Chombezo : Kitanda Cha Mpangaji Mwenzangu
Sehemu Ya Nne (4)
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
We Halima! aliita mama Tina akiwa ameshafika.
Abee baba Tina mkeo ameshafika, ananiita nje, Halima alisema kwa sauti ya chini huku akitoka chumbani kwake.Halima alikata simu ya kuongea na baba Tina, akawa ameshafika kumsikiliza mama Tina
JIACHIE MWENYEWE SASA
Halima ulifuata nini hospitali alikolazwa mume wangu?
Kumwangalia mjomba angu mzee Semsela.
Kalazwa wodi gani?
Khaa! Sasa mama Tina kwani ilikuwa lazima ukamwangalie mpaka unanijia kwa hasira hivi?
We uliyekwenda kumpelekea chakula ni mume wangu, uongo?
Uongo.
Kweli.
We una ushahidi gani? aliuliza Halima huku akionesha dalili zote kwamba liwalo na liwe tu kuliko kunyanyaswa na mwanamke
mwenzake.
Mama Tina huku akiwa amejishika kiuno sasa, alijibu
Nimeona mabaki ya chakula chini ya kitanda cha baba Tina wakati anasema hajala na wewe ndiye uliyetoka hapa na chakula
ukasema unampelekea mjomba ako ambaye hayupo pale Palestina Hospitali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hayo mabaki ni ya chakula gani?
We ulipeleka chakula gani?
Ugali wa muhogo na kisamvu.
Muongo mkubwa wewe, ulipeleka ndizi za kupika na nyama, bisha.
Nabisha.
Halima...Halima kuwa makini sana na mume wangu, nakwambia kweli. Nikigundua...
Mimi nimeshagundua vingapi?
Kama vipi?
Iko siku utavijua tu, alisema Halima huku akizama ndani kwake.
Mama Tina aliondoka akiwa na hasira sana. alitamani sana kumvaa msichana huyo hasa alipogundua amekuwa akimfuatafuata sana na
kumtangaza kwa watu kwamba anatembea na Os Anjelus.
***
Baba Tina alitoka hospitali na siku hiyo alikuwa nyumbani. Mpaka hapo hakuwa amemwambia mke wake maneno aliyoambiwa na Halima
kuhusu mpangaji mgeni, Os Anjelus.
Halima alikuwa akitoka kwenda kwenye saluni yake, akamuona baba Tina...
Shikamoo baba Tina.
Marhaba, mzima?
Mimi ni mzima. Haijambo familia yako?
Ipo sawa. Naona unakwenda kuwajibika sasa?
Hivi Halima, mume wangu amekuwa wa kumzoea siku hizi siyo? mama Tina aliingilia kati huku akitoka nje. Halima hakumjibu
kitu zaidi ya kumtumbulia macho tu, naye akaondoka zake.
Alipofika saluni aliwaza sana kuhusu hali ya mama Tina kwa sasa, akajiuliza yeye na mama Tina nani anastahili kuwa mkali kwa
mwenzake?
Dawa yako inachemka, iko siku nitashikana naye mbele ya mtoto wake, nitamchakaza ile sura anayoringia, alisema moyoni
Halima.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mara meseji iliingia kwenye simu yake kutoka kwa baba Tina...
Samehe kwa yote yaliyotokea Halima, huyu mwanamke kachanganyikiwa.
Halima hakuijibu mapema meseji hiyo, lakini ulipofika wakati wa kujibu alisema...
Nadhani hujamwambia kama umepata habari analala na mpangaji mgeni ndiyo maana anatamba mbele yangu.
Halima, sijamwambia. Kwanza nataka nisaidie jambo moja tu, hakikisha unawafuatilia kwa karibu hata kukulipa nitakulipa
ilimradi niwanase.
Hilo dogo kwangu, nipe siku tatu.
Halima aliona amepwa dili, kwake suala si kulipwa bali ni kuhakikisha anamchomoa mama Tina kwenye ndoa yake.
***
Siku ya pili, saa kumi na moja jioni, Halima alirudi nyumbani akiamini Os Anjelus naye atakuwa amerudi. Alijua lazima mama
Tina atataka kuonesha kumjua sana kijana huyo na kuingia kwake.
Baba Tina alikuwa kazini siku hiyo, mama Tina alikuwepo nyumbani, Os Anjelus aliingia muda aliofikia Halima na walisalimiana.
Kuna wakati mama Tina alitoka ndani kwake, akaenda kwa Os Anjelus na aliingia bila kubisha hodi akijua kama angefanya hivyo
Halima angesikia...
Baby nimekumisi ile mbaya, please kama hutajali leo tutoke kabla mume wangu hajarudi, humu ndani kidudu mtu ameshaingia
hatuwezi kufaidi chochote, mama Tina alimwambia Os Anjelus.
Os Anjelus alikubali na walipatana wakutane kwenye gesti moja waliyoelekezana.
Mama Tina ndiye aliyetangulia kutoka, akampeleka Tina kwa shoga yake jirani.
Wakati anaufunga mlango wake kwa funguo, Halima alisikia, akawa makini kufuatilia. Aligundua mama Tina ametoka. Akaanza kuwa makini na Os Anjelus ambaye naye alitoka baada ya dakika kumi na tano.
"Hapa patamu sasa," alisema Halima na yeye akitoka kwa machale asionekane.
Alifuata nyendo za Os Anjelus hadi alipoingia kwenye gesti hiyo. Lakini akawa hajui kama mama Tina alishaingia au atafuata nyuma. Akampigia simu baba Tina kumpa taarifa.
"Unasema kweli Halima?"
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kweli kabisa, mimi nimebana mahali hapa jirani."
"Basi nakuja sasa hivi. Lakini unasema mama Tina hujamwona?"
"Sijamwona, huenda ameshaingia ndani au anakuja. Nitakwambia."
Baba Tina alijikusanya na kwenda mpaka alipo Tina na kukutana naye. Walizungumza mawili matatu jinsi ya kufanya maana mpaka muda huo, mama Tina hakuonekana kuingia.
"Sasa tufanyeje Halima?" aliuliza baba Tina.
"Twende tukachukue chumba na sisi, halafu kiwe jirani na mlango na dirisha lake liwe linaangalia nje. Tutafanya upelelezi tukiwa mlemle ndani tutajua kila kitu," Halima alitoa wazo.
"Kweli, si watatuchenga ndani kwa ndani?"
"Watapitia wapi kama chumba chetu ni cha dirishani. Maana ujue kwamba tukikurupuka tumetibua kila kitu."
"Lakini kweli, basi twende."
Walitembea na kuzama kwenye gesti hiyo, wakaomba chumba.
"Lakini tunataka chumba ambacho dirisha lake liwe jirani na mlango mkubwa wa kutokea," alisema Halima.
"Kipo kimoja lakini feni halifanyi kazi."
"Tupe tu," alidakia baba Tina.
Mhudumu aliwapa chumba cha namna hiyo. Kabla hawajatoka mapokezi, Halima alimuuliza...
"Eti, kuna kijana ameingia, mrefu kiasi, mweupe, ana nywele nyingi?"
"Ndiyo."
"Amejaza jina gani?"
"Amejazaaa...aaa. amejaza Os Anjelus."
Halima na baba Tina walitazamana baada ya jibu hilo la mhudumu, Halima akauliza tena...
"Ameingia na nani?"
"Kaingia peke yake, lakini amesema kuna mgeni wake anakuja muda si mrefu."
"Chumba namba ngapi?" aliuliza baba Tina.
"Sita, kile kama unatoka uani."
Halima alimshika mkono baba Tina na kumwingiza haraka kwenye chumba chao ambapo kwa maelezo ya mhudumu kuwa mgeni wa Os Anjelus anakwenda, alijua wakiwa kwenye chumba hicho wataweza kumwona vizuri mama Tina akiingia.
Sasa walikuwa chumbani wamekaa kitandani. Kila baada ya dakika moja, mmoja wao alisimamisha shingo na kuchungulia nje kupitia dirishani.
Hata pale waliposikia kama mtu anatembea kuelekea gesti hiyo walisimamisha shingo wote kwa pamoja na kuchungulia.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Joto ndani ya chumba hicho lilikuwa kubwa kiasi kwamba, Halima alianza kulalamika. Feni ilikuwa haifanyi kazi kweli kama alivyosema mhudumu.
"Du! Hili joto tutaishije humu ndani yarabi?"
"Labda uvue hicho kijaketi chako cha jinsi," baba Tina alimshauri.
"Mh! Tatizo kiblauzi nilichovaa ndani kinaonesha kila kitu, ni kama nitakuwa sijavaa nguo."
"Basi vumilia," alisema baba Tina akiwa ameinua shingo kidogo kutazama nje.
"Mh! Mwenzangu afadhali nivue tu, nitakosa pumzi bure kwa joto," alisema Halima huku akianza kuvua jaketi hilo.
Kweli ndani alivaa blauzi yenye kitambaa chepesi sana kiasi kwamba baba Tina aliweza kuona kila kitu, sasa angefanyaje Halima na joto lile.
"Kumbe binti umeumbika! Naona kifua chako kiko vizuri kweli, umejaliwa," baba Tina alimtania Halima...
"Mmmh! Kwani cha mama Tina kikoje?"
"Cha mama Tina si kama chako, hebu angalia hizi nido zako zilivyochongoka," hapo baba Tina alishikwa tamaa, akapeleka mkono kushika nizo za Halima, akasisimka.
"Baba Tina bwana, huko nako wapi sasa? Tunatamanishana bure," alisema Halima.
"Aaa! Kivipi bwana? We vumilia tu, hapa tumekuja kikazi," alijibu baba Tina bila kutoa mkono wake kwenye nido za Halima.
Kitendo hicho kilimfanya Halima azidi kuchanganyikiwa kiasi kwamba alijikuta akiangukia kitandani puu.
Baba Tina naye kama binadamu, kama mwanaume rijali alipagawa kwa kuona sehemu ya mwili ya Halima.
"Lakini lazima tujikaze Halima ili heshima yetu iwe palepale, mimi ni kama baba yako."
"Si ndiyo nakushangaa wewe unaanza uchokozi wako."
"Sikuchokozi tena Halima, sawa mama?" alisema baba Tina na kumshika begani Halima...
"Sawa, lakini sasa mbona unanishika jamani si ndiyo uchokozi wenyewe huo?" alilalamika Halima huku akikatakata sauti yake.
Baba Tina alimwinamia mpangaji mwenzake huyo na kumkodolea macho hali iliyomfanya Halima naye kuwa hivyohivyo. Walitazamana kwa karibu dakika moja nzima huku hakuna mwenye sura inayoonesha kuna utani wala kucheka.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Halima alijikuta akiinua kichwa chake polepole na kumgusa baba Tina kwenye midomo kwa kutumia midomo yake.
"Baba Tina," aliita kwa sauti iliyojaa uvivu wa hali ya juu.
"Mm."
"Sasa?"
"Kuhusu nini?"
"Mmh! Mwenzako nimepatikana bila kutarajia. Unajua mimi nani zangu ziko karibu sana, yaani mwanaume akinigusa tu, hasa tukiwa sehemu ya faraga kama hii basi nakuwa hoi."
"Sasa?"
"Sidhani kama kuna cha kusubiri, ila imebidi tu baba angu kutokana na hali yenyewe."
"Kwa hiyo?"
"Tuingie kazini tu, tutafanyaje sasa unadhani?"
"Lakini Halima wewe ni mwanangu."
"Najua baba. Kwa hiyo?"
"Mimi nadhani tuwe wavumilivu tu, tuhangaikie lililotuleta."
"Please baba Tina, niko vibaya," alisema Halima huku nyuso zao zikiwa umbali wa kiganja cha mkono.
"Unajua nini Halima?"
"Ee?"
"Tukivunja amri ya sita tutashindwa hata kuwashitaki wenzetu ambao tunaona wanatusaliti."
"Noo. Mama Tina alikosea, yeye alidhamiria kutembea na yule kijana, sisi tumejikuta katika bahati mbaya kutokana na mazingira," alisema Halima akimvutia kwake baba Tina, naye akaenda mpaka akalala kwenye kifua.
"Baba Tina."
"Naam."
"Kimebaki nini sasa?"
* * *
Mama Tina alipita mapokezi, mhudumu hakumwambia chochote kama aliuliziwa na watu ambao walichukua chumba cha mwanzo ndani ya gesti hiyo.
"Habari gani anti?" mama Tina alimsalimia mhudumu.
"Nzuri, karibu sana."
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nina mgeni, kaniambia chumba alicho."
"Sawa karibu sana."
Mama Tina alisukuma mlango na kuzama ndani alikokuwa Os Anjelus. Kijana huyo aliona ni nafasi ya kumwonesha mwanamke huyo mapenzi ya dhati ambapo alisimama na kumkumbatia, kisha akampiga mabusu yasiyo na idadi yaliyomchanganya kabisa mama Tina mpaka akajikuta akilegea miguu na kutamani kukaa.
"Baby, unajua nakupenda sana?" alisema Os Anjelus...
"Hata mimi baby, nakupendaaaa..."
"Basi tuzidi kupendana," alisema kijana huyo na kumkumbatia tena, wakala denda tulivu huku wakigugumia kwa sauti za mahaba mazito.
* * *
Kule chumbani kwa baba Tina na Halima, sasa wote walikuwa kama walivyozaliwa. Baba Tina alishasaula bila kushurutishwa, weupe wa mapaja ya Halima ulimchengua, akahisi atafaidi sana kwa mchepuko huo.
"Jamani, yaani tumekuja kufumania lakini matokeo yake tunaweza kufumaniwa sisi," alisema baba Tina, Halima akacheka kwa sauti ya juu, ikaingia chumbani aliko Os Anjelus, mama Tina akashtuka kuisikia maana aliijua.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment