Chombezo : Aah Shemeji ... Achaaa !
Sehemu Ya Tano (5)
AISHA alimpigia simu shemejiye akamweleza kisha kumtaka aende akamchukue. Bw. Abdul aliingiwa na woga aliwaza kuwa pengine watu wote walishagundua uhusiano wake na Aisha hivyo alimtaka Aisha achukue teksi na kuelekea mahali ambapo yeye atakuwepo. Aisha baada kupaki mizigo yake yote alifanya kama alivyoagizwa. Muda mchache Aisha alifika pale na kukuta Bw. Abdul amepaki gari lake. Bw. Abdul alitoka ndani ya gari, wakasalimiana na Aisha kisha akamlipa yule dereva pesa alizokuwa akidai, walipakiza mizigo kisha nao wakaingia ndani ya gari. Aisha alikuwa akibubujikwa na machozi aliwaza jinsi atakavyomkabili dada yake. Bw.Abdul alimsihi Aisha aache kulia kisha alimshauri kuwa siku ile ni vyema wakarudi wote nyumbani kwa kuwa ujauzito wenyewe bado ni mdogo hivyo haitakuwa rahisi dada yake kugundua. Alimwahidi kuwa baada ya mwezi mmoja atampangia nyumba . Pia alimshauri kuwa endapo dada yake akimuuliza, aseme kuwa amepewa ruhusa kwa kuwa anaumwa.
Bw. Abdul alijua kuwa haitakuwa rahisi kwa Nasra kugundua kuwa mdogo wake ni mjamzito, ukizingatia kuwa hawajaonana kwa kipindi kirefu sana. Aisha alikubali wazo la shemejiye. Bw. Abdul aliwasha gari taratibu na kuelekea nyumbani. Aisha alijifanya yu mgonjwa kwelikweli, hali iliyomfanya dada yake kumwonea huruma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****
Ilikuwa majira ya saa mbili asubuhi wakati Nasra akiwa anafanya usafi wa nyumba. Akiwa chumbani kwa Aisha akifanya usafi aliona karatasi nyeupe sakafuni iliyofungwa vizuri. Nasra aliiokota na kuifungua taratibu kisha kuanza kuisoma. Nasra hakuamini alichokisoma katika karatasi ile. Aliiweka karatasi ndani ya mfuko wa suruali aliyoivaa kisha akaendelea na usafi. Muda mfupi Aisha alitoka bafuni na kuelekea chumbani kwake ambapo alimkuta dada yake akiendelea kufagia. Walisalimiana kwa furaha kama hakukuwa na kitu kilichotokea. Wakati Aisha akitafuta nguo ya kuvaa ndani ya begi lake ndipo alipogundua kuwa ile barua ya kufukuzwa chuo haikuwamo ndani ya begi. Alipigwa na butwaa na kushindwa la kufanya. Mawazo yalimzidi, alihisi kuwa huenda dada yake amegundua. Nasra alikumbuka maneno aliyoambiwa na mama Sada ndipo siku moja alipoamua kukagua simu ya mumewe. Nasra hakuamini macho yake, kwani zilikuwa ni meseji za mapenzi tu zilizotawala ndani ya simu ambazo alitumiwa na Aisha. Bw. Abdul hakuwa na wasiwasi wa kuzifuta kwa kuwa Nasra hakuwa na tabia hata ya kugusa simu ya mumewe. Hata ikiwa inaita huiacha kisha mwenyewe akirudi humwambia kuwa kuna mtu alikuwa akimpigia simu.Hicho ndicho kilichomtia imani Bw.Abdul hadi kusahau kuzifuta.Ama kweli siku ya kufa hakuna anayeijua.
Nasra aligundua kuwa Aisha alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na shemejiye, pia mimba aliyokuwa nayo ilikuwa ya Bw.Abdul. Nasra hakuonyesha kuwa kuna kitu alichokigundua alikaa kimya kama asiyejua lolote.
Chakula cha mchana kilikuwa tayari. Nasra aliandaa chakula ndani ya chumba cha Aisha kwa kuwa alimwona mdogo wake kuwa ni mgonjwa hivyo hakutaka kumsumbua kwenda kula sebuleni. Kmbe alikuwa akionyesha upendo wa dhati huku akiwa na jambo lake moyoni. Aliandaa juisi nzuri kwa ajili ya mgonjwa.
“Jitahidi kunywa juisi mdogo wangu itakusaidia kupata nguvu.”
“Sawa dada nitajitahidi.”
Dakika chache tu kupita kabla ya Aisha kumaliza chakula ghafla alianza kuugulia maumivu ya tumbo. Nasra alijifanya kushtushwa na ugonjwa . Alihangaika huku na huko asijue cha kufanya. Baada ya kuona sasa mipango yake inaelekea kukamilika ndipo alipotwaa simu yake ya mkononi na kubofya namba mbalimbali kisha kuiweka sikioni.
“Haloo!Mume wangu njoo haraka nyumbani kuna tatizo.”
“vipi tena dear mbona unanitisha kuna nini?”
“Aisha anaumwa.”
“Sawa nakuja.”
Bw. Abdul alitoka ofisini kwa haraka bila ya kuongea na mtu. Watu walimshangaa kwani haikuwa kawaida yake.Siku zote anapotaka kutoka huwa anawaaga wenzake. Alifungua milango kwa haraka na kuanza kutimua mbio hadi mahali alipoegesha gari lake. Alifungua mlango na kuingia kisha akaanza kuendesha kwa mwendo wa kasi bila kuangalia kilichokuwa mbele yake. Ghfla alifunga breki baada ya kumkosakosa mwanamke mmoja aliyekuwa akivuka barabara.
Mpumbavu we! Unaendesha gari kama mwendawazimu huangalii hata kilichopo mbele. Bw. Abdul hakujali maneno ya yule mwanamke kwani akili yake ilikuwa kwa Aisha, kipenzi chake cha roho aliyeweza kumwonesha raha za dunia. Dakika chache alikuwa amefika nyumbani . Alisimama kwa haraka kisha akashuka ndani ya gari alitembea kwa haraka hadi chumbani kwa Aisha aliingia ndani bila ya kubisha hodi.
“Ehee!Vipi jamani.”
“Hali ndo’ kama hiyo unayoiona.”
“Basi bila ya kupoteza muda,jiandae tumpeleke hospitali.”
“Mbona amekuwa kama mtu aliyekunywa sumu, mpe maziwa kwanza.”
Nasra alishtuka kusikia maneno hayo alihisi kuwa huenda mipango yakeikagundulika. Alienda sebuleni, akafungua jokofu na kutoa paketi moja ya maziwa. Alifungua na kuyamimina ndani ya glasi kisha alielekea chumbani. Bw. Abdul alimpokea ile glasi na kumnywesha Aisha. Baada ya dakika chache Aisha alitapika. Bw. Abdul alihisi kuwa huenda mke wake amemwekea sumu mdogo wake. Pamoja na kutapika lakini hali ya Aisha haikuwa nzuri hivyo walikubaliana kumpeleka hospitali. Walimnyanyua mmoja kichwani na mwingine miguuni. Walimwingiza ndani ya gari huku Nasra akiwa amempakata. Bw. Abdul aliingia ndani ya gari na kuendesha kwa haraka .
Iliwachukua takriban dakika kadhaa kuwasili hospitali. Bw.Abdul ndiye aliyekuwa wa kwanza kushuka ndani ya gari. Aliwashauri wabaki kwanza wakati yeye akielekea mapokezi.Daktari alimshauri ampeleke mgonjwa. Bila ya kuchelewa Bw Abdul alielekea mahali walipokuwa wameegesha gari. Walimbeba mgonjwa na kumpeleka kwa daktari. Daktari alishtuka baada ya kumwona Aisha akiwa katika hali mbaya aliwashauri kumpatia maziwa lakini Bw Abdul alieleza kuwa tayari walishampatia maziwa.
“Baada ya kumpa maziwa ilikuwaje.”
“Alitapika sana.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sawa basi nyinyi nendeni nje kidogo ili niendelee kumfanyia uchunguzi kisha nitawaita baadaye. Bw Abdul na mke wake walitoka nje. Daktari akaanza kumhoji Aisha.
“Vipi unajisikiaje.”
“Tumbo ndilo linalonisumbua.”
“Lilianzaje.”
“Nilikuwa nakula chakula baada ya kunywa juisi ndipo mara tumbo likaanza kuniuma.”
“Sawa.”
Daktari aliendelea na uchunguzi. Majibu yalionyesha kuwa mgonjwa alikuwa amepewa sumu.Daktari hakusita kumweleza ukweli Aisha.
“Samahani kwani yule dada unamwitaje.”
“Ni dada yangu, baada ya kuzaliwa yeye ndo nkazaliwa mimi.”
“Wakati anaandaa chakula alikuwa na nani.”
“Alikuwa peke yake.”
“Ok! Majibu yanaonyesha kuwa umekunywa juisi iliyowekwa sumu, je unadhani dada yako anaweza kukufanyia hivyo?”
“Inawezekana.”
“Basi mi nataka nikusaidie ila tukubaliane.”
“Tukubaliane nini.”
“ Mimi nimetokea kukupenda niko tayari kukuoa kwani mi sina mke.”
Daktari alijikuta akitupa vidongo vyake kwa Aisha kwani alishindwa kuvumilia kuliacha lile liumbo kumpita hivihivi. Aisha naye kwa kuwa alikuwa ni mwingi wa habari hakusita kumkubalia. Daktari alifurahi baada ya Aisha kukubali ombi lake hivyo alifanya kila njia kunusuru maisha ya binti yule ilimradi tu mwishowe aje kula tunda. Baada ya mazungumzoyale daktari alimwita Bw Abdul na kumpatia majibu ya mgonjwa wake ambayo yalionyesha kuwa alikuwa amekunywa juisi iliyowekwa sumu. Pia alikuwa na ujauzito ambao umeharibika kutokana na sumu hiyo. Hivyo inatakiwa afanyiwe operesheni.
Daktari alijikuta akitupa vidongo vyake kwa Aisha kwani alishindwa kuvumilia kuliacha lile liumbo kumpita hivihivi. Aisha naye kwa kuwa alikuwa ni mwingi wa habari hakusita kumkubalia. Daktari alifurahi baada ya Aisha kukubali ombi lake hivyo alifanya kila njia kunusuru maisha ya binti yule ilimradi tu mwishowe aje kula tunda. Baada ya mazungumzoyale daktari alimwita Bw Abdul na kumpatia majibu ya mgonjwa wake ambayo yalionyesha kuwa alikuwa amekunywa juisi iliyowekwa sumu. Pia alikuwa na ujauzito ambao umeharibika kutokana na sumu hiyo. Hivyo inatakiwa afanyiwe operesheni.
Wakati akifanyiwa operesheni iligundulika kuwa kizazi kilikuwa kimeoza hivyo waliamua kumtoa.Baada ya matibabu daktari mkuu aliitisha kikao cha madaktari wote.
“Madaktari wenzangu, kama mlivyoona yule mgonjwa amepewa sumu nami naona huu ni ukatili wa hali ya juu hivyo itabidi tuwapigie simu polisi au mnasemaje?
“Hata mimi nimesikitika sana na jambo hili, huo ni uamuzi wa busara.”
Wote walikubaliana. Kikao kikafungwa daktari mkuu alielekea katika ofisi yake kisha alitwaa simu yake ya kiganjani na kubofya namba mbalimbali kisha aliiweka sikioni.
“Haloo!Kituo cha polisi cha kati hapa tukusaidie nini.”
“Mimi ni daktari mkuu katika Hospitali ya Msomeni, kuna mgonjwa aliletwa jana hapa hospitali lakini imegundulika kuwa amepewa sumu hivyo tunaomba msaada wenu.”
“Hao wahusika wapo hapo?
“Ndiyo.”
“Sawa tunakuja sasa hivi.”
Baada ya mazungumzo yale daktari aliiweka simu yake mfukoni kisha aliwaita Bw Abdul na mkewe. Aliwaeleza gharama zote za matibabu. Bw Abdul aliingiza mkono mfukoni na kutoa kitita cha fedha kilichozidi gharama ya matibabu na kumkabidhi daktari. Daktari bila kusita alikipokea na kukitia mfukoni. Bw Abdul alijua kuwa hapo aliweza kumziba mdomo daktari ili asitoe siri lakini haikuwa hivyo. Kabla ya kuagana ghafla mlango ulifunguliwa. Walikuwa ni polisi. Waliwafunga pingu Bw Abdul na mkewe kisha waliwapandisha ndani ya basi kuwapeleka kituoni. Baada ya kufika kituoni kila mmoja kwa muda tofauti aliitwa ndani ya chumba cha kutolea maelezo. Polisi waliwakabidhi karatasi kwa ajili ya kuandika maelezo. Kila mmoja alijaza porojo zake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya kuandika maelezo wote walifungiwa katika chumba kimoja. Baada ya muda mfupi rafiki wa Bw Abdul aliyejulikana kwa jina la Dickson ambaye walikuwa wakifanya kazi pamoja aliwasili kwa ajili ya kumtolea dhamana rafiki yake. Bw Abdul alifanikiwa kutoka lakini Aisha hakuruhusiwa.
Wakati kesi ikiendelea Bw. Abdul alimchukua Aisha na kuishi naye kama mke na mume. Kwa wakati wote huo Aisha hakuonekana mwenye furaha kwani aliwaza kuwa hataweza kuzaa tena katika maisha yake yote. Bw. Abdul alijitahidi kumfariji kwa kumpeleka sehemu mbalimbali za starehe.
Hata hivyo Aisha alijitahidi kusahau hali aliyokuwa nayo lakini hakuweza kuwa na raha kama alivyokuwa hapo awali.
Nyakati za usiku katika ile kona ya watu wazima Aisha hakuweza kuonyesha manjonjo kama yale ya awali yaliyomfanya Bw. Abdul kupagawa hadi kumsahau mkewe. Bw. Abdul alijitahidi kumstarehesha kwa kila hali ilimradi tu aweze kupatiwa mapenzi adimu.
Kadiri muda ulivyozidi kwenda ndipo Aisha alipozidi kusahau na kujikuta mwenye furaha. Aisha alipatiwa kila alichokihitaji na kujiona kama mke wa ndoa kwa Bw. Abdul.
******
Ilikuwa siku ya Jumapili asubuhi wakati Bw. Abdul akijiandaa kwenda kazini ndipo alipomtaka Aisha kujiandaa ili jioni akirudi kazini waende kujivinjari,kula bata kwenye sehemu zinakofanyika starehe.
“Mpenzi mi natoka lakini sitachelewa kurudi naomba ujiandae ili jioni twende katika sehemu zinakofanyika starehe, sijui we unapenda twende wapi?”
“Ehee! Tena ni bora ulivyopanga siku ya leo. Si unajua mi ninavyopenda Taarabu.Leo Five Stars wanatumbuiza Dar Live naomba twende huko mpenzi.”
“Hukuna shida mpenzi kwani hata mimi si unajua kuwa ni mbovu wa Taarabu. Basi naomba upendeze sana ili tukifika huko kila mmoja atushangae.”
Bw. Abdul alimshika mikono Aisha na kumnyanyua kutoka pale alipokuwa amekaa kisha akambusu shavu la kulia halafu akamgeuza shingo ili kumbusu shavu la kushoto halafu akaigeuza tena shingo na kumfanya watazamane, alikutanisha midomo yao kisha akaingiza ulimi wake ndani ya mdomo wa Aisha kwa ajili ya kubadilishana mate. Hii ilikuwa ni kawaida yao wanapoagana. Kwa kuwa Bw. Abdul alikuwa ni mtu wa mikiki muda wote basi kwa kitendo kile tu tayari alishapandwa na mihemko na kutaka kufanya mikiki. Hata hivyo Aisha alijitahidi kumtuliza na kumtaka awahi kazini pia alimwahidi kuwa watakutana baadaye kunako sita kwa sita. Aisha alichukua begi la Bw.Abdul kisha wote walitoka nje.Walielekea mahali wanapoegesha gari lao.Bw Abdul aliingia ndani ya gari kisha Aisha alimkabidhi lile begi. Bw. Abdul aliwasha gari na kuanza kuondoka taratibu huku akimpungia mkono Aisha. Pale aliposimama Aisha alimwangalia Bw. Abdul huku akimpungia mikono na machoni alikuwa akibubujikwa na machozi. Aisha alishamzoea sana Bw. Abdul hivyo muda anaokaa peke yake hujihisi mpweke.
Jioni ilpofika Bw. Abdul aliwasili nyumbani. Alimkuta Aisha akiwa tayari kwa safari.
“Habari za kushinda mpenzi?”
“Nzuri tu habari za kazi?”
“Njema kabisa, vipi upo tayari kwa safari?”
“Kwani we unanionaje?”
“Hakika tangu nianze kukujua siku ya leo ndo umependeza kuliko siku zote. Sina imani na huko tuendako nahisi kama nitaibiwa.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Acha utani wako dear, ni mwanamume gani anayeweza kumtoa Aisha katika ubavu wa Bw Abdul?”
“Sawa mpenzi najua kuwa wanipenda sana, asante.Tutoke basi.”
Walitoka nje huku wameshikana mikono. Bw Abdul alimkabidhi funguo Aisha na kumtaka aendeshe gari.
“Mmm! Mpenzi nitaweza kweli?”
“Mbona yale mambo mengine unayaweza, utashindwaje kuendesha gari?”
“Acha utani bwana.”Aisha alisema huku akimpiga kikofi cha mahaba Bw Abdul.
Bw Abdul alichukua funguo na kuanza kuendesha gari kwa mwendo wa polepole. Aisha kama kawaida yake na vile viguo vyake. Leo alikuwa amevaa kimini kilichoacha wazi sehemu kubwa ya miguu hadi mapaja. Alikaa ule mkao wa kukunja nne. Basi na yale mamiguu yake yalivyo manene, mipaja myeupe, inayomelemeta ilikuwa imejaa katika ile siti aliyokuwa amekaa. Ilimfanya Bw Abdul kupoteza mwelekeo wa kuendesha gari na kujikuta akiikodolea macho ile mipaja. Bw Abdul uvumilivu ulimshinda hivyo alipaki gari pembeni na kuanza kumparamia Aisha. Aisha hakukubali kuruhusu kitendo kile kuendelea lakini mwishowe alilegea na kuruhusu lolote litakalotokea. Bw Abdul alipandisha vioo vya gari ambavyo vilikuwa na rangi nyeusi isiyomruhusu mtu wa n je kuona ndani. Dakika kama mbili hivi kupita gari lilianza kutikisika pasipo kuendeshwa. Watu waliokuwa karibu walishangaa lakini wengine walielewa kinachofanyika ndani. Basi mechi ilichezwa na katika dakika ya kumi hatimaye mpira uliweza kutikisa nyavu na kupata ushindi. Walikuwa kama watu waliotoka kupandisha kilima walitokwa na jashopia walikuwa na uchovu mwingi.
“Daah!Mpenzi hii ni aibu lakini na wewe umezidi sana kunitega.”
“Kwenda zako huko kwanza mi nimechoka hata huko sitaweza kwenda tena,ni bora turudi nyumbani tutaenda tena siku nyingine.” Walikubaliana kurudi nyumbani kisha walipanga wikiendi ijayo kwenda tena wakati Jahazi Modern Taarab ikitumbuiza.
Wiki moja haina siku nyingi ni saba tu na hatimaye zilifika. Aisha kama kawaida yake na viguo vyake wala hakuhofia kuvunjika tena kwa safari. Leo alivaa kagauni kafupi ka rangi ya kijani kisha akafunga mkanda mnene wa rangi nyekundu na viatu vyekundu pia alitengeneza nywele zake kwa staili ya kuvutia. Siku zote Aisha hupendeza lakini leo amependeza sana. Bw Abdul naye alitinga pamba za kisharobaro na micheni. Walitoka nje huku kila mmoja akimsifia mwenzake kuwa amependeza sana. Pia walikubaliana kutokuvunja safari kwa uchu wa mapenzi. Walielekea mahali walipoegesha gari.Walipofika waliingia ndani ya gari bila ya kupoteza muda.Bw Abdul hakurudia tena ule ezembe alioufanya mwanzo. Aliendesha gari kwa mwendo kasi. Kwa kuwa barabara ilikuwa imekamilika hivyo haikuwachukua muda mrefu waliwasili Mbagala. Bango lililoandikwa DAR LIVE liliwaambia kuwa ni hapa. Walipaki gari kisha taratibu waliingia ukumbini. Kila aliyemwona Aisha alishindwa kuendelea na kazi aliyokuwa akiifanya, macho yote yalikuwa kwa Aisha. Hadi wanaopiga vyombo vya muziki walitahayari. Bw Abdul alimshika Aisha mkono na kujongea hadi kwenye kona na kuanza kuserebuka. Wanaume waliwaacha wanawake waliokwenda nao na kwenda kucheza na Aisha. Bw Abdul alichukia lakini Aisha hakujali alicheza na watu wote waliokuja kucheza naye. Majira ya saa nane walikuwa wametosheka na muziki hivyo waliamua kuondoka. Muziki uliendelea lakini watu waliona ukumbi umepooza baada ya kuondoka kwa Aisha hivyo wengine waliamua kuondoka.
*****
Kesi ya Nasra ilikuwa imesomwa na kupangiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja. BwAbdul alikuwa akienda kumwona mke wake mara kwa mara na kumpelekea zawadi. Nasra alikuwa akimuuliza mume wake kuhusu Aisha lakini Bw Abdul alimweleza kuwa alimpeleka nyumbani kwao. Muda wa kuwa kifungoni Nasra ulikuwa umeisha ingawa Bw Abdul hakuwa na kumbukumbu. Mawazo yake yote yalikuwa kwa Aisha.
Ilikuwa siku ya Jumapili ambayo ni siku ya mapumziko kwa Bw Abdul. Majira ya saa kumi na mbili jioni Aisha na Bw Abdul walikuwa chumbani wamepumzika. Nasra alifika mlangoni na kukuta mlango ukiwa wazi. Aliingia sebuleni lakini hakuona mtu.Alielekea chumbani. Ghafla alishtuka baada ya kumkuta Bw Abdul akiwa na Aisha chumbani wamelala. Alijikaza na kutoka taratibu. Alielekea sebuleni na kuchukua kisu, alitembea kwa kunyata hadi chumbani. Alishika kisu kwa mikono miwili, alifumba macho na kukitua kwa nguvu hadi kifuani kwa Aisha. Ulisikika mguno mdogo ambao usingeweza kumwamsha mtu toka usingizini kisha alikichomoa kwa haraka na kurudia tena ambapo safari hii kilimpata Bw Abdul shingoni. Alisali sala ya mwisho kisha naye alijichoma tumboni.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****MWISHO******
0 comments:
Post a Comment