Chombezo : Asia Digitali
Sehemu Ya Tano (5)
Laiti kama Branco angejua ni kwanini Asia anatabasamu kamwe asingemdhihaki na kumweka katika orodha ya wasichana wake.
Huenda alikuwa sawa kumweka katika orodha ya wanawake aliowapitia kama kawaida lakini tatizo lilikuwa moja tu.
Asia hakuwa katika mfumo wa analojia kama wanawake waliotangulia.
Kumtumia Asia lazima ulipie.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . . . . . . . . . ******
. . FARIDA alikuwa katika sebule yake kubwa, alikuwa akicheza cheza na mtoto wake wa mwisho.
Lakini hakuwa na furaha hata kidogo. Hali hii ilitokana na kujishtukia kuwa ameingizwa mjini kwa namna ya kipekee huku akiulaumu ujinga wake na visasi vya kipuuzi.
Farida aliamini kuwa Asia hakuwa na harakati zozote za kuweza kumkomoa Branco, mwanaume ambaye alimdhulumu furaha yake kwa kumtenda kimapenzi.
. . Farida alijutia pesa ambayo aliitoa na kumpatia Asia baada ya kuaminishwa na Husna kuwa pale ni mwisho wa matatizo.
Farida alijisonya mara kwa mara huku akibanwa na hasira. Wazo la kuwa Asia amekolea kwa Branco lilimuumiza kichwa sana, akajiona mpumbavu namba moja ambaye hajawahi kutokea duniani.
. . Pesa nimempa na bwana nimempa……aliwaza Farida.
Akainama kwa uchungu mkubwa, chozi likadondoka.
Kikataka kufuata kilio cha kwikwi lakini mlio wa ukasikika ukamkatisha.
. . Simu yake iliita, akaitazama…..hasira zikamzidi baada ya kugundua kuwa mpigaji ni Asia.
Aliamini kuwa zilikuwa ni longolongo tu. Alitamani kumtukana lakini nafsi ikamsihi ajishushe.
. . “Najishusha kwa mara ya mwisho….” Aliapa Farida kisha akapokea simu.
. . “Nipigiee sasa hivi…” Asia alisema kisha akakata simu.
Farida akajikuta anatokwa na tusi zito la nguoni. Yaani ampigie tena….
. . “Huyu Malaya huyu hanijui eeh hata kama tuliandikishana atazitema pesa zangu…yaani milionii…” alisema kwa sauti ya juu akiwa amehamakinika.
Akabofya namba akampigia Asia huku akijaribu kuidhibi hasira yake.
. . “Nambie shoga..” Asia alianza.
. . “Poa tu nipe ripoti..”
. . “Branco ulisema ana pesa nzuri eeh….”
. . “Ndio anazo kwani vipi…tuzungumze yetu aisee..” alisema kwa jazba.
. . “Sikia sasa nishamaliza yangu….lakini nataka kukusaidia jambo moja.”
. . “Jambo gani? Na umemfanyaje hadi unasema umemaliza yako..”
. . “Taarifa utazipata muda si mrefu….ninachotaka kukusaidia ni kurejesha pesa zako na ziada kama inabidi. Ukwapi sahivi….” Aliongea kwa furaha kubwa Asia.
Farida akajieleza mahali alipo. Bahati nzuri Asia alikuwa hayupo mbali sana.
. . “Nakuja muda si mrefu…”
. . Farida alipokata simu ambayo alikuwa amempigia Asia, hapohapo ikaingia simu kutoka kwa rafiki yake mwingine.
Akapokea upesi kumsikiliza. Hata kabla hajasema neno lolote. Mpigaji alianza kuzungumza.
. . “Mwenzangu Mungu ametulipia…..yaani huku mbona kitimtimu…”
. . “Nini mbona sikuelewi…”
. . “Branco shosti…”
. . “Amefanyaje Branco…”
. . “Amenatiana huku mbona kazi ipo huku….”
. . “Amenatiana kivipi?”
. . “Mwenzangu yaani hata mimi sijui…halafu ilivyo aibu yupo na mke wa mtu….ni aibu huku…”
. . Farida alikuwa katika fumbo hakujua nini kinaendelea, alishikwa na mshawasha, akataka kutimua mbio achukue usafiri kwenda kwa Branco lakini akakumbuka alikuwa na ahadi ya kuonana na Asia baada ya muda mfupi.
. . Hakika baada ya dakika kadhaa simu ya Asia iliingia, tayari alikuwa amefika eneo ambalo Farida alikuwa amemueleza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . Farida akatoka nje wakaonana.
. . Asia akamsimulia Farida juu ya tego la kisu na ala yake alilomuwekea.
. . Farida hakuelewa chochote. Maneno ya Asia pekee yalikuwa hayajitoshelezi. Wakaongozana kuelekea sehemu ya tukio.
. . Mwanzoni palikuwa na watu wachache lakini baada ya taarifa kusambaa hapakuwa hata na upenyo wa kuweza kuchungulia nini kinaendelea.
Farida alimtazama Asia kwa jicho la wizi wizi. Alishngaa sana aibu hii kuwa kubwa kiasi hicho.
. . Katu hakuwahi kutegemea kuwa ingekuwa namna ile.
. . “Huyu binti ni kiboko…” alikiri katika nafsi yake.
Baada ya muda kila mtu alikuwa macho juu juu kutazama nini kinatolewa katika nyumba ile.
Alikuwa ni Branco akiwa amenatiana na mke wa mtu.
Aibu ya karne. Farida hakuamini kabisa. Lakini kilichoonekana ndo hicho kilikuwa mbele yake.
. . Asia alimsogelea Farida kisha akamnong’oneza “ Nimalizie changu…”
Farida akatabasamu. Alikuwa amemkubali Asia kwa kila namna.
Akamkonyeza kidogo ishara ya kuwa hakuna kitakachoharibika.
. . . . . . . . . . ****
. . Asia alijitia kuwa jasiri sana mbele ya Farida lakini kwa hali halisi alikuwa ameshangazwa sana na utaalamu ule wa TEGO…..hakujua kama kuna imani kali kama zile zinaweza kufanya kazi katika maisha halisi.
Kile kisu ambacho alikiweka chini ya godoro kikiwa katika ala yake kilikuwa kimezua haya.
. . Asia anakumbuka kuwa sharti la kuwanasua wawili hawa ilikuwa ni kukichomoa kisu kutoka katika ala yake.
. . Hapa ghafla wazo la kibiashara likamuingia.
Nani wa kukichomoa kisu?
. . Farida alionekana kuridhika sana na aibu ambayo Branco alikuwa ameipata lakini hakukumbuka kuwa Asia alimweleza kuwa anaweza kujipatia pesa baada ya tego lile.
. . Asia akapiga akili ya upesi upesi. Akagundua kuwa ipo njia ya kumwingizia pesa nyingi zaidi tena bila jasho.
. . Ndege wawili kwa jiwe moja. Asia alijipa kichwa.
. . Akachukua simu akabofya namba fulani.
. . “Kamanda nataka kukuuzia ugomvi…”
. . “Shilingi ngapi msaghane.” Sauti ya mwanadada wa kikurya, Janeth ilijibu.
. . “MIlioni mbili, yako moja na yangu moja…aahh hapana milioni nne, yako mbili na yangu mbili” Asia alimjibu kwa uchangamfu huku akitweta.
. . “Wewe Asia acha zako…wewe…ugomvi gani huo.”
. . “Ugomvi wa amani…sikia tukutane posta nikupange tule pesa.”
. . “Poa.” Janeth alijibu.
. . . . . . . . . . ****
. . Janeth alijiandaa upesi, akaona kuchukua daladala ama taksi ni kupoteza wakati. Akachukua pikipiki.
. . Kona hapa na pale hatimaye wakafika posta.
. . Asia naye alikuwa amefika tayari.
Akamsimulia Janeth juu ya lile janga la kumwekea tego Branco, tego lililonasa baada ya Branco kuingiza mke wa mtu chumbani kwake kisha kutumia kitanda kilichowekewa tego…..
. . Tego likanasa, nao wakanatana.
. . “Wewe jifanye ndo mwenye lile tego, tafuta nafasi ya kusema na Branco kisha mtajie dau akiingia laini unaenda nyumbani kwake, cha kufanya ni kuchomoa kile kisu kutoka katika ala yake.
. . Mwisho wa mchezo.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . Mwanadada wa kikurya akaingia kazini.
Siku hiyohiyo baada ya hospitali kushindwa kuwasaidia Janeth akafanikiwa kuteta na Branco.
Kwa aibu kubwa Branco akakubaliana na Janeth. Akampa maelekezo rafiki yake. Akamsindikiza nyumbani kwa Branco.
. . Akapewa pesa yake, kisha akafanya kama alivyoelekezwa na Asia.
Amakweli digitali haina mfanowe.
Palepale kisu kilipotoka katika ala, jogoo wa Branco naye akatoka katika mwili wa mke wa mtu.
Maajabu.
. . Milioni nne kibindoni. Biashara ikaishia hapo.
Branco akatoweka mjini na hakujulikana ni wapi alipopotelea hata marafiki zake hawakujua ni wapi amekwenda.
. . Hayo hayakumuhusu Asia digitali maana yeye tayari alishamaliza yake.
. . . . . . . . . . ****
. . . . . . *********ASIA MATATANI.**********
. . HASSAN TEMBO, kijana machachali mzaramo wa asili. Mkazi wa jiji la Dar es salaam wilaya ya Temeke.
. . Jina lake lilikuwa midomoni mwa watu wengi sana, wakubwa kwa wadogo, wazee kwa vijana.
. . Sio utajiri wake wa ghafla tu uliomstaajabisha mshangaaji bali pia umri mdogo na umbo dogo la Hassan.
. . Hakuwa muumini safi wa dini ya kiislamu lakini kila ijumaa hakuwahi kukosa msikitini.
Utajiri wake ulikuja kama utani, kwanza alikuwa mvuvi. Mvuvi mdogo kupita wote.
Maisha yake yalikuwa ya kulala na kuamkia majini.
. . Hakuwa na mahali pa kujihifadhi. Baadaye akapata kazi ya kuwa anauza samaki za bwana mkubwa mwingine. Bwana huyu alimpatia mahali pa kulala.
. . Hassan akaacha rasmi maisha ya kuishi majini, lakini aliendelea kuwa na undugu na maji.
Hassan alikuwa anakutana na wadau wengi sana katika biashara ya kuuza samaki.
. . Kuna mteja ambaye kila siku alikuwa akitembelea bishara ya Hassan Tembo, cha ajabu hakuwa akinunua mkitu zaidi ya kupiga soga na Tembo, kwa jinsi siku zilivyozidi kwenda ndivyo walivyoonekana kuwa marafiki wakaribu zaidi. Hakuna aliyehoji ukaribu wao.
Kuna kipindi alipotea ghafla kwa majuma mawili. Alitoweka bila kumuaga bosi wake, na alikuwa hajakabidhi mahesabu ya siku hiyo. Hali hii ilizua sintofahamu, hakuna aliyekuwa anajua Tembo amepotelea wapi.
. . Bosi akaanza kumsaka bila mafanikio. Siku ambayo Hassan anaonekana tena pale feri yule bosi wa kihindi alipewa taarifa na wapambe wake akafika upesi akiwa na kikosi cha polisi watatu wakamtia Tembo nguvuni.
. . “Hii mwiji ondoka na pesa mingi sana..” muhindi akiwa amebadilika rangi ya uso na kuwa nyekundu alitoa karipio huku akitaka kumpiga Hassan kibao usoni. Polisi wakawahi kuepusha.
. . “Dogo pesa ya jamaa iko wapi?” polisi walimjuuliza Tembo Hassan.
. . “Muulizeni ni shilingi ngapi?” Tembo bila hofu aliwauliza wale askari ambao walikuwa wamemshika shati na suruali yake.
. . Umati wa watu ulikuwa unashuhudia tukio hilo. Wengi wao walikuwa wakimuhurumia Hassan Tembo kutokana na ucheshi wake aliokuwanao pia umri wake mdogo kuingia katika misukosuko hiyo lilikuwa jambo baya sana.
. . Walisikitika lakini nani wa kuweza kutoa walau shilingi yake kumuepusha na mkasa huo?
Hakuwepo…..
. . Muhindi akaanza kuhesabu vidole ili amuangushie mahesabu makubwa Hassan.
. . “Laki mbili na efu shirini..” muhindi akatoa mahesabu yake. Kila mkazi wa pale feri aliguna.
. . Mzigo aliokuwa anapewa Hassan Tembo kuuza haukuwa na thamani walau ya shilingi laki moja.
. . Miguno yao ilikuwa haina maana, polisi walingoja jibu la Hassankama anayo hiyo pesa alipe ama hatua ya kwenda mbele zaidi ichukuliwe.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . “Amesema laki mbili na nusu?” Hassan alisema kwa sauti tulivu sana. Kila aliyeujua umasikini na maisha magumui anayoyapitia Hassan alishangaa.
. . Polisi walimkamata vyema asiweze kukimbia.
. . “Ngoja nimpe pesa yake.” Hassan aliwaomba askari, nao bila hiana wakalegeza mikono yao.
. . Akapata upenyo wa kuzama mifukoni, akachomoka na kibahasha kidogo.
Akafungua akatoka na pesa za kitanzania mpya zilizofungwa katika mpangilio mzuri.
. . Akahesabu noti moja baada ya nyingine.
Akawakabidhi wake askari, nao wakahesabu.
. . “Ni laki tatu hii..” askari mmoja alidhani Tembo amekosea kuhesabu alimkumbusha. Wakati huu hawakuwa wamemshikiria. Pesa ililainisha mikono yao.
. . “Hiyo hamsini ya kwenu msijali.” Tembo aliwaambia, huku akitoweka.
Muhindi, askari na umati wote ulibaki ukistaajabu.
. . Mbwembwe za Tembo hazikuishia hapo. Akaendelea na kufuru pale feri. Akanunua meza kubwa ya kuuzia samaki, akaajiri watu.
. . Matumizi yake yalikuwa makubwa sana. Kila mtu aliyekuwanaye karibu alimfaidi.
Wapo waliosema kuwa alipata dhahabu kubwa tumboni mwa samaki, wapo waliosema kuwa alikuwa akimuibia sana yule muhindi.
Lakini aliwanyamazisha wote kwa pesa. Tembo atake nini akikose?
Rafiki yake na dereva wake kwa kipindi hicho, Nyamang’asa akampachika jina.
. . “Munyama mkubwa kamba fedha”
. . Jina likamkaa.
. . Akafupishwa na kuwa anaitwa Mnyama.
. . Jina lake la kuzaliwa likasahaulika.
. . Mnyama akawa mnyama kweli.
. . Kuhusu alipata wapi utajiri…alijua mwenyewe.
. . . . . . . . . . *****
. . SIFA kemkem kuhusu tabia njema ya Hassan kujitolea katika msikiti ambao huwa anasali mara kwa mara, zilipenya huku na kule na hatimaye zikamfikia kimwana machachali Husna. . . . . Akapeleleza huku na kule akapata nafasi ya kumuona kijana yule.
. . Huyu naye kama kawaida yake hakuweza kuzifanyia kazi bila uwepo wa Asia mdigitali.
Husna akazifikisha salamu zile kwa shoga yake.
. . Asia akazipokea katika namna ya kipekee. Lilikuwa ni dili jingine ambalo lingeendelea kuwapatia pesa ya kununua mafuta ya kuweka kwenye gari kila siku.
Kama ilivyo kawaida ya Asia, hakumwambia lolote Husna juu ya mipango ambayo ataitumia kumuingiza mkenge kijana yule.
. . Asia akapanga kuingia kazini ijumaa ya juma hilo.
. . Jua lilikuwa kali, kilammoja alifanya jitihada za kupambana na joto la jijini Dar es salaam.
Hekaheka za hapa na pale Kariakoo ziliufanya mji kuonekana mdogo sana.
Kanzu nyeupe na mabaibui meusi yalitapakaa huku na kule ishara ya sala ya ijumaa.
. . Asia naye alikuwemo katika hekaheka za siku hiyo.
. . Muda wa sala ulipowadia kila mtu alikuwa mahala pake akiswali.
. . Asia naye alikuwa mmoja kati ya waliojumuika kuswali katika msikiti ambao hajawahi kuswali hapo kabla.
. . Asia aliswali huku mahesabu yake yakienda sawa kabisa juu ya mipango yake madhubuti kichwani.
. . Muda wa swala ulipomalizika Asia alitoka nje ya msikiti.
. . Akaangaza macho huku na kule.
. . Aliyategea mawindo yake yaweze kunasa.
. . Hatua kwa hatua Asia alijitembeza, kwa kasi huku akipigia mahesabu makali ya tukio ambalo litatokea.
. . Asia alikuwa akimtazama mwanaume mfupi mweusi ambaye huenda alikuwa amependeza kuliko wote ndani ya kanzu yake yenye thamani ya juu.
Asia alimtazama jinsi alivyokuwa amejikita katika kutumia simu yake. Asia akatumia upenyo ule.
. . Akajipitisha mbele yake, bwana yule pasipokumwona Asia akajikuta amemkanyaga. Asia akajilegeza akatua chini.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . Aliyemgonga alikuwa ni Hassan Tembo, Munyama mukubwa kamba fedha.
Hassan alikuwa anajulikana sana, asingeweza kumkimbia Asia ama kumpuuzia, aliheshimika kutokana na moyo wake wa kujitolea.
. . Tukio la Asia akalitumia kama nafasi nyingine ya kuthibitisha kuwa ana pesa.
Akaamuru apelekwe katika gari lake binti yule.
Wafuasi wakambeba Asia hadi ndani ya gari la Tembo.
. . Akisindikizwa na wanaume wawili Hassan alimchukua Asia hadi katika hospitali ya watu binafsi maeneo ya mnazi mmoja.
Hapa sasa hakuwahitaji wale watu tena, akabaki peke yake.
. . Hassan baada ya kuelezwa kuwa binti yule hakuwa amepata majeraha makubwa sana aliamua kuondoka naye aweze kumrejesha nyumbani.
Wakiwa ndani ya gari Hassan Tembo akakumbuka kuwa siku hiyo hakuwa ametimiza kile ambacho alikuwa akikitumikia.
. . Dini ya shetani.
Hassan alitakiwa kumwongezea wafuasi shetani. Na wafuasi waliokuwa wakihitajika ni wasichana.
. . Hassan alitakiwa kuwa anawaingiza wasichana katika utumwa ambao utawaweka dhambini.
Tayari alikuwa amewavuruga wasichana wapatao sita. Wasichana hawa sita kadri walivyokuwa nao wanaunda cheni kubwa zaidi ndivyo Tembo alivyozidi kutajirika.
Hii iliitwa biashara ya mtandao ambayo Tembo alijiunga ili aweze kujikwamua kutoka katika umasikini.
. . Mitindo yake ya kizaramo, ujanja katika mapenzi ulimuwezesha kuwakamata wasichana wengi sana.
. . Sasa aliona hata Asia alikuwa msichana sahihi sana kwake.
. . “Binti..unaishi wapi kwani?” Tembo alivunja ukimya.
. . “Mbagala rangi tatu..” Asia alidanganya.
. . “Ok..naomba tupite mahali nimesahau kifaa changu halafu nikupeleke nyumbani.” Tembo akaingiza ujanja.
. . Asia hakupinga, kwani hata yeye alikuwa anataka Tembo ajilengeshe aweze kumtapeli kidigitali.
. . Tembo aliendesha gari hadi akaifikia hoteli maarufu na ghali mitaa ya Kinondoni.
Akamuacha Asia garini, upesi upesi Tembo akachukua chumba.
. . Akamwendea Asia garini.
. . Akamsihi wapate chakula kabisa. Asia hakupinga akakubali.
Moyoni kila mmoja alikuwa akifurahia kuwa na mwenzake zaidi na
zaidi.
. . Kila mmoja alikuwa akiwaza la kwake lakini lililofanana na la mwenzake. Asia alikuwa akiwaza namna ambavyo atamuingiza mkenge Hassan Tembo na kisha kujipatia pesa za bwelele, Hassan Tembo naye alikuwa akiwaza na kuwazua namna ambavyo atamtumia Asia kupata pesa nyingi zaidi.
. . Kila mmoja alikuwa kidigitali zaidi. Pagumu hapo…
. . Tembo hakuwa na wasiwasi kuhusu kufanikiwa kwake kwani alikuwa anaamini kuwa yupo ambaye alikuwa akifanya kzi badala yake.
. . Asia alilazimika kutumia akili zaidi.
. . Baada ya kupata chakula Tembo nd’o alizuga kukumbuka kitu ambacho alikuwa amekisahau katika chumba kimojawapo katika hoteli hiyo.
. . “Vipi nikusindikize?” Asia aliingiza ujanja wake. Tembo akafurahia ombi lile.
Asia digitali na Hassan Tembo wakaongozana hadi chumbani.
Kama ilivyokawaida ya Asia akazuga hapa na pale mara ajikalishe vibaya.
Tembo akatabasamu kisha akafanya kitendo cha ghafla ambacho Asia hakukiona lakini taratibu hali ikabadilika.
. . Matiti ya Asia yakaanza kumwasha taratibu, akayakuna kidogo. Mara yakaendelea kumwasha tena.
. . Hali hii ikamshangaza kidogo, muwasho huu ulikuwa wa aina yake. Haukuwa katika namna ya kukera lakini ulikuwa wa kusisimua.
. . Asia anasisimka? Maajabu.
Matiti yakaendelea kuwasha kwa fujo.
. . Asia sasa alikuwa anamuhitaji mkunaji.
. . Nani zaidi ya Tembo?
. . Tembo alielewa ni nini kinaendelea. Alimsikitikia sana Asia kwani alikuwa anaenda kuingizwa katika mtiririko wa aina yake ambao unamaana moja tu. Kumtumikia shetani.
Ni kweli Asia alikuwa amemtumikia shetani kwa kipindi kirefu, lakini hii ya sasa ilikuwa ni utumikiaji wa kilazima.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . Tembo alikuwa anamuingiza katika ajira mbaya.
Asia akiwa pale kitandani jicho limemlegea hakuelewa ni nini kinaendelea lakini hakika alikuwa anahitaji huduma kutoka kwa Tembo.
Hassan Tembo akajawa na huruma akamvagaa Asia pale kitandani.
. . Kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa Asia alikuwa akifurahia penzi. Hisia zilikuwa juu mno na alionyesha ushirikiano wa hali ya juu.
Wazo la kutumia upenyo ule kumwibia Tembo lilipotea, Asia alikuwa katika dunia nyingine.
. . Laiti kama Asia angekuwa anamtambua Tembo vizuri, asingethubutu kujiingiza katika jaribio la kumdhulumu.
. . Tembo alikuwa mwanaume kama wanaume wengine kwa sababu anavaa suruali kama wengine lakini Tembo hakuwa mwanaume wa kawaida.
Alikuwa anasambaza ajira ya kutoka kuzimu. Ajira ya kumtumikia shetani.
. . Baada ya tendo Asia alikuwa amechangamka sana. Alikuwa amepata faraja ya mwili wake.
Asia akaijiwa na wazo la kuzungumza zaidi na Tembo ikiwezekana wawe wapenzi.
Akapanga kusema haya kwa Tembo baadate wakiachana.
. . Tembo kama alivyoahidi alimwendesha Asia hadi Mbagala akamwacha kituo kikuu. Wakapeana namba na kuagana. Asia akiwa anashangaa Tembo ni mwanaume wa aina gani hadi ameweza kumpagawisha namna ile.
. . Siku iliyofuata kizungumkuti kikaanza.
. . Asia akiwa peke yake chumbani, alianza kupatwa na hisia za maajabu.
Zile hisia za kuwashwa matiti na kupata hamu ya kufanya ngono.
. . Asia alizipuuzia lakini mara zikaendelea kumnyanyasa. Asia alihitaji kukunwa, lakini mkunaji angetoka wapi?
. . Mkusanya uchafu alisikika akiugonga mlango wa Asia. Kinyume na siku zote Asia alimkaribisha ndani. Mkusanya uchafu akaingia, Asia akafika hadi sebuleni akiwa na kanga moja.
. . Mkusanya uchafu akashangaa lakini hakuweza kufumba macho. Alibaki katika mduwao wake katika sekunde kadhaa. Asia hakumruhusu aendelee kuduwaa akaiangusha ile kanga chini sasa alibaki mtupu, cheni ya dhahabu ikiking’arisha kiuno chake. Mzoa uchafu alikodoa macho asijue nini cha kufanya!!!
. . Asia alikuwa katika mateso makubwa.
. . Mzoa uchafu akiwa anakodoa macho Asia akamrukia pale alipokuwa.
. . Mkusanya uchafu akaona hii ilikuwa nafasi ya kipekee ya kutuliza hamu zake. Akamvamia Asia kwa nguvu kama wanaoshindana katika hilo kila mmoja akitaka kuwa mjuzi kuliko mwenzake.
. . Kilichofuata Asia hawezi kukisimulia zilikuwa ni raha za kipekee. Walishindana, Asia akikizungusha kiuno chake kwa bidii zote, mzoa uchafu naye akionyesha ujuzi mchanga aliokuwanao.
Baada ya tendo Asia akakimbia chumbani kwa aibu kubwa. Mkusanya uchafu akaondoka zake huku akistaajabu nini kimetokea. Ilikuwa kama muujiza tu katika jumba la asia. Mzoa uchafu akahisi labda Asia alipandwa na majini na kujimuta akifanya kile alichokifanya.
Lakini kama ni majini ama la! Yeye haikumuhusu, aliambulia raha!!
Huu haukuwa mwisho wa sintofahamu ile!!
. . Hali hii ya utumwa iliendelea tena siku nyingine.
Siku hii mwili wa Asia ukawa mali ya ‘Mr. kucha’…….
Ugonjwa ulimuanza punde baada ya Mr Kucha kuanza kumsafisha miguu yake tayari kwa kumsafisha kucha na hatimaye kumpa rangi, Asia alikuwa akijiandaa kwa mtoko usiku huo!!
Lile janga la mzoa uchafu alikuwa ameamua kulipuuza na kuiita ajali tu!!
Mikono ya Mr Kucha ikaleta msisimko fulani ambao ulikuwa unatambaa, ulianzia kidoleni, ukayasisimua mapaja na hatimaye ukafanya utekenyo katika kitovu na matiti yake. Msisimko ule ukasafiri na kutawala mgongo wake.
Naam!! Yaleyale yalikuwa yamejirudia, Asia alikuwa kama anayepapaswa nma mwanaume mtaalamu katika Nyanja hizi ajuaye nini maana ya kumwandaa msichana.
Zile chuchu zilizokuwa zinawashwa akatamani kuzibugia na kuzinyonya huenda muwasho ule utapungua. Lakini zilikuwa wima sana hata asingeweza kuzilamba. Bila shaka alihitaji mtu wa kuzilamba.,
Nani sasa katika mazingira hayo!!
Hakuna mwingine zaidi yam r kucha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Katika siku za nyuma bwana huyo alikuwa amejaribu mara kadhaa kurusha ndoano kwa asia lakini hakufanikiwa kwa sababu Asia alikuwa kibiashara na hakuona huyo msafisha kucha atamnufaisha kwa lipi.
Labda kumsafisha kucha bure!!!
Sasa yule aliyepuuzwa leo hii thamani yake inaonekana.
Asia akaanza kuguna kimahaba kila Mr Kucha alivyokuwa akimpapasa mguu wake wakati anausafisha.
Miguno ikayafikia masikio ya Mr Kucha, akajiongeza.
Badala ya kusafisha kucha mikono yake ikatambaa hadi mapajani!!!
Asia kimya!!
Akaongeza akaifikisha katika….katika…..mgongo wa Asia.
Bado Asia kimya akizidi kuhema kwa nguvu!!
Mr Kucha akaondolewa uoga baada ya Asia kupitisha mikono yake na kuufungua mkanda wa suruali yake!!
Akajiongeza maradufu akamsaidia kuivua!!
Waa!!! Wote wakawa uchi wa mnyama!!
Tatizo Mr Kucha alikuwa na usongo.
Akapaparuka kwa pupa zote.
Afadhali Mzoa uchafu alikidhi haja za asia, Mr Kucha hovyoooo!!
Akamwacha Asia hoi zaidi ya awali!!! Akabaki kujifinyafinya mwenyewe.
Alitia huruma kumtazama!!
“Jamani Tembooo!!” alilalamika Asia akikumbuka mikito ya mtoto wa kizaramo.
. . Hii nayo ikapita.
Asia hakuwa kibiashara tena bali alikuwa analiwa bure tena alikuwa akipata faraja ya hali ya juu.
. . Asia yule wa digitali akajikuta amewingizwa mkenge. Sasa akawa mfuasi wa mapenzi. Tena bora yangekuwa mapenzi.
Ngono!! Alikuwa mfuasi wa ngono!!!
Hakujua kama mapenzi hayo alipachikwa na Hassan Tembo ili amsaidie kuongeza idadi ya waumini katika kontena lake la kishetani.
Kila muumini mpya mmoja, pesa ya Tembo ilikuwa inaongezeka.
Asia hadi kufikia wakati huo alikuwa amevuta wateja wapya sita na alikuwa anaendelea kuvuta wengine.
. . Fedheha na aibu zikamtawala na kumpelekesha Asia, akajikuta katika maamuzi mabaya sana.
Maamuzi ya kukataa kurejea alipotoka.
. . Asia alikuwa mfuasi wa mapenzi hapo zamani, alikuwa akipenda amependa kweli lakini baadaye akayageuza mapenzi hayo kuwa biashara. Akapata pesa nzuri. Lakini tangu akutane na Hassan Tembo basi mambo yakabadilika, hazikuwa zikipita siku tatu, Asia alikuwa anahitaji mwanaume wa kukidhi haja zake.
. . Alikuwa anawashwa sana matiti yake, ni mwanaume pekee alihitajika kwa ajili ya kumkuna.
Kila alivyokunwa akajikuta akitoa na utupu wake.
Hii kwake ilikuwa dharau isiyostahimilika.
. . Asia akaamua kwenda kwa waganga wa kienyeji. Hawa nao wakamtaka kimapenzi.
Akawapa huduma bila mafanikio.
. . Baadhi ya waganga wakampa maelekezo kuwa kila anapowashwa awe anawatembelea wampe tiba. Huu akaona ni upuuzi.
. . Waganga wa jadi hawakumsaidia chochote.
. . Hospitali napo walisema lugha zao ngumu ambazo Asia hakuzielewa, wakampatia vidonge lakini bado hali ikawa tete.baadhi ya madaktari nao wakaonja ladha ya tunda jekundu la Asia.
Hamu kwa Asia ikadumu. Na alipoipata haikupoa hadi pale alipopata wa kumpooza. Leo akipoozwa na huyu kesho anapoozwa na yule.
. . Wanaume wakahadithiana na sasa wakawa wanamlia ‘taiming’ akiwashwa wamkune.
Hali hii ikamdhoofisha Asia. Na kumweka katika hali ya kukata tamaa.
Hakuwa mchakarikaji tena. Hakuwa kidigitali tena.
Asia hakungoja ukurasa huu ujifunge wenyewe akaamua kuufunga kwa nguvu.
. . Ilikuwa siku kama siku nyingine, wanaume kadhaa walikuwa wakiranda randa jirani na nyumba ya Asia wakingoja akumbwe na pepo muwasho waweze kujilia vya bure.
Walingoja sana kwa siku hiyo lakini hapakujiri chochote. Hali ambayo iliwakera sana, kwani waliufanya mwili ule kama mali yao halali.
. . Wengine waliendelea kuvuta subira hadi usiku lakini cha kustaajabisha Asia hakusikika walau kujishughulisha katika chumba chake.
Ajabu na kweli. Au kapona??
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
. . Siku nzima bila kutoka kitandani.
. . Wanaume wenye uchu wakaamua kuingia ndani, kutazama kulikoni.
. . Wakatumia tochi zilizo katika simu zao.
. . Wakapekua huku na kule, hawakuona mtu.
Mwisho wakalifikia jiko.
Ni huku walipoukuta mwili wa Asia ukiwa unaning’inia juu ukipewa msaada na kipande cha kanga kilichofungwa vyema na kuunganisha kiwiliwili chake na mbao juu ya dari.
Ulimi nje.
Asia hakuwa hai tena. Alikuwa ameamua kujiua
. . Alizaliwa kianalojia akaishi kidigitali na hatimaye anakufa kianalojia akiwa na upande wa kanga shingoni kwake, ulimi nje. Miguu ikining’inia.
. . Wale waliokuwa marafiki zake walikana kumjua. Wale walioshiriki naye kuzitumia pesa alizochuma kidigitali wote wakajiweka mbali na mwili ule.
Serikali ikachukua maamuzi baada ya kutangaza na ndugu kukosekana.
Asia akazikwa na serikali.
Huu ukawa mwisho wa simulizi yake ya maisha.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MWISHO.....................
0 comments:
Post a Comment