Search This Blog

Monday, October 24, 2022

NILAMBE HUMO HUMO - 4

 





    Chombezo : Nilambe Humo Humo

    Sehemu Ya Nne (4)



    Nikijua mtego ndio unakaribia kufyatuka, sikumgusa!

    Badala yake nilikwapua mwanamke mwingine nikatokomea nae migombani na kwenda kuneng’eneka nae, Nikamuacha Havijawa pale pale uwanjani. Mwanamke niliyemchukua hakuwa haba, alikuwa bora kwa kila hali.

    Nikamuuliza kama ameolewa akasema bado, nikamuomba niwe mgeni wake kwa siku hiyo akakubali. Sikurudi uwanjani nikaenda kulala kwa mwanamke huyu mpya.

    Asubuhi na mapema nilikuwa ndani ya gari nikielekea Daresalaam.

    Ukawa mwisho wa kuwasiliana na Havijawa. Ikawa mwanzo wa mawasiliano na yule mpiga ngoma, nikaendelea kuhudhuria katika ngoma hata iwe wapi. Ni hapa nilipojua ni kwanini ngoma inapendwa sana uzaramuni.

    Nami nikawa mfuasi mtiifu na mkamilifu wa ngoma!.

    * * *

    Naam, niliyainua tena macho yangu na kuutazama ubao wa matangazo No! Ubao wa matokeo. Nao haukunidanganya. Uliniambia tena kama unaonidhihaki. Kwamba nilipata alama F katika mitihani yangu ya mwisho pale chuoni.

    Kwa sekunde kadhaa niliduwaa nikiwa siuoni ubao huo wa matokeo sawasawa. Akilini niliona kama kitu cha kawaida huku nikitabasamu kiwazanga kama niliyefurahishwa na matokeo yale. Wenzangu wachache niliofeli pamoja nao walikuwa wakilia. Wengine wakisikitika.

    Wachache waliokuwa na roho ya paka wakaniangalia kwa mshangao.

    ‘’He Ibra anacheka!” Mmoja aliropoka ’’Wakati amefeli vibaya!” mwingine akadakia ‘’Lazima kuna analotarajia sio bure!” Mwingine akahitimisha.

    Shamsa alikuwa miongoni mwa wanafunzi wachache waliofanya vizuri sana kiasi cha kupata A+. Wakati huu alikuwa hajiwezi kwa furaha machozi yakimtoka hovyo asiyaamini macho yake.

    Wengine wakashangaa, aliyefeli anacheka, aliefaulu analia! Akimu alikuwa mbali sana, alikuwa na alama za wastani hazikuwa mbaya wala nzuri sana alipata grade C, yeye pia alikuwa akisononeka. Alitaka apate grade A!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wabongo kwa kutoridhika? Mie niliyepata mswaki je?

    Kadiri muda ulivyokuwa ukipita ndivyo nami nilivyokuwa nikipambazukiwa na ukweli, ukweli kwamba nimefeli vibaya! Ukweli kwamba miaka yangu mitatu pale chuoni ilikuwa bure, bure kabisa! Bure kwa maana ya kwenda na maji.

    Nikawafikiria wazazi wangu waliopoteza mamilioni kwa malaki ya shilingi kunisomesha mwana wao. Kunisomesha nisihangaike na maisha kwa namna itakayoikwaza mioyo yao na kuwasononesha.

    Kunisomesha ili nije niwatunze wao mara nguvu zitakapowaishia. Kunisomesha ili nije nitimize wajibu wangu kama binadamu wa kuisaidia jamii kupata unafuu katika sekta fulani. Kunisomesha… kunisomesha…! Niliendelea kutafakari pasipo kupata majibu.

    Sikuwa nimewahi kufeli kwa mtindo huu toka nilipoanza elimu ya Awali, chekechea kwa maana halisi. Nikafuatia ile ya msingi hadi sekondari! Lakini leo… My God nitawaambia nini wazazi wangu?

    Chozi la uchungu likateleza na kuanguka shavuni.

    Roho na moyo vikaniuma kwa pamoja na kuufanya mwili wangu kuwa handaki la mateso kwa muda.

    Nikiwa katika hali hii mwili ulitikisika na kutetemeka kwa nguvu wakati mawimbi ya kilio yakitoka kifuani mwangu na kunifanya nitoe mlio mithili ya gari ndogo yenye mzigo mkubwa inayopanda mlima na kushindwa kuumaliza.

    Nililia na kulia na kulia! ’’Hatimae mapenzi yameniliza!” Niliwaza kwa uchungu nikiendelea kulia kwa nguvu.

    ‘’Ibra… Ibra… Ibra!’’

    Sauti nzuri nzuri ikapasua anga, ikakizidi kilio changu na kuzifikia mboni za masikio yangu, mwito huu ulienda sambamba na mtikiso wa bega langu la kushoto. Sio siri ulikuwa mguso wa faraja. Nikainua uso na kumwangalia huyu aliyeingia chumbani kwangu bila hodi na kujipa mamlaka ya kuniita.

    Ana kwa ana na Shamsa Nuhu, msichana wa maisha yangu!

    ”Pole!’’ Akaniambia kwa upole hali akinihurumia.

    Huruma hii ikanifanya niangue kilio upya. Kilio cha nguvu, kilio cha simanzi. Nililia haswa, nililia mno. Ukweli nililia kweli kweli. Shamsa alijaribu kunibembeleza kwa muda mfupi akashindwa na kuniacha nilie. Nadhani aliniacha nafasi nimalize machungu niliyo nayo moyoni.

    Na niliyamaliza.

    Ilikuwa baadae sana niliponyamaza na kupitiwa na usingizi moja kwa moja. Shamsa aliniamsha jioni kabisa nikaamka! Alikuwa ndani ya vazi la usiku! Mwili wake mzuri ulionekana vizuri zaidi ndani ya vazi lile la kulalia.

    ‘’Amka ukaoge!’’ Akaniambia, nikamtazama kwa matamanio.

    ‘’Nataka nikutoe out!‘’ Akaongezea akitabasamu alipoona namwangalia tu pasipo kuinuka. Nikainuka, nikajinyoosha nikatwaa taulo, mswaki pamwe na sabuni na kuelekea bafuni.

    Nilipotoka yeye, akaingia.

    Akanichagulia nguo za kuvaa alipotoka bafuni, nae akavaa za kwake ambazo zilikuwa katika mkoba aliokuja nao. Tulipokuwa tayari akainua simu akabofya nambari kadhaa na kuipeleka sikioni. Akatamka neno moja tu

    “Unaweza kuja!’’ Halafu akakata simu.

    “Huyo ni Tax Drive ambae huwa anapaki gari lake hapo nje. Anaitwa Sudi’’ akaniambia. Nilimjua vizuri sana dereva huyo na nilikuwa nikimtumia sana mara kwa mara katika harakati zangu.

    ‘’Hutaki nikutoe out?’’ akaniuliza tena

    ‘’Hata kama sitaki unafikiri mbele yako nitakuwa na ubavu wa kukataa?’’ Nikamwambia kiutani, akatahayari na kunikabili tena.

    ‘’Ina maana hutaki?’’

    ‘’Hapana nataka sana, fursa hii nimeililia kitambo, nasikitika imekuja wakati mbaya! Wakati nimefeli!’’

    ‘’Usijali, kupanda na kushuka ni mojawapo ya safari za kimaisha, na ili mwanadamu ukamilike kabla hujaumbika haswa ni lazima uzipitie!‘’ Akatua. Nikamuuliza.

    “Kuumbika haswa?! Unamaana gani?”

    ‘’Umesahau ule msemo?”

    ‘’Msemo gani?’’

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Hujafa hujaumbika!’’

    ‘’Naufahamu, kwa hiyo una maana kuumbika hasa ni kufa siyo?’’

    ‘’Yes!’’

    Akajibu kwa bashasha. Nikatabasamu naye akatabasamu. Tukatengeneza njozi mbili adimu sana. Nilipotaka kusema kitu, akaangalia simu na kuniambia “Sudi yuko nje!”

    ‘’Mie nipo tayari!”

    Akaukwapua mkoba wake toka pale sofani na kuutia begani, nikauchukua ufunguo wa chumba nikafunga mlango na kutoka.

    ‘’Kwa nini uliniuliza vile?’’ Nikamuuliza tukitoka nje.

    ‘’Vipi?!”

    ‘’Kwamba sitaki nikutoe out?’’

    ‘’Ulionekana kuwa na fikara sana Ibra. Sijui ulikuwa ukifikiria nini’’

    Tukaifikia gari, tukaingia nyuma na kumsalimia Sudi, akawasha gari na kumuuliza Shamsa ‘’Haya niambie wapi Shamsa?’’

    ‘’Sudi bwana, unakuwa kama sio Born Town?! Nimekwambia sehemu yoyote tulivu!’’

    “Sehemu tulivu ziko nyingi Shamsa! Kuna hoteli za kitalii, majumba ya kifahari na makumbusho, fukwe na n.k.!”

    Ukazuka mjadala mfupi wa wapi atupeleke kutokea pale chang’ombe. Mjadala ambao ulimalizika kwa kuamuliwa atupeleke Coco beach. Hii ni kwa vile watu wangekuwa wachache sana kwa kuwa sio mwisho wa wiki. Hivyo iliaminika kule tungeweza kupata utulivu wa haja.

    Tukaondoka.

    Njiani nilimwambia Shamsa kuwa chanzo cha fikara zangu kule bwenini ni kumfikiria yeye, kwamba aliwezaje kuingia katika bweni la wanaume, akapata hadi ujasiri wa kubadili na kuvaa night dress achilia mbali kuniandalia maji kana kwamba nilikuwa mpenzi kama sio mume wake!

    Shamsa akatabasamu kabla hajaniambia kuwa aliamua kuhamishia kambi katika chumba changu kwa muda kabla ya kunitoa out ili awe pamoja na mimi katika kipindi hiki kigumu.

    Ilitosha! Alikuwa kama amenitonesha donda upya. Sura yangu ikasawijika na kupoteza nuru, alipoligundua hili akabadili mada haraka na niliporejea katika mood yangu, hatukuzungumza tena hadi tulipofika Coco Beach.

    * * *

    ‘’Katika mambo yote, hili sikulitarajia!’’ Shamsa alianza taratibu mara tu tulipochagua mahala patulivu pa’ kuketi pale Coco Beach na kufungua vinywaji vyetu vya kopo, ‘’Naapa hili sikulitarajia kabisa!”

    Sauti yake ilikuwa ndogo yenye mchanganyiko wa mizizimo ya upendo wa dhati, huruma pamoja na uchungu. Machozi pia yalikuwa yakitafuta njia katika kingo za macho yake. Kwa kila hali alikuwa katika majonzi!

    ‘’Ibra niliyekuamini, Ibra niliyekuthamini, Ibra niliyekutegemea ukweli wa kukutegemea! Bado siamini dear! Kwanini ukafanya hivi? Enhe kwa nini Ibra?’’

    Machozi yakamtoka.

    Moyo wangu ukazizima kwa simanzi ingawa nilihisi nitakuwa namuumiza, nikajikakamua na kumuuliza

    ‘’Kufanya nini Shamsa?”

    Akageuka na kuniangalia kwa mshangao, akafuta machozi na kuniuliza,

    ‘’Bado hujui tu? Hujui ulichofanya?! My God are you serious Ibra?”

    ‘’Sijui!” Nikajibu na kuapia

    “Mungu mmoja sijui!! Ningejua nisingeuliza!” Nikatua.

    Akaendelea kunitazama nikaona kama hanielewi, nikamsogelea na kumshika mkono kwa upendo uliotukuka, “Shamsa?” Nikaita taratibu nikingali nimeushikiria mkono wake

    “Mimi ni miongoni mwa watu wachache sana wasiopenda kuwakwaza wenzao hasa wewe! Kuendelea kunilaumu kana kwamba nimeua bila kunieleza nilililolifanya, hunitendei haki Shamsa! Unaniweka katika kimuhemuhe ambacho kinanifanya nishindwe kujua nastahili kuwemo katika fungu gani kati ya wastaarabu na washenzi. Tafadhali niambie, niambie tu usihofu!’’

    Shamsa akashusha pumzi na kuzivuta tena akauliza

    “Kwa hiyo hujafanya kitu?’’

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Kitu gani? kwa kadiri ninavyokumbuka na kufahamu, sijafanya lolote la kumchukiza mtu yeyote! Na kama nilivyokwambia sipendi kumkwaza mtu!’’

    ‘’Kweli!?’’

    ‘’Kabisa!’’

    ‘’Sasa kule Chuoni ulikuwa unalia nini?”

    Akili ikazibuka.

    Macho yakazibuka pia na fahamu kufunguka. Masikio, moyo na hata vinyweleo vya mwili ambavyo wakati huu vilikuwa vikikiruhusu kijasho chembamba kupenya na kuteleza juu ya paji la uso wangu, juu ya mashavu, juu ya mikono, juu ya kila mahali, sasa nikaelewa! Kwamba Shamsa alikuwa akizungumzia kufeli kwangu.



    ‘’Machozi yakafurika upya katika macho yangu. Shamsa alikuwa amenitonesha donda. Amegusa mahali ambapo sikutaka paguswe. Halafu kilio kidogo kikanianguka. Nilijitahidi kukizuia mpaka nikafaulu.

    ‘’Mapenzi Shamsa!” Nikasema huku nikipenga kamasi na kufuta machozi

    ‘’Mapenzi?!” Shamsa hakuamini!.

    “Yeah, Mapenzi! Naweza kusema ni mapenzi kwa kila hali ndiyo yaliyonifanya nifeli. Ukweli huu huniumiza zaidi. Huniumiza kwa vile ni ukweli unaoashiria upumbavu ulikithiri nilionao. Ni upumbavu tu maana ujinga unatibika, upumbavu hautibiki!”

    ‘’Bado sijakuelewa!’’ Alikuwa Shamsa kwa upole kabisa.

    ‘’Ni mapenzi Shamsa, nilikupenda sana mfano wa maua, ninakupenda hata sasa na nitaendelea kukupenda daima!’’

    ‘’Kunipenda huko ndio kukakufanya ufeli?’’

    Nikatikisa kichwa juu na chini kukubali.

    ‘’Si kweli!’’ Akasema kwa sauti thabiti nae akitikisa kichwa kushoto na kulia kukataa ‘’Si kweli hata kidogo!‘’ Akaongezea na kuendelea ‘’Nahisi unajaribu kunificha kama sio kunichezea shere. Naomba uniambie ukweli Ibra, ili niangalie namna ya kukusaidia tafadhali!’’

    Sikujua nimwambie ukweli upi

    ‘’Mbona hata mie ninakupenda sana na nimefaulu vizuri tu? Mbona nilikuwa nikikufikiria na kutamani kuwa nawe mahala kama hapa nikila raha na kustarehe na wewe? Mimi nina nini niweze na wewe una nini ushindwe? Hapana niambie ukweli Ibra’’

    Akatua. Furaha na bashasha vikiuvaa moyo akili na mwili wangu kwa zamu. Shamsa ananipenda! Ulikuwa ukweli ulionitoa machozi ya furaha, machozi ya upendo! Upendo wa dhati. Upendo uliotukuka!

    ‘’Shamsa’’ Nikaita nisiamini masikio yangu, “Ni kweli unanipenda?!’’

    “Ni kweli Ibra, nakupenda sana! Nakupenda mno! Nakupenda kuliko unavyofikiria. VETA nzima watu wa Compass wanajua jinsi nilivyokufa na kuoza juu yako, Najua hata wewe unanipenda tu ila hujiamini na pengine unanipenda kupita kiasi, kiasi umekuwa kama unaniogopa uongo?’’

    Akasuta! Ulikuwa ukweli, ukweli halisi. Ukweli Original kama alitegemea kunisuta kule kungenifanya nione haya kama sio aibu, alikosea! Badala yake nilitahayari na kuinamisha uso kwa fedheha, nilipoinua bado alikuwa akinitazama. Nikanong’ona.

    “I love you Shamsa!’’

    ‘’I love you too Ibra!’’

    Moyo wangu ukachanua kwa raha, akili ikapigwa dafrao na furaha huku mate ya uchu kama sio utamu yakijaa mdomoni. Nikamsogelea akanisogelea! Tukakutana katikati na kukumbatiana kwa nguvu na kudumu katika hali hiyo kwa muda.

    Hatimaye! Nikawaza kwa furaha nikingali nimekishikilia kifua chake Hatimaye Shamsa ameanguka mikononi mwangu, Ananipenda! Kwa mara ya kwanza nimepata hifadhi katika moyo wa mwanamke!’

    Ilikuwa ajabu na kweli.

    Tulipoachiana matendo halisi ya mapenzi yalifuatia. Tulilishana, tukacheza na kuogelea pamoja. Tulipotosheka tukarudi mchangani tena. Shamsa akaniita kwa upendo uliotukuka. Sauti yake ilikuwa tamu vibaya sana

    “Ibra mpenzi?”

    ‘’Naam!’’

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ‘’Bado hujanishibisha dear!’’

    ‘’Lakini biskuti, Chocolate na Ice cream hazishibishi!’’

    Akatabasamu, vishimo vikatokea hapa na pale katika mashavu yake na kidevuni.

    “Unanielewa vizuri sana Ibra! Ni kuhusu kufelishwa na mapenzi! Hebu niambie ukweli!’’

    ‘’Ni ukweli mpenzi!’’

    Nikamwambia, kabla sijaanza kumsimulia safari ya maisha yangu toka Shule ya Msingi, Sekondary, hadi pale VETA. Nikamwambia jinsi nilivyokuwa nampenda na namna nilivyoshindwa kumkabili licha ya yeye kunionyesha dalili za waziwazi.

    Nikamwambia pia namna nilivyopateua uwanja wa fisi kama mahala mbadala, ushauri niliopewa na Akimu baadae ambapo nilijikuta nikianguka tena katika ngoma za kizaramo. Nikashindwa kujisomea, kufuatilia masomo na kuendekeza ngono, mpaka ninamaliza kusimulia, Shamsa alikuwa bado ana hamu ya kunisikiliza.

    “Huo ndio mkasa wangu Shamsa! Unadhani kitu gani naweza kusema kimenifelisha kama sio mapenzi?”

    “Duh! Pole sana Ibra una bonge la mkasa! Mkasa ambao umeusisimua moyo wangu katika namna inayonifanya nikuogope! Nikuulize swali jingine?”

    ‘’Uliza tu laaziz!”

    ‘’Mbona siku ile nilipokuuliza kama unanipenda ulikataa kata kata?”

    Nikatabasamu, “Mbona hilo umeshalijibu katika maelezo yako? Shamsa mpenzi nilikuwa sijiamini, nilikuwa nakuogopa! Akili zako, uzuri na uwezo wako kifedha vilinifanya niufyate, nikawa nakufa kiofisa tai shingoni!”

    Akacheka. Nami nikacheka. Ikawa raha juu ya raha

    ‘’Siku nyingine usiogope ukubwa wa samaki! Uliza bei!’’ Akasema kati kati ya kicheko, tukacheka zaidi.

    ‘’Lakini kufeli kwako hakutokani na mapenzi! Naweza kusema hivyo!’’ akaniambia baadae kwa uhakika kabisa.

    ‘’Kumbe kunatokana na nini na au nikuiteje?”

    ‘’Kunatokana na tamaa kali ya ngono na niite tu umalaya, kwa sababu hata ngoma unazozizingizia huzifuati zenyewe! Hii ni kwa vile hujui kucheza kabisa, unayo ifuata ni ile mijimama na kile kipindi muhimu cha kuzima ngoma uongo?”

    Nikashindwa kumjibu.

    “Mapenzi ya kweli ni zaidi ya ngono Ibra! Unadhani ni kwanini mimi imeniuma wewe kufeli? Kwanini nilikuja kukufariji katika bweni lenu? kwanini nimekuleta huku?! Sababu ni moja tu Ibra wangu. MAPENZI! Ni mapenzi ya dhati niliyo nayo kwako, hilo tu!” Akahitimisha.

    Alikuwa sahihi.

    Tuliendelea kufurahi na kula maisha pale ufukweni hata msiba wote wa kufeli ukaondoka. Nilichogundua tu ni kuwa Shamsa alikuwa mwangalifu sana wakati huu. Hakujiachia sana kama alivyokuwa akijiachia wakati ule kabla sijampa full story yangu.

    Jioni tuliondoka na kuelekea mabwenini.

    Siku ya pili yake tulikuwa kwenye hoteli moja ya kitalii huko baada ya maongezi yetu ya kawaida ndipo alipo nitwanga swali..

    ‘’Sasa Ibra Chuo ndio tumemaliza, baada ya kutunukiwa shahada zetu yatupasa kuondoka. Mwenzangu una mipango gani? Mie mwenzio Mzee ameniunganishia Tanesco na mwakani nitaajiriwa!’’

    Swali zito. Nikachoka kabisa, dakika zikayoyoma pasipo kujibu

    “Sikiliza Ibra, kufeli masomo sio kufeli maisha. Kwa hiyo usifikirie sana kuhusu hilo, mimi nina ushauri mzuri kwako!’’ Akatua na kunitazama.

    ‘’Enhe upi?’’

    ‘’Kwanza nataka mimi na wewe tuoane unasemaje?”

    Sura yangu ikachanua mithili ya maua katika jua la asubuhi. Nikamwambia, “Sina kipingamizi Shamsa nakupenda mno!”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Naye akatabasamu kufuatia kauli yangu hii. Akasema.

    ‘’Basi kama hivyo ndivyo, huna budi kujifunza udereva haraka sana, ili nimwambie mzee akuajiri katika kampuni yake. Nitamshauri akulipe mshahara mzuri sana unaonaje?”

    ‘’Nitashukuru kupita kiasi!” Nikasema haraka nikiwaza hata kama Lady Jay dee ataniita mwanaume kama binti na Bushoke kuniita Mume bwege shauri yao! Nitafanyaje hali nimesha ulowanya?” Nikakubali.

    Lakini kabla haya hayajafanyika inakubidi uanze taratibu za uchumba na kwa hili hatuna budi kwenda kupima afya zetu kwanza ili ulete barua ya posa wakati huo huo ukianza Driving School! Sawa mpenzi?!”

    ***HE MAMBO YA KUPIMA TENAAA…….IBRA ANALOOOO!!!!



    ITAENDELEA 

0 comments:

Post a Comment

Blog