Search This Blog

Monday, October 24, 2022

JAMANI KAKA CHENI …NDIYO NINI SASA?! - 1

 





      IMEANDIKWA NA : GLOBAL PUBLISHERS





    *********************************************************************************



    Chombezo : Jamani Kaka Cheni … Ndiyo Nini Sasa?!

    Sehemu Ya Kwanza (1)





    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sijui nini kiliendelea, nilipitiwa na usingizi moja kwa moja na kuja kushtuka saa kumi usiku nikiwa napitisha kumbukumbu kichwani, nikakumbuka mara ya mwisho ilikuaje. Nikakumbuka nilifikia sehemu moja na kaka Cheni na mwanamke wake, nikakasirika sana.

    ***

    Asubuhi ilifika, kulikucha, nikatoka kufanya kazi za ndani uani huku nikiwa nalenga kuona kama yule mwanamke wa kaka Cheni aliondoka au alilala palepale. Nilifanya kazi kwa umakini wa macho. Muda mwingi nilikuwa nakazia macho mlangoni kwa kaka Cheni.

    Saa moja, kaka Cheni alifungua mlango wake. Akatoka yeye akiwa amevaa bukta nyeusi tu, juu alikuwa kifua wazi. Akakutana macho na mimi, akaachia tabasamu. Mimi nilihisi aibu, nikaangalia pembeni, moyoni nikasema; ‘kaka Cheni bwana’.

    “Mama ameamka?” aliniuliza.

    “Kaenda kwenye maji,” nilimjibu nikiendelea kuangalia pembeni.

    “Hujanijibu swali. Nimekuuliza mama ameamka, unajibu kaenda kwenye maji.”

    “Sasa kaka Cheni anaweza kwenda kwenye maji akiwa amelala?” nilimjibu ki hovyo maana hata yeye alijua kwa nini nilimjibu vile.

    “Yamekwisha…kwenye maji wapi?”

    “Kwa mama Tabu.”

    Kaka Cheni akarudi chumbani kwake. Nikajua kwa nini aliniuliza vile. Nikajua alilala na yule mwanamke wake sasa alitaka kujua alikoenda mama ili amtoe mwanamke wake.

    Baada ya dakika tatu, kaka Cheni alitoka akiwa amevaa traki suti, nyuma yake akafuatiwa na mwanamke. Jamani! Ninaposema mwanamke nieleweke kwamba ni mwanamke. Sijui kama Cheni alimpendea nini maana si saizi yake. Muwowowo huo, mpaka nikacheka mwenyewe moyoni.

    Nikasema loo!

    Akitembea sasa, mbengenyu… mbengenyu…mbengenyu. Hapo alikwenda chooni. Akiwa bado chooni, baba akatoka na kiti, akakaa nje…

    Nilimwona kaka Cheni akishtuka sana. Hata mimi nilishtuka kwani nilijua baba ameshakwenda kazini kwake, kumbe alikuwepo bwana.

    “Shikamoo baba,” kaka Cheni aliamkia huku wasiwasi wake ukiwa umegundulika na baba.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Marhaba.”

    Baba yetu alikuwa na tabia hiyo ya ajabu, ukimwamkia akiitikia hana cha kusema umeamkaje wala habari za leo! Hilo hata mama alikuwa akimshangaa.

    Mwenyewe msimamo wake ni kwamba, kumuuliza aliyekuamkia shikamoo umeamkaje ni kupoteza sauti kwani angekuwa ameamka vibaya asingeamkia shikamoo angeeleza ugonjwa wake au tatizo lake.

    Nilianza kutetemeka mimi badala ya kaka Cheni licha ya kwamba naye kaka Cheni hakuwa sawasawa hata kidogo.

    Ishu ilikuwa lile jimwanamke kutoka chooni. Kwani ilikuwa lazima kaka Cheni amfuate akamstopishe au aache atoke mwenyewe akumbane na baba, mzee wa Kingoni, mkali kama nini! Ukimwangalia tu hivi unajua mkali maana amefuga msitachi mrefuuu! Mpaka amekuwa kama yule mtu wa kwenye dawa ya kuchulia misuli.

    Ghafla kaka Cheni alikwenda chooni, akachukua kama dakika mbili, akatoka. Nilimwona akitoka jasho jembamba la woga. Nikajua leo kazi ipo. Wasiwasi wangu ulizidi zaidi pale nilipowaza itakuaje kama baba angeamua kwenda chooni baada ya kaka Cheni kutoka.

    Mara, nilisikia kitu kimeanguka sebuleni, baba akashtuka na kuingia ndani. Kaka Cheni akatoka mbio hadi chooni akatoka na jimwanamke lake akiwa amemshika mkono.

    Mbona ilikuwa kichekesho, mdada anavyokimbia na kaka Cheni anavyomkimbiza, miye mbavu sina!

    Walitokomea huko, baba alipotoka akakuta hakuna kitu!

    “Mwite kaka yako,” aliniamuru baba…

    “Katoka…”

    “Kaenda wapi?”

    “Nadhani yuko nyuma ya nyumba.”

    “Kamwite.”

    Nilizunguka nyuma ya nyumba lakini sikumwona kaka Cheni, nikampigia simu…

    “Baba anakuita.”

    Kaka Cheni alikata simu. Iliashiria kwamba, alielewa kwamba baba anamuita. Baada ya sekunde tu alitokea akiwa mbio.

    Cha ajabu ni kwamba, mambo aliyokuwa akiyafanya kaka Cheni pale nyumbani na ukali wa baba ni vitu viwili tofauti kabisa!

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Naam baba…”

    “Wewe usiku huwa unakuaga na nani chumbani kwako?”

    “Marafiki zangu baba…”

    “Mbona mchana siwaoni?”

    “Ha! Baba…mbona mchana pia wanakuja sana, muulize sista,” alisema kaka Cheni huku akinitupia macho mimi…

    “Ni kweli baba, marafiki zake huwa wanakuja hata mchana. Ila kwa usiku mimi sijawahi kuwaona.”

    “Mh! Huyu mara kwa mara usiku nikitoka kwenda chooni nawasikia wakiongea na wenzake.”

    “Ni marafiki zangu baba.”

    Moyoni nilisema baba ungejua wala usingeuliza. Huyo mwanao kazi yake kubwa ni wanawake kila siku.

    Basi, baba alionekana kukubaliana na maelezo ya kaka Cheni, akanyamaza. Mara akatokea mama akiwa na ndoo ya maji…

    “We Cheni,” mama aliita hata kabla ya kutua ndoo chini…

    “Naam…”

    “Yule mwanamke ulikuwa unampiga busu pale kwenye kona ni nani?”

    Nilimwona kaka Cheni akikunja sura na macho yakisinzia kama anayesema ‘ohooo! Kimenuka sasa!’

    “Namjua mama.”

    “Unamjulia wapi? Anakaa wapi?”

    “Mama yule anakaa kule kwa mzee Masumbuko…”

    “Wewe mtoto wewe! Usije ukaniletea wajukuu wasiokuwa na mpangilio hapa kwangu,” alisema mama kwa uso wenye hasira za kweli…

    “Kwani kumjua ndiyo kulikufanya umbusu?” hapo sasa aliingilia baba mwenyewe. Ilibidi kaka Cheni akae…

    “Kwanza ni mwanamke mtu mzima au?” aliuliza baba…

    “Ah! Anaonekana ni binti tu lakini ana mwili mkubwa sana. Mimi mwenyewe nilishangaa, nikaogopa maana walivyosimama utasema ni mtu na mtoto wake wa kiume,” mama alikoleza.

    Ajabu sana! Nilimwona baba akiachia tabasamu ambalo sijawahi kuliona hata siku moja. Nilivyomjua baba yangu, pale kaka Cheni asingekaa. Lakini pia moyoni nilisema kama baba angejua mwanamke anayesemwa alikuwa chooni wakati yeye amekaa kwenye kiti cha nje, pangechimbika kama siyo kufumka!

    Kutabasamu kwa baba, kulimpa nguvu kaka Cheni, naye akatabasamu lakini mama aliendelea kuwa siriasi. Akaingia ndani na kuendelea na mambo mengine…

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Hodi,” sauti ya msichana ilisikika kutoka nje ya geti dogo la uani ambalo lilikuwa wazi…

    “Nani? Pita,” nilisema mimi huku nikiwa nimetumbulia macho pale kwenye geti…

    Msichana wa umri wa kama miaka saba aliingia, anaitwa Mai…

    “Karibu Mai,” nilimkaribisha…

    “Asante…shikamoo babu,” yaani baba…

    “Shikamoo anko,” yaani kaka Cheni…

    “Anko, Mwanamaua anasema amesahau kitambaa chake cha kichwani chumbani kwako kitandani, kasema nipe nimpelekee ataulizwa na mama yake asiporudi nacho…halafu kasema hujamwambia usiku wa leo aje au asije maana simu yake ina matatizo ya chaja.”



    Nilimwona baba akitetemeka, akamkazia macho kaka Cheni, akasimama maana alikaa…

    “Cheni,” aliita mama akitoka ndani na si baba…

    “Abee…” kaka Cheni alichanganyikiwa, ilibidi aitike kama mwanamke, kama binti…

    “Bee nini? Bee wewe mwanamke?” mama alimjia juu…

    “Naam mama…”

    “Mwanamaua ni nani?” aliuliza baba akiwa bado amesimama…

    “Dada mmoja tunafahamiana.”

    “Kitambaa chake alichokisahu kimefikaje kitandani kwako?”

    “Alikuja jana jioni akakisahau alipotoka.”

    “Alikuja jana jioni hapa?”

    “Ndiyo baba.”

    “Kumbe wewe wanaokuja kwako si wanaume, ni wanawake siyo? Nikisikia umempa mtoto wa watu mimba, Cheni utanibeba bila mbeleko ya kijani,” alisema baba na kuingia ndani.

    Nje tukabaki mimi, mama na kaka Cheni mtuhumiwa. Mama akaanza…

    “Hivi we Cheni kwanza mimi naomba kukuuliza…wewe unafanya kazi gani usiku mpaka unashindashinda ndani mchana kutwa umelala?”

    “Sina kazi mama, sasa nitakwenda wapi?”

    “Ndiyo ushinde ndani umelala kitandani?” mama aliuliza tena, nikamwona kaka Cheni akinikazia macho mimi. Nikainamia chini kwa aibu…

    “Dada yako ndiyo anayekusaidia kulala ndani mchana kutwa? Maana naona unamwangalia,” alisema mama, ikabidi mimi nicheke kidogo.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kifupi maneno ya mama yaliashiria kwamba, hapendezwi na kitendo cha kaka Cheni kulala tuuu…mpaka giza linaingia ndiyo anatoka kwenda kutembea. Na hii ndiyo ilikuwa kawaida yake. Mbaya zaidi sasa, akitoka usiku kwenda kutembea, akirudi ndiyo amebebana na akina Mwanamaua, mara Consolata, mara Jemina yule mtoto wa mzee Ukawa.

    Wakati wote huo, yule mtoto aliyetumwa kitambaa alishaondoka nyumbani tena kwa kukimbia. Nadhani alipeleka taarifa kwa Mwanamaua kwamba kimenuka!

    Mama aliendelea na shughuli zake, baba akatoka kwenda zake wapi sijui. Kaka Cheni aliingia kuoga, alipotoka alivaa akaniaga anakwenda kuzurura, nikijua anayafanyia kazi maneno ya mama.

    Ilipita saa tatu, saa nne, saa tano, saa sita, saa saba, saa nane, kaka Cheni akanipigia simu…

    “Halo sista…”

    “Niambie my braza.”

    “Mmeshapika?”

    “Yes! Tumekuwekea chakula, mama amekwenda kwenye msiba wa mzee Timo.”

    “Dingi?”

    “Dingi hajarudi, lakini mama alisema naye atakwenda hukohuko msibani na watalala hukohuko leo.”

    Kaka Cheni alikata simu. Baada ya dakika kumi tu, akatokea. Safari hii alikuwa na msichana mwingine kabisa, mgeni machoni pangu.

    Kusema kweli hapo kaka Cheni akiamuaga kuchagua utamkubali. Huyu msichana aliumbika jamani! Kila sehemu ya mwili wake ilikuwa ya wastani. Wowowo la wastani. Miguu ya wastani, kiuno cha wastani, macho ya wastani. Kila kitu ni wastani. Nilipapenda zaidi kifuani pake. Palikuwa panalipa!

    “Suu, huyu ni sista ‘angu,” kaka Cheni alimtambulisha, akaniangalia mimi…

    “Sista huyu ni wifi yako wa ukweli kabisa.”

    “Hata mimi namwona, karibu wifi ‘angu,” nilimwambia.

    “Asante sana wifi.”

    Waliingia chumbani. Baada ya muda, kaka Cheni akanitumia meseji kwamba anaomba nimwingizie msosi wake ndani. Nikafanya hivyo.

    Kwa sababu nilikuwa sina kazi, baada ya kumwingizia chakula na maji ya kunawa na ya kunywa na matunda, niliingia chumbani kulala.

    Niliwasikia wakila huku wakizungumza mambo ya kimahaba zaidi. Wakati fulani niligundua kuwa, hapo Suu anamlisha kaka Cheni au hapo kaka Cheni anamlisha Suu.

    Sasa nikaja kubaini kuwa, wameshamaliza kula, wanachombezana, maana nilisikia Suu akisema…

    “Cheni nini bwana…subiri…aaa Cheni wewe…sasa huko nako nini?”

    Mara nikasikia ukimya tuliii. Halafu ghafla nikamsikia Suu akihema kwa kasi na kusema kimahaba, nikajua tayari.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nililala mlalo wa kuwaunga mkono, nikawa najipapasa na mimi katika kila hatua yao…nikafumba macho, nikafumbua, nikahisi giza, nikachezacheza kitandani.

    Mara, nikasikia simu ikiita, nikamsikia Suu akiongea…

    “Eee…nani? Kaanguka? Nakuja…nakuja sasa hivi,” alisema Suu na nikasikia kitanda kikilia, kuashiria anatoka kitandani. Nikachukia sana maana na mimi nilikuwa pazuri.

    Suu alifungua mlango huku akimwambia kaka Cheni…

    “Baby acha niende tu. Nitarudi baadaye…”



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog