Chombezo : Nilambe Humo Humo
Sehemu Ya Pili (2)
“Eeh!’’ Akakubali kwa msisitizo. Moyo wangu ukazizima kwa furaha nikajua naweza kutumia moja wapo kati ya njia hizo, mambo yakajipa na nikaweza kummiliki Shamsa Nuhu moja kwa moja.
‘’Ila’’ Akimu akanizindua tena, “Itakubidi usubiri muhula huu wa mitihani uishe ili usichanganye mapenzi na masomo. Ukianza wewe kuvichanganya vyenyewe vitamalizia, na hupata zaidi ya hasara!’’
‘’Nitasubiri!” Nikamwambia
“Good!’’ Akashangilia baadae akaniambia lile alilokuwa akinitafutia, nami nikampa ushauri alioutaka. Mpaka tunaagana tabasamu lilikuwa bado limeupamba uso wake.
* * *
Usiku ule hali ilikuwa ngumu Sana niliufikiria mlolongo wa maisha yangu, mahusiano yangu na wanawake hatimaye Shamsa “…ndio maana nakupenda Ibra…!” Mvumo wa sauti yake tamu ukatetema akilini mwangu na kuendelea ’’…wewe sio muhuni na hupendi mambo ya kipumbavu!’’
Mambo yepi wakati mie nampenda? Hivi wakati anaongea yale alikuwa seriously au? Sasa kama aliyasema kwa dhati itakuwaje atakapopokea sms yangu ya mapenzi? Atasemaje atakapopata barua au kadi kama sio uwaridi?
Maswali yalikuwa mengi majibu yakiwa haba. Dakika kadhaa zikapita kichwa kikinichemka. Kutahamaki nikawa nimeinuka na kuikabili kabati nikaifungua na kuitwaa albamu ya picha nikarejea nayo kitandani.
Katikati ya albamu ile kulikuwa na picha nzuri ya Shamsa akiwa ufukweni ndani ya mavazi ya kuogelea. Picha hii nilimpigisha kwa wizi baada ya kumuomba mpigapicha mmoja ampige kwa siri na kuniletea picha hiyo kwa malipo ya kutakata.
Vile alipigwa bila ya kuwa na taarifa, alitoka vizuri sana! Rangi yake adimu ya chocolate iliupendezesha mwili wake na kutokeza kwa mng’aro uliovutia hasa katika yale maeneo ambayo ni aghalabu kuonekana wazi hovyo hovyo, ila pale anapoamua kubaki na chupi na sidiria tu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Vishimo vya kuvutia vya hapa na pale katika kidevu na mashavu yake, miraba miraba mizuri yenye ukubwa wa wastani iliyoizunguka shingo yake na kuikata kata vizuri sana, achilia chuchu zilizosimama vizuri; vilikuwa ni baadhi tu ya vitu viliyoyafanya mate ya uchu yaanze kujaa mdomoni.
Wakati nikiyameza, macho yakashuka chini tumbo dogo na zuri lenye kitovu maridhawa lilikuwa likinisubiri! Mwili ukaanza kupata joto hali mheshimiwa akianza kushtuka, niliposhuka chini zaidi kwenye mapaja. My God! Shamsa!? Acheni niwe zezeta.
Hali niliyoiona pale chini ikayafanya mapigo yangu ya moyo yaende joshi kana kwamba yanataka kuzimika. Yule mheshimiwa kule ‘somewhere’ sasa akasimama barabara kutaka kukagua gwaride la heshima.
Nikatazama mbele ya dressing table yangu kulikuwa na kopo la Rays, sabuni ya Give na Lotion ya E9. Akili ikafanya kazi kuchagua niende bafuni na nyenzo ipi kati ya zile.
Kabla sijachagua, masikio yangu yakanasa kitu. Macho yangu yakageuka haraka kuiangalia TV iliyokuwa humo chumbani. Nikaona polisi wakifanya kuwasukuma watu kwenye Defender. Ilikuwa ile Operation maalum iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dare s salaam ya kuondoa machangudoa waliozagaa huku na huko katika jiji la Dar es salaam.
Akili yangu ikapata chaji mpya.
Kumbe kuna mahala ninakoweza kupata tiba muafaka bila taabu, mahali ninakoweza kutibiwa bila kuangaliwa usoni, nikasuuzika mimi na mtima wangu hata nikaona raha na utamu wa dunia.
Bila ya kufikiria mara mbili nikachukua pesa kiasi, nikaweka ndala miguuni na kutimkia stendi. Ilikuwa saa mbili usiku. Nikaparamia daladala moja, baadae nikashuka na kupanda nyingine, niliposhuka nikatemba kidogo nikiuliza hapa na pale, nikiingia kichochoro hiki na kile, hofu ya kukabwa ikawa puani kabisa.
Kutahamaki nikawa nimeibukia nilipopataka
Uwanja wa fisi!
Harufu ya nyama choma ikanipokea, kelele za kanisa hali kadhalika. Katikati kulikuwa na uwanja mkubwa uliosheheni visichana vidogo vidogo vya wastani na wanawake kadhaa ambao mavazi, vitendo na jinsi walivyo walikuwa mwito tosha.
Macho ya wengi wao yalikuwa malegevu mithili ya mtu aliyekula kungumanga. Wengi walikuwa na ndala na miguu yao ilikuwa michafu wenye mchanganyiko wa vumbi masizi na pumba ambazo nyingi zilikuwa zikingali zimeanikwa hadi usiku huo.
“Hoyaaa…!’’ Mmoja akaita.
“Bro!” Mwingine akadakia.
Nikainua macho kuangalia huyo aitwae, mmoja akajaribu kunikonyeza. Nikajikuta nikitabasamu! Sio kwa kufurahishwa na konyezo lake, hasha! Yale macho. Alikuwa na macho mabaya ajabu.
“Twenzetu tuka…!’’ likamtoka neno baya yule wa kwanza. Yule wa pili akajaribu kutabasamu. Likaondokea kuwa tabasamu lililokosa ladha. Zaidi lililochusha na kuudhi. Kicheko kidogo kikaniponyoka.
Vibinti hivi vilikuwa viathirika vikubwa vya madawa ya kulevya. pamoja na kiu yangu kubwa ya ngono, nikavipuuza macho yangu yakasafiri tena na kufanya ziara ndefu katika maeneo anuai ya viwanja vile vilivyolaaniwa.
Muziki mkubwa uliokuwa ukitoka katika baa mbili tatu za kienyeji zilizolizunguka eneo hilo, lile kundi la wachoma nyama ambazo hazikujulikana ni za mnyama gani, walevi waliotamalaki huku na kule wakiyumba, kutukana na kucheza muziki, wacheza kamari, vile visichana vichangudoa pamoja na zile kelele za kanisa kwa pamoja zilipafanya mahala pale sio tu uwanja wa fisi hasa. Bali uwanja wa fujo! Tena fujo lililo chukizo.
Katika kuendelea kuperuzi, nikaona vijana wengi waliokuwa wakiingia na kutoka katika uchochoro mmoja uliokuwa ukipita pembezoni mwa kanisa. Wengi mno.
Pasipo kujitambua na pengine bila ushirikiano maalumu na akili yangu ambayo kwa kawaida ndio mwenyekiti wa mwili wangu, kwa maana ya mfanya maamuzi, miguu yangu ikaanza kurefuka na kupiga hatua ndefu ndefu kuelekea kule kulipokuwa na sumaku iliyokuwa ikiwavuta na kuwatema vijana.
“Sasa vipi mpenzi?” Sauti moja ikaniwahi
’’Mchumba niko hapa, njoo tuyamalize!!” Nyingine ikadakia. Sikuwasikiliza, niliendelea kupiga hatua ndefu kama ninayewahi kitu fulani
“Achana nae!’’ Mmoja akafoka
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
’’Anawahi kwa wahaya! Angejua kama wahaya ni spare tire! He he he halooow!” wakacheka kishangingi kwa sauti zao zilizo toka mfano wa sauti ya redio yenye betri zisizo na nguvu. Sikuwasikiliza!
Nikaingia katika uchochoro ule. Mungu wangu! nikamudu kutamka. Sekunde chache baada ya kuingia nikatokezea katika mnada wa machangudoa hasa, ilikuwa ni mitaa miwili myembamba sana yenye vyumba vidogo vilivyotazama nje.
Ukingoni mwa kila nyumba, mwanamke mmoja aliketi juu ya stuli au kigoda akiwa na kijivazi kilichoacha nje sehemu kuubwa ya mapaja yake, taa inayoyowaka ndani iliachwa iyamulike mapaja yale makubwa na mazuri na kutufanya wakware kutokwa na mate ya uchu.
Mapaja wazi mtaa wote!
Kazi yako ni kupita mbele ya nyumba hiyo huku ukichagua mapaja yaliyonona kupita yote, huku kila uliyemkaribia akikurabisha kwa tabasamu taamu, tabasamu maridhawa. Nikachoka! nisikuamni macho yangu. ‘’Eeeh Tanznia hii hii, tena Dare s salaam!” Nikawaza kwa mshangao
Nikapiga moyo konde na kupita taratibu nikitazama mapaja hayo kushoto na kulia kwangu, kundi la vijana nilioingia nao katika mtaa huo mwembamba wakipotea mmoja baada ya mwingine kwa zamu na ndani ya vyumba vile na milango kufungwa nyuma yao.
Wakati haya yakitokea; milango mingine iliyokuwa imefungwa, inafunguliwa mmoja baada ya mwingine kwa zamu. Ndani yake wanatoka vijana kama sio wanaume wanaovuja jasho, wengine wakiwa vifua wazi.
Nikaendelea kutembea, kutahamaki nikatokea mtaa mwingine.
Huu haukuwa na vituko, mbele yangu kulikuwa na vijana fulani kama wanne hivi waliokuwa wakitafuta kitu fulani. Nami bila ya kuwaambia nikawa nimewageuza kuwa wenyeji wangu. Nikawafuata kila walipokwenda. Tutukaingia mtaa mwingine.
Huu ulikuwa wa mijimama tipwa tipwa mikubwa yenye maumbo makubwa ya kibantu. Hawa walikuwa ni wazuri maradufu kuliko wale wa awali nikafanya kukaza moyo na kuwapita.
Mtaa uliofuata ulikuwa wa wazee! Hawa sikuwatupia macho japo marambili, nikiwa na wenyeji wangu tukaingia mtaa wa tatu, huu ulikuwa wa mashoga!! nikasikia kinyaa na kutoka mara moja nikawaacha wenyeji wangu wakishughulikiwa katika mtaa huo.
Nikarudi kuzunguka mara ya pili na hatimaye nikajikuta nikiangukia katika mikono ya jimama moja lililokatika kibantu khaswaa ambalo lilikuwa na weupe wa papai bivu.
‘’Mambo?’’ Nikalisalimia
‘’Safi, vipi unataka huduma?’’ Akarembua na kutabasamu, alikuwa na mwanya alikuwa na dimples!! My God, ugonjwa wangu!.
‘’Ndiyo! Nikakubali haraka
‘’Basi karibu ndani!’’ Akafanya kunipisha niingie ndani
‘’Kiasi gani?’’
“We mgeni hapa?”
‘’Ndiyo! Hii ni mara yangu ya kwanza kufika hapa!
’’Si siunataka mapenzi ya kawaida tu?!”
Sikujua mapenzi ya kawaida ni mapenzi gani. Ila kulingana na ukubwa wa mama huyu ambae alinizidi umri kwa kila namna, hali weupe na uzuri wake ukinitisha, nikajikuta nikitikisa kichwa kukubali.
‘’Elfu tatu tu’’ Nikajibiwa.
Nikaingiza mkono mfukoni
‘’Nimekwambia uingie ndani ebo?” Akanikaripia na kuongeza “Kama umetumwa ujue kutuchunguza, sijui kutuchoma ujue hutatoka salama! Tutakupigia kelele za mwizi, wakutwange wakutie mafuta na kukuchoma moto!’’ Akanihitimisha
Nikaogopa na kuruka ndani haraka.
Chumba kilikuwa cha wastani chenye ndoo kadhaa za maji kitanda cha wastani futi nne kwa sita, jiko la mchina beseni lenye vyombo vichache nadhifu na stuli moja tu.
Ukutani kulikuwa na picha kubwa za wanawake wa kizungu walio uchi ambao walikuwa wamelala kitandani katika namna ya kutamanisha kulikovuka mipaka, yule mheshimiwa akaanza fujo tena.
Jimama likaingia na kufunga mlango!!!
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Likaondoa kanga kifuani na kile kijisketi kilichokuwa kimemsitiri kwa chini na kubaki kama lilivyozaliwa. Mwanga hafifu uliotoka katika balbu ukimpiga vilivyo katika mwili wake mtepe na kuufanya uwe mwekundu na kuvutia vitamu, jimama likapiga hatua za maringo na kuketi kitandani.
Mkono wake ukazama uvunguni na kuibuka na boksi la kondomu!
‘’Changamka! Hesabu haijatimia, nataka niendelee kula vichwa na kijua ndio hiki nisipouanika nitautwanga mbichi!’’ Nikaelewa nikavua shati, wakati najiandaa kuvua suruali akaniuliza
“Unataka kulala hapa hapa?”
‘’Hapana!’’
‘’Sasa unatoa nguo za nini?’’
‘Nikamshangaa ‘’si tunataka ku…ku…!’’
“Najua’’ akaniwahi kwa karaha ‘’Haina haja ya kuvua nguo shusha tu suruali kidogo kama huwezi kuipitisha hapo katika zipu! Halafu nipe hela yangu kabisa!”.
Nikatoa hela na kumpa nikimwambia “Lakini hapa hatuwezi…”
‘’Ukitaka starehe kamili kaoe! Mimi niko kazini na nilishakwambia hesabu haijatimia hivyo sitaki mizungu!’’
Nikamtumbulia macho
Alipoona simuelewi akanisogelea pale akaivuta chini sarawili yangu na kumkamata jamaa aliyekuwa nusu akilia na nusu akitetemeka akamvisha koti la mvua na kumkaribisha uwanjani akague gwaride.
Hakukuwa na busu, sijui romance wala kunyonyana ndimi. Nikaanza kazi mara moja. Alikuwa fundi wa kuzungusha viuno na kunung’unika. unadhani nilichukua round basi!? dakika zangu mbili unusu tu, ikawa kitu na boksi! Akanitoa kunisukumia pembeni. Kazi ikawa imekwisha.
‘’Ukitaka kurudia je?” Nikamuuliza nikimwangalia kwa matamanio. Kusema kweli nilikuwa sijaridhika hata kidogo.
‘’Haturuhusu! Hapa goli moja, unatambaa!“
Nikamuelewa.
Dakika iliyofuata nikawa nje katika upande mwingine.
Elfu kumi niliyoichukua kwa kazi hii ilibaki elfu saba! Kwa bei ya elfu tatu ningeweza kupata wanawake wengine wawili na kubaki salio la elfu moja ambayo ningelitumia kama nauli na kurudi bwenini chuoni Chang’ombe.
Katika chumba hiki cha pili nikiwa na mwanamke mwingine tena nilikuwa nimeshakaa kifuani kwa zaidi ya dakika tano pasipo jibu kuonekana, ndipo mambo yalipoanza kwenda mrama.
‘’Changamka bwana muda wako umeisha!’’ Alinihimiza nikazidisha spidi. Dakika zingine tatu yule mama akanisukumia pembeni na kuliangalia koti la baridi alilonivika akidhani namuongopea.
‘’Alipokuta halijaloa akaniangalia vizuri na kunitwanga swali
“Umeshatoka kupata sehemu nyingine siyo?”
‘’Ndiyo!” Nikamjibu.
Akaachia mfyonzo mrefu uliotoka vizuri haswaa. Halafu akainuka kwa ghadhabu na kuvaa nguo zake, alipomaliza akaniambia “Haya toka!’’
‘’Lakini hatujamaliza bado!’’
‘’Tumemaliza umeniongopea kuwa hujapata kumbe umeshapata toka nakwambia!’’ Sasa alinifuata na kuniinua pale kitandani.
‘’Hatukuongea hivyo!’’
‘’Toka nitakupigia kelele za mwizi!’’ Sauti yake haikuwa ndogo, alikuwa akipayuka.
“Basi nipe chenji yangu nakudai elfu mbili, nimekupa elfu tano!’’
“Elfu tatu ni dakika tatu wewe umetumia kumi! Nikingali nakudai elfu tano!” Akabweka.
Nikachoka. “Haiwezekani!” Nami nikapandisha na kukomaa. “Lazima unipe chenji yangu’’
Akaufuata mlango na kuufungua nje kulikuwa na shehena ya kutosha ya watu, Baadhi wakitaka kujua kulikoni wengine wakipaza sauti nikomeshwe! “Betty mtoe fasta tumjeruhi!” Sauti kutoka nje ikaomba.
Akanivuta na kunisukumia nje akawageukia wale wanawake na kuwaambia “Alitaka kunitumia dabo dabo bila malipo!”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kufikia hapo moyo ulikuwa ukinipiga vibaya nikijua sasa ndio naadhirika. Kwa ajili ya ngono! Nikawaza kwa uchungu. Maana sikupewa hata nafasi ya kujieleza.
Pale nje nilipokelewa kama mpira wa kona, nikatukanwa matusi ya kila aina waloweza kunitia singi walinitia, walioweza kunipiga na viatu na makopo ya mkojo pia walifanya hivyo.
Mara wakatokea watoto kadhaa machokoraa wakanikwapua kama kipanga na kunipeleka mahala walipopaita Chakabovu! Kule wakanisachi na kunipokonya kila nilichokuwa nacho.
Simu, fedha kidogo, viatu, kofia! Halafu halafu wakaniambia nipotee!
Niliondoka roho ikiniuma na nikiwa nimewachukia wanawake wote wa Uwanja wa fisi. Niliwachukia isivyo kawaida. Kutoka pale Manzese Bahresa hadi magomeni makonda waliweza kunielewa na kunipa lifti.
Lakini kutoka Magomeni hadi Chang’ombe hawakunielewa ikanilazimu nitembee kwa mguu kutoka Magomeni baada ya kuona masaa yakiyoyoma bila kupata lifti. Nilifika chuoni usiku nikiwa hoi bin taaban.
Siku ya pili sikuingia darasani nikabaki bwenini nikijisomea na kuuguza majeraha madogo toka kwa wale machangu pamoja na machokoraa wao.
Jioni Akimu na Shamsa walikuja kunitazama na kunipa pole. Nikajisingizia ugonjwa. Shamsa akanisisitiza kwenda hospitali kuangalia afya pengine nina malaria
‘’Nitakwenda!’’ nikawaambia kuwapa moyo.
* * *
Miezi kadhaa baadae nilishaweza kuyasoma mazingira na kwenda nayo sawasawa. Niligundua kuwa uwanja wa fisi sio mahala pa’ kwenda na fedha nyingi, simu ya kifahari, mavazi mazuri sana na kadhalika.
Sio mahala pa’ kusema utapata bao mbili kwa mwanamke mmoja. Na muda wa kuwa na mwanamke kitandani usizidi dakika kumi,
Niligundua pia kuwa yako mamia kwa mamia ya wanaume wanaofuata ngono za bei raisi katika maeneo hayo kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo hapo hakuna haja ya kutongoza.
Hakuna pia kuombwa hela ya vocha, Saloon, hela ya mtindo mpya n.k pale ni mahala pa’ kulipa, kupata huduma utakayo na kutoweka! Mahala pa nipe nikupe.
Niligundua pia kwa siku moja pale mwanamke ambae mapato yake sio mazuri hulala na angalau wanaume kumi kwa siku na kupata elfu thelathini! Wale wenye mapato mazuri hupata wanaume kati ya ishirini na ishirini na tano kwa siku.
Hawa pato lao kwa mwezi lilifukuzia pato la mafisadi kwa karibu tu kwa vile ni kati ya milioni 1.2 na milioni 5, ambapo pia nao hulazimika kulala na wanaume 600 hadi 750!
Unashangaa nini? Wewe endelea tu kuhudhuria huko uwanja wa sifa kama ibada ujue hauko peke yako.
Niligundua mbali ya walevi, wanywa pombe na wabwia unga; wapo baadhi ya wanawake ambao wamelitumia pato hilo kwa kujenga makwao kusomesha watoto na n.k.
Niligundua tena kuwa wengi walikuwa ni waathirika wa ukatili wa kijinsia ambao uliwakumba katika familia zao na mikondo ya maisha waliokuwa wakiishi.
Wengine ndugu zao wa kiume walikuwa wamewadhulumu mali za urithi walioachiwa na wazazi wao, wengine walikuwa yatima walioondokewa na wazazi wao na kukosa mtu wa kuwaangalia! Wengine walikuwa wametupwa na wazazi wao baada ya kuzaliwa wengine… wengine!
Basi ilimradi kulikuwa na mlolongo wa matatizo ambayo kwa hakika yalichusha na kuudhi.
Hofu ya ukimwi je?
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walikuwa nayo lakini wangefanyaje? Waliona bora waishi kwa furaha leo kwa kuwa hata kesho wasipokufa kwa ukimwi kama watajitunza, basi watakufa kwa njaa, umasikini na adha zingine kadha wa kadha.
Ugunduzi huu ukanifanya nisiwatizame kwa jicho baya tena, bali nikawaona kama wahanga fulani hivi!
Nikajitengenezea utaratibu mzuri wa kwenda pale na kuhudumiwa mara nne kwa wiki! ulikuwa utaratibu nilioupenda na kuufuatisha kama ibada, utaratibu mtamu kweli, mtamu haswaa.
* * *
**IBRA keshagundua mambo kadhaa juu ya Uwanja wa fisi…sasa amejiwekea utaratibu wa mara 4 kwa wiki…….HATARIII…
Tukutane tena kesho saa mbuli na nusu usiku…tuendelee kuchombezana
0 comments:
Post a Comment