Search This Blog

Monday, October 24, 2022

ASIA DIGITALI - 3

 





    Chombezo : Asia Digitali

    Sehemu Ya Tatu (3)



    DENISS aliondoka kurejea nyumbani akiwa na furaha ya aina yake. Hakuwa na moyo wowote wa majuto juu ya kitendo chake cha kufanya mapenzi na Asia wakati yu katika ndoa.

    Alikuwa akiwaza kuwa ameweza kumzunguka mbunge fulani na kulala na mkewe. Nafasi ya kipekee kabisa.

    Jambo jingine lililompagawisha ni uamuzi wa kushangaza wa Asia wa kumnunulia kiwanja na ikiwezekana kumsaidia katika ujenzi.

    “Wabunge wetu wana pesa hawa pumbavu zao…” alitokwa na kauli hiyo Deniss huku akiwa makini na barabara.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akiwa katika kumuwazia Asia mara ukaingia ujumbe katika simu yake, akasubiri alipoyafikia mataa ya kuzuia magari, akaichukua simu.

    Alikuwa ni Asia ametuma ujumbe.

    “I have never been fuc*ed like this. Thanx.”

    Ujumbe ule mfupi, Deniss aliurudia mara mbilimbili, hakuamini hizo sifa alikuwa anapewa yeye.

    Alikuwa amefanikiwa kumteka Asia kwa penzi la muda mfupi tu.

    “Hapa huyu mbunge asahau kabisa kama ana mke. Na mimi ndo sitoki hapa.” Aliongea kwa sauti ya juu, tabasamu likiutawala vyema uso wake.

    Deniss alitamani sana kuendelea kuwa na ujumbe ule katika simu yake, lakini tatizo alikuwa na mke. Akalazimika kuufuta huku moyo ukimuuma.

    ****

    HATIMAYE baada ya mwezi mzima wa kujtengana na rafiki zake Asia alihitisha kikao cha dharula. Japo awali alitaka kuyamaliza mambo haya kimya kimya, lakini akajikuta harakati zake akimuhitaji mtoto wa kikurya Janeth, na wenzake wawili akiwemo Messi ambaye ni mtaalamu wa mipango.

    “Jamani nimekuwa kimya mwezi mzima, najua mmechonga sana ooh Asia anaringa, sijui nini……hayaaishi midomoni nyie watoto kama Janeth ulivyokuwa mpana kama magagulo ya wasomali sikuezi.” Akazungumza Asia kwa nyodo, kimya kikatanda kisha kama wameambizana akaanza kucheka Janeth, Messi ambaye jina lake halisi ni Husna akafuatia, mara Asia, mwishowe meza nzima wakawa wanacheka.

    “Imetosha sasa.” Aliwakatisha Asia.

    “Nimeleta kazi mezani.” Alisita akagida maji kisha akaendelea, “Messi unamkumbuka jamaa uliyekutana naye benki mwezi ule.”

    “Jamaa gani?” Husna akauliza.

    “Yule ambaye ulinipa namba ya simu.”

    “Eeeh nimemkumbuka vipi kwani?”

    “Mambo yameiva ni sisi tu kupakua.” Asia aliwashirikisha wote kwa pamoja.

    Akawasikiliza anasema nini.

    Akausikiliza ushauri wa Husna, haukuwa ushauri mzuri sana, ushauri wa kumuibia Deniss kadi ya benki na kwenda kuvuta pesa.

    “Hapana Messi hiyo mbaya…mi nataka ile ya kisasa mbona hiyo imekaa kinjaa njaa sana. Kama tunachuna mwanachuo banaaa.” Aligoma Asia.

    Janeth alikuwa kama hawasikilizi vile, lakini aliponyan yua kinywa na kusema neno mambo yakaonekana kua sawa. Akakubaliana na Janeth.

    Wakaagana huku wakiisubiri siku ya siku.

    Milioni kumi.

    Hazikuwa pesa ndogo. Isitoshe Asia hakuwa ametumia zaidi ya laki tano katika kufanikisha hili.

    SIKU IKAWADIA.

    ASIA alikuwa ameikalia vyema gari aina ya Harrier, alikuwa anaikanyaga vyema kana kwamba ni ya kwake.

    Ndani ya gari aikuwa yeye na Deniss, siku hiyo Asia aligoma kutumia gari ya Deniss alihitaji naye kumuendesha.

    “Mapenzi ya kihindi haya…” alijisemea Deniss wakati akikubaliana na Asia.

    “Au umechukia baby.” Asia alibembeleza kiwiziwizi.

    “Hamna jamani mbona sawa tu…” alijibu Deniss.

    Sasa alikuwa katika gari la Asia, ilikuwa ni saa sita mchana.

    “Tuanzie kwangu ama kwako.” Asia aliuliza ka kuridhika akia anaikanyaga gari kwa umakini.

    “Mh. Kwani we unachukua wapi?”

    “Standard chattered Posta kule.” Alijibu Asia.

    “Mimi Crdb yoyote tu…lakini huwa napendelea ya kule mtaa wa Lumumba. Hakuna foleni na uhakika wa pesa ndefu upo.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Pesa ndefu? Kwako pesa ndefu ni ipi? Hao CRDB walioshindwa kunipa ki milioni hamsini kwa wakati unasema wanatoa pesa ndefu? Benki za kibongo ushenzi tu…walinifanya nionekane mwongo mbele za watu ” alijibu Asia ka kuonyesha kukereka.

    Deniss, kimya aliogopa kujibu kitu maana kwake pesa ndefu alihesabia hiyo milioni kumi, kumbe mwenzake aliwahi kukosa ki-milioni hamsini.

    Ipi pesa ndefu sasa?.

    Deniss hakujua kama mfumo wa digitali hauhitaji kupandisha antenna juu ili kuondoa chenga chenga. Hakujua kama ni kuseti kidogo tu king’amuzi na mambo yanaenda sawa.

    Deniss naye alikuwa analojia.

    Wakalifikia ghorofa kubwa ambalo chini kuna benki ya Standard chattered…….

    “Tushuke basi si unajua kuna kukabwa……’ Asia akamsihi Deniss. Wakashuka.

    Ðeniss aliposhuka, asia akamfuata na kumnong’oneza kwa tahadhari.

    “Jiweke mbali kidogo si unajua tena wavimba macho, nisije nikatolewa magazetini nikaivunja ndoa.” Maneno yale yakamtia wivu mkali Deniss, Asia alihitaji sana hali ile.

    Akazama ndani ya benki Asia, akamwacha Deniss amekaa mbali kabisa akiwa hana habari na yule binti.

    Asia akajaza karatasi kadha wa kadha.

    Deniss akiwa amezubaa katika gazeti mara ukaingia ujumbe.

    “Njoo unisaidie.’ Mtumaji alikuwa Asia. Deniss akaangaza huku na kule akamwona, akasimama na kumfuata.

    “Nisaidie kujaza” Asia alisema kwa sauti ya kimahaba.

    Deniss akaanza kujaza.

    “Nitolee 45 kabisa. Nimekumbuka nina safari juma lijalo.” Asia alimpa maelekezo Dennis, Deniss akajaza milioni arobaini na tano kutoa.

    Asia akachukua ile karatasi akaenda dirishani.

    Akafanya tukio la sekunde kadhaa.

    Akabadili karatasi.

    Akamkabidhi yule dada aliyekuwa dirishani.

    Akamkabidhi na pesa kiasi cha shilingi elfu hamsini.

    Alikuwa anaweka katika akaunti ya Janeth.

    Aliporudishiwa ‘paying slip’ akafungua koba lake kwa mbwembwe akaweka ndani.

    Akatoa karatasi nyingine tena akamkabidhi yule muhudumu.

    Akaweka elfu thelathini katika akaunti ya Husna.

    Nayo kama ile ya awali akatia karatasi katika koba lake.

    Mchezo ulienda kama alivyotaka.

    Akasogea pembeni akazugazuga kisha akaondoka.

    “Twende zetu afisa.” Alimshtua Deniss.

    Wakatokomea.

    Walipoifikia zamu ya Deniss kutoa pesa ikazuka ile dhana ya wanaume wengi kupenda sifa mbele ya msichana hasahasa akiwa mrembo. Sifa hizi za kijinga huwatokea wanaume wengi puani, yaani hupenda kujionyesha kuwa wana pesa nyingi, kujidai kuwa hawajali hata pesa zao zikitumika hovyo.

    Lakini mwisho wa siku akilala kitandani anasema. NINGEJUA.

    Pepo hilo likamkaba Deniss pia.

    Akataka kujiweka daraja moja na Asia.

    “Na mimi njoo unisaidie.” Alijifanya kudeka.

    Asia ambaye katika filamu hii ni mke wa mbunge, akarembua jicho. Kisha akachukua kalamu.

    Alipofikia kiwango cha kutoa.

    “Nitolee kumi na tano kuna jambo nataka kufanya na hiyo tano.”

    Asia akacheka kidogo kisha akamjazia, moyoni akafurahia dau kupanda.

    Deniss akapanga foleni, baada ya nusu saa akarejea akia na bahasha yenye chapa ‘CRDB BANK’

    Ujazo wake ulikuwa wa kulidhisha.

    Asia akarukwa na mate mdomoni, lakini kama alivyoanza taratibu alitaka kumaliza hivyohivyo.

    Wakaondoka.

    “Yaani pesa bwana hicho hapo kimilioni kumi na tano eti….duuh.” alisema Asia huku akiingalia ile bahasha kwa dharau kiasi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Deniss hakujibu.

    Akiwa anaendesha mara simu ikaita.

    Akaegesha gari pembeni kidogo. Akapokea.

    Ilikuwa simu ya kuigiza kutoka kwa mmiliki wa kiwanja ambacho walikuwa wanaenda kununua.

    “Wakati mwingine nachukia kufanya biashara na wabongo.”

    “Kuna nini?”

    “Eti hadi saa kumi na mbili, sijui kuna mambo gani gani aaargh. Fuck” alighafirika.

    Deniss akaanza kushusha chini kihulka. Alifanya vile kama anafanya kwa mpenzi wake wa siku nyingi.

    “Baby…nahitaji kupumzika pliiz…..we have to go somewhere..we unadhani sasa hivi saa nane hadi ifike saa kumi na mbili ni leo…”

    Kauli hiyo ikamfurahisha Denny, akaikumbuka ile siku alipoonja tunda la mke wa mbunge.

    Kama alivyotaka Asia baada ya saa zima walikuwa ndani ya chumba wakila raha.

    Deniss kichwani akiamini kuwa ndani ya kile chumba kuna milioni hamsiniAsia ndiye aliyeijua hesabu sahihi.

    Asia Digitali akachezesha kiuno kwa umakini huku akicheza na muda, alimpa Deniss kitu roho inapenda akamzidishia makusudi viuno ili afikie lengo.

    Lengo la kumchosha.

    Kweli akachoka mwishowe akalala.

    Asia naye akazuga kulala.

    Akamshtua Denis saa kumi na mbili na nusu.

    Walikuwa wamechelewa.

    Wakajiandaa upesi wakatoweka.

    Asia akiwa ameukamata usukani.

    Wakapita hapa na pale.

    Foleni ikawa kikwazo Asia akaamua kupitia njia za panya, ni huku walipokutana na dhahama.

    Wakakutana na gari nyingine, hakuna aliyetaka kumpisha mwenzake.

    Kigiza kile kila mmoja akammulika mwenzake.

    Asia akaghafilika. Deniss akagundua hilo.

    Ama kwa hakika ukitaka mwanaume apigane basi mdharau mbele ya msichana.

    Deniss akashuka mbiombio kuwakabili wale walioziba njia.

    Asia naye akashuka.

    Akakutana na kimya cha hatari.

    Mara akazolewa mtama. Akatua chini kama mzigo alipojaribu kupiga kelele alikutana na mdomo wa bunduki.

    Kidogo Asia acheke kwa jinsi Deniss alivyokuwa anatetemeka lakini akaumbuka kuwa alikuwa katika kuigiza filamu.

    Hakutakiwa kucheka, akaendelea kulia.

    Mmoja kati ya watekaji akaiendea gari. Badala ya kupekua akaiwasha. Ikaunguruma kisha ikageuzwa na kupotea.

    Deniss alikuwa amejikojolea tayari.

    Watekaji walificha nyuso zao.

    Wawili walikuwa wanaume. Mmoja mwanamke.

    “Ole wako usimame.” Alipewa onyo Deniss aliyekuwa amelala chini.

    Asia kitambo alikuwa amejifanya kuzimia. Alikuwa ametulia tuli.

    Baada ya dakika kumi eneo lile lisilokuwa na nji za magari walikuwepo watu wawili, Asia na Deniss.

    Deniss alikuwa amepagawa.

    Lazima apagae, hakutegemea shambulizi hili, halafu mbaya zaidi wameondoka na gari la Asia na pesa zote......kizungumkuti

    Alijaribu kumwamsha Asia, hakuamka. Akamtikisa lakini hali ikawa vile vile.

    Deniss akaamua kujijali kwanza yeye, Asia baadaye, akatimua mbio kali.

    Kuna kichwa kilikuwa kimejibanza mahali kikisubiri jambo hilo litokee.

    “Amka wewe bwege kasepa.” Sauti tulivu ya Janeth maji ya shingo.

    Asia akainuka, akasahau viatu, pekupeku akajikongoja.

    Wakaikuta taksi inawasubiri.

    Wakatokomea.

    “Janeth wewe mbayaaaa.” Asia alimsifu mkurya yule.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati Deniss anachanja mbuga kuitafuta barabara aweze kupata daladala ya kumrudisha nyumbani.

    Asia alikuwa anasikilizia ladha mbaya ya vidonge vya majira alivyotoka kunywa muda mfupi baada ya kuzinduka kutoka katika kuzimia feki.

    “Bwege asije akawa amenitia mimba mtoto wa Razak mie.” Asia alibetua midomo na kuyasema hayo.

    Janeth hakuweza kumsikia alikuwa amejikita katika kutafuta ni namna gani simu aliyoikamata mkononi aina ya iPhone inafunguliwa aweze kutoa kadi ya Deniss na kuweka yak wake.

    “Mh Janeth ushajimilikisha mtoto weee.”

    “Si nilikwambiaga nataka iPhone si ndo hii au? Watanikomaje?” alijibu bila wasiwasi kana kwamba ni yeye aliyefanikisha Deniss kujiingiza mkenge.

    Asia hakuwa na neno, na roho ya kwanini hakubarikiwa nayo.

    ****

    Milioni kumi na tano mezani.

    Wale wanaume walioambatana na Janeth kwa ajili ya kuwateka akina Asia na kuondoka na gari, hawakutambua kama dili lilikua kubwa kiasi kile.

    Walipewa shilingi laki mbili wagawane.

    Habari yao ikaishia hapo.

    Mashujaa watatu wa kike walikuwa wanazikodolea macho pesa zile ambazo baada ya kuguswa na yule dada wa benki aliyemkabidhi Deniss basi hazikuwa zimeguswa tena.

    “Milioni kumi na tano hizo” Asia aliuvunja ukimya.

    “Hapa sasa tunatakiwa kumiliki gari yetu…..” Husna alidakia.

    “Na nyumba kubwa ya kupanga….” Aliongezea Janeth.

    “Mh…mna mahesabu nyie wadada……” Asia alichombeza kisha akacheka kidogo.

    Akamtazama Janeth kisha akamtazama Husna. Akafumba macho kidogo, akawafikiria jinsi walivyokuwa wa muhimu kwake wakati anaingia jijini Dar es salaam.

    Hakuwa na hili wala lile, japo walimwingiza katika biashara ya uchangudoa ambayo Mwanza alifanyishwa bila malipo.

    Hakika, hakuwa analipwa, kila mwanaume alijipitia kwa kumpa ahadi kedekede za kumtoa kimaisha.

    Asia alikuwa ni msanii wa maigizo anayechipukia.

    Kwa kuligundua hilo kila mdau wa mambo ya sanaa aliyesikiliza kilio cha Asia aliahidi kumkutanisha na wasanii wakubwa na wanaofahamika Tanzania.

    Huyu aliwambia ana namba ya JB, huyu akadai Johari wamesoma naye, mara mwingine akadai kuwa kama Kanumba asingekufa basi walikuwa wanakaribia kufanya naye filamu.

    Asia akadanganyika, akatekenywa akatekenyeka.

    Mwisho wakamvua vinguo vyake vya kishamba na kufanya yao kisha sanaa ya maigizo inaishia hapo. Wale wanaojuana na JB anakutana nao wakipiga debe katika magari ya kwenda Buhongwa na Nyegezi, na wale waliosoma na Johari anakutana nao vijiweni wakivuta bangi.

    Alikuwa amedanganywa.

    Jambo hili lilimtesa sana.

    Aliyafanya yote haya ya kuipigania sanaa ya maigizo na kuamini kuwa itamtoa kwa sababu akimtazama mama yake mzazi alikuwa hajiwezi kiuchumi na kama hiyo haitoshi alikuwa mgonjwa wa mara kwa mara.

    Asia muhitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi Nyegezi, kisha hakupata bahati ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza. Akapiga konde kuwa sanaa itamwokoa yeye na mama yake.

    Sanaa ikamfanya kuwa changudoa wa mkopo, asiyelipwa zaidi ya kupewa ahadi kedekede.

    Mwishowe ahadi hazitimizwi na mwili unatumika.

    Wasanii wa maigizo wapo Dar….Asia akaamua kutoroka na kukimbilia Dar.

    Ni huku alipokutana na mshikemshike wa kuitamani pepo kisha ufufukie Mwanza.

    Jasho, hofu, wasiwasi, mateso na chuki nichukie. Vyote vikawa vyake. Mara leo kikundi hiki cha sanaa, kesho kile mara leo alale kwa msanii huyu mchanga mara kesho afukuzwe.

    Hatimaye akakutana na Janeth. Walikutana katika kikundi kimoja cha sanaa, Janeth alikuwa amemsindikiza rafiki yake.

    Wakajikuta katika mazungumzo na Asia.

    Mwishowe akaenda kulala kwa Janeth siku hiyo.

    Huu ukawa mwisho wa sanaa ya maigizo, hatimaye wakaingia katika sanaa ya mapenzi ya wiziwizi. Ni huku alipomkuta Husna Messi.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Asia alikuwa na faida mbili katika tasnia hii, kwanza alikuwa ameuona mfumo wa analojia unavyotesa, na hakika ulimtesa sana Mwanza. Maongezi mengi kisha mwili wake unatumiwa.

    Akaamua kuubadilisha, ni yeye alitakiwa kuongea na kutenda sana kisha achume pesa. Hakuwa na haja na mwili wa mwanaume.

    Pili alikuwa muigizaji mbunifu. Hili lilimsaidia kuwa tofauti na wenzake. Alikuwa ni mwepesi wa kuunda maneno, mwepesi wa kutokwa machozi na mwepesi kujifanya hamu zimempanda amesisimka na anataka huduma.

    Asia akawa Asia digitali.

    Akakiri kimya kimya kuwa wawili hawa walikuwa msaada mkubwa sana kwake, japo si kihalali.

    “Mimi nahitaji milioni nne tu….nimtumie mama nyumbani.” Hatimaye Asia alisema neno baada ya kuwa amefumbua macho.

    Hakuna aliyepinga.

    “Halafu Asia….hebu ngoja nikiri kwamba wewe ni mtaalamu. Naomba unisaidie jambo moja. N ahitaji pesa ya mafuta ya gari letu.” Husna alizungumza.

    “Kivipi?”

    “Kuna kitoto changu kimoja huko Mwanza kina pesa pesa ni kianafunzi pale SAUT…..nahitaji kwenda kuchuma.”

    Asia akacheka sana na kujisikia fahari kukubalika namna ile.

    “Kwa hiyo hapo unataka nini labda Messi.”

    “Kadi yake ya benki niweze kuchomoa walau milioni hata mbili tu mi inanitosha.”

    Asia akapiga kimya muda mrefu kidogo, kisha akazinduka.

    “Huyo mwepesi, dozi yake hata buku tano haifiki na anatoa utakacho.” Alijibu.

    “Kivipi?”

    “Ngoja nikaifanyie majaribio hiyo njia yako kwa yule K-Matelefoni halafu nitakuambia cha kufanya.” Aliufunga mjadala Asia, Husna akangoja majibu.

    Pesa ikahesabiwa Asia akachukua milioni tano, nne ya kutuma nyumbani na moja ya kuhifadhi katika amana yake.

    Milioni kumi ikatulia kwa mdada wa kikurya, mrembo usoni katili moyoni. Janeth. Kila mmoja alimuamini.

    Biashara bora kupita zote tangu wahamie digitali.

    Wale wa analojia waliendelea kutanua mapaja kwa shilingi elfu tano kwa mshindo.

    ****

    Kelvin aliiona siku hii kuwa ya kipekee sana kwake.

    Tangu afumaniwe na Asia akiwa na msichana mwingine hakutegemea kama binti huyu anaweza kumtafuta kwenye simu tena.

    Mara ya mwisho walionana mtaa wa Agrey jijini Dar.

    Asia alimsalimia Kelvin kijuu juu na hakutaka kumsikiliza zaidi maana ubaya aliomfanyia Mwanza, licha ya Asia kumpenda haukuwa wa kusameheka.

    Mara ya pili Asia alimuna Kelvin katika luninga, alikuwa akilinadi duka lake la simu.

    Hakuwa Kelvin tena bali K-matelefoni.

    Asia akapuuzia.

    Sasa Asia si yule wa analojia tena. Yu katika digitali na anataka kukutana na Kelvin.

    Lengo si mapenzi bali mapenzi ya kidigitali.

    Kelvin akashtuka sana kumsikia Asia.

    Licha ya kwamba siku nyingi sana zilipita, lakini Kelvin aliikumbuka ile kadha ya kiuno cha Asia katika kitanda cha futi yoyote ile, na hata miguno yake sakafuni pia ilimkumbusha mbali.

    Akatamanika.

    Asia akanung’unika katika simu kisha akamkumbusha Kelvin kuwa siku hiyo ilikuwa tarehe kumi na nne, siku ya wapendanao.

    Kelvin akashtuka kwa furaha, kumbe Asia bado anampenda.

    “Mtoto nilimkuna vizuri hawezi kunisahau yule. Nilijua tu atarukaruka kwa mahanithi wa hapa mjini kisha atarejea kwangu.” K alikitapa kwa rafiki zake.

    “Vipi kuhusu Amina sasa akigundua.” Aliulizwa.

    “Amina ni Amina na Asia anabaki kuwa Asia, nilipotoka na Asia ni mbali jamani niacheni.” Kelvin alikuwa amepagawa.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye wakapanga kuwa pamoja na Asia siku hiyo ya wapendanao.

    “Lakini uelewe kuwa nafanya kwa kuwa nakupenda na nilikupenda sana, kwa sasa nina mchumba tunafanya kuiba usije ukanogewa.” Asia alimtumia ujumbe wa kumremba Kelvin.

    Kijana akaingia katika mtego.

    Sasa tatu usiku. Asia alikuwa yu na kanga moja pekee katika kikubwa cha kifahari katika hoteli yenye hadhi ya juu.

    Kelvin mapapara alikuwa anahaha, mara amtekenye mara vidole visafiri katika masikio.

    Kelvin alijaribu kuonyesha ujanja ambao kwa Asia yalikuwa marudio tu.

    “Ngoja nikaoge kwanza mpenzi wangu, mimi ni wako jamani. Haraka ya nini.” Asia akachombeza kisha akazama bafuni, akarejea baada ya dakika chache.

    “Na wewe kaoge.” Asia alimwambia K.

    Kosa alilolifanya K ni kukubali kwenda kuoga.

    Asia upesi akazama katika mkoba wake akaibuka na unga unga unaofanana na rangi ya matiti yake.

    Akajipaka katika matiti yote, akaufunga mkoba na kumngojea Kelvin.

    Mwanaume akarejea huku akiona aibu kwa jinsi taulo ilivyonyanyuka maeneo fulani, Asia akamcheka.

    K akamvamia.

    Asia akahamia katika maigizo. Akajirejesha digitali.

    Kama K alidhani amekutana na Asia muanalojia ambaye alikuwa akikubali kila kitu huku akitoa vilio vya mahaba vya hisia, basi alikuwa anajidanganya.

    “Baby…suck my breast….” Alilalamika Asia huku akiyakamata vyema ‘manyonyo’ yake.

    K akamrukia kama bwege vile au kama ndama anavyorukia maziwa ya mama yake.

    Akaanza kuyanyonya kwa ustadi mkubwa.

    Tatizo la kitandani ni moja. Yaani hata kitu utakachokilamba kikiwa kichungu, hakuna namna itakubidi umeze tu.

    Ukitema mpenzi atajishtukia kuwa umemuona mchafu.

    Wangapi wanalamba masikio machafu, wanajikausha na kumeza?

    Wangapi wanakosea njia badala ya kulala matiti wanalifikia kwapa. Nao wanajikausha.

    Na ni wangapi wakikuta chumvi imezidi ukali kunako wanameza hivyo hivyo.

    Kwani chumvi kitu gani??

    K- matelefoni naye akawa kama wanaume wenzake. AKAMEZA…..

    Mara mwendo wa kunyonya ukapungua.

    Akaanza kuongea lugha zisizoeleweka.

    Mara akatulia na kuanza kukoroma.

    Asia akamsukuma pembeni.

    Akasonya kisha akauendea mkoba tena.

    Akarejea na vijiko viwili vya kulia chakula.

    Akavikamata ipasavyo.

    Akaingia kazini.



    Asia akamsogelea Kelvin, akafumba macho yake kisha akaomba mbinu hiyo aliyofunzwa usukumani iweze kufanya kazi.

    Mbinu ambayo hutumiwa na wanafunzi wenye imani hiyo kufanya wizi ama kugundua siri kadhaa. Kwa wale wataalmu wa afya njia hii kwa usasa wanaaita ‘haipotenaizesheni’ hutumika hasahasa jeshini, mjeshi hata afiche siri vipi, mbele ya haipotenaizesheni hana ujanja.

    (Sifundishi zaidi ya hapa maana watu hawakawii kuifanyia kazi na kuwasumbua wenzao mitaani)

    Asia akagonganisha vijiko mara mbili katika sikio na Kelvin upande wa kulia, kisha akafanya hivyo katika sikio la kushoto.

    Kisha ukafuata utendaji.

    “Kelvin…Kelvin..” Asia akaita japo kwa uoga.

    Maajabu, Kelvin akiwa amefumba macho aliitika japo kizembezembe.

    “Mama yako anaitwa nani?”

    “Mama yangu anaitwa Monica.” Alijibu kama mtoto mdogo.

    “Unaishi wapi?”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naishi huko Temekeee Mokoroshini.”

    Asia akataka kucheka. Akajikaza, yale yalikuwa maajabu makubwa.

    “Una akaunti benki?”

    “Ndio ninayo akaunti.”

    “Wapi na wapi Kelvin?”

    “NBC, CRDB, na AZANIA.”

    “Wapi kuna pesa nyingi?”

    “CRDB kuna milioni nane.” Alijibu, Asia akafanya tabasamu.

    “Kadi ya CRDB ipo wapi?”

    “Kwenye suruali, mfuko wa nyuma kuna wallet ipo humo katikati.”

    “Namba za siri unazikumbuka?”

    “Ndio..”

    “Ni zipi?”

    “6798”

    Asia hakuwa na swali la ziada.

    Akafuata suruali. Kama yule bwege pale kitandani alivyotoa melekezo, naye akayafuata.

    “Mh…imani hizi??” alijisemea Asia wakati anakumbana na kadi ya benki. Ilikuwa mahali palipotajwa.

    Asia akaikwapua ile kadi na kuzamisha katika mkoba wake.

    Kisha akaibuka na mtandio, akakitanda kichwa chake.

    Kama vile anaigiza filamu ya mapigano huku yeye akiwa kinara akapiga hatua kadhaa akatoka nje.

    Uhakika wa usingizi kwa masaa zaidi ya matano kwa ‘doromee’ aliyomeza Kelvin katika matiti ya Asia ulimpa jeuri msichana yule.

    Akaufunga mlango.

    Akachikichia mtaani. Huku na huko akakutana na ‘ATM’ ya CRDB….akaingia ndani.

    Akabofya kama alivyoelekezwa na jamaa aliyepo usingizini.

    Mashine ikaunguruma.

    Ule uboreshaji wa kuweza kutoa hadi shilingi milioni moja kwa siku katika ATM ulikuwa faida kwa ASIA akachomoa milioni moja.

    Alipoitazama saa yake zilikuwa zimebakia dakika kumi saa sita usiku iweze kutimia, hii ilimaanisha kuwa ile inakuwa siku nyingine.

    Asia akzuga zuga hapa na pale, ikatimia saa sita akazama tena katika ATM akachomoa milioni moja nyingine.

    Akazisweka kibindoni milioni mbili ndani ya muda mfupi tu..na hapo alikuwa hajaugawa mwili wake.

    Baada ya zoezi kukamilika, msichana yule aliyejitanda baibui, alirejea katika chumba chake akamkuta Kelvin ametlia vilevile. Akairejesha kadi ya benki na kujirusha kitandani kama vile hakuna lililotokea.

    Akapitiwa na usingizi hadi alipoisikia mikono nikimpapasa majira ya saa kumi.

    Akajifanya kusisimka.

    Akampa kile alichotaka yule bwana K matelefoni.

    Asubuhi, supu ya maana ikaagizwa wakanywa kujipooza na uchovu.

    Asia akiigiza kuchoka kuliko K matelefoni.

    Wakati wa kuagana bwana Kelvin akamzawadia Asia nauli shilingi elfu hamsini.

    Asia akashukuru.

    Wakaagana.

    Maskini K Matelefoni aliishia kupewa picha ya mtu amejiziba sura.

    “Kamtafute huyu ndiye ulimpa kadi akakutolee pesa.” Benki walitoa tamko hilo hawakuwa na la kumsaidia kwa namna nyingine.

    Hata ‘RB’ aliyochukua pia alitakiwa kumtafuta mwizi wake mwenyewe.

    Wazo la kwamba alilishwa vitu na kuchezewa kamchezo zikamfanya asimuwaze Asia kama muhusika wake.naume asiyekuwa makini.

    Mbinu ile ambayo ilifanya kazi ipasavyo. Husna alipewa majibu naye akafunga safari kuelekea mjini Mwanza.

    Kwenda kumchuna mwanaume wake kidigitali.

    ****

    ASIA DIGITALI ATIA TIMU VYUONI.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya kuzipanda ngazi ndefu za ghorofa mbili, kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka, alizamisha mkono wake katika mkoba akatoka na kitambaa cha kujifutia jasho. Akajipangisa kidogo.

    Kwa kutumia simu yake ya mkononi akajitazama jinsi alivyokuwa amependeza.

    “Kumbe ukiwa na gari unakuwa na weupe mzuri hivi.” Alijisemea Asia, kisha akapiga hatua kadhaa hadi akaufikia mlango wa ofisi ambayo alikuwa anaihitaji katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

    “Department of Business Administration” palisomeka hivyo mlangoni.

    Asia akavuta kumbukumbu ya mambo ya msingi ya kuzungumza akiwa katika ofisi ile.

    Sauti yake nyororo iliyobeba kiingereza cha kuombea maji lakini kinachofanana na huenda kuzidi lafudhi ya mzungu kilimbeba.

    Asia akaugonga mlango, akaruhusiwa kuingia. Akapiga hatua kadhaa akauruhusu uso wake kutabasamu. Lile tabasamu linalowakosha wanaume wengi.

    Akaruhusiwa kuketi.

    Ndani ya ofisi hiyo alikuwemo muhusika mmoja ambaye aliweka mambo yake kando baada ya ujio wa Asia.

    “Karibu sana.”

    “Asante sana kaka, aah samahani sijui nd’o Mr. Lucas?” aliuliza kwa utafiti kiasi.

    “Yeah ni mimi. Umeagizwa kwangu.”

    “Offcoz nimekuja kwako, na ninashukuru kuwa sijapotea….walionielekeza hawajakose kabisa maelekezo yao.” Alijieleza kwa furaha Asia.

    “Karibu sana.”

    “Aaah labda niende moja kwa moja kwenye point yangu ya msingi. Ni kwamba naitwa Halima…na hii ni business card yangu unaweza kuipitia kwa kifupi, aah mimi kuna msaada ama kuna jambo nalihitaji sana kutoka kwako.”

    “Jambo gani dada.” Alihoji kwa utulivu Lucas.

    “Wewe ni mkufunzi katika chuo hiki, hasa hasa katika masomo ya biashara. Nahitaji uwe mwalimu wangu katika topiki kadha wa kadha….kwa kifupi nimeishia kidato cha sita, kuna mambo kadha wa kadha katika biashara yangu yanaanza kunizidia. Si unajua tena mambo ya kukimbia shule, sasa kama hautajali tunaweza kufanya hivyo.

    Muda wa kurejea shuleni sina kiukweli. Nahitaji tu kujua mambo kadhaa ndo maana nimekufata wewe moja kwa moja.” Alimaliza kuzungumza Asia huku funguo ya gari ikicheza katika kidole chake.

    Bwana Lucas akatulia kwa muda kama anayefanya tafakari.

    “Basi nadhani kwa kuwa nina kadi yako basi nitakupigia tutapanga, maana suala hilo lipo nje ya ajira yangu.” Alijibu huku akionyesha macho yanayompa tumaini Asia ambaye alijitambulisha kama Halima.

    “Ok basi hamna shaka nitaingojea simu yako kwa hamu kubwa. Utakuwa msaada mkubwa sana kwangu, ujue mambo ya final accounts sijui manini nini yananiumiza sana.” Alimaliza Asia huku akionyesha kuwa anajua vitu kadhaa.

    “Usijali mambo yote yatakuwa poa.”

    Waliagana, Asia akaondoka akiwa ametimiza azma moja ya kupata miadi kutoka kwa bwana Lucas.

    Hiyo ilikuwa hatua kubwa sana……

    ***ASIA amemjulia wapi bwana LUCAS na anataka kitu gani kwake???

    Je atafanikiwa kama alivyowaliza wengine……..



    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ITAENDELEA……….



0 comments:

Post a Comment

Blog