Search This Blog

Monday, October 24, 2022

ASIA DIGITALI - 4

 





    Chombezo : Asia Digitali

    Sehemu Ya Nne (4)



    Waliagana, Asia akaondoka akiwa ametimiza azma moja ya kupata miadi kutoka kwa bwana Lucas.

    Hiyo ilikuwa hatua kubwa sana……

    Asia aliondoka huku tabasamu likiishi katika midomo yake.

    Alikuwa na haki ya kutabasamu maana kwa kiasi kikubwa alikuwa amefanikiwa katika malengo yake. Lengo la kuanza kuichota akili ya mkufunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, bwana Lucas.

    Asia alizama katika gari alilokujanalo. Akatia moto, akaondoka zake.

    Baada ya masaa kadhaa alikuwa chumbani, alikuwa akijiuliza maswali iwapo ni kweli alichoambiwa kitafanya kazi ama la.

    Asia akanyanyua simu yake akapiga namba fulani.

    “Nakuja hapo sasa hivi.” Alizungumza.

    Kisha akabadili nguo, akatoka nje.

    Asia alijivuta hatua kadhaa, akatazama kushoto na kulia akaliona gari.

    Akapunga mkono wakamwona, gari likasogea upande wake.

    Gari ikaegeshwa, wakashuka wanawake watatu.

    “Mambo Asia…..”

    “Poa wadada karibuni….”

    Asia aliwakaribisha wakachukua nafasi wakaketi, ilikuwa mara yao ya pili kuonana.

    Walianza kuongea wakianzia walipoishia, akina mama hao walikuwa na shida ya kumkomoa mwanamke ambaye alikuwa akijitamba hasahasa baada ya kufunga ndoa na mwanaume ambaye alikuwa hawara wa mmoja kati ya wanawake wale.

    Shida yao kubwa ilikuwa kumkomoa mama yule, kumfunza ajue kwamba mume wake si lolote si chochote.

    Wakaelekezwa kwa Asia.

    Aliyeusuka mchezo huu na kumuunganisha Asia na wanawake hawa alikuwa ni yuleyule mtaalamu wa mipango ya nje na ya ndani.

    Husna Messi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sasa Asia alikuwa amechukua tenda hii na aliamini ataitendea haki.

    Siku hii ilikuwa ya kupewa pesa ya awali ya malipo kwa ajili ya kuendelea na kazi hii.

    Laki nne zikawekwa mezani, Asia hakuzihesabu akazikita katika pochi yake.

    “Kwa hiyo tutegemee lini..” mama yule aliyekuwa na uchungu kupita wote aliuliza.

    “Nampika kwa sasa, nitakupa taarifa ya maendeleo. Lakini hautazidi mwezi mmoja.” Alijibu kiuhakika Asia.

    “Umeonana naye tayari?”

    “Yeah si ndo anaitwa Lucas, amepanda hewani na ana mwili wa mazoezi.” Alijibu Asia. Hakika alikuwa anamzungumzia yuleyule Lucas. Mkufunzi wa chuo kikuu.

    Mazungumzo yakamalizika. Akasimama na kuondoka zake.

    Kitendo cha kuchukua pesa za watu kilimfanya Asia awaze mara mbilimbili atafanya nini kumkomoa yule bwana ili aweze kuaminiwa zaidi na wale wanawake waliompa kazi ile.

    Asia akaijiwa na wazo, akatuma ujumbe kwa mtu aliyemfahamu yeye.

    Majibu yaliyokuja yakamfanya atabasamu.

    Kisha akalala, akiwa ameingiza pesa nyingi.

    ****

    Siku iliyofuata kama alivyotarajia, majira ya jioni. Asi akapokea simu. Ilikuwa namba mpya.

    “Halow Halima…..Lucas hapa.”

    “Lucas yupi, samahani.” Aliuliza maksudi Asia.

    “Yule wa jana chuo…”

    “oooh habari bwana mkubwa…nambie.”

    “Leo jioni tunaweza kuonana kwa ile ishu?”

    “Bila shaka tutafanya hivyo….mi nakusikiliza wewe.”

    Mazungumzo yakaenda sawia, hatimaye wakakubaliana kukutana katika hoteli mojawapo katikati ya jiji.

    Asia alikuwa anaifahamu.

    Baada ya kukata simu ile Asia alipiga simu kwa bwana aliyemtumia ujumbe usiku uliopita.

    Akazungumza naye, akamuelekeza wapi alipo wakenda kuonana.

    Hayakuwa mazungumzo ya muda mrefu. Wakaachana baada ya Asia kukabidhiwa kifuko kidogo.

    Akamkabidhi noti kadhaa bwana yule.

    ****

    Majira ya saa moja usiku, Asia na Lucas walikuwa katika mazungumzo mazito. Mazungumzo juu ya namna ambavyo watakuwa wakifundishana. Wakafikia makubaliano, Asia akabadili mada. Mara aseme hiki mara kile.

    Hatimaye akaamua kuirusha karata yake.

    Akayakumbuka maneno ya yule bwana aliyempatia ile dawa.

    “Hii Bukoba wanayo SHUNTAMA….huku sisi tunaiita hii Daiko…..akichomoka hapo basi mwanaume.”

    Asia akachomoa pipi akabugia moja kisha akawahi kuomba samahani kwa kula peke yake.

    Akatoa nyingine akampatia.

    Maongezi kadha wa kadha yakaendelea kisha wakaagana.

    Asia akayangoja majibu. Na hakika usiku huo haukupita, mara ukaingia ujumbe Lucas alihitaji kumpigia simu.

    Asia akakubaliana naye.

    Lucas alivyopiga simu akakosa la kuzungumza badala yake akawa anabwabwaja kama tahira.

    Asia akawa anamuunga mkono.

    Hatimaye wakakubaliana kesho waonane mida ya usiku.

    Hicho kitu Asia alikuwa anakisubiria ili amalize mchezo.

    Akili ya Lucas na usomi wake alikuwa amekamatwa kimadawa, hakuwa akijielewa.

    Lakini ni bora hali ile ingeishia pale lakini akafanya kosa kujiruhusu kuonana na Asia faragha.

    Ulikuwa usiku wa namna yake.

    Asia akakolezea mapenzi. Akazidi kujikita katika mapenzi ya kijanja janja, nia yake ikiwa kumkamata vyema Lucas.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ile hali ya kuelezwa kuwa Lucas si mcha Mungu sana ilimpa nafasi Asia ya kuamini kuwa hata kinga yake kijana huyu itakuwa ndogo na hakika ilikuwa hivi.

    Iwapo unaifahamu shuntama na madhara yake basi Daiko huwa ni mara mbili yake.

    KWA WASIOJUA: Shuntama, hii dawa maarufu kabisa mkoani Kagera, ukifanyiwa hii na mwanamke utarukaruka wee huko unapojua lakini kila atakalosema utamsikiliza. Unakuwa kama umeshikiwa akili vile, na iwapo akikutishia kukuacha unaweza kufa kwa presha.

    Usiku huu Asia alivyoipata nafasi ya kukutana kimwili na Lucas asiyejielewa, akamwongezea pigo jingine.

    Sasa hii ilikuwa ni aina ya ‘GENDA UGERUKE’…hii nayo ni ya aina yake, ukimpenda mtu ambaye yupo Mwanza, akikufanyia hii, hauutamani mji mwingine zaidi ya Mwanza. Yaani kila mara unatamani kuwa katika mji ambao mpenzi yupo. Hii hutumiwa sana na wale wapenzi wenye wasiwasi wa kuwa mbali na wapenzi wao.

    Asia akajipakaa vyema kabla ya kumkabili Lucas.

    Lucas alikuwa amekolea kumbe mwenzake ni king’amuzi anang’amua chaneli mpya mpya za burudani na michezo.

    ****

    Baada ya siku nne Asia alikuwa na wale wanawake waliompa dili hilo la kumkamata yule mwanaume hadi amsahau mkewe na familia kwa ujumla.

    “Tutaaminije kama kweli umefanikiwa?” mwanamke alimuuliza.

    “Mnataka nimfanyie nini kwa sasa.” Aliuliza Asia, kwa mujibu wa saa zao ilikuwa saa tatu usiku.

    “Mwambie aje sasa hivi.” Mmoja wao alijibu.

    Asia bila kusema neno alichukua simu yake, akabofya jina la Lucas. Akaweka sauti ya juu simu ikaanza kuita wote wakisikia.

    Ikapokelewa.

    “Samahani mpenzi wangu kwa kuchelewa kupokea simu.” Alianza kujitetea Lucas.

    “Nataka kukuona Luka.” Aliamrisha Asia kwa nyodo.

    “Lakini….”

    “Luka unakuja hauji?”

    “Upo wapi sasa hivi..nakuja.”

    “Sinza kwa Remmy.” Alijibu Asia kisha akakata simu.

    Wale wanawake walitazamana, kisha wakajikuta wakiwa midomo wazi bila kujua kama wapo katika hali ile.

    Kazi imefanyika namna ile kwa nini wasifanye malipo?

    “Sasa tunataka kumuumiza yule mkewe.”

    “Msijali nawapa mwezi mmoja wanaachana naye.”

    Malipo yakafanyika.

    Baada ya mwezi mmoja wakakutana kupongezana juu ya kutalikiana kwa Lukas na mkewe wa ndoa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ASIA APATA MIMBA.

    KOSA kubwa alilokuwa anafanya Asia lilikuwa kufanya mapenzi bila kinga. Binti huyu hakujali lolote. Ni sawa sawa alikuwa ameyaweka maisha yake rehani kwa sababu moja tu, mama yake aishi maisha mazuri hata kama yeye atakufa mapema lakini atakuwa ametimiza kile ambacho aliahidi.

    Asubuhi moja Asia alihisia mabadiliko katika mwili wake, alikuwa mchovu na alihisi kichefu chefu.

    Hakusita kuwashirikisha marafiki zake.

    Janeth akiwa mkongwe na mjuzi wa mambo haya hakungoja vipimo vya hospitali.

    “Asia umeikamata mimba hiyo.” Alimweleza huku akitabasamu.

    Asia alipagawa kusikia habari za mimba, akasimama wima akiwa amekodoa macho yake.

    Hakuitaka mimba, na wala hakuhitaji kuacha mtoto duniani ambaye atarithi tabia zake chafu zisizosimulika.

    Asia akaamua kwenda kupata uhakika hospitalini.

    Hakika alikuwa ana mimba.

    Hapa sasa alizidi kupagawa.

    Lakini ghafla akili ya kidigitali ikamwingia tena, akakumbuka kulialia baada ya kupata mimba ni akili za kianalojia.

    Akafanya tabasamu kisha akajitazama tumbo lake.

    “Naiuza mimba yangu….” Akajisemea.

    “Tena itakuwa biashara bora kupita zote nilizowahi kufanya.” Akaongezea kisha akacheka kwa madaha, matiti yake yakarukaruka kwa furaha





    ASIA AUNDA FUMANIZI.

    . . Kitendo cha kumkamata akili Lucas na kumpelekesha anavyotaka kilimfanya ajijengee heshima kwa waliomfahamu. Asia akaonekana ni kiboko ya viboko.

    Wanawake na mikasa yao ya kimapenzi hawakuisha kumfikiria iwapo anaweza kuwasaidia.

    . . Fundi mitambo wa kikundi chao ambaye alikuwa na cheo cha waziri wa mipango, Husna Messi alikuwa anazurura huku na kule kujaribu kusaka dili lolote linaloweza kuwapatia pesa.

    Husna alikuwa mzungumzaji sana na pia alikuwa msikilizaji mzuri sana.

    . . Neno linalomtoka mtu kwake lilikuwa biashara.

    Alichokuwa anafanya Husna ni kutembelea saluni za kike kadha wa kadha, ni huku alipoweza kupata siri kadhaa.

    . . Wanawake wasiokuwa na staha waliyataja mapungufu ya wapenzi wao huku wengine wakitumia nafasi hizo hata kusema siri zao za ndani.

    Husna akapata jipya huku.

    . . Alipomaliza kusukwa nywele zake akateta kidogo na yule mwanamke.

    . . Alimweleza kuwa dawa ya kilio chake ipo na huyo mtoaji dawa hakuna kinachoshindikana kwake.

    . . “Wewe shida yako ni kumkomoa tu…”

    . . “Ndio hiyo tu kumkomoa maana yaani sijui hata nisemeje. Yaani mimi ni wa kuchezewa na kuachwa kijinga jinga vile. Amenikuta nina mpenzi wangu, nimemuacha nikijua kuwa jamaa atanioa kumbe laghai. Tapeli mkubwa…Malaya mzoefu.” Mwanamama alijieleza kwa uchungu, uchungu mkubwa.

    . . Husna akainusa harufu ya pombe. Bila shaka mama yule alikuwa anajihusisha katika ulevi ilimradi tu kuondoa ama kupunguza msongo wa mawazo ambao ulikuwa unamkabili.

    . . Husna akafurahia kimoyomoyo alipogundua kuwa yule mama alikuwa anamiliki usafiri wake mwenyewe. Bila shaka alikuwa na pesa ya kutosha.

    . . Biashara njema kabisa.

    . . Mwisho wa maongezi wakabadilishana namba za simu.

    . . “Yaani mimi muda wowote nipigie usijali…nahitaji sana kumwonyesha mimi ni nani huyo mjinga….” Alisema kwa hasira yule mama ambaye kwa makadirio alikuwa na miaka isiyopungua arobaini.

    . . Husna alifika nyumbani kwa Asia baada ya kuwa amempigia simu na kupewa maelekezo kuwa mwanadada alikuwa yu nyumbani.

    . . Asia alikuwa amejikita katika kutazama filamu za kiingereza hasahasa za mapenzi. Huku alijifunza mengi sana yaliyomuwezesha kufanya utapeli wake ipasavyo.

    . . Asia alisimamisha ile filamu baada ya Husna kuingia.

    . . “Shoga hadi sa’hivi umejikalisha tu nyumbani.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    . . “Niende wapi sasa wakati hujanipa dili mtaalamu wangu…si unajua tena madili hayajileti mpaka yasetiwe.” Alijibu kichovuchovu Asia huku akijinyoosha.

    . . Mapaja yake yalikuwa nje na wala hakujishughulisha katika kuyasitiri.

    . . “Nd’o nimekuja mwenzangu….mguu wangu kama ilivyo kawaida ni mguu wa pesa…sema siwezi kuzichukua bila akili yako mpenzi.” . . . . Husna akazungumza haya huku akijiweka sawa katika kochi.

    Asia akafanya mfano wa tabasamu hafifu. Tabasamu la ujivuni.

    Alifurahia namna ambavyo alikuwa anakubalika kwa wenzake.

    . . Husna Messi hakutaka kupoteza muda, akaanza kupepeta mdomo wake juu ya mwanamama anayetaka kumkomesha mwanaume ambaye alimtenda.

    . . Asia akasikiliza kwa makini kabisa. Ni kama alikuwa ana shahada ya jambo alilokuwa anashrikishwa. Akalitafakari kwa kina kisha akanyanyua kinywa chake.

    . . “Ana bei gani? Maana mambo ya kugandana kama alivyoniganda huyo Lucas sitaki sahivi.” Alilalama Asia.

    . . Husna akamtazama kisha bila kusema neno akachukua simu yake akabofya kisha akaipeleka sikioni.

    . . “Mambo shosti za mida….nipigie.” alizungumza upesi upesi akakata simu. Husna alikuwa na tabia ya ubahili.

    Baada ya dakika moja, simu ikaita.

    . . “Huyu hapa…” akajisemea Husna. Kisha akapokea simu.

    Sasa hakuwa akizungumza harakaharaka tena.

    . . “Nipo naye hapa yule mtaalamu….ongea naye basi nimemweleza nia yako.” Alibwabwaja Husna kisha akampatia simu Asia.

    Baada ya salamu na kufahamiana majina, ikazungumzwa bei.

    . . “Jamani dada nifanyie kitu kimoja basi chukua milioni moja na nusu halafu hiyo laki tano nitakumalizia baada ya kumkomoa…..” alibembeleza yule mama akiwa amewekwa katika ‘loud speaker’.

    . . Asia akafanya tabasamu kisha akamkubalia mteja wake.

    Wakapanga siku na mahali pa kukutana ili waweze kupeana maelekezo kadha wa kadha.

    . . Husna akamwachia rasmi jemedari Asia kazi.

    Yeye akabaki kusubiri majibu.

    Husna alikiri kuwa Asia alikuwa mwanadada wa maajabu sana.

    . . . . . . . . . . ****

    . . . . GARI aina ya Toyota Rav4 liliegeshwa katika ukumbi maarufu wa burudani, ukumbi mkongwe kabisa unaoenda kwa jina la Lango la jiji.

    Ukumbi uliopo maeneo ya Magomeni mikumi.

    . . Baada ya kuegeshwa gari ile ilidumu

    ama kuwapoozesha.

    Baada ya nusu saa gari nyingine iliingia. Nayo ikaegeshwa kwa fujo.

    Baada ya gari hii kufika kelele za hapa na kwa muda mrefu bila mmiliki kutelemka chini. Hakuna aliyejali, kila mmoja alikuwa na mambo yake.

    . . Waliokuwa na kampani walijikita katika kampani hizo na waliokuwa peke yao peke yao walibaki na upweke wao huo ambao aidha uliwapendeza pale zilizuka, huenda mwenye gari hilo alikuwa anafahamika.

    Kitendo cha gari hili kuwasili kilienda sambamba na milango ya Toyota Rav4 kufunguliwa.

    . . Marashi ya aina yake yalitawala baada ya mlango ule kufunguliwa, kisha ndani ya lile gari akatelemka mwanadada, alikuwa amevaa nguo nyekundu na alipendeza kumtazama masikioni kwa jinsi hereni zake zilivyorandana na gauni lake.

    Gauni lake lilikuwa katika mfumo wa kichokozi, lilikuwa fupi na liliacha mapaja yake kwa kiasi kikubwa yakitalii kwa nje.

    Kwa jinsi alivyopendeza aliamini kuwa kila jicho lilikuwa likimtazama japo kwa wizi wizi na alijua ni kiasi gani alikuwa akiwaumiza wasichana wengine roho, huku wale ambao waume zao walikuwa dhaifu wakianza kuingia wasiwasi.

    . . Mwanadada huyu hakuwa na shida ya kianalojia ya kumfikia kila mtu ilimradi anayo luninga na kiantena, shida yake ilikuwa kidigitali na alitaka kama ingewezekana jicho la mwanaume mmoja tu nd’o limuone.

    . . Na alijua kuwa lazima atatizamwa.

    . . Mwanadada akaifunga vyema milango ya gari lake.

    . . Kisha akageuka. Hatua kwa hatua hadi akaufikia mlango wa kuingilia.

    . . Walinzi wakampisha, siku hiyo ilikuwa ni ladies free.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    . . Akaingia kwa pozi na viatu vyake vya mchuchumio lakini ambavyo havikumsumbua katika kutembea.

    . . Akatazama huku na kule akajichukulia nafasi.

    . . Akaanza kunywa vinywaji vya bei ghali sana, vinywaji ambavyo viliwababaisha wanaume wengi na kuhofia kuweza walau kumkaribia.

    . . Jicho lake lililofichwa nyuma ya miwani lilikuwa makini sana kumhesabia muhusika wake muda wa kumshambulia.

    . . Bahati nzuri muhusika mwenyewe tamaa alizionyesha mapema sana.

    . . Kama alivyotegemea yule mwanadada. Mara akiwa ameketi akijikita katika kutumia simu aina ya iPhone5 ambayo waliichota katika tukio la kumhamishia Deniss digitali, mara akakaribiwa na mwanaume ambaye kwa sifa moja unaweza kumweka katika kundi la watanashati.

    . . Bila kusema lolote akamwekea mbele yake chupa ya kinywaji alichokuwa anatumia.

    . . “For what?” mwanadada akauliza.

    Yule mwanaume akajiumauma kujieleza lakini mwanadada hakukubali ofa ile.

    Jaribio la muhusika wake likawa limeshindikana.

    . . Majira ya saa sita usiku, taarabu ikanoga.

    . . Taarabu nd’o asili ya lango la jiji, kila ambaye hutembelea pale hufuata taarabu.

    Asia akasimama, mkoba wake kwapani, akajiunga katika kucheza taarabu ile iliyokuwa imenoga.

    . . Alicheza kwa uwezo huku akiruhusu mara kwa mara kiuno chake kucheza faulo na kuonesha mali kadha wa kadha katika kiuno chake.

    Jwa kila ambaye angemtazama angekiri kuwa mwanadada yule alifuata taarabu pekee katika ukumbi huo.

    . . Yule mwanaume ambaye alikuwa amemtamani Asia tangu alipomuona wakiwa nje alitumia nafasi hii kujipenyeza na kujikuta akituliza mikono yake katika kiuno cha yule dada.

    Mwanadada akakatika vyema sana, kijana naye akazidi kukamatilia.

    Asia alitambua nini kinaendelea lakini akajifanya hajui lolote.

    . . Wakati wakicheza muziki huo wa mwambao yule bwana akajitambulisha.

    . . “Naitwa Branco……”

    . . “Mimi Fatuma…” alidanganya Asia kama kawaida yake.

    Branco lilikuwa jina lake halisi. Kijana ambaye alimtesa mwanamke ambaye sasa alikuwa amemlipa Asia kwa shughuli moja tu…kumkomesha Branco ikiwezekana kumfanya aukimbie mji.

    . . Asia alikuwa amejipanga vyema, sasa alikuwa katika utendaji.

    Hatua ya kwanza ilikuwa kumtambua vyema Branco, mwanzoni alipewa picha yake na kisha kuelezwa kuwa kijana huyo huwa hakosekani katika taarabu, ni tabia yake kuhudhuria sehemu hizo ili akwapue watoto wa kike wanaojua nini maana ya kitanda.

    . . Branco aliamini kuwa wacheza mduara mara nyingi ni watundu kitandani.

    Sasa Asia yupo na Branco walikuwa wakianza kufahamiana.

    Baada ya muda Asia akarejea katika kiti chake na Branco akiendelea na mambo yake.

    Asia wa kidigitali alikuwa anaungojea ule muda ambao alikuwa ameuseti kidigitali. Muda ambao ungeamua hatma ya Branco na tabia zake za kubadili wanawake hovyo.

    . . Msema chochote (MC) alisimama mbele ya jukwaa baada ya mziki kusitishwa kwa muda.

    Kila mmoja alikuwa na hamu ya kusikia washindi wa siku hiyo ni nani na nani.

    Mashindano ya binti na bwana waliotoka vyema kimavazi..kisha washindi wa kuucheza mduara.

    Asia alikuwa anatabasamu peke yake alipokuwa anawatazama wadau wengine wakifanya ubashiri wa nani kuibuka kimwana wa usiku huo.

    . . Asia alikuwa na haja ya kutabasamu, kwani kabla ya mkesha huo wa taarabu, tayari alikuwa amepitia mlango wa nyuma na alikuwa ametoa rushwa kwa MC…hivyo kwa namna yoyote ile ni jina lake lingependekezwa kuwa kimwana wa taarabu aliyependeza usiku huo.

    Asia hakuwa mpumbavu ajiweke yeye peke yake, alilipia pia jina la mwanaume ambaye anataka atajwe usiku huo.

    . . Pesa ikazungumza.

    . . Wakati ulipowadia MC akawaamsha vitini.

    . . “Huyu mwanadada ni mgeni…sijamjua jina lakini nimetuma vyombo vyangu vya usalama vimemtambua jina……FATUMAAAAAA…..” akapayuka MC, Asia akazuga kushtuka, akasimama kama asiyeamini kabisa alichokisikia.

    . . Hakika alikuwa muigizaji mzuri.

    Akajikongoja kuelekea mbele. Mate yakawajaa midomoni wanaume wenye tamaa……lakini binti huyu alionekana kuwa matawi mengine kabisa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati shangwe zikizagaa wakati Asia akipiga hatua kwa madaha kuelekea jukwaani, msema chochote akamtaja mwanaume matata wa siku hiyo.

    Hapa napo Asia alipangoja kwa hamu maana alikuwa amepapika na ilikuwa lazima papikike.

    . . “Papaaaaa Brancooooooo” akatajwa Branco. Kijana huyu machachari akaruka juu, hakutegemea kabisa iwapo ataitwa.

    Mbio mbio akakimbia mbele na kumkumbatia Asia.

    . . Hili nalo Asia alilitegemea.

    . . Baada ya kukutana katika jukwaa lile wakiwa wawili huu ukawa mwanzo wa kufahamiana vizuri.

    Papaa Branco akatumia ukaribu ule kumchombeza Asia.

    . . Mwisho wa siku majira ya saa tisa usiku, Asia akiwa na gari yake na Branco katika gari yake walikuwa wanaelekea nyumbani kwa Branco.

    Majira ya saa kumi walikuwa katika chumba cha Branco. Asia akakiri kuwa yule mama aliyempa biashara hiyo alikuwa amesema ukweli tupu.

    . . “Branco ana tabia ya kuingiza hovyo wanawake chumbani kwake.”

    Hakika ilikuwa hivi, Asia naye alikuwa ameingia katika chumba cha Branco.

    Papara za hapa na pale kitandani, tayari walikuwa wapenzi kufikia dakika hiyo.

    Branco alimgalagaza Asia huku na kule, Asia alitamani kucheka lakini akasita. Branco alikuwa ni mlafi sana, na pia mwenye haraka kupitiliza.

    Mara alambe huku mara ashike kule.

    Hisia za Asia zilikuwa zimesafiri mbali kabisa na hakujiruhusu kudanganyika.

    Baadaye ikafuata zamu ya Asia kumfanya Branco mtumwa.

    Lakini Asia hakuwa mlafi na mwenye papara.

    . . “Kaoge bwana….” Alimsihi Branco.

    Branco akamtaka waende wote Asia akakataa akidai kuwa anahitaji faragha ya kike, kujisafisha. Baranco akamwachia Asia chumba.

    Hili lilikuwa kosa la jinai alilofanya Branco.

    Asia alipoachiwa chumba, akiwa amebakiwa na chupi pekee mwilini aliparamia mkoba wake akatoka na kimfuko kidogo.

    . . Bila kutetemeka akafunua kitanda cha Branco na kuweka kisha akarejesha godoro katika hali ya kawaida.

    . . Branco alivyorejea Asia naye akaingia kuoga.

    . . Akiwa bafuni akamuita Branco ambaye alikuwa amelegea macho kutokana na hamu kubwa ya kufanya ngono.

    Mbio mbio Branco akamfuata bafuni akiwa bado yu uchi.

    . . “Nisugue mgongo baby…” Asia alilalamika.

    Branco akachukua cha kusugulia.

    . . “Noo honey kitaniumiza hicho…mi nataka unisugue kwa mikono.” Asia alifanya kudeka. Branco akaanza kumpapasa.

    . . Asia wa digitali akaanza kuhema juu juu. Branco akazidi kupapasa, sasa vidole vyake vikahama kutoka mgongoni vikaingia kunako katikati ya mapaja ya Asia. Hapa Asia akapiga yowe kuu la hamu.

    . . Kisha akajiweka katika pozi ambalo Branco akiwa kama mzoefu wa mambo hayo alijua ni kipi anamaanisha.

    . . Wakaanza kuvurugana kuanzia bafuni, mchezo wao ukaja kuishia sakafuni.

    Wakasinzia waliposhtuka tena walimalizia sebuleni.

    . . Asia akajifanya kuwa amechoka sana. Lakini haikuwa hivyo.

    Aliondoka akiwa na tabasamu usoni, Branco alidhani kuwa Asia anatabasamu kwa kuwa ameahidiwa ahadi hewa ya kuolewa.

    . . Branco akajiona kuwa mjanja kuliko Asia.

    Katika orodha yake akamuhesabia kuwa msichana wa arobaini na tano tangu ajitambue kuwa yeye ni mwanaume.

    ASIA KAFANYA NINI TENAAA……..



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog