aachane na Mzee Samwel.



    “Duh, itakuwa ngumu, Saad,” Mwajuma alisema. “Kwa kweli siwezi kumwacha ghafla kiasi hicho.”



    “Kwa nini? Ina maana unampenda sana?”



    “S'o ivo, Saad. Kwa kweli simpendi hata kidogo! Lakini nimemzoea, na sidhani kama nitakuwa mwungwana kama nitamtema ghafla.”



    “Zua sababu.”



    Kimya kifupi kilipita. Mwajuma alikuwa akiitafakari kauli hii ya Saad. Mara akashusha pumzi ndefu. “Huo ni mtihani, Saad,” hatimaye alisema.



    “Mtihani gani, Mwajuma?” Saad alimbana. “Kwa mwanamke mjanja kama wewe, hapo kuna mtihani gani katika kumtema huyo mzee wako? Unataka kun'ambia kuwa hilo ni jambo lisilowezekana?”



    Kimya kingine kilifuata. Kwa mara nyingine Mwajuma alionekana kuzama katika fikra nzito. Na Saad naye hakutaka kumwingilia, alimwacha auchemshe ubingo wake katika kuchambua pumba na mchele.



    Mara wakakutanisha macho. Sasa Mwajuma akaonekana kuwa yuko tayari kuzungumza.



    “Inawezekana,” hatimaye alisema. “Nitafanya hivyo, lakini siyo leo au kesho. Vinginevyo itakuwa tumezua kimbembe cha aina yake, kimbembe ambacho huenda suluhisho lake likawa gumu kupatikana.”



    Baada ya kusema hivyo, Mwajuma alionekana kuwa na haraka zaidi. “Siki'za, Saad, lazima niende sasa. Hayo tuliyozungumza yanawezekana lakini tutapanga vizuri siku nyingine.”



    “Lakini kwa nini usilale tu, Mwajuma?” Saad alikuwa king'ang'anizi.



    “Haiwezekani,” Mwajuma alisisitiza. “Kama bado una hamu na mimi, basi twende kwangu. Lakini kwa kweli siwezi kulala nje.”





    “Sawa, twende.”



    “Hapo umesema. Siku nyingi, Saad.”



    “Siku nyingi, Mwajuma.”



    **********



    TEKSI waliyokodi iliwashusha nje ya nyumba aliyopanga Mwajuma, Magomeni Mwembechai, dakika kumi baada ya kutoka kwa Saad.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Karibu, karibu ndani, Saad,” Mwajuma alimkaribisha huku akiufungua mlango.



    Saad aliingia na kushangazwa na jinsi chumba hicho kikubwa kilivyosheheni samani za thamani kubwa. Papohapo akayakumbuka maneno aliyoambiwa na Hadija, “...na kamjazia mifenicha ya nguvu ndani. Nakwambia ukifika kwa Mwajuma, utakubali mwenyewe.”



    Naam, sasa amejionea mwenyewe, na amekubali.



    “Kula, tu'shakula kule Travertine Hotel, au bado una njaa?” Mwajuma alimuuliza.



    Tabasamu hafifu lilimtoka Saad. Kisha akajibu, “Ndio, nina njaa, lakini siyo njaa ya wali, kuku, chipsi s'jui na vidubwasha gani. Hapana. Njaa yangu hata wewe unaijua.”



    Mwajuma alicheka. “Okay, kilichobaki ni kuoga na kulala. Vua nguo ukaoge.”



    Hakwenda Saad peke yake, walikwenda wote, na huko bafuni walioga huku wakichezeana, michezo iliyoziamsha hisia fulani nafsini mwao kiasi cha kuoga harakaharaka na kuharakisha kurudi chumbani.

    “Lala chali kitandani nikukande kidogo,” Mwajuma alimwambia mara tu walipoingia chumbani.



    Saad alifanya kama alivyoambiwa. Ikafuata huduma ambayo ilimsisimua na kumburudisha, huduma ambayo hakuwahi kuipata kwa Halima wala kwa mwanamke mwingine yeyote.



    Kisha: “Lala kifudifudi,” aliambiwa tena. Sasa akaminywaminywa mabega na kutomaswatomaswa mgongoni. Mwanamume akajihisi yu paradiso. Akajisikia kama apaaye mbinguni nusu usingizini.



    “Tayari. Sasa lala tena chali.”



    Kwa mara nyingine Saad alifuata maelekezo, ashiki za mapenzi zikiwa zimeutawala mwili wake. Mwajuma akamtazama kwa yale macho yazungumzayo mapenzi, macho yaliyochoka kukodoa, akionyesha dhahiri yu mgonjwa mahtuti.



    Saad alimtazama katika taabu yake ya hitaji la starehe ya mapenzi.



    “Saad,” Mwajuma alimwita, sasa akiachia tabasamu dhaifu, macho yake yakiendelea kusihi.



    “Mwajuma...” Saad naye aliita lakini akasita.



    Mwajuma akamrushia kanga usoni. Alipojaribu kuitoa, Mwajuma alimzuia. Kisha akauhisi uzito wa mwili wa Mwajuma maungoni mwake. Hakuwa na uwezo wa kumzuia, akili yake ilikuwa mbali zaidi, akiihisi starehe aliyoihitaji, pumzi zikimpanda na kushuka kwa awamu. Mwajuma alikuwa akiwajibika ipasavyo.



    “Minya chuchu...” kuna wakati Saad aliambiwa.



    “Nipapase kiunoni...” Mwajuma alibwabwaja katikati ya starehe yao.



    Hatimaye walishtuka!



    Mlango uligongwa!



    Ukimya ukatawala. Mlango ukagongwa tena, safari hii kwa nguvu zaidi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nani?” Mwajuma aliuliza huku akiwa amejing'atua kidogo, lakini bado akiwa amekaa katika hali ya 'kuendelea,' miguu kaisimika kama mwanariadha aliyeambiwa “on your marks,” mikono nayo kaipachika kando ya kifua cha Saad aliyelala chali, katikati ya mapaja manene ya Mwajuma.



    “Mimi!” sauti nzito iliunguruma kutoka nje ya chumba.



    “Wewe?! Wewe nani?” Mwajuma alihoji kwa ukali.



    “Samwel!” sauti ilijibu.



    “Mungu wangu!” Mwajuma alinong'ona. Ujasiri ukamwishia. Akatoka kitandani huku akitetemeka. Akasimama kimya huku akikodoa macho mlangoni.



    Kilikuwa ni kipindi kigumu kwake. Lakini hakukubali kuwa bwege. Hakuiruhusu akili yake kudumaa. Ubongo ukachemka. Akapata uamuzi wa kuutekeleza haraka iwezekanavyo.



    Mara, kama aliyezinduka usingizini, alimvuta Saad na kumpeleka kwenye kabati kubwa ya nguo iliyojengewa ukutani. “Usikohoe wala kutikisika,” alimnong'oneza huku akimtazama kwa macho makali na kumpatia ufunguo wa kabati hiyo.



    Akaongeza, “Mambo yakiwa shwari utafungua na kutoka, lakini ni mpaka nikushtue. Sawa?”



    Hata hivyo Saad hakuwa mtu wa kuambiwa hivyo. Tayari alishakiona kifo hatua chache sana mbele yake. Hakuweza kuwaza chochote cha kumwokoa. Uhai wake alimwachia Mungu. Alikuwa akizisikia tu simulizi za watu kufumaniwa.



    Leo ni yeye aliyefumaniwa!



    “Mwajuma!” sauti kutoka nje iliita kwa ukali.



    “Subiri!” Mwajuma alisema huku akimtupia Saad shati lake kisha akafunga mlango kwa funguo.



    Alipogeuka akaziona soksi na viatu vya Saad sakafuni; akazisukumia uvunguni mwa kitanda kwa mguu. Akaangaza tena macho huku na kule kwa haraka, akitafuta chochote kinachoweza kumletea hisia mbaya Samwel pindi atakapoingia.



    Hakuona kitu!



    Akaufuata mlango!



    MLANGO uligongwa!



    Ukimya ukatawala. Mlango ukagongwa tena, safari hii kwa nguvu zaidi.

    “Nani?” Mwajuma aliuliza huku akiwa amejing'atua kidogo, lakini bado akiwa amekaa katika hali ya 'kuendelea,' miguu kaisimika kama mwanariadha aliyeambiwa “on your marks,” mikono nayo kaipachika kando ya kifua cha Saad aliyelala chali, katikati ya mapaja manene ya Mwajuma.



    “Mimi!” sauti nzito iliunguruma kutoka nje ya chumba.



    “Wewe?! Wewe nani?” Mwajuma alihoji kwa ukali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Samwel!” sauti ilijibu.



    “Mungu wangu!” Mwajuma alinong'ona. Ujasiri ukamwishia. Akatoka kitandani huku akitetemeka. Akasimama kimya huku akikodoa macho mlangoni. Kilikuwa ni kipindi kigumu kwake. Lakini hakukubali kuwa bwege. Hakuiruhusu akili yake kudumaa. Ubongo ukachemka. Akapata uamuzi wa kuutekeleza haraka iwezekanavyo.



    Mara, kama aliyezinduka usingizini, alimvuta Saad na kumpeleka kwenye kabati kubwa ya nguo iliyojengewa ukutani. “Usikohoe wala kutikisika,” alimnong'oneza huku akimtazama kwa macho makali na kumpatia ufunguo wa kabati hiyo. Akaongeza, “Mambo yakiwa shwari utafungua na kutoka, lakini ni mpaka nikushtue. Sawa?”



    Hata hivyo Saad hakuwa mtu wa kuambiwa hivyo. Tayari alishakiona kifo hatua chache sana mbele yake. Hakuweza kuwaza chochote cha kumwokoa. Uhai wake alimwachia Mungu. Alikuwa akizisikia tu simulizi za watu kufumaniwa.



    Leo ni yeye aliyefumaniwa!



    “Mwajuma!” sauti kutoka nje iliita kwa ukali.



    “Subiri!” Mwajuma alisema huku akimtupia Saad shati lake kisha akafunga mlango kwa funguo.

    Alipogeuka akaziona soksi na viatu vya Saad sakafuni; akazisukumia uvunguni mwa kitanda kwa mguu. Akaangaza tena macho huku na kule kwa haraka, akitafuta chochote kinachoweza kumletea hisia mbaya Samwel pindi atakapoingia.



    Hakuona kitu.



    Akaufuata mlango.



    **********



    KULE kabatini Saad hakuwa yule Saad wa kawaida, Saad aliyekuwa na pumzi tosha za uwanaume, Saad ambaye kwa kutumia nguvu zake alimudu kumfanya Mwajuma abwabwaje maneno yasiyoeleweka muda mfupi uliopita. Saad, ambaye hakuwa hata na chembe ya woga pale alipokaribishwa katika kitanda kipana, akadiriki kuchojoa nguo zake zote, na kujigeuza yeye ndiye mmiliki halali, ndiye 'mwenye mali.'



    Hapana, huyu alikuwa ni Saad mwingine, Saad aliyenyong'onyea kimwili na kiakili. Ndiyo, hakuwa na nguvu yoyote. Kabatini humo alijiuliza kwa fadhaa, “Suruali yangu? Viatu vyangu?” majibu hakupatikana, tayari alishachelewa.



    Moyo ukamdunda kwa wasiwasi huku kasimama katikati ya sketi, suruali, magauni hata sidiria za Mwajuma zilizotundikwa kabatini humo.



    Kwa vyovyote vile, kama ni wewe ndiye ungekuwa humo, ukiwa na akili zako timamu, ingekuchukua muda kuituliza akili kufuatia hali halisi ya mazingira uliomo.



    Kwanza, kuna kupaniki; ukitaka kujiokoa, hakuna jingine linalokuja akilini isipokuwa kujaribu kutoroka. Baadaye, mafichoni humo huja woga; fedheha, ugoni, woga wa kupigwa hata kuuawa. Hatimaye hufika wakati wa visingizio; nani wa kulaumiwa, mwanamume au mwanamke? Kisha huja matumaini; labda hatajali, au hatagundua, na wala hatashuku.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Humohumo kabatini Saad aliamua kuvaa shati lake. Lakini shati bila suruali ingemfikisha wapi? Akainama na kuchungulia katika tundu la ufunguo. Akamwona Mwajuma ameshavaa kanga na kandambili akiufungua mlango na kumpisha huyo Samwel.



    Ni hapo ndipo Saad alipofanikiwa kumwona huyo Samwel. Samwel alikuwa mrefu na pande la mtu. Hakuonekana dhahiri kuwa yu mzee kama Hadija alivyodai. Alionekana bado yu mkakamavu kwa kiasi fulani japo kwa mwonekano alionekana kuikanyaga miaka hamsini hivi. Hakutofautiana na jini dume.



    **********



    MWAJUMA alifungua mlango na kumpisha Samwel. Na kabla hata Samwel hajaketi, Mwajuma alimdaka na swali, “Samwel, unatafuta nini saa'izi?! Saa saba!”



    “Yeah, nilikuwa napita tu, nikaona taa inawaka humu ndani. Yaani ulikuwa hujalala hadi saa hizi?”



    “Saa saba hii unapita ukitoka wapi?”



    “Haikuhusu. Hujanijibu swali langu, ulikuwa hujalala mpaka saa hizi?”



    “Ndiyo,” Mwajuma alijibu kwa sauti dhaifu. “Kazi. Kuna viporo vya kazi nilikuwa navishughulikia.”



    “Hadi saa hizi?” Samwel alimkazia macho.



    “Kwani kipi cha ajabu?” Mwajuma naye alijikaza kisabuni.





    Samwel alimtazama kwa macho makali, hali iliyomtia mashaka Mwajuma kwa kuhisi kuwa huenda amezigundua nywele zake zilivyokuwa timtim na macho yake yaliyomwiva. Akashusha pumzi ndefu huku akipiga moyo konde, akiamua kukabiliana na hali yoyote itakayojiri.



    Mzee Samwel aliangaza huku na kule chumbani humo. Kisha akamsogelea zaidi Mwajuma na kumuuliza, “Mwajuma umelewa?”



    “Nimelewa?!” Mwajuma alikuja juu.



    “Jibu swali.”



    “Swali gani hilo?” Mwajuma alimaka. “Kwani tuko mahakamani hapa? Tangu umeingia swali juu ya swali. Kha! Nd'o mambo gani hayo?”



    Mzee Samwel akacheka kidogo, kicheko ambacho kwa hakika hakikuwa hata na chembe ya furaha. Akaendelea kutupa macho humo chumbani. Kisha akauliza, “Ulikuwa busy na nguo za wateja wako?”



    “Kumbe?” Mwajuma alibibitua midomo kisirisiri.



    Licha ya kuajiriwa huko Kariakoo, lakini pia Mwajuma alikuwa na utaalamu wa kushona nguo. Mzee Samwel alishamnunulia cherehani na baada ya mafunzo ya miezi kadhaa hatimaye akawa fundi kamili.



    Mara kwa mara zabuni zikawa zikimfuata hapohapo nyumbani. Lakini kwa siku kadhaa zilizopita, siku kama tano hivi, Mwajuma hakuwa na kazi mpya, na hilo alimwambia Mzee Samwel juzi wakati alipokuja na kukuta kasha la nguo likiwa limefungwa.



    Eti leo anasema alikuwa busy na kazi za watu!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/-

    Viporo!



    Halikumwingia Samwel akilini. Zaidi, mzee huyo alistaajabishwa na harufu ya pombe iliyotoka kinywani mwa Mwajuma huku pia nywele na macho yake vikitoa taswira ya zaidi ya 'ukweli' alioambiwa na mwanamke huyo.



    Akaamua kuuendeleza uchunguzi wake. Akayatupa macho kitandani. Akashangaa zaidi. Kitanda kilikuwa shaghalabaghala! Akayapeleka macho sakafuni ambako aliiona sehemu ndogo ya suruali.



    Akainama na kuivuta. “Hii suruali vipi?” alihoji huku kaining'iniza, akiiangalia kwa makini.



    Ya mteja!” Mwajuma alijibu haraka huku akiinyakua kutoka mkononi mwa Samwel na kuitupa kando, lakini mikono ya Samwel ilikuwa myepesi; aliidaka juu-juu.





    “Ya mteja?” Samwel alihoji kwa kejeli, macho yake makali yakiendelea kuikodolea suruali hiyo. “Hii kali. Suruali hii mpya! Ya dukani! Ina hitilafu gani?”



    “Huwezi kujua,” Mwajuma alizidisha ukali. Akampora tena suruali ile.



    Sasa Samwel akacheka kwa sauti kubwa, sauti iliyofurika tani kadhaa za hasira. Akamtazama kidogo Mwajuma kisha akapapasa uvunguni huku kainama kwa taabu. Huko akazifuma soksi. Akazitoa!



    “Haya! Na hizi soksi pia ni za mteja?” akarusha swali tena. Kisha, bila ya kusubiri jibu, akaongeza, safari hii kwa sauti ya chni zaidi, akisema, “Soksi za nailoni. Ni sawa. Sikatai, lakini nadhani zingeletwa zikiwa zimefuliwa. Au siku hizi una tenda ya udobi?”



    Ganzi ilimvaa Mwajuma. Akakosa jibu.



    Samwel aliendelea kurandaranda huku na kule chumbani humo. Hatimaye akaifuata kabati kubwa ya nguo. Akajaribu kuifungua, haikufunguka.



    “Ufunguo,” alimwamuru Mwajuma. “Nipe ufunguo.”



    “Nini?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ufunguo!”



    “Sina!”



    “Nasema tena... lete ufunguo!”



    “Na mimi nasema, sina ufunguo!” Mwajuma alifoka. “Kwanza unanipotezea muda! Toka! Au nitaita polisi!”



    “Hebu sema tena!”Samwel ni kama alikuwa akiunguruma. Macho yake makali hayakutofautiana na macho ya simba mwenye ghadhabu.



    Mwajuma hakuirudia kauli yake, badala yake alimvaa Samwel na kumvuta huku akimvurumishia ngumi kifuani, ngumi ambazo hazikumtia madhara yoyote ya kutisha Samwel. Kwa usemi mwingine zilikuwa ni “ngumi za kike.” Kuna imani kuwa ngumi yoyote ya mwanamke ituapo maungoni mwa mwanamume, hufananishwa au hulinganishwa na pigo la unyoya.



    Kwa Samwel, magumi yote yaliyotua mgongoni mwake, hayatofautiani na ukunaji wa mtu aliyewashwa upele au ukurutu. Kilichomdhihirishia kuwa Mwajuma alimshambulia kwa dhamira ya kumdhuru ni tusi moja zito, tusi lililofuatishwa na kauli nzito ya kumdhalilisha kijinsia kufuatia udhaifu katika uwajibikaji wake kwenye tendo la ndoa.



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Labda angekuwa ni mwanamume mwingine, angevumilia na kuyasahau maneno hayo ya Mwajuma sekunde chache baadaye. Ndiyo, angekuwa ni mwanamume mwingine, siyo Samwel. Samwel, mtu mzima, ambaye akiwa na akili timamu, na akitambua fika kuwa ana mke na watoto watano wanaozitegemea huduma zake, amediriki kumwinua Mwajuma kimaisha kwa kiwango cha juu kiasi cha kuonekana bayana kuwa yu mwanamke kati ya wanawake mitaani.



    Naam, Samwel hakuvumilia; alimchapa makofi mawili mazito kwa kasi isiyotarajiwa akilini mwa Mwajuma na makofi hayo yakamtupa kitandani sawia.



    “Ufunguo!” kwa mara nyingine Samwel alifoka. “Unatoa ufunguo au hutoi? Ukileta za kuleta, nitaifungua kabati hii kwa njia ninayojua mwenyewe!”



    Kwa mbali machozi yalianza kumtoka Mwajuma pale pale kitandani alipolala.



    “Usilie! Nataka ufunguo!” Samwel aliendelea kufoka, safari hii akiutingishatingisha mlango wa kabati na wakati huo huo akichungulia katika tundu la kitasa.



    Mlango ulikuwa mgumu.



    Samwel akaifuata cherehani iliyokuwa pembezoni mwa ukuta. Akafungua saraka na kutoa bisibisi. Akaifuata tena ile kabati. Akahangaika na bisibisi hiyo kwa takriban dakika moja, akachoka.



    Akaitupa chini.



    Sasa wazo jingine likamjia. Nguvu. Aliona kuwa ni vema atumie nguvu katika kufanikisha azma yake. Akarudi nyuma hatua moja na kurusha teke zito la uzito wa kilo tisini nyuma yake.

    Paa!!



    Lango la kabati likafunguka!



    Uso kwa uso na Saad!



    Papo hapo Mwajuma akazima taa. Labda alifanya hivyo katika kumlinda mwindwa, lakini alikuwa amechelewa. Kwa kasi ya ajabu, mzee Samwel alimkwida shati Saad shingoni.

    Sekeseke likazuka. Japo Saad alivutwa hadi nje ya kabati, hata hivyo hakuwa tayari kufa kikondoo. Alijitutumua na kujinyofoa mikononi mwa Samwel. Lakini Samwel hakukubali, alimwahi Mwajuma na kumshika madhubuti.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwajuma naye hakukubali, wakabiringishana huku na kule kama wendawazimu.

    Lilikuwa ni timbwili-timbwili la aina yake!



    “Nitakuua,” Samwel aliunguruma huku akiisaka shingo ya Mwajuma bila ya mafanikio.



    “Niue! Niue! Nasema niue kama kweli we' ni mwanaume rijali!” Mwajuma naye alibwata, sauti yake ikitoka huku akihemea juujuu. Na papo hapo akafuatisha tusi zito la nguoni.



    Mara Mwajuma akapata upenyo. Akajinasua katika himaya ya Samwel. Akampindua Samwel na kumweka chini. Akamkaba shingo. Kisha akapiga kelele ambazo aliamini zingemsaidia kwa kuwafanya majirani, hata wapita njia waje kumwokoa.



    “Jamanii nakufaaa! Nakufaaa!”



    Naam, yowe hilo lilimsaidia. Muda mfupi baadaye watu wanne, wanaume waliingia ndani humo, mmoja wao akiwa ni Mjumbe wa Nyumba Kumi.



    **********



    WAKATI tandabelua hiyo ikiendelea kati ya Samwel na Mwajuma, kule kabatini Saad aliamua kuchukua uamuzi wa kujinusuru bila ya kusubiri kibali cha Mwajuma. Akafungua mlango wa kabati taratibu na kutioka.



    Kisha akaikimbilia suruali yake na kuvaa haraka haraka huku akishuhudia Mwajuma kamkandamiza Samwel sakafuni na kumwagia matusi ya 'kufa-mtu.'



    Akaamini kuwa siyo rahisi Kwa Samwel kujinasua haraka, hivyo naye kwa wepesi uleule akavaa viatu na soksi. Akafungua mlango na kutoka, lakini akasita. Umati wa watu ulishafurika nje ya chumba.



    “Fumanizi!” kijana mmoja aliropoka.



    “Ni walevi hao,” mwingine alisema.



    “Tusiwaachie hivi hivi, tuingie tuwasuluhishe!” wa tatu alisema.

    Mara wakauvaa mlango na kwenda kuingilia kati tandabelua baina ya Mzee Samwel na Mwajuma. Mzee Samwel akanywea.



    Huyu alisema hivi, yule akasema vile. Lakini Saad hakuwajali. Alitoka taratibu na kuwaacha baadhi ya watazamaji wakimshangaa. Ilikuwa ni usiku wa manane, lakini alikuwa na matumaini....



    Akatokomea!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog