Chombezo : Ladha Ya Tunda Bivu
Sehemu Ya Tano (5)
SIYAJALI alimtazama kidogo na kutikisa kichwa akionesha kukubaliana na kauli yake.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kwa hiyo naomba kwa leo nikuache dada' angu,” Linda aliendelea. Mara akawatazama wale wanawake wengine na kurusha swali lililoonekana kuhitaji jibu kutoka kwao. “Utaratibu wa mazishi ukoje?”
Mmoja wa wale wanawake alinyanyua mabega na kuyashusha. “Kwa kweli mambo hayo yatajulikana hiyohiyo kesho,” hatimaye alijibu.
Linda alimgeukia Siyajali na kumpa mkono. Kisha akafungua mkoba na kutoa shilingi 20,000. Akampatia Siyajali huku akisema, “ Pumzika dada. Kesho nitakuja asubuhi.”
“Asante,” sauti dhaifu ya Siyajali iliyafikia masikio ya Linda kwa usahihi.
**********
FRANK aliendelea kujilaza kitandani, chumbani mwa Catherine akiwa hana wasiwasi wowote. Aliitwaa simu yake na kuanza kusoma baadhi ya meseji ambazo alimwandikia na alizoandikiwa na Linda; meseji za mapenzi. Kwa kiasi fulani akajiona ni mwenye hatia na anatenda usaliti mkubwa kwa hatua hii aliyofikia. Hakujitofautisha na kiberenge mkomavu.
Alitambua fika kuwa Linda alikuwa akimpenda sana. Na alionyesha upendo huo kwa maneno na vitendo. Je, kama atatambua kuwa kuna mchezo mchafu unaofanyika kati yao, atajisikiaje, na atachukua hatua gani? Lakini atajuaje? Nani atamwambia?
Kama hadi leo hajajua, basi hatajua, Frank alijisemea kimoyomoyo. Aliamini hivyo kwa kuwa ilikwishatimu saa 4 usiku, muda ambao ni vigumu kwa Linda kuaga huko msibani kuwa anarudi nyumbani. ‘Kwa vyovyote vile hawatanielewa, kwa mara nyingine aliwaza.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akashusha pumzi ndefu na kuiweka simu kwenye kistuli. Akanyanyuka na kuanza kuvua nguo kisha akarudi kitandani na kujitupa kivivu-vivu. Kwa siku hii, na usiku huu alitaka ajisikie huru zaidi kuwa na mrembo Catherine. Aifurahie siku hii na aufurahie usiku huu.
Wakati akiendelea kumsubiri Catherine, alizirejesha kumbukumbu kwa Linda. Akawa akimlinganisha na Catherine.
Linda hakuwa mrefu, hakuwa mfupi; hakuwa mnene wala mwembamba. lakini aliumbika kwa namna inayoweza kumvutia mwanamume yeyote mpenda wanawake wazuri. Alijaaliwa maarifa mengi na pumzi ya kutosha kila walipohitaji kuistarehesha miili yao.
Kwa jumla alikuwa ni mwanamke mwenye mvuto hadharani na anayejua nini cha kumfanyia mwanamume ampendaye wanapokuwa sirini.
Catherine alikuwa tofauti. Kwanza alikuwa na umri mdogo. Mwili wake ulikuwa ukizidi kubadilika siku hadi siku. Unene ulimwandama kwa nguvu kiasi cha kuashiria kuupoteza ule uzuri ambao baadhi ya wanaume huupenda, uzuri wa umbo lililogawanyika; hapa pamejaa na hapa pamenywea.
Tofauti na Linda ambaye alikuwa mtundu sana kabla na wakati wa burudani halisi, Catherine alikuwa na umbumbumbu wa kiasi chake. Hata hivyo, kwa Frank, kama ilivyo hulka ya wanaume wengi, yeye alijisikia ‘kubadili mboga’ na kupata walao ladha tofauti, ladha ya tunda bivu, ladha kutoka kwa mwanamke mpya, itakayomsisimua na kumhamasisha.
Ni hilo lililomfanya ajikute akiliiba penzi lake kwa huyu mfanyakazi wa Linda. Alikwishaionja asali, sasa alitaka kuchonga mzinga!
Akiwa bado anawawazia wanawake hao, mara mlango wa chumbani humo ukafunguliwa. Akashtuka na kumtazama aingiaye. Pamoja na kujenga imani kuwa Linda hatarudi usiku huo kutokana na mazingira ya Kigogo na Magomeni yalivyo usiku, na pia kwa kuzingatia uzito wa msiba aliokwenda kuhani, hata hivyo bado hakujiamini, na hakutaka kuipa asilimia mia moja imani yake.
Akakodoa macho mlangoni hapo bila ya kupepesa. Hata hivyo hakuwa Linda aliyeingia, alikuwa ni Catherine. Ndiyo, ni Catherine ambaye tofauti na wakati walipokutana kule dukani, sasa alionekana kupendeza zaidi ndani ya kanga, vazi pekee lililouhifadhi mwili wake mnene na teketeke.
Mwili ukamsisimka Frank kadri alivyozidi kumtazama. Akanyanyuka na kumkumbatia. Miili yao ikagusana, kila mmoja akilihisi joto na mapigo ya moyo wa mwenzake. Kila mmoja akawa mbali zaidi kifikra, akihitaji hatua nyingine muhimu iliyokuwa mahususi kwao.
Hawakuwa na wasiwasi wowote, waliamini kuwa hakuna chochote kitakachoingilia starehe yao. Dakika chache baadaye wakawa katika hatua nyingine muhimu kwao. Wakaishughulisha miili yao kwa namna waliyotaka, staili hizi na zile zikipewa kipaumbele huku kila mmoja akiropoka ovyo, uropokaji uliokuwa ukizidi kumhamasisha mwenzake.
**********
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
KUTOKANA na afya yake kubadilika ghafla, na kwa kuzingatia mazingira ya eneo la Magomeni Mikumi yalivyomtia shaka, Linda alijua kuwa ilimlazimu kutumia usafiri wa teksi au pikipiki ili aweze kufika nyumbani kwake salama.
Alihisi viungo vikimuuma, hali iliyomfanya ajenge imani kuwa alikumbwa na malaria. Hivyo alitambua kuwa hakupaswa kutembea umbali mkubwa hadi katika Barabara ya Kawawa, kule jirani na Kanisa Katoliki Parokia ya Mashahidi wa Uganda, kwenye kituo cha daladala cha Morocco. Kwa umbali ule ambao ingemlazimu kutumia zaidi ya dakika ishirini, aliamini kuwa kufanya hivyo itakuwa ni kuutesa zaidi mwili wake.
Jambo jingine ambalo lilimfanya alazimike kuchukua teksi au pikipiki ni kutokana na mazingira ya eneo hilo. Kutoka hapo kwao marehemu Mwajuma hadi kufika huko kituo cha daladala, kwa usiku huo wa saa 3 kuelekea saa 4, ilikuwa ni kama vile kuwapa chakula vibaka. Kulikuwa na taarifa za mara kwa mara kuwa eneo hilo hutumiwa sana na vibaka kuwapora watu pesa, simu na kadhalika nyakati za usiku hususan kinamama.
Hivyo mara tu alipotoka ndani ya nyumba hiyo alimwita kijana mmoja na kumwagiza amtafutie teksi. Hakutaka kutumia pikipiki maarufu kama ‘bodaboda’ kwa kuwa alikosa imani ya usalama safarini. Alishashuhudia mara kadhaa ajali ambazo aliamini kuwa zilitokana na uzembe wa madereva wa pikipiki hizo kutokana na haraka zao. Na ajali hizo mara nyingi zilikuwa zikiyapoteza maisha ya dereva na abiria papohapo!
Hapo nje kulikuwa na pikipiki tano zikisubiri abiria, ‘akazitolea nje.’ Akasubiri kwa takriban dakika tano kabla hajaupata usafiri huo. Hatimaye teksi ilifika na safari ya kurejea nyumbani ikaanza. Akiwa njiani alitwaa simu yake na kutaka kumpigia Frank ili amjulishe kuhusu hali ya afya yake. Lakini akasita kufanya hivyo. Akaona kuwa itakuwa ni kumtia wasiwasi bure mpenzi wake!
Akairejesha simu kwenye mkoba na kutulia kitini, akihema kwa taabu na kuihisi baridi ikizidi kumwingia. Akajikunyata bila ya kusema neno, macho akiwa ameyakaza mbele.
Walipoingia eneo la Kigogo ndipo alipoanza kumwelekeza dereva njia ya kumfikisha kwake. Wakapita mtaa mmoja hadi mwingine hadi wakasimama nje ya nyumba ya Linda. Eneo hilo lilikuwa tulivu, na ilionekana kuwa wakazi wengi walishaingia ndani mwao.
Linda alimlipa dereva teksi na kuteremka. Akavuta hatua kwa udhaifu akiufuata mlango wa uani. Alikuwa na ufunguo wa mlango huo hivyo hakuiona sababu ya kumwamsha Catherine kwa ajili tu ya kufungua mlango. Akatumbukiza ufunguo ndani ya kitasa na kuuzungusha. Kitasa kikaitika.
Akausukuma mlango taratibu na kuingia ndani. Akaufunga mlango kwa nguvu, safari hii akiongezea na makomeo kwa kuwa aliamini kuwa hakukuwa na mtu mwingine ambaye hajaingia.
Akawasha taa na kuangaza macho katika sebule yake kubwa kwa muda. Maumivu ya viungo yakamfanya asizidi kuduwaa hapo. Akazima taa na kuanza kujikokota akielekea chumbani mwake. Alipoingia chumbani tu aliitupa pochi chini na kujitupa kitandani. Akashusha pumzi ndefu, maumivu ya viungo yakizidi kumtawala.
Mara akahisi kiu kali. Koo likamkauka. Akajikokota kwenda kwenye friji na kutwaa maji. Akajaza glasi moja na kuyanywa taratibu. Kichefuchefu kikamjia kadri alivyokuwa akinywa maji hayo lakini akajitahidi hadi akayamaliza.
Aliamua kujitahidi kunywa maji yote kwa kuwa alikwishaambiwa na wataalamu wa afya kuwa malaria hukausha maji mwilini kwa kasi ya kutisha, na yeye alishahisi kuwa malaria imeshamvaa hivyo hakuwa tayari kuichekea. ‘Wakati Tanzania tunapigania kupambana na Ukimwi, kuna nchi ambazo vita vyake vikubwa ni kupambana na malaria,’ aliwaza.
Sasa maumivu ya kichwa yakaanza kumtesa. Ndipo alipokumbuka kuwa majuzi alimpa Catherine vidonge takriban kumi vya kutuliza maumivu, akimtaka avitunze hukohuko chumbani kwake. Kwa usiku huo, alijua kuwa hakukuwa na namna nyingine ya kupambana na maradhi hayo, zaidi ya kunywa vidonge vya kutuliza maumivu. Apate tiba ya kutuliza maumivu na kukipambazuka ndipo aende hospitali kupima na kuanza kupata tiba halisi.
Akaamua kwenda kumgongea Catherine. Akajivutavuta hadi kwenye mlango wa chumba cha Catherine. Akagonga taratibu!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
**********
HAWAKUWA katika hali ya kawaida. Kila mmoja alijihisi yu katika dunia nyingine yenye kila raha ambayo binadamu anaihitaji. Ni majuzi tu Catherine alijigundua kuwa ana upungufu fulani kila alipomkaribisha Frank maungoni mwake. Alijigundua hivyo baada ya kwenda tena kwa Latifah na kuangalia mkanda wa ngono wa Wamarekani weusi.
Siku hiyo alishangaa kumshuhudia mwanamke mwenye mwili mkubwa kama huu alionao lakini Mmarekani huyo akionekana kujituma vilivyo katika burudani na mwanamume aliyekuwa naye. Alimshangaa jinsi alivyomdhibiti mwanamume wake kwa zaidi ya robo saa, mwili wake teketeke ukionekana dhahiri kuwa mwepesi kuliko ulivyotarajiwa.
Mmarekani Mweusi huyo wa asili ya Brazil aligeuka hivi, akakaa hivi, akabinuka vile, ilimradi alijua kila kitu na akafanya kila kitu hatimaye akafikia hatua ya kufanya jambo lililomsisimua na kumweka kwenye wakati mgumu zaidi Catherine pale alipomshuhudia mwanamke huyo akitumia kinywa chake katika kuhitimisha zoezi zima huku nwanamume wake akitapatapa na kugunaguna kwa kukolezwa na raha.
Kwake, Catherine hatua hii ya mwisho iliyohitaji ujasiri na kutokuwa na kinyaa ilikuwa ni ngumu sana kiutekelezaji. Hata hivyo, alijipa ujasiri na kuwa tayari kama tu Frank naye atahitaji kufanyiwa hivyo.
Ni usiku huu ndipo alipoamua kuiga uwezo wa yule Mmarekani Mweusi. Akajitahidi na kujitahidi kiasi cha kumshangaza Frank. Shughuli ikawa pevu zaidi!
“Frank...nakupenda...” kuna wakati Catherine aliropoka huku akiendelea kumng'ang'ania Frank.
“Catherine...Catherine...” kilifikia kipindi ambacho Frank naye aliunguruma, meno yakiwa yameumana, akikosa neno jingine la kusema.
Ndiyo, walikuwa wakistarehe na hawakujisikia kusitisha kila walichokuwa wakikifanya. Lakini walipofikia tamati na kutulia kwa muda bila ya yeyote kutamka chochote, ndipo masikio ya Catherine yaliponasa kelele kama vile za kufungwa kwa mlango na makomeo yakialika kutoka sebuleni. Akatega masikio vizuri.
Kimya kikatanda tena. Hakutaka kuamini kuwa huenda masikio yake yamepotoka. La hasha. Aliyaamini masikio hayo kwa asilimia mia moja. Hivyo akajitoa kitandani na kusimama chumbani humo huku akiendelea kusikiliza. Alikuwa hata hajajifunga kipande cha nguo mwilini mwake. Akasogea mlangoni kwa kunyata na kuendelea kusikiliza.
Mara akashtuka. Akageuka na kumtazama Frank. Macho yao yakakutana. Frank akaibaini hofu iliyomkumba Catherine.
“Vipi?” Frank alimuuliza kwa mnong'ono.
Catherine hakujibu. Akamwashiria kwa mkono atulie huku yeye akikimbilia kanga na kujifunga mwilini. Akilini mwake alihisi kuwa huenda vibaka ndiyo wameingia. Hisia kuwa huenda ni Linda aliyerejea hazikupata nafasi akilini mwake, na hata hivyo alijua kuwa kama angerejea ni lazima angemgongea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini pia alijua fika kuwa Linda ana ufunguo mwingine utakaomwezesha kuingia moja kwa moja. Hata hivyo asingeingia kwa kunyata kama hivi. Mtu anaingia kwake, ya nini kuingia kama mwizi? Zaidi ya zile kelele za mlango na makomeo, hakukusikika sauti nyingine, jambo ambalo huwa siyo la kawaida kwa Linda.
Mara nyingi alipokuwa akirudi, awe peke yake au awe na Frank lazima muziki ungefunguliwa. Linda alipenda sana muziki, hakuwa tayari kulala bila ya kupiga walao muziki kidogo.
Au kwa kuwa katoka msibani? Lakini kwani hii ni mara ya kwanza kwake kwenda msibani? Mara ngapi amekwenda misibani? Na mbona kuna misiba mingine ilikuwa hapo jirani sana lakini alikuwa kila akirudi lazima aburudike na muziki sebuleni kwake?
Ni hilo lililomfanya ajenge imani kuwa huyo aliye ndani humo si Linda, ni kibaka au vibaka. Akamfuata Frank kitandani na kumwambia kwa mnong'ono: “Kuna vibaka wameingia.”
“Vibaka?” Frank hakuamini. “Una hakika? Sio Linda?”
Catherine hakujibu. Akabaki katumbua macho mlangoni huku akihema kwa nguvu. Frank naye akajua kuwa tayari kuna jambo zaidi ya jambo. Hakuhofia kupambana na vibaka, alijiamini. Lakini kukutwa na Linda humo ndani ingekuwa ni fedheha kubwa si kwake tu bali hata kwa Catherine na huenda huo ungekuwa ni mwisho wa ajira ya binti huyo.
Kwa hali hiyo, akakurupuka na kuvaa nguo zake haraka. Ni wakati alipokuwa akimalizia kuvaa shati, ndipo wote waliposhtuka.
Mlango uligongwa!
Wakatazamana!
Mlango ukagongwa tena, kistaarabu kama awali. Sasa kila mmojawao akawa na hisia nyingine. Kwamba, ni Linda aliyeingia humo ndani. Ni kibaka gani atakayegonga mlango kistaarabu hivyo ilhali amekuja kuiba?
Ukagongwa kwa mara ya tatu na kufuatiwa na sauti, “Catherine!”
Mioyo ya Frank na Catherine ikapiga paa! Sasa hawakuhitaji uthibitisho mwingine kuwa ni nani huyo. Wakatazamana tena, nyuso zao zikionesha bayana taharuki iliyowakumba.
“Catherine...Cathy...” sauti iliongezeka.
“Itika,” Frank alinong'ona huku akiangaza huku na kule chumbani humo kama vile atafutaye mahali pa kuchomokea.
Bado Catherine aliduwaa. Kisha akavuta hatua akiusogelea mlango, na alipoufikia akageuka na kumtazama tena Frank. Hakukuwa na popote ambapo pangeweza kumsitiri Frank kwa wakati huo.
“Catherine...Catherine...!” sauti ilipaa zaidi, sanjari na ugongwaji mlango mfululizo.
Sasa Catherine alijua kuwa hata kama angejifanya kapitiwa na usingizi, ingekuwa ni hila ambayo Linda angeibaini mara moja. Akawaza, kama Linda ataingia humo na kumkuta Frank, ni kipi kitakachofuata? Je, kutazuka tandabelua ya aina yoyote? Je, yeye akiwa ni mfanyakazi tu, hana undugu hata wa mbali na Linda, atanusurika?
Hasira zitakazompata Linda pindi atakapomfumania hawara yake chumbani humo zitastahimilika? Na kama hatavumilia, hatua atakayochukua atayatafakari matokeo yake kabla ya utekelezaji? Hili la mwisho lilimtia wasiwasi. Ni vigumu sana kwa mtu kumfumania mpenziwe na kuamua kuyamaliza matatizo kidiplomasia.
Inauma!
Ndiyo, inauma kupita kiasi, hivyo, huenda mfumaniaji akaamua hata kuua bila ya kujali kuwa kitendo hicho kinaweza kumfikisha pabaya pale Jamhuri itakapoamua kufanya kazi yake.
Wakati huohuo, aliwaza kuwa huenda hasira za Linda zikahamia zaidi kwa Frank na yeye akaishia tu kutimuliwa humo ndani usiku huohuo. Je, kama atatimuliwa ataenda wapi usiku huo? Lakini pia aliona kuwa kitendo cha kufukuzwa bila ya kuguswa hata kidogo kitakuwa na nafuu kwake. Atatafuta pa kujibanza na asubuhi ndipo atakapopata akili mpya.
Mlango uligongwa tena. Sasa Catherine akaamua kuwa liwalo na liwe. Akakikamata kitasa na kukizungusha taratibu huku mikono ikimtetemeka. Akageuka nyuma tena kumtupia jicho Frank aliyekuwa ameketi kitandani kanyong'onyea.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akakirudia kitasa na kufungua mlango!
**********
KAMA ni malaria basi ilizidi. Kama ni ndoto basi hii ilikuwa ni zaidi ya ndoto. Kama ni kiinimacho basi hiki kilijidhihirisha bayana. Kwa jumla Linda alishindwa kuyaamini macho yake. Alisimama kama sanamu, akishindwa hata kuyapepesa macho, na akishindwa hata kupumua vizuri. Vinyweleo vilisimama kama mbwa aliyeona chochote kile cha kumsisimua. Vitone vya jasho vikajiunda katika paji la uso wake!
Alimtazama Frank kama atazamaye mzimu! Hakuhitaji ushahidi mwingine kuwa Frank alikuwa amelisaliti penzi lao. Aliduwaa kwa muda kabla ya kuanguka chini na kuzirai!
Alipozinduka ilikuwa ni asubuhi. Alikuwa palepale sakafuni. Akajizoazoa na kuamka. Akaangaza macho huku na kule chumbani humo. Hakukuwa na mtu!
Akatoka na kuingia chumbani kwake. Mara akatoka tena na kwenda chumbani kwa Catherine ambako baada ya kufanya uchunguzi kidogo tu akabaini kuwa Catherine alikuwa ametoroka na nguo zake zote. Zaidi, alibaini pia kuwa simu yake haikuwepo na aliporudi chumbani kwake na kufanya upekuzi wa kina akakuta pesa zilizokuwa ndani ya begi lake, shilingi 380,000 zimechukuliwa!
Naam, kama kuna wakati ambao kwake ulikuwa ni mgumu maishani, basi ni huu. Catherine kaenda wapi? Haijulikani! Atakuwa karudi Sengerema? Hapana, hilo halikumwingia Linda akilini.
Ni yeye Linda aliyemtoa Catherine katika kituo cha kulelea watoto yatima huko Sengerema. Leo hii Catherine akiwa amekua kimwili na kiakili, akiwa tayari amejanjaruka ndani ya Jiji la Dar es Salaam, atakuwa na mawazo ya kurudi Sengerema ambako hana hata ndugu?
Kama tayari ana pesa hizo alizoiba, atashindwa vipi kuyaanza maisha ndani ya jiji hilo kubwa lenye wakazi zaidi ya milioni kumi, vitongoji lukuki, wilaya zilizoungana, manispaa zilizobanana na majumba yaliyokabana?
Catherine wa leo siye yule wa enzi zile kule Sengerema. Leo Catherine kanenepa, kanawiri, kanang’anika! Catherine wa leo ‘anamjua mwanaume’! Aanzie wapi kumsaka? Labda kwa rafikiye, Latifah.
Akakurupuka na kuelekea kwa mzee Atupele. Huko akawakuta wote na alipomuuliza Latifah kuhusu rafiki yake, Latifah naye akashangaa.
“Hatujamwona hapa!” Latifah alijibu.
Mke wa Mzee Atupele na Atupele mwenyewe nao wakathibitisha hivyo!
Atampata wapi?
Alitamani kulia, hakuweza.
Akajaribu kucheka, kicheko kikakwama.
Akafikiria kujiua, akasita.
Afanye nini?
Na kama ungekuwa wewe ungefanya nini?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
*****MWISHO*****
0 comments:
Post a Comment