Chombezo : Kitanda Cha Mpangaji Mwenzangu
Sehemu Ya Tano (5)
"Jamani, yaani tumekuja kufumania lakini matokeo yake tunaweza kufumaniwa sisi," alisema baba Tina, Halima akacheka kwa sauti ya juu, ikaingia chumbani aliko Os Anjelus, mama Tina akashtuka kuisikia maana aliijua.
JIACHIE MWENYEWE..."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ha! Mbona kama nimesikia sauti ya Halima akicheka?"
"Halima gani?" alihoji Os Anjelus...
"Halima yule binti malaya wa nyumbani."
"Labda umefananisha."
"Labda maana nimemwacha nyumbani."
Baada ya kujiridhisha kwamba amefananisha sauti, wawili hao walijitupa kitandani bila kushauriwa na mtu. Kila mmoja alikuwa moto.
Ilikuwa mara yao ya kwanza kukutana nje ya nyumbani kwa hiyo waliamini wako huru kuliko siku nyingine yoyote ile.
"Leo nataka tuweke kumbukumbu ya kudumu," alisema mama Tina...
"Ipi hiyo?"
"Tulisakate kandanda hadi tuseme basi. Tena naomba nikwambie kabisa, noo kubaniana."
Os Anjelus alicheka kwa mbali lakini alipomaliza kucheka alimshika mwanamke huyo na kumlaza chali, akamchojoa. Baada ya muda wote wakawa hawana nguo.
Mechi iliangushwa, mama Tina alijiachia kupita kama anavyokuwa kwa mume wake.
* * *
Chumbani kwa baba Tina, hali ilikuwa tete. Baba Tina licha ya umri lakini alibahatika kuwa na nguvu mpaka muda huo. Halima alitingishwa sawasawa mpaka akawa anataka kupiga kelele kama si jitihada za mwanaume huyo za kumziba kinywa kujitokeza.
"Usipige kelele sasa, si watasikia watu, sasa tutatokaje?" alisema baba Tina akiwa anaendelea kumzungusha.
Halima alikwenda mbali zaidi sasa akawa kama anamkomoa mwanamke mwenzake mama Tina kwani akiwa anaendelea na mechi aliweka mbwembwe kwa kushika maiki na kuanza kuimba hali iliyozidi kumchanganya baba Tina na kuhemea juujuu huku miguno ikichukua nafasi.
* * *
Wakati kwa baba Tina kukiwa hivyo, chumbani aliko mama Tina nako hali ilikuwa tete zaidi. Mama Tina aliamua kutoa kilio cha waziwazi lakini kwa sauti ya chini sana ambacho kilisikika kwa mle chumbani tu. Mama Tina alikuwa kama anaomboleza vile...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Os! Os!" aliita.
Lakini kijana huyo hakuitika kwa kawaida bali kwa mguno huku jasho jembamba likianza kumtoka mwilini. Hapo alikuwa anatumikia kauli ya mama Tina kwamba siku hiyo waweke historia na hakuna kubaniana.
* * *
Mhudumu wa gesti hiyo alitatizwa na jambo moja. Swali aliloulizwa na akina mama Tina. Kutaka chumba chenye dirisha linaloangalia nje. Lakini pia swali lake kichwani likawa hili...
"Yule mzee kaingia na msichana mdogo kabisa. Halafu yule mama kaingia na kijana wa kiume naye mdogo tu. Sasa kwa nini wasikubaliane, wakabadilishana?" akakumbuka kwamba ni jambo lisilowezekana kwani kila mmoja alitoka kwake.
Yalipita masaa mawili, kila chumba kilikuwa na uhitaji wake. Wakati chumbani kwa baba Tina, Halima alihitaji mechi nyingine ya pili na baba Tina akiwa hoi, chumbani kwa mama Tina, Os Anjelus yeye ndiyo alikuwa akimsumbua mama Tina akitaka mwendelezo wakati mama huyo alisema wapumzike kwanza...
"Bana baby nini? Tupumzike kwanza jamani," alisema mama Tina akimlaza kwa nguvu kifuani kijana huyo.
"Si ulisema mwenyewe kwamba lazima leo tuweke kumbukumbu?"
"Ndiyo, si ndiyo nasema tutulie kwanza!"
* * *
"Baby si ulianza mwenyewe kunishikashika nikaamsha muwashawasha wangu, sasa tuendelee mimi mwenzio nimepamba moto sasa," alisema Halima akimng'ang'ania baba Tina pale kitandani.
* * *
Yalipita masaa manne tangu wote waingie kwenye gesti hiyo na kila mmoja sasa alifikiria kutoka kurudi nyumbani. Baba Tina na Halima waliamini wamechemsha, kwamba mama Tina na Os Anjelus kama walikutana kweli kwenye gesti hiyo walishaondoka zao muda mrefu.
"Unajua tumechemsha sana baba Tina. Kilichotuleta hapa sicho tulichokifanya," alisema Halima.
"Lakini kosa ni la wewe."
"Kosa langu lako? We si ndiyo ulianza kunishika. Unajua mi mwanamke ulitegemea nini sasa?" alisema Tina akivaa.
"We si ndiyo ulitoa wazo la kuchukua chumba ili iwe rahisi kufumania, ulitegemea nini mimi na wewe kuwa chumbani?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Tuache hayo, twende sasa," alisema Halima akifungua mlango.
Os Anjelus naye alikuwa akifungua mlango nyuma yake akiwa anafuata mama Tina ili kutoka, akashtuka kumwona Halima akiwa anatoka kwenye chumba, akageuka na kumsukuma mama Tina ambaye aliangukia kiti na kupasuka sehemu ya juu ya jicho la kulia, akapiga kelele...
"Mamaa."
Halima na Baba Tina walishtuka sana kusikia mama Tina akipiga kelele, wakaenda kwenye chumba hicho wakiwa na mhudumu ambaye pia alishtuka.
Os Anjelus alipoona tukio hilo alifunga mlango ili watu wasiingie, akiwemo Halima ambaye yeye alimuona. Hakujua kama alikuwa na baba Tina....
"Ngo ngo ngo," mhudumu aligonga mlango...
"Nani?" aliuliza Os Anjelus.
"Mimi mfanyakazi wa gesti hii."
"Unasemaje?"
"Nimesikia mlio ndiyo maana nimekuja kujua kuna nini?"
"Hakuna kitu."
Mama Tina aliendelea kulia kwa maumivu huku damu zikimtoka kwa wingi...
"Sikia mama Tina, kilichonifanya nikusukume nimemwona Halima hapo nje."
"Sasa si atakuwa amekuja kwa mambo yake jamani! Mimi nimeumia hivi, nitamwambia nini mume wangu? Nitasema nilikuwa wapi?"
"Tulia basi."
Baba Tina alimwambia mhudumu kwamba aliyepiga kelele ni mke wake hivyo akaomba ruhusa ya kuingia hata kwa nguvu ndani ya chumba hicho.
"Sasa mbona na wewe umekuja na huyu?"
"Ndiyo tulikuja kuwafumania."
"Sasa mbona mliingia chumbani mkajifungia?"
"Ndiyo kufumania kwenyewe huko, ulitaka tukae wapi? We niruhusu niingie."
Ilibidi mhudumu amwambie Os Anjelus kuwa mwenye mke amefika na anataka kumwona mke wake...
"Sasa sikia we kaka..."
"Nakusikiliza."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mwenye mke amefika, yupo hapa nje anataka kumwona mke wake."
"Huyo siye mwenye mke bwana. Huyo ni mpangaji mwenzake tu. Kwanza mwenye mke anawezaje kuwa naye mwanamke? We dada vipi?"
"Siyo mwanamke, mumewe kabisa."
"We kijana, mimi baba Tina hapa, fungua mlango tafadhali," baba Tina aliunguruma.
Mama Tina kidogo ajisaidie haja ndogo. Damu zilikatika zenyewe akajiona kama hajaumia. Alijua kimenuka!
"Mungu wangu, nitasema nini mimi? Ina maana yupo na Halima?" aliuliza mama Tina...
"Ndiyo maana yake. Lakini mbona nilimwona Halima akitokea chumbani?"
Mama Tina akakumbuka kuna wakati alisikia kicheko cha Halima mpaka akashtuka.
"Sasa nifungue?" Os Anjelus alimuuliza mama Tina huku akitetemeka miguu.
"Ujue yanaweza kutokea mauaji hapa. Please usifungue," alisema mama Tina huku akiangaza juu kama anaweza kuona sehemu ya kutokea. Alipoona hakuna akasema anajinyonga kwa kitenge alichovaa.
Cha ajabu pamoja na kusema hivyo, Os Anjelus hakuonesha kushtuka kwani na yeye alikuwa kwenye mpango huohuo wa kujimaliza kuliko kuyaona yatakayomtokea.
"Mnafungua hamfungui?" alihoji mhudumu huyo kwa sauti ya hasira.
Hakuna jibu lililopatikana zaidi ya ukimya kutawala huku kila mmoja mle ndani akiwa katika harakati za kutaka kujimaliza. Mama Tina alipanda kwenye kitanda, sasa alikuwa akijaribu kufunga kitenge kwenye nondo za dirisha ili atengeneze kitanzi cha kutumbukiza kichwa chake na kujining'iniza.
"Sikia binti, mimi nabomoa mlango, ukivunjika nakupa pesa yako wala usiwe na wasiwasi, hata kitasa nitakinunua, sawa?"
"Sawa."
Baba Tina alijipinda kwa kurudi nyuma kidogo kisha akaenda mbele na kuzama ndani.
Alimkuta mkewe ndiyo kwanza anajichomeka kwenye kitanzi huku Os Anjelus akiwa amelala sakafuni amepoteza fahamu...
"Ha! Yaani unataka kujinyonga siyo?" aliuliza kwa ukali baba Tina, akapanda kitandani na kumvuta mke wake, akaanguka chini puu mbaya zaidi akafikia upande uleule wa jicho lililoumia damu zikatoka tena kwa wingi...
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Yaani mama Tina hii ndiyo faida ya usaliti sasa, ona uso wako ulivyo," alisema Halima huku akicheka...
"Mume wangu nisamehe, naomba sana nisamehe."
"Ha! Yaani unataka kujinyonga siyo?" aliuliza kwa ukali baba Tina, akapanda kitandani na kumvuta mke wake, akaanguka chini puu mbaya zaidi akafikia upande uleule wa jicho lililoumia damu zikatoka tena kwa wingi...
"Yaani mama Tina hii ndiyo faida ya usaliti sasa, ona uso wako ulivyo," alisema Halima huku akicheka...
Mume wangu nisamehe, naomba sana nisamehe."
"Ni vigumu sana kwa sababu usaliti huu na mimi umeniingiza kwenye usaliti."
"Upi mume wangu?"
"Umenifanya nitembee na Halima bila kupenda."
"Haa! Mume wangu kumbe na wewe umenisaliti."
"Si nimekwambia mwenyewe."
"Sasa kama umenisaliti kwa nini usinisamehe mume wangu?"
"Kwa sababu tumesalitiana, basi tuamue wote kuachana."
"Mimi siko tayari mume wangu kwa kuwa nakupenda na ndiyo maana niko tayari kwa adhabu yoyote ile. Ndiyo maana kuliko kukupoteza nikaona bora nijiue," alisema mama Tina huku akilia ukijumlisha na damu zile za kuumia, baba Tina aliamua kumsamehe mke wake.
Alimsogelea akamshika na kumkumbatia...
"Nimekusamehe mke wangu, hata kama watu watasema mimi ni mwanaume ----- sawa tu, lakini najua tumetoka mbali ni shetani tu."
Halima kuona wanandoa hao wameamua kupatana kiasi kile aliamua kuondoka kimyakimya huku moyoni akisema...
"Ama kweli wapenzi wakigombana shika jembe ukalime, ukiingilia na wakipatana utabaki na aibu."
***
Mama Tina alitibiwa akapona, akajiahidi moyoni mwake kwamba hatakubali kutoka nje ya ndoa tena kwani kwa kijana Os Anjelus hakupata kitu zaidi ya kuumia na uwezekano wa kupata maambukizi ya Ukimwi.
Os Anjelus alihama kwenye nyumba hiyo, kwa vyovyote vile asingeweza kukaa na mbaya wake, baba Tina. Halima yeye aliishi kwa ugumu tu, hakuwa na salamu na mama Tina wala mumewe, achilia mbali mtoto wao.
***********************
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO
UJUMBE:
BAKI NJIA KUU MICHEPUKO SIYO DILI,KWA NAMNA YOYOTE ILE HAKUNA BINADAMU ALIYEMKAMILIFU KILA BINADAMU NA MAPUNGUFU YAKE DUMU NA MPENZI WAKO KWAKUWA UNAJUA MAPUNGUFU YAKE HIVYO HATA NJIA YA SAHIHISHA NI WEWE HUKO UNAKO TANGATANGA BADO HAUTAPATA KILE UKITAKACHO
0 comments:
Post a Comment