Search This Blog

Monday, October 24, 2022

KITANDA CHA MPANGAJI MWENZANGU - 1

 





    IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS





    *********************************************************************************



    Chombezo : Kitanda Cha Mpangaji Mwenzangu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    “Samahani anti, unaweza kuniazima fagio kama unalo?”

    “Sawa anko, ngoja nikuletee.”

    Baada ya dakika moja mlangoni…

    “Ngoo ngoo ngooo.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Ooo, asante anti, nakurudishia sasa hivi.”

    Baada ya dakika kumi…

    “Anti…anti…antieee…”

    “Mama hayupo, kaenda dukani.”“Haya, basi akija mwambie nimerudisha fagio.”



    Baada ya dakika tano, mama Tina anarudi ndani, mkononi ameshika kimfuko cha rambo, kwenye korido anapishana na Os Anjelus…

    “Anti nashukuru sana kwa fagio.”

    “Tayari ee?”



    “Tayari, nimempa binti yetu.”

    “Sawa anko. Vipi sasa, naona unatoka.”

    “Ee anti, nakwenda kwenye ile nyumba niliyokuwa naishi, niliacha vitu vyangu.”

    “Haya karibu sana, si tupo,” mama Tina alisema huku akiingia chumbani kwake.

    ***

    Ilikuwa mara yake ya kwanza Os Anjelus kulala kwenye nyumba hiyo ambayo ina wapangaji watatu tu. Yeye alikuwa na chumba kimoja ambacho pia alikitumia kama sebule kwani mlikuwa na masofa.

    Mpangaji mwingine ni Halima, yeye anamiliki saluni ya kusuka nywele wanawake, inaitwa Yero Masai. Mara nyingi anakuwa kwenye hiyo saluni na msichana mmoja wa kumsaidia.



    Halina hajaolewa, ila rekodi yake kwenye nyumba hiyo ni kubadili wanaume wa kulala naye. Leo akiingia na Abdi, kesho asubuhi anatoka naye, jioni anarudi na Saimon.



    Mpangaji wa tatu ni mama Tina. Yeye ana mume, ndiye baba Tina. Ni dereva wa magari ya manispaa. Muda mwingi anakuwa kazini. Mtu anayepatikana nyumbani hapo ni mama Tina tu, Tina naye anakuwaga shuleni, anasoma darasa la kwanza ila siku hiyo ilikuwa Jumamosi kwa hiyo hakwenda shule.



    ***

    Usiku wa siku hiyo, Os Anjelus hakupata usingizi aliouzoea kule alikohama. Ni kawaida, watu wengi hukosa mtiririko mzuri wa usingizi wanapolala eneo geni…

    “Iko haja ya kumwita mke wangu sasa. Si nilimpeleka nyumbani ili nitafute chumba kingine? Si nimeshakipata? Sasa nini tena?

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Lakini loh! Yule mama mwenye nyumba kule nilikohama kiboko. Mama mdomo mchana kutwa! Uchafu kidogo wa kuufagia sekunde kumi yeye anafoka nusu saa? Sijawahi kuona mimi.



    “Sasa kwa mfano siku ile alipotupa notisi kwa ule uchafu wa kuufagia dakika mbili tu kama nisingemtishia kwenda polisi, si angeongea siku nzima?” aliwaza Os Anjelus huku akihisi kizunguzungu cha ugeni, lakini msisitizo wake mkubwa ndani ya moyo ni kumwita mkewe, Happy.



    ***

    Asubuhi kulikucha, Os Anjelus alikuwa wa pili kutoka nje. Wa kwanza alikuwa mama Tina, baada ya yeye ndiyo akatoka Halima ambapo alimtengea maji ya kuoga mwanaume aliyerudi naye usiku uliopita.

    Ilikuwa mara ya kwanza kwa Halima kuonana uso kwa macho na Os Anjelus kiasi kwamba, mwanzoni Halima alijua ni mgeni wa mama Tina…

    “Za leo anko?”



    “Nzuri sista, mzima wewe?”

    “Mzima, karibu sana.”

    “Asante nimekaribia.”



    Lakini Halima hakumuuliza Os Anjelus kama yeye ni nani kwenye nyumba ile, aliogopa kuonekana ni ‘mshankupe’ wa mtaa.

    Kila mmoja aliendelea na lake, Os Anjelus aliingia chooni, Halima alitenga maji akaenda ndani kumwita jamaa yake, anaitwa Mabange.



    ***

    Halima alitoka na Mabange kwenda kwenye saluni yake, kwenye korido akakutana na mama Tina…

    “Za asubuhi mama Tina?”

    “Nzuri Halima, umeamkaje?”

    “Salama tu,” alisalimia Tina, akapunguza sauti…



    “Eti huyu kijana ni nani, mgeni wako?”

    “Mgeni wangu?! Aka! Si mpangaji mpya aliletwa na mwenye nyumba juzi.”

    “Ooo, kwa sababu sikuwepo. Anafanya kazi wapi?”



    “Mi sijui Halima.”

    “Ana mke?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Halima, mimi sijui lolote."

    "Ana gari?"

    "Halima bwana, mi sitaki," alisema mama Tina huku akiondoka kwa mwendo wake wa madaha.

    Halima aligeuka kumwangalia huku akimtamani maana japokuwa ni mwanamke mwenzake lakini moyoni amekuwa akikiri kwamba, mama Tina aliumbika kuliko yeye.



    Mama Tina alijaliwa. Kwenye bodi nyuma alikuwa amefungashia, kiuno kilikatika vizuri, japokuwa alishazaa mtoto mmoja lakini bado nido zake zilikuwa zinadai kama za binti aliyeingia ukubwa.

    Mviringo wa miguu yake na kuitwa jina la bia lilimfanya azidi kutamanika hata machoni pa wanawake wenzake. Sura yake ilijaliwa duara lenye upole na macho ya kulewa huku midomo ikishibishwa na unene wa rangi nyeusi.



    Sauti ya mama Tina ilikuwa na uwezo wa kuwafanya wananchi wenye hasira kali wamsamehe kumchoma moto kibaka aliyemkwapulia simu mzee maarufu wa mtaa.

    Siku mojamoja, hasa Jumapili alipokuwa akienda kanisani, aliwaacha hoi watu wa mtaani kutokana na magauni yalivyokuwa yakimkaa.



    Umri wake wa miaka 32 ulimtosha kuendelea kuonekana msichana mbichi kutokana na kujitunza na kujaliwa ngozi nzuri na Muumba.



    ***

    Asubuhi iliyofuata, Os Anjelus alitoka chumbani kwake na kukutana na mama Tina kwenye korido

    "Za asubuhi anko?"

    "Nzuri anti, umeamkaje?"

    "Salama tu. Naona kumekucha?"



    "Ee, kumekucha anti, nataka kufua kwanza halafu ndiyo niende kibaruani."

    "Pole sana. Ungetafuta mtu wa kukusaidia kazi kama hizo anko."

    "Ni kweli, unajua nina mke lakini yupo kwao, nadhani mwisho wa mwezi huu atakuja."

    "Hapo itakusaidia."



    Mazungumzo yao yalitumia kama dakika moja, kila mmoja akaendelea na mambo yake.

    Baba Tina aliondoka kwenda kazini, Os Anjelus alikuwa amemaliza kufua na sasa alikuwa akijiandaa kwa kutoka

    "Ngongo;ngo," mlango wake uligongwa.

    "Karibu," alisema kijana huyo huku akifungua mlango

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Oo anti, karibu."

    Mama Tina mkononi alishika sinia lenye chupa ya chai, sukari, kikombe na vitafunwa

    "Karibu chai anko."

    "Ooo. Anti mbona unasumbuka jamani?"

    "Usijali anko, we kunywa tu."

    "Asante sana."



    Os Anjelus alipokea sinia hilo na kurudi ndani kwake, akanywa chai na kurudisha vyombo

    "Anti vyombo hivi."

    Mama Tina alitokea, akapokea sinia lake huku akishukuru

    "Baadaye basi anti."



    "Sawa anko, nilikuwa na wazo moja anko. Ungeacha funguo nikufanyie usafi chapuchapu."

    "Hapana nitafanya mwenyewe anti, nisikusumbue."

    "Noo, hunisumbui anko, we acha tu."

    "Jamani, nitakuchosha anti."

    "Wala ndiyo kazi zetu akina mama tukiwa nyumbani."



    Os Ajelus aliacha funguo, mama Tina akaipokea na kuifunga kwenye pindo la khanga aliyovaa.

    Nusu saa mbele, mama Tina alikuwa ndani ya chumba cha Os Anjelus akifanya usafi. Baadhi ya vitu havikuwa vimepangwa, akapanga yeye alivyoweza huku moyoni akimsifia kijana huyo kwa kuwa na vitu vizuri na vya kisasa.



    Alibabaika zaidi kwenye kitanda na mashuka. Ilifika mahali alijitupa kitandani na kunesanesa huku moyoni akisema

    "Kinaonekana kinatoa usingizi mnono."





    ********************************

    ********************************************

    **********************************************************

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    "Nimekuletea chakula anko," mama Tina naye alitumia sauti ya chini.

    "Da! Asante sana anti."

    Wakati Os Anjelus anapokea, sauti ya Halima mlangoni ilibisha hodi

    "We kaka wa Kingoni."



    Ukimya ulitawala kwa muda kwani Os Anjelus alishindwa kuitikia kutokana na uoga kwamba angeingia angemkuta mama Tina

    "Wenyewe humu ndani, hodini," alikomaa Halima.



    "Sikia, nenda, fungua mlango lakini usimruhusu aingie ndani hata sekunde moja," mama Tina alimwambia Os Anjelus kwa sauti ya chini sana ili asisikie Halima kule mlangoni.

    "Sawa," Os Anjelus alikubali huku akienda kufungua mlango. Mama Tina akijibana kwenye kona ya chumba ili asionekane maana mlangoni hapakuwa na pazia.

    "Vipi we Mngoni, mzima?"



    "Mzima dada angu, karibu sana."

    Mama Tina kule ndani aliposikia karibu sana, alishtuka sana, alijua kijana huyo atamruhusu Halima apite kuingia

    "Mwenzetu ujio wako kufahamiana ni muhimu, ulikuwa ukiishi wapi zamani?"

    "Mburahati."

    "Una mke?"



    "Nina mke na mtoto mmoja."

    "Wako wapi sasa?"

    "Wako kijijini."

    "Watakuja lakini?"

    "Mwisho wa mwezi huu watakuwa hapa."



    "Sawa, sasa unakula nini maana napika."

    "Hapana anti, usijali kuhusu suala la chakula, mi tayari."

    "Kwani unapika humu ndani?"

    "Nakula gengeni."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hivi hiki chumba ni kikubwa kweli?" Hebu nione ndani," Halima alisema akionesha dalili za kutaka kuingia kwa kuinua mguu mmoja na kukanyaga mbele.

    "Sista samahani, iko siku utaingia lakini si leo," alisema Os Anjelus huku akiinamia chini kwa aibu.

    "Yaani mimi kuingia kwako anko mpaka unipangie siku, unajua ni kwa kiasi gani nimekupenda?" Halima alipasua jipu kwa mara ya kwanza

    "He!" kule ndani mama Tina alijikuta akisema kwa sauti ya mshangao

    "Yaani mwanamke anajitongozesha hivihivi, ama kweli Halima ni malaya sana jamani," alisema mama Tina lakini huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi.

    "Sista utanipendaje wakati nimekwambia nina mke wangu? Mimi hapa ndani hakuna mwanamke nitakayetembea naye kwa sababu kati ya mambo siyataki ni pamoja na usaliti."

    "Ina maana hujawahi kumsaliti mkeo?"



    "Na wala sina wazo hilo."

    "Basi mwenzetu kumbe ana bahati ya mtende, kuota jangwani."

    Mama Tina alimsifia kijana huyo, hasa kwa msimamo wake aliouonesha kwa Halima kwamba hawezi kumsaliti mke wake.



    Halima aliondoka, Os Anjelus akafunga mlango kwa funguo na kurudi, akakaa kitandani huku akimwangalia mama Tina kwa macho ya huruma kwa jinsi alivyokuwa amejibanza kwenye kona

    "Pole sana anti."

    "Usijali anko, kawaida tu. Unajua huyu msichana ana mdomo sana, angeniona hapa angekwenda kuyatangaza nje."



    "Ni kweli kabisa, umetumia busara kushauri usiingie."

    "Sasa mi nitatokaje humu?" alihoji mama Tina.

    "Ngoja nitoke mimi niangalie hali ya hewa."

    "Sawa."

    "Mama Tina," aliita Halima kule nje..

    "We mama Tina."



    Mama Tina aliogopa zaidi, alijua Halima ataingia kwake na atamkuta mtoto. Na ikawa hivyo kweli

    "We Tina mama yuko wapi?"

    "Katoka."

    "Kaenda wapi?"

    "Sijui, aliweka chakula kwenye sufuria akatoka."

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tina alijua hotipoti ni sufuria.

    Halima alishtuka kusikia mama Tina aliondoka na sufuria yenye chakula

    "Kaenda nacho wapi? Atakuwa kampelekea yule kijana."

    ***

    Wiki moja tu mbele, siku hiyo mama Tina alikuwa akitoka gengeni, akakutana na mama mmoja jirani yake anaitwa mama Sindilia.



    "Nilikuwa nakutafuta sana mama Tina."

    "Kuna nini tena mama Sindilia."

    "Mwenzangu si umbeya wa mtaani, uhujui?"

    "Upi huo mama Sindilia."



    "Nasikia unatembea na kijana mpangaji mwenzenu ndani."

    "Eti nafanyaje?"

    "Nasikia kuna kijana mmoja kahamia kwenu, ndiyo unatoka naye. Nikasema mama Tina huyuhuyu ninayemjua mimi anaweza kufanya upuuzi huo kweli?"



    ITAENDELEA





0 comments:

Post a Comment

Blog