Search This Blog

Monday, October 24, 2022

LADHA YA TUNDA BIVU - 3

 





    Chombezo : Ladha Ya Tunda Bivu

    Sehemu Ya Tatu (3)





    HATA hivyo haikuwezekana. Frank na Linda walijichimbia chumbani humo hadi saa 1.30, giza likiwa limekwishaingia. Na baada ya mlo Frank aliondoka.



    Siku hiyo ilipita. Siku ya pili nayo ikafika na kupita. Ya tatu, hali kadhalika. Frank hakuonekana tena hapo, Frank ambaye tayari sura yake ilishaganda akilini mwa Catherine, na utaalamu wake wa michezo ya mahaba ukiwa umekwishajipenyeza hadi katika mishipa ya fahamu za Catherine kiasi cha kujikuta akitunza kumbukumbu kila wakati. Sasa kitu kingine kilimjia akilini dhidi ya Frank.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alimpenda!



    Alimtamani!



    Alimhitaji!



    Lakini atamwona wapi? Na atamwona lini ilhali hata hajui anaishi wapi?



    **********



    TANGU serikali ya Awamu ya Pili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipoingia madarakani, chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi, maarufu kwa jina la 'Mzee Ruksa,' miongoni mwa zile bidhaa zilizoitwa 'Bidhaa muhimu na adimu' zilianza kutapakaa mitaani. Takriban kila duka lilikuwa na hizo zilizoitwa bidhaa adimu.



    Bidhaa mbalimbali za ndani na nje ya nchi zilipatikana katika maduka mbalimbali nchini, bei yake ikiwa haitishi wala kuwastaaajabisha Watanzania wengi.



    Hakukuwa na ulazima wa kwenda katika duka la RTC kufuata sukari au ngano, bidhaa ambayo japo utauziwa, tena kwa kiwango utakachopangiwa, pia utashinikizwa kununua na bunda la vibiriti au chochote kile watakachotaka wao.



    'Ruksa' ile ilisababisha kila mfanyabiashara mwenye uwezo aagize chochote kutoka nje ya nchi na auze kwa bei aitakayo. Inadaiwa kuwa ile Tume ya Bei ilivunjiliwa mbali, hivyo kila mmoja akawa huru kununua kile anachokitaka na kukiuza kwa bei atakayotaka, awe amenunua ndani au nje ya nchi.



    Tanzania ilikuwa na wafanyabiashara wengi wenye uwezo wa kuagiza bidhaa nje ya nchi. Kuna ambao waliamua kuagiza vipuri vya magari. Wengine walizamia kwenye vifaa vya ujenzi mathalani saruji, mabati, nondo na kadhalika na kadhalika.



    Walikuwapo pia ambao waliagiza magari kutoka huko ng'ambo huku wengine wakiichangamkia 'ruksa' hiyo kwa kuagiza vifaa vya muziki. Pesa zilisambaa mifukoni mwa watu. Na miongoni mwa walionufaika na kipindi hicho ni Linda.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Yeye, siku moja usiku, miaka mitano iliyopita, alikutana na Mgiriki mmoja Southern Sun Hotel Barabara ya Ghana katikati ya Jiji la Dar es Salaam wakati huo hoteli hiyo ikiitwa Holiday Inn, wakazoena kwa muda mfupi walioketi pamoja, Linda akinywa soda na Mgiriki huyo akinywa toti kadhaa za pombe kali.



    Mgiriki akavutiwa na Linda. Akarusha ndoana. Ikanasa. Baadaye waliondoka pamoja hadi Beachcomber Hotel alikoishi Mgiriki huyo. Na ni huko ndiko pia palipoyabadilisha maisha ya Linda. Akitumia ujuzi aliojaaliwa maungoni mwake, alimfanyia yote ambayo Mgiriki yule aliyahitaji na aliyoyapenda. Ukawa ni usiku wa aina yake kwa Mgiriki huyo kiasi cha kujikuta akimpatia Linda dola 500 usiku uleule!



    Ni asubuhi ndipo Linda aliposhushiwa nyota nyingine ya jaha. Aliamka mapema alfajiri na kuingia bafuni kuoga. Alipotoka huko bafuni akamkuta mzungu wa watu bado anakoroma. Linda akaamua kulifungua begi la mzungu huyo na kupekua. Hakuzichekea noti alizozikuta ndani ya begi hilo.



    Dola 3,000!



    Pauni 1,500!



    Shilingi 5,000,000 za Tanzania!



    Aziangalie tu? Azichekee?



    Hapana, hakuwa 'bwege' kiasi hicho. Alichofanya ni kuzitwaa nguo zote zilizokuwamo na kuzimwaga chini pamoja na vikorokoro vingine. Ni pesa pekee alizoziacha. Kisha akalitwaa begi hilo na kutoka taratibu, kwa kujiamini. Hakukuwa na yeyote aliyemtilia shaka, takriban kila mfanyakazi alikuwa katika pilikapilika za kikazi, hivyo hakuna aliyemwangalia mara mbili, mbili. Akatoka taratibu hadi nje ambako alikodi teksi iliyomwacha Mwenge.



    Hapo alipanda daladala hadi eneo la Kinondoni ‘A’ Kwa Manyanya ambako kwa mara nyingine alikodi teksi iliyomfikisha Kinondoni Shamba katika chumba alichopanga.



    Kwa pesa zile aliweza kuubadili mfumo wa maisha yake. Sasa akawa mfanyabiashara. Akawa akisafiri mkoa huu hadi ule, akipeleka bidhaa hizi na zile. Biashara ikakubali hadi akafanikiwa kununua nyumba huko Kigogo Mburahati.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jirani yake alikuwa ni mzee Atupele, mzee mcheshi kwa kila mtu, aliyekuwa na mke na watoto. Ujirani wa Linda na Mzee Atupele ulikuwa wa heri zaidi kwani hata watoto wake walipazoea sana kwa Linda. Na hata Catherine alipokuja hapo ni watoto wa mzee Atupele ndio waliokuwa watu wake wa karibu.



    Latifah ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani kwa Mzee Atupele kama alivyokuwa Catherine, ndiye aliyekuwa akishinda sana nyumbani na kwa hali hiyo akatokea kuzoeana zaidi na Catherine kuliko wengine.



    Ni uhusiano huo mkubwa kati yao ndio uliomfanya siku moja Catherine amweleze Latifah kile walichokifanya na Frank. Alimsimulia kwa kina na kwa utulivu, na alipomaliza, Latifah alicheka kidogo, akamtazama kwa makini Catherine, akionekana kama mwenye maswali mengi.



    Kisha alimuuliza, “Kwani Cathy, hujawahi kuwa na bwana?”



    “Akha! Mwenzio sijawahi,” Catherine alijibu huku akinyanyua mabega na kuyashusha.



    “Una umri gani?”



    “Miaka...” Catherine alijibu na kusita kidogo. “Nina miaka kumi na saba.”



    “Miaka kumi na saba!” Latifah alishangaa. “Miaka kumi na saba hujamjua mwanamume?! Umechelewa wapi wewe? Uko katika dunia gani? Mwenzako hapa nd'o naingia miaka kumi na minane. Usilione hili lijimwili langu likakudanganya kuwa nina umri mkubwa. Akha! Mwenzio bado mbichi kabisa! Mimi na wewe hatupishani. Lakini mie ni'shakutana na wanaume watatu...”



    “Mbona sikuelewi, Latifah?” Catherine alimkata kauli. “Unashangaa eti sijamjua mwanamume. Kumjua mwanamume kivipi wakati tayari nimekwambia kuwa n'namjua Frank siku nyingi? Si mara moja au mbili amekuja nyumbani.



    “Wewe unasema u'shakutana na wanaume watatu. Yaani miaka yote hii umekutana na wanaume watatu tu! Ka' si uongo n’nini? Na huko kukutana na hao wanaume watatu kunahusiana nini na haya niliyokwambia?”



    Latifah alizidi kumshangaa Catherine. Akamtazama kwa makini. Kisha akaachia tabasamu dhaifu. Nyuma ya tabasamu hilo kulikuwa na wazo moja kichwani mwake. Kwamba, Catherine bado ni mshamba. Lakini hakupenda kutamka chochote kitakachomfanya Catherine alitambue hilo.



    Badala yake, akamwambia, “Cathy, ili nikwambie na unielewe vizuri, itanilazimu kutumia saa nzima. Lakini pia siyo vizuri kukuacha gizani. Chumbani kwangu kuna mkanda mmoja wa filamu ya mapenzi. Ni mkanda mzuri uliochezwa huko Ugiriki. Kesho asubuhi, hadi mchana, nitakuwa peke yangu. Jitahidi uje uucheki japo kwa nusu saa tu ili uijue dunia ya mapenzi ilivyo. Utapata nafasi?”



    Catherine alifikiri kidogo kisha akajibu, “Nafasi nitaipata. Mama huwa na kawaida ya kutoka na wakati mwingine hurejea saa sita mchana au hata jioni.”



    “Basi nafasi unayo,” Latifah alisema. “Fanya hivi; uje saa tatu au nne hivi. Nitakusubiri. Sawa?”



    “Sawa.”



    Siku iliyofuata, saa 3:30 asubuhi, Catherine alifika kwa Latifah. Wakati huo mwajiri wa Catherine, Linda hakuwapo nyumbani, na mabosi wa Latifah, Atupele na mkewe pia hawakuwepo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Catherine alikaribishwa sebuleni huku Latifah akiufunga mlango mkubwa kwa komeo kuepuka mtu kuingia wakati wakiwa wanauangalia mkanda huo. Latifah akaingia chumbani na kurejea muda mfupi baadaye, mkononi akiwa na mkanda huo.



    “Hii kanda nilipewa na bwana'ngu,” alisema huku akishughulika kuuweka katika deki. Akaendelea, “Kwa kweli huyo bwana siwezi kumsahau. Japo ndiye aliyeniingiza katika dunia mpya ya mapenzi, pia ndiye aliyenifundisha mengi ya kumridhisha mwanamume.”



    Akasita kidogo na kuifuata deki ya televisheni. Wakati akiweka kanda hiyo, japo hakugeuka kumtazama Catherine, hata hivyo aliendelea kuzungumza. “Sikufichi, shosti. Ili mambo yakuendee vizuri, usiwaringie wanaume. Sina maana uwe mtu wa kumkubali kila mwanaume. Hapana. Lakini pia usiwe mwepesi wa kumkataa kila akutongozaye. Kumkataa kila mwanaume inaweza kuwa ujanja au ushamba. Ukae ukijua hivyo.”



    Labda angeendelea kuzungumza kama ule mkanda aliouweka kwenye deki usingeanza kuzunguka, picha ikaanza kuonekana!





    *********



    HAIKUWA picha ya kawaida akilini mwa Catherine. Ilimshtua, ikamtisha na kumshangaza. Yaliyofanyika katika picha ile ya mapenzi hakuwahi kuyashuhudia hadharani wala sirini, zaidi ya kusikia katika vinywa vya watu.



    Kwa muda aliduwaa, akishuhudia tendo kwa tendo katika picha hiyo. Akashangazwa na hayo aliyoyaona. Hatimaye mshangao huo ulipotea na badala yake msisimko ukatwaa nafasi. Akapenda kuendelea kuitazama filamu hiyo. Akayakodoa macho, akili yote ikiwa imezama katika kila kilichofanyika.



    Sasa utulivu ukamtoka. Mara akawa akinyoosha miguu, mara akiikunja. Akagunaguna huku akiizamisha mikono katikati ya mapaja. Kwa kutumia vidole, alijaribu bila ya mafanikio kuuzima ‘moto uliomwakia’ huku pumzi zikimpaa na kushuka kwa nguvu.



    Latifah alimtazama kidogo tu, kwa chati na kugundua kuwa hayuko katika hali ya kawaida. Lakini akamwacha ataabike kwa muda. Dakika kama tatu, nne hivi baadaye akamhurumia na kuamua kuusitisha mzunguko wa filamu ile.



    “Vipi, umeionaje picha hii?” hatimaye alimuuliza huku kamkazia macho.



    Ni kama vile Catherine hakuwepo. Kwa jumla ni kiwiliwili chake tu ndicho kilichokuwa hapo wakati huo, lakini akili yake ilikuwa mbali, alikuwa akiyakumbuka yale aliyofanyiwa na Frank siku chache zilizopita. Yote aliyofanyiwa na Frank aliyaona katika mkanda huo, lakini kulikuwa na ziada. Na ni ziada hiyo iliyomchanganya vilivyo kiasi cha kuhisi kuwa kuna kitu fulani muhimu zaidi alichokikosa siku ile Frank alipouchezea mwili wake.



    Alimsikia Latifah akimuuliza swali lile. Lakini japo alilielewa, hata hivyo hakuwa na nguvu ya kujibu. Ni pale Latifah alipoamua kumgusa begani na kumtikisa kidogo kabla ya kulirusha swali lile ndipo Catherine alipoipata sauti yake.



    “Ni mkanda wa ajabu,” alijibu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Wa ajabu?”



    “Ndiyo.”



    “Hakuna chochote cha ajabu. Huo ndio mkanda unaopaswa kuuangalia,

    uielewe dunia ya mapenzi ilivyo.”



    Catherine alibaki akimtazama Latifah bila ya kutamka chochote.

    Latifah akaendelea, “Si umemwona jinsi mwanamke mwenzetu, mwanamke mweusi anavyoweza kuvimudu vifua vya wanaume watatu? Mwanamke pumzi shosti. Mwanamke, mbinu za 'mchezo' na mwanamke ni kujituma. Ukifuata kanuni hizo kwa bwana'ako, nakuapia, utajikuta unamiliki gari au nyumba hivihivi siku si nyingi. Sikudanganyi shoga, huo nd'o ukweli.”



    Lilikuwa ni somo zito kwa Catherine. Akajiona kuwa yu gizani, tena ndani ya giza zito. Na hakutaka kuendelea kudumaa humo gizani, alitaka kuwa nuruni. Aielewe dunia ya mapenzi. Awe kama wanawake wengine.



    Ndipo ikaja siku nyingine, siku ambayo Frank alikuja tena mchana, kitu kama saa 7 hivi. Na kwa mara nyingine akamkuta Catherine peke yake.



    “Amekwenda wapi?” Frank alimuuliza Catherine.



    “Huwa haniambii anakokwenda. Anajiandaa tu na kuondoka zake.”



    “Katoka saa ngapi?”



    “Kama saa tatu hivi.”



    Frank akiwa ameketi katika moja ya masofa makubwa yaliyoipendezesha sebule hiyo, alimtazama Catherine kwa macho ya utulivu na kuongeza swali, “Alionekana kama anayekwenda mbali?”



    Catherine alijibu kwa kutikisa kichwa, akiashiria kukubali.



    Frank alishusha pumzi ndefu. Akamwangalia kwa makini Catherine na kuvutiwa na uvaaji wake wa mchana huu. Akiwa ni msichana mbichi, Catherine alikuwa amevaa kanga tupu aliyofungia fundo shingoni na sehemu ya mgongo wake kubaki wazi. Wakati huo alikuwa amesimama, kaegemea mlango wa chumba chake na alionekana kupendeza zaidi machoni mwa Frank.



    Akilini mwa Frank, hii ilikuwa ni nafasi nyingine nzuri kwake. Alishaingiwa na tamaa ya kimwili dhidi ya Catherine. Na tangu siku ile alipopata wasaa wa kutalii katika mwili huo uliofinyangwa vyema na muumba, uchu wa kuhitaji jambo, zaidi ya utalii ule ulimganda kichwani.



    Japo alikuwa na uhusiano wa mapenzi na Linda, na kujikuta akizifaidi fedha zake mara kwa mara, hata hivyo kwake, uhusiano huo haukuwa wa dhati, hakuwa akimpenda kutoka moyoni. Kwa jumla hakuwa akimpenda bali alizipenda fedha zake na 'fujo' zake kitandani.



    Alimpenda Catherine.



    Alimhitaji Catherine.



    Siyo Linda!



    Ni Catherine aliyekuwa ameuteka moyo wake tangu siku ile aliyopata fursa ile, hivyo taarifa kuwa Linda hayupo, kwake ilikuwa ni taarifa njema kuliko ilivyo. Alijipa matumaini kuwa lolote lile aliloamua kulitekeleza lingefanikiwa.



    Catherine naye alikuwa akiitafuta nafasi hiyo kwa udi na uvumba. Lile somo alilopewa na Latifah lilimwingia vilivyo kinadharia, hivyo alitaka aanze kulifanyia zoezi kwa vitendo. Hakutaka kuipoteza nafasi hii ambayo hakujua kama ataipata tena.



    Hakuutarajia ujio huu wa Frank. Alijua kuwa lazima angekuja tena, lakini hakuijua siku. Na hata kama angekuja, hakuwa na hakika kuwa atamkuta Catherine peke yake. Labda Linda angekuwepo, labda wangekuja wote, na au labda angemkuta mgeni yeyote hapo na hivyo kuwa ni ujio usiokuwa na faida yoyote kwake, Catherine.



    Leo kaja na kamkuta peke yake! Furaha ilimtawala Catherine, furaha iliyoambatana na woga wa kiasi fulani. Pamoja na kusisimuliwa kwa kiwango kikubwa na ile sinema ya mapenzi, hata hivyo alishawahi kusikia kuwa kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza kwa msichana yeyote huambatana na maumivu makali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini, pia ni kwamba maumivu hayo huwa ni ya muda mfupi tu na kitakachofuata ni raha ya kipekee, raha ambayo kila mwanamke anaihitaji. Yeye hakuyaogopa sana maumivu hayo, aliihitaji zaidi raha iliyozungumziwa. Hivyo, mara nyingi usiku, kabla hajalala alikuwa akisali kuwa Mungu amlete tena Frank, tena amlete wakati Linda hayupo.



    ‘Mungu kayapokea maombi yangu,’ alijisemea kimoyomoyo huku akiyaepuka macho ya Frank. Akawa akiutumia muda mwingi kuuinamisha uso wake.



    “Cathy, una kazi yoyote saa hizi?” Frank alimuuliza.



    Catherine hakujibu. Alimtazama kidogo tu Frank na kuyarejesha macho yake sakafuni. Akakitia kidole kimoja mdomoni na kuwa kama anayekinyonya kitoto-toto huku wakati huohuo vidole vya miguu vikisugua sakafu. Ni kama vile alikuwa akiandika kitu fulani sakafuni hapo kwa kuvitumia vidole hivyo.



    “Cathy,” Frank alimwita tena.



    Kama awali, Catherine hakuitika bali safari hii alimtazama Frank usoni sawia.



    “Una kazi nyingi?”



    Catherine alitikisa kichwa akionyesha ishara ya kukataa.



    “Njoo basi, tupige stori kidogo.”



    Catherine aliinua mabega akionyesha ishara ya kukataa.



    “Unaogopa nini? Linda hawezi kurudi sasa hivi. Au unamwogopa?”



    Bado Catherine hakujibu kwa sauti. Aliendelea na mchezo wake wa kusuguasugua vidole sakafuni.



    Frank alisimama, akamfuata pale ukutani na kumkumbatia. Ni hilo alilolihitaji Catherine. Na safari hii hakuwa 'mshamba' kama ile siku ya kwanza. Alijikusanya kifuani kwa Frank huku naye akiitumia mikono yake kumpapasa-papasa.



    Wakajisahau kwa muda, wakiiruhusu mikono yao kupita kila walipotaka. Catherine akiwa na kumbukumbu ya ile sinema ya ngono, akamruhusu Frank ambusu kinywani, busu ambalo lilimchanganya zaidi binti huyo na kumfanya asahau kuwa yuko wapi na yuko na nani.



    Walipotenganisha vinywa vyao, Catherine alikuwa zaidi ya mgonjwa wa kawaida, akionekana dhahiri kuhitaji tiba zaidi ya tiba hii aliyopewa.



    “Twende chumbani kwako,” hatimaye Frank alimwambia.



    ******CATHERINE YUKO NA FRANK. ANAAMBIWA WAENDE CHUMBANI. NI KIPI KITAFUATA?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA



0 comments:

Post a Comment

Blog