IMEANDIKWA NA : INNOCENT A. NDAYANSE (ZAGALLO)
*********************************************************************************
Chombezo : Ladha Ya Tunda Bivu
Sehemu Ya Kwanza (1)
KWA mara nyingine alisimama, akajitazama kupitia kioo kirefu kilichokuwa chumbani humu. Akajisifu kimoyomoyo kwa jinsi Mungu alivyomjaalia umbo la kipekee, umbo aliloamini kuwa ni miongoni mwa sumaku thabiti dhidi ya wakware. Akaachia tabasamu dhaifu, tabasamu ambalo pia lilimtia kiburi kwa kuamini kuwa mpangilio mzuri wa meno yake ulimzidishia urembo, zaidi ya urembo aliokuwa nao.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara akayashikashika matiti yake yenye ukubwa wa wastani. Akazifinya kidogo chuchu za matiti hayo. Hakuwa na sababu ya kutoringa kwa kujaaliwa matiti hayo ambayo si mara moja wala mbili tu, wanaume kadhaa alioanguka nao kitandani walionyesha dhahiri kuyashupalia, zaidi ya walichokihitaji.
Sasa aliyaacha matiti hayo. Akaipeleka mikono kichwani. Akazishikashika nywele nyingi na nyeusi tii zilizodhihirisha kurutubishwa kwa chakula chenye protini zote sanjari na bia mbili tatu za afya. Akacheka kidogo alipomkumbuka mwanamume mmoja aliyezipenda sana nywele hizo kiasi cha kujikuta akifika kileleni mapema kila azishikapo wakati wanapokuwa faraghani.
Mikono iliziacha nywele hizo, ikashuka taratibu hadi nyongani. Hapo haikutulia sana, ikahamia tumboni na kuteleza hadi kwenye maungio ya miguu ambako alitumia vidole vyake kupapasa taratibu kama ambavyo yule mwanamume, na yule mwingine, na mwingine tena walivyokuwa wakimfanyia pindi kila mmoja, kwa siku yake walipojihifadhi ndani ya gesti au popote pale walipoona kuwa panawafaa, wakati huo nguo zao zikiwa kando ya miili yao.
Kuna mwanamume mmoja alidiriki kumpa shilingi 50,000 ili tu autembeze ulimi wake kutoka nyongani hadi kwenye mapaja hayo, ombi ambalo mrembo huyo hakuwa na sababu ya kulikataa. Alimruhusu, lakini tofauti na wanaume wengine ambao ruhusa hiyo ingewafanya wafikie hatua ya kubembeleza jambo jingine muhimu, huyo aliondoka akiwa amekidhi haja yake ya mwili kwa njia hiyo.
Mara akaipeleka mikono nyuma, viganja vyake laini vikagota kwenye makalio. Alijitambua kuwa alibarikiwa makalio makubwa, ambayo kila atembeapo, awe amevaa sketi au gauni pana kiasi gani bado yalimuumbua. Mtikisiko wake ni kama vile ulikuwa ukimsuta kwa kumwambia: “HATA UKITUFICHA, WANAOTUTAMANI WATATUONA TU.”
Kicheko cha huzuni kikamjia alipokumbuka kuwa siku hizi kuna teknolojia mpya ya kutumia dawa za kukuza makalio na matiti. Akawaonea huruma hao wanaotumia dawa hizo kwa kuwa alikwishazipata taaarifa za kitaalamu kuwa dawa hizo zina athari kubwa katika mwili wa mtumiaji.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 33 kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere miaka kadhaa iliyopita, alihudhuria katika mabanda mbalimbali viwanjani humo. Moja ya mabanda aliyotembelea ni banda la Mamlaka ya Chakula na Dawa ambako alikumbana na taarifa za kutisha na kusikitisha kuhusu madhara ya dawa za kuongeza ukubwa wa viungo.
Mtaalamu alikuwa akitoa maelezo kwa waliotembelea hapo kuwa, dawa za kuongeza matiti ambazo kitaalamu ziliitwa BUST UP CREAM pamoja na zile za kukuza ukubwa wa makalio zilizoitwa HIP LIFT UP zina sumu ya Zebaki hivyo zikipakwa kwenye ngozi hupenya taratibu mwilini na sumu yake kuingia kwenye damu. Athari zake ni kwa mtumiaji kupata kansa ya ngozi, mtindio wa ubongo na hata figo huathirika kwa kiwango kikubwa. Na madhara hayo hujitokeza muda mrefu baada ya kutumiwa kwa dawa hizo.
Kumbukumbu hiyo ya maelezo ya mtaalamu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa yalimfanya amshukuru Mungu kwa kujaaliwa umbo hilo na kuwalaumu wale wanaotumia dawa za kukuza makalio na matiti na akawachukulia kuwa ni watu wanaoikosoa kazi ya muumba.
“Eee Mungu wangu nakushukuru kwa kunijaalia umbo hili,” alijikuta akinong'ona kwa sauti ambayo hata haikuyafikia masikio yake mwenyewe.
Akaendelea kujishika, na sasa akageuka upande na akajitazama kwa kupitia kioo hikihiki. Ndipo aliridhika kuwa robota hilo lililomininwa chini ya nyonga yake lilitosha kumtia wazimu rijali yeyote na kuwafanya wanawake wenzake wamtazame kwa husuda.
**********
ALIITWA Catherine. Historia ya maisha yake inaanzia miaka kumi na minane iliyopita huko Sengerema mkoani Mwanza alikozaliwa. Mama yake, Miriam hakuitarajia mimba iliyomleta duniani Catherine. Ni ile siku alipokubali kumchojolea nguo jamaa mmoja aliyemsumbua kwa kumtaka penzi, ndipo mimba ilipotunga. Dawa za mitishamba alizotumia mara kwa mara safari hii hazikuyatii matakwa yake. Mimba haikuchoropoka. Hatimaye akainua mikono, akaiacha mimba hiyo ikue, na ikakua hadi miezi tisa ikagota.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ndipo alipojifungua mtoto mzuri wa kike, mtoto ambaye alimpa jina la Catherine. Mwezi mmoja baadaye, kila jirani alitambua kuwa mtoto wa Miriam anaitwa Catherine. Lakini Mama Catherine hakuwa radhi kumtunza mtoto kwa kipindi hicho.
Alikuwa ni mtoto aliyepatikana kwa bahati mbaya, kilichomshinda ni ile hatua ya kumtupa chooni au popote pale baada ya kujifungua. Kumtupa mtoto aliona kuwa ni dhambi zaidi ya dhambi alizozijua, na ni dhambi isiyosameheka.
Ndiyo, hakumtupa lakini hakuwa tayari kumlea. Akapanga mbinu. Siku moja, saa 4 asubuhi alimbeba Catherine na kwenda naye kwa jirani ambako alimwomba amlee kwa muda wakati yeye anakwenda kuteka maji kisimani.
Jirani hakuwa na hiyana. Isitoshe, alikuwa na mapenzi makubwa na watoto, hususan watoto wazuri kama huyo Catherine. Hivyo alimpokea na kumpakata.
Robo saa ilipita, Miriam hajarudi.
Nusu ikakatika.
Hatimaye saa nzima!
Jirani yule akashtuka. Akaamua kumfuatilia huko kisimani alikodai kwenda. Hakumkuta! Akatoa taarifa kwa watu wengine. Sasa ukafanyika msako rasmi. Ndipo ikabainika kuwa katoroka! Ujumbe wa maandishi aliouacha nyumbani kwake na pia kubainika kuwa kabeba nguo zake ilikuwa ni taswira tosha kuwa katoroka. Ndiyo, aliikimbia Sengerema, lakini hakujulikana aliko. Catherine akabaki chini ya malezi ya yule jirani.
Lakini mama huyo naye alikuwa na familia yake, watoto wanne kutoka tumboni mwake na watoto wawili wa ndugu zake. Hivyo, akaafikiana na mumewe kumpeleka mtoto huyo katika ofisi za Ustawi wa Jamii.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ni huko alikolelewa hadi akatimiza umri wa kuanza masomo ya elimu ya msingi. Lakini hata kwenye hayo masomo hakufika mbali. Alitoroka akiwa darasa la nne. Alitoroshwa na mama mmoja ambaye alimshawishi, akimwahidi kumpatia kazi na malipo mazuri.
Siku ya tatu walikuwa wakiteremka kutoka kwenye treni jijini Dar es Salaam. Wakakodi teksi iliyowaacha Kigogo Mburahati, nyumbani kwa mama huyo aliyeitwa Linda.
Linda alikuwa anakaribia umri wa miaka arobaini na mitano, na alikuwa hajajaaliwa kupata mtoto. Alikuwa ni mfanyabiashara ambaye alilazimika kusafiri huku na kule, mikoani. Aliwahi kuolewa, lakini siku alipomfumania mumewe akifanya mapenzi na mwanamke wa mtaa wa pili, ndani mwao, katika kitanda chao, alijiona kuwa kadhalilishwa kwa kiwango kisichokadirika.
Ndoa ilivunjika, na kuanzia hapo Linda hakutaka kusikia neno 'kuolewa' tena. Hakumwamini mwanamume yeyote kwa suala la kuolewa. Akaamua tu kuwa na mtu wa kumtuliza kiu yake.
Walipofika nyumbani alimkaribisha Catherine na kumtayarishia chakula, na kisha akampatia nguo nyingine. Ni jioni ndipo alipompa majukumu.
“Utakuwa ukifanya kazi za ndani kama kusafisha nyumba, kuosha vyombo, kufua na shughuli nyingine ndogondogo. Mshahara wako utakuwa ni shilingi elfu kumi kwa mwezi; kulala,
kula ni juu yangu.”
Catherine akawa ameyaanza maisha mapya, maisha ambayo yalilibadili umbo na sura yake kwa kasi ya kutisha. Mwaka mmoja tu baada ya kuanza kuishi hapo hazina ya urembo wake ilijidhihirisha bayana. Hata hawara za Linda walipokuja hapo hawakukosa kumtupia macho yenye kila aina ya kumhitaji.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akiwa hajui hili wala lile kuhusu ngono, hakuweza kukibaini kilichojificha katika macho yale ya wanaume wakware. Lakini siku moja, kijana mmoja mtanashati alikuja nyumbani hapo. Si mara moja au mbili Catherine aliwahi kushuhudia kijana huyo na mama mwajiri wake wakijifungia chumbani usiku lakini hakujua kuwa kulikuwa na ziada huko chumbani kabla ya usingizi kuwapata.
Kijana huyo aliyeitwa Frank, alipofika na kugundua kuwa Linda hayupo, alianza kumchokonoa Catherine. “Siku hizi mambo yako s'o mabaya, Cathy.”
Catherine hakuwa na la kusema. Akaishia kucheka tu.
“Cheki mishavu ilivyonona,” Frank aliendelea huku akimpapasa Catherine mashavu.
Mara mkono huo ukahamia kifuani na kuzitomasa chuchu za matiti. Catherine akahisi damu ikimwenda mbio. Akaushika mkono huo na kuutoa taratibu. Frank alitii, lakini mara tena akaurejesha mkono huo palepale na kuendelea kukifanya kilekile ulichokuwa ukikifanya awali. Na zaidi, alidiriki kutalii hadi katika sehemu nyingine za mwili huo ulionona, nafsi yake ikiburudika huku damu ikimchemka kwa kiwango cha juu.
Catherine aliihisi starehe ambayo hakuwahi kuipata. Alizidiwa kiasi cha kujikuta akiachia kinywa wazi, tendo lililompa mwanya mwingine Frank, mwanya wa kuendelea na hatua nyingine muhimu. Akausogeza mdomo jirani na mdomo wa Catherine. Taratibu akaupenyeza ulimi wake kinywani mwa Catherine.
Likawa ni tukio jingine lililompeleka binti huyo katika ulimwengu mpya. Akakaribia kuzirai. Hili lilikuwa ni tukio la kwanza kwake kutendewa, lakini likawa ni tukio lifurahishalo na lililomsisimua kwa kiwango kikubwa. Na hakutaka ulimi huo wenye joto linalosisimua utoke kinywani mwake. Wala hakutaka mikono ile iliyozunguka kiunoni mwake isitishe zoezi la kutomasatomasa. Alihitaji zoezi hilo liendelee, na liendelee zaidi.
Kama siyo ngurumo ya gari lililoegeshwa nje ya nyumba hiyo, huenda wangefika mbali zaidi katika mchezo huo. Walishtuka na kutengana huku Catherine akijitupa sofani kwa 'uchovu.' Frank, yeye aliketi katika sofa jingine na kujitahidi kujiweka vizuri ili isije ikatokea taswira yoyote itakayomshtua huyu aliyekuja na gari.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda mfupi baadaye, Linda aliingia sebuleni humo, mkononi akiwa ameshika kapu lililosheheni vyakula alivyovinunua sokoni. Akawatupia macho Catherine na Frank, akitabasamu. Frank akaepuka kutazamana naye usoni, akijisikia kuwa na hatia. Wakati huohuo, Catherine akanyanyuka na kumpokea lile kapu.
“Leo njaa inasumbua, bibie,” Linda alimwambia Catherine. “Kaandae mapema na chapchap. Kila kitu kiko humo. Sawa?”
“Sawa, mama,” Catherine alijibu akitokomea jikoni.
Linda aliketi sofani kwa kujitupa puu! Akashusha pumzi ndefu na kumtupia jicho Frank.
“Vipi, umechoka sana?” Frank alimuuliza.
“Aaah… s'o sana. Kiasi tu. Umenisubiri sana?”
“S'o sana,” Frank aliongopa. “N'na kama dakika tano tu tangu nifike.”
Linda hakusema kitu. Kwa mara nyingine akashusha pumzi ndefu. Wakatazamana, safari hii Frank akijitahidi kuwa jasiri na kutoyaepuka macho ya Linda. Macho ya kila mmojawao ni kama vile yalikuwa yakizungumza jambo fulani muhimu. Lakini Linda, kama kawaida yake mikono yake ilikuwa miepesi, hivyo hakuishia kutumia macho tu, bali aliutupa mkono wa kushoto kwenye paja la Frank, akawa akipapasa kwa namna iliyomtia Frank katika hali isiyoelezeka kwa urahisi.
Hatimaye ni kama vile walijisahau. Mikono ya kila mmoja ikawa ziarani, kila mmoja akiutalii mwili wa mwingine. Sasa wakawa wakitazamana kwa karibu zaidi, kila mmoja akizisikia pumzi za mwenzake. Tayari macho ya Linda yalikuwa yakizungumza mengi, na mengi hayo yalionekana dhahiri kuwa anahitaji adhabu nyingine, adhabu inayofariji na kuliwaza.
Pamoja na hayo, Linda naye hakuwa mbumbumbu katika nyanja ya mapenzi. Hadi alipofikia hatua hii ya kukutana kimwili na Frank hakuwa na takwimu sahihi ya wanaume aliokwishaanguka nao kitandani. Kwa makisio ya karibu hawakupungua kumi japo hawakutimu ishirini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kuna ambao pindi alipotazamana nao, alibaini kuwa walimtaka. Wengine walishangaza; wao walimtongoza, wakatanguliza dau la pesa lisiloepukika, lakini wakachukua dakika chache sana faraghani wakawa hoi bin taabani!
Sio hao tu. Kuna wale wanaume wawili ambao kamwe asingeweza kuwasahau. Hao, kila mmoja kwa siku yake walikwenda naye dansini. Ni huko dansini kulikomfanya asiwasahau.
Mmoja, yeye alimpeleka kwenye muziki wa ‘rusha-roho’ katika ukumbi fulani eneo la Magomeni Mikumi. Mwanamume huyo hakuwa mpenzi sana wa muziki wa taarabu, lakini alikuwa na taarifa kuwa katika kumbi hizo huwa kuna vituko vya kiuchezaji kutoka kwa wanawake ambao huwa wanahudhuria kwa wingi. Na uchezaji huo wa 'kihasara-hasara' aliwahi kuushuhudia kupitia vipindi vya televisheni.
Walipokwenda hapo, mwanamume huyo alimnunulia bia kadhaa ili achangamke, na alipochangamka akamwambia acheze. “Nasikia unajua sana kucheza taarabu, hebu cheza basi, tena ucheze bila ya aibu.”
Linda alikuwa na umbo la wastani, teketeke na makalio yake yakiwa yamebinuka kiasi. Kucheza muziki wa taarabu kwake lilikuwa ni jambo la kawaida sana na alilolipenda. Na alijiamini kwa fani hiyo. Aliwahi kutuzwa pesa nyingi siku moja kwenye ukumbi fulani huko Ilala alipolivamia jukwaa na kufanya vitu vyake, bia kadhaa zikiwa zimekwishatambaa kwenye mishipa ya fahamu zake.
Hivyo, hata usiku huu akiwa na huyu bwana wake ‘mpole-mpole’ hakuona haya kulitekeleza ombi hilo. Alisimama na kulivamia jukwaa. Akaanza kucheza. Uchezaji wake ukawavutia wengi. Akatuzwa pesa mfululizo.
Hata huyu mwanamume alivutiwa kwa kiwango kikubwa. Lakini walipoondoka hapo na kuelekea nyumbani kwa mwanamume huyo, ndipo Linda alipoishia kustaajabu na kumshangaa mwanamume huyo. Hakukuwa na cha ziada chumbani, zaidi ya mwanamume kuridhika kwa kumkumbatia-kumbatia na kumpapasa-papasa!
Hali hiyo ilitokea takriban mara tatu walizokutana, na ikafikia hatua ya Linda kumhoji, “Kwa nini uko ivo? Una matatizo gani?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Dunia imeharibika siku hizi, Linda,” lilikuwa ni jibu la mwanamume huyo. “Wewe hunijui, mimi sikujui. Tumekutana kimjini-mjini tu.”
“Najua unaogopa Ukimwi,” Linda alisema huku akibibitua midomo. “Tumia kondomu. Ninazo.”
Mwanamume yule alitikisa kichwa akiashiria kukataa. “Hata kondomu haziaminiki sana. Unaweza kuvaa kondomu na ikakupasukia. Tutakuwa tumefanya nini?”
Linda hakujisumbua zaidi kumhoji, lakini aliamini kuwa mwanamume huyo siyo mzima katika maungo yake. Na katika kutaka kuthibitisha kuwa huyu mwanamume ni mzima au mbovu, aliamua kufanya upekupeku kwa mashangingi wawili, watatu. Shangingi mmoja aliyeitwa Maimuna akamwambia, “Kha! Yule!…Nikikusimulia hutaamini! Namjua nje-ndani!”
“N’ambie mwenzangu…” Linda alisihi, macho kayatoa pima.
Maimuna akapasua!
** ** ** ** ** **
****HUYO NDIYE LINDA...HUYO NDIYE CATHERINE NA HUYO NDIYE FRANK. MAMBO YANAZIDI KUWA MAMBO.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment