Chombezo : Ladha Ya Tunda Bivu
Sehemu Ya Nne (4)
***** ***** ***** *****
BADO Catherine hakujibu kwa sauti. Aliendelea na mchezo wake wa kusuguasugua vidole sakafuni.
Frank alisimama, akamfuata pale ukutani na kumkumbatia. Ni hilo alilolihitaji Catherine. Na safari hii hakuwa 'mshamba' kama ile siku ya kwanza. Alijikusanya kifuani kwa Frank huku naye akiitumia mikono yake kumpapasa-papasa.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakajisahau kwa muda, wakiiruhusu mikono yao kupita kila walipotaka. Catherine akiwa na kumbukumbu ya ile sinema ya ngono, akamruhusu Frank ambusu kinywani, busu ambalo lilimchanganya zaidi binti huyo na kumfanya asahau kuwa yuko wapi na yuko na nani.
Walipotenganisha vinywa vyao, Catherine alikuwa zaidi ya mgonjwa wa kawaida, akionekana dhahiri kuhitaji tiba zaidi ya tiba hii aliyopewa.
“Twende chumbani kwako,” hatimaye Frank alimwambia.
Dakika ishirini baadaye Frank alikuwa akitoka chumbani mwa Catherine, moyoni akiwa amefarijika kwa kiasi kikubwa. Alibaini kuwa japo Catherine alikuwa na umbo kubwa, umbo lililofinyangwa kike, na vituko vingi viburudishavyo, hata hivyo bado alikuwa hajawaruhusu wanaume waroho wauchezee mwili wake kwa namna wanavyotaka.
Kabla ya kuchojoa nguo zao, Catherine alionyesha utaalamu wake wa mapenzi, akitumia mikono na ulimi kiasi cha kumshangaza Frank hadi akafikia hatua ya kumfikiria kuwa ni changudoa. Hakutambua kuwa ule utundu wote Catherine aliuchota kwenye vimbwanga alivyoviona kwenye ule mkanda wa ngono alioonyeshwa na Latifah. Na zaidi, Frank alijisikia faraja pale alipobaini kuwa ni yeye ndiye aliyeivumbua ile hazina ya tunda bivu iliyokuwa imehifadhiwa mwilini mwa Catherine.
Alipoondoka alimwachia shilingi 20,000 na kumwambia aitunze hazina hiyo bila ya kumzawadia mtu mwingine.
Linda aliporudi jioni alishangaa kumkuta Catherine kalala na alipohoji akajibiwa,“Sijisikii vizuri mama.”
Linda hakufuatilia sana ni kipi kinachoendelea. Kwa kuwa alimpenda sana Catherine, kwa siku mbili mfululizo alimtaka apumzike na wakati mwingine akawa akiondoka anamwacha Latifah hapo akizungumza naye!
**********
FRANK alikwishaionja asali, sasa alitaka tena na tena. Kwa kipindi cha wiki tatu akawa ameshakutana kimwili na Catherine mara tatu na kuyatenda yaleyale waliyotenda siku ile ya kwanza.
Sasa Catherine akanogewa. Hakuwa na kipingamizi pindi Frank alipomhitaji. Akazidi kukomazwa, na akakomaa. Hatimaye akakaribia kuwa 'kichaa' kwani hakutaka zipite siku tatu bila ya kutupwa kitandani na Frank.
Ulikuwa ni uhusiano wa siri, uhusiano ambao Linda hakuwahi kuushtukia. Walijitahidi kuyafanya mambo yao kwa utaratibu ambao isingekuwa rahisi kwa mtu mwingine yeyote kujua, achilia mbali Linda.
Mara mbili, tatu waliwahi kukutana katika gesti moja iliyokuwa mafichoni eneo la Kinondoni Moscow mchana na kuyafanya waliyohitaji kuyafanya. Kwa ujumla walizoeana na walinogewa.
Ikaja siku. Ilikuwa ni Jumatano, saa 10 jioni, Frank alikuwa akitoka kazini na siku hiyo aliamua kupitia kwa Linda kabla ya kwenda kwake. Siyo kwamba dhamira yake ilikuwa ni kumwona Catherine tu, la hasha. Hii ilikuwa ni siku ya pili hajaonana na Linda.
Kabla ya kuamua hivyo, alimpigia simu na kumtaarifu. Wakakubaliana kukutana muda huo. Frank alikodi teksi hadi nyumbani kwa Linda. Akamkuta kishafika, lakini alionekana kutokuwa na furaha. Frank akashangaa, hisia kuwa huenda Linda amegundua kuwa kuna uhusiano wa mapenzi kati yake na Catherine zikamjia. Hata hivyo, akapiga moyo konde na kuketi sofani akijiandaa kwa lolote lile, liwe baya au zuri.
Linda alikuwa ameketi katika sofa dogo, Frank katika sofa kubwa. Wakatazamana. Uso wa Linda ulionekana kujawa na simanzi na ni kama vile alikuwa akilia muda mfupi uliopita.
Frank alikohoa kidogo na kujipa ujasiri wa kiume. Akauliza, “Vipi, naona kama hauko katika hali yako ya kawaida. Una tatizo gani?”
Linda alishusha pumzi ndefu na kumtazama kidogo Frank. Kisha akatwaa kitambaa na kujipangusa machoni. Akamtazama tena Frank. “Nimepata taarifa ya msiba,” alisema.
“Msiba?” Frank alimuuliza kwa mshangao, moyoni mwake akifarijika kuwa zile hisia zake hazikuwa sahihi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiyo.”
“Nani kafariki?”
“Rafiki yangu,” Linda alijibu na kupiga chafya. Akatwaa tena kitambaa na kujifuta machozi yaliyoanza kujiunda machoni mwake.
Frank alihama kutoka kwenye sofa alilokuwa amekaa na kumfuata. Akamwinamia. “Sikiliza, Linda,” alimwambia kwa upole. “Acha kulia, mpenzi. Tulia, unieleze vizuri. Ni nani kafariki?”
“Huwezi kumjua.”
Ni kweli Frank asingeweza kumjua. Japo kuna baadhi ya rafiki wa Linda aliowafahamu, lakini huyo hakuwa mmojawao.
“Siwezi kumjua?” hatimaye Frank alijikuta akiropoka.
“Ndiyo,” Linda alijibu huku sasa akijitahidi kujikaza na kutulia. Kwa mara nyingine akashusha pumzi ndefu. Kisha akaongeza, “Ulikuwa hujawahi kumwona. Kaanza kuumwa muda mrefu, na alikuwa kalazwa Mwananyamala.”
Frank alibaki kimya akimtazama Linda.
“Itanibidi niende,” Linda aliendelea. “Alikuwa rafiki yangu wa siku nyingi, na tulisoma pamoja Makongo Sekondari. Nisipoonekana huko msibani, jamii haitanielewa.”
“Kafariki lini?” Frank aliuliza.
“Leo. Nimepata taarifa saa moja iliyopita, muda mfupi tu baada ya kuongea na wewe.”
“Dah, pole sana,” Frank aliungana naye. “Kama kweli alikuwa mtu wako wa karibu, itabidi uende. Maiti iko wapi?”
“Bado iko hospitali Mwananyamala, lakini walikuwa kwenye utaratibu wa kuipeleka nyumbani. Nadhani mpaka nitakapofika huko watakuwa wamekwishaifikisha.”
“Msibani kwenyewe ni wapi?”
“Magomeni. Ni kwao marehemu.”
Frank alifikiri kidogo, akakuna kidevu chake chenye ndevu changa. Kisha: “Kwa hiyo utalala huko au utarudi?”
“Hilo siwezi kujua. Yote nitayajulia hukohuko. Utanisindikiza?”
Lilikuwa swali ambalo Frank hakulitarajia. Akilini mwake alikwishaomba Linda alale hukuhuko. Na alipenda iwe hivyo ili apate wasaa wa kustarehe na Catherine kwa uhuru usiku kucha. Lakini atamjibu nini huyu Linda? Amjibu kuwa hatamsindikiza? Na, je, jibu hilo litachukuliwa vipi na Linda ambaye kwa vyovyote vile anatarajia kuwa watakuwa pamoja?
Huenda akatoa sababu ya kutomsindikiza. Lakini, je, ni sababu gani nzito atakayoitoa kwa muda huu mfupi aliorushiwa swali? Ni lazima awe na sababu itakayomfanya Linda akubaliane nayo bila ya wasiwasi wowote!
Labda Mungu alikuwa upande wake kwani wakati huohuo akakumbuka kuwa majuzi alimwambia mwenye nyumba wake aliahidi kuja kati ya leo na kesho. Taarifa hiyo Linda alikuwa nayo, lakini taarifa ya pili kuwa hatakuja katika siku hizo bali wiki ijayo, Linda hakuwa nayo. Kwa hali hiyo, aliamua kuutumia mwanya huo kuikwepa safari hiyo ya Magomeni.
“In gewezekana, lakini...” alisema na kusita. Kisha akaendelea, “Lakini si unakumbuka kuwa majuzi nilikwambia kuwa mwenye nyumba wangu anakuja leo?”
“Aaaah!” Linda alibwata kwa masikitiko na kuonyesha kuvuta kumbukumbu. “Nakumbuka. Na si ulisema kuwa mwenye nyumba wako ni mtu wa njaa-njaa?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yeah. Hana maana. Anaishi kwa nguvu ya mpangaji.”
“Ye' mwenyewe anakaa wapi?”
“Yuko huko Kisarawe na familia yake. Kwa hiyo akija ni siku hiyohiyo anachukua chake. Hakuna cha ooh, nitakupa wiki ijayo au subiri siku mbili, tatu. Hasikii maneno ya aina hiyo!”
“I see. Basi kamsubiri. Inabidi upaheshimu sana unapolaza ubavu. Anakuja saa ngapi?”
“Aliponipigia simu alisema ataingia jioni kama saa kumi na moja au kumi na mbili.”
“Anakuja muda huo? Na atalala wapi?”
“Ana chumba chake. Hukitumia chumba chake hicho kwa kulala kila anapokuja kuchukua kodi yake au kufanya marekebisho ya nyumba na mambo mengine.”
“Ok, usijali. Acha mi' n'ende. Lakini sina uhakika kama nitalala huko. Kama sitauona umuhimu wa mimi kuendelea kuwepo kwa wakati wote, basi nitaaga na kurudi zangu. Kumwacha msichana wa kazi peke yake si vizuri.”
“ Ni kweli,” Frank aliafikiana naye. “Lakini hata hivyo usalama hapa kwako ni mkubwa. Siyo rahisi vibaka kuvamia. Ni bora ulale huko ili uondoe minong'ono-nong'ono kwa watu wanaojua kuwa wewe ulikuwa rafiki mkubwa wa marehemu.”
Walipoachana walikuwa wamekubaliana kuwa Linda atalala huko msibani. Na wakati Frank akinyanyuka ili aondoke, alimtupia jicho la siri Catherine na kumkonyeza. Catherine akaachia tabasamu la siri na kuyainamisha macho.
**********
SAA 1:30, giza likiwa limekwishaitawala anga, Frank alikuwa nyumba ya tatu tu kutoka kwenye nyumba aliyoishi Linda. Hapo alipokuwa kulikuwa na duka dogo la bidhaa za rejareja. Alipofika hapo aliagiza soda na kuanza kunywa taratibu.
Alikuwa na sababu maalumu iliyomweka hapo. Macho yake yakawa yakiangaza huku na kule kama atafutaye kitu. Mara akamwona kijana mmoja aliyekuwa amevaa nguo chakavu akitaniana na muuza duka. Sura yake haikuwa ngeni. Mara kadha alikuwa akimwona katika eneo hilo akifanya kazi za kuwabebea watu mizigo na kuwachotea maji baadhi ya wakazi wa eneo hilo.
Akili ikamtuma kumtumia kijana huyo katika kufanikisha lengo lake. Wakati kijana huyo alipoamua kuondoka huku akivuta sigara yake kwa madaha, Frank akaimalizia soda haraka na kumfuata.
“Oyoo…msh’kaji…” alimwita.
Kijana huyo akageuka na kumtazama Frank. Ikamlazimu Frank kutengeneza tabasamu la kirafiki ili kumfanya kijana huyo awe rafiki kabla ya kuzungumza.
“Vipi mshkaji wangu?” ndivyo Frank alivyomwingia mara tu alipomfikia.
“Barida tu. N’ambie.”
“Nina ishu ndogo mwanangu. Nitakudakisha.”
“Yap… hayo maneno…n’ambie kwanza ishu yenyewe.”
Frank akaona mambo yanaanza kumnyookea. Hakuchelewa, akafunguka: “Unamfahamu demu mmoja anaishi nyumba ile?” akamwonesha kwa kuigeukia tu nyumba ya Linda bila ya kutumia kidole.
“Demu gani? Linda?”
“Siyo Linda. Yule mwingine.”
“Mwingine yupi we’ msh’kaji wangu?” kijana huyo aliuliza kwa sauti yenye mkwaruzo wa kilevi-levi. “Mi najua pale kuna Linda na hausigeli wake! Nani mwingine?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yap! Namzungumzia huyo hausigeli.”
“Cathe?”
“Huyohuyo!”
Ok, funguka basi. Unaogopa kutia mguu nikakuitie?”
“Kama umeota mwanangu,” Frank alisema huku akichanua zaidi tabasamu la kirafiki.
“Poa. Mi’ pale naingiaga kama homu kwangu dadadadek! Nawapelekeaga maji mara kibao tu. Una mkwanja kiasi gani nikutolee mtoto huko ndani.”
“Frank alichomoa noti ya shilingi 1,000 na kumpatia. Kijana akaguna huku akiishikilia noti hiyo. Kisha akasema, “Ni shombo tu hii msh’kaji wangu. Ongeza buku mbili kieleweke!”
Frank hakutaka kupoteza muda. Pesa alikuwa nazo. Akachomoa shilingi 1,500 na kumwongeza huku akisema, “Us’konde wangu. Tuko pamoja, hata kesho nitakupoza tu.”
“Poa,” kijana huyo alijibu huku akionekana kutaka kuondoka. Akasita na kuuliza, “Nimwambie nani?”
Frank akafikiri kidogo kisha akasema, “Ukiwa na uhakika Linda hayupo, mwambie Frank. Tatizo demu mwenyewe hana simu, dah!”
“Na kama Linda yupo?”
“Uzugezuge kisha usepe zako.”
“Poa. Ganda hapohapo nikakuburuzie mzigo wako.”
Kijana huyo akatokomea ndani ya nyumba ya Linda. Baada ya dakika kama tano hivi, akarudi. Alipomfikia Frank alitamka neno moja tu:“Anakuja.”
“Umemkuta peke yake?”
“Ndiyo.”
“Alikuwa anafanya nini?”
“Amekaa tu anacheki muvi kwenye TV.”
“Poa. Kesho nitakuona tena msh’kaji.”
“Barida.”
Wakaachana.
Frank aliendelea kutulia palepale, na baada ya kama dakika tano hivi, Catherine akatokea. Akaja moja kwa moja hadi pale kando ya barabara kwa kuwa alikwishaelekezwa na kijana yule kule ndani.
Frank akamshika mkono na kumvuta kando zaidi, sehemu iliyokuwa na kijigiza cha wastani.
“Vipi, Linda karudi?”
“Hajarudi. Kwani hatalala huko msibani?”
“Tulikubaliana alale huko,” Frank alijibu. “Lakini sijui kama kweli atalala au atarudi.”
Kimya kikatawala kwa muda mfupi. Kila mtu alikuwa akiwaza lake. Kisha Frank akauvunja ukimya huo. “Kwa hiyo inakuwaje?” aliuliza.
“Poa tu.”
“U'shakula?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Tayari. Saa'izi nilikuwa naangalia zangu tamthilia kwenye tiivii. Na
wewe?”
“Mimi?”
“Ndiyo. U’shakula?”
“Mimi sina njaa ya chakula chochote cha kawaida,” Frank alijibu huku akiachia tabasamu la mbali.
“Huna njaa ya chakula cha kawaida?” Catherine alimuuliza akionesha mshangao.
“Nd'o mana’ake.”
Catherine aliguna kisha akasema, “Sijakuelewa.”
“Mimi n'na njaa na wewe tu,” Frank alichomeka.
Catherine akasonya na kumpiga kijikofi dhaifu mgongoni. “Lione, hata hauna haya,” aliongeza.
Frank alicheka na kumtomasa kidogo mbavuni. Catherine akaruka na kuguna.
“Kwa hiyo?” Frank aliendelea kuuliza.
Kwa mara nyingine kimya kikatawala. Kisha Catherine akasema, “Pitia uani. Nitakufungulia mlango uende moja kwa moja chumbani kwangu.”
Frank alifuata maelekezo. Na alipokwishaingia ndani alipitiliza moja kwa moja chumbani mwa Catherine na kujitupa kitandani. Humo alikuwa kimya, hakukiruhusu hata kikohozi! Na kwa muda wote alikuwa akitega masikio kusikiliza kama Linda atarejea.
Nusu saa ilikatika akiwa peke yake huko chumbani. Catherine alikuwa akisafisha vyombo, zoezi ambalo alipolikamilisha aliingia bafuni kuoga kisha akafunga mlango vizuri na kuzima taa ya sebuleni. Hadi kufikia wakati huo, si Frank wala Catherine aliyekuwa na fikra kuwa Linda atarejea usiku huo.
Ilikuwa imetimu saa 4. Kwamba, Linda atarejea kutoka msibani Magomeni Mikumi usiku huo, lilikuwa ni jambo ambalo halikuwaingia akilini.
**********
SIMANZI ilitawala ndani ya nyumba ya mzee Khassim, eneo la Magomeni Mikumi. Umati wa watu ulifurika ndani na nje ya nyumba hiyo. Nyuso za wengi, hususan wanawake zilionekana kukumbwa na huzuni kubwa. Minong'ono ya hapa na pale ilisikika, na mara chache vilio vya watoto navyo vilizuka na kupotea baada ya muda mfupi.
Linda alikuwa miongoni mwa waliofika hapo. Naye, kama wanawake wengine alikuwa ndani akiwa amejitanda kanga kutoka kichwani. Baadhi ya watu waliokuwa wakiufahamu vizuri uhusiano baina yake na marehemu, walimpa mkono wa pole.
Kulikuwa na msiba wa kifo cha Mwajuma, mtoto wa mzee Khassim ambaye alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kichomi kwa muda mrefu. Maiti ililetwa hapo nyumbani jioni hiyo, na mipango mingine ilikuwa ikiendelea kufanywa.
Ulikuwa ni msimu wa baridi kwa Jiji la Dar es Salaam. Katika eneo hilo kulikuwa na upepo mkali ulioambatana na baridi ya wastani. Linda alihisi baridi kuwa ni kali, zaidi ya siku nyingine. Awali alitulia tu akihisi kuwa ni hali ya mpito na baada ya muda mfupi ingetulia. Lakini haikuwa kama alivyotarajia. Nusu saa baadaye akahisi kukumbwa na maumivu ya kichwa. Hisia kuwa huenda anaandamwa na homa zikamjia.
Dakika kama kumi baadaye hakuyaona mabadiliko ya kupungua kwa maumivu ya kichwa wala baridi, na hapo ndipo alipojiwa na wazo la kuondoka. Akajitanda kanga yake vizuri na kunyanyuka akielekea ndani ya chumba ambacho alikuwamo Siyajali, dada yake marehemu Mwajuma.
Alipoingia aliwakuta wanawake wengine watatu wakimfariji Siyajali aliyekuwa kainamisha kichwa akilia kimyakimya. Linda naye aliketi na kujiunga na wanawake wengine kumpa maneno ya faraja. Hatimaye Siyajali alitulia na kufuta machozi.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Dada Siyajali,” Linda alisema, akiwa anamwangalia usoni. “Hali yangu siyo nzuri. Naumwa. Nitajitahidi kuja kesho lakini kwa kweli nahisi kuandamwa na malaria.”
Siyajali alimtazama kidogo na kutikisa kichwa akionesha kukubaliana na kauli yake.
“Kwa hiyo naomba kwa leo nikuache dada' angu,” Linda aliendelea. Mara akawatazama wale wanawake wengine na kurusha swali lililoonekana kuhitaji jibu kutoka kwao. “Utaratibu wa mazishi ukoje?”
Mmoja wa wale wanawake alinyanyua mabega na kuyashusha. “Kwa kweli mambo hayo yatajulikana hiyohiyo kesho,” hatimaye alijibu.
Linda alimgeukia Siyajali na kumpa mkono. Kisha akafungua mkoba na kutoa shilingi 20,000. Akampatia Siyajali huku akisema, “ Pumzika dada. Kesho nitakuja asubuhi.”
“Asante,” sauti dhaifu ya Siyajali iliyafikia masikio ya Linda kwa usahihi.
****HAYA FRANK YUKO CHUMBANI MWA CATHERINE. HANA WASIWASI....ANASUBIRI KUZAWADIWA KILE ANACHOKIHITAJI. WAKATI HUOHUO, LINDA YUKO MSIBANI MAGOMENI MIKUMI, LAKINI AFYA YAKE INAKUMBWA NA MGOGORO, HIVYO ANAAMUA KURUDI NYUMBANI.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment