Search This Blog

Monday, October 24, 2022

KITANDA CHA MPANGAJI MWENZANGU - 3

 





    Chombezo : Kitanda Cha Mpangaji Mwenzangu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    "Hamna bwana, mwenzio najisikia," alisema Halima akimshikashika kijana huyo na kumvutia kwake.

    "Halima unatangaza kwa watu mimi nalala na huyo kijana mbona na wewe upo kwake tena usiku huu?" sauti ya mama Tina ilisema mlango ukiwa wazi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wote walishtuka mle chumbani, mama Tina alisimama. Halafu alivyo jasiri alipenyeza mkono wake na kuwasha taa ya ukutani, tap! Kukawa na mwanga mkubwa.



    Mi nimekuja tu mara moja," alijitetea Halima;

    "Ungekuja mara moja kungekuwa na giza?"

    "Hatukutaka kuwasha taa."



    "Mmmh! Jamani, muwe wakweli, siyo mnawasingizia wenzenu kumbe na nyie ni mulemule," alisema mama Tina akiondoka kwa hasira.

    Hasira zake zilikuwa mara mbili, kwanza Os Anjelus ni;mtu' wake, pili Halima ameingilia penzi lake, aliumia sana, basi tu.



    Hakwenda chooni, alirudi chumbani kulala huku akiwa anasonya kila wakati

    "Vipi, una nini?" mume wake alimuuliza baada ya kushtuliwa na sonyasonya nyingi.

    "Si hao wapangaji, sijui nani kaingia chooni wala hajamwaga maji!"



    "Atakuwa nani, labda huyo mpangaji mgeni, maana hiyo tabia sijawahi kuiona wala kuisikia."

    "Mm! Yule wala, sidhani kama anaweza kuwa na ustaarabu sifuri kama huo."

    "Atakuwa yeye tu, mbona unamtetea au unamjua aliyefanya hivyo?"

    "Mimi simjui mume wangu na wala simtetei, ila nasema haoneshi kama ana ustaarabu mbovu kama huo."



    Walilala baada ya mazungumzo hayo.

    ***

    Halima aliamka kwake baada ya kutoka kwa Os Anjelus usiku ule hata bila ya kucheza mechi, mama Tina alimtibulia ingawa pia haijulikani kama kijana huyo angemkubalia au la!

    Alifikicha macho akiwa uani huku kaaibu kwa mbali kakimtawala usoni.



    Mama Tina alichomoka kwake na kutokea uani, hakumsalimia Halima licha ya kwamba alimkuta

    "Za asubuhi mama Tina?"

    Kimya;

    "Mama Tina nakusalimia."



    "Kwani lazima kuitika salamu yako Halima?"

    "Khaa! Mke wangu kwani kuna nini? Mtu anakusalimia unasema kwani lazima? Mna ugomvi? Eti Halima kuna ugomvi?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hatuna ugomvi," alijibu kwa haraka mama Tina. Aliamini kwamba kama angechelewa kusema lolote, Halima angeweza kufichua yaliyofichika ambapo yeye asingetaka mambo yafikie huko

    "Sasa kwa nini unakataa salamu yake? Eti Halima kuna ugomvi?" baba Tina alirudia tena kumuuliza Halima maana awali alimuuliza akajibu mke wake



    "Muulize mkeo, si anajua mimi niko singo sijaolewa, yeye kaolewa, muulize sasa," alisema Halima kauli iliyojaa utata wa kutosha kumfanya baba Tina ahisi kuna jambo hasa kwa kauli hii;

    ";si anajua mimi niko singo sijaolewa, yeye kaolewa"

    "Mama Tina kuna nini?"



    "Hakuna kitu mume wangu, amesema tu. Salama Halima mdogo wangu jamani, umeamkaje?"

    "Mimi sijambo."



    Baba Tina ambaye alikuwa akienda kazini alifungua mlango mkubwa na kutoka, lakini akili ikakumbuka mazungumzo yake na mkewe usiku uliotangulia kuhusu chooni

    "Si hao wapangaji, sijui nani kaingia chooni wala hajamwaga maji!"



    "Atakuwa nani, labda huyo mpangaji mgeni, maana hiyo tabia sijawahi kuiona wala kuisikia."

    "Mm! Yule wala, sidhani kama anaweza kuwa na ustaarabu sifuri kama huo."

    "Atakuwa yeye tu, mbona unamtetea au unamjua aliyefanya hivyo?"

    "Mimi simjui mume wangu na wala simtetei, ila nasema haoneshi kama ana ustaarabu mbovu kama huo."



    "Hili suala la leo asubuhi lina jambo zito ndani yake, Halima na mke wangu sijawahi hata kuwasikia wako kwenye mgogoro wowote, ni nini kipya kimetokea?



    "Halafu kwa nini Halima amekimbilia mambo ya kuolewa na kutoolewa, ina maana msingi wa mzozo wao ni huo?" alijiuliza mwanaume huyo hata alipokuwa amefika kazini;



    "Lazima nianze ufuatiliaji, hapa penye ndoa na usingo pana kitu, mimi ni mtu mzima na ule ni ujumbe nilipewa kwa akili," alisema moyoni baba Tina.

    Akiwa katika harakati za kazi, simu ya baba Tina iliita, namba ngeni

    "Halooo," alipokea baba Tina.

    "Halo, wewe ni baba Tina?"



    *******************

    *****************************

    ***************************************8



    "Bee!"

    "Hebu njoo mara moja."

    Halima alitoka akiwa anajifunga kanga vizuri, akasimama kumsikiliza mama Tina;

    "Ulisema hospitali anaumwa nani?"

    "Mjomba angu. Kwani vipi?"

    "Una uhakika Halima?" Endeleaa......



    "Khaa! Nitashindwaje kuwa na uhakika wakati anayeumwa ni mjomba?"

    "Mbona kuna mtu kaniambia baba Tina amelazwa hapohapo Palestina, ana presha?"

    "Mimi sijamwona baba Tina."

    "Mh! Haya poa."

    "Poa ndiyo."



    Mama Tina aliingia ndani, akajikusanya na kukimbilia hospitali ambapo kweli alimkuta mumewe amelazwa.

    "Mwenzetu imekuwaje tena?" alimuuliza mumewe kwa sauti ya upole.

    "Presha ilipanda."

    "Kisa nini?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Sijui."

    "Sasa mbona hukuniambia?"

    "Sikuwa na uwezo hata wa kuongea."

    "Umeletwa na nani?"



    "Wafanyakazi wenzangu."

    "Kha! Sasa mimi kanipigia simu mama Kanisia, kasema amekuona lakini we hujamuona."

    "Ni kweli sijamuona."



    Mama Tina akatupia macho chini akiamini anaweza kuona mabaki ya chakula, kweli akaona masalio ya mchuzi na ndizi

    "Sasa umekula nini?"

    "Sijala kitu."

    "Mh!" aliguna;



    "Sasa nikakutengenezee chakula gani cha haraka?"

    "Hapana, nimeshiba sana."

    "Mh!"



    Mama Tina alikuwa katika wakati wenye maswali mengi kuhusu mumewe na Halima

    "Eti kuna wodi nyingine ya wanaume hapa Palestina?" alimuuliza mumewe.

    "Sina uhakika."



    Alisimama na kutoka nje. Akakutana na muuguzi mmoja;

    "Samahani sana, eti kuna wodi nyingine ya wanaume hapa Muhimbili?"

    "Ile pale, nyingine ingia kwenye mlango ule, ukaulizie."



    Mama Tina alikwenda kote, akawaangalia wagonjwa wanaume na kila mmoja alimuuliza tatizo lake. Hakuna aliyesema ana presha ya kupanda wala kushuka.

    Akaenda mapokezi

    "Samahanini jamani, eti kuna mgonjwa kaletwa hapa kwa tatizo la presha?" alimuuliza mtu wa mapokezi.

    "Nenda kwa daktari wa zamu."

    Mama Tina akaenda kwa daktari wa zamu

    "Samahani dokta, kuna mgonjwa wa presha ameletwa leo?"

    "Yeah! Yupo mmoja."



    "Siyo wawili?"

    "Hapana. Kwa nini unataka wawe wawili?"

    "Nina sababu zangu."

    "Kama zipi?"

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Aaa! Kuna mtu kaniambia kaja kumwangalia mjomba;ake ana presha lakini nahisi alikuja kumwangalia mume wangu maana ndiyo mwenye presha, kuna kitu nimekitilia shaka."

    "Huyo mtu ni mwanamke?"

    "Ndiyo."



    "Ni jirani yako?"

    "Tunakaa nyumba moja."

    "Sasa mtu mkikaa naye nyumba moja ni tatizo kuja kumjulia hali mume wako? Au kwa sababu ni mwanamke?"



    "Dokta haiko hivyo unavyofikiri wewe."

    "Basi kumbe mna mambo yenu. Hapa mwanaume mwenye presha ni mmoja tu. Aliletwa na wafanyakazi wenzake."



    Mama Tina hakukubali, akatoka nje na kumpigia simu Halima...

    "Eti huyo mjomba ;ako amelazwa wodi gani na anaitwa nani? Nataka kumpa pole maana nimekuja kumwangalia baba Tina."





    Yupo hapohapo we ulizia tu, utampata.”

    “Anaitwa nani?”

    “Mh! Mzee Semsela.”



    Basi, mama Tina akaingia kwenye woda ya kwanza waliolazwa wanaume…

    “Jamani wagonjwa samahanini sana, eti kuna mgonjwa anaitwa mzee Samsela humu ndani?”

    Wagonjwa wote na wanaowahudumia walibaki kimya, kila mmoja akitembeza macho kwa mwenzake kama kuna atakayesema yeye ndiye mzee Semsela.



    Mbaya zaidi, karibu wagonjwa wote hakuna aliyekuwa na vigezo vya kuitwa mzee.

    “Mama nadhani hakuna, si umeona mwenyewe?” mgonjwa mmoja ambaye ni msela tu alisema.

    Mama Tina akaondoka, akaenda kwenye wodi aliyolazwa mume wake…



    “Samahani wagonjwa jamani!” aliposema hivyo mama Tina akamtumbulia macho mume wake, akawatumbulia wagonjwa wengine ili kuona kama wamepokea samahani yake, akaendelea…

    “Eti kuna mgonjwa anaitwa mzee Semsela humu wodini?”



    Kulikiwa na wazee wengine wawili mbali na mume wake, baba Tina lakini hakuna aliyesema yeye ndiye mzee Semsela…



    “Una nini wewe kwani?” mumewe alimuuliza.

    “Halima alileta chakula hapa leo, akasema mjomba wake amelazwa, kisa ana presha, sasa namuuliza huyo mgonjwa wake amelazwa wodi gani nimjulie hali, akasema niulizie mzee Semsela…



    “Kwani lazima umuone huyo mzee Semsela?”

    “Si mjomba wa mpangaji mwenzangu jamani!”

    “Sitaki hiyo tabia mama Tina.”



    “Basi kama hutaki ina maana Halima alikuja kukuangalia wewe?”

    “Mimi sijamwona.”

    “Ulimwona, unanidanganya tu.”



    “Mama Tina hebu rudi nyumbani tafadhali sana.”

    “Oke, oke. Lakini Halima atakwenda kuniambia ukweli leo,” alisema kwa ukali mama Tina huku akiondoka kwa hasira.



    Katika maisha yake ya kuwa na baba Tina hakuwahi kujisikia wivu kama siku hiyo, hasa akizingatia kwamba, kama kweli mumewe atakuwa anatembea na msichana huyo basi ndoa yake iko hatarini kwa mambo mawili. Kwanza, Halima ni mwanamke malaya tu, hivyo Ukimwi njenje.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Pili, licha ya umalaya wake, lakini pia ni msichana mzuri sana. Ana sifa zote za kumvutia mwanaume anayejua wanawake warembo.



    Alipokwenda hospitali alipanda Bajaj lakini wakati anarudi, ili kumuwahi Halima aliamua kupanda bodaboda huku akimwambia dereva wake kwamba, kama hawezi kukimbiza amshushe apande bodaboda nyingine…



    “Suka vipi, mbona kama unapangusa meza iliyomwagikiwa uji wa mtoto, nishuke nipande nyingine nini?”

    “Anti inakimbia sema tu kwa vile una haraka sana ndiyo maana unadhani haikimbii.”

    “Mimi najua pikipiki ikikimbia na ikitembea kama yako, hii unatakiwa uiingize kwenye msafara wa magari ya kusindikiza harusi za kifahari.



    ***



    Haloo baba Tina,” Halima alipokea simu ya baba Tina ambaye alipiga mara baada ya mke wake kuondoka…

    “Mwenzako alikuja hapa, amekwambia?”

    “Kaniambia, nikamyeyusha.”



    “Sasa anakuja huko, utajua cha kumwambia, sawa?”

    “Wala usikonde. Ye anadhani mimi na wewe tunaweza kuwa wapenzi kweli?”

    “Hapana.”



    “Sasa? Mi nilichukulia ubinadamu tu, wewe ni mpangaji mwenzangu kwa hiyo natakiwa kukuonesha ubinadamu wangu hasa pale nilipogundua kwamba, aliyekusababishia matatizo hayo ni yeye.”

    “Kweli kabisa Halima.”



    “Sasa kwa nini yeye anataka kuchukulia jambo hili kama vita?”

    “Hata mi sijui.”



    “We Halima!” aliita mama Tina akiwa ameshafika.

    “Abee…baba Tina mkeo ameshafika, ananiita nje,” Halima alisema kwa sauti ya chini huku akitoka chumbani kwake.

    Halima alikata simu ya kuongea na baba Tina, akawa ameshafika kumsikiliza mama Tina…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog