Chombezo : Mwagia humo humo
Chombezo : Kumbe Vikiungwa Vitamu
Sehemu Ya Pili (2)
Lakini pamoja na yote sikuwa na sifa ya kumteka mwanaume kimapenzi zaidi ya kunionja na kuniacha. Wasiwasi wangu huenda mwili wangu hauna asali itakayo mfanya mwanaume yoyote atakaye nionja anirudie mara mbili. Basi baada ya kupokea aligeuka na kuondoka kurudi ofisini kwangu.
Nilipofika mlangoni nilikumbuka kitu nilitaka kumuuliza bosi, niligeuka ili nimuulize kitu. Niligeuka ghafla na kukutanisha macho na bosi ambaye kumbe nyuma yangu alikuwa akinifuatia. Maskini kaka wa watu alishtuka mpaka akadondoka chini, nilijikuta namuonea huruma.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilirudi hadi chini alipokuwa amekaa bila kuonesha kujinyanyua, mwili wake haukuwa mkubwa sana nilimshika mkono ili kumnyanyua.
“Hapana Manka nitanyanyuka mwenyewe.”
“Hapana bosi naomba unipe mkono,” nilimwambia kwa sauti ya huruma yenye kubembeleza. Alinipa mkono na kumnyanyua, baada ya kunyanyuka nilitoa kitambaa changu na kumfuta sehemu yenye vumbi.
“Tosha Manka sehemu zingine nitafuta mimi.”
“Hapana bosi ni wajibu wangu kufanya hili.”
Aliniacha nimfute kisha nilimtengenezea kiti na kumuomba akae.
“Unaweza kukaa.”
Bila kuongeza neno alikaa kwenye kiti chake huku uso wake ukionesha aibu imemtawala.
“Pole bosi,” nilimwambia kwa sauti ya chini.
“Asante.”
“Hukuumia?”
“Nipo sawa.”
“Pole sana.”
“Asante Manka, nipo sawa kaendelee na kazi.”
Niligeuka na kuondoka hata nilichotaka kumuuliza nilikiacha na kupanga kumuuliza kupitia simu yangu ya mezani. Nilitoka hadi ofisini kwangu kuendelea na kazi, kabla ya kuanza kazi nilijikuta nikijiuliza kilichomdondosha bosi wangu ni nini.
Wasiwasi ulikuwa uleule bosi kapagawa na mimi, kitu ambacho sikutaka kinitokee kwa muda ule kwani ilikuwa mapema sana. Niliamini kabisa bosi kwa mtazamo wa nje alikuwa amepata bonge la mwanamke, lakini ndani sikuwa na sifa zile za kukaa na mwanaume kwa muda mrefu.
Niliyapuuza na kuendelea na kazi, nilikumbuka kuna kazi nilitaka kupata maelekezo kwa bosi. Nilimnyanyua simu kumpigia baada ya kuita kwa muda ilipokelewa.
“Haloo bosi.”
“Ooh..Aah...Nani Manka,” maskini bosi wangu alionesha kiwewe bado hakijamtoka.
“Bosi mbona hivyo?”
“Aah, kawaida tu, unasemaje?”
“Ok, bosi nilikuwa nauliza hii kazi ya malipo kuna maandishi ya mkono nayo niyaandike?”
“Hakuna tatizo, yaandike kama ilivyoandikwa.”
Nilikata simu na kuendelea ka kazi yangu kama kawaida, baada ya muda nikiwa bize simu ya mezani iliita, nilinyanyua na kupokea.
“Haloo bosi.”
“Ndiyo Manka jiandae tukapate lunch.”
“Nashukuru bosi.”
Baada ya kukata simu, niliangalia saa kubwa ya ukutani iliyokuwa mbele yangu, ilionesha ni saa saba kasoro kumi mchana. Nilimalizia kazi yangu ili nipate muda wa kwenda kula, nikiwa bado nimeinama nikirekebisha tatizo la kisarufi nilishtuliwa na sauti ya bosi.
“Manka tunaweza kwenda.”
“Hakuna tatizo bosi, namalizia kurekebisha sarufi.”
“Utamalizia tukirudi.”
Nilisave kisha nilizima computer na kunyanyuka, nilijitengeneza vizuri nguo niliyovaa. Kwa chati nilimuona bosi wangu koo likimcheza kama mtu mwenye kiu kikali. Baada ya kuhakikisha nipo sawa tulitoka hadi kwenye gari lake kisha tulikwenda kwenye moja ya hoteli ya kifahari ambayo ilinikumbusha mbali enzi nipo kwenye ndoa yangu.
Tulipofika Mateja alionesha kutojiamini sana kwangu kitu ambacho sikuamini mwanaume kama yeye kuwa katika hali ile. Sikuwa na sifa kubwa zaidi ya mwanamke aliyepoteza matumaini ya kupata hadhi mbele ya mwanaume. Niliamini kaniona kwa nje hanijui ndani nilivyo ndio maana ananipapatikia.
Nilijua akikipata anachokitafuta kwangu pengine ndiyo siku ya kunifukuza kazi, lakini sikuwa na jinsi kila mwanaume mwenye pesa aliamini mwanamke sahihi wa kukaa naye ni mimi. Baada ya kuketi kwenye viti vyetu muhudumu alifika na kutaka oda zetu.
“Manka agiza chochote ukitakacho kwa bei yoyote.”
“Asante, nataka kula unachokipenda wewe,” utanishangaa kwa nini nimesema vile, nilifanya vile ili kumtoa wasiwasi na kumfanya awe huru kwangu japo si katika suala la mapenzi.
“Hapana Manka nataka wewe leo ndio uchague chakula tutakacho kula.”
“Sawa,” nilichagua chakula ambacho wote tulikuwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya chakula wakati wa kunywa vinywaji Shaka aliniuliza.
“Samahani.”
“Bila samahani.”
“Manka, umeolewa?”
“Sijaolewa.”
“Una mchumba sina?”
“Sina.”
“Rafiki wa kiume?”
“Sina.”
“Manka mbona unanidanganya.”
“Kweli bosi.”
“Hivi Manka kwa umbile alilokujali muumba usiwe na mwanaume?”
“Si kwamba sijawahi mwanaume ila kwa sasa sina.”
“Kweli?”
“Kweli kwa nini nikufiche ili iwe nini?”
“Mara nyingi watu wamekuwa si wakweli.”
“Huo ndio ukweli wangu.”
“Kwa nini mrembo kama wewe huna rafiki wa kiume?”
“Sina bahati nimeamua kuishi peke yangu.”
“Ina maana hata ombi langu litagonga ukuta?”
“Ombi gani?”
“Kwa vile huna mtu nilifikili unafaa kuwa mke wangu.”
“Aaah, bosi,” kauli ile ilinishtua sikupenda kuisikia masikioni mwangu.
Sikuwa na jibu la moja kwa moja, moyo mapigo ya moyo walinienda mbio na machozi yalinitoka. Mateja alishtuka kuniona nikitoka machozi badala kumpa jibu lake.
“Manka vipi?”
“Hataa,” nilitikisa kichwa.
“Mbona machozi yanakutoka.”
“Kauli yako imenishtua.”
“Kivipi?”
“Sikutegemea kuniambia neno hilo mapema kiasi hiki.”
“Manka, penzi limuingiapo mtu huwa kama kichaa aliyekatikiwa na mishipa ya fahamu. Niyasemayo si mimi ni moyo wangu naomba unihurumie.”
“Ni kweli, lakini sina bahati kila siku mapenzi limekuwa likinitesa.”
“Kivipi?”
“Mpaka leo sijajua sababu ya kuachwa na wanaume.”
“Ni wazi wote waliopita walikuwa na tamaa ya kukujua ulivyo na si mapenzi ya dhati. Lakini nakuamini mimi ndiye mwanaume sahihi kwako.”
“Hiyo kauli kwangu nimeizoea, lakini mwisho wa siku mambo huwa kinyume.”
“Niamini Manka, nitakuwa mume mwema.”
“Mmh nitashukuru, lakini usinitende utaniumiza.”
“Siwezi.”
Baada ya chakula tulirudi ofisini, hatukufanya sana kazi Mateja alikuwa na uchu wa fisi. Aliniomba tufunge ofisi twende tukastarehe, sikuwa na pingamizi nilifunga kazi na kuongozana naye kwenye gari lake. Mateja alinipeleka kwenye hoteli ya kifahari ya nyota tano.
Kwa vile shida yake niliijua sikushtuka kumsikia akiuliza chumba cha VIP, baada ya kulipia tulikwenda kwenye chumba kilichokuwa ghorofa la pili. Chumba kilichokuwa cha kifahari, ambacho kilikuwa kipo katika hadhi ya juu. Katika maisha yangu sikuwahi kuingia kwenye chumba kizuri kama kile.
Chumba nilikiona kilikuwa kinapendeza lakini wasiwasi wangu bosi wangu atakipata alichokifikilia kukipata mwilini mwangu. Sikutaka nami kijiweka nyuma kwani nilikumbuka kauli za Bi Shuu mama mlezi wangu shangingi mstaafu, kuwa niwapo mbele ya mwanaume nijionesha nipo tayari kumpa kile anachokitaka.
Siku zote aliniambia nijiamini ili kumfanya mwanaume naye ajiliuze mara mbili mbili ataniingiaje. Sikupoteza wakati baada ya kuingia tu chumbani nilivua nguo zote na kubakia kama kuku aliyenyonyolewa. Sikuchelewa kumsaula na yeye tukawa sale sale maua.
Nilitembea kama miss kuelekea kwenye kabati kuchukua taulo kwa makusudi nimuoneshe umbile langu ambalo mwanzo huwa utata kwa wanaume.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini wakiisha nipata nakuwa kama Big G iliyotafunwa na kuisha utamu mwisho wake hutemwa. Kwa kweli sikupenda kutongozwa siku moja na siku hiyo hiyo kumvulia mwanaume nguo ya ndani.
Niliamini kabisa kujilahisi vile lazima thamani yangu ingepungua lakini kama ningemzungusha, kidogo thamani yangu kwake ingepanda. Nilijua lazima ataniona maharage ya Msanga maji nusu kijiko. Lakini sikuwa na jinsi kutokana na njia aliyotumia kwa kweli nilijikuta siwezi kuuruka mtego wake mwepesi. Sikuwa ndege mjanja lakini nilinaswa kijinga sana, japo sikujua tatizo langu lakini nilipokuwa natembea na kumuachia umbile la nyuma lililokuwa linawatesa wanaume wengi. Niliinama makusudi kama najikuna mguu ili tu nizidi kumpagawisha.
Kitu kilichofanya Mateja azidi kuwa katika wakati mgumu, wakati nafungua kabati nitoe taulo Mateja alikuwa tayari yupo nyuma yangu na kunikumbatia kwa nyuma. Nilijua uzalendo ulikuwa umemshinda, mambo yalianzia pale.
Tulianza kubadilishana mate palepale kwenye kabati, baada ya muda aliona anachelewa, mwanaume alinibeba juujuu mpaka kitandani. Kwa vile mchicha ulikuwa umeishakolea nazi tuliumwaga juu ya ubwabwa na kuanza kujimegea tataribu. Mateja alionekana ana pupa kama mamba mwenye njaa, hakuchelewa kukifikisha chombo ukingoni mwa bahari.
Baada ya mapumziko mafupi tulirudi ndani ya ngarawa kuendelea na safari, katika vitu ambavyo katika maisha yangu nilikuwa sivipendi ni usumbufu ndani safari. Ooh geuka hivi, lala hivi, inama hivi, nyanyuka hivi, kwa upande wangu niliona usumbufu lakini nilivumilia kwa vile ndiyo ilikuwa siku yetu ya kwanza kukutana.
Kama ningekuwa nimemzoea ningempasha, kwani hakuna starehe ya mapenzi mpaka kusumbuana kumgeuza mwenzako kituko,ile kwangu sikuona mapenzi zaidi ya adhabu. Siku zote niliamini baada ya safari ndefu mtu humwaga mzigo na kutelemka. Siku ile tulikaa kaa mpaka saa tatu usiku baada ya kuoga na kula alinirudisha nyumbani.
Kabla ya kuondoka Mateja aliniahidi vitu vingi ikiwemo kunijengea nyumba kuninunulia gari na kuyabadili maisha yangu kwa ujumla. Siku ile moja tu alinipatia laki tano taslimu, sikuamini niliona miujiza kupata raha na kiasi kikubwa cha pesa kama kile.
Nilipofika nyumbani nilimkuta Bi Shuu yupo chumbani kwake, Nilifungua mlango wa chumba changu na kuingia ndani. Nilipowasha taa nilishtuka kumuona Bi Shuu kanisimamia nyuma, akuzungumza chochote ila alinikata jicho kali.
“Shikamoo Bi Shuu”
“Hainisaidii kitu”
“Mbona hivyo mama yangu”
“Kazi gani ya kutoka saa moja asubuhi kurudi saa tano za usiku?”
Mmh, makubwa nimekuwa mtoto mdogo wa kuwa chini yake kwa kila kitu. Nilijua uchawi wa Bi Shuu ni nini, niliinama na kuchukua mkoba wangu na kufungua. Nilihesa nyekundu tano na kumpa.
“Za nini?”
“Katumie tu”
“Za kodi?”
“Walaa, nimekutunuku tu mama yangu.”
“Kweli!?”
“Kweli unafili uliyonifikiza madogo”
Bi Shuu alifurahi na kunikumbatia na kusahau aliyobwatuka muda mfupi, baada ya kunipandisha na kunishusha alisema.
“Weee mwana kulikoni”
“Kaa chini nikupashe kazi imekuwa kaziiiii”
“Usiniambie”
“Habari ndiyo hiyo shilingi moja kwa sekunde ndio mpango”
“Wacha wee leo Mchaka kawa mzaramu”
“Umenifundisha wewe, ngoja nikaoge nikupashe upashike”
Nilimuacha Bi Shuu chumbani kwangu akizirudia kuzihesabu pesa nilizompa mimi nikaenda kujimwagia maji.
Nilipotoka kuoga nilimkuta akinisubiri kwa hamu kubwa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“mmhu, hebu nipe raha”
“Bi shuu nitakueleza yote kesho”
“Mwana wee siwezi kulala mpaka unipe siri ya rangi nyekundi kupendeza na kusikitisha”
Huku nikijifuta maji nilimueleza yote bila kumficha hata moja, mwisho wa yote nilielezea masikitiko yangu ya bahati ya kupendwa na mkosi wa kuachwa.
“Bi Shuu, japo nimepata lakini wasiwasi wangu sichelewi kumwagwa”
“Kwani una tatizo gani?”
“hata silijui hakuna hata mwanaume mmoja aliyenieleza tatizo langu”
“Mmh, kuna umuhimu wa kulifanyia kazi”
“Siamini kama tatizo langu litaisha”
“Hebu kila ukiwa na huyu bwana msikilie na muulize an apenda nini chochote usimnyime”
“mmh, Bi Shuu wanaume wengine waharibifu ukimchekea anakuharibu”
“Sio unavyo fikiria’
“Kuna nini wanaume wanacho taka zaidi ya kuwaharibu wanawake, sijazaa babu wee cha kuwekewa matambala”
“Sina maana hiyo si wote wana penda mchezo huo.”
“mmh, nitamsikiliza”
“Sasa mwana wee lala nakuomba muheshimu mpenzio kama Mungu wako huoni muda si mrefu nasi tutatembelea gari”
“Ndicho ninachokiomba, sijui yatakuwa yale yale.”
“Basi mwali lala usingizi unono.”
“Nawe pia Bi shuu”
Bi Shuu aliniaga na kuondoka na kuniacha nikimalizia kujifuta maji ili nilale.
******
Siku ya pili wakati namalizia kujipodoa kabla ya kwenda kujifusha udi kwa Bi Shuu simu ya Mateja iliingia, niliipokea na kuzungumza naye.
“Haloo ma’ Sweet.”
“Ooh, ma honey girl.”
“Ni mimi, mhu baba nipe habari naona simu za asubuhi asubuhi?”
“Aah, kawaida ila kuna dereva nimemtuma atakupitia muda si mrefu.”
“Hakuna tatizo Sweet.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Mateja kukata simu, kwa vile nilikuwa tayari nimeisha jipodoa nilikwenda chumbani kwa Bi Shuu. Kabla ya kuingia nilikutana na moto uliokuwa ukinukia vizuri, harufu ya asubuhi ile ilikuwa zaidi na ya jana yake
Niliingia na kumkuta akiweka udi kwenye kitezo, aliponiona alitabasamu na kusema.
“Haya mwali jifushe uwahi kazini.”
Niliinama na kufunikwa shuka ili moshi wote wa harufu nzuri uishie kwenye nguo na mwilini, baada ya muda alifunua shuka na kuninusa kama mbwa anayesaka chakula jaani. Asikuambie mtu Bi Shuu havumi lakini yumo, mtu mzima lakini ovyooo.
“Umevaa kufuri gani?” Bi Shuu aliniuliza swali ambalo sikufikiria kuniuliza.
“Nyeupe.”
“Hebu nione.”
Mmh, makubwa nilinyanyua gauni na kuiona nilikuwa nimevaa kufuli la mikanda ‘Bikini’.
“Mwali ndio nini?” Bi Shuu alishtuka.
“Mbona umeshangaa?”
“Unakwenda kwenye starehe au kazini?”
“Kazini.”
“Sasa mbona umevaa kufuri kama unakwenda kwenye kilimo cha mihogo.”
“Babu weee kwenda na wakati.”
“Acha ushamba vaa kufuri la kawaida, hilo kufuri unalivaa siku unayokutana na mpenzi ukitoa nguo tu akiona anaingia kimuhemuhe.”
Mmh, sikutaka kubishana naye nilirudi hadi chumbani kubadili kufuri, wakati namaliza kuvaa honi ya gari ilipigwa nje nilijua mtu aliyetumwa kunifuata amefika. Nilikimbilia chumbani kwa Bi Shuu kumuaga.
“Bi Shuu naondoka.”
“Umebadili kufuri?”
“Ndiyo.”
“Hebu nione.”
Nilinyanyua tena gauni na kunitazama, nilikuwa nimevaa ya kawaida tena ya rangi nyekundu, alipoiona alisema.
“Ewaaa, sasa hapo ndipo nilipopataka.”
“Basi nawahi kuna mtu ananisubiri hapo nje katumwa na mzee,” nilisema huku nikiteremsha gauni ili niwahi nje.
“Wee Manka ndio nini?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Vipi tena Bi Shuu mwenzio nachelewa kazini.”
“Hebu jifushe na hiyo kufuri linukie.”
Nilirudi haraka na kuchutama kwenye kitezo kwa kulitanua gauni langu moshi wote uingie chini. Baada ya kufanya yote niliyoelekezwa na Bi Shuu nilimuaga kwa kumbusu kisha nilipitia mkoba wangu na kutoka nje. Nilimkuta gari likinisubiri, niliingia kwenye gari na gari liliondoka.
“Mambo?”
“Poa, sijui yako?”
“Hata mimi ipo poa.”
Safari iliendelea hadi ofisini, nilipofika nilipita moja kwa moja hadi ofisini kwa Mateja, alivyokuwa ameisha ingia ofisini. Baada ya kufungua mlango wa ofisi niliingia huku nikiachia tabasamu pana na kutanua mikono yangu, Mateja aliponiona alizunguka meza yake kunipokea. Tulikutana katikati na kukumbatiana.
Tuliporomosheana mabusu moto moto huku tukigandisha midomo kwa muda na kubadilisha mate.
“Mmh, tosha,” nilisema huku nikijitoa mikononi kwa Mateja.
“Mhu, za nyumbani?”
“Mmh, mzuri sijui kwako?”
“Kwangu ilikuwa ngumu kidogo kutokana na kuwa na wakati mgumu baada ya kukuota tupo pamoja niliposhutuka nilijikuta nipo peke yangu.”
“Pole sana, basi ndio ufanye haraka kunichukua.”
“Kwa mateso ya jana kuna umuhimu wa kufanya hivyo.”
“Basi mengine baada ya kazi.”
“Haya mama, mimi niseme nini.”
Nilimbusu tena na kurudi kuendelea na kazi yangu, baada ya kukaa kwenye kiti nilijikuta nikikumbuka jinsi bosi wangu Mateja alivyochanganyikiwa na mimi.
Nilimbusu tena na kurudi kuendelea na kazi yangu, baada ya kukaa kwenye kiti nilijikuta nikikumbuka jinsi bosi wangu Mateja alivyochanganyikiwa na mimi. Pamoja na furaha ile bado wasiwasi wangu ulikuwa nini hatima yangu kwake, nitaendelea naye au ndiyo atanitosa kama waliotangulia.
Wazo la awali lilikuwa kuomba msaada kwa Bi Shuu ili niweze kumdhiniti. Niliendelea na kazi zangu kama kawaida, muda wa mchana tulikwenda kula pamoja kama wapenzi wasiojificha.
Siku ile baada ya kurudi nyumbani aliniomba tuwe wote usiku wa siku ile, sikumkatalia kwa vile ndiye aliyekuwa mmiliki wa mwili wangu. Usiku alinipitia na kuondoka kwenda kulala naye mpaka asubuhi, kaonja kaona tamu sasa anataka kula kabisa. ...
Ni kweli nilifurahi kulala na Mateja mpaka asubuhi kuonesha jinsi gani alivyopagawa kwangu, lakini usiku kwangu ulikuwa wa karaha sana yaani mambo nisiyoyapenda ya kusumbuana wakati wa mapenzi yalijirudia tena. Nilishindwa kumkatalia kwa vile alikuwa bosi wangu kwa kuogopa kufukuzwa kazi na maisha ya kutangatanga yalinichosha. Usiku mzima kugeuzwa kama chapati ooh geuka hivi, lala hivi fanya hivyo, basi kero mtindo mmoja. Nilijiuliza bila kunisumbua vile hawezi kukidhi haja zake, mpaka kunakucha nilikuwa nimekasirika mtoto wa kike kila kona ya mwili iliniuma hayakuwa mazoezi bali adhabu ya mapenzi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi Mateja alifurahi sana na kuniahidi kabla ya yote kukibadili chumba changu kwa kuninunulia sofa za nguvu, alinipa pesa nyingi za kutumia na kunirudisha nyumbani. Huwezi amini nilipofika nyumbani nilimkuta Bi Shuu akinisubiri, kutokana na uchovu nilimsalimia na kuingia ndani nijilaze.
Kabla sijabadili nguo na kuvaa kanga nyepesi Bi Shuu aliingia.
“Mankaaaaa,” aliniita kimbea.
“Unasemaje Bi Shuu,” nilimuuliza huku nikimuangalia jicho zito la usingizi.
“Mmh, sikuwezi.”
“Kwa nini Bi Shuu?”
“Mambo yako mazito.”
“Mmh kawaida tu, vipi ushakunywa chai?”
“Nilikuwa nakusubiri wewe.”
“Mimi kwa sasa hivi siwezi nimechoka sana.”
“Eeeeh Manka weee, mlikuwa mnakomoana.”
“Wee Acha tu,” niliona kama ananichelewesha kulala kutokana na umbea wake wa utu mzima. Nilivuta pochi na kutoa noti kadhaa za kumi kumi na kumpatia Bi Shuu bila kuzihesabu.
“Za nini?”
“Za kwako.”
Bi Shuu alichanganyikiwa na kunivamia kwa furaha na kujitahidi kunibeba japo uzito wangu ulikuwa mkubwa. Kweli pesa sabuni ya roho Bi Shuu alipagawa na kuniona kama malaika niliyetumwa kuja kumpa furaha ya asubuhi ile.
“Bi Shuu niache nipumzike.”
“Mwali weee lala, tena utakutana nimekuandalia chakula kizuuuri.”
Bi Shuu alitoka na kuniacha nikimalizia kuondoa nguo mwili kisha kuchukua kanga nyepesi kisha kujitupa kitandani. Nililala kwa muda wa saa zaidi ya nane kutokana na uchovu wa mbilinge za Mateja usiku kucha.
Majira ya jioni Mateja alifanya kweli kwa kuleta sofa za nguvu kitu kilichofanya Bi Shuu kunipa chumba kikubwa cha nyumba kubwa. Niliamini ule ulikuwa mwaka wangu wa mimi kurudi katika maisha ya kutanua. Niliamini muda si mfupi lazima niwe na gari langu mwenyewe.
Baada ya kukipamba chumba changu na kupendeza Bi Shuu aliniweka chini na kunipa somo.
“Manka Mungu akupe nini, ukishikwa shikamana mwali wee.”
“Hata mimi najua Bi Shuu.”
“Unaonekana mwanzo ulikuwa ukifanya makusudi mbona sasa hivi mwanaume kapagawa muda si mrefu utakuwa dunia ya wenye nazo.”
“Ndio maana yake.”
“Basi Manka nitakuongezea vikorombwezo akigusa amenata.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Usiniambie!”
“Kwanini wazee wenzangu pamoja na umri wangu wakionja wanapagawa itakuwa wewe ukioga maji yanatelemka.”
“Tena kweli ufanye haraka maana ameisha tangaza ndoa.”
“Basi hiyo kazi niachie.”
Mateja alinipigia simu kuwa siku ile angekuja kulala ili jumatatu twende kazini pamoja nami sikumkatalia. Kweli usiku alikuja kulala kwenye chumba changu kilichokuwa na hadhi kubwa kwa mtu yoyote. Kama kawaida ya usiku wa jana yake yalijirudi ya kusumbuliwa lala hivi geuka hivi fanya hivi, basi taabu mtindo mmoja.
Na siku ile nilivumilia lakini moyoni nilijisemea siku nyingine nitampasha kweli wake hawezi kunigeuza kama mwanasesele na kunichezea apendavyo. Nikajikuta siyachukia mapenzi na kuyaona kwangu ni karaha na si starehe, mwanaume alikuwa akipanda juu ya mnazi hashuki mpaka nahisi kichefuchefu.
Niliamini kabisa alitaka kunikomoa kwa vitu alivyonipa, kwangu sikuona mapenzi zaidi ya mateso. Uvumilivu uliponishinda nilianza kuwa mkali kwa kumgomea kwa usumbufu wake kwa kumueleza makavu kuwa sitaki kama hawezi kifo cha mende tuache.
Mateja alinielewa na kustarehe bila usumbufu, nilishangaa kumbe anaweza kukwea mnazi bila kujifunga kamba za miguu. Kilichonishangaza ndani ya mapenzi yetu yaliyochukua miezi minne, Baadhi ya mambo yalianza kutoonesha dalili zozote za kutimiza ahadi yake.
Siku zilivyozidi kwenda mbele ndivyo uhusiano na Mateja ulivyozidi kulega, hata kuwa pamoja baada ya kazi ikafutika kila muda alionekana yupo bize. Kitendo cha kutokuwa karibu na Mateja kilimshtua sana Bi Shuu kwani hata vizawadi navyo vilikatika. Siku moja aliniweka chini na kuniuliza.
“Manka kulikoni?’
”Hata mimi sijui.”
“Manka kila siku hujui wakati unaharibu.”
“Bi Shuu unanilaumu bure.”
“Hivi kama na huyu atakuacha unafikiri utampata nani?”
“Bi Shuu nimejitahidi kwa kila ulilonifundisha nililifanya lakini matokeo yake ndio hayo lazima kuna mkono wa mtu.”
“Manka kuna kitu gani alichokipenda Mateja hukumpa?”
“Mmh, kila kitu nimempa.”
“Kweli?”
“Kweli kabisa, nikudanganye ili iweje.”
“Sasa itakuwa nini?”
“Hata mimi sijui, huu utakuwa ni mkosi tu”
“Basi naomba kesho ukienda kazini niitie Mateja.”
“Mmh, sijui kama atakuja, lakini nitafikisha ujumbe.”
Siku ya jumatatu nilikwenda kazini kama kawaida huku nikifikilia jinsi ya kufikisha wito kwa Mateja wa kuitwa Bi shuu. Hakuwa Mateja niliyekuwa namfahamu. Ilionesha mapenzi yalikwisha kabisa. Kila alipoingia ofisini alinisalimia lakini hakuna kilichoendelea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilipomuuliza alinijibu kwa kifupi “Nipo bize,” nilijikuta nikiiona kazi ngumu kama si Bi Shuu ningeacha kazi kutokana na kujiona sina thamani tena kwa Mateja. Siku moja roho iliniuma sana baada ya msichana mmoja kuingia ofisini kwa Mateja bila kumuulizia kwangu kama ilivyokuwa kwa wateja wengine.
Niliacha kazi zangu na kumfuata ndani, nilipoingia ofisini mbona lilinishuka mtoto wa kike. Niliwakuta wamekumbatiana na Mateja huku midomo yao ikiwa imegandiana. Nilitamani ardhi ipasuke inimeze, nilisimama kama sanamu nisijue cha kufanya, machozi yalinitoka bila kizuizi, pamoja na kuniona hawakushtuka ndio kwanza walizidisha kutomasana kimahaba. Niliona wazi kabisa penzi langu na Mateja limefika ukingoni.
Nilirudi ofisini kwangu na kukaa chini kazi ilikuwa chungu nilijikuta nikilia peke yangu, nilitamani kuondoka niiache kazi. Lakini niliyakumbuka maneno ya Bi Shuu kuwa siku zote penzi tamu ni lile lisilo sukumwa ninalosukumwa lina kasoro.
Nikiwa nimeinama nafuta machozi nilishtushwa na sauti ya Mateja.
“Manka.”
Bila kuitika nilinyanyua uso kumuangalia huku kitambaa kikiwa karibu na macho kufuta machozi. Mateja alikuwa amesimama mbele ya meza yangu akiwa ameshikana kimahaba mmoja alimshika mwenzake mkono shingoni na mwanaume kiunoni.
“Vipi mbona unalia?” Mateja aliniuliza kwa kunikujeli, sikumjibu niliendelea kufuta machozi.
“Manka huyu ndiye mke wangu mtalajiwa.”
Sikumjibu niliinama chini na kulia kilio cha kwikwi ambacho Mateja na mpenzi wake hawakukijali. Niliwasikia wakiondoka, niliwasindikiza kwa macho mpaka walipotoweka, baada ya kutoweka machoni mwangu nilijikuta nikijiuliza nalia nini kwani tukio lile halikuwa la kwanza upande wangu kutendewa.
Ni kweli lazima moyo uniume kutokana na ahadi nzuri za Mateja ambazo nilijua zitanibadilisha katika maisha yangu. Ndoto yangu ya mchana ya kumiliki gari na nyumba iliyeyuka kama bonge la mafuta katika kikaango cha moto. Baada ya muda Mateja alirudi na kunipita kuingia ofisini kwake bila kunisemesha jambo lolote.
Nilikumbuka wito niliopewa na Bi Shuu wa kwenda kuzungumza naye juu ya matatizo yangu, kila nilipotaka kumwambia moyo ulisita na kuamua kuipotezea tu. Muda wa kutoka nilijikuta nikijikaza kike na kumueleza.
“Samahani bosi.”
“Bila samahani,” Mateja alinijibu kistaarabu.
“Bi Shuu alikuwa anakuita.”
“Bi shuu naye ana shida gani tena?”
“Hata sijui.”
“Mmh, yule bibi na umri wake yuko vile wakati wa usichana wake alikuwaje?”
“Mmh, sijui.”
“Basi mwambie nitamtembelea wikiendi.”
Jamani kauli ya Mateja ilinipa matumaini labda atarudisha moyo wake, siku zote nilimuamini Bi Shuu kwa maneno yake matamu yaliyojaa misemo nahau na methani ili kumlainisha mtu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Jamani bosi kwa nini usiende leo?”
“Manka nipo bize sana atanisamehe, lakini mwambie sijamdharau nitaitikia wito wake.”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment