Chombezo: Vitilivyogo ( Papa na Muhogo )
Sehemu Ya Nne (4)
Wakati huo muda nao ulikuwa umekwenda sana, hakutaka kujilaza kwa kuhofia kumkuta kama aliyokutana nayo kwa Stella alipojikuta akirudi nyumbani usiku mkubwa kitu ambacho kingeanza kuwatia wasiwasi wazazi wake pia hata kwa mpenzi wake Betty.
Muda wote aliokuwa amejilaza pembeni ya Diana, mwenzake alikuwa amejilaza akionesha si wa kuamka muda ule kutokana na kuonekana amechoka sana.
Ilibidi amuamshe kwa kumwita huku akimtikisa.
“Diana.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Bon niache nimechoka,” Diana alijikuta akichanganya madawa kwa kufikiri yupo na mpenzi wake wa siku zote Bon, lakini hiyo haikumshtua Shaka aliendelea kumuamsha.
“Muda umekwenda sana Diana amka tuondoke.”
“Bon, imeanza lini kuamshana kuwa muda umekwenda au leo una mwanamke mwingine?”
“Diana mimi siyo Bon,” Shaka alisema baada ya kuona Diana anachanganya madawa.
Kauli ile ilimfanya afumbue macho na kumkuta ni Shaka, alishtuka na kumuuliza:
“Eti Shaka nimekuita nani?”
“Bon.”
“Ooh! Sorry Shaka,” Diana alisema kwa aibu.
“Samahani ya nini?”
“Kukuita Bon.”
“Kwani Bon ndiye nani?”
“Aa..aah! Wacha tu,” Diana alionesha uso wa taharuki.
“Au ndiyo shemeji?”
“Hakuna ni mdogo wangu hupenda kunisumbua ninapokuwa nimelala.”
“Mmh! Sawa,” Shaka alijibu kwa sauti ya chini.
“Jamani Shaka usinifikirie vibaya.”
“Kuhusu nini Diana mbona unajishtukia, nimekuamsha ili nikueleze tuondoke na si kubishana.”
“Lakini naomba usinielewe vibaya, nina imani utajua tu nina mwanaume mwingine.”
“Diana kipi cha ajabu sijakukuta na usichana hivyo wala lisikuumize kichwa, la kawaida, la muhimu nimekuamsha ili tuondoke nitachelewa nyumbani si unajua nimeondoka bila kuaga.”
“Sawa, lakini naomba kwanza uamini sina mwanaume anayeitwa Bon.”
“Ila?”
“Sina kabisa mwanaume kwa sasa, nilitaka niwe na wewe lakini Stella kaniwahi.”
“Kwa hiyo?”
“Basi tuache,” Diana hakuwa na jibu baada ya kuchanganya madawa na kujiuliza siku akiwa na Bon na kumtaja Shaka sijui itakuwaje kutokana na Bon kuwa na wivu kama dume la mbwa.
Baada ya kwenda kuoga kwa pamoja walirudi kuvaa nguo na kutoka huku Diana akimpa Shaka elfu hamsini japo alipanga kumpa elfu kumi kwa kujua atampaka shombo. Lakini alichokutana nacho na kosa la kuchanganya madawa alitoa elfu hamsini bila kupenda katika laki moja aliyopewa na bwana yake Bon ambaye pamoja na kuwa mtu mzima kidogo lakini hakuwa mtundu kama Shaka.
Hakujua utundu ule aliongezewa na Betty na kumfanya Shaka awe moto mkali kutokana na uwezo wake wa damu changa na utundu mdogo alioongezewa.
“Shaka lakini naomba usinielewe vibaya,” bado Diana aliendelea kujitetea kwa kuhofia Shaka kumtema mapema.
“Sikiliza Diana wewe si mke wangu hata kama yupo Bon siwezi kumkasirikia, pengine Bon ndiye anayetufanya tupendeze. Basi wewe kuwa na amani moyoni mwako,” Shaka alimtoa Diana wasiwasi.
“Sawa nimekuelewa.”
Diana alimkodia teksi Shaka mpaka kwao, alipofika waliteremka pamoja na kumsindikiza kidogo, walipofika kwenye uchochoro Diana alimweleza Shaka:
“Shaka naomba siri asijue Stella, lazima tutakorofishana anakupenda sana.”
“Diana hivi mnaniona mtoto mdogo sana?” Shaka alimuuliza huku amemkazia macho.
“Hapana Shaka huenda akakudodosa na wewe ukajisahau.”
“Siwezi labda wewe umwambie.”
“Siwezi, Shaka tutaonana kesho shule.”
“Ila acha kupagawa tukifika kila mtu ajifanye hamjui mwenzake siyo kujifanya unanijua sana nitakutoa nishai.”
“Siwezi Shaka namheshimu sana Stella.”
“Mbona umekula raha zake?”
“Uzalendo ulinishinda.”
“Haya, siku njema.”
“Bai Shaka.”
“Bai Ste..ooh! Sorry Diana.”
“Shaka najua unalipa kisasi cha kukutajia Bon.”
“Walaa, ulimi hauna mfupa tu, lakini sina mawazo hayo.”
“Haya, mimi nifanyeje na nimeishalikoroga mwenyewe.”
“Walaaa usiwe mnyonge, ili kujua sina hata moja, siku utakayoniita utajua kweli ninayo au sina.”
“Nitashukuru sana Shaka.”
“Haya wahi mama.”
“Asante....mmmwa.”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Diana alifurahishwa na maneno ya Shaka na kumbusu kisha alikimbilia kwenye gari na kumwacha Shaka akienda kwao huku akishukuru siku ile Betty kutokuwepo maeneo yale alimueleza angerudi usiku na kukubaliana kuonana siku ya pili. Kutokana na kuchoka sana alishukuru kutokuwepo kwani lazima angetaka mchezo angechemka.
***
Siku ya Jumatatu Shaka alikwenda shuleni akiwa na wasiwasi wa kugombana na kipenzi chake Stella kwa kuhofia kujua uhusiano wake na shoga yake Diana. Lakini ilikuwa tofauti hata alipokutana na Stella akiwa ameongozana na Diana hakukuwa na kitu chochote zaidi ya kumwita Shaka shemeji.
“Za wikiendi mpenzi?” Stella alijishaua mbele ya mpenzi wake bila kujua jana yake shoga yake katia mkono kwenye kapu lake la burudani.
“Nzuri.”
“Nilikuwa na mzuka na wewe ile mbaya sema tu nilikwenda shamba na mama.”
“Siku si zipo.”
“Yaani nilikasirika kidogo nipasuke baada ya kuvimba kwa hasira, tena ndiyo nilikuwa najiandaa kuja kwenu mama akaniita eti nimsindikize shamba.”
“Pole mpenzi,” Shaka alisema huku akimshukuru mama Stella kuepusha shari.
“Shaka leo lazima unipe raha nilizozikosa jana lazima unipe.”
“Hakuna tatizo mpenzi.”
Kengele ya mstarini iliwakatisha mazungumzo.
“Shaka tutazungumza mapumziko,” Stella alisema huku akimpatia Shaka elfu kumi ya matumizi.
Shaka alipokea na kukimbilia mstarini na kumuacha Stella akimsindikiza kwa macho na kujitapa kwa shoga yake:
“Yaani sema tu bado tunasoma, tungekuwa kidato cha sita, baada ya mtihani angenioa hata chuo nisingeenda.”
“Shoga acha kuchanganyikiwa.”
“Lazima nichanganyikiwe mara ngapi nimeteswa na Twalipo, ni wewe uliyekuwa ukinipa sifa za Bon kukuliza kilio cha mbwa mwizi mwenzio nilikuwa naumia ile mbaya lakini sikuwa na jinsi. Lakini toka nilipokutana na Shaka, kweli udogo wa mchi wa kutwangia viungo vya pilau lakini ndio unaoleta harufu nzuri ya chakula.”
“Sawa lakini unachanganyikiwa vibaya kila mtu atajua Shaka mpenzi wako na kukudharau na kukuona umepotea njia kwa kuwakataa wakina Steve mwenye mishiko ya haja.”
“Steve wa nini, kwanza nasikia umeshadondoka na Steve kwa hiyo ulitaka tuchangie mwanaume?”
“Wewe! Umejuaje?”
“Japo ulifanya siri lakini kila kitu chako kipo hapa mkononi.”
“Mmh! Si alijipendekeza siku ya kwanza kukutana naye alinipa laki tatu niziache nimerogwa.”
“Basi mimi kwa Shaka nataka penzi si pesa, huyo Steve aliishawahi niahidi milioni kama nitamvulia nguo yangu ya ndani siku moja. Lakini nilimwambia sina dhiki ya fedha wala mimi si dada poa.”
“Basi shoga yanatosha, tuwahi mstarini,” Diana alibadili mada baada ya kuona amechokoza nyuki na mbio hana.
“Bado hayajatosha, tena nina mpango wa kujitangaza kuwa Shaka ni mchumba wangu ili wasio na haya wamkome.”
“Stellaaa! Unataka ufukuzwe shule.”
“Wana ubavu huo, ehe! Nilitaka kusahau nasikia Steve anatembea na mwalimu Monica.”
”Muongo!”
“Wala sishangai kwa yule mwalimu anapenda sana usister du.”
“Mmh! Kwa hiyo mke mwenzangu?”
“Lakini Diana wewe si umesema Bon anakupa kila kitu?”
“Ndiyo.”
“Sasa kwa nini usitulie naye kuliko kurukaruka ona mnavyochanganywa na mwanaume mmoja. Unafikiri Steve ana mpenzi mmoja hapa shuleni? Acha tamaa mtoto wa kike tulia na mmoja!”
“Dada wewee! Alijipendekeza na vijihela vyake niviache nimerogwa?”
“Ulijipendekeza mbona bado nasikia unakwenda naye kila siku.”
“Shoga, ukimchunguza sana bata humli.”
“Nimekuelewa tuwahi mstarini.”
***
Jioni ya siku ile Stella hakuwa na hamu na Shaka kwani alitaka apumzike angalau kwa siku mbili ndipo alianzishe tena. Lakini ilikuwa tofauti na shoga yake Diana ambaye alitamani mchezo wa marudiano.
Pamoja na kupata kipigo cha pweza bado aliamini Shaka alibahatisha. Lakini ukabaji wa Stella wa kutompa nafasi Shaka ulimnyima raha alikosa hata nafasi ya kutia neno. Alipanga kama atamkosa siku za kawaida basi wikiendi kama kawaida atamzukia kwao.
Stella alimkodia Shaka Bajaj huku akimweleza dereva.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Kaka hakikisha unamshushia mlangoni kwao.”
“Hakuna tatizo.”
“Bai my husband,” Stella alimuaga Shaka kwa kumbusu mbele ya Diana ambaye aliangalia pembeni kwa wivu.
“Bai my wife,” Shaka naye alimbusu na kumkumbatia Stella huku akimminya jicho Diana.
Dereva aliondoa Bajaj na kuwaacha Stella na Diana wakimsindikiza kwa macho.
“Dogo vipi?” dereva wa Bajaj alimsemesha Shaka.
“Poa bro.”
“Yule demu mkaliii, wako?”
“Kwani vipi?”
“Naona kama maigizo vile hamuendani.”
“Elewa ulivyoelewa.”
“Au shemeji yako?”
“Bhana eeh, sipo mahakamani, awe asiwe demu wangu wewe unapungukiwa na nini?” Shaka alikuwa mkali kidogo.
“Basi dogo yameisha, lakini kama kweli wee mkali.”
“Haikuhusu.”
***
Shaka akiwa anaelekea nyumbani kwao baada ya kushuka kwenye Bajaj alishtuliwa kwa sauti iliyokuwa ikimwita nyuma:
“Shaaaka..Shaaaka.”
Shaka aligeuka kuangalia nani anayemwita, alikuta ni shoga wa Betty.
“Aah! Da’ Edna shikamoo.”
“Asante, za shule?”
“Nzuri tu.”
“Shaka una kazi gani ukifika nyumbani?”
“Mmh! Sina ila Betty aliniambia nikitoka shule niende kwake.”
“Sasa ni hivi nilikuwa na shida na wewe mara moja.”
“Shida gani?”
“Nitakwambia kabadili nguo basi.”
“Kwa hiyo nije kwako?”
“Mmh! Fanya hivi,” Edna aliweka kidole mdomoni kutafuta neno na kumfanya Shaka amtazame usoni na kumuuliza.
“Kwani shida ni kubwa?” Shaka aliuliza.
“Fanya hi..hi..vi....”
“Shaaakaaaa.”
Sauti ya Betty ilikatisha mazungumzo, walipogeuka walimuona akija akiwa amependeza kimtoko.
“Shaka akikuuliza usimwambie tulichozungumza.”
“Poa.”
“Diana vipi unazungumza nini na mpenzi wangu?” Betty aliuliza huku akisogea walipokuwa wamesimama
“Jamani Betty nizungumze nini na Shaka?” Diana alijibalaguza.
“Inawezekana umeanza kumzengea, oho! Tutatoana meno.”
“Shoga mbona mi namchukulia Shaka kama mdogo wangu tu.”
“Shaka unazungumza nini na Diana?” Betty alimkazia macho Shaka.
“Betty kwa nini umeniuliza swali hilo?”
“Shaka nataka jibu siyo swali juu ya swali,” Betty alisema kwa ukali.
“Au kwa vile mi mdogo ndo unanikosea heshima mbele ya rafiki yako, yaani unaniuliza kama mtoto mdogo?” Shaka naye aligeuka mbogo.
“Siyo hivyo Shaka siku hizi mashoga hatuaminiani, naweza kumuamini akanigeuzia kibao.”
“Kwa hiyo mi nimekuwa baba huruma wa mtaa siyo?”
“Hapana shaka nilikuwa na wasiwasi tu,” Betty ilibidi awe mpole.
“Kwa hiyo ndiyo kazi yenu kuchukuliana wanaume?”
“Walaa, lakini siku zote nyuki mkali kwa asali yake.”
“Basi ondoa wasiwasi asali yako ipo salama.”
“Shaka, tuzungumze pembeni.”
“Safari ya wapi mbona umependeza?”
“Tutazungumza.”
Betty alimshika mkono Shaka na kusogea naye pembeni mbali na Diana na kumuacha kasimama peke yake.
“Vipi mpenzi? Shaka alimuuliza.
“Poa, Shaka nakwenda kwa Jimmy kaniita sijui kuna sherehe gani.”
“Sasa itakuwaje nami leo nilikuwa na hamu na wewe?” Shaka alitikisa kiberiti.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Jamani shaka imeanza lini?” Betty alijitetea.
“Leo.”
“Sasa itakuwaje mtu nimeshamkubalia nakwenda, heri ungenieleza mapema nikajua cha kumweleza.”
“Kwa hiyo itakuwaje?”
“Shaka naomba basi leo uniache niende nikirudi nitakushtua.”
“Ili?”
“Ujilie vyako.”
“Yaani mimi nile makombo?”
“Siyo makombo bebi, simpi mchezo akitaka nitasingizia ugonjwa ili nikuletee kitu kamili.”
“Kama kweli unanipenda mi nataka usiende.”
“Sawa Shaka siendi,” Betty alisema kwa shingo upande.
“Naona kama hujaridhika?”
“Walaa nataka kukuonesha jinsi gani nakupenda, twende basi ukabadili twende homu.”
“Nikuambie kitu?” Shaka alimuuliza Betty aliyekuwa amegeuka warudi nyumbani.
“Niambie mpenzi.”
“Nimeamini unanipenda.”
“Shaka hilo jibu uliza swali.”
“Betty nenda kwa Jimmy.”
“Nikafanye nini?”
“Kwani ulikuwa unakwenda kufanya nini?”
“Nimeshaghaili.”
“Hapana mpenzi sikuwa na nia ya kukuzuia bali nilitaka kuona kama kweli nina sauti mbele yako.”
“Kwa hiyo ulikuwa unanitania?”
“Si kukutania bali kutaka kujitambua mimi nani kwako.”
“Wewe ni zaidi ya Jimmy wacha kunikataza kwenda hata ukiniambia niachane naye nipo tayari.”
“Usifanye hivyo muwahi mshikaji.”
“Umeridhika?”
“Kiroho safi.”
“Basi acha niwahi, usiku na kazi na wewe.”
“Poa.”
“Edna baadaye shoga.”
“Wapi tena?”
“Aah! Nilikuaga nakwenda wapi?”
“Ooh! Nimekumbuka, ndo kesho hiyo?”
“Walaa lazima nirudi.”
“Wewe nani asiyekujua lazima uutwike kisawasawa.”
“Na Shaka nimuachie nani?”
“Mmh! Haya basi wahi.”
Betty alifungua pochi na kutoa wekundu wawili na kumpa Shaka.
“Mpenzi utakunywa soda.”
“Asante.”
Wakati wakizungumza teksi ilisimama mbele, Betty alimbusu Shaka na kuingia ndani ya gari ambalo liliondoka. Baada ya gari kuondoka Shaka alimrudia Edna aliyekuwa bado amesimama.
“Da Edna ulikuwa unasemaje maana Betty amekatisha mazungumzo yetu?”
“Kwani Betty amekwambia anarudi saa ngapi?”
“Edna tuzungumze yetu ya Betty hayakuhusu.”
“Shaka kuna kazi nilitaka unisaidie nyumbani.”
“Kazi gani?”
“Kupigilia msumari ukutani.”
“Poa basi nakuja.”
Shaka aliagana na Edna bila kujua ule ulikuwa mtego wa panya, alikwenda mpaka kwao na kubadili nguo kisha alikwenda kwa Edna aliyekuwa akikaa jirani na Betty.
***
Edna baada ya kuachana na Shaka alikwenda kwake kujiandaa kwa ajili ya kutimiza lengo lake. Alipofika alikwenda haraka bafuni kuoga na kujifunga upande wa khanga bila nguo ya ndani.
Kutokana na maji kulowesha khanga aliyojifunga ilifanya kugandia mwilini na kuchora ramani ya mwili wake mantashau wenye kuwatoa udenda wanaume mashababi ambao hakuwaza hata siku kumvulia nguo ya ndani mtoto mdogo kama Shaka.
Japokuwa mwanzo alimponda shoga yake kutembea na mtoto mdogo na kuona anajidhalilisha, lakini sifa alizozitoa kwa Shaka zilimshauri kutoka nje ya ndoa yake na kuuonja utamu wa mtoto mdogo.
Alitumia nafasi ile kupima maji kama ya magoti au ya shingo yanayoweza kumzamisha mtu. Alimfahamu vizuri shoga yake Betty ni mwanamke wa shoka ambaye hawakufichana kitu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alimweleza udhaifu wa mpenzi wake naye alimueleza udhaifu wa mume wake. Lakini alimmwagia sifa Shaka kijana mdogo kuwa shughuli alikuwa akiiweza.
Sifa zile zilimfanya naye aingie kichwakichwa ili kutaka kujiridhisha maneno ya shoga yake japokuwa bado aliamini Shaka asingekidhi haja zake.
Baada ya kutoka kuoga alifunga vioo vya madirisha ili mchezo ukichezwa kelele zisitoke nje na kuwapa faida majirani. Akiwa anamalizia kufunga dirisha la mwisho alisikia hodi mlangoni.
Sauti ilimjulisha ni Shaka amefika, alikwenda haraka mlangoni na kufungua na kukutana naye uso kwa uso. Vazi la khanga moja lilimshtua sana Shaka na kuamini Edna alikuwa ndani na mumewe.
“Karibu Shaka.”
“Asante,” Shaka aliitikia bila kuingia ndani.
“Mbona huingii?” Edna alimshangaa Shaka.
“Na..na..”
“Hebu ingia,” Edna alimshika mkono Shaka na kumvutia ndani.
Kabla Shaka hajajua nini kinaendelea, Edna alifunga mlango na funguo kisha aliuchomoa na kuutupia kwenye kochi. Baada ya kugeuka alikuta Shaka amesimama akimshangaa.
“Shaka mbona hukai?”
“Nionyeshe kazi uliyoniitia niwahi nyumbani kuna kazi nimepewa na mama.”
“Hakuna tatizo njoo basi nikuoneshe uwahi kwenu.”
Edna alisema huku akimshika mkono na kuingia naye chumbani.
Shaka aliingia chumbani huku akitetemeka kitu ambacho Edna alikigundua na kumtoa wasiwasi.
“Shaka,” alimwita huku akimtazama usoni kwa jicho la huruma.
“Naa..aam.”
“Mbona nakuona kama una wasiwasi?”
“Hata nipo sawa.”
“Sasa mbona hujiamini.”
“Hapana niko poa.”
“Muongo! Sijui kama kazi yangu utaifanya vizuri.”
“Nitaifanya, nioneshe niifanye.”
“Panda kitandani usimame upande wa ukutani nikuonyeshe hiyo kazi.”
“Msumari na nyundo vipo wapi?” Shaka aliuliza baada ya kupanda kitandani na kusimama karibia na ukutani.
“Hebu teremka kwanza.”
Shaka aliteremka kitandani na kusimama chini kusubiri maelekezo. Edna alipanda kitandani na kumpa mgongo, akiwa kama anataka kumuelekeza jambo aliidondosha khanga kwa makusudi na kumfanya Shaka ashtuke.
Kiunoni kwa Edna kulisheheni chachandu za rangi za aina mbalimbali. Kitu kama kile aliwahi kukiona kwa dada mmoja jirani yake aliyekuwa akioga na kumpiga chabo, lakini siku ile alikiona ‘live’.
Edna hakuijali khanga iliyodondoka aliendelea kutoa maelekezo.
“Sasa Shaka unaona sehemu hii...”
Shaka alijikuta akiganda macho katika mzigo wa haja ambao haukuwa tofauti na wa Betty lakini ile ilizidi kidogo na kuwa vidimpozi vilivyoongeza ushawishi wa kutamani kulalia godoro lile la Mchina.
Hali ya Shaka ilikuwa mbaya baada ya jogoo kukurupuka bandani na kuanza kuwika ovyo kama kapandwa na wazimu. Alijitahidi kuzuia mwinuko kwa mkono, lakini ilikuwa kazi kubwa kuuzuia kwani alikuwa kama umeumuliwa kwa hamira.
Alishindwa kumuelewa Edna shida yake ilikuwa nini. Kufanya vitu kama vile ikiwa mke wa mtu, hata kama angekuwa anamtaka basi angetafuta sehemu nyingine lakini sio pale nyumbani kwake.
“Shaka,” Edna alimwita huku akiteremka kitandani na kumfuata alipokuwa amesimama kama sanamu.
“Mmh!”
“Vipi?” Edna alisema kwa shida kwa kujilazimisha huku pumzi za ashki zikimtoka kwa shida.
“Sa..sa..fi.” Shaka alipata kigugumizi.
Alijibu kwa kukata maneno baada ya kusisimkwa na mwili kutokana na kushikwa na Edna na kuvutiwa kwenye mwili mtupu uliokuwa umechemka kwa joto tamu lenye hamu isiyoisha utamu.
“Na..na..na.”
Edna alijikuta akikosa kujiamini kwa mtoto mdogo kama Shaka wakati siku zote alijiamini ni mwanamke wa shoka mbele ya mwanaume yeyote shababi.
Lakini alijishangaa kwa kijana ambaye hata mkononi hajai kujiona kama ndiyo siku ya kwanza kukutana na mwanaume baada ya kuvunja ungo.
“Mmh!”
Shaka naye alishindwa kunyanyua mdomo, joto la hofu lilimpanda na kujikuta akivuja jasho. Edna baada ya kukosa la kumweleza alijikuta akimbeba juujuu mpaka kitandani.
Baada ya kumtanguliza chini aliona kufungua vifungo anachelewa kwa hamu ya juisi ya madafu. Alijikuta akikata vifungo vya kaptura na kuiteremsha ambayo ilitoka mbili kwa moja, chumba na sebule.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kutokana na kupandwa na maruhani ya burudani alijikuta akirusha nguo za Shaka bila kuangalia zinaangukia wapi, kama mtu anayebaka kichakani.
Kwa vile moto ulishawaka, alitega chungu jikoni na kuanza kupika. Edna alihaha kama mbwa wa polisi aliyemuona kibaka. Hakuchukua muda dafu lilimpiga kichwani na kupasuka.
“Sha..Sha..kaaa, siamini,” alimkumbatia kwa nguvu kuacha dafu limwage maji.
Shaka kutokana na kucheza mchezo kwa woga alijikuta akizuia sana kuliko kushambulia na kumfanya Edna apate wakati mgumu muda wote.
Muda wote wa mchezo Shaka hakuwa mchezoni mawazo yote yalikuwa katika kufumaniwa kitu kilichomfanya Edna apate kipigo cha mwana ukome kwa kudondokewa na kole la madafu matano yaliyompasukia na kumfanya awe hoi.
“Sh..Sha..Sha..ka hujafika tu?” alimuuliza kwa sauti ya mtu aliyekuwa akipanda mlima na pumzi kumtoka kwa shida.
Kauli ile ilimshtua Shaka na kujikuta akirudi mchezoni. Alijishangaa kuacha kufurahia utamu wa nyama iliyonona.
“Shaka wee kiboko, maliza basi mwenzio nimechoka.”
Shaka baada ya kurudi mchezoni hakuchelewa kumwaga mzigo na kutulia. Edna alikuwa kama mgema aliyedondoka kwenye mnazi kwa kuti aliloliamini.
“Shaka unatisha, umenigeuza Goliati.”
Shaka hakujibu kitu, akili yake ilikuwa katika kufumaniwa tu. Edna alijilaza kwa kujiachia kutokana na kuchoka sana, hakuchukua muda usingizi ulimpitia.
Shaka hakutaka kusubiri kitu, alivaa nguo zake haraka bila kumuaga, alitoka hadi sebuleni na kuutafuta ufunguo. Baada ya kuupata alifungua mlango akitaka kutoka.
Alipochungulia nje ili atoke alishtuka kumuona mume wa Edna akiwa uani akizungumza na majirani zake. Alirudi ndani haraka huku akitetemeka, alijiuliza ajifiche wapi.
Wazo la haraka alirudi chumbani kwenda kumuamsha Edna.
“Da’ Edna amka mumeo karudi.”
“Wewe acha utani!” Edna alikurupuka alipokuwa amelala na kujifunga upande wa khanga huku macho akiyatoa pima.
“Umemuona wapi?”
“Uani anazungumza na jirani zake.”
“Mungu wangu!”
“Sasa nitafanya nini? Ndiyo niliyakataa sasa itakuwaje?” Shaka aliuliza huku akitetemeka.
“Hebu tulia, twende.”
Edna alimshika mkono na kutoka naye nje, alipofika sebuleni alipitia noti ya elfu tano iliyokuwa juu ya meza.
“Nitakupa hela ukaninunulie dawa.”
“Kisha nilete?” Shaka alishtuka.
“Hapana, usinunue wala nini wewe nenda zako natumia njia ya kukutoa ili mume wangu asijue chochote.”
“Sawa.”
Alifungua mlango na kusema kwa sauti iliyowafanya wote waangalie akiwemo mumewe.
“Shaka kaninunulie dawa ya kichwa fanya haraka,” alimpa noti ya elfu tano.
Alimpa hela ile mbele ya macho ya watu, kauli ile ilimshtua mumewe na kuuliza.
“Vipi honey unaumwa?”
“Shaka hebu wahi dukani,” Edna alimtoa kwanza Shaka ndipo azungumze na mumewe.
Shaka aliondoka kwa kukimbia kwa vile alikuwa hajiamini alijikwaa na kuanguka.
“Shaka taratibu jamani siyo haraka kihivyoo.”
Shaka alinyanyuka bila kusema na kutokomea zake, baada ya kuondoka eneo lile aliona kama ametoka katika mdomo wa simba na kuapa hatafanya tena mapenzi na Edna.
Shaka hakujiamini mpaka alipofika nyumbani kwao, hakukaa, aliondoka kuogopa kutafutwa na mume wa Edna. Alirudi nyumbani majira ya saa nne usiku na kuingia ndani kimyakimya bila kula na kujifungia ndani.
Betty alirudi usiku mkubwa na kumgongea Shaka aliyekuwa amelala. Kwanza moyo ulimlipuka na kujua amefuatwa na mume wa Edna. Lakini sauti ya Betty ilimshusha pumzi zake.
Alipojaribu kujigeuza mwili ulikuwa umechoka sana kutokana na kazi ya kuulaza chini mbuyu kwa panga. Pamoja na kuchoshwa sana na Edna hakutaka kutoka usiku ule kwenda kwa Betty kwa kujua lazima atachemsha kwani wote walikuwa na miili mikubwa na nguvu kama nyati tofauti na Stella na Diana. Ili asiondoke na Betty alisingizia ugonjwa.
“Bebi naharisha.”
“Shaaaka! Mpenzi wangu jitahidi hata kidogo.”
“Betty yaani hata nguvu sina.”
“Shaka si heri ningekwenda kulala na Jimmy!”
“Bebi vumilia kwa leo.”
“Yaani Shaka hali ni mbaya mipombe niliyokunywa yote imekimbilia chini,” Betty alisema kwa sauti ya kilevi.
“Bebi naomba unielewe, usinigeuze chombo chako cha starehe,” Shaka alijifanya kuwa mkali.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Jamani Shaka yamekuwa hayo!”
“Ni wazi Betty hunipendi bali unataka kunigeuza chombo cha kumaliza hamu zako.”
“Siyo hivyo Shaka, mpenzi wangu nilijua unakuja kumaliza hamu zangu na kumkacha Jimmy kwa kusingizia ugonjwa ili nije kwako mpenzi wangu.”
“Ndiyo hivyo hali yangu leo tata, nina imani unanijua vizuri.”
“Mmh! Sawa nitafanyaje?” Betty alikubali kwa shingo upande.
Shaka ili kuonesha anaharisha alikimbilia msalani, alitulia kwa muda na kurudi huku ameinama ameshikilia tumbo.
“Vipi Shaka tumbo linauma sana?”
“Yaani wee acha tu.”
“Basi nikupeleke hospitali.”
“Acha tu nimeshameza dawa acha nilale tuangalie kesho.”
“Pole sana mpenzi wangu,” Betty alisema kwa sauti ya huruma.
“Asante.”
“Basi mpenzi kalale tutaonana kesho.”
“Usiku mwema.”
Betty aliondoka roho ikiwa haimpi kabisa kutokana na kupandwa na maruhani nyumbani alipaona pachungu alikodi gari kwenda kulala kwa mpenzi wake.
***
Siku ya pili Shaka alikwenda shule, kama kawaida Stella aliendelea kuwa naye karibu. Wakati wa mapumziko Stella akiwa amekaa na Shaka na shoga yake Diana. Alimwambia maneno ambayo yalikuwa mkuki moyoni kwa shoga yake.
“Bebi hamu zangu za jana leo nataka ukazimalize.”
“Hakuna tatizo.”
“Yaani jana nililala vibaya baada ya kuondoka ghafla wakati nikijua ilikuwa zamu yangu.”
“Kwani una zamu na nani?” Shaka alishtuka.
“Si kwa vile siku nyingine unawahi nyumbani.”
“Basi mama leo kazi ni kwako kama Voda.”
“Waaawooo mpenzi wangu,” Stella alimkumbatia Shaka bila kuogopa wanafunzi wenzao waliokuwepo wakipata vinywaji.
Jioni ya siku ile Stella alimlazimisha shoga yake amsindikize. Wakati wanajiandaa kuondoka Shaka aliitwa ofisini na mwalimu na kuwafanya watangulie nje kumsubiri.
Muda ulikwenda bila shaka kuonekana, Diana alimshauri Stella waondoke.
“Stella tutakaa mpaka saa ngapi huoni kama Shaka anaweza kuchelewa.”
“Tatizo lipo wapi, kama nakuchelewesha unaweza kuwahi,” Stella alijibu kwa hasira.
“Sina maana hiyo, kwani shida yako kuzungumza tu au kurusha roho kabisa?”
“Shoga nina ugwadu kama nimetoka gerezani.”
“Mmh! Si mtakesha?”
“Walaa, leo atanipa penzi jepesi ili niwahi nyumbani.”
“Mmh! Ninavyomjua Shaka akionja utataka tena.”
“Hamna kidogo tu.”
“Usinidanganye Shaka si mwanaume wa kuonja kidogo ukaridhika.”
“Umejuaje, shoga tunazungukana nini?”
“Aah..noo kwani vipi?” Diana alijikuta akipata kigugumizi baada ya kujisahau na kuchanganya madawa.
“Hapana umejuaje uwezo wa Shaka kama siyo kuzungukana?”
“Jamani Diana si ni wewe uliyenieleza kuwa Shaka ukikutana naye huwa hutamani muachane upesi.”
“Ooh! Kweli nilikuwa na wasiwasi unatia mkono kwenye mzinga wangu ya nyuki kulamba asali yangu.”
“Jamani shoga wanaume wote wameisha mpaka nimchukue mpenzi wako, kwanza Shaka kwangu mtoto mdogo.”
“Mdogo kwako lakini kwangu mkubwa mwenzangu.”
“Mmh! Tena huyoo anakuja,” Diana alisema baada ya kumuona Shaka kwa mbali akija.
“Diana tuachane na habari za Shaka asije kusema tukiwa peke yetu kazi yetu kumsema,” Stella alimwambia Diana.
“Mmh! Sawa.”
Wakati huo Shaka alikuwa amefika na kwenda moja kwa moja kwa Stella na kumbusu shavuni.
“Samahani sweet kuna somo nilikuwa naelekezwa na mwalimu ambalo sikulifanya vizuri.”
“Mmh! Sawa, ndiyo mwaka mzima?” Stella alilia wivu.
“Jamani kwanza tuliofanya vibaya tulipewa adhabu ya kuokota uchafu kisha nikaitwa ofisini kwa maelekezo.”
“Ofisini kulikuwa na walimu wangapi?”
“Watatu,” Shaka aliongopa ili kumfanya Stella asiwaze vingine.
“Sasa?”
“Nakusikiliza mama,” Shaka alijibu huku amtupia jicho Diana aliyebinua midomo kwa wivu.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nataka akanipe nusu dozi.”
“Wewe tu mimi tivii rimoti yangu ni wewe.”
“Diana twende zetu basi,” Stella alisema huku akinyanyuka kwenye kiti.
“Wapi?” Shaka aliuliza.
“Pa siku zote.”
“Sasa Stella mi si niende nyumbani tu,” Diana alimwambia shoga yake kwa kuamini ugwadu wake na utundu wa Shaka lazima wangekesha.
“Diana mbona leo sikuelewi tumekubaliana vipi, si nimekueleza hata nikichelewa nitarudi na wewe nyumbani ili nipate kujitetea.”
“Mi namjua Shaka akikushika huwezi kunikumbuka na kunifanya nikae niking’aa macho.”
“Mbona sikuelewi maneno yako yanaonesha kuna vitu vya Shaka unavielewa tofauti na nilivyokueleza.”
“Kwa sababu gani?”
“Kwa nini ung’ang’anie akinishika siwezi kutoka upesi?”
“Jamani, hivi unavyosema una ugwadu ni penzi jepesi tu mnaachana, lazima pachimbike bila jembe,” Diana alitengeneza uongo uliokubalika.
“Mimi si ndiye niliyekueleza nitawahi kutoka, vilevile Shaka anatakiwa kuwahi nyumbani kwao.”
“Kwani tatizo nini, kama ana haraka anaweza kwenda,” Shaka alisema.
“Shaka, Diana ni mtu muhimu sana nikichelewa kurudi nyumbani nikienda naye napata sababu ya kujitetea.”
“Sasa kama anajua hivyo mbona analeta mashauzi?” Shaka alijifanya kukasirika Diana.
“Basi shemu nitawasubiri,” Diana alikubali shingo upande.
Walikodi teksi hadi kwenye uwanja wa nyumbani, Shaka na Stella waliingia ndani na kumwacha sehemu Diana akisubiri huku donge la wivu likiwa limemtanda kwa kujua shoga yake anakwenda kufaidi mautundu ya Shaka.
Baada ya kuingia ndani, Stella alionekana ana uchu wa fisi, baada ya kuingia tu alimvamia Shaka na kumsaula kisha naye alisaula na kwenda naye bafuni kuoga. Shaka akiwa na matirio mapya alianzia kumpa mshikemshike kulekule bafuni kama alivyofundishwa na Betty.
Stella alizidi kuchanganyikiwa baada ya kulizwa machozi mawili bila msiba.
“Jamaniii.. Shaka yote haya umeyajulia wapi?”
“Kwa nini?”
“Si Shaka yule niliyekuwa nikijitahidi kumfundisha, sasa hivi wewe ni mwalimu tena mwalimu wa walimu.”
“Mmh! Kwa nini?”
“Huku hivi, kitandani sijui itakuwaje? Shaka kubali unioe.”
“Nitakuoa tukimaliza masomo.”
“Hapana Shaka tufunge hata ndoa ya siri.”
“Tutapanga.”
Baada ya kutoka bafuni Shaka akiwa mpya tofauti na aliyemzoea alimchanganya. Kila alichokifanya kulibadili raha na utamu. Baada ya kuchanganywa na utundu wa Shaka, Stella alijikuta akiangua kilio.”
“Unalia nini tena baby?” Shaka aliuliza.
“Kwa nini unampa raha zangu Diana?”
“Diana?” Shaka alishtuka.
“Ina maana hujui, nani kamwambia kuwa wewe mtamu?”
“Stella si shoga yako kakuumbua mbele yangu, kumbe tunachofanya unakwenda kumwambia shoga yako.”
“Muongo... muongo mkubwa yule,” Stella alijitetea.
“Mbona hukukataa mbele yake.”
“Unamuamini yule?”
“Amejuaje kama si wewe uliyemwambia?”
“Lakini si kujua uwezo wako wa kitandani nilimwambia wewe mtundu.”
“Sasa sema moja tumekuja kupeana raha au kuulizana maswali ya kijinga?” Shaka alijifanya kumjia juu Stella baada ya kujua akilegea ameumbuka.
“Kula raha mpenzi wangu.”
“Sasa huo upuuzi umetoka wapi ikiwa ni wewe uliyesema, mimi na wewe nani wa kumlaumu mwenzake?”
“Basi nisamehe mpenzi,” Stella alikuwa mpole.
Shaka alijua Stella ana wasiwasi lakini hana uhakika, aliamini dawa yake ni kumpa penzi mseto la kumrusha akili. Hukuwepo shetani wako alikuwepo. Maskini mtoto wa kike alimaliza maneno yote mdomoni kuusifia uwezo wa Shaka.
“Asante mpenzi sijawahi ila leo ndiyo nimeonja tamu ya penzi, kila kona ya mwili naisikia tamu. Asante mpenzi wangu, chondechonde usimpe mtu utamu huu haki ya nani nitaporwa. Shaka unajua, kweli wewe ni reli nyembamba lakini inabeba treni yenye mabehewa na watu wake.”
Shaka hakujibu kitu kwa vile alijua hawezi kula karanga huku anapiga mluzi, alinyamaza kimya na kuwakusanya mabeki na kuachia shuti kali lililomfanya Stella apige kelele na kwenda juu, aliporudi chini alitulia na kutembeza mikono hewani kama anataka kudaka kitu.
***
Nje ya hoteli, Diana aliteseka akiamini Stella alikuwa akifaidi mavituz ya Shaka, miguu ilikuwa haitulii wadudu wadogowadogo walimtesa, alijikuta akiteseka hata hamu ya kuendelea kuwa pale hakuwa nayo zaidi na yeye kumpata mtu kama Shaka ili ampunguze muwasho wa ulimi usiokunwa kwa vidole.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijitahidi kuvumilia kwa saa moja lakini hakumuona mtu akitokea zaidi ya kuendelea kupigwa na baridi huku akikumbuka machejo ya Shaka akiamini lazima shoga yake hatakubali bao moja kama mguu wa jini lazima atataka kichane cha ndizi na kuzidi kumuweka lindo.
Aliamini hawawezi kutoka mapema hasa baada ya kuonja tamu ya Shaka na kujua siri inayomfanya shoga yake kuingia kichwakichwa na kumng’ang’ania kama ruba.
Moyoni aliapa kulipa kisasi kwa Stella kufanya mambo ambayo yatamfanya Shaka amsahau shoga yake siku wakikutana. Aliamini kabisa shoga yake si mjanja katika mambo ya kitandani kama yeye kwa sababu ya geti kali. Kila alivyokuwa akijiuliza uwezo wa Shaka na umbile lake alichanganyikiwa.
Aliwazidi wanaume wengi wenye maumbile na umri mkubwa aliofanya nao mapenzi wakiwa wamelewa na kushindwa kumkidhi haja zake na yeye kwa vile huwa anataka fedha kujikuta akifa kizungu na tai shingoni lakini mara nyingi hupakwa shombo tu.
Aliamini siku akimtia mikononi Shaka atahakikisha na yeye anakamuliwa zote za muda aliokuwa naye mbali. Muda nao ulikuwa ukikatika kama hauna akili nzuri hakuonekana Stella wala kivuli chake.
Aliamua kumpigia simu ambayo iliita mpaka inakatika bila kupokewa alirudia zaidi ya mara tano. Mwisho wake ilizimwa kabisa, kitendo kile muudhi sana na kuona amedharauliwa na kujiuliza kama mpaka simu imezimwa ina maanisha hawatoki mapema amenogewa na kuona simu yake kero heri angepokea na kumweleza anatoka saa ngapi.
Stella aliamua kuongeza nusu saa kama itavuka hatakuwa na silimile zaidi ya kuondoka. Lakini saa nzima ilipita bila kuonekana alijaribu tena kupiga simu lakini haikupatikana aliamua kuondoka.
Ndani ndiyo kwanza Stella alikuwa akishtuka usingizini na kumkuta Shaka amelala lakini bakora ilikuwa juu kama mkungu wa ndizi, saa ya mkononi ilimuonesha muda umekwenda na kamuweka shoga yake saa mbili zaidi ya makubaliano.
Alijifikiria waondoke au aendelee, lakini hamu ilikuwa kubwa kuliko woga wa kurudi nyumbani. Alimshtua Shaka aliyekuwa usingizini, alipoamka na kuona muda umekwenda alimuuliza:
“Vipi ndo tunaondoka?”
“Shaka umenichoka?” Stella alimuuliza Shaka huku akimshika kifuani.
“Vipi tena mpenzi?”
“Hivi Shaka hujisikii kuwa na mimi, tuna muda gani hujanipa haki yangu mimi mkeo?”
“Ni muda mrefu lakini sipendi upate tatizo kwa ajili yangu.”
“Tatizo gani Shaka, hakuna tatizo lolote.”
“Na kuhusu Diana?”
“Shaka unamjua Diana kuliko mimi?”
“Kumjua siyo sababu zaidi ya makubaliano yenu, siku zote tunakutana peke yetu kama umemleta lazima uheshimu makubaliano.”
“Nikubaliana na wewe lakini mimi na Diana tunajuana.”
“Mmh! Kumbe huo ndiyo mtindo wenu.”
“Mtindo gani?”
“Na yeye akienda kwa mwanaume wake unamsindikiza?”
“Hata siku moja.”
“Lakini wewe huwa anakusindikiza.”
“Mara nyingi.”
“Kwa rafiki zako.”
“Shaka hayo maneno gani, unaniona malaya siyo kwa kukuvulia nguo yangu ya ndani siyo?” Stella aling’aka
“Hilo si jibu, nijibu nililokuuliza,” Shaka kwa mara ya kwanza alimkazia Stella sauti ya kiume Stella.
“Siyo hivyo Shaka, mara nyingi ninapokuwa na wewe huwa anajua nipo wapi hunipitia na kunisindikiza nyumbani, kwa vile ni shoga yangu humuamini kuwa nimepitia kwao.”
“Bado sijakuelewa, inaonekana hii ndiyo tabia yenu?”
“Tabia gani tena baby mbona najuta kulizua.”
“Siyo kulizua nafahamu kabisa mtindo huu haukuanza leo kwa vile sikukuta msichana.”
“Mungu wangu, yaani umefika huko?”
“Mimi nani yako?”
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mume wangu.”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment