Search This Blog

Monday, October 24, 2022

MWAGIA HUMO HUMO - 5

 





    Chombezo : Mwagia humo humo

    Chombezo : Kumbe Vikiungwa Vitamu

    Sehemu Ya Tano(5)



    Nilimweleza huku nikimuongeza mahanjamu yaliyomfanya ajikute katikati ya shamba akipalilia mazao bila kutumia nguvu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kama alivyonielezea Bi Shuu tulikuwa tukizimua ili kuuchangamsha mwili kutokana na mtanange wa kukata na shoka. Hatukutumia nguvu sana zaidi ya kuichangamsha miili yetu. Baada ya kila mmoja kupata kifungua kinywa kikombe kimoja kikavu kijasho kilitutoka na kwenda kuoga. Huwezi amini Bi Shuu muda wote alikuwa karibu yangu kwa kila hatua.

    Nilikuta maji ya moto tayari yapo bafuni, tulioga pamoja huku tukishikana hapa na pale. Baada ya kuoga tulirudi ndani, juu ya meza kulikuwa na chupa ndogo ya chai na sahani iliyokuwa imefunikwa sikujua kwenye chupa kuna nini na kwenye sahani kumefunikwa kitu gani. Mateja alipoona chupa ya chai na vikombe vya udongo ambavyo vilionekana mahususi alisema. “Mmh, kweli toka jana umenipania, alfajiri yote hii umeamka saa napi kuandaa kila kitu.” “Kila mwanamke anajua wajibu wake.”

    “Asante nimekubali.” Moyoni nilibakia na maswali Bi Shuu amelala saa ngapi maji ya moto na kifungua kinywa amevitayarisha saa ngapi. Nilijikuta nikumuonea huruma bibi wa watu na kujiona kama namtesa bure.

    Lakini kwa upande mwingine alinisaidia sikuamini vitu vile kama mwenyewe ningeviweza. Nilisogea kwenye meza na kuangalia kwenye chupa kulikuwa na tangawizi na kwenye sahani kulikuwa na mayai manne. Mateja alipoviona vile vitu aliniambia.

    “Nikuambie kitu Manka?” “Niambie.” Mateja anataka kumwambia nini Manka? Kuyajua yote tukutane wiki ijayo. “Kipi nilikifanya kwa ufasaha?” Nilimuuliza kutaka kujua hizo maksi tisini nilizipata vipi. “Vingi sana.” “Vipi hivyo?” “Mwana wee, hata hujapumzika una pupa kama umemuona Mateja kadondosha taulo?”

    “Jamani Bi Shuu yamekuwa hayo!” “Umerudi pumzika jimwagie maji kisha uache mwili upumue kwa muda, kwa vile muda bado tunaweza kuzungumza kwa kituo, siyo juu juu kama malaya wa Magoti, lamba raha, nipe changu.

    ” Mmh! Maneno ya bibi huyu yalinifanya niwe mdogo kama pilitoni na kukoma kuuliza swali kama lile.

    “Basi wacha nikaoge.” “Haya ndiyo maneno, mtoto wa kike huambiwa sio aulize vingine aibu, ushanizoea eeeh.

    ” Bi Shuu aliniuliza huku akinikata jicho la dharau.

    “Hapana Bi Shuu.” “Ndivyo nilivyokufunda, eeeh jambo la ndani kulisema hadharani?”

    He! Makubwa Bi Shuu aligeuka mbogo. “Bi Shuu, samahani basi.” “Samahani basi, ndiyo nini?” Bi Shuu alishika pua. Mmh, niliamini kisebusebu changu ndicho kilichoniponza baada ya kuamini Bi Shuu wa kawaida wa kumuuliza kila nitakacho. “Bi Shuu samahani sana kama nimekukosea.”

    “Nshakusamehe, nenda kaoge pumzika kisha njoo.

    ” Nilikwenda chumbani kwangu kubadili nguo kisha niliingia bafuni kuoga, baada ya kuoga nilijilaza kitandani na kupuliziwa upepo mwanana wa feni. Nikiwa nimejilaza nilikumbuka Mateja alitaka chakula cha usiku, nilikurupuka na kumfuata Bi Shuu aliyekuwa amekaa sebuleni kwake akiangalia cd ya taarabu. “

    Vipi?”

    Aliniuliza baada ya kuniona. “Bi Shuu Mateja anataka chakula cha usiku.” “We mwali! Chako amekiona hakifai anataka na changu?” “Jamani Bi Shuu maneno gani hayo?” Jamani Bi Shuu alinipeleka sipo kabisa. “Sasa kosa langu nini, kama angetaka chako usingeniambia ungempa tu, lakini baada ya mwali anataka na vya kungwi wake, naona kanogewa sasa anataka kuku na mayai yake.”

    “Jamani Bi Shuu sina maana hiyo.” “Ulimaanisha nini?” “Chakula ulichompikia jana kimemrusha akili kimeniongezea maksi mtoto wa kike na kutaka awe anakula kila siku, kitu kitakacho harakisha ndoa.” “Na mchumbake?” “Amechoka kula vya kuchemshwa bila kuungwa.”

    “Hooooya weee, kweli kula uhondo kwahitaji matendo, umeona eeeh?”

    “Nimeamini mtembea bure si mkaa bure, Mateja kachanganyikiwa ingekuwa ndoa ni viocha ya simu, mbonaangenifuta na kuniiingiza na sasa hivi angekuwa hewani kwa raha zake.”

    “Manka huyoo, ushakuwa mtoto wa Kizaramo mineno kama umebemendwa.” “Bi Shuu kweli wewe nyani huoni makalio yako.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    TEMBELEA TANGAZO HILI CHINI KWA KU-CLICK HAPA “Haya tuachane na hayo anataka chakula gani?” “Kama cha jana.” “Lakini leo utapika mwenyewe.”

    “He! Bi Shuu mbona unaniumbua mchana, nitaweza wapi kupika chakula kitamu au ndiyo unanivua nguo ukweni.”

    “Wachina wana methari zao kuwa ukitaka kumsaidia mtu usimpe samaki bali mfundishe kuvua ili aweze kupata zaidi.” “Kwa hiyo nami unanifunza kuvua?” “Ndiyo maana yake, kama ningejitoa kwa Mateja angekupenda wewe au mimi?” “Wewe?” “Basi, leo nina kazi ya kukufundisha kupika baadhi ya vyakula, ushaona chai ina paliliwa.” “Ha!” “Unashangaa, kupika kunataka kituo kutuliza akili sio nyanya hazijaiva wewe unatosa kitoweo, ndiyo maana vikiiva havieleweki kila kitu kipo kivyake.”

    “Si kuna mafunzo ya kupika mtu anapata cheti?” “Cha darasani si kitamu kama cha asili, wee nenda kanunue vitu ili tuingie jikoni pamoja, siku ya pili umuandalie peke yako bila msaada wangu.” “Nikijua kupika nitafurahi.” “Unatosheka? Hata ukijua kupika bado utajigundua una mapungufu.” Bi Shuu alinielekeza vitu vya kwenda kununua, sikutaka kupoteza muda nilibadili nguo na kwenda kudandia daladala mpaka sokoni, baada ya manunuzi yote muhimu.

    Nilirudi mara moja na kumkabidhi Bi Shuu ambaye alinieleza nitulie atanishtua. Nilirudi chumbani kwangu na kujilaza chali nikiwa kama nilivyozaliwa na kula upepo wa feni kwa raha zangu. Nilijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu juu ya mambo ya Bi Shuu, mtu mmoja alikuwa na mambo mia moja. Nilikubali mzee wa watu kutoa huduma pasina kinyongo, kweli alipewa mambo yaliyo katika mzani.

    Majira ya jioni Bi Shuu aliniamsha na kuanza maandalizi ya kupika, maandalizi ya awali ya kumenya vitunguu maji na swaumu nyanya na viungo vingine nilijua kuandaa baada ya kuandaa tuliingia jikoni. Niligundua makosa yangu mengi katika kupika. Kwa upande wangu nilikuwa natumia muda mchache kupika tofauti na Bi Shuu hakuwa na papara katika kupika hata chuzi lilionekana kweli linajitengeneza tofauti na kina sisi wakina mama kuchemsha, kweli niliamini vitamu vinahitaji utulivu. Nini kitaendelea? Kuyajua yote tukutane wiki ijayo.

    Baada ya kuandaa chakula kwa kufuata maelekezo ya Bi Shuu, nilikiandaa kwa ajili ya Mateja. Mtoto wa kike nilioga na kumuandalia Mateja maji ya kuoga niliyoweka viungo. Nilirudi chumbani kujiandaa kumpokea mpenzi wangu, kama nilivyoelekezwa na Bi Shuu mwanamke anayetaka kumpokea mpenzi wake hasa penzi linapokuwa changa.

    Nilijifukiza udi wa manukato kila kona ya mwili hata kanga zangu nilizokuwa nimejifunga na shuka nilizotandika nazo zilikuwa zinanukia. Yote haya yataka kituo huwezi kuyafanya kwa kulipua utaona mzigo. Kujipulizia manukato ya al udi, jicho lililoregea kwa ajili ya kungu manga liliongezwa uzuri na wanja mwembamba wa mwezi mchanga.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilijilaza kitandani huku nikisindikizwa na muziki wa taarabu wa zamani kidogo ulioporomoswhwa na kikundi cha taarabu cha TOT, kilichoimbwa na bibi Hadija Kopa kisemacho ‘TX mpenzi.’ Niliyakumbuka baadhi ya mashairi yake: Tx mpenzi daktari wangu wa thamani, Kiitikio: Ayaa ayaa ayaaa.

    Amesipeshalaizi digii yake surgeon (Mtaalamu wa upasuaji) Kiitikio: Aya aya Ayaaa. Aminyapo dawa zake ganzi tele maungoni, Tx nipasua toa maradhi ya ndani. Kiitikio: Nipasue Tx nipasue eeh toa maradhi ya ndani wee nipasue. Siku za nyuma nilipousikia wimbo huo sikuuelewa, lakini nilipojua zuri na baya na kuelezewa maana ya wimbo huo. Nilijitambua kumbe mimi mgonjwa na daktari wangu Mateja niliyemsubiri kwa hamu aje atoe maradhi ya ndani kwa kunifanyia upasuaji.

    Wimbo huu ukiusikiliza kisha uusikie wimbo wa Mwanaidi Shaabani uitwao Dereva akiwa na kikundi cha Muungano Culture Troop, wimbo huunao kuna maneno kama haya: Dereva nimempata ananiendesha vyema sukani akikamata chombo hakiendi mrama. Breki akikamata wakati wa kusimama ziozile za kugota za kishindo na kuzama.



    Uniacha naitaita kwa uroda nihema. Hebu niambie mumeo sifa hizi za dereva makini anazo, basi wimbo huu niliupanga baada ya mtinange na Mateja nimewekee.

    Mwa kwetu sina haja ya kukuwekea wimbo, la hasha nakuomba hasa wewe msichana wa siku hizi tafuta nyimbo hizi kisha zisikilize na upate mnaana zake hakika utaungana nami kumwita mumeo au mpenzio Tx wa mapenzi na mwisho wa safari lazima umwite dereva wako makini mwenye reseni ya kimataifa. Basi mwa kwetu najua nilikupeleka mbali lakini kina mama na dada zetu waliokuwa wakitesa enzi za miaka 95 watakubaliana na yote niliyoyasema, basi nikiwa nimejiandaa vilivyo mtoto wa kike.

    Jicho lililoregea la kungu manga nilinogeswa na wacha mwembamba wa mwezi mchanga niofundishwa kujipaka na Bi Shuu wanja huu aliniambia unaitwa karibu mpenzi. Baada ya kukamilisha na kujifisha udi mpaka kwa bi mkubwa. Nilijilaza kitandani nikiendelea kutumbuizwa na wimbo wangu wa Tx mahususi ya Mateja wangu.

    Nikiwa nimejilaza Mateja aliwasiri, kwa vile mlango ulikuwa wazi alipogonga tu mtoto wa kike nilinyanyuka kwenda kumpokea huku nikideka, jicho langu liliongea kama nina usingizi mzito, yote haya mwanzo sikuwa nayo kazi kubwa ya Bi Shuu. “Karibu Tx wangu.” “Una maana gani kuniita Tx.” “Sikiliza huu wimbo” Mateja alisikiliza kwa muda kisha alishusha pumzi ndefu na kutikisa kichwa huku akiniangalia mara mbili mbili.

    “Vipi Tx wangu?”

    “Mmh! Haya.”

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sema tu naona kama una maswali yanayohitaji majibu toka kwangu?” “Sina swali, ila kila naona mambo mapya, wee mchaga mambo ya pwani umeyajulia wapi?”

    “Kwani Bi Shuu ni mtu wa Pwani, Mmanyema mtu wa Kigomayeye kayajulia wapi? Si watu wa mwambao wa Pwani tu wanajua mapenzi.” “Mmh, nimekubali.”

    Nilimpokea koti lake na kuliweka kwenye kochi, alipokaa alimvua viatu kisha nilihamia kwenye shati nikatelemka kwenye suruali, nikatoa na nanihii kisha nikampa upande wa kanga ili nimpeke bafuni tukaoge.

    Utajiuliza kwa nini nimempa kanga badala ya taulo, mwa kwetu kanga ina raha yake, huwezi kwenda nyumba ya wageni ukakuta kanga lazima utakuta taulo. Kama mpenzi wako alizoea kwenda nyumba ya wageni ukimpa kanga lazima akili yake ataona kuna tofauti ya nyumba ya wageni na nyumbani kwa mpenzi wake.



    Baada ya kuoga tulirudi ndani kisha nilijifanya kama kuna kitu kinaniwasha na kujikuna kwa kuipandisha nguo, nilijua lazima Mateja ataangalia, nilirudisha haraka mtego wangu ulinasa, ukimuoneshamaungo nyeti nusu, lazima atataka aone kabisa kufanya vile ilikuwa kumuongezea mahanjamu. Mmh! Mtoto wa kume uzalendo ulimshinda, nimnyime ili iweje, shoga mwili wako mali ya mpenzio, hasa yule mliyeshibana.

    Alipotaka nikampa kwa nguvu zote, huku nikumuuliza baba chagua kipapatio ili usichoke sana kabla ya kula au paja ushibe kabisa. Mateja alitaka kipapatio, ushaanza- kipapatio ni nini? Wapo waliotafuta maana zao, jamani kipapatio penzi jepesi lisilochosha, nina imani hata paja ushajua. Haya twende kazi, mmh, mtoto wa kike nilijisahau na kumuongezea paja baada ya kumuona kabisa kipapatio hakimtoshi. Mwisho wa shughuli nilimwacha kajilaza na kumuwekea wimbo wa dereva huku nikimbadili jina toka Tx mpaka Dereva.

    Mateja kila aliponiangalia alitikisa kichwa. Nilimnyanyua na kumpeleka bafuni kisha nilimualika mezani. Baada ya kutafuna tonge la kwanza alitikisa kichwa na kusema: “Hakika wewe ni chura,” kauli ile ilinitisha iweje aniite chura mdudu tena nisiye mpenda. “Mpenzi kwa nini umeniita chura?” “Sina nia mbaya, nina maana chura anaishi kotekote majini na nchi kavu. Umekamili kila idara, nikiwa na na wewe raha zangu hazitakuwa na kikomo.”



    “Ha! Kumbe, Asante mpenzi.” Nilimkumbatia Mateja kwa furaha. Baada ya chakula tulipumzika chakula kiende sehemu zake baada ya hapo mtoto hakutumwa dukani. Sitaki kukuchosha sasa hivi mimi ni mke halali wa Mateja, tunapendana kwa dhati huku nikiendelea kupokea mawazo ya Bi Shuu bibi ambaye sitamsahau mpaka nakufa. Mwisho nawaomba wanawake wenzangu kutafuta dawa ya mapenzi ambayo ni kujifunza kwa waliotutangulia ili viungwe viwe vitamu wa wapenzi wetu kwani siku zote ukikitoa hamu kitakosa utamu.

    CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog