Search This Blog

Monday, October 24, 2022

MWAGIA HUMO HUMO - 3

 





    Chombezo : Mwagia humo humo

    Chombezo : Kumbe Vikiungwa Vitamu

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Baada ya kusema vile aliingiza mkono mfukoni na kutoa pochi alihesabu noti tatu za kumi kumi na kunipa.



    “Mpelekee hizi mwambie nitakuja.”



    Nilizipokea na kufunga kazi zangu, pamoja na penzi letu kufa bado nilipelekwa na kurudishwa nyumbani na gari. Nilipofika nyumbani nilikwenda chumbani kwangu, kabla ya kufanya kitu chochote nilivua nguo zangu na kubakia mtupu kama nilivyozaliwa mbele ya kioo kikubwa na kujitazama upya kasoro katika mwili wangu.



    Nilituliza macho na kuyazungusha taratibu mwilini mwangu kuangalia nina kasoro gani inayonifanya kila kukicha nipoteze wanaume. Kila hatua niliyokuwa nikipiga katika kusafirisha macho yangu nilijigundua nina sifa kubwa sana ya kuitwa mwanamke mrembo tena mwenye kumtia hamu ya mapenzi mwanaume rijali.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Umbile langu kwa mimi mwenyewe kama ningekuwa mwanaume na kukutana na mwanamke mwenye umbile kama langu ningemganda kama ruba, lakini kwangu ilikuwa na tofauti kubwa sana. Baada ya kujigundua sina kasoro mwilini nilijikuta nikilia huku nikisema kwa sauti ya chini.



    “Hali hii mpaka lini?”

    ”Hali ipi?” Sauti ya Bi Shuu iliuliza nyuma yangu ilionesha Bi Shuu alikuwa ameingia kitambo bila mwenyewe kujua. Niligeuka na kwenda kujitupa kifuani kwake huku nikilia kwa uchungu.



    “Vipi tena mwali?”



    “Bi Shuu huu mkosi.”



    “Wa nini?”



    “Na Mateja kanimwaga.”



    “Kwa nini unasema hivyo?” Nilimweleza yaliyotokea ofisini  huku nikilia.



    “Ulimwambia namwita?”



    “Amesema atakuja wikiend.”



    “Basi kazi hiyo niachie mimi.”



    “Siamini kama atakusikiliza.”



    “Ngoja aje, nitajua mbichi na mbivu.”



    “Mmh, sina matumaini.”



    “Hebu kaoge nikupe michapo.”



    Nilikwenda kuoga ili nipate michapo ya Bi Shuu ambaye alinihakikishia kunipigania mpaka mwisho.



    Nini kitaendelea? Tukutane wiki ijayo.



    Mwisho wa wiki Mateja alikuja kuonana na Bi Shuu, alipofika waliingia kwa Bi Shuu. Nilikuwa na hamu ya kusikia alitaka kumuuliza nini juu yangu, nilijitahi kusikiliza dirisha la sebuleni la Bi Shuu lakini sauti walizokuwa wakizungumza zilikuwa za chini sikuweza kusikiliza waliyokuwa wakizungumza japo kuna muda nilisikia Mateja akisema.



    “Ilikuwa vigumu kuja kuyasema haya kwako, kwa vile mpaka anafikia umri alionao niliamini ni vigumu kubadilika.”



    “Mmh kama ni hivyo nina kazi nzito, naomba unipe muda vinaonesha chukuchuku havijaungwa.”



    “Hapana Bi Shuu nakuheshimu sana, lakini tumechelewa ungeniita mapema tungeweza kulipatia ufumbuzi. Sasa hivi nipo katika mipango ya harusi na kila kitu kipo katika hatua za mwisho,” kauli ile ilinikata maini.



    “Mmh, sawa nimekuelewa.”



    “Basi bibie wacha nikuache tutaonana,” nilimsikia Mateja akiaga ili aondoke.



    “Lakini naomba usimfukuze kazi mjukuu wangu.”



    “Bi Shuu suala la kazi haliingiliani na mapenzi, sitamgusa katika kazi hilo usihofu.”



    “Kama ni hivyo nashukuru, lakini Manka kapoteza dume la haja.”



    “Kila kitu mipango ya Mungu.”



    Nilimshuhudia Mateja akihesabu nyekundu tano na kumpatia Bi Shuu ambaye alishukuru nusra amlambe viguu Mateja kwa pesa aliyompa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Asante bwana yangu,” Bi Shuu alishukuru.



    “Kawaida Bi Shuu ukiwa na shida mtume Manka usiogope.”



    Mateja aliaga ili aondoke, nilitoka haraka dirishani kwa Bi Shuu na kukimbilia chumbani haraka. Nilijikuta nikiangua kilio kutokana na niliyoyasikia nusu kwa Bi Shuu, niliamini nilikuwa nimechelewa kuyasikia ya mwanzo kuhusu tatizo langu.



    Niliamini kosa lilikuwa langu nilitakiwa nimueleze mapema Bi Shuu kuhusiana na mabadiliko ya Mateja. Kwa kauli ya Mateja kama ningewahi ningeweza kulikoa penzi langu. Nikiwa nimejiinamia kitandani nilikia nilishtushwa na mlango kugongwa.



    Nilijua ni Bi Shuu ambaye hakutakiwa kugonga, lakini sikutaka kumlazimisha nilipaza sauti yangu ya kilio.



    “Ingia mlango upo wazi.”



    Mlango ulifunguliwa macho yangu yalimshuhudia Mteja akiingia ndani mwangu baada ya miezi sita toka alipokata mawasiliano na mimi. Alikuwa wa kwanza kuniuliza baada ya kukutana na michirizi ya machozi kwenye mashavu yangu.



    “Vipi Manka unaumwa?”



    “Ndiyo,” nilidanganya kwa vile sikuwa na cha kumwambia.



    “Nini tena?”



    “Kichwa.”



    “Ooh, pole sana, umemeza dawa?”



    “Bado.”



    “Basi nyanyuka nikupeleke hospital.”



    “Kitapoa tu.”



    “Basi kama utazidiwa utakwenda hospitali.”



    Mateja alisema huku akinisogelea mkononi alikuwa ameshikilia  pochi na kunikabidhi elfu hamsini huku akisema.



    “Kama utazidiwa zitakusaidia kwenda hospital.”



    Nilitaka kuzikataa zile pesa kwa vile shida yangu haikuwa pesa bali yeye mwenyewe. Nilitaka kumuuliza tatizo langu nini lakini niliamini nilikuwa nimechelewa nilitakiwa kuuliza mapema na si muda ule ambao alinionesha mpenzi wake mbele ya macho yangu.



    Nilipokea zile pesa Mateja aligeuka na kuondoka akiniacha nilikilia kilio cha kwikwi, baada ya kuondoka Bi Shuu aliingia na kunisimamia kama jini la kutumwa mkono kiunoni.



    “Manka kwenu hakuna unyago?” Lilikuwa swali la kwanza bila kujali kilio changu.



    “Unyago! Ndio nini?”



    “Mafunzo ya msichana kujitambua na jinsi ya kumridhisha mwanaume kitabia na kimapenzi?”



    “Sikuwahi kuyasikia.”



    “Mmh, ndiyo maana.”



    “Una maana gani kusema hivyo?”



    “Umepoteza wapenzi kwa kutojua mwanamke anatakiwa kumridhisha vipi mwanaume.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwani kuna kitu gani amekueleza Mateja?”



    “Tutazungumza na kulifanyia kazi.”



    Baada ya kusema vile alitoka na kuniacha na mawazo kibao juu ya maswali yake na kitu alichoambiwa na Mateja. Nilijiuliza kutopata mafunzo ya usichana yanahusiana vipi na kukataliwa na wanaume. Nilijikuta nikijizoazoa hadi kwa Bi Shuu kutaka kujua Mateja kamwambia nini.



    Nilipofika nilimkuta akizurudia kuzihesabu pesa alizopewa na Mateja, aliponiona aliziweka pembeni na kunitupia macho.



    “Mmh, mwali una jipya gani?”



    “Bi Shuu naomba unieleze ulichopelezwa na Mateja juu yangu?”



    “Nitakueleza kwa vitendo si la maneno.”



    “Matendo! Una maana gani?”



    “Nimepata sababu ya wewe kukorofishana na wanaume, inaonesha wazi hukupitia mafunzo ya usichana. Nina kazi na wewe, mi ndo Bi Shuu bwana kila mwali aliyepitia mikononi mwangu kila aliyeonja hakutema. Najua wanakutema kwa vile unawalisha vya chukuchuku.”



    “Vya chukuchuku! Una maana gani?”



    “Utajua baada ya kuviunga kisha uwaonjeshe kama hukuolewa narudi kijijini kwetu japo toka nitoke kwetu kumebakia magofu. Lakini nakuhakikishia nakutia mikononi mwangu halafu nisikie, eti bwana  bwana kaniacha,” Bi Shuu alishikilia pua na kusemea puani.



    “Nakwambia najua kuviunga vya chunguni mpaka vya mwilini, wala hujachelewa sasa hivi mtu akigusa amenasa.”



    “Utafanyaje?”



    “Nataka uombe likizo ya mwezi mmoja tena nitakuombea mimi kwa Mateja ili niviunge viwe vitamu.”



    “Vitamu! Vipi hivyo?”



    “Nataka ukiguswa usisimke, ujue mwiko upo katika chungu au upo juu ya mfuniko, kumpa mwanaume mpaka asuse. Usilale kama gogo uoneshe basi  upo safarini na si kukapua macho kama kibaka akimvizia mtu.”



    “Mmh, mbona umeniacha njia panda.”



    “Leo nataka kumbadili Mchaga awe kama Mmakonde.”



    Mmh, kila alilozungumza kwangu lilikuwa geni, nilisubiri niungwe ili niwe mtamu kwa mwanaume.



    Niliendelea na kazi yangu huku moyo ukiniuma kulipoteza penzi la Mateja, na mpenzi wake kutaka sifa kila muda wa chakula cha mchana lazima ampitie na wakitoka walikumbatiana na kuzidi kuniumiza. Lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo.



     Wiki moja baadaye Bi Shuu alinituma nimwite Mateja, kama kawaida nilimfikishia ujumbe wake, naye hakuwa na hiyana alikubali wito. Ilikuwa ajabu katikati ya wiki Mateja kukubali kwenda kumsikiliza Bi Shuu, tena aliniomba nikitoka kazini niongozane nae.



    Baada ya muda wa kazi niliongozana na Mateja hadi nyumbani, tulipofika aliingia kwa Bi Shuu na kuniacha nikiingia chumbani kwangu. Nilijikuta nikijawa na mawazo juu ya wito ule Bi Shuu alikuwa na kitu gani ambacho alichomuitia Mateja.



    Niliamini kabisa kama kutaka kumrudisha kwangu itakuwa ngumu kutokana na kila kitu kujionesha juu ya Mateja na mpenzi wake mpya. Nilipofika ndani hata hamu ya kuvua nguo iliniisha na kujikuta nikitoka na kujipitisha jirishani ili nisikie alichoitiwa na Bi Shuu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Lakini sauti ya Bi Shuu ilinishtua kwa kuniita, moyo ulinishtuka kutaka kujua naitiwa nini? Niliingia sebuleni na kumkuta  Mateja amekaa kwenye kochi akiwa ametulia. Bi Shuu aliponiona aliniambia.



    “Manka kwenye friji yako kuna soda?”



    “Mmh, jana nilimalizia nilikuwa na mpango wa kuweka leo.”



    “Basi nifuatie dukani.”



    “Bi Shuu si lazima achana nayo,” Mateja aliingilia kati.



    “Hapana babu lazima unywe soda.”



    Siku zote Mateja hakuwa na makuu alimkubalia Bi Shuu, baada ya kupewa pesa nilipitia chupa na kwenda dukani haraka ili niwahi mazungumzo yao.



    Nilipofika dukani nusra nipasuke kwa hasira baada ya kukuta wateja wengi kwenye duka la Mpemba. Sikutaka kusubiri nilikimbilia kwenye grosary iliyokuwa mbali kidogo. Nilinunua soda haraka haraka na kurudi hadi karibu na nyumba na kuanza kunyata hadi dirishani ili nisikilize wanazungumza nini.



    Nilipofika dirishani nilimsikia Mateja akisema.



    “Hakuna tatizo Bi Shuu kila kitu kitakwenda kama unavyotaka.”



    “Kama hivyo nitashukuru.”



    Baada ya mazungumzo yale palipita ukimya mfupi huku sauti za nyayo zikielekea mlangoni, nilichepua mwendo hadi mlangoni na kukutana uso kwa uso na Bi Shuu.



    “Vipi  mwali mbona umechelewa?”



    “Dukani kwa Mpemba kumejaa watu ilibidi nisogee mbele kwenye grosary.”



    Bi Shuu aliipokea soda na kuingia nayo ndani, nilibakia mlangoni nikijiuliza niingie au niende chumbani kwangu. Kupata jibu la nifanye nini lilinifanya nisimame kwa muda pembeni ya mlango. Kabla sijapata jibu nilishtushwa na sauti ya Mateja.



    “Manka kumbe upo hapa?”



    “Ndi..ndi..yo,” maskini nilipata kugugumizi cha ghafla.



    “Wacha niondoke zangu.”



    “Haya, karibu,” nilijibu kwa aibu huku nikiangalia chini.



    Mateja kweli alinichoka bila kuongeza neno alinitipa na kuelekea kwenye gari lake, Bi Shuu alimsindikiza mpaka kwenye gari. Nilibakia nikimsindikiza kwa macho.



    Baada ya Mateja kuondoka Bi Shuu alirejea, alipofika alinishangaa kunikuta nimetawaliwa na simanzi usoni mwangu.



    “Vipi mwali?”



    “Aah, kawaida tu.”



    “Acha kujitia ukiwa, kila kitu kina wakati wake na wakati ndio unakuja.”



    “Kwani Mateja kasemaje?”



    “Aseme nini?”



    “Kwa hiyo amekubali?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Akubali nini?”



    “Kwani ulimuitia nini?”



    “Kuhusu likizo yako.”



    “Kasemaje?”



    “Amekubali.”



    “Naanza lini?”



    “Sijajua lakini amekubali.”



    “Mmh, haya.”



    Niliachana na Bi Shuu na kwenda chumbani kwangu kujiandaa na kujimwagia maji ili nipumzike.



                                                         *********



    Siku ya pili nikiwa ofisini niliitwa na Mateja kunitaarifu kukubaliwa likizo yangu ambayo ingeanza wiki itakayofuata kwa kukamilisha kazi zangu zote muhimu. Nilipewa pesa ya likizo na kujiandaa kwenda kwenye unyago wa kiutu uzima ili niugwe niwe mtamu mwanaume akigusa anate.



    Baada ya kumalizia kazi za ofisi kwa wiki niliyopewa, niliruhusiwa kurudi nyumbani kuanza likizo. Nilirudi nyumbani na kumkuta Bi Shuu ambaye kabla ya kuweka makalio chini aliniuliza.



    “Mmh, umepewa likizo?”



    “Nimepewa.”



    “Basi kazi yote niachie mimi.”



    Siku ile nilipumzika bila kugusiwa kitu chochote, lakini alfajiri niliamshwa na kupelekwa kuogeshwa maji baridi kisha nilifungwa upande wa kanga bila nguo ingine ndani. Aliniongoza hadi katika chumba kimoja cha ndani kilichokuwa kitupu.



    Chini kwenye sakafu kulikuwa na maji kuonesha amemwagwa, baada ya kuingizwa mule ndani wakati huo kibaridi kilikuwa kikinichanyata. Bi Shuu alifunga mlango kwa nje na kuniacha nimesimama nikijiuliza ameleta mule ndani nifanye nini? Ajabu muda ulikatika nikiwa nimesimama, miguu ilichoka na kujiuliza mbona harudi ameniweka mule ndani ili iwe nini.



    Kukaa chini nilishindwa kutokana chini kuwa na maji na muda ule ubaridi kilikuwa kikali sana. Niliposhika mlango ulikuwa umefungwa kwa nje nilijaribu kuita kwani nilikuwa nimechoka kusimama zaidi ya saa moja. Hakukuwa na jibu la mtu yoyote.



    Nilijawa na mawazo juu ya kuwekwa chenye chumba chenye maji kisha kusimamishwa kwa muda mrefu. Nilijiuliza unyago wenyewe kama ndio ule  kwangu niliamini nitashindwa. Niliamua kukaa kwenye maji huku kibaridi kikizidi kunichonyota, kutokana na uchovu nilijiegemeza kwenye ukuta na usingizi ulinipitia.



    Nilishtushwa na maji ya baridi niliyomwagiwa ndoo nzima, Bi Shuu alikuwa mbele yangu akiwa amekunja uso kwa hasira na kunifokea kwa sauti ya juu.



    “Haya ndiyo yanakufanya ukose wanaume kila kukicha, mwanamke mvivu kama nini, kukuacha muda mfupi umeshindwa kuvumilia na kuuchapa usingizi kwenye maji.”



    “Samahani Bi Shuu.”



    “Haya fanya usafi haraka,” alisema huku akinitupia tambara kukausha maji.



    Nilichukua tambara na kuanza kufanya usafi kwa kukamilia maji kwenye ndoo mpaka nilipokausha, Bi Shuu alirudi na mkeka ambao aliutandika kisha alitoka na kurudi na chai. Tulikunywa chai kisha aliniacha nipumzike kwa kuniacha na kipande cha kanga tu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Jioni ilipofika Bi Shuu aliingia ndani na kuniketisha kitako na kuanza kuniuliza maswali.



    “Manka kitu gani wakati wa mapenzi hukipendi?”



    “Mmh, vingi lakini tabia ya wanaume kunisumbua wakati wa kilimo huna sikupendi.”



    “Mmh, kingine?”



    “Ni hilo hilo tu.”



    “Nimekuelewa, kuna vitu vingi vya kike vimekupita kushoto,  siku hizi wanaume hawapendi mwanamke anayelala kama gogo, husisimki wala hutingishiki.”



    “Bi Shuu nitikisike vipi au nisisimke vipi?”



    “Ndiyo maana leo umo humu ndani, ukitoka utajua unasisimka vipi na unatikisika vipi?”



    “Mmh, haya.”



    Mmh, hukuwepo ila malaika wako alikuwepo, sikujua alichonipa Bi Shuu kilikuwa adhabu au mateso. Niliwekwa mikao ambayo haikuwa tofauti na ile niliyokuwa nikiwakatalia wanaume, kila nilipotegea nilitandikwa bakora ya mgongo iliyotua sawia kwenye mgongo mtupu.



    Kila siku nilikuwa nikifanyishwa mazoezi yagumu ya viungo ambayo yalikuwa mateso mazito, kuna kipindi nilifikiria kumwambia bora aniache nilivyo kuliko mateso yale. Lakini Bi Shuu alikuwa mkali kama pilipili hakutaka mchezo hata kidogo hata nilipochoka bado alinilazimisha huku akisema.



    “Kushinda kuchoka ndiyo siri ya kumkata kiu mwanaume.”



    Nilibebeshwa mzigo kichwani nikiwa mtupu na kuanza kuchomwa na sindano kiunoni kitu kilichinifanya nishtuke kwa kuchezesha kiuno. Haikuishia hapo nililazwa chini na kubebesha mzigo kiunoni na kuendelea kuchomwa na kitu cha ncha ambacho kilinifanya nijinyonge nyonge bila kupenda.



    Niliendelea na mazoezi makali chini ya kungwi wangu Bi Shuu huku akinipa mbinu nyingi za kumchanganya kimapenzi mwanaume. Kuna mambo mengine siwezi kuyasema gazetini lakini Bi Shuu koma. Toka nizaliwe sikuwahi kukutana na mwanamke Shankupe kama yeye.



    Mtoto wa kike nilifundishwa maneno ya kusema mtu akiwa juu ya mnazi wangu, pumzi za kutoa wakati mwiko upo ndani ya chungu na akianza kugeuza maini nilitakiwa nilegee vipi huku macho na pumzi nizifanye vipi. Najua mwenzangu mie mwenye viuno kama vimefungwa mbao na wakati wa mapishi unatulia unasubiri mtu amwage mzigo akimaliza anyanyuke. Lakini ukikutana na bibi huyu lazima bwana akutaje jina.



    Mwezi mmoja mtoto wa kike nilipikwa nikapikika, baada ya mafunzo mazito Bi Shuu kwa ushambenga wake alinitafutia mwanaume ili kutaka kunipima baada ya mazoezi. Sikukataa kwa vile nilijua kile ndicho kipimo, mtoto wa kike nilijiandaa kuonesha kilichoniweka ndani kwa mwezi mzima. Cha ajabu Bi Shuu alitaka mchezo ule nichezee chumbani kwake, mmh, makubwa madogo yana nafuu.



    Sikutaka kumbishia kwa vile nilikuwa na usongo na mafunzo ya Bi Shuu ambayo yalinifanya nijiamini na kumtamani mwanaume nimtoe kamasi nyembamba. Baada ya kijana aliyechaguliwa na Bi Shuu kufika alikaribishwa chumbani kwa Bi Shuu, nilijikuta  nikiwa na usongo na yule kijana ambaye alikuwa mmoja wa vijana walioninanga sijui kucheza nilipokutana naye siku ya kwanza.



    Baada ya kuingia ndani nilimpokea juu juu na kumtoa nguo maungoni kama kuku aliyechinjwa na kunyonyolewa manyoya. Baada ya kumuandaa mtoto wa kike huku mwili ukinisisimka baada ya kukiona kijiti cha kupokezana kwenye mbio fupi.



     Mtoto wa kike nikiwa nataka kufanya mtihani wangu wa kwanza kwa umakini mkubwa huku nikipitia hatua moja baada ya nyingine. Nilimlamba mwili mzima kama mama mbuzi akimsafisha mwanaye baada ya kumzaa, nilijua kutumia ulimi wangu.



    Nilipofika kwenye shina la mnazi mtoto wa kike nilitulia kwa muda huku vidole laini na ulimi ukifanya kazi yake. Mara nilimuona kijana wa watu akitetemeka kama amekunywa coka ‘ngriiiiiiiiii’, maskini kumbe alikuwa akilia chozi lisilo na msiba.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kijana wa watu naye akabadili upepo na kunirudishia mashambulizi.



    Mtoto wa kike nilipoguswa nililegea na kuzitoa pumzi huku jicho likipoteza kiini cheusi. Kwa mara ya kwanza niligundua kumbe mwili kila sehemu una raha yake kuishinda nyingine. Kama nilivyofundishwa na Bi Shuu kila nilipoguswa nilisema neno lake.



    Baada ya mshike mshike wa maandalizi cha chakula, hatimaye kiliiva na kutengwa mezani. Nilimpokea juujuu huku nilionesha jinsi gani mtoto wa kike nilivyoshikika, mtoto wa kike sikuwa na haraka nilifuata mwiko ulivyogeuza maini ili kumfanya mpigaji na mwimbaji wasitofautiane.



    Mtoto wa kike nilimaliza maneno yote mdomoni, sikuamini kutatalika kama bisi kwenye chungu cha moto. Mpaka mchezo unakwisha nilikuwa nipo hoi kwani niliamini vilikuwa vitamu kijana wa watu kila alipomaliza alileta sahani aongezewe. Nami nilimpakulia naye alijilia huku akigugumia kama dume la njiwa lenye wivu. Huku nikilia mara nne kwa utamu wa msiba.



    Lazima niseme ukweli kuna kipindi nilitaka kunyanyua mikono, maji yalikuwa shingoni, nyonga iligoma kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kuyakata mawimbi.



    Bi Shuu alinieleza kumfurahisha mwanaume si nyonga tu, hata kujua kuyapangilia maneno hasa kumsifia hakuna mwanaume kama yeye pia anajua kumshikisha punda adabu kwa kumtandika bakora balabala. Baada ya nyonga kugoma na kukiona kiuno kikiwaka moto, nilitumia sauti kumsindikiza mwenzangu mpaka alipofika juu ya mnazi.



    Kijana wa watu hakuamini ilibidi aniulize.



    “Manka, kumbe mambo unayaweza mbona ulikuwa uninikatili, mambo haya ungenipa tokea zamani sasa hivi ungekuwa mke wangu.”



    “Nilikulisha vya chukuchuku lakini sasa vimeungwa ndio maana unaviona vitamu.”



    Kijana wa watu bila kutegemea alinipa elfu 50 kama asante ya kumpa penzi tamu ambalo alikiri hakuwahi kulipata kwa mwanaume yoyote. Baada ya kuondoka na kuniacha nimejilaza baada ya kuhisi uchovu kila kona ya mwili kutokana na mshike mshike wa kufanya majaribio ya vitendo. Bila ya kujigeuza usingizi mzito ulinipitia juu ya kitanda cha Bi Shuu.



    Nilishtuka baada ya masaa matatu nikiwa nausikia mwili mchovu kila kona, Bi Shuu aliniamsha na kukuta ameniandalia maji ya kuoga. Nilioga kupunza uchovu na kurudi ndani ambako chakula kilikuwa tayari. Tulikula pamoja kisha tulipumzika sebuleni, cha ajabu niligundua Bi Shuu akiniangalia kwa kuniibia kitu kilichonifanya nimuulize.



    “Bi Shuu vipi?”



    “Kuhusu nini?”



    “Naona kama unanivizia kunitazama kuna nini si uniambie.”



    “Mmh, kweli ulikuwa na usongo.”



    “Wa nini Bi Shuu?”



    “Kazi umeifanya vizuri japo kuna kipindi ulichemsha.”



    “Ulijuaje?”



    “Nilikuwepo muda wote toka unaanza mpaka unamaliza, kwenye maandalizi nakupa mia kwenye sauti na pumzi sabini kwenye mchezo wenyewe hamsini.”



    “Jamani Bi Shuu kujitahidi kote unanipa hamsini.”



    “Manka kwanza nashangaa mtu ulikuwa hujui lolote umeweza kupata hamsini wengi huwa chini ya hapo.”



    “Bi Shuu kama nina hamsini nimeweza kupewa zawadi nikipata mia itakuwaje?”



    “Mia kupata ni kazi kwa vile maungo yako yalikakamaa muda mrefu lakini utaweza kufika hata sabini kwa bidii yako.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mapungufu yangu ni nini?”



    “Kutumia nguvu nyingi ambazo hukufanya upumue kwa kasi sana kitu kinachokufanya uchoke sana, pia papala ya kukata nyonga. Mwanzo uliweza kwenda sawa lakini ulipoanza kuchoka alifanya bora liende. Lakini mwanzo ni mzuri.



    Kwa uwezo wako huo na kuonesha ulikuwa makini kwa kuyashika mafunzo, inaonesha nikikuongezea matirio kama kwenye mpira ni ujanja wa kuweza kumsoma mwanaume. Kila mwanaume ana amambile tofauti na mwenzake na wengine wana nguvu kama kirafu unatakiwa kufanya nini.”



    “Bi Shuu nitashukuru nimeteseka sana, kwa nini sikuyapata mafunzo haya mapema ili kuweza kumdhibiti Mateja,” Nilijikuta nikidondosha chozi kulikumbuka penzi la Mateja nililolipoteza kutokana na kutokujua sheria za kitandani na kunifanya niendeshe ovyo na kusababisha ajali za kutoelewa alama za kitandani.



    “Manka usiwe kama kipofu aliyefumbua macho na kumuona chura na kuamini hakuna kama chura chini ya jua, mbona kuwa wanaume zaidi ya Mateja”



    “Bi Shuu ni kweli usemayo lakini Mateja niliamini ni mwanaume sahihi kwangu.”



    “Ni kweli, lakini kisicho riziki hakiliki we jipange ukikolea utamu nakuhakikishia nitakutafutia bwana Mateja cha mtoto. Kwanza nataka niyafanyie kazi makosa madogo madogo ambayo yatakufanya kila atakaye gusa atangaze ndoa. Nataka umlize mwanaume kama mtoto mdogo, umeisha ona mtoto akinyang’anywa ziwa jinsi anavyolia?”



    “Ndiyo.”



    “Basi nataka mwanaume chozi limtoke, kuna vitu vidogo wanawake hawajui, vitu hivyo ukimfanyia mwanaume kama ameoa lazima aitelekeze nyumba yake. Mchele mmoja lakini unatofautiana katika mapishi, hii nyumba jasho la mwili wangu pale nilipompata mume wa mtu. Leo hii naishi kwangu nawe nataka uwe mara mbili yangu.”



    “Bi Shuu mbona wasichana hatuna vitu hivi?”



    “Siku hizi uzungu umetawala na kujikuta wakipoteza vitu vingi vya kumfurahisha mwanaume. Kumfurahisha mwanaume kitandani si kigezo pekee cha kuilinda nyumba yako. Kuna vitu vingi ambavyo vipo nje ya kitanda.



    “Kuna wasichana wengi wana nyonga laini kama unakula keki lakini wana mapungufu kama chujui la nazi ambayo hayawezi kumfanya atulie kwa kwenye ndoa yake. Kama tabia yako nzuri ulichanganya na machejo ya kitandani hata utakita hata ndege utanunuliwa japo mwenzio hana uwezo wa kununua baskeri.”



    “Mbona hujanifunda na hivyo?”



    “Siwezi kukuichanganya kimoja kimoja, kwanza tunatengeneza mtego akiingia anase, ukimaliza mafunzo ya mwili tunarudi tena kilingeni ili mumeo aone tofauti ya magumegume na mwanamke.”



    “Bi Shuu mbona nimechoka sana.”



    “Umelia mara ngapi?”



    “Mara nne.”

    “Mara ya mwisho ulilia mara ngapi ulipokutana na mwanaume kabla ya leo?”

    “Mara mbili sijawahi kulia zaidi ya hapo.”

    “Ndio maana, lazima uchoke  umeukamua mwili sana na shughuli haikuwa ya kitoto kuna kipindi kidogo nisimamishe mpambano mlikuwa kama mnataka kutoana roho.”

    “Bi Shuu umejuaje?”

    “Nikuambie mara ngapi nilikuwa nafuatilia toka mwanzo mpaka mnamaliza”

    “Jamani Bi Shuu kumbe ulikuwa unanipiga chabo,” Mbona niliona aibu mtoto wa kike, jamani bibi huyu ana mambo kumbe mwenzie nahenyeka yeye anapiga chabo.

    “Sasa ningejuaje mapungufu yako.”

    “Mmh, makubwa madogo yana nafuu.”

    “Na hayo mengine lini maana muda wa kurudi kazini umekaribia.”

    “Wiki iliyobakia inatosha, kapumzike jioni kama kawa mpaka kieleweke.”

    “Wacha nikalale naona mwili sio wangu, kwenye pesa hiyo chukua nusu niachie nusu”

    “Asante mwali, nina imani sasa umeamini nilichokisema kinatimia”

    “Wee mwisho Bi Shuu je, ungenikamata ndio unavunja ungo naona kila aliyenionja angeniganda kama ruba.”

    Baada ya mazungumzo nilimuomba Bi Shuu nikapumzike mwili ulikuwa na uchovu, nilikwenda chumbani kwangu kulala kwa kulifungulia feni mpaka mwisho mtoto wa kike nilijiachia kitanda kizima.

                                                                        *******

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama kawaida Bi Shuu aliniamsha kwenye chakula cha mchana na baada ya chakula cha mchana nilioga na kupanda tena kitandani. Sikuamini mwili kuchoka kiasi kile, Bi Shuu alinieleza ni kutokana na kuzoea kulala kama gogo kitandani lakini siku ile niliushughulisha mwili hata kumwaga machozi manne kitu ambacho hakikuwa kawaida yangu.

    Nilipogusa kitandani usingizi haukuchelewa kunichukua, Bi Shuu aliniamsha saa mbili za usiku nilikwenda kuoga kisha nilipata chakula cha usiku. Baada ya chakula nilipumzika kidogo na kuingizwa unyagoni kumalizia muda ulipobakia kwa kunipa mbinu za kummiliki mwanaume kwa sauti na matendo huku tabia ikiwa ndiyo uliyochukua sehemu kubwa.

    Katika mafunzo siku moja alinipa nipike chakula baada ya kupika tulikula wote, kesho yake alinipa nipike tena chakula kilekile, lakini hakunipa chumvi. Nilipomuuliza alisema nipike vile vile na muda wa kula nilishindwa kumuelewa baada ya kunieleza nipakue, nilipakua na kukila bila chumvi. Tulikula wote bila kujua chakula kile kwa nini tulikila  bila chimvi.

    Sikutaka kumuuliza kwa vile hakikuwa kingi tulikuwa na kukimaliza wote. Baada ya chakula usiku Bi Shuu akiwa ameniweka chini aliniuliza.

    “Manka kuna tofauti gani ya chakula ulichopika jana na leo?”

    “Tofauti yake cha jana kina chomvi lakini cha leo hakina chimvi.”

    “Kipi chakula kizuri?”

    “Cha jana.”

    “Kwa sababu gani?”

    “kina chumvi lakini cha leo hakina chimvi.”

    “Mbona umekila.”

    “Nilishindwa kuelewa ulikuwa na maana gani.”

    “Lakini bila hivyo usingekula?”

    “Nisingekula.”

    “Unajua nilikuwa nina maana gani?”

    “Hata sijui”

    “Hii nakuonesha yaisha ya ndani ya ndoa, wanawake wengi wanawalisha wanaume chakula kisicho na chumvi. Wapo wanaokosa uvumilivu huvunja ndoa lakini wanaoburuzwa na mapenzi hula chakula kisicho na chumvi kila siku na kuishia kunung’unika moyoni.”

    “Lakini Bi Shuu kama mkewe hamuwekei chumvi anashindwa vipi  kuchukua mwenyewe kuweka kwenye chakula”

    “Swadakta swali zuri, ndio maana kukuweka huku ndani vitu vingi huvifanya kwa mafumbo jibu lake huwa ndio maisha yako ndani ya mahusiano yako. Chakula na chumvi sikuwa na maana hiyo bali kukueleza matatizo ndani ya nyumba nyingi wanawake wengi ndoa zao uziondoa chumvi bila wao wenyewe kujua”

    “Kivipi?”

    “Nyumba nyingi mwanzo wa mapenzi huwa moto moto kama kumpokea mpenzio akirudi kumtengea chakula kula pamoja kuoga pamoja kuwa karibu yake kumpoza uchovu wa kutwa nzima ambao ndiyo tiba ya mwanaume kutoitafuta faraja nje ya ndoa yake.

    “Wengi baada ya muda baadhi ya vitu hundoka kabisa na ndoa kuendeshwa kimazoea, moyoni lazima utasema hivi nisivyofanya kuna nini kwani hawezi kufanya mwenyewe. Kuacha kuyafanya hayo ni sawa kuondoa chumvi kwenye mahusiano yako na kumfanya mpenzio kula chakula kisicho na chumvi.

    “Wengi huvumilia na kuumia moyoni lakini wasio na uvumilivu huitafuta chumvi hiyo nje ya ndoa. Hapo ndipo tatizo linapoanza na kuipoteza ndoa yako bila kujua tatizo ni wewe mwenyewe. Kuondoa baadhi ya vitu ndani ya ndoa yako kama kutompokea mumeo au kutokula na kuoga pamoja ni vitu vinavyo mwanaume huona vya kawaida lakini ni ufa mkubwa katika ndoa.

    “Penzi halizeeki bali mwili ndio unazeeka, vyote nilivyokueleza usikipunguze hata kimoja ukiingia katika ndoa yako. Nakuhakikishia bwana atakaye kuoa watu watasema umemuwekea libwata, limbwata mwali ni kumlea mumeo kama mtoto. Nina imani umenielewa”

    “Mmh, kweli nimekubali Mungu kakujalia kumtengeneza mwanamke, nina imani ungenieleza  kwa maneno ningekuelewa nusu lakini kwa vitendo nimekuelewa zaidi. Asante Bi Shuu”

    “Nashukuru kuonesha ni muelewa na mtu mwenye usongo na mafunzo”

    “Lazima Bi Shuu niwe na usongo nimeteseka sana”

    Nilimalizia mafunzo huku akilekebisha mapungufu aliyoyaona kwenye mtihani wangu wa kwanza.”

    Nilikuwa sijawahi kula kungu mtoto wa kike nilikula kungu jicho ukiniangalia utanionea huruma. Nilimaliza mafunzo salama, kabla ya kuanza kazi alinitafutia tena mwanaume mwingine naye alikuwa mmoja wa wale walioninanga mwanzo.

    Nilikuwa na imani alikuja akijua ni yule Manka wa mwaga msigo babangu kisha uondoke. Mafunzo niliyopata ya mwisho mtoto wa kiume chozi lilimtoka, kwenye maandalizi tu alilia zaidi ya mara tatu. Mtindo huu nilifundishwa kama sitaki kutumika sana kwanza namchosha mwanaume mwenye maandalizi.

    Hata ulipoingia baharini nusra anifie maji baada ya kushikwa na pumu katikati ya safari, machejo yalimfanya aifukuze Land Curuser VX kwa bajaj. Ilibidi niingie kazi ya kumpepea asinifie, baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida aliniangalia mara mbili.

    “Ni wewe Manka au naota”

    “Kwani vipi?”

    “Hata siamini, kumbe ulikuwa unafanya makusudi”

    “Ulikuwa vya chukuchuku sasa vimeungwa”

    ”Una maana gani?”

    “Si umeona mwenyewe si la kusimuliwa”

    “Nimekubali lazima nirudie”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ”Mmh, cha kunifia kifuani hapa namefungulia injini moja katika injini nne si ungebadilika jina.”

    “Manka naomba nikuoe.”

    “Ni haraka sana vuta subra”

    “Lakini niwe mmoja wa watu wa mbele kufikiriwa.”

    “Hakuna tatizo”

    Yule kijana ambaye alikuwa kama mlevi aliniachia laki moja ya asante”

    Baada ya kuondoka Bi Shuu kama kawaida yake alitoa tathimini yake.

    “Mwali japo mpinzani wako hakuonesha upinzani lakini umejitahidi sana tena sana, sasa nina uwezo wa kukueleza kapambane na mtu yoyote. La muhimu kuzingatia niliyokueleza hakika kila atakayehusa lazima anate sasa hivi mwili wako ni asali yenye ulimbo”

    Maneno ya Bi Shuu yalinifanya nijiamini nimeanza kuiva kimapigano, kwa vile muda ulikuwa umekwisha jumatatu ilipofika nililipoti kazini kwangu. Nilimkuta aliyekuwa amenishikia, baada ya kunipokea alinielekeza kazi za kufanya na yeye kuendelea na majukumu mengine. Kuna kitu kimoja nilisahau kukueleza baada ya kukaa ndani kuchezwa nilipotoka nilitakata na kunawili mtoto wa kike.

    Nikiwa naendelea na kazi bosi wangu dear zilipendwa aliingia ofisini, ilionesha hakujua kama naanza kazi siku ile. Alipofika hakuniangalia alinisalimia.

    “Za saizi?”

    “Nzuri”

    “Ile kazi tayari?”

    “Ndiyo namalizia”

    ’Baada ya muda gani”

    ”Dakika kumi”

    “Ok, fanya haraka.”

    Baada ya kusema vile aliingia ofisini kwake, ilionesha hakujua kama nipo mimi. Baada ya kumaliza kazi niliyoikuta niliprinti na kumpelekea, alikuwa bado ameinama nilipofika mbele yake nilisema.

    “Bosi kazi tayari”

    Sauti yangu ilimshtua na kunyanyua macho, kwa mshangao wa ajabu alisema.

    “Ha! Manka umekuja saa ngapi?”

    “Toka asubuhi”

    “Ina maana nimekupita kwenye ofisi yako?”

    “Ndiyo bosi”

    “Ooh, samahani sana”

    “Kawaida tu bosi wala usijisikie vibaya,” mtoto wa kike nilikuwa nimekwenda kimitego na kumuomba Mungu Mateja ajichanganye sijui aonje kidogo. Niliapa ningefanya aliyofundishwa na mengine nisiyo yajua ili kuhakikisha anakutana na vitu vipya katika medani ya mapenzi.

    Mtoto jicho lilikuwa limelegea kidogo jicho lilionekana kwa kujipaka wanja chini na juu na kuongeza uzuri wangu. Japo nilijijua mi mzuri, lazima mzuri ujijue kabla hujasifiwa na watu, lakini mapungufu yangu Bi Shuu aliyamaliza mengi niliyokuwa nayo.

    Mateja ilionekana kama kuchanganyikiwa kuniona nimebadika nimependeza na ninavutia tena kimitego ya kike hasaa.

    “Manka ulikuwa unakula nini?”

    “Kwa nini bosi?” nilimuuliza kwa sauti laini huku nikimchanulia tabasamu ya kufa mtu huku jicho nalo likizungumza.

    “Hapana, umependeza na unavutia”

    “Nashukuru kwa hilo ila moja umesahau”

    “Lipi hilo?”

    “Sasa hivi si Manka chukuchuku ila Manka huyu kaungwa akaungika”

    “Una maana gani?”

    “Bosi nitakuomba kesho nikukaribishe chakula cha usiku”

    “Mmh, hakuna tatizo kwa vile wiki hii ni ya mwisho baada ya hapo nitakuwa katika maandalizi ya harusi.”

    “Hakuna tatizo kazi njema.”

    “Na wewe pia.”

    Baada ya kumkabidhi kazi yake nilirudi kuendelea na kazi yangu, moyoni niliapa kama kweli atakubali mwaliko wangu amekwisha.Muda wa mchana Mchumba wake alimuijia kama kawaida na kwenda naye kupata chakula cha mchana.

    Japo moyo uliniuma lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo kutokana na makosa kuyafanya awali. Jioni niliporudi nilimueleza Bi Shuu mwaliko niliompa Mateja kuja kula chakula cha usiku.

    “Mwali akiingia amekwisha, hakikisha anaisahau ndoa yake”

    “Bi Shuu la kuuliza hilo”

    “Nakuaminia mtu wangu.”

    “Naiona kama kesho inachelewa”

    “Itafika punguza munkari, usije yakakamia maji”

    “Si hivyo Bi Shuu nakuhakikishia kuyafanya yote kwa umakini mkubwa labda asije.”

                                                                 *****

    Siku ya pili nilikwenda ofisini na kuendelea na kazi bosi alipokuja alinisalimia.

    “Mrembo hujambo”

    “Sijambo bosi simshindi wifi”

    “Manka mbona umefika mbali salamu umeijibu sivyo”

    “Samahani bosi, za nyumbani”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mmh, salama sijui zako.”

    “Nami namshukuru Mungu, haya nipo ndani”

    “Sawa bosi”

    Kabla ya kuingia ofisini aligeuka na kuniuliza.

    “Mwaliko wa usiku upo vile vile au kuna mabadiliko”

    “Hakuna mabadiliko”

    “Haya,” alisema huku akifungua mlango na kuingia ofisini kwake.

    Baada ya kuingia ofisi nilibaki nilikuwa siamini kama nimesikia vizuri kuulizia mwaliko, niliona dalili njema zimeanza asubuhi jioni ni kumalizia tu. Huwezi amini siku hiyo nilifanya kazi kwa furaha ya ajabu kama Mateja amenikubali nirudiane naye.

    Jioni kabla ya kuondoka aliniaga na kuniahidi angekuja usiku.

    “Kweli Mateja utakuja?”

    “Kama siji ningekuambia”

    “Karibu sana mpe..” Mungu wangu nilitaka kujisahau kumwita mpenzi wakati tuliisha achana long time a go.

    “Niite tu mpenzi wala usijisikie vibaya,”

    “Hapana bosi”

    “Haya baadae”

    Mateja aliondoka na kuniacha nikipanga vizuri vitu vyangu kabla ya kurudi nyumbani.

                                                          *********

    Nilkipofika nyumbani Bi Shuu aliniomba siku ile aandae chakula cha mgeni, sikuwa na hiyana mtoto wa kike nilimuacha afanye mambo yake. Nilikiandaa chumba changu na kukiweka katika hali ya usafi wa hali ya juu, kama kawaida Bi Shuu alinipatia mafusho ya manukato mazuri.

    Baada ya kuhakikisha chumba changu kinapendeza niliingia kuoga mtoto wa kike na kujifusha utuli huku nikipaka wanja wa sina mume ambao lazima mwanaume barabarani akusalimie.

    Baada ya kusimama mbele ya kioo kujitathimini, nilizidi kujisifia mtoto wa kike kwa upendeleo niliopewa na mwenyezi. Baada ya kuhakikisha nipo sawa, nilikunywa kungu na kuanza kujisikia nikisisimka mtoto wa kike kama mamba mwenye njaa.

    Nikiwa nimekaa mkao wa kula kumsubiri Mateja, mara aliingia Bi Shuu na kuniongezea mambo fulani ya muhimu pindi Mateja akiingia chumbani kwangu.

    “Mwali nilitaka kusahau kwa vile anajua anakuja kula chakula na kuondoka cha kufanya akiingia tu, ukimvamia kwa kumkumbatia huku akimbusu hakikisha mikono yako inafanya kazi ya haraka kumvua nguo bila kuchelewa mpatie upande wa kanga.

    Wakati huo mimi nitakuwa tayari nimepeleka maji ya kuoga bafuni niliyoyawekea viungo. Nani alikuambia wanawake wa Tanga ndio wanajua mahaba, nataka Mateja akiondoka kila kitakachokuja mbele yake akione shombo.”

    “Nimekuelewa Bi Shuu.”

    “Sio umenielewa bahati hairudi mara mbili, itumie kubadili matokeo.”

    “Matokeo ya nini Bi Shuu?”

    “Ukimaliza kilicho tupotezea muda nitakwambia.”

    “Nitafuata maelekezo yako.”

    Baada ya kutoa maelekezo Bi Shuu alirudi kumalizia kutengeneza maajumati ya mgeni rasmi.

    Majira ya saa moja na nusu gari la Mateja lilisimama mbele ya nyumba yetu, ajabu usongo wote niliokuwa nao uliyeyuka kama donge la mafuta katika kikaango cha moto. Nilijikuta nikijawa na hofu juu ya nilichokipanga kumpa Mateja kama ataingia katika mtego wangu.

    Nilijihisi kupoteza ujasiri niliokuwa nao kabla ya Mateja hajaja, niliikandamiza mikono yangu kifuani na kubana pumzi na kukaa kwa muda kuvuta ujasiri kisha niliitoa na kushusha pumzi nzito.

    Baada ya kujipa ujasiri nilijitengeneza haraka haraka ili kujiweka sawa japo nilikuwa nimejiweka kimitego ya kike hasa. Ndani nilivalia kufuri la bikini la rangi nyekundu juu nilivalia kanga nyepesi ukituliza macho unaona kila kitu cha ndani.

    Wakati huo chumba kilikuwa kikinukia utuli kila kona mimi mwenyewe nilikuwa kama Hululaini malaika wa daraja la juu. Jicho mtoto lilikuwa lemelegea kwa kungu huku mwili ukisisimka kama nyoka mwenye hasira aliyepandisha sumu kwa ajili ya kumgonga mtu.

    Wakati nikifanya matayarisho ya mwisho kabla ya kumpokea Mateja mbele ya kioo, Bi Shuu muda huo alikuwa amempokea.

    “Wawooo mwanaume huyo.”

    “Niambie kipenzi changu?” Sauti ya Mateja ilisikika.

    “Niseme nini mkeo nawe umetupa jongoo na mti wake.”

    “Bi Shuu kama ningetupa leo ningeonekana hapa?”

    “Mateja kula nisishibe heri nisipewe.”

    “Bi Shuu heri nusu shari kuliko shari kamili na kidogo si haba kuliko kukosa kabisa.”

    “Nitakuwezea wapi mtoto wa Kisukuma aliyejifanya Mzaramo kwa kujifanya unajua kuyageuza maneno.”

    “Vipi nimewakuta?” Mateja aliuliza mimi ndani kiroho paa!

    “Umewakuta wamejaa tele wewe tu,” mmh, maneno ya Bi Shuu yalijaa nahau na misemo na kuzidi kuniweka njia panda.

    Wakati nikijua hodi itapigwa wakati wowote nilipandisha tena pumzi na kuzishusha kisha nilijiandaa kumpokea. Mara mlango uligongwa.

    “Hodi ndani?”

    “Karibu,” nilimkaribisha huku nikikaa mkao wa chura kuruka.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara mlango ulifunguliwa na Mateja aliingia, mtoto wa kike nilijizoazoa na kumkumbatia.

    “Ooh, karibu mpenzi.”

    “Asante za hapa?”

    “Nzuri.”

    Mtoto wa kike niliutambaza mdomo wangu na kutua kwenye mdomo wa Mateja ambaye alikuwa bado amepigwa na butwaa, nikihema kama mgonjwa wa pumu. Mateja alinipokea na kubadilishana mate, mikono yangu alipata nafasi ya kumvua shati.

    Baada ya kumvua shati nilimsukumia kitandani na kumlalia juu, kwa haraka nilimalizia na vilivyokuwa vimebaki chini kisha nilimpatia upande wa kanga. Kila nililolifanya siku ile kwa Mateja kilikuwa kigeni kwake niliamini alijua bado Manka wa mwaka 47 hohehahe asiyejua chochote.

    Niliamini muda huo Bishuu alikuwa ameisha peleka maji yaliyochanganywa na viungo bafuni. Nilimshika mkono Mateja na kutoka naye  nje kumpeleka bafuni kuoga, Bi Shuu kweli alikuwa amepania mlangoni nilikuta kuna ndala mpya. Mateja alivaa na kuongozana naye hadi bafuni.

    “Karibu mpenzi uoge.”

    “Asante.”

    Nilimwacha Mateja bafuni na kurudi ndani kujiandaa kumlisha vilivyoungwa na Bi Shuu. Kabla sijaweka tako chini Bi Shuu aliingia bila hodi na kusema kwa sauti ya juu.

    “Wee mwana, ndio unafanya nini?” Kauli ile ilinishtua sana.

    Kutokana na makosa ya kuruka baadhi ya sehemu katika hadithi ya wiki iliyopita kufikia hatua ya kuwachanganya wasomaji. Leo tutaelezea kwa ufupi toka Mateja alipomuona Manka ofisini mpaka kufikia hatua ya kumsubiri chumbani. Baada ya Mateja kushtuka kumuona  Manka jinsi alivyopendeza kwa muda ambao hakuwepo kazini alimsifia kuwa amependeza mara dufu. Naye Manka alitumia nafasi ile kumkaribisha Mateja chakula cha jioni kwake. Mateja alimkubalia na kumuahidi angefika jioni kwa ajili ya chakula.

    Manka aliporudi nyumbani alimueleza Bi Shuu kuwa Mateja amekubali kuja kula chakula cha jioni. Bi Shuu alimueleza asiipoteze nafasi ile adimu ahakikishe kama atakubali kuvila vilivyoungwa basi achanganyikiwe. Bi Shuu alimuomba kazi ya kupika chakula aifanye yeye ya kuandaa chakula cha ujanani kwake pale alipokuwa akimtengenezea mpenzi wake.

    Baada ya makubaliano na Bi Shuu Manka aliingia ndani kujiandaa kwa ajili ya kumpokea Mateja kwa kufanya usafi wa mwili na chumba huku akifusha udi na asumini kumwagia kitandani. Yalikuwa mafunzo tosha ya Bi Shuu ambayo Manka aliyafanyia kazi.

    Baada ya kila kitu kuwa tayari Manka alimsubiri kwa hamu Mateja mpaka alipofika. Baada ya kumuandalia maji na kumuacha aoge peke yake ndipo Bi Shuu alipomfuata na kumuuliza amefanya nini.

    Ili kujua kosa lake nina imani mpaka sasa tupo pamoja, haya tuserereke pamoja...

    Kauli ya Bi Shuu ilinishtua na kujiuliza nimefanya kosa gani tena.

    “Bi Shuu nimefanya nini?”

    “Manka haya ndiyo makosa mnayafanya sana wanawake wengi, kwa nini umuache aoge peke yake. Nenda kaoge naye ikiwezekana anza kumliza kilio cha raha bafuni.”

    Mmh, mtoto wa kike haraka nilitelemsha nguo ya ndani na kubakia na upande wa kanga nyepesi na kumuwahi Mateja kabla hajajipaka sabuni. Nilipokaribia bafuni Mateja alikohoa kumaanisha kuna mtu.

    “Mm..mm..mmh.”

    Nilisukuma mlango na kumkuta amejipaka sabuni usoni, alipofumbua macho aliniona nipo mbele yake.

    “Aah, kumbe wewe?”

    “Ulidhani nani?”

    “Nilifikiri kuna mtu kaingia kwa bahati mbaya.”

    “Nilikwenda kutoa nguo ili tuje tuoge wote,” nilidanganya.

    “Sasa mbona hukuniambia kama tunaoga wote uliondoka kimya kimya.”

    “Nilijua nakuwahi.”

    “Haya tuoge.”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog